Thursday, 7 January 2021

Waziri Mkuu Majaliwa: Ubora Wa Miradi Ulingane Na Thamani Ya Fedha


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema miradi yote inayotekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini lazima isimamiwe vizuri ili kuhakikisha inakuwa na viwango vinavyoendana na thamani ya fedha iliyotolewa na Serikali.

“Maelekezo ya Serikali kwenye maeneo yote muhimu ya miradi isimamiwe kwa kina na hasa thamani ya fedha na viwango vya ujenzi wa miradi yenyewe. Tumeona Sekondari ya Tunduru, majengo ya halmashauri ya wilaya ya Mbinga, barabara ya Mbinga-Mbamba Bay na uwanja wa ndege utaalamu umetumika na thamani ya fedha ipo.”

Ametoa agizo hilo jana (Jumatano, Januari 6, 2021) alipozungumza na viongozi wa mkoa wa Ruvuma katika Uwanja wa Ndege wa Songea akiwa njiani kuelekea Dar es Salaam. Uwanja huo kwa sasa unakarabatiwa ili kuimarisha huduma za usafiri wa anga mkoani Ruvuma.

Amesema zaidi ya shilingi bilioni 37 zimetumika kuimarisha uwanja huo kwa lengo la kuboresha utoaji wa huduma. Ukarabati huo umehusisha njia ya kurukia ndege yenye uwezo wa kupokea abiria zaidi ya 150, jengo la abiria na maeneo ya maegesho yenye uwezo wa kuegesha ndege kubwa sita. Uwanja huo utakapokamilika utaruhusu ndege kutua usiku na mchana.

Waziri Mkuu amewataka viongozi hao waendelee kuwahamasisha wananchi kutumia fursa hiyo ya uwepo wa miradi mikubwa ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali katika kufanya biashara ili kukuza uchumi wao kwa kuwa wana miundombinu ya kutosha.

Kadhalika, Waziri Mkuu amewasisitiza viongozi hao wahakikishe wanasimamia matumizi ya miundombinu ya miradi mbalimbali iliyokamilika ili iweze kutumika vizuri zaidi na kwa muda mrefu.

 (mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU


Share:

Simu na kamera zapigwa marufuku katika vituo vya kupiga kura Uganda


Tume ya uchaguzi nchini Uganda imepiga marufuku wapiga kura kwenda na simu au kamera kwenye kituo cha kupiga kura wiki ijayo tarehe 14 au kubaki kituoni kusubiri matokeo, agizo hilo limetolewa jana na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Jaji Simon Byabakama mjini Kampala.

Huku mashirika yasiyo ya serikali yakitaka tume kufafanua kuhusu teknolojia itakayotumiwa katika uchaguzi mkuu zikiwa zimesalia siku saba kufanyika zoezi hilo.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini Uganda Jaji Simon Mugenyi Byabakama ametangaza kanuni zitakazotumiwa katika uchaguzi huo, ikiwa ni pamoja na kupiga marufuku waandishi habari kuingia ndani kwenye vituo vya kupiga kura ,kuvaa sare za chama chochote cha siasa au za mgombea yoyote, simu za mkononi pamoja na kamera

Agizo la Jaji Byabakama kuzuia wapiga kura kubaki kwenye vituo vyao vya kupiga kura zinakinzana na zile za baadhi ya wagombea wa kiti cha rais ambao wamesikika katika kampeni zao za uchaguzi wakiwataka wafuasi wao baada ya kupiga kura wabaki kituoni kulinda kura zao.

Mwenyekiti wa tume ameongeza kuwa wapiga kura wakibaki kwenye vituo vya kupiga kura watasababisha msongamano mkubwa wa watu na kuvunja kanuni za watalaam wa afya za kudhibiti virusi vya corona.


Share:

Serikali kuendelea kutekeleza ahadi zake ujenzi wa Meli Ziwa Nyasa, MV Mbeya II yakamilika, yaanza kazi.


 Na Grace Semfuko, MAELEZO
Katika kuhakikisha azma ya Serikali ya kuwa na miundombinu bora katika maziwa makuu ya Tanzania na inachangia katika kukua kwa uchumi wa nchi, Serikali ya awamu ya tano imeendelea utekelezaji wa ahadi zake za kuimarisha miundombinu hiyo ambapo katika Ziwa Nyasa sasa suala la usafirishaji limepatiwa ufumbuzi.

Wakati akilihutubia Bunge kwa mara ya kwanza mara baada ya kuchaguliwa na Watanzania kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Novemba 20, 2015 Rais Dkt John Pombe Magufuli alisema pamoja na mambo mengi ya kimaendeleo yatakayofanywa na Serikali yake lakini kuimarisha miundombinu na ujenzi wa uchumi ni miongoni mwa mambo ya kipaumbele.

“Masuala mengine tutakayoyawekea mkazo katika utawala wa Serikali ya awamu ya tano ambayo ninaamini yatasaidia katika kujenga uchumi wetu ni pamoja na masuala ya miundombinu, utekelezaji wa masuala haya yamefafanuliwa vizuri katika ilani ya CCM ya mwaka 2015 hivyo tutatekeleza ipasavtyo” alisema.

Miongoni mwa ahadi za Serikali ya awamu ya tano tangu ilipoingia madarakani ilikuwa ni kuimarisha sekta ya miundombinu pamoja na kuwahakikishia wakazi waishio kando ya Bahari na maziwa nchini usafiri salama na wa uhakika.

Wakazi waishio kando ya Ziwa Nyasa kwa muda mrefu walikuwa wakihitaji usafiri wa njia ya maji ambao sasa jawabu lake limepatikana kufuatia kukamilika kwa meli kubwa ya mizigo na abiria na kusababisha wakazi hao kuondokana na adha ya usafiri katika maeneo yao.

Iliwachukua mwendo wa muda mrefu wakazi wa maeneo hayo wanaohitaji kwenda kwenye mikoa ya Mbeya na maeneo mengine kuzunguka umbali mrefu kwa njia ya gari huku suluhisho la njia ya mkato kwenye ziwa hilo ikiwa inafanyiwa kazi.

Jumanne January 5, 2021 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa alizindua rasmi Meli ya MV Mbeya II mara baada ya ujenzi wa meli hiyo kukamilika.

Meli hiyo mpya ya MV Mbeya II ni miongoni mwa ujenzi wa meli tatu za ambazo mbili kati yake  ni za mizigo ikiwepo MV Ruvuma na MV Njombe zote zikiwa ni za mizigo zinazogharimu kiasi cha shilingi Bilioni 11 na hiyo moja iliyokamilika ya MV Mbeya II iliyogharimu shilingi Bilioni 9.1 za Kitanzania.

Pamoja na kukamilika kwa ujenzi wa Meli hiyo mpya pia Serikali inaimarisha Bandari zilizopo kwenye ziwa hilo ikiwepo ujenzi wa Bandari ya Ndumbi

Ziwa Nyasa lenye jumla ya Bandari 15 kwa upande wa Tanzania zikiwepo sita za mkoani Ruvuma, Sita za Mkoani Njombe na tatu za Mkoani Mbeya limekuwa na tija ya kiuchumi kwa wananchi waishio kwenye mikoa hiyo ambapo sasa mpango wa Serikali ni kuhakikisha wananchi wananufaika zaidi.

Ujenzi wa Meli hiyo itakayokuwa ikifanya safari zake katika Ziwa Nyasa kutoka Bandari ya Kyela Mkoani Mbeya hadi Mbambabay Mkoani Ruvuma na kwenye maeneo ya nchi jirani za Malawi na Msumbiji  umegharimu shilingi Bilioni 9.1 za kitanzania na ina uwezo wa kubeba abiria 300 na tani 200 za mizigo.

Meli hiyo imejengwa na Kampuni ya Kitanzania ya Songoro Marine huku lengo la Serikali ni kuhakikisha kampuni za kitanzania zinanufaika katika ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya kijamii.

Lengo la ujenzi wa Meli hiyo pamoja na nyingine zitakazokuwa zikifanya kazi kwenye Ziwa Nyasa ni kuboresha uchumi wa wakazi wa maeneo hayo pamoja na Taifa kwa ujumla kupitia sekta ya usafirishaji.

Katika uzinduzi huo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Tanzania inapakana na nchi nane ambazo zinategemea kupata bidhaa mbalimbali kutoka Tanzania na kuwataka wakazi nchini kutumia fursa ya meli hiyo kufanya biashara ili kujinufaisha kiuchumi.

Amesema kutokana na kuona umuhimu wa kuwajengea uwezo wananchi kiuchumi na ndio maana Serikali inaamua kuimarisha miundombinu ya usafirishaji ikiwepo ujenzi wa Meli za kisasa za Abiria na Mizigo, ujenzi na ukarabati wa barabara, Ujenzi wa Bandari za kisasa pamoja na miundombinu ya reli lengo likiwa ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma zote za kijamii.

Deusdedit Kakoko ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini Tanzania anasema kukamilika kwa ujenzi wa meli hiyo kunaendelea kuleta ufanisi katika utendaji kazi wa bandari huku akisema bado mamlaka inaendelea na uboreshaji wa bandari pamoja na ujenzi wa meli.

Ujenzi wa Meli katika Ziwa Nyasa unakwenda sambamba na uimarishwaji wa miundombinu ya barabara ambapo ujenzi wa barabara ya Mbinga-Mbambabay yenye urefu wa kilomita 66 iliyogharimu shilingi Bilioni 129.361 umekamilika ambapo wakazi wa maeneo hayo sasa wananufaika na matunda ya kazi hiyo iliyofanywa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya amesema ujenzi wa barabara hiyo ni ndoto za Rais Magufuli za kuzidi kuimarisha miundombinu ya usafirishaji nchini na kwamba Wizara ya yake itahakikisha inasimamia kikamilifu bandari nchini katika kukusanya mapato kwa njia ya kielektroniki ili ziweze kujiendesha.


Share:

Zaidi Ya Watanzania Milioni 12 Waishio Vijijini Wafikiwa Na Huduma Za Mawasiliano


Na Celina Mwakabwale, UCSAF
Mtendaji Mkuu wa mfuko wa mawasiliano kwa wote (UCSAF), Justina Mashiba amesema mpaka sasa zaidi ya wananchi millioni 12 waishio maeneo ya vijijini na yasiyo na mvuto wa kibiashara pamoja na wale wa mipakani na kanda maalum wamefikiwa na huduma mbalimbali za mawasiliano ikiwemo simu, runinga, radio pamoja na mawasiliano ya posta.

Bi. Mashiba ameyasema hayo wakati wa ziara ya Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Faustine Ndugulile aliyetembelea tasisisi hiyo na kufanya kikao na wajumbe wa bodi, menejimenti pamoja na wafanyakazi. Katika ziara hiyo aliambatana na Katibu Mkuu, Dkt. Zainab Chaula, Naibu Katibu Mkuu Dkt. Jim Yohazi pamoja na baadhi ya watendaji wa Wizara hiyo.

Dkt Ndugulile ameipongeza UCSAF kwa kufikisha huduma za mawasiliano kwenye maeneo mbalimbali nchini huku akiitaka kuwekeza zaidi katika teknolojia yenye gharama nafuu ili kuyafikia kwa haraka maeneo ambayo bado hayajafikiwa na huduma za mawasiliano. Hivi sasa UCSAF inatumia shilingi milioni 350 kujenga mnara mmoja wa mawasiliano.

Ameongeza kwa kusema kuwa, sekta ya Mawasiliano na Teknolojia ya habari inabadilika kwa kasi hivyo ameitaka wizara kukamilisha uandwaaji wa sheria ya TEHAMA ili kuendana na kasi ya mabadiliko hayo.

Akizungumza na wajumbe wa bodi Dkt Ndugulile ameagiza kuwepo na utaratibu mzuri wa kufanya kazi kwa ukaribu na kwa ushirikiano kati ya Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) na UCSAF ili kuongeza kasi ya upelekaji wa huduma mbalimbali za mawasiliano katika maeneo wanayoshirikiana.

Nae Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Zainab Chaula ameipongeza UCSAF huku akiitaka kuendelea kufikisha huduma za mawasiliano ili kuendana na malengo ya kuanzishwa kwa wizara hiyo.

Hadi sasa mfuko wa mawasiliano kwa wote umefanikiwa kufikisha huduma mbalimbali za mawasiliano ikiwa ni pamoja na kuwasha minara katika kata 633 zenye vijiji 2,320, kuunganisha mtandao wa intaneti na kutoa vifaa vya TEHAMA kwa shule 711, kutoa mafunzo ya TEHAMA kwa walimu 2,213 wa shule za UMMA kutoka Mikoa yote ya Tanzania Bara pamoja na kujenga vituo 10 vya TEHAMA visiwani Zanzibar.

 Mfuko wa Mawasiliano Kwa Wote (UCSAF)


Share:

Walimu Wahamasishwa Kujiendeleza Kielimu


 Na Veronica Simba
Serikali imewahamasisha Walimu wa Shule za Msingi na Sekondari nchini, kujiendeleza kielimu katika ngazi mbalimbali ili kuboresha zaidi utendaji wao wa kazi.

Wito huo umetolewa jijini Dodoma leo, Januari 7, 2021 na Kaimu Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Moses Chitama wakati akizungumza na Wajumbe wa Mkutano wa Pili wa Umoja wa Walimu Wakuu wa Shule za Msingi Tanzania Bara.

Akifafanua, amesema kuwa, kujiendeleza kielimu ni haki ya msingi kwa watumishi wote wa umma wakiwemo walimu, ndiyo maana Serikali kupitia Tume imekuwa ikiwahamasisha kuitumia fursa hiyo ipasavyo.

Chitama amekemea tabia ya baadhi ya Walimu Wakuu wa Shule za Msingi na Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania Bara, ambao hukataa kutoa ruhusa kwa watumishi walio chini yao wenye nia ya kujiendeleza kielimu.

Hata hivyo, Kaimu Katibu huyo amesisitiza kuwa Walimu wote wa shule za umma wenye nia ya kujiendeleza kielimu, wanapaswa kuzingatia taratibu zilizowekwa na Mamlaka ikiwemo kufuata Mpango wa Mafunzo.

Aidha, amewasisitiza kuhakikisha wanapata ruhusa ya maandishi kutoka kwa Wakuu wao, kabla ya kwenda masomoni kwani kinyume chake watakabiliwa na mashtaka ya utoro kazini ambayo adhabu yake ni kufukuzwa kazi.

 “Tumekuwa tukipata rufaa nyingi za kesi za Walimu ambao walitoroka kazini na kwenda masomoni hivyo kufukuzwa kazi. Serikali inapenda walimu msome lakini fuateni taratibu zilizowekwa,” amesisitiza.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi wa Ajira na Maendeleo ya Walimu kutoka TSC, Mecktildis Kapinga, akifafanua kuhusu utaratibu wa kupanda vyeo, ameueleza Mkutano huo kuwa, kanuni inaelekeza kutompandisha cheo mtumishi yeyote wa umma akiwa masomoni, hadi pale anapohitimu ndipo mchakato wa kumpandisha hufanyiwa kazi.

“Naomba mtambue kuwa utaratibu huo ni kwa watumishi wote wa umma, na siyo kwa walimu pekee kama ambavyo baadhi yenu mmekuwa mkinung’unika,” amefafanua Kapinga.

Mkutano huo wa siku tatu, ulianza Januari 5, 2021 huku ukiongozwa na kaulimbiu isemayo uongozi na usimamizi makini wa elimu, utaimarisha Tanzania katika uchumi wa kati.

Tume ya Utumishi wa Walimu ni Mamlaka ya Ajira na Nidhamu kwa walimu wa shule za msingi na sekondari Tanzania Bara, walio kwenye utumishi wa umma.


Share:

Ukaguzi wa Dawa kwenye vituo vya kutolea Huduma – Rukwa


Nteghenjwa Hosseah, Rukwa
Mkurugenzi wa huduma za Afya Ustawi wa Jamii na Lishe Dr. Ntuli Kapologwe amewaagiza waganga wafawidhi wote wa vituo vya kutolea huduma za Afya kuhakikisha wanafanya ukaguzi wa dawa (Medicine Audit) kila robo mwaka kwa mujibu wa sheria na taratibu.

Dr. Ntuli ameyasema hayo wakati alipokua akiongea na timu za usimamizi wa huduma za afya Mkoani Rukwa wakati wa ziara ya usimamizi shirikishi mkoani humo tarehe 02/01/2020.

Akizungumza katika kikao hicho Dr.Ntuli amesema hakutakuwa msamaha kwa kituo cha kutolea huduma ambacho hakitafanya ukaguzi wa dawa na taarifa ya kila Mkoa kuwasilishwa Ofisi ya Rais – TAMISEMI.

“ Kwa kufanya ukaguzi wa dawa tutaweza kujua namna dawa zilivyotumika, dawa gani eneo fulani inatumika sana na kwanini na hivyo kubaini mahitaji zaidi kwa wakati unaokuja.

Pia itawezesha kufahamu kiasi cha Fedha kilichopatikana kutokana na mauzo ya dawa ambacho kitatumika tena kurudi kununua dawa MSD’ alisisitiza Dr Ntuli.

Aliongeza kuwa ukaguzi wa dawa ukifanyika kikamilifu itasaidia Kubaini upotevu wa dawa pamoja na wizi wowote uliotokea katika kituo husika.

Dr. Ntuli alisistiza umuhimu wa kufanya ukaguzi wa dawa kuwa ni pamoja na kuwa na uwezo wa kufanya mlinganisho wa kiasi cha dawa kilichotumika sambamba na wagonjwa halisi waliohidumiwa na kuwa na takwimu halisi za Serikali katika kutoa Fedha za dawa.

Aidha Dr. Ntuli aliwakumbusha wataalam wa afya kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr. John Joseph Pombe Magufuli mwezi Novemba 2020 alitoa shilingi Bil. 41 kwa ajili ya ununuzi wa dawa na fedha hizo zimeelekezwa MSD.

‘Fedha hizo zitawezesha kila kituo kupata dawa za kutosha sasa ni jukumu la kila kituo kuhakikisha kinazungusha(REVOLVE) fedha baada ya kuwa wametoa huduma kwa kurejesha MSD ili upatikanaji wa dawa uwe endelevu na wananchi waweze kupata dawa wakati wote watakapohitaji” alisisitiza Dr Ntuli.


Share:

Polisi wanne wasimamishwa kwa utovu wa nidhamu Arusha


Na Woinde Shizza ,ARUSHA
Jeshi la Polisi nchini limewafukuza kazi kwa fedheha askari wake wanne kutokana na makosa mbalimbali ya utovu wa nidhamu ,rushwa na wizi.

Akiongea na vyombo vya habari Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha ,Salumu Hamduni alisema kuwa askari hao wametimuliwa kazi jana januari 6,Mwaka huu .


Alisema kabla ya kufukuzwa  kazi kwa askari hao ,walifikishwa kwenye mahakama ya kijeshi na kukutwa na hatia na kwamba watafikishwa mahakamani Kama vibaka wengine wanaojihusisha na matukio ya uhalifu


“Askari hao tumewafukuza kazi baada ya kuwafikisha kwenye mahakama ya kijeshi na watashtakiwa Kama vibaka wengine wa kawaida”alisema Kamanda


Aliwataja askari hao kuwa ni pamoja na  askari mwenye namba G. 5134 DC Heavenlight Mushi  aliyekuwa Askari kitengo Cha Intelijensia Mkoa wa kipolisi kinondoni jijini Dar es Salaam,H.125 PC Gasper Paul kitengo Cha Intelijensia makao makuu Dodoma na H.1021 PC Bryton Murumbe aliyekuwa askari wa kawaida mkoani Dodoma.


Kamanda alifafanua kwamba askari hao wamefukuzwa kazi kutokana kwa kosa la kumteka mfanyabiashara wa Madini jijini Arusha,Sammy Mollel ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya madini ya Germs and Rocks Venture ya jiji Arusha na kujipatia kiasi cha sh, milioni 10 kinyume cha sheria.


Alisema askari hao wakikamatwa desemba 24,2020 katika ofisi za mfanyabiashara huyo baada ya kufika kwa ajili ya kuchukua mgao wa pili wa shilingi milioni 20 kati ya milioni 30 walizohitaji na kupatiwa sh,milioni 10.


Mwingine aliyefukuzwa kazi ni askari mwenye namba F.1445 CPL Koplo William Joseph mkazi wa Muriet jiji Arusha ambaye alikamatwa jana nyumbani kwake akiwa na na bidhaa mbalimbali haramu ikiwemo misokoto ya bangi.


Alisema kuwa askari huyo alikutwa na misokoto 20 ya bangi bhangi kwenye gari lake ,kukiunganishia umeme wa wizi kinyume cha sheria,kupatikana na pombe ya gongo lita tano na lita mafuta ya Dizel Lita 85.


Pia alikutwa na vyuma vya bomba kinyume na taratibu,pombe ya viroba boksi 84 iliyookatazwa na serikali,chupa 9 za konyagi na pakti 3 za pombe aina ya kiroba .


Kamanda alisema kuwa upelelezi wa matukio hayo umekamilika na majalada yamepelekwa ofisi ya taifa ya mashtaka kwa ajili ya hatua zaidi na majalada hayo yakirudi watafikishwa mahakamani.




Share:

Mume Auawa Baada ya Kumfumania Mkewe na Mwanaume Mwingine


Mtu aliyetambuliwa kwa jina la Juma Kitemango (48) mkazi wa Matundasi Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya, ameuwawa kwa kushambulia na vitu vyenye ncha kali na mgoni wake, Juma Sunzima (40) baada ya kuwafumania na mkewe wakiwa ndani ya chumba chake. 


Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Jerome Ngowi,  amewaambia waandishi wa habari Januari 6 jijini humo kuwa tukio hilo lilitokea Januari 4 wilayani humo, baada ya marehemu kufika nyumbani kwake na kumkuta mkewe Merry Daimon, akiwa na mwanaume aliyedaiwa kuwa ni mpenzi wake. 


"Marehemu aliwafumania mkewe na mtuhumiwa wakiwa wanafanya yao ndani ya nyumba yake waliyokuwa wakiishi na mkewe na ndipo ulipotokea mzozo na mtuhumiwa kumjeruhi na vitu vyenye ncha kali na sehemu za kichwani na utosini na kusababisha kifo chake," alisema.


Asema mara baada ya tukio hilo mke wa marehemu na mtuhumiwa  walikimbia  na kwamba  jeshi la polisi linaendelea na msako ili wafikishwe mikononi mwa sheria.


Alisema uchunguzi wa awali umebaini kuwa mareheme kabla ya umauti kumkuta walikuwa na migogoro isiyokwisha na mkewe ya kimahusiano iliyohusihwa na wivu wa kimapenzi.



Share:

Video Mpya : NYAKABAYA - KWENDA MBINGUNI

Msanii  Nyakabaya ameachia wimbo mpya mwaka 2021 unaitwa Mbinguni Hatuendi...Tazama video hapa chini

Share:

NECTA: Important Announcement to All FORM FOUR and QT Candidates 2021

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

NECTA: Important Announcement About FORM FOUR and QT Candidates Registration, 2021   The National Examination Council of Tanzania (NECTA)   Summary of NECTA’s History: After Tanzania Mainland had pulled out of the East African Examinations Council, in 1971 and before NECTA was established by Law, in 1973, the Curriculum and Examinations Section of the Ministry […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Secretary at Mziray Oil Company Limited

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Overview We Mziray Oil Company Limited a Retail Oil supply to final consumer based in Tanga, Tanzania fully licensed and incorporated under the Company Act 2002 is currently looking for dynamic result oriented individual to fill the following position (Women are highly preferred) Job Tittle: Secretary Duties and responsibilities   Receive, interview and direct visitors accordingly […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Accountants at Mziray Oil Company Limited

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Overview We Mziray Oil Company Limited a Retail Oil supply to final consumer based in Tanga, Tanzania fully licensed and incorporated under the Company Act 2002 is currently looking for dynamic result oriented individual to fill the following position (Women are highly preferred) Job Tittle: Accountants (4 Posts) Reports to: Finance Manager Department: Finance and Accounting   […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Wimbo Mpya : NTEMI O MABALA 'NG'WANA KANG'WA' - ILHUMBI


Msanii wa nyimbo za asili Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa' anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa Ilhumbi..Huu hapa
Share:

Wimbo Mpya : NTEMI O MABALA 'NG'WANA KANG'WA' - YOMBO


Hii hapa Ngoma Nyingine ya Ntemi O Mabala 'Ng'wana Kang'wa' inaitwa Yombo.... Sikiliza hapa chini
Share:

TETESI ZA SOKA LEO ALHAMISI JANUARI 7,2021



Mazungumzo mapya ya kandarasi kati ya Liverpool na kiungo wa kati wa Uholanzi Georginio Wijnaldum, 30, yamegonga. (Sky Sports).

Mgombea wa rais katika klabu ya Barcelona Agusti Benedito anasema kwamba hafikirii kwamba Lionel Messi 33 ataongeza mtakaba wake katika klabu hiyo unaoisha mwezi Juni 2021. (Goal)

Manchester City inaamini wako mbele ya mstari kumsaini lionel Messi iwapo mshambuliaji huyo wa Argentina ataondoka Barcelona katika majira ya joto. (Telegraph - subscription required)
Lakini Barcelona inasema kwamba itajaribu kuzungumza na Messi ili kumshawishi kuongeza mkataba wake baada ya kusema kwamba angependelea kucheza nchini Marekani mwisho wa mchezo wake. (AS)

Everton inataraji kupokea ofa za Moise Keane 20 kutoka klabu ya PSG , ambapo mshambulaji huyo wa Itali yuko katika mkopo lakini pia Everton haina haraka kuamua kuhusu hatma yake ya baadae.. (Liverpool Echo)

Kiungo wa kati wa Arsenal na Ujerumani Mesut Ozil, 32, amekubali mkataba wa miaka mitatu na nusu na klabu ya uturuki Fenerbahce. (DHA - in Turkish
Hatima ya Ozil itaamuliwa hivi karibuni , lakini lengo la mshindi huyo wa kombe la dunia ni kusalia Arsenal hadi kandarasi yake itakapokamilika katika majira ya joto.. (ESPN)

CHANZO - BBC SWAHILI
Share:

Utafiti : MBUZI WANAVUTIWA NA BINADAMU WANAOTABASAMU


Utafiti wa muonekano wa furaha wa mbuzi umefanyika Uingereza

Wanasayansi wamebaini kwamba mbuzi wanavutiwa na binaadamu wanaotabasamu.

Utafiti huo umeelezea kwa kina namna ambavyo wanyama huwa wanatambua hisia za watu zaidi ya ilivyokuwa inafikiriwa awali.

Watafiti wamewaonesha mbuzi picha za mtu mmoja, moja iliyomuonyesha akiwa amekasirika na nyingine mtu huyo akiwa na furaha.

Katika jarida la Open Science, watafiti wameeleza kwamba mbuzi hao walifanikiwa kuifuata picha ya mtu aliye na furaha.

Matokeo hayo yanadhihirisha kwamba uwezo wa wanyama kutafsiri hisia za binadamu sio mdogo ikilinganishwa na mbuzi ambao wameishi na kufugwa kama mbwa au farasi.

Badala yake inaonekana kuwa wanyama wanaofugwa kwa chakula. kama mbuzi pia wanaweza kutambua hisia usoni mwa binaadamu.

Watafiti wamebaini kwamba mbuzi wanapenda zaidi watu wanaotabasamu na kuzifuata picha za watu wenye furaha kabla ya kutambua picha za watu waliokasirika. Na pia walitumia pua zao zaidi kuzitambua vizuri picha za watu wanaotabasamu.

Lakini picha hizo za muonekano wa furaha ziliwapendeza zaidi zilipowekwa katika upande wa kulia.

Watafiti wanaamini huenda ni kwasababu mbuzi wanatumia upande wa kulia wa ubongo wao kutathmini matukio - jambo linalodhihirika kwa wanyama wengine.

Na picha hizo zilipowekwa katika mkono wa kushoto mbuzi hao hawakuonekana kuvutiwa nazo.

Inaweza ikawa upande wa kushoto wa ubongo ndio unatafakari hisia chanya au upande wa kulia wa ubongo ambao hauonesha sura ya hasira.

Dr. McElligott kutoka chuo kikuu cha Roehampton anasema utafiti huu ni muhimu kwa sababu umeonyesha namna ambavyo mnyama anaweza kuhusiana na viumbe hai wengine kwa sababu uwezo wa mnyama kuelewa hisia za binaadamu huenda umesambaa na sio tu kwa wanyama wa kufugwa nyumbani.

 CHANZO - BBC SWAHILI

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMIS JANUARI 7,2021













Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger