Wednesday, 15 July 2020

MWENYEKITI WA CHAMA CHA WALIMU MANISPAA YA SHINYANGA MESHACK MASHIGALA AJITOSA KUWANIA UBUNGE SHINYANGA MJINI


Mwenyekiti wa Chama Cha Walimu Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga,Mwalimu Meshack Elias Mashigala amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya Kuwania nafasi ya Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mwalimu Meshack Elias Mashigala leo Jumatano Julai 15 amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kupitishwa na chama chake kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.
Mwenyekiti wa Chama Cha Walimu Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga,Mwalimu Meshack Elias Mashigala akionesha fomu ya kuomba ridhaa ya Kuwania nafasi ya Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM.

Share:

Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda Achukuwa Fomu Kuwania Ubunge Jimbo La Kigamboni

MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda leo Julai 15 amechukuwa Fomu ya kuomba ridhaa ya Kuwania nafasi ya Ubunge Jimbo la Kigamboni kupitia tiketi ya Chama cha mapinduzi CCM.


Share:

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Achukua Fomu Za Kuwania Tena Ubunge Wa Ruangwa

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na Mkewe Mary Majaliwa wakikaribishwa na Katibu wa CCM wa Wilaya  ya Ruangwa, Barnabas Essau (kulia) wakati walipowasili kwenye Ofisi ya CCM ya wilaya hiyo kuchukua fomu za kuwania tena Ubunge wa Jimbo la Ruangwa, Julai 15, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)




Share:

Upande wa Serikali Wapinga Wadhamini wa Tundu Lissu Kujiondoa

Upande wa Jamhuri umewasilisha pingamizi la awali mahakamani kupinga maombi yaliyowasilishwa na wadhamini Ibrahim Ahmed na Robart Katula wa mbunge wa zamani wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, ukidai kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza na kutaka maombi hayo yatupwe.

Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wadhamini hao wamefungua maombi wakiitaka itoe hati ya kumkamata Lissu kwa kuwa wao wameshindwa kumpata.

Kesi hiyo imetajwa jana katika mahakama hiyo iliyoketi chini ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon, alidai kuwa upande wa Jamhuri unaomba maombi hayo kutupiliwa mbali kwa sababu mahakama hiyo haiwezi kushughulikia jambo hilo.

Alidai kuwa kupitia hati ya kiapo kinzani mahakama hiyo haiwezi kusikiliza na kutolea uamuzi wa maombi hayo ya walalamikaji na yatupwe.

Walalamikaji wanaomba mahakama itoe hati ya kumkamata Lissu kwa kuwa wameshindwa kumpata na kumfikisha mahakamani hapo.

Hati ya pingamizi la awali, iliwasilishwa mahakamani na Wankyo kwa sababu ndiye aliyepewa mamlaka ya kuendesha kesi ya msingi na maombi hayo.

Maombi hayo, yalipangwa jana mbele Hakimu Simba kwa ajili ya kusikiliza.

Hata hivyo, Wankyo aliomba mahakama itoe siku 14 ili aweze kujibu maombi hayo kwa njia ya maandishi.

Wankyo alidai kuwa anaomba siku hizo ili aweze kupitia jalada la kesi ya msingi na pia kupitia kesi mbalimbali ambazo zilishatolewa uamuzi.

Hata hivyo, mmoja wa wadhamini hao (Katula), aliomba muda wa kujibu pingamizi hilo na hakimu alisema kisheria pingamizi la awali ndiyo linatakiwa kuanza kusikilizwa.

Hakimu Simba aliwauliza wadhamini hao kama wanapingamizi na suala la upande wa Jamhuri kuwasilisha majibu yao kwa njia ya maandishi na waleta maombi walidai kuwa hawana pingamizi.

Alisema upande wa Jamhuri unatakiwa kuwasilisha majibu hao Julai 28, 2020, waleta maombi wanatakiwa kujibu hoja hizo Agosti 11, 2020, kama kuna majibu ya ziada yatawasilishwa Agosti 18, 2020 na kesi itatajwa Agosti 19, mwaka huu na kupangwa tarehe ya uamuzi.

Wankyo alidai katika majibu yake hati ya kiapo kilichowasilishwa mahakamani na waleta maombi hao kuwa Lissu aliruka dhamana toka tarehe ambayo alipona na kutoka hospitali.

Alidai kuwa wadhamini hao walikuwa na taarifa za kutosha mahali alipo kwa sababu ilitangazwa na alieleza hivyo hivyo mahakamani, kwamba wadhamini wa mshtakiwa namba mbili (Lissu) wana wajibu wa kuhakikisha kwamba anafika mahakamani kwa mujibu wa amri ya mahakama iliyotolewa Januari 20, mwaka huu na hakimu Simba.


Share:

Maalim Seif Sharif Hamad Arudisha Fomu ya Kugombea Urais Zanzibar

Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Maalim Seif Sharif Hamad leo amerudisha fomu kwenye ofisi za chama zilizopo Vuga Zanzibar yakuomba dhamana ya chama ya kuteuliwa kuwa mgombea Urais Zanzibar kwenye Uchaguzi wa Oktoba 2020.



Share:

COSOTA yahamia Rasmi Wizara ya Habari

Na Shamimu Nyaki –WHUSM
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe ameeleza kuwa lengo la kuihamisha Taasisi ya Hakimiliki (COSOTA) kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara kuja katika Wizara anayoisisimamia ni kuhakikisha wadau wa Sanaa wanapata huduma sehemu moja  kwa sababu asilimia 86% ya wadau wake ni Wasanii. 
 
Dkt. Mwakyembe ameyasema hayo jana Jijini Dodoma katika Mkutano na Waandishi wa habari ambapo amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli jana tarehe 13/07/2020 amesaini Waraka unaogawa majukumu kwa wizara kuruhusu mabadiliko hayo muhimu ambayo yanawagusa wabunifu,watunzi  waandishi wa vitabu,kazi za Sanaa na Sanaa na jadi. 
 
“Namuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hii ndani ya saa ishirini na nne awe amekutana na Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara ili waweze kukabidhiana nyaraka muhimu za uendeshaji wa COSOTA”alisema Dkt.Mwakyembe. 
 
Aidha Waziri huyo ameeleza kuwa ujio wa COSOTA katika Wizara ya Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo utarahisisha ushirikiano na Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) katika kulinda na kusimamia maslahi ya wasanii wa filamu na muziki pamoja na kupanua wigo wa malipo na stahili za wasanii kwa kazi zao katika majukwaa mbalimbali ya Sanaa kielektroniki. 
 
Mhe.Waziri amesisitiza kuwa lazima COSOTA ya sasa iingie mikataba na nchi za nje ambazo vyombo vyake vya habari vimekua vikipiga muziki wa wasanii wa Tanzania bila kuwapatia gawio au kufaidika kwa namna yoyote ile. 
 
…MWISHO..


Share:

Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Profesa Kitila Mkumbo na Aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Kigoma Brig. Jenerali Emmanuel Maganga Wajitosa Ubunge CCM

Aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Kigoma Brig. Jenerali Emmanuel Maganga amekabidhiwa fomu ya kuwania kuteuliwa kugombea Ubunge Jimbo la Mvomero  huku Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Prof. Kitila Mkumbo, akichukua fomu kugombea Ubunge katika Jimbo la Ubungo kupitia CCM


Profesa Mkumbo amekabidhiwa fomu leo Jumatano tarehe 15 Julai 2020 katika ofisi ya wilaya ya Ubungo na Katibu wa CCM Wilaya yhiyo, Sylvester Yared.

Mbunge anayemaliza muda wake wa jimbo hilo ni Saed Kubenea wa Chadema




Share:

Katibu Mkuu CHADEMA John Myika Atangaza Kutogombea Ubunge Uchaguzi wa Mwaka huu 2020

Katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John  Myika,  amesema hatagombea ubunge, katika jimbo la Kibamba jijini Dar es Salaam

Mnyika ambaye amekuwa mbunge wa Kibamba ambayo ilikuwa sehemu ya jimbo la Ubungo, kwa miaka 10 mfululizo, amesema amechukua hatua hiyo ili  apate muda wa kutosha kutumikia nafasi yake ya sasa ya Katibu Mkuu CHADEMA.

"Haya nilisema kabla ya kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu 2019, Nyerere aliwahi kuachia Uwaziri Mkuu akabaki kuimarisha TANU, nami sitagombea ubunge 2020, nitumikie ipasavyo Ukatibu Mkuu CHADEMA tushinde chaguzi." - ameandika John Mnyika, Katibu Mkuu CHADEMA kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Mnyika alichaguliwa kuwa katibu mkuu wa chama hicho Desemba mwaka 2019 akichukua nafasi ya Dk. Vicent Mashinji ambaye jina lake halikupendekezwa na Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa chama hicho .

Katika mkutano wa kura za maoni uliyofanyika  jana Jumanne, tarehe 14 Juni 2020, Ernest Mgawe, mwenyekiti wa Chadema katika jimbo la Kibamba, alitangazwa mshindi. Mgawe alipata kura 30, kati ya 71 zilizopigwa.


Share:

Washindi wa uchaguzi kwenye kura za maoni za Ubunge wa CHADEMA waliopita kwenye majimbo yao

Washindi wa uchaguzi kwenye kura za maoni za Ubunge wa CHADEMA waliopita kwenye majimbo yao ni  kama ifuatavyo:

1.Mshindi Jimbo la Kawe ni Halima Mdee mwenye kura 63  (71.5%).

2.  Tarime Mjini mshindi ni Esther Matiko mwenye kura 80 (97. 6%) 

3. Tarime Vijijini mshindi ni John Heche ambaye amepata kura 268 (99.2%) .

-Heche alikuwa Mgombea pekee na alihitaji tu kura za Ndio au Hapana, kwenye kura zilizopigwa, kura za Ndio ni 268 (99.2%),zilizoharibika ni 2 (0.74%) hakuna kura ya Hapana

4. Mshindi Jimbo la Bunda Mjini ni Ester Bulaya mwenye kura 126 

5. Jimbo la Iramba mshindi ni Jesca Kishoa mwenye kura 134 (98%) .

- Jesca alikuwa Mgombea pekee na alihitaji tu kura za Ndio au Hapana, kwenye kura 136 zilizopigwa, kura za Ndio ni 134 (98%), zilizoharibika ni 2 na hakuna kura ya Hapana.

6. Jimbo la Isimani mshindi ni Patrick Ole Sosopi mwenye kura 115 (82.6%).

7.Mshindi jimbo la Mbeya Mjini ni Joseph Mbilinyi (Sugu) mwenye kura 294

- Sugu alikuwa ni Mgombea pekee na alihitaji tu kura za Ndio au Hapana ambapo amepata Ndio 294 na Hapana 5.


Share:

HEAD AND CHAIR OF SURGERY Job vacancy at Aga Khan Health Service July 2020

HEAD AND CHAIR OF SURGERY Job vacancy at Aga Khan Health Service July 2020 The Aga Khan Health Service, Tanzania (AKHST) an institution of The Aga Khan Development Network, has completed a major expansion of the Aga Khan Hospital, Dar es Salaam. This expansion aims at enhancing the Hospital’s facilities, technology and capacity which will […]

The post HEAD AND CHAIR OF SURGERY Job vacancy at Aga Khan Health Service July 2020 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Sales and Marketing Officer Job Opportunity at HLB MEKONSULT July 2020

About the Vacancy HLB MEKONSULT on behalf of one of our intriguing clients, has a thrilling opportunity for a motivated Sales and Marketing person to join its friendly, supportive and thriving team environment that will nurture your skills and significantly contribute to your professional development and career growth. We welcome applications from experienced background to join the […]

The post Sales and Marketing Officer Job Opportunity at HLB MEKONSULT July 2020 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Teacher – Education Job vacancy at Kazini Kwetu Limited July 2020

Teacher – Education Job vacancy at Kazini Kwetu Limited July 2020 Responsibilities: Develop and issue educational content including notes, tests, and assignments. Supervise classes to ensure all students are learning in a safe and productive environment. Organize supplies and resources for lectures and presentations. Deliver personalized instruction to each student by encouraging interactive learning. Plan […]

The post Teacher – Education Job vacancy at Kazini Kwetu Limited July 2020 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

TB ADVISOR at MDH Boresha Afya Project July 2020

Management and Development for Health (MDH) is a non-profit, non-governmental organization whose primary aim is to contribute to address public health priorities in Tanzania and world at large. The priorities include: HIV/AIDS, Tuberculosis, Malaria; Reproductive, Maternal, New-born and Child health (RMNCH), Nutrition; Non-Communicable Diseases of public health significance; as well as Health System Strengthening. MDH […]

The post TB ADVISOR at MDH Boresha Afya Project July 2020 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

FACILITY BASED TRACKER JOBS (3) at MDH Boresha Afya Project July 2020

FACILITY BASED TRACKER (3) at MDH July, 2020 In Dar es Salaam, MDH supports the Government of Tanzania through the Regional Government and Municipal councils of Ilala, Temeke, Kinondoni, Ubungo and Kigamboni in the provision of comprehensive facility-based HIV prevention, care and treatment services and program management. In order to strengthen care and treatment of […]

The post FACILITY BASED TRACKER JOBS (3) at MDH Boresha Afya Project July 2020 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Director of Operations Job vacancy at Tanzanian Children’s Fund July 2020

Tanzanian Children’s Fund (TCF) is looking for a compassionate, committed, dynamic, and experienced partner to help lead operations at the Rift Valley Children’s Village (Children’s Village) in the Karatu region of northern Tanzania. The Tanzanian Children’s Fund provides a loving and permanent home to 102 marginalized children living at the Rift Valley Children’s Village. They […]

The post Director of Operations Job vacancy at Tanzanian Children’s Fund July 2020 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Senior Technical Advisor at PSI July 2020

Job title: Senior Technical Advisor Department: PMI Impact Malaria project in Tanzania Based at PSI in Dar es Salaam, Tanzania Reports to the Chief of Party   Who we are As the flagship global service delivery project of the U.S. President’s Malaria Initiative (PMI), the PMI Impact Malaria team works with national malaria programs to fight malaria and save […]

The post Senior Technical Advisor at PSI July 2020 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Serikali Kuendelea Kununua Mazao Ya Wakulima

Wakulima nchini wamehakikishiwa kuwa serikali itaendelea kununua mazao yao kwa ajili ya kuongeza hifadhi ya kutosha ili kuwa na uhakika na usalama wa chakula nchini.

Kauli hii ya serikali imetolewa jana wilayani Mbalali na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya wakati alipotembelea kituo cha ununuzi zao la mpunga kijiji cha Uturo unaofanywa na Wakala wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula ( NFRA) kanda ya Makambako

“Serikali kupitia wizara ya Kilimo itaendelea kununua mazao ya wakulima hususan mahindi na mpunga kwa wingi hivyo wakulima msidanganywe kuwa muda umebaki mfupi wa kupeleka mazao yenu NFRA. Leteni hapa mpunga wenu tutaununua wote” alisema Kusaya.

Akiwa katika ghala la Ushirika Uturo Mbarali Katibu Mkuu huyo aliongea na wakulima wa mpunga na kuwahakikishia kuwa wizara imejipanga kuona nchi inaendelea kuwa na usalama wa chakula ndio maana anapita mikoani kujionea hali ya uzalishaji mazao

Kwa mujibu wa Kaimu Meneja wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Makambako Frank Felix alisema tayari wakala umeshanunua tani 1,700 za mpunga kati ya malengo ya tani 5,000 na mahindi tani 2,933.174 kati 25,000 msimu huu.

Akizungumza kwa niaba ya wakulima wa mpunga Mbarali Said Nkenja alishukuru Serikali kwa uamuzi wake wa kununua mpunga kwani umesaidia kuongeza ushindani wa bei sokoni.

“Tunamshukuru sana Rais Dkt.John Pombe Magufuli kwa uongozi wake unaowajali wakulima nchin.Leo Mbarali tunafurahia kuuza mpunga kwa NFRA tena bei ni nzuri .Tunaomba iendelee kununua zaidi mpunga upo mwingi tunavuna bado” alisema mkulima Said Nkenja.

Katika hatua nyingine  Katibu Mkuu Kusaya alitembelea  Chuo cha mafunzo ya Kilimo na Mifugo  ( MAMRE) cha Wanging’ombe mkoani Njombe  na kutoa agizo kuwa wanafunzi wanaoshindwa kulipa ada ya mafunzo wasifukuze badala yake utafutwe utaratibu rafiki.

Kusaya alitoa agizo hilo kufuatia malalamiko ya wanafunzi kusema baadhi yao wameshindwa kuendelea na masomo baada ya kushindwa kulipa ada na michango mingine.

“Vyuo vyote 29 ( 14 vya serikali na 15 vya binafsi) ni vyangu kwani vinalenga kuzalisha maafisa ugani watakaokwenda kuhudumia wakulima nchini.Nitaendelela kuvisaidia bila kuangalia nani  anakimiliki muhimu vitoe mafunzo bora kwa wanafunzi wa kitanzania” alisema Kusaya.

Kusaya aliusihi uongozi wa chuo cha MAMRE  kutafuta njia rafiki kuwasaidia wanafunzi wenye mazingira magumu yanayosababisha kutolipa ada kwa muda.

Katika ziara hiyo Katibu Mkuu huyo ameahidi kutoa kompyuta  ili kuwezesha kuanzisha maktaba mtandao ( e- learning) na kugharimia mwanafunzi mmoja kwenda kujifunza kanuni bora za ufugaji kuku kisasa katika vhuo cha Ihemi Iringa kwa gharama za serikali.

Katibu Mkuu amesema katika kuboresha mafunzo kwa vitendo atakipatia Chuo hicho Kitalu nyumba moja (Green House) ili wafundishe klimo cha mbogamboga na matunda ( horticulture).

Chuo cha MAMRE kina wanafunzi 103 wa ngazi ya astashahada na stashahada.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Chuo hicho Geofrey  Mapesa alisema changamoto kubwa Kwa sasa ni kukosekana kwa mfumo wa udahili wa pamoja ( Central Admission System) hali inayopelekea upungufu wa wanafunzi.

Tayari wanafunzi 169 wamehitimu mafunzo ya kilimo na mifugo tangu chuo hicho kilipoanzishwa mwaka 2014 chini ya Kanisa Katoliki Jimbo la Njombe.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger