Monday, 20 July 2020

Picha : MGOMBEA URAIS CCM ZANZIBAR DK MWINYI APATA MAPOKEZI MAKUBWA PEMBA, ASISITIZA KUIENZI AMANI NA MAPINDUZI



Mgombea urais wa Zanzibar kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi (kwenye gari mbele) akiwapungia mkono wananchi na wana-CCM waliojitokeza katika mapokezi njiani mara baada ya kumpokea Uwanja wa Ndege wa Karume, Mkoa wa Kusini Pemba.
Mgombea urais wa Zanzibar kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi (kwenye gari mbele) akiwapungia mkono wananchi na wana-CCM waliojitokeza katika mapokezi njiani mara baada ya kumpokea Uwanja wa Ndege wa Karume, Mkoa wa Kusini Pemba. PICHA ZOTE NA MWINYI 2020. 
Mgombea urais wa Zanzibar kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi akishuka kwenye ndege kwenye Uwanja wa Ndege wa Karume, Mkoa wa Kusini Pemba. 
Mgombea urais wa Zanzibar kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi (kushoto) akifishwa taji la uwa mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Karume, Mkoa wa Kusini Pemba. 
Mgombea urais wa Zanzibar kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi pamoja na mkewe wakishuhudia burudani mbalimbali mara baada ya kumpokea Uwanja wa Ndege wa Karume, Mkoa wa Kusini Pemba. 
Mgombea urais wa Zanzibar kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na wageni mbalimbali mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Karume, Mkoa wa Kusini Pemba. 
Mgombea urais wa Zanzibar kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi pamoja na mkewe wakishuhudia burudani mbalimbali mara baada ya kumpokea Uwanja wa Ndege wa Karume, Mkoa wa Kusini Pemba. 
Mgombea urais wa Zanzibar kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi pamoja na mkewe wakishuhudia burudani mbalimbali mara baada ya kumpokea Uwanja wa Ndege wa Karume, Mkoa wa Kusini Pemba. 
Mgombea urais wa Zanzibar kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi pamoja na mkewe wakishuhudia burudani mbalimbali mara baada ya kumpokea Uwanja wa Ndege wa Karume, Mkoa wa Kusini Pemba. 
Mgombea urais wa Zanzibar kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi akiwapungia mkono wageni na wanaCCM mara baada ya kumlaki kwenye Uwanja wa Ndege wa Karume, Mkoa wa Kusini Pemba. 
Msafara wa mgombea nafasi ya urais wa Zanzibar kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi mara baada ya mapokezi yake katika Uwanja wa Ndege wa Karume, Mkoa wa Kusini Pemba. 
Mgombea urais wa Zanzibar kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi (kwenye gari) akiwapungia mkono wananchi na wana-CCM waliojitokeza njiani katika mapokezi yake.
Mgombea urais wa Zanzibar kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi (kwenye gari mbele) akiwapungia mkono wananchi na wana-CCM waliojitokeza katika mapokezi njiani. 
Msafara wa mgombea nafanafasi ya urais wa Zanzibar kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi mara baada ya mapokezi yake katika Uwanja wa Ndege wa Karume, Mkoa wa Kusini Pemba. 
Umati wa Wana-CCM pamoja na Wananchi wengine wakimsindikiza mgombea nafanafasi ya urais wa Zanzibar kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi mara baada ya kumpokea Uwanja wa Ndege wa Karume, Mkoa wa Kusini Pemba. 

Mgombea urais wa Zanzibar kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi (kwenye gari ) akionesha ishara ya kuwashukiuru wananchi waliojitokeza njiani kumpokea. 
Wananchi na wanaCCM wakiambatana na mgombea nafasi ya urais wa Zanzibar kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi mara baada ya kumpokea Uwanja wa Ndege wa Karume, Mkoa wa Kusini Pemba. PICHA ZOTE NA MWINYI 2020. 

Na Mwandishi Wetu, Pemba

MGOMBEA nafasi ya urais wa Zanzibar kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi amepata mapokezi makubwa alipowasili Kisiwani Pemba kwa ajili ya kutoa shukrani kwa kuaminiwa.

Mapokezi makubwa ya mgombea huyo yalianzia katika Uwanja wa Ndege wa Karume, Mkoa wa Kusini Pemba na kupita Barabara Kuu kuelekea Viwanja vya Tibirinzi akiwa katika gari la wazi, huku akisindikizwa na umati wa watu wenye sare za CCM na wengine wakimpungia mikono kando ya barabara.

Katika viwanja vya Tibirinzi, Chakechake, Kusini Pemba, vilifurika watu hadi mamia ya wananchi wakijikuta wamekosa nafasi ndani ya uwanja huo na kubaki nje ya viwanja hivyo wakiendeleza shamrashamra za mapokezi.

Akizungumza na wananchi, Dk. Hussein Mwinyi alianza kwa kukishukuru chama chake kwa kumaliza uteuzi kwa haki jambo ambalo limefanya waliokuwa wakiomba ridhaa pamoja naye sasa kuungana na kuwa kitu kimoja kuhakikisha CCM inashinda na kuchukua dola.

"...Nashukuru chama kwa kumaliza uteuzi wake kwa kwa haki, na sasa sote tumekua wamoja, hakuna timu Mwinyi wala timu Mbarawa, na lengo letu sasa ni moja kushika dola," alisema.

Dk. Hussein Mwinyi aliwahakikishia wananchi kuwa akifanikiwa kushinda atahakikisha anaenzi Mapinduzi matukufu ya Zanzibar ya Mwaka 1964, pamoja na kudumisha Muungano.

Alisema suala kubwa akifanikiwa kuingia Ikulu ya Zanzibar ni kudumisha amani ili kuchochea maendeleo. Nchi nyingi za jirani hakuna amani jambo ambalo linakwamiasha suala la maendeleo.

"...Namshukuru sana Mheshimiwa Rais Dk. Ali Mohamed Shein kwa kuongoza nchi kwa amani. Jukumu langu ni kuhakikisha amani inadumu. Lazima tudumishe umoja wetu. Kusiwe na Upemba na Uunguja, kusiwe na ukusini na Ukaskazini. Sote ni Wazanzibari," alisema Dk. Mwinyi.

Aidha aliongeza kuwa akiingia madarakani suala la ajira atahakikisha analishughulikia hasa kwa vijana, huku akimpongeza Rais Dk. Shein na viongozi wote wa Serikali na chama wanaomaliza muda wao kwa kufanya vizuri, jambo ambalo linamfanya aendeleze walipoishia.

"Nitaendeleza miundombinu, huduma za jamii, ustawi wa watu, maendeleo ya jamii, afya, elimu, na yote yanayogusa watu. Nitahakikisha Mzazibari anakua na maisha bora. Ukitaka kuyafanya hayo, lazima uwajibike. Huwezi kuwa na program kukawa na wala rushwa, wabadhirifu, Wazembe," alisema mgombea huyo.

Alibainisha kuwa Serikali yake itafanya kazi kwa maslahi ya Wazanzibari wote bila ubaguzi. Aliwatoa hofu wanaosema yeye ni mpole katika utendaji, kwamba hiyo si kweli bali ni kutokana na nafasi yake ya Waziri wa Wizara ya Ulinzi sehemu ambayo mambo mengi ni ya siri kiutendaji.

"...Nasema haya kwa sababu pengine hamjanisikia nikiongea sana kwenye vyombo vya habari. Sababu kubwa ni kwamba Wizara ya Ulinzi huko mambo yetu ni ya siri hatufanyi hadharani. Siwezi kusema ila kwa wale wabadhirifu, wala rushwa, wazembe, wasiowajibika, hao watawajibika," alisisitiza Dk. Mwinyi.

Aliahidi kusimamia maslahi ya Zanzibar kwenye Muungano, Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya za Kimataifa. Dhamira yake ni moja tu ya kuwatumikia Wazanzibari wote bila kubagua endapo atafanikiwa kushinda.

"Mwaka huu, tunataka tupate ushindi wa kishindo usiwe mwembemba tukapata malalamiko. Na niliyoyaona Unguja na hapa Pemba kwa sasa sina shaka ushindi ni mkubwa. Sina shaka ushindi utakua ni mkubwa. Nasema tena kwamba ‘Yajayo yanafurahisha.’ Ni ahadi naichukua mbele ya Mungu na mbele yenu. Nitahakikisha nawahudumia wananchi."
Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu July 20



















Share:

Sunday, 19 July 2020

WANAWAKE 12 WARUDISHA FOMU KUGOMBEA UBUNGE VITI MAALUMU,UDIWANI 63 TARIME

MgombeaUbunge viti maalumu Suzana Senso kupitia CCM akirudisha fomu kwa Katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Tarime Sauda Kashombo (kulia)

Na Dinna Maningo - Malunde1 blog Tarime
Wanawake kumi na mbili kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Tarime wamechukua na kurudisha fomu za kuomba kugombea nafasi za Ubunge  uwakilishi na viti maalumu na kwa Udiwani viti maalumu wakiwa 63.


Akizungumza na Malunde 1 blog, Katibu wa Umoja wa wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Tarime Sauda Kashombo aliwataja wagombea hao kuwa ni Patricia Rhob Kabaka kundi la Viti maalumu wanawake,Bitrice Raya Kundi la wasomi,Getruda Emanuel kundi la wanawake,Beatrice Kebaso kundi la Wafanyakazi,Mosi Magere kundi la Wanawake,Rosemary Masirori kundi la Walemavu .

Wengine ni Suzana Senso Kesogwe kundi la wafanyakazi, Ghati Chomete,Nansi Msafiri,Salma Hamidu Musa na Bhoke John  wote wakigombea kundi la wanawake.

Kashombo alisema kuwa nafasi ya Udiwani viti maalumu watia nia wako 63 ambapo Tarafa ya Ingwe ni 15,Inchage 28,Inano 10,na Inchugu 10.

Aliongeza kuwa katika nafasi ya Kata watia nia wanawake ni 6.
Share:

Tazama Picha : MUONEKANO WA SHY PARK HOTEL ILIYOPO SHINYANGA MJINI... ITAFUNGULIWA RASMI AGOSTI 2020

Jumamosi Julai 18,2020 : Muonekano wa majengo ya Hoteli Mpya ya Kisasa yenye Ubora wa hali ya juu 'SHY PARK HOTEL'  inapatikana Lubaga Mjini Shinyanga karibu na Ikulu pembezoni mwa Barabara ya Old Shinyanga.

SHY PARK HOTEL itafunguliwa rasmi  Rasmi mwezi Agosti 2020,ambapo  Uongozi wa SHY PARK HOTEL Julai 18,2020 umefanya usaili kwa watu  waliosomea na wenye uzoefu wa Masuala ya Usimamizi wa Hoteli na unaendelea kufanya maandalizi kabambe tayari kabisa kwa uzinduzi rasmi ya SHY PARK HOTEL mwezi ujao.

Miongoni mwa Huduma zinazopatikana SHY PARK HOTEL ni  malazi ,vyakula, vinywaji, kumbi za sherehe/harusi na mikutano, Swimming pool kwa watoto na watu wazima, michezo mbalimbali ya watoto, Sauna, Massage, Gym, Car wash, Car Parking n.k

Kwa Mawasiliano zaidi piga simu namba 0621288344, Whatsapp namba 0759096494
Au Email info@shypark.co.tz

Karibu SHY PARK HOTEL


Jumamosi Julai 18,2020 : Muonekano wa majengo ya Hoteli Mpya ya Kisasa yenye Ubora wa hali ya juu SHY PARK HOTEL. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Wananchi kutoka ndani na nje ya mkoa wa Shinyanga walioomba nafasi za kazi SHY PARK HOTEL wakisubiri kufanyiwa usaili/Interview Julai 18,2020.


Muonekano wa majengo ya  SHY PARK HOTEL
Muonekano mandhari ya SHY PARK HOTEL
Muonekano mandhari ya SHY PARK HOTEL
Muonekano majengo SHY PARK HOTEL
Muonekano mandhari ya SHY PARK HOTEL
Muonekano majengo ya SHY PARK HOTEL
Muonekano mandhari ya SHY PARK HOTEL
Muonekano majengo ya SHY PARK HOTEL
Muonekano wa majengo ya SHY PARK HOTEL
Muonekano wa majengo ya Hoteli Mpya ya Kisasa yenye Ubora wa hali ya juu SHY PARK HOTEL

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Share:

CHARLES SHIGINO AJITOSA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA SHINYANGA MJINI KUPITIA NCCR MAGEUZI

Share:

Hotuba Ya Mgombea Wa Urais Wa Zanzibar Dk Hussein Ali Hassan Mwinyi ,kisiwani Pemba

Nianze kwa kumshukuru Mwenyezimungu, mwingi wa rehma kwa kutuwezesha kukutana hapa hii leo. Kuwashukuru wananchi wa Pemba kwa mapokezi makubwa sana. Napata faraja kazi yetu sasa itakamilika mapema sana.

Nashukuru chama kwa kumaliza uteuzi wake kwa kwa haki, na sasa sote tumekua wamoja, hakuna timu Mwinyi wala timu Mbarawa, na lengo letu sasa ni moja kushika dola.

Kabla ya yote tuwaombee wale waliopata maafa Mwenyezi Mungu awarehemu, na wengine waliopata ajali ya kuezuliwa mapaa nyumba zao Mungu awafariji.

Sitosema mengi. Muwe na hakika nitaenzi Mapinduzi matukufu ya Zanzibar ya Mwaka 1964. Nitadumisha Muungano wetu ni wa aina yake, na unatiliwa mfano duniani kote.

Kuna suala kubwa, nalo ni suala la amani na ndio maana tunapata maendeleo. Nchi nyingi za jirani zetu hakuna amani. Namshukuru sana Mheshimiwa Rais Dk.Ali Mohamed Shein kwa kuongoza nchi kwa amani.

Jukumu langu ni kuhakikisha amani inadumu. Lazima tudumishe umoja wetu. Kusiwe na Upemba na Uunguja, kusiwe na ukusini na Ukaskazini.

Sote ni Wazanzibari. Suala la ajira tutalishughulikia hasa kwa vijana. Niwapongeze hasa Rais Dkt. Shein na viongozi wote wa serikali na chama.

Nihakikishe alipoachia yeye nitaendeleza. Nitaendeleza miundombinu, huduma za jamii, ustawi wa watu, maendeleo ya jamii, afya, elimu, na yote yanayogusa watu. Nitahakikisha Mzazibari anakua  na maisha bora.

Ukitaka kuyafanya hayo, lazima uwajibike. Huwezi kuwa na program kukawa na wala rushwa, wabadhirifu, Wazembe. Sitokua na huruma kwa wenye tabia hizo. Serikali itafanya kazi kwa maslahi ya Wazanzibari wote.

Wapo wanaosema Mwinyi ni mpole. Mimi Nasema wataniewa.

Nasema haya kwa sababu pengine hamjanisikia nikiongea sana kwenye vyombo vya habari. Sababu kubwa ni kwamba Wizara ya Ulinzi huko mambo yetu ni ya siri hatufanyi hadharani. Siwezi kusema ila kwa wale wabadhirifu,wala rushwa, wazembe, wasiowajibika, hao watawajibika.

Nitasimamia maslahi ya Zanzibar kwenye Muungano, Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya za Kimataifa.

Nikwambieni nimeamua nigombee na ili  nitakaposhinda dhamira yangu ni moja kuwatumikia Wazanzibari wote.

Tukishika dola, tutakuja na miradi ya kusaidia Wazanzibari ikiwemo ajira kwa wote bila ubaguzi.

Panapo dhamira njema Mwenyezi Mungu atatupa neema.

Mwaka huu, tunataka tupate ushindi wa kishindo usiwe mwembemba tukapata malalamiko. Na niliyoyaona Unguja na hapa Pemba kwa sasa sina shaka ushindi ni mkubwa. Sina shaka ushindi utakua ni mkubwa.

Nasema tena kwamba ‘Yajayo yanafurahisha.’ Ni ahadi naichukua mbele ya Mungu na mbele yenu. Nitahakikisha nawahudumia wananchi.

Sasa na wakati huu nina hakika tunafanya  mambo mazuri kwa maisha yetu yawe mazuri . Kazi iliyobakia ni kwenda kushika dola na si vyenginevyo. Kwa sasa lililobakia ni umoja mshikamano na ushirikiano ndani ya CCM.

Katika risala ya mikoa miwili ya Pemba ya Kusini na Kaskazini salamu nimezipokea na kuondoka Pemba nikiwa na faraja kubwa hivyo hayo yanaonekana ni mapenzi ya dhati ninaahidi kuitumikia Zanzibar kwa moyo wangu wote. Ihsani hulipwa kwa Ihsani .

Maneno yanayosemwa na wagombea kama wametumwa na Hussein , nataka kuwaambia hapa leo, sijamtuma mtu, kila mtu apambane na hali yake, maana wengine wanasema eti wachaguliwe ili nitakapounda Baraza la
Mawaziri, niwateuwe, nawaambia sijamtuma mtu.

Nataka kurudia maneno aliyosema Kama Makamu Mwenyekitu wetu Rais Dkt Shein kuwa tutumie uchaguzi huu ndani ya Chama kupata wagombea bora.

Baada ya kusema hayo sasa naomba nimalizie kwa kuwashukuru wana CCM na wananchi wote waliojitokeza katika mapokezi yetu na hapa uwanjani.

 Zanzibar ni njema atakae aje


Share:

Serikali Yatoa Mabilioni Kulipa Madeni Ya Wakulima Wa Korosho

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imetoa sh. bilioni 20 za kulipa madeni ya wakulima, wasafirishaji, wapuliziaji dawa na waendesha maghala ya korosho.

"Rais Magufuli ametoa fedha hizi kwa ajili ya Tandahimba, Masasi, Mtwara na Kibiti kwa ajili ya waliokuwa wamelipwa nusu, waliolipwa kiasi na wasiolipwa kabisa. Fedha hizi zitaanza kulipwa kesho asubuhi," amesema.

Ametoa kauli hiyo leo (Jumapili, Julai 19, 2020) wakati akizungumza na wanachama wa Chama cha Msingi (AMCOS) cha Matogoro na wakazi wa Tandahimba mkoani Mtwara alikoenda kuhamasisha maandalizi ya msimu wa ununuzi wa korosho.

Amesema uhakiki uliofanywa kwa wakulima wa Kibiti, Rufiji, Mkuranga, Ruangwa, Liwale, Lindi, Tunduru na wilaya zote za mkoa wa Mtwara ulibaini kuwa wakulima na watoa huduma wote walikuwa wakidai zaidi ya sh. bilioni 23.

“Katika hao, Tandahimba wanadai zaidi ya sh. bilioni 9, Masasi wanadai sh. bilioni 2.3 na Mtwara Vijijini wanadai sh. milioni 884. Nyingine ni za Pwani na Lindi," amefafanua.

Waziri Mkuu amesema fedha hizo zimetokana na mfumo uliotengenezwa na wanunuzi ili kumnyonya mkulima katika msimu wa 2018/2019 kwa kununua kilo ya korosho kwa sh. 1,500 badala ya sh. 3,000 hali iliyolazimu Serikali kuingilia kati na kuamua kuzinunua korosho zote.

Waziri Mkuu alishuhudia Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Kilimo (TABD), Bw. Japhet Justine akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bw. Gelasius Byakanwa hundi ya sh. 9,050, 846,030 ambaye pia aliikabidhi kwa viongozi wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Tandahimba na Newala (TANECU) na AMCOS ya Matogoro.

Awali, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mtwara, Bw. Yusuph Nanila alimuomba Waziri Mkuu atoe majibu ya lini wakulima wa Tandahimba watalipwa fedha zao, ambazo zimefikia zaidi ya sh. bilioni 9.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu amevitaka Vyama Vikuu vya Ushirika na AMCOS waweke kipaumbele cha kununua mashine ndogo ndogo za kubangulia korosho ili waache mtindo wa kuuza korosho ghafi.

"Ukibangua kilo tatu za korosho yenye maganda, unapata kilo moja ya korosho zilizobanguliwa. Kilo moja ya korosho yenye maganda inauzwa sh. 2,400 kwa hiyo kilo tatu ni sh.7,200, lakini ukizibangua, kilo moja inauzwa sh.25,000. Ninawasihi tuanzishe viwanda vidogo vya kubangua korosho ili tupate fedha zaidi kwenye vyama vya msingi."

"Matogoro mnaweza kununua hata mashine 100 kutoka SIDO ili mzibangue hapahapa na kuongeza pato la wakulima wenu. Tena mashine za viwanda vidogovidogo zinatoa korosho nzuri zenye ubora sawa na zilizotoka kwenye mashine kubwa," aliongeza.

Kuhusu msimu wa ununuzi wa korosho, Waziri Mkuu alisema msimu mpya unaanza Septemba hadi Desemba na akawataka viongozi wa ushirika wasimamie ununuzi wa korosho mapema.

Aliwataka wakulima wa korosho wa wilaya hiyo wabadili mfumo wa kilimo cha zao hilo kwa kuanza kupanda miche mipya ambayo inazaa kwa wingi na inachukua muda mfupi kukomaa. “Pandeni miche mipya kwa sababu inazaa ndani ya mwaka mmoja na nusu, ondoeni mikorosho iliyozeeka.”

Pia aliwataka wanachama hao walime mazao mbadala kama chikichi na alizeti ambayo yanakubali kwenye ardhi yao ili waongeze wigo wa sgughuli za kiuchumi kwenye wilaya hiyo. “Michikichi inakubali sana kwenye ukanda wa pwani, kwa hiyo jaribuni muone ukuaji wake.”

Kuhusu malipo ya wasafirishaji, Waziri Mkuu alisema kati ya fedha zilizolipwa, wasafirishaji wametengewa sh. bilioni 3.3. Alikuwa akijibu swali la Mwenyekiti wa Chama cha Wasafirishaji wilayani Tandahimba, Bw. Maulid Mussa ambaye alisema walisafirisha korosho kutoka kwa wakulima hadi kwenye maghala na madai yao yaliyofikia sh. milioni 600 yamekuwa yakiwanyima usingizi kwa muda mrefu.

Kuhusu bei dira ya korosho, Waziri Mkuu amewaelekeza viongozi wa vyama vya msingi na vyama vikuu nchini kote wakae na kuandaa gharama ambazo mkulima anakuwa amezitumia na gharama zitakazokubaliwa ndiyo iwe msingi wa bei dira.

“Vyama vikuu vifanye hiyo kazi kabla msimu haujaanza Septemba 2020. Mniletee ofisni kwa maandishi ili tumshirikishe Waziri wa Kilimo na kisha tutangaze kitaifa bei dira ni ipi,” amesema.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,


Share:

Benard Membe Arejesha Fomu ya Kugombea Urais Kupitia ACT Wazalendo

Aliyewahi kuwa waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe, leo Julai 19, 2020 amerejesha fomu za kuomba kuteuliwa kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya ACT Wazalendo.

Makabidhiano hayo yamefanyika Ofisi ya ACT Wazalendo Magomeni, jijini Dar es salaam ambapo amekabidhi fomu hizo kwa Naibu Katibu Mkuu Bara wa ACT Wazalendo Ndugu Joran Bashange.

Membe ambaye kauli mbiu yake alitaja kuwa ni Kazi na Bata, alikubali kuwania nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia ACT Wazalendo, kwa kile alichodai kwamba huo ni wakati muafaka kwake wa kushiriki mazungumzo na vyama vingine ili waweze kusimamisha mgombea mmoja.



Share:

Jeshi la Polisi Nchini latoa taarifa kwa vyombo vya habari




Share:

Lema apita kura za maoni kugombea ubunge Arusha mjini

Aliyekuwa mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema ameshinda kwenye kura za maoni za chama hicho kwa kupata kura 181 kati ya kura 207 hivyo anakuwa mgombea atakayepeperusha bendera ya CHADEMA kugombea ubunge jimbo la Arusha mjini


Share:

Mageuzi Ya Mifumo Na Utendaji Heslb Yameimarisha Elimu Ya Juu

Na Mwandishi Wetu,HESLB
KATIKA kuhakikisha taifa letu linajenga uchumi ulio imara na jamii inayoheshimu na kufuata misingi ya uwajibikaji na ubunifu, Serikali pamoja na mambo mengine imeendelea kuwekeza katika elimu ya juu.

Serikali imeendelea kuhakikisha Watanzania wote wenye sifa wanapata elimu ya juu kwa kupewa mikopo kupitia Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, iliyoanzishwa chini ya kifungu cha Sheria Na. 9 ya mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi Julai, 2005.

Bodi ya Mikopo pamoja na majukumu mengine, ina jukumu la kutoa mikopo au ruzuku kwa wanafunzi wenye sifa na wahitaji wa Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu na mwombaji stahiki na mhitaji anaweza kuomba mkopo /ruzuku ili kugharamia sehemu ya gharama au gharama zote za masomo ya elimu ya juu.

Tangu kuingia madarakani kwa Rais Dkt. John Magufuli, Serikali ya Awamu ya Tano imeweza kuongeza bajeti ya maendeleo kutoka wastani wa asilimia 26 hadi asilimia 40 na hivyo kuweza kupanua wigo na kuboresha upatikanaji wa huduma za mbalimbali za jamii ikiwemo elimu ya Juu.

Katika kipindi cha miaka mitano cha Uongozi wa Rais Dkt. John Magufuli Serikali imeongeza bajeti ya mikopo ya elimu ya juu kutoka Tsh. bilioni 348.7 mwaka 2014/2015 hadi Tsh. bilioni 450 mwaka huu wa Fedha 2019/2020.

Kutokana na msukumo na juhudi kubwa zilizofanywa na Serikali katika kuboresha elimu ya juu nchini, Serikali imeiwezesha na kuijengea uwezo Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kutekeleza vyema majukumu yake ya kisheria na kuongeza uwazi na ufanisi katika  upangaji, utoaji na ukusanyaji wa mikopo.

Akiwasilisha Hotuba ya Makadirio ya Bajeti ya Mapato na Matumizi ya mwaka 2020/2021, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako anasema katika kipindi cha mwaka wa fedha 2019/20, Serikali kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu hadi   kufikia machi 2020 imetoa mikopo yenye thamani ya Tsh. Bilioni 449.99 kwa wanafunzi 132,119 sawa na asilimia 99 ya fedha iliyoidhinishwa.

Prof. Ndalichako anasema katika ya hao, wanafunzi 49,799 ni wa mwaka wa kwanza na 82,320 wanaoendelea na masomo hatua inayolenga kutoa fursa na kupanua wigo kwa wanafunzi wenye sifa za uhitaji kujiunga na masomo katika vyuo na taasisi za elimu ya juu nchini.

Kwa mujibu wa Prof. Ndalichako anasema HESLB katika mwaka 2019/2020 pia imefanya ukaguzi kwa waajiri 2,406 nchi nzima na kutambua wanufaika wapya 14,731 wenye mikopo iliyoiva yenye thamani ya Shilingi Bilioni 100.7 ambapo kati yao wanufaika 13,969 (94%) wameanza kulipa.

‘Aidha, hadi kufikia Disemba, 2019 idadi ya wanufaika wanaorejesha mikopo ilikuwa imefikia 176,952 kati ya 184,166 waliotarajiwa sawa na asilimia 96 ya lengo’’ anasema Prof. Ndalichako.

Kwa mujibu wa Waziri Ndalichako anasema Bodi ya Mikopo imeendelea na ukusanyaji wa mikopo iliyoiva ambapo kiasi cha Tsh. Bilioni 144.3 kati ya Tsh. Bilioni 166.1 zilizolengwa katika kipindi cha mwezi Juni 2019 hadi Machi 2020 sawa na asilimia 86.9 zimekusanywa, ambapo lengo la makusanyo kwa mwaka lilikuwa  ni kiasi cha Tsh. Bilioni 221.5.

Prof. Ndalichako anasema katika kusogeza huduma ya mikopo ya elimu ya juu karibu na wananchi pamoja na pamoja na kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mikopo iliyoiva, HESLB imefungua ofisi ya Kanda katika Mkoa wa Mtwara na kufikisha jumla ya ofisi sita zilizopo katika Mikoa ya Dodoma, Mwanza, Arusha, Mtwara, Mbeya na Zanzibar.

Akifafanua Zaidi Prof. Ndalichako alisema Bodi ya Mikopo imeendelea kuboresha mifumo ya uendeshaji ili kuongeza uwazi na ufanisi wa utoaji huduma katika upangaji, utoaji na ukusanyaji wa mikopo iliyoiva, ambapo kwa sasa mifumo hiyo inamuwezesha mwanafunzi kupata taarifa za mkopo wake kupitia simu ya mkononi au mtandaoni na kuondoa usumbufu wa wanafunzi kufuatilia taarifa hizo kwenye ofisi za Bodi.

‘Bodi imebuni mfumo unaoviwezesha vyuo kuambatisha nyaraka muhimu kama vile matokeo ya mitihani kupitia mtandao badala ya kutuma nakala ngumu, vilevile uboreshaji wa mifumo umehusisha uunganishaji wa mifumo ya TEHAMA ya Bodi ya Mikopo na ya Tume ya Vyuo Vikuu ambapo taarifa za udahili za waombaji wa mikopo zinapatikana kwa urahisi na kwa wakati’’ alisema Prof. Ndalichako.

Ni dhahiri kuwa wigo wa utoaji elimu nchini unapanuka, hivyo ili kulinda ubora wa elimu ni wajibu wa mamlaka zote zinazohusika na usimamizi na udhibiti wa ubora wa elimu zitekeleze majukumu yao ipasavyo kwa kutoa miongozo na kufanya kaguzi za mara kwa mara.

(Mwandishi ni Afisa Mawasiliano Mwandamizi HESLB, anapatikana kwa ingayonga@heslb.go.tz)

MWISHO


Share:

Polepole: Viongozi Wasioridhika na Wenye Tamaa Hawatufai

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama tawala cha Mapinduzi (CCM) Humphrey Polepole , amesema viongozi wa umma wasioridhika na nyadhifa zao, hawana nafasi ndani ya chama hicho.

Polepole ametoa kauli hiyo jana Jumamosi tarehe 18 Julai 2020, wakati akizungumza katika mkutano wa kuelezea utekezaji wa Ilani ya CCM, katika Mkoa wa Ruvuma.

Licha ya kwamba Polepole hakuweka bayana viongozi hao wa umma hawaridhiki kivipi, katibu huyo wa uenezi amesema CCM inawasubiri kuwaona wakati wa uteuzi huku akiwapongeza viongozi wa kuteuliwa Mkoa wa Ruvuma kwa kutokuondoka.

Juzi Ijumaa saa 10 jioni, ndiyo ilikuwa mwisho wa mchakato wa uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kuomba ridhaa ya chama hicho katika nafasi za Ubunge, Udiwani na Uwakilishi.

Baadhi ya wakuu wa mikoa, wilaya, katibu tawala wa mikoa na wilaya, wakurugenzi wa halmashauri, mashirika ya umma pamoja na makatibu wakuu wameziacha nafasi zao na kwenda kugombea

 Kwa mujibu ya ratiba ya CCM, Tarehe 20 na 21 Julai 2020 itakuwa ni mikutano mkuu ya majimbo na wilaya kupiga kura za maoni za wagombea wa ubunge na ujumbe wa baraza la wawakishi.


Share:

RAIS MAGUFULI AFANYA MABADILIKO YA UTEUZI ALIOFANYA JULAI 17... MHANDISI MARWA MWITA RUBIRYA SASA RC NJOMBE


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya mabadiliko ya uteuzi alioufanya  Julai 17,2020 ambapo amemteua Mhandisi Marwa Mwita Rubirya kuwa Mkuu wa mkoa wa Njombe


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger