Tuesday, 3 November 2020
Mbowe na wenzake waachiwa kwa dhamana
Wengine walioachiwa ni wajumbe wa kamati kuu ya Chadema, Godbless Lema na Boniface Jacob ambao pamoja na Mbowe walikamatwa na polisi usiku wa kuamkia Novemba 2, 2020 wakiwa kwenye kikao. Zitto alikamatwa leo mchana alipokwenda kuwatembelea kina Mbowe polisi.
Wakili wa Chadema John Mallya amesema viongozi hao wameachiwa kwa dhamana na kutakiwa kuripoti polisi Novemba 5, 2020 saa 3 asubuhi.
Mallya amesema viongozi hao wameachiwa baada ya kujidhamini wenyewe na kutakiwa kutotoka nje ya mkoa wa Dar es Salaam na kuhakikisha wanaripoti kituoni hapo tarehe waliyopangiwa
JAMAA AIBA MBUZI WA WAZAZI WA MREMBO ALIYEKULA 'NAULI' YAKE BILA KWENDA 'AJILIPE FIDIA'
Mambo 15 Yanayoongelewa Kuhusu Ubora wa Simu ya TECNO Spark 5Pro
TECNO Spark 5 pro ilizinduliwa rasmi tarehe 18/10/2020 ambapo ilikutanisha wadau wa simu za TECNO na wasanii mbalimbali akiwemo mchekeshaji maarufu Eric Mondi na DJ Maphorissa kutoka South Africa.
Tangu kuzinduliwa kwa simu hiyo imekuwa ni neema kwa watumiaji wa simu za Spark. TECNO Spark 5pro imeonekana kukonga mioyo ya watu wengi hasa kutoka na uwezo wake wakuifadhi files nyingi pasipo uhitaji wa memory ya ziada.
Spark 5pro inaukubwa wa memory ya GB 64ROM + GB 3RAM. Sifa nyengine za TECNO Spark 5pro ni uhimili wake wa kudumu na chaji kwa muda mrefu kutokana na battery yake kuwa na ujazo wa mAh 5000.
Kwa wapenzi wa picha kali Spark 5pro ni suluhisho kwetu, Spark 5pro imekuja na selfie ya megapixel 8 na nyuma in megapixel 16M+2M+2M+AI Lens za kamera.
“Spark 5pro ni mkombozi kwetu sisi wanafunzi simu hii inamambo mengi mazuri sana napenda kasi yake ya kimtandao wa 4G, kasi ya processor 1.8 octa-core na mfumo wa uendeshaji wa Android 10” alisema mwanafunzi wa chuo cha IFM Bwana Frank Peter.
Baada ya huu uchunguzi inaonyesha kampuni ya simu TECNO imefaulu kwa hasilimia 100 kwenye toleo hili la Spark 5pro.
Ili kufurahiya huduma za TECNO Spark 5pro tafadhali usiache kuwatembelea katika maduka yao ya TECNO Smart Hub Kariakoo na Mlimani City lakini pia tembelea link https://bit.ly/2Hftrh6 hii kufahamu mengi mazuri kutoka TECNO.
Dk Tulia Ackson Achukua Fomu ya Kuwania Unaibu Spika wa Bunge
Mbunge mteule wa Mbeya Mjini (CCM), Dk Tulia Ackson amesema hajachukua fomu ya kuwania uspika wa Bunge la 12 ili apate nafasi ya kuwatumia wananchi waliomchagua.
Badala yake, Dk Tulia ambaye katika Bunge la 11 alikuwa naibu spika, amechukua fomu kuwania tena nafasi hiyo.
Dk Tulia ameeleza hayo leo Jumanne Novemba 3, 2020 mjini Dodoma baada ya kuchukua fomu katika ofisi za CCM makao makuu.
BOBI WINE AKAMATWA PUNDE TU BAADA YA KUTEULIWA KUGOMBEA URAIS UGANDA
KIJANA ABUNI KOFIA MAALUM KWA AJILI YA MBWA
JOB NDUGAI ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA USPIKA WA BUNGE
Spika wa Bunge anayemaliza muda wake, Job Ndugai amechukua fomu kwa ajili ya kutetea nafasi hiyo kwa kipindi cha pili.
Ndugai ambaye amekuwa katika nafasi hiyo katika Bunge la kumi na moja amechukua fomu ya kugombea nafasi hiyo na kuirejesha leo katika ofisi makao makuu ya CCM jijini hapa.
Akizungumza baada ya kurejesha fomu kwa Katibu msaidizi idara ya oganaizesheni CCM Taifa, Solomon Itunda, Ndugai amewaomba Watanzania wamuombee ili chama kimteue katika nafasi hiyo.
"Ni utaratibu wa chama chetu wa kidemokrasia kuruhusu wanachama wenye sifa kugombea nafasi ya Spika na Naibu Spika kisha kufanya uteuzi. Niwaombe Watanzania waniombee ili niteuliwe na niwaambie kuwa wakati ukifika tutaongea nao," amesema Ndugai.
ZITTO KABWE, HALIMA MDEE WATAKIWA KUJISALIMISHA POLISI
Jeshi la Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam, limetangaza kuwasaka wanasiasa Halima Mdee na Zitto Kabwe, huku likiwataka wajisalimishe ili wajibu tuhuma zinazowakabili.
Taarifa iliyotolewa leo Jumanne Novemba 3 na Kamanda wa kanda hiyo, Lazaro Mambosasa imeeleza wanaendelea na opareshini ya kuwakamata watu wanaofanya mipango kuhamasisha maandamano nchini.
Mambosasa ameeleza kuwa hadi sasa jeshi hilo linawashikilia watu 14 wakiwemo viongozi wa Chadema ambao ni Freeman Mbowe, Godbless Leman a Boniface Jacob.
Kamanda huyo ameeleza kuwa hali ya jiji la Dar es Salaam imeendelea kuwa shwari, huku akiwataka wanasiasa kuacha kufanya fujo na badala yake kufuate sheria.
Mbunge wa mteule wa CHADEMA asema hatowasaliti wananchi waliomchagua
Aida Khenan, Mbunge Mteule wa Nkasi Kaskazini kupitia CHADEMA amesema, hatowasaliti wananchi waliomchagua hivyo atakwenda Bunge kuapishwa ili aweze kuwatumikia.
Aida ni Mgombea pekee wa Ubunge kupitia CHADEMA aliyetangazwa mshindi katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28, akimshinda Ally Kessy wa CCM aliyekuwa anatetea jimbo hilo aliloongoza kwa miaka 10.
Kauli hiyo imekuja baada CHADEMA na ACT-Wazalendo kutangaza kutoyatambua matokeo ya Uchaguzi yaliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) hata kwenye maeneo waliyoshinda.
Katika Bunge lililopita, Aida alikuwa Mbunge wa Viti Maalum. Lakini sasa amesema yeye ni Mbunge ambaye anasubiri kuapishwa.
Kesi ya Mr.Kuku yaendelea kupigwa Kalenda
Kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili mfanyabiashara maarufu, Tariq Machibya(29) maarufu Mr. Kuku, imeahirishwa hadi Novemba 16, mwaka huu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kutokana na upelelezi kutokamilika.
Wakili wa serikali Mwandamizi, Wankyo Simon, ameileza Mahakama kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamailika.
Katika hati ya mashtaka mshtakiwa anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 60/2020, miongoni mwa mashtaka hayo yapo ya kusimamia na kuendesha biashara ya haramu ya upatu, kupokea maingizo ya fedha kutoka kwa umma bila kuwa na leseni na kutakatisha fedha.
Inadaiwa kuwa kati ya Januari 2018 na Mei 2020, katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam, mshtakiwa anadaiwa kusimamia biashara ya upatu.
Pia Machibya anadaiwa alijihusisha na biashara ya upatu kwa kukubali na kukusanya fedha kutoka kwa umma, akijifanya kwamba watafanya ujasiriamali wa ufugaji wa kuku na wangepata faida ya asilimia 70 ya mtaji wa awali waliowekeza kwa miezi minne na asilimia 90 ya mtaji wa awali waliowekeza kwa kipindi cha miezi sita, kiasi ambacho ni kikubwa katika biashara kuliko mtaji uliokusanywa.
Inadaiwa kati ya April 26, 2019 na Januari 26, 2020 maeneo ya Jiji la Dar es Salaam, alijihusisha na miamala ya Shilingi bilioni 6.4 kwa kutoa fedha hizo kutoka katika akaunti inayosomeka kwa jina la Mr Kuku Farmers Ltd, iliyopo katika benki ya CRDB, wakati akijua kuwa fedha hizo ni zao tangulizi la biashara haramu ya upatu.
Pia anadaiwa kupokea fedha za maingizo ya umma kiasi cha Shilingi bilioni 17 bila kuwa na leseni.
WAKULIMA WA KILIMO CHA UMWAGILIAJI NCHINI WAPEWA WITO
Mhandisi John Chacha Nyamuhanga, mratibu ufundi katika mradi wa Regrow, akizungumza kuhusiana na utekelezaji wa mradi huo katika kilimo cha umwagiliaji. |
Kaimu Mkurugenzi Mkuu kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Daudi Kaali akitoa wito kwa wakulima w akilimo cha umwagiliaji kuhusiana na tozo na utunzaji wa miundombinu ya kilimo hicho. |
NA MWANDISHI WETU - DODOMA
Wakulima wakilimo cha umwagiliaji nchini wamepewa wito wakuchangia tozo za umwagiliaji katika skimu za kilimo cha umwagiliaji katika ukanda wa nyanda za juu kusini ili kuweza kuimarisha miundombinu ya kilimo hicho kwakufanyia maboresho ya miundombinu hiyo inapotokea kuharibiwa na dharura kama mafuriko yatokanayo na mvua kubwa.
Hayo yamelezwa mapema leo mjini Dodoma na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagliaji Bw. Daudi Kaali ambapo akitolea mfano wa skimu za kilimo cha umwagiliaji zilizoko katika ukanda wa nyanda za juu kusini hususani katika mkoa Mbeya, ambako ni kati ya sehemu ambapo mradi wa REGROW unatekelezwa.
Bw.Kaali alisema kuwa,miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji itakapotunzwa vizuri na kuwaendelevu kutakuwa na ufanisi wa matumizi ya maji yatakayoleta matokeo makubwa katika upatikanaji wa maji katika mto Ruaha mkuu hasa wakati wa kiangazi.
Kwa upande wake Mhandisi John Chacha Nyamuhanga, Mratibu wa kiufundi wa mradi wa Regrow kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji alisema kuwa,kupitia mradi huo Tume ya taifa ya Umwagiliaji inajukumu la kuimarisha miundombinu ya umwagiliaji kwa kujenga mabanio, mifereji mikuu na midogo,nakuhakikisha kuna ufanisi mkubwa wa matumizi ya maji katika shughuli za Umwagiliaji.
Akizungumzia kuwepo kwa mfuko wa Maendeleo ya kilimo cha umwagiliaji, Afisa Mwandamizi kutoka katika Idara ya Uendeshaji na mafunzo Bw. Clavery Makoti, alisema kuwa,Sekta yakilimo cha umwagilaji ilikuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo za uchakavu na uharibifu wa miondombinu ya umwagiliaji hivyo kupitia sheria ya umwagiliaji serikali ikaona kila sababu yakuanzisha mfuko huo ilikuweza kukabiliana na changamoto zilizopo katika sekta hivyo.
“Mfuko huo ulioanzishwa mwezi September mwaka huu mpaka sasa umewezakurekebisha skimu ya Ruaha Mbuyuni, na Pawaga na kiasi cha fedha shilingi milioni 410 zimetengwa kutumika kuboresha miondombinu ya Iringa na kilolo.” Alisema.
Awali, Mkurugenzi msaidizi idara ya uendeshaji kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw.Enterbert Nyoni alisema,idara yake inajukumu la uendeshaji wa mafunzo katika skimu za umwagiliaji ili skimu hizo ziweze kuimarika na kuleta tija ,idara huwafundisha wakulima mambo mbalimbali yakiwemo yanayohusu sheria ndogondogo za umwagiliaji matumizi sahihi ya fedha na matumizi bora ya maji kupitia kalenda.
Aliongeza kw akusema kuwa, mapokeo na muitikio wa mafunzo kwa wakulima ni chanya na kwani mpaka sasa wameshaanza kuona faida yakuwepo kwa mfuko wa maendeleo ya umwagiliaji.
Mradi huo wa Regrow unaotekelezwa na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Maliasili na utalii kwa kushirikiana na taasisi zingine za serikali ikiwemo Tume ya Taifa ya Umwagiliaji na bodi ya maji bonde la Rufiji, unalenga kuongeza utalii kusini mwa Tanzania na kukuza shughuli mbaadala za kiuchumi katika jamii zinazozunguka eneo unakotekelzwa Mradi katika hifadhi za Taifa za Ruaha, Mikumi,Udzungwa na MwalimuNyerere.
Prof. Lipumba: CUF Hatutashiriki Tena Uchaguzi
Chama cha Wananchi (CUF), kimesema hakitashiriki tena katika Uchaguzi Mkuu mpaka itakapopatikana Tume Huru ya Uchaguzi
Pia, chama hicho kimesema hakikubaliani na matokeo yaliyotangazwa katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 28, mwaka huu.
Kwa mujibu wa CUF, uamuzi huo umetokana na Kamati ya Uongozi ya Baraza Kuu la Uongozi la Taifa na Kamati ya Utendaji ya Taifa ya chama hicho iliyofanya kikao cha pamoja cha dharura kutathmini mwenendo na matokeo ya uchaguzi huo, Novemba 2, mwaka huu.
Akitoa tamko hilo jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba, alisema kuanzia sasa kwa kushirikiana na wadau wengine, kitajikita katika kuwahamasisha Watanzania kupigania Katiba mpya.
Profesa Lipumba alisema chama hicho kimepanga kufanya maombi maalum siku ya Alhamisi wiki hii.
“Tunawaomba Watanzania wote wanaopenda haki nchini kote, kufanya ibada maalum siku ya Alhamisi, kwa kufunga kula mchana na kufanya dua na maombi baada ya kufungua, kila mtu kwa imani yake,” alisema Profesa Lipumba.
Atiwa Mbaroni Kwa Kumuua Mkewe na Shemeji Yake
Jeshi la Polisi mkoani Kagera linamshikilia mtuhumiwa Faraji Yunus (44), mkazi wa Kijiji cha Kikagati wilayani Muleba mkoani Kagera, kwa tuhumza za mauaji ya mkewe na shemeji kwa shoka.
Anadaiwa kuwaua mkewe, Nadia Coroneli (35) na shemeji yake, Shadia Yunusu (25), wakazi wa kijiji hicho.
Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, Revocatus Malimi, alisema kuwa Oktoba 29, mwaka huu majira ya saa 12 jioni, mtuhumiwa akiwa Kijijini hapo alisababisha ugomvi uliosabanisha mauaji hayo.
Kamanda alisema, mtuhimiwa alipata taarifa kuwa mkewe alikuwa akifanya usaliti wa ndoa na kufikia hatua ya kutaka kwenda kuolewa sehemu nyingine, hivyo mtuhumiwa kuanza matukio ya kuzua ugomvi.
"Alipopata taarifa hizo alianza ugomvi na mkewe, ambao ulipelekea kumuua mkewe Nadia na Shadia Yusuph, mke wa mdogo wake Yusuf Yunusu kwa kutumia shoka," alisema Kamanda Malimi.
Aidha, alisema akiwa katika ugomvi huo, alifika mtu ambaye ntuhumiwa alikuwa akidai kuwa ana mahusiano na mkewe, na kutaka kuamulia ugomvi huo.
Kamanda alisema mtuhumiwa alimuua shemeji yake kutokana na kumtuhumu kuwa alikuwa anamtafutia mabwana mkewe, huku akijua kuwa ni mke wake wa ndoa.
Alisema baada ya tukio hilo, mtuhimiwa alijaribu kukimbia , lakini juhudi za Polisi wilayani Muleba ziliwezesha kukamatwa na kufikishwa kituoni.
Alisema, upelekezi wa tukio unaendelea ili kubaini sababu zaidi kabla ya kufikishwa mahakamani.
Marekani kuchagua rais mpya leo
Hadi jana Jumatatu, Biden alikuwa mbele ya Trump kwenye kura za maoni ya umma kuelekea uchaguzi wa leo unaofanyika chini ya kiwingu cha janga la virusi vya corona ambalo limewauwa mamia kwa maelfu ya watu nchini Marekani.
Trump, rais wa 45 wa Marekani anajivunia rikodi ya kuimarisha uchumi na kupunguza kwa kiwango kikubwa ukosefu wa ajira lakini anakosolewa kwa jinsi alivyoshughulikia janga la virusi vya corona.
Biden, mwanasiasa anayegemea sera za wastani za mrengo wa kushoto ameahidi kulinda haki ya wamarekani kupata huduma za afya, mafao kwa wazee na kutengeneza nafasi mpya za kazi kupitia sekta ya nishati .
Mchuano ni mkali na wasiwasi umetanda juu ya kuzuka mabishano baada ya uchaguzi huu, baada ya Rais Trump kutishia kujitangazia ushindi hata kabla ya matokeo kukamilika.
Credit: DW
Monday, 2 November 2020
VIONGOZI WA DINI SHINYANGA WATOA MSIMAMO KUHUSU MAANDAMANO YA KUKATAA MATOKEO YA UCHAGUZI
Na Suzy Luhende, Shinyanga
BAADHI ya Viongozi wa dini mkoani Shinyanga wametoa msimamo wao juu ya kinachoendelea nchini baada ya zoezi la upigaji kura kukamilika Oktoba 28, mwaka huu, huku baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa kutoka upinzani wakihamasisha Watanzania kuandamana kwa kile kinachotajwa kupinga matokeo ya uchaguzi huo yaliyompa ushindi Rais Dk. John Magufuli.
Wakizungumza na Shinyanga Press Club Blog kwa nyakati tofauti mjini Shinyanga, viongozi hao wamesisitiza amani na umoja katika kipindi hiki, huku wakieleza kwamba maandamano yanayoitishwa na vyama vya siasa siyo sahihi kwani ni kuchochea vurugu na kuwagawa Watanzania.
Mmoja wa viongozi hao, Askofu wa Kanisa la Evangelical Assembiles of God Tanzania (EAGT) Kanda ya Kagera, Geita, na Shinyanga, Raphael Machimu ambaye pia ni Katibu wa Kamati ya amani mkoa wa Shinyanga amesema, tamko lililotolewa na viongozi wa siasa la kuandamana sio sahihi wanatakiwa wafuate kanuni na sheria ya tume ya uchaguzi.
Askofu Machimu ambaye anachunga kanisa la EAGT lililoko Tambukareli manispaa ya Shinyanga ameyasema hayo Novemba 1, 2020 ofisini kwake, ambapo amesema utaratibu unaotaka kuchukuliwa sio sahihi kwa sababu hata kama wameona kuna mambo hayakuenda sawa yalitakiwa yafuatiliwe kisheria na kikatiba.
Amesema kuhamasisha watu watoke barabarani ni kitendo kibaya kinachoweza kusababisha vurugu ambayo haitakuwa na majibu, tume ya uchaguzi ambayo ina miongozo yake ambapo walitakiwa kwenda kusaidiwa huko.
"Watu wakitoka barabarani kuandamana wataumia hata watu wengine wasiohusika, mimi mwenyewe kama kiongozi naona utaratibu unaotaka kuchukuliwa sio sahihi kwa sababu hata kama wameona kuna mambo hayakuenda sawa yalitakiwa yafuatiliwe kisheria na kikatiba sio kuandamana "amesema Machimu.
Amesema tangu kuanza kwa mchakato wa uchaguzi yeye kama katibu wa amani pamoja na viongozi wenzake wamekuwa wakiomba ili Mungu ahusike kuwapa viongozi watakaoongoza vizuri na kufanya maendeleo katika kata, majimboni na ngazi ya Urais ikiwa ni pamoja na kudumisha amani.
"Katika vikao vyetu vyote tulikubaliana kuelimisha watu katika kudumisha amani kwa watu wote, na tumewaelimisha wachungaji mashehe wawaelimishe waumini wao ili kulinda amani ya Tanzania"amesema Machimu.
"Tunatakiwa tuliombee Taifa letu kwa ajili ya kudumisha amani na utulivu watu wasijiingize kwenye mkumbo wa mafarakano, sisi kazi yetu kanisa ni kuomba,yeyote atakayepita ni diwani wetu, ni mbunge wetu na ni Rais wetu awe mkristo awe muislamu"ameongeza.
Naye Askofu wa Kanisa la Philadelphia Miracle Temple lililopo Ndembezi Manispaa ya Shinyanga, Baraka Laizer aliwaomba waumini wake waendelee kuliombea Taifa na waendelee kuwa watulivu wasijiingize kwenye mikusanyiko isiyokuwa ya amani badala yake wadumishe amani na upendo.
"Namshukuru Mungu kwa sababu tumekutana tena tukiwa wazima, kama nilivyowaasa kwamba msijihusishe kwenye mambo ambayo yatasababisha vurugu badala yake tuwe watulivu, kweli mmekuwa watulivu na sasa tuendelee kutulia katika nyakati hizi tusijichanganye tukajiingiza kwenye makundi ya kuvuruga amani tuendelee kuomba ili amani yetu iendelee kuwepo"amesema Laizer.
CHANZO - SHINYANGA PRESS CLUB BLOG