Saturday, 18 July 2020

Breaking : CCM SHINYANGA YASHTUSHWA KASI YA UTOAJI RUSHWA WAGOMBEA UBUNGE SHINYANGA MJINI…YAKUTANA NAO KIKAO CHA DHARURA KUWAONYA


Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Shinyanga Donald Magesa akizungumza katika kikao cha dharura cha wanachama 60 wa CCM waliorudisha fomu kuomba kugombea ubunge jimbo la Shinyanga Mjini na kuwatahadharisha kuhusu mienendo ya baadhi ya wagombea kutoa rushwa ili wachaguliwe kuwa wagombea ubunge.



Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Katika kile kichoonekana kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimechoshwa na vitendo vya rushwa kwa wagombea wa nafasi za Uongozi, CCM mkoa wa imeitisha kikao cha dharura cha wanachama 60 wa CCM waliorudisha fomu kuomba kugombea ubunge jimbo la Shinyanga Mjini na kuwatahadharisha kuhusu mienendo ya baadhi ya wagombea kutoa rushwa ili wachaguliwe kuwa wagombea ubunge.

Akizungumza katika kikao hicho cha dharura kilichofanyika leo Julai 18,2020 majira ya saa tano na robo asubuhi, Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Shinyanga Donald Magesa amesema kama wagombea hao wa ubunge wataendelea kujihusisha na vitendo vya rushwa Chama Cha Mapinduzi kitafuta majina ya walioomba kugombea ubunge.

Magesa ambaye ni Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi Jimbo la Shinyanga Mjini ambaye amekutana na wagombea hao kutokana na Agizo la Katibu Mkuu wa CCM Taifa Humphrey Polepole amekemea vitendo vya rushwa kwa wagombea kwani uchaguzi huo na kwamba atakayetoa rushwa chama kitamshughulikia kwani uchaguzi ni wa haki hauhitaji kutumia fedha ili uchaguliwe kuwa kiongozi.

“Kutafuta fedha,kutafuta wapiga kura na kuwapa chochote ni marufuku kuanzia sasa. Kuanzia sasa fanya kazi zako fanyia nyumbani kwako, na hao mawakala mnaowatuma kwenda kugawa fedha tutawakamata. Na tutafuta uchaguzi. Hapo mlipofikia kugawa nasema sasa marufuku, sitaki kusikia mgombea anajihusisha na vitendo vya rushwa. Mkiendelea tutagawa fomu upya za kuomba kugombea ubunge na hamtaruhusiwa kugombea”,amesema Magesa.

“Niwaombe sana ndugu zangu kama umeingia kutafuta kura watu watakufahamu, usiende kushawishi,hao mawakala wenu tutawashika. Baadhi yenu wanatoa rushwa, ni uchaguzi wa aina gani huo?. Mnaenda kununua kura kwanini??,mnatembelea watu kwanini? Hiki mnachofanya Shinyanga Mjini ni fujo..Naomba kugawa fedha kuishe,kugawa vitenge kuishe”,amesema Katibu huyo wa CCM.

“Kushinda kura za maoni siyo kuteuliwa kugombea, tuna vigezo zaidi ya 15 vinavyomfanya mtu ateuliwe kugombea Ubunge. Unaweza kuongoza kura za maoni lakini usiletwe. Hapo mlipofikia panatosha, mistake kuharibu uchaguzi. Mkiendelea kutafuta kura kwa kutembelea miji ya watu kutoa rushwa tufatuta uchaguzi, tutafuta majina yote. Ikishindikana tutaleta hata wagombea wengine ambao hawakuomba kugombea",ameongeza Magesa.

Magesa amemuagiza Katibu wa wilaya ya Shinyanga Mjini kuwaandikia barua ya maagizo wagombea kufanya uchaguzi kwa ustaarabu,kutofanya kampeni wasubiri siku ya mkutano wa kura za maoni utakaofanyika Julai 20,2020.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Shinyanga Donald Magesa akizungumza katika kikao cha dharura cha wanachama 60 wa CCM waliorudisha fomu kuomba kugombea ubunge jimbo la Shinyanga Mjini leo Julai 18,2020. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Shinyanga Donald Magesa akikemea vitendo vya rushwa kwa wagombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini na kwamba atakayetoa rushwa chama kitamshughulikia.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Shinyanga Donald Magesa akizungumza katika kikao cha dharura cha wanachama 60 wa CCM waliorudisha fomu kuomba kugombea ubunge jimbo la Shinyanga Mjini leo Julai 18,2020.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Shinyanga Donald Magesa akizungumza katika kikao cha dharura cha wanachama 60 wa CCM waliorudisha fomu kuomba kugombea ubunge jimbo la Shinyanga Mjini leo Julai 18,2020.


Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Shinyanga Donald Magesa akizungumza katika kikao cha dharura cha wanachama 60 wa CCM waliorudisha fomu kuomba kugombea ubunge jimbo la Shinyanga Mjini leo Julai 18,2020.

Wanachama wa CCM waliochukua fomu kuomba kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.
Wanachama wa CCM waliochukua fomu kuomba kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.

Viongozi wa CCM wakiwa kwenye kikao hicho
Share:

WANACHAMA 323 WA CCM WAMERUDISHA FOMU KUGOMBEA UBUNGE MAJIMBO SITA YA SHINYANGA


Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Shinyanga Donald Magesa akionesha kitabu cha Kanuni na Maadili ya Uongozi CCM wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 18,2020 akitoa taarifa kuhusu wanachama wa CCM waliojitokeza kuchukua na kurudisha fomu kuomba kugombea nafasi ya Ubunge katika majimbo sita ya Mkoa wa Shinyanga ambayo ni Kishapu,Solwa, Msalala, Ushetu, Kahama Mjini na Shinyanga Mjini. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Shinyanga Donald Magesa akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 18,2020.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Jumla ya wanachama 324 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamejitokeza kuchukua fomu kuomba kugombea ubunge katika majimbo ya  Kishapu,Solwa, Msalala, Ushetu, Kahama Mjini na Shinyanga Mjini ambapo 323 ndiyo wamerudisha fomu.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari  leo Julai 18,2020 Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Shinyanga Donald Magesa amesema kati ya wanachama 324 waliochukua fomu mmoja pekee kutoka Jimbo la Ushetu hajarudisha fomu hivyo kufanya idadi ya waliorudisha fomu kuwa 323 kati yao wanawake ni 26, wanaume 297.

Magesa amefafanua kuwa kati ya wanachama wa CCM walioomba kugombea ubunge katika Jimbo la Kishapu ni 78 (wanawake wanne), Shinyanga Mjini 60 (wanawake 7), Solwa (wanawake wanne), Kahama Mjini 70 (wanawake 8), Msalala 44 (wanawake wawili) na  Ushetu 18 (mwanamke mmoja).

Aidha amesema jumla ya wanachama 43 kupitia UWT walichukua fomu za kuomba kugombea nafasi ya Ubunge Viti maalum ambapo mmoja hajarudisha fomu, walioomba ubunge viti maalumu kupitia kundi la Vijana ni 14 na kupitia Umoja wa Wazazi waliochukua na kurudisha fomu ni watatu.

 Amesema mkutano wa kura za maoni kuwapigia kura wagombea utafanyika Julai 20,2020 huku akiwatahadhalisha wagombea kutojihusisha na vitendo vya rushwa.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JULAI 18,2020












Share:

MOTO WATEKETEZA MAJENGO SHULE YA MUSLIM KINONDONI

Madarasa 11 kati ya 15 ya Shule ya Sekondari ya Kinondoni Muslim iliyoko Kinondoni Shamba jijini Dar es Salaam yameteketea kwa moto.

Mbali ya majengo hayo vifaa na samani za shule hiyo vimeteketea kwa moto huku walimu na wanafunzi wote wa shule hiyo wapatao 218 wakisalimika.

Moto huo ulianza majira ya alasiri Julai 17,2020 wakati shughuli za kila siku zikiendelea.

Maafisa wa Jeshi la Zimamoto wamesema ni muhimu maeneo yote ya shule yakawa na maji ya dharura ili kujikinga na madhara ya moto.

Share:

Friday, 17 July 2020

BONIPHACE BUTONDO ARUDISHA FOMU KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KISHAPU

Aliyekuwa Mwenyekiti Halmashauri ya wilaya ya Kishapu mwaka (2006-2010) na (2016-2020), Boniface Butondo (kulia) amerudisha fomu ya kuomba kugombea Ubunge Jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM). 

Boniface Butondo ambaye alikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC) mwaka 2012 - 2017 na Mwenyekiti Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) mkoa wa Shinyanga mwaka 2002- 2008 amerudisha fomu amerudisha fomu ya kuomba kugombea Ubunge Jimbo la Kishapu katika ofisi ya CCM wilaya ya Kishapu leo Julai 17,2020.
Share:

HAMIS BORI RAJABU ARUDISHA FOMU KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KOROGWE MJINI


Kada wa Chama Cha Mapinduzi Hamisi Bori Rajabu (kulia) akirudisha fomu ya kuomba kugombea Ubunge Jimbo la Jimbo la Korogwe Mjini mkoani Tanga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo Ijumaa Julai 17,2020. 
Share:

COSTANTINE MOLLO NKUBA ARUDISHA FOMU KUGOMBEA UBUNGE SHINYANGA MJINI


Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Costantine Mollo Nkuba akirudisha fomu ya kuomba kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Agnes Bashemu (kushoto) leo Ijumaa Julai 17,2020 katika ofisi za CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini.
Share:

BASI LA KYELA EXPRESS LAPATA AJALI


JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia Dereva wa Basi la Kampuni ya Kyela Express DENIS LAMECK [48] aliyekuwa akiendesha Gari yenye namba za usajili T. 756 DEF Scania Basi baada ya kusababisha ajali iliyopelekea kifo cha mtu mmoja aitwaye AIDA IPONJA [42] Mkazi wa Masukulu.


Ajali hiyo imetokea mnamo tarehe 16.07.2020 majira ya saa 22:20 Usiku huko Kijiji cha Kyimbila kilichopo Kata ya Mpuguso, Tarafa ya Pakati, Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya katika barabara ya Tukuyu – Kyela ambapo Gari hilo Basi la Abiria Mali ya Kampuni ya Kyela Express lilikuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Kyela iliacha njia na kupinduka na kusababisha kifo kwa abiria mmoja.

Aidha katika ajali hiyo abiria wanne walijeruhiwa ambao ni:-
  1.     SALOME SHIMITA [43] Mkazi wa Kyela.

  2.     SABINA JOSEPH [19] Mkazi wa Kyela.

  3.     TALAMPE KANYENYE [41] Mkazi wa Kyela.

  4.     PASCHAL MERIMERI [36] Mkazi wa Jijini Mbeya.
Majeruhi wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Rungwe Makandana. Chanzo cha ajali ni mwendo kasi katika eneo lenye mkungu na mvua. Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitalini hapo. Upelelezi unaendelea.

KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO].
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia GWANTWA ELIAS [30] Mkazi wa Itunge Wilayani Kyela akiwa na pombe haramu ya moshi (gongo) ujazo wa lita 100.

Mtuhumiwa amekamatwa mnamo tarehe 16.07.2020 majira ya saa 09:30 Asubuhi huko Kijiji na Kata ya Itunge, Tarafa ya Unyakyusa, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya. Mtuhumiwa ni muuzaji wa Pombe hiyo na atafikishwa mahakamani leo tarehe 17.07.2020.

 Imetolewa na;
[ULRICH O. MATEI -SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


Share:

BENARD MEMBE ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA URAIS TANZANIA KWA TIKETI YA ACT-WAZALENDO

Leo Julai 17, 2020, aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe, amechukua fomu ya kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya ACT-Wazalendo ambapo amekabidhiwa fomu hiyo na Katibu Mkuu wa chama hicho Ado Shaibu



Share:

ANDREW CHALE ACHUKUA NA KUREJESHA FOMU YA UBUNGE CCM JIMBO LA MBAGALA

Mtaalam wa Kodi na  Maendeleo ambaye pia ni Kada wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Andrew Chale (kushoto) akikabidhi fomu ya kutia nia kiti cha Ubunge CCM-Mbagala wakati wa kurejesha.
**
Mtalaamu wa Kodi na  Maendeleo ambaye pia ni Kada wa Chama Cha Mapinduzi CCM , Andrew Chale, amechukua na kurejesha fomu ya kutia nia kiti cha Ubunge CCM-Mbagala.

Andrew Chale amekuwa ni miongoni mwa Vijana walioguswa na utekelezaji wa CCM kuruhusu Demokrasia pana kwa kila mwenye nia kujitokeza kuongoza.

"Nimekuwa mdau mkubwa wa Maendeleo kwa kusaidia masuala ya mbalimbali ya  kijamii Vikundi vya Vijana na makundi maalum ndani na nje ya Wilaya yangu.

"Kwa sasa shauku yangu ni kuongoza wananchi ndani ya Jimbo hivyo nimetimiza haki yangu ya kuchukua na kurejesha fomu na kwa sasa nasubiria hatua ndani ya chama" Alisema Andrew Chale.

Aidha, Alieleza kuwa, kwa sasa Vijana wanataka kuona safari ya Mbagala mpya yenye maendeleo na miondombinu ya kisasa inatimia.
Share:

EMMANUEL KAMARA AJAZA NA KUREJESHA FOMU UBUNGE CCM- DODOMA MJINI

Mjumbe wa Halmashauri CCM Wilaya ya Dodoma Mjini, Emmanuel Japhet Kamara (kulia) amechukua na kurejesha fomu ya kutia nia kiti cha Ubunge  ndani ya CCM Jimbo la Dodoma Mjini.

Kamara amepiga hodi katika hatua yake hiyo ya kwanza huku akisubiria maamuzi ya chama yatakayofuata.


"Nashukuru nimefanikiwa kurudisha fomu niliyoichukua na kuijaza. Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha nguvu ya kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Ubunge Jimbo la Dodoma Mjini na kunipa kibali cha kuijaza na kuirudisha nikiwa salama na Malaika wake wakinizunguka", amesema

Kamara alisema sasa hatua iliyobaki ni kuwaomba Wananchi na Wanadodoma kumuombea kwa Mungu azidi kumpa uhai na afya.
Share:

Mkandarasi Wa Maji Iringa Apewa Wiki Nne Kukamilisha Mradi

NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga ametoa Wiki Nne kwa Mkandarasi Kampuni ya GNMS Contractors ya Iringa na Kampuni ya Hematec Investiment ya Dar es Salaam kukamilisha ujenzi wa mradi wa maji wa Pawaga- Mlenge, Wilayani Iringa.

Mhandisi Sanga ametoa maelekezo hayo Julai 16, 2020 alipofanya ziara kwenye mradi huo ili kujionea hatua ya utekelezwaji wake sambamba na kuzungumza na wakandarasi wanaoutekeleza ambapo alielezwa kuwa mradi utaanza kutoa maji baada ya miezi miwili ijayo.

Mhandisi Sanga hakuridhishwa na kasi ya utekelezwaji wa mradi na hakukubaliana na maelezo ya kukamilisha mradi baada ya miezi miwili hasa ikizingatiwa kwamba lengo la Serikali ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma kwanza kabla ya kukamilisha shughuli zingine za mradi.

“Serikali ilikwishaelekeza miradi yote ya maji inapasa kwanza itoe maji ili wananchi waanze kunufaika na sio kusubiri hadi ujenzi wa matenki ukamilike ndipo wananchi wapate huduma wakati inawezekana kabisa wakapata maji kabla hayajafika kwenye haya matenki mnayojenga,” alisisitiza Mhandisi Sanga.

Alisema miradi haipaswi kuchelewa bila kuwa na sababu ya msingi na alibainisha kwamba malipo kwa wakandarasi yamekuwa yakifanyika kwa wakati lakini hayaakisi hali halisi ya kasi ya utekelezaji inayodhamiriwa na Serikali.

Mhandisi Sanga alisema Pawaga ni eneo lenye ukame na kwamba wananchi wanapata tabu kukosa huduma ya maji na wakati huohuo wakandarasi wanalipwa kwa wakati lakini kasi yao sio ya kuridhisha.

Alielekeza Mamlaka ya Maji Iringa (IRUWASA) na Wakala ya Maji Vijijini (RUWASA) kushirikiana kusimamia utekelezaji wa miradi.

“Hatuwezi kutoka Dodoma kuja huku kusisitiza wakandarasi waongeze kasi wakati nyie huku ni wasimamizi wa miradi kwa niaba ya Wizara, hakikisheni miradi mnayoisimamia inakamilika kwa wakati na kipaumbele ni wananchi kwanza kupata maji,” alisisitiza Mhandisi Sanga.

Aidha, Mhandisi Sanga aliwakumbusha wasimamizi wa miradi kote nchini kuhakikisha kwenye utekelezaji wa miradi wanaanza na maeneo yatakayoleta matokeo ya haraka ili wananchi waanze kupata huduma na baadaye waendelee na maeneo mengine wakati ambao tayari wananchi wanakuwa na huduma.

“Mnatakiwa kuwa wabunifu wakati wa ujenzi wa miradi, mnapaswa kuanza na maeneo yatakayoleta matokeo ya haraka ili kwanza wananchi wapate huduma na huku mkiendelea kutekeleza maeneo mengine,” alisisitiza Mhandisi Sanga.

Kwa upande wake Meneja Ufundi wa IRUWASA, Mhandisi Fabian Maganga akizungumzia utekelezawaji wa mradi, alisema unatekelezwa kupitia Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji (WSDP) na Programu ndogo ya maji na usafi wa mazingira vijijini (RWSSP) kwa gharama ya Shilingi Bilioni 5.2.

Mhandisi Maganga alisema mradi umelenga kuwaondoshea kero ya maji wananchi wa Kata za Ilolompya, Mboliboli, Itunundu na Mlenge waliopo katika vijiji 14 na kwamba utanufaisha wakazi wapatao 30,258.

Mara baada ya kamilisha ziara yake kwenye mradi wa Pawaga-Mlenge, Naibu Katibu Mkuu, Mhandisi Sanga alihitimisha ziara yake kwenye mradi wa Tenki la Ilula la lita 500,000 ambalo linahudumia zaidi ya wakazi 35,000 kutoka Kata za Nyalumbu na Ilula ambapo alisisitiza kutazama namna ya kupanua utoaji wa huduma kwa maeneo mengine ya jirani.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger