Thursday, 7 January 2021

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMIS JANUARI 7,2021













Share:

Wednesday, 6 January 2021

Software Engineer at AA TANCH Holding Company LTD

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Job title: Software engineer (1 position)   Location: ARUSHA, Head office Reports to: Managing director Projects: SOKOKUUONLINE AND TANCH EXPRESS APP SUMMARY: AA TANCH holding company ltd is a private limited company established in 2018.It focused on connecting buyers to seller, dedicated in providing easy, reliable and secure trades as well as shipment and delivery of products from china. As […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

TANAPA: Names Called for Interview at UTUMISHI on 16th – 19th January, 2021 | Walioitwa Usaili TANAPA 2021 | Tanzania National Parks, 2021

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Tanzania National Parks (TANAPA)   PRESIDENT’S OFFICE PUBLIC SERVICE RECRUITMENT SECRETARIAT (PSRS) Ref.No.EA.7/96/01/L/11 – Posted: 05th January, 2021 Overview: The Public Service Recruitment Secretariat (PSRS) is a government organ with a status of independent Department established specifically to facilitate the recruitment process of employees to the Public Service. Public Service Recruitment Secretariat was established by […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

PROF.MKENDA APANIA KUREJESHA HADHI YA USHIRIKA NCHINI

 

 

Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda akizungumza na Warajis Wasaidizi wa mikoa ya Tanzania Bara leo 6.1.2021 katika hafla ya kukabidhi vitendea kazi yakiwemo magari pamoja na kompyuta katika Ofisi za Tume ya Maendeleo ya Ushirika Jijini Dodoma.

Mrajis Mkuu na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt. Benson Ndiege akitoa taarifa wakati hafla ya kukabidhi vitendea kazi yakiwemo magari pamoja na kompyuta katika Ofisi za Tume ya Maendeleo ya Ushirika Jijini Dodoma.

Sehemu ya Warajis kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara wakimsikiliza Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda leo Jiji Dodoma.

Waziri wa Kilimo Prof.Adolph Mkenda (Katikati) akimkabidhi kompyuta mpakato (laptop)Afisa Ushirika wa Mkoa wa Geita Dorah Mwabeza(Kushoto)kwa niaba ya Mrajis wa Mkoa huo.Prof. Mkenda amekabidhi laptop 20 pamoja na kompyuta za kawaida 50 zilizotolewa naTume ya Maendeleo ya Ushirika leo 6.1.2021 jijini Dodoma kwa warajis.Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt.Benson Ndiege

Waziri wa Kilimo Prof.Adolph Mkenda (Katikati) akimkabidhi funguo za gari Mrajis Msaidizi wa Vyama Vya Ushirika Mkoa wa Simiyu Ibrahimu Kadudu (Kushoto).Prof. Mkenda amekabidhi magari matano yenye thamani ya milioni 275/= yaliyotolewa na Tume ya Maendeleo ya Ushirika leo 6.1.2021 jijini Dodoma Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt.Benson Ndiege

Waziri wa Kilimo Prof. Adolph Mkenda (Katikati) akimkabidhi funguo ya gari Mrajis Msaidizi wa Vyama Vya Ushirika Mkoa wa Kilimanjaro Henjewele John (Kushoto.

Waziri wa Kilimo Prof. Adolph Mkenda (Katikati) akikimkabidhi kompyuta mpakato (laptop)Mrajis Msaidizi wa Vyama Vya Ushirika Mkoa wa Njombe Bi.Consolata Kiluma (Kushoto).Prof. Mkenda amekabidhi laptop 20 pamoja na kompyuta za kawaida 50 zilizotolewa na Tume ya Maendeleo ya Ushirika leo 6.1.2021 jijini Dodoma.Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt.Benson Ndiege

Sehemu ya magari manne aina ya Nissan Hard N 300 Double Cabin 4WD yenye thamani ya Shilingi 275,091,670/- kwa pamoja yalikabidhiwa kwa Warajis Wasaidizi wa mkoa wa Simiyu, Kilimanjaro, Njombe na Dar es Salaaam na gari moja lililotumika kwa mkoa wa Kigoma.

 Na Alex Sonna, Dodoma 

SERIKALI imeahidi kuendelea kutatua changamoto ya vitendea kazi kwa watumishi Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini(TCDC) ili wafanye kazi kwa ufanisi na kurejesha hadhi na heshima ya ushirika nchini. 

Sambamba na hilo, imeapa kutofumbia macho mtu yeyote atakayebainika kuchezea fedha za ushirika. 

 

Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda hafla ya kukabidhi magari matano na komputa 70 kwa ajili ya kurahisisha utendaji kazi kwa watumishi wa Tume hiyo.

 Amesema anafahamu watumishi hao wanafanya kazi kwenye mazingira magumu hivyo serikali inapambana ili kuhakikisha wanaondoa kero zinazowakabili. 

Hata hivyo ameeleza bado kunahitajika mapambano ya wizi na ubadhirifu kwenye vyama vya ushirika licha ya kuonekana kupungua kutokana na jitihada zilizofanywa na serikali za kurudisha mali za ushirika. 

"Hatutachekeana na mtu anayecheza na mali za ushirika kwasababu ukifanya hivyo unakatisha watu tamaa, watakuwa hawana hamu ya kujiunga na ushirika, Warajis Wasaidizi tusimame kidete kwenye hilo,"amesema. 

 Pia amesema licha ya ubadhirifu kupungua lakini bado kuna tatizo la vyama kushindwa kuandaa vyema hesabu zake na kusababisha kukosa hati safi. 

Kuhusu Sheria, Waziri huyo amesema kuna kazi ya kurudisha imani za watu kwenye ushirika kwa kupitia upya Sheria ya Ushirika na tayari kazi imeshaanza. 

Awali  Mtendaji Mkuu wa Tume hiyo ambaye pia ni Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini, Dk.Benson Ndiege, amesema Tume itaendelea kupambana na kero zinazoukabili ushirika ikiwamo ubadhirifu na uongozi mbovu kwenye vyama hivyo.

 Aidha, Dk.Ndiege amesema Tume ipo kwenye mpango wa kuimarisha ofisi za ushirika nchini na itahakikisha kila mkoa una gari kabla ya mwaka wa fedha 2020/21 kukamilika.

 "Leo kwa kutumia mapato ya ndani Sh.Milioni 275 zimenunua magari manne ambayo yataenda kwa Warajis wa mikoa ya Dar es salaam, Simiyu, Kilimanjaro na Njombe na pia tutatoa gari moja kwenda Kigoma kutokana na umuhimu wa kilimo cha michikichi,"amesema.

 

Aidha amesema wamegawa komputa 70 ambapo kati ya hizo 20 ni komputa mpakato(laptops) ambapo komputa 50 zimetolewa na Benki ya CRDB na hizo zingine zimenunuliwa kwa mapato ya ndani.
Share:

WAFUGAJI WA NYUKI NA WAFANYABIASHARA WA MAZAO YA NYUKI NCHINI WATAKIWA KUJIUNGA NA VYAMA VYA USHIRIKA

MSUYA.JPG
Kamishna Msaidizi - Ufugaji Nyuki, Hussein Msuya akiwaeleza Mipambo mbalimbali ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania katika kuhakikisha wananufaika na fursa mbalimbali wanazozitoa kwa vikundi na kuwataka wajiunge ili waweze kuwa na sifa wakunufaika.


MWENYEKITI TABEDO.JPG

Rudia Issa ni Mwenyekiti wa  iliyokuwa TABEDO  akiwasisitizia wanachama wake umuhimu wa kujiunga na Chama vya ushirika vilivyopo na vile vitakavyoanzishwa.
WADAU.JPGWajumbe wa mkutano
WADAU2.JPGWajumbe wa mkutano
MJUMBE.JPGMjumbe wa mkutano
WAJUMBE.JPGWajumbe wa mkutano
MWENYEKITI NA NAIBU MWENYEKITI WA TABEDO.JPG

Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa TBEDO  Ayubu Kamwaga na  Mwenyekiti wake Rudia Issa ni wakicheka kwa Furaha baada ya kuthibitishiwa kuzaliwa uya kwa chama hicho kama chama cha ushirika baada ya kufutwa rasmi na Serikali kwa mujibu wa Sheria.


Wafugaji wa nyuki na wafanyabiashara wa mazao ya nyuki nchini wametakiwa kuimarisha na kujiunga na vyama vya msingi vya ushirika ili waweze kunufaika na huduma zitolewazo na vyama hivyo.
 
Wito huo umetolewa jana Januari 5,2021 na Kamishna Msaidizi - Ufugaji Nyuki, Hussein Msuya alipokuwa akifungua mkutano maalumu wa Jukwaa la Ufugaji Nyuki  nchini – TABEDO katika ukumbi wa Chuo cha Ushirika Moshi tawi la Dodoma.
 
Msuya alisema, baada ya Serikali kufuta kampuni  zenya ukomo wa ahadi na yasiyo na mtaji ambayo hayafanyi shughuli za kukuza biashara na ukwekezaji yaliyokiwa yamesajiliwa na msajili wa Makampuni (BRELA). TABEDO ikiwemo, imelazimika kukutana na wanachama wake kwa lengo la kujadili hatma yao na kuunda kamati itakayokwenda kufanya tathimini ya vyama vya msingi vya ushirika wa wafugaji nyuki nchini. 
 
“Hivi sasa hatuelewi “status” ya vyama vya msingi hivyo kamati hii itakayokwenda kuundwa leo itafanya tathimini kuona ni nini kinaendelea, tukishaelewa sasa tutaenda kuangalia ni nini hasa kilichopelekea vyama hivi kusinzia au kufa,
 
“na kwa kushirikiana na watu wa ushirika kamati itaangalia ni mambo gani itafanya kuhakikisha vyama hivi vinasimama na kushauri namna bora ya kuunda muunganiko utakakuwa mbadala wa TABEDO na kuja na mfumo mwingine wa kuunganisha vyama vya mushirika vya  msingi” anasema Kamishna Msaidizi huyo.
 
Msuya alitoa wito kwa wananchama kutoa ushirikiano kwa kamati itakayoundwa ili kujitendea haki kwa kile alichokisema “unakata mti unapanda mti sio unaenda kulala”. 
Azima  ya kukuza viwanda haitatimia ikiwa hakutakuwa na ushirika wa wafugaji nyuki ulio imara, ushirika  wa wafugaji nyuki utawezesha kuapta nguvu ya kukuza mitaji na kuongeza uzalishaji wa mazao ya nyuki, ambayo ni malighafi ya viwanda vya mazao ya nyuki.
 
Rudia Issa ni Mwenyekiti wa  iliyokuwa TABEDO anasema wako tayari kushirikiana na kamati itakayoundwa ili kuweza kuunda vyama vya ushirika vitakavyokwenda kutoa ufumbuzi wa mahitaji ya wafugaji nyuki nchini.
 
Alisema kila mfugaji nyuki akitambua umuhimu wa kuwa mwanachama wa ushirika, atanufaika na mafao mbalimbali ikiwamo kupatiwa mikopo kutoka katika taasisi za fedha pamoja na soko la uhakika la mazao yake.
 
Lemiona Kimeshua ni mfugaji nyuki na mwananchama wa TABEDO anasema aliacha shughuli za ufugaji nyuki na kubaki kuwa mnunuzi kutokana na kulegalega kwa vyama vya ushirika lakini kutokana na mkazo mkubwa wa Serikali kwenye sekta hiyo ameamua kufufua na kuanzisha mashamba mapya ya nyuki.
 
 
Tulizo Kilaga
Corporate Communication Specialist
Tanzania Forest Service Agency (T F S), 
P.O. Box 40832, 
Mpingo House, Nyerere Road,
Dar es Salaam, Tanzania. 
Mobile phone: +255715/ 623 888887
Office: +255 23 2604387
Share:

THIS IS SIMBA BWANAA!!! YAITANDIKA PLATNUMS YA ZIMBABWE 4G


Na Shishira Mnzava, DAR ES SALAAM
MABINGWA wa Tanzania, Simba SC wamefanikiwa kwenda hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa 4-0 dhidi ya FC Platinums ya Zimbabwe leo Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Simba SC inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 4-1 kufuatia kufungwa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza Jumatano iliyopita mjini Harare.

Hii inakuwa mara ya tatu kwa Wekundu hao wa Msimbazi kutinga hatua ya makundi baada ya mwaka 2003 walipoitoa Zamalek ya Misri waliokuwa mabingwa watetezi na 2018 walipoitoa Nkana FC ya Zambia.
Simba SC inayofundishwa na Mbelgiji, Sven Ludwig Vandenbroeck ilikwenda kupumzika ikiwa inaongoza kwa bao 1-0 lililofungwa na Erasto Edward Nyoni kwa penalti dakika ya 39 baada ya beki mwenzake, Shomari Salum Kapombe kuvutwa jezi na Tawana Chikore.

Kipindi cha pili Kapombe akaifungia Simba SC bao la pili dakika ya 61 akimalizia mpira uliotemwa na kipa Francis Tizayi kufuatia shuti la kiungo Mzambia Rally Bwalya.

Nahodha John Raphael Bocco aliyetokea benchi kipindi cha pili kuchukua nafasi ya mshambuliaji mwenzake, Mnyarwanda Meddie Kagere akaifungia Simba SC bao la tatu dakika ya 90 na ushei akimalizia pasi ya Bwalya tena.

Mzambia mwingine, Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Tanzania, kiungo Clatous Chotta Chama akaifungia Simba SC bao la nne kwa penalti dakika ya 90 na ushei baada yay eye mwenyewe kuvutwa kwenye boksi na Gift Bello.

Kagere aliingia dakika ya 76 kuchukua nafasi ya mshambuliaji mwingine, Mkongo Chris Mutshimba Kope Mugalu lakini akaumia dakika ya 85 na nafasi yake ikachukuliwa Bocco.

Baada ya msimu mbaya uliopita timu za Tanzania, Simba na Azam FC zikitolewa mapema michuano ya Afrika – hatimaye mwaka huu mambo mazuri, kwani na Namungo FC imetinga kwneye mchujo wa kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho. 

Namungo FC imefanikiwa kusonga mbele kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika baada ya sare ya 3-3 na wenyeji, na Al Hilal Obayed jana Uwanja wa Al-Hilal mjini Omdurman, Sudan.

Kwa matokeo hayo Namungo FC inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 5-3 na sasa itamenyana na moja ya timu zitakazotolewa kwenye Ligi ya Mabingwa kuwania kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho.

Droo ya hatua ya makundi ya michuano hiyo itafanyika Ijumaa Saa 8:00 mchana makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) mjini Cairo, Misri.

Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Joash Onyango, Pascal Wawa, Erasto Nyoni, Rally Bwalya, Said Ndemla/Ibrahim Ame dk60, Chris Mugalu/Meddie Kagere dk76/John Bocco dk85, Clatous Chama na Luis Miquissone.FC Platinums; Francis Tizayi, Gift Mbweti, Nomore Chinyerere, Gift Bello, Ralph Kawondera, Donald Dzvinyai, Kelvin Madzongwe, Rahman Kutsanzira, Khumalo Denzel/Raphael Muduviwa dk58, Perfect Chikwende na Tawana Chikore.

CHANZO - BINZUBEIRY BLOG

Share:

WATAALAM SEKTA YA MAJI WATAKIWA KUTUMIA TAALUMA ZAO VIZURI

 

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akikagua tenki la maji mradi wa Gamasara Wilayani Tarime Mkoani Mara.

Na Mohamed Saif, Tarime

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amewataka wataalam Sekta ya Maji kote nchini kutumia utaalam wao ili wananchi wapate huduma ya uhakika na toshelevu ya majisafi na salama

Ametoa maelekezo hayo Januari 5, 2021 wakati wa ziara yake ya kukagua mradi wa maji wa Gamasara Wilayani Tarime Mkoani Mara na kuzungumza na wanufaika wa mradi huo ambao kwa nyakati tofauti walimueleza changamoto zilizopo kwenye mradi.

Miongoni mwa changamoto zilizoelezwa na wananchi hao ni pamoja na mradi kushindwa kutoa maji inavyopasa kwani kuna wakati mabomba hua hayatoi maji.

Mara baada ya kujionea hali halisi ya mradi na maelezo ya wananchi wa maeneo husika, Waziri Aweso alisisitiza kuwa dhamira ya Serikali ya Rais. Dkt. John Pombe Magufuli ni kuwafikishia huduma ya maji wananchi wake na kwamba hatokubali kuwa kikwazo cha kufikiwa kwa dhamira hiyo na hivyo aliwataka wataalm wote kwenye Sekta ya Maji kujitathmini.

Waziri Aweso aliielekeza Wakala wa Majisafi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Mara kuhakikisha maboresho yanafanyika ili mradi uweze kutoa maji kama inavyopasa kwa lengo la kuhudumia wananchi wengi zaidi.

Alisema kuwa wananchi wanachohitaji ni maji na aliwaelekeza wataalam katika Sekta ya Maji kujiepusha na porojo badala yake wahakikishe wanajikita na kudumu kwenye falsafa ya maji bombani.

“Wataalam wetu kwenye Sekta ya Maji acheni porojo, elekezeni taaluma zenu na ubunifu katika kuhakikisha wananchi wanaondokana na kero ya maji,” alielekeza Waziri Aweso.

Aliongeza “unapokuwa mtaalam lazima utoe ushauri kulingana na utaalamu wako, tunapoanzisha mradi maana yake ni wananchi wapate huduma, wataalam tutumie taaluma zetu kusaidia wananchi wapate maji,” alielekeza Waziri Aweso

Aidha, Waziri Aweso alizielekeza Jumuia za Watumia Maji kote nchini kuhakikisha zinasimamia vizuri miradi ya maji kwenye jumuia zao ikiwa ni pamoja na kuongeza umakini kwenye makusanyo kwa lengo la kuwa na miradi endelevu.

“Miradi mliyokabidhiwa inapaswa kuwa endelevu, sasa ni jukumu lenu kuhakikisha hili linafikiwa, hakikisheni mnashirikiana, mnaitunza na mnisimamia vizuri,” alielekeza Waziri Aweso.

 

Share:

SHIRIKA LA RAFIKI SDO LACHANGIA MIFUKO YA SARUJI UJENZI WA MADARASA MAZINGE SEKONDARI

Kulia ni Meneja Miradi wa Shirika la Rafiki SDO, Dk. Nyamkongi Lucas akimkabidhi mifuko ya saruji Afisa Mtendaji wa Kata ya Ndembezi, Timothy Timoth kwa ajili ujenzi wa madarasa ya shule ya Sekondari Mazinge iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga. 

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Shirika la Rafiki Social Development Organization (Rafiki SDO) limechangia mifuko 10 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mawili kwenye shule ya Sekondari Mazinge iliyopo katika Kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga. 

Meneja Miradi wa Shirika la Rafiki SDO, Dk. Nyamkongi Lucas amekabidhi mifuko hiyo yenye thamani ya shilingi 190,000/= leo Jumatano Januari 6,2021 kwa Afisa Mtendaji wa Kata ya Ndembezi, Timothy Timoth katika shule ya Sekondari Mazinge. 

Dk. Lucas amesema Shirika la Rafiki SDO limetoa msaada huo wa mifuko ya saruji kutokana na kwamba wao ni wadau wa maendeleo hivyo wameguswa ili kufanikisha zoezi la ujenzi wa madarasa kwa sababu linawahusu watu wote katika jamii. 

“Tunahitaji kujenga jamii yenye watu wasomi, hivyo hatuwezi kupata wasomi kama hatujawatengeneza sisi wenyewe. Ni sisi wanajamii tunahusika katika kujenga wasomi hawa hivyo kama sehemu ya jamii tumechangia mifuko 10 ya saruji yenye thamani ya shilingi 190,000/= kuongeza nguvu katika ujenzi wa madarasa”,amesema Dk. Lucas. 

“Tutazidi kushirikiana na serikali katika shughuli za maendeleo kwa sababu sisi jina letu ni Rafiki Social Development Organization kwa hiyo maendeleo ya jamii ni sehemu yetu. Tunapoona jamii inafanya maendeleo sisi kama wadau wakuu wa maendeleo tunawiwa zaidi kushirikiana nao”,ameongeza Dk. Lucas 

Akipokea mifuko hiyo ya saruji, Afisa Mtendaji wa kata ya Ndembezi Timothy Timoth amelishukuru Shirika la Rafiki SDO kwa mchango huo wa mifuko ya saruji akieleza kuwa itasaidia katika kumalizia ujenzi wa madarasa 

Aidha Timoth amewaomba wadau wengine wa maendeleo kujitokeza kwani jambo la ujenzi wa madarasa ni la watu wote katika jamii. 

Amesema shule ya Sekondari Mazinge ina uhitaji wa madarasa manne hivi sasa wanaendelea na ujenzi wa madarasa mawili unaotarajiwa kukamilika Januari 10,2021 huku akibainisha kuwa jumla ya wanafunzi 230 kuanza masomo ya kidato cha kwanza tofauti na mwaka 2020 ambapo wanafunzi walikuwa 196. 
Kulia ni Meneja Miradi wa Shirika la Rafiki SDO, Dk. Nyamkongi Lucas akimkabidhi mifuko ya saruji Afisa Mtendaji wa Kata ya Ndembezi, Timothy Timoth kwa ajili ujenzi wa madarasa ya shule ya Sekondari Mazinge iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga leo Jumatano Januari 6,2021. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog 
Kulia ni Meneja Miradi wa Shirika la Rafiki SDO, Dk. Nyamkongi Lucas akimkabidhi mifuko ya saruji Afisa Mtendaji wa Kata ya Ndembezi, Timothy Timoth kwa ajili ujenzi wa madarasa ya shule ya Sekondari Mazinge iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga.
Mifuko ya saruji iliyotolewa na Shirika la Rafiki SDO kwa ajili ujenzi wa madarasa ya shule ya Sekondari Mazinge iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga.
Kulia ni Meneja Miradi wa Shirika la Rafiki SDO, Dk. Nyamkongi Lucas akizungumza wakati akikabidhi mifuko ya saruji kwa ajili ujenzi wa madarasa ya shule ya Sekondari Mazinge iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga.
Kushoto ni  Afisa Mtendaji wa Kata ya Ndembezi, Timothy Timoth akilishukuru Shirika la Rafiki SDO kwa kuchangia mifuko ya saruji kwa ajili ujenzi wa madarasa ya shule ya Sekondari Mazinge.
Wadau wa maendeleo wakiwa katika eneo la ujenzi wa madarasa ya shule ya Sekondari Mazinge iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga. 
Wadau wa maendeleo wakiwa katika eneo la ujenzi wa madarasa ya shule ya Sekondari Mazinge iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Share:

Walimu Wakuu shule za msingi watakiwa kusimamia fedha zinazotolewa na Serikali


Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi Joseph Nyamhanga amewataka walimu wakuu wa shule za msingi nchini kuhakikisha wanasimamia fedha zinazotolewa na Serikali  kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya elimu  kwa kufuata sheria na taratibu katika matumizi.

Akifungua mkutano mkuu wa pili wa umoja wa walimu wakuu wa shule za msingi Tanzania Bara jana , Jijini Dodoma Mhandisi Nyamhanga amesema serikali inapeleka fedha  za ruzuku mashuleni kwa kila mwezi ili ziweze kununua vifaa vya kufundishia, kujifunzia hivyo ni jukumu la  walimu  kusimamia kwa umakini na kuhakikisha wanafunzi hao wanapata elimu bora.

Mhandisi Nyamhanga anafafanua kuwa Serikali inafanya kila linalowezekana kuhakikisha elimu ya msingi hapa nchini inakuwa bora kwa kuboresha miundombinu ya elimu, hivyo ni wajibu wa Wakuu wa Shule za Msingi kuhakikisha fedha hizo zinasimamiwa kikamilifu.

“Serikali iko makini kuhakikisha suala la elimu linakuwa mbele zaidi kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya maboresho ya miundombinu katika ujenzi wa vyoo,nyumba za walimu na mabweni ni kazi yenu kuhakikisha fedha hizo zinasimamiwa ili ziweze kutumika katika miradi iliyokusudiwa ,”amefafanua Mhandisi Nyamhanga

Mhandisi Nyamhanga amesema Serikali imeweka mikakati ya kuimarisha elimu ya msingi na kusisitiza kuwa fedha za programu ya elimu bila malipo zitatumika kufidia malipo ya ada,posho kwa walimu wakuu pamoja na huduma nyingine za msingi.

Aidha, Nyamhanga ametumia fursa hiyo kuweka wazi kuwa Serikali inalaani vitendo vya udanganyifu wa mitihani na kuwataka walimu wakuu nchini kuendelea kudhibiti vitendo hivyo ili kuboresha elimu ya msingi.

“ Ni jambo la kusikitisha kuona katika ulimwengu huu bado walimu hamuwezi kudhibidi wizi wa mitihani,tunawakatisha tama wanafunzi wanaojituma,”amesema Mhandisi Nyamhanga.

Mhandisi Nyamhanga amesema vitendo vya udanganyifu wa mitihani bado ni tatizo ambalo lipo linatia doa  doa  kubwa kwani kwa kipindi cha mwaka jana pekee jumla ya wanafunzi 1065 walifutiwa matokeo ya mitihani kwa udanganyifu na kuwataka walimu hao wakuu kuangalia namna ya kudhibiti na kwamba hatua za kinidhamu zitachukuliwa kwa watakaovujisha .

Wakati huo, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais –TAMISEMI anayeshughulikia Elimu Gerald Mweli ametoa rai kwa umoja huo kujituma katika kutoa elimu bora kwa jamii ili kuzalisha wataalamu watakaotosha nchini.

Naye Rehema Ramole Mwenyekiti wa umoja wa walimu wakuu wa shule za msingi Tanzania Bara ameishukuru serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kulipa walimu mishahara yao kipindi chote shule zilipofungwa kutokana na ugonjwa wa Corana.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger