Monday, 6 July 2020
Rais Magufuli awasimamisha kazi viongozi wa polisi, Afisa Usalama kwa uzembe
Rais Magufuli ameagiza kusimamishwa kazi kwa Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Arumeru na Afisa Usalama wa Wilaya hiyo mkoani Arusha kwa kushindwa kutumiza majukumu yao.
Akizungumza wakati wa kuwaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni, Rais Magufuli amesema kuwa viongozi hao wameshindwa kutimiza wajibu wao wa kukabiliana na dawa za kulevya, hadi maofisa kutoka makao makuu walipofika na kubaini uwepo wa kiwango kikubwa cha bangi.
Wakati huo huo, Rais Magufuli amempandisha cheo James Kaji kuwa Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ambapo awali alikuwa akikaimu nafasi hiyo.
Akitangaza uamuzi huo wa kumthibitisha Kaji pamoja na kumuapisha, Rais Magufuli amesema anachotaka kuona ni matokeo ya kazi wanazofanya wasaidizi wake.
Monitoring & Evaluation Officer Job vacancy at Plan International
The Organisation Plan International is an independent development and humanitarian organisation that advances children’s rights and equality for girls. We believe in the power and potential of every child. But this is often suppressed by poverty, violence, exclusion and discrimination. And it’s girls who are most affected. Working together with children, young people, our supporters […]
The post Monitoring & Evaluation Officer Job vacancy at Plan International appeared first on Udahiliportal.com.
RAIS DKT MAGUFULI AMEWAAPISHA VIONGOZI MBALIMBALI ALIOWATEUA IKULU CHAMWINO JIJINI DODOMA LEO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Bi. Mriam Perla Mbaga kuwa Katibu Tawala wa mkloa wa Simiyu kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Dodoma Julai 6, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha baada ya kumthibitisha Bw. James Kaji kuwa Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Udhibiti wa Dawa za Kulevya nchini (DCEA) kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha wa Polisi Thobias Emir Andengenye kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Dodoma
Wateuliwa wakila kiapo cha maadili ya Viongozi mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea baada ya kuwaapisha viongozi mbalimbali aliowateua kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti akimuapisha Kanali Mathias Kahabi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia Mkuu wa Morogoro Mhe. Loatha Ole Sanare akimuapisha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza (SACP) Ismail Twahir Mlawa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo kwenye haflailiyofanyika Ikulu Chamwino Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia Mkuu wa Mkoa wa Pwani akimuapisha Mhandisi Martine Ntemo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kibaha kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Dodoma Julai 6, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea mara baada ya kuwaapisha viongozi aliowateuwa katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiondoka sehemu ya tukio baada ya kuwaapisha viongozi aliowateuwa katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma
PICHA NA IKULU
IGP SIRO AWAPA MTIHANI WAKUU WA POLISI WILAYA NCHINI.
MKUU wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro kulia akionyeshwa michoro mbalimbali ya kituo cha Polisi cha zamani wilayani Pangani na Mkuu wa Polisi wilaya ya Pangani (OCD) Georgina Matagi wakati alipokwenda kuwashukuru wasamaria wema wilayani humo waliojitolea ujenzi wa kituo cha Polisi ili kutokomeza uhalifu
Sehemu ya wadau wa maendeleo wilayani Pangani wakimsikiliza kwa umakini Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro
MKUU wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro kushoto akipata maelezo mapokezi wakati alipoingia kwenye kituo cha Polisi Pangani akiwa na kulia Mkuu wa Polisi wilaya ya Pangani (OCD) Georgina Matagi na Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassani Nyange
Awali akizungumza Kaimu Mkuu wa wilaya ya Pangani Mhandisi Mwanasha Tumbo ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Muheza alisema huo ni utekelezaji wa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli kupitia CCM kwamba lazima askari wawe na maeneo mazuri ya kufanyia kazi na wananchi waweze kupata huduma nzuri wadau hao wamejitolea kwa kushirikiana na serikali kazi kubwa imefanyika
Sehemu ya wadau wa maendeleo wilayani Pangani wakimsikiliza kwa umakini Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro
Sehemu ya wadau wa maendeleo wilayani Pangani wakimsikiliza kwa umakini Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro
MKUU wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro kushoto akipata maelezo mapokezi wakati alipoingia kwenye kituo cha Polisi Pangani akiwa na kulia Mkuu wa Polisi wilaya ya Pangani (OCD) Georgina Matagi na Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassani Nyange
MKUU wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro akikitembelea kituo cha Polisi Pangani wakati alipokwenda kuwashukuru wasamaria wema kwa kujitokea kufanikisha ujenzi wa kituo cha Polisi kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi wilaya ya Pangani (OCD) Georgina Matagi
MKUU wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amewapa mtihani mkubwa wakuu wa Polisi wa wilaya nchini (OCD) ambao watakutwa kwenye maeneo yao hawajafanya jambo lolote la kimaendeleo atalazimika kuondokana nao kutokana na kwamba watakuwa hawana tija.
IGP Siro aliyasema hayo wakati alipofika wilayani Pangani kwa lengo la kuwashukuru wasamaria wema waliojitolea kufanikisha ujenzi wa kituo cha Polisi wilayani humo juhudi ambazo zimefanywa na Mkuu wa Polisi wa wilaya hiyo Georgina Matagi.
Alisema kwamba kazi kubwa iliyofanywa na Mkuu huyo wa Polisi wilaya kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo inapaswa kuigwa na wakuu wengine hapa nchini huku akiwataka kuacha kuwa watu wa kulialia bali wahakikishe wanakuwa wabunifu kwa kuiga mfano wa OCD wa Pangani.
“MaOCD msiwe watu wa kulia muwe wabunifu kuiga mfano wa Mkuu wa Polisi Pangani (OCD) huku akimtaka kuendelea hivyo hivyo kwa sababu kwani kuna ma ocd mawe hawafikirii namna ya kusaidia jeshi anachojua ni kumsubiri IGP ampelekee fedha…IGP yupo sawa,Amri Jeshi Mkuu yupo,wewewni ODC na RPC kuna vitu unaaweza kujiongeza kwa kuwatumia wadau werevu kuweza kusaidia”Alisema IGP Siro.
“Lakini pia OCD umenipa changmoto mimi niko smati sana sijua imekuwaje nikaisahau Pangani mpaka wewe bwana mdogo ukaja kufanya hii kazi nzuri hongera sana kwa kazi kubwa na nzuri ya kuhakikisha ujenzi huo unafanyika na kukamilika “Alisema
Aidha aliwashukuru wadau hao na OCD kwa kazi kubwa ya kulisaidia Jeshi la Polisi kujenga kituo hicho huku akiwaambie kwamba walichokifanya kwa faida ya watanzania wote kwa kuacha alama ya kesho na kesho kutwa haupo watu watakukumbuka hivyo kwa niaba ya Rais niwashukur sana kwa kazi nzuri mliyofanya kituo hiki huku nyuma hahakikuwa hivi msione mmepoteza bali mmeongeza fursa.
Hata hivyo alisema kwamba kuna vitu ambavyo havijakamilika hivyo nitatoa milioni tano huku akiwaomba wadau wa maendeleo nchi nzima walisaidie Jeshi la Polisi kwa sababu usalama ndio kila kitu wanakwenda msikitini na kanisani kwa sababu ya usalama na usipokuwepo ni hatari hivyo kila mtu ambaye mungu amemjalia kipato akiona mahali kuna shida ya kituo cha Polisi asaidie,kwani vituo hivyo vitawasaidia.
Akizungumzia suala la usalama IGP Siro alisema suala hilo ni muhimu sana na ukishavurujika ni vigumu sana kuweza kuurudisha huku akitolea mfano watu wa msumbuji kwa sabau usalama haupo hapa ni mpakani wakati wa uchaguzi watu wenye nia mbaya wanaweza kuleta mambo ya hivyohovyo watoe taarifa wasimuamini kila mtu ni vuzuri wakavijulisha vyombo vya ulinzi na usalama.
Alisema kwamba wakati wa uchaguzi lolote linaweza kufanyika wabaya wetu wakachukua nafasi kufanya mambo maovu wanaweza kuingia hivyo niwaombe mkiona ya namna hiyo hakikisheni mnatoa taarifa kwenye vyombo vinavyohusika ili kuweza kufanyiwa kazi mambo hayo.
Hata hivyo alisema usalama watanzania walioukuta wajitahidi sana kuulinda huku akisema wachache wanaotaka kuleta figisufigisu watahakikisha wanashughulikiwa na kurudishwa kwenye mstari.
Mtandao Wa Maji Ruangwa Wamtua ‘wamtua Ndoo Mama Kichwani’
Na Mwandishi Wetu, MAELEZO
SERIKALI kupitia Wizara ya Maji imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maji katika maeneo ya mijini na vijijini kupitia Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji kwa mujibu wa Sera ya Taifa ya Maji ya mwaka 2002.
Sera ya Taifa ya Maji ya mwaka 2002 inaelekeza kuwapatia wananchi waishio vijijini maji safi na salama katika umbali usiozidi mita 400 kutoka kwenye makazi yao, hatua inayolenga kuwaondelea changamoto mbalimbali ikiwemo maskini na magonjwa yanayosababishwa na maji.
Wizara ya Maji kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeendelea kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi waishio vijijini kwa kujenga, kupanua na kukarabati miradi ya maji, lengo ikiwa ni kufikia asilimia 85 ya wananchi wanaopata huduma ya maji safi na salama katika maeneo ya vijijini ifikapo mwaka 2020.
Miradi ya Maji Vijijini inatekelezwa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kushirikiana na wananchi pamoja na sekta binafsi ambapo katika kuwapunguzia wananchi gharama, Serikali kwa kushirikiana na wadau inaandaa mifumo itakayofaa kusimamia na kuendesha miradi ya maji ikiwa ni pamoja na kuviimarisha Vyombo vya Watumiaji Maji.
Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi inatekeleza miradi mbalimbali ya maji katika vijiji mbalimbali vya Wilaya hiyo hatua inayolenga katika kutoa huduma endelevu kwa wakazi waishio mijini na pembezoni mwa miji.
Wananchi wanaendelea kupata huduma ya maji safi na salama kutoka katika vyanzo vya Visima vifupi, Visima vya kati, Visima virefu ambavyo vimefungwa pampu za mikono, miradi ya maji bomba ya maporomoko na miradi ya maji ya kusukumwa na mitambo.
Tangu kuingia madarakani kwa Serikali ya Awamu ya Tano, hali ya upatikanaji wa huduma ya maji vijijini imeongezeka kutoka 38.5% mwaka 2015 hadi kufikia 51.20% kufikia mwezi Novemba, 2018 ikiwa ni ongezeko la 12.7% ambapo jumla watu 64,498 waishio vijijini wanapata huduma ya maji.
Miongoni mwa miradi hiyo ni pamoja na Mradi wa Maji wa Naunambe-Mpekenyera unaosimamiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kwa kushirikiana na Kamati za Vijiji vya Naunambe na Mpekenyera katika kuhakikisha kuwa Serikali inamtua mama ndoo kichwani na kumuondolea changamoto ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya maji.
Kufuatia juhudi kubwa zilizofanywa na Serikali ya Wilaya ya Ruangwa mradi huo ulikamilika mwezi Juni, 2018 na jumla wananchi 7,000 wameanza kupata maji na salama na kiasi Tsh. Milioni 828 zimetumika kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo, ikiwemo ununuzi wa vifaa mbalimbali ikiwemo mashine za kusafisha maji na miundombinu mbalimbali kwa ajili ya kurahisisha upatikanaji wa maji kutoka katika vyanzo na kuwafikia wananchi.
Akizungumza na Timu ya Maafisa Habari wa Idara ya Habari (MAELEZO) waliofanya ziara Wilayani humo, hivi karibuni, Katibu wa Mradi huo, Selemani Nyamiri anasema mradi huo ulianza kuibuliwa na wananchi mwaka 2010 kwa kaya mbalimbali katika vijiji hivyo kuchangishana fedha kwa ajili ya kuhakikisha mradi huo unatoa huduma endelevu ya maji katika vijiji hivyo vyenye wakazi zaidi ya 10,000.
‘Maji yaliyokuwa yakizalishwa katika chanzo cha Mpekenyeara yalikuwa yana chumvi sana, pia yalipatikana katika vyanzo visivyo safi na salama hivyo ilitulazimu kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya kwa ajili ya kutumia mafundi na utaalamu wa ziada ili kuhakikisha kuwa maji yanarejea katika ubora wake’’
Nyamiri anasema kwa sasa kiwango cha chumvi katika maji hayo kimepungua na kufanya maji hayo kuwa na ubora wa matumizi kwa binadamu, ambapo watumiaji wanalazimika kuchangia gharama ya Tsh. 200 kwa kila ndoo, ikiwa ni fedha zinazokusanywa na kamati hiyo kwa ajili ya kufanya matengenezo na ukarabati wa miundombinu ya mradi.
Akifafanua zaidi anasema wananchi wa vijiji hivyo wataendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali katika kuboresha huduma za maendeleo ya jamii ikiwemo huduma ya maji ambapo wananchi wamekuwa na mwamko wa kusimamia uhifadhi wa maeneo ya vyanzo vya maji ili kufanya vijiji vyote vinapata maji ya uhakika.
Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Naunambe Bi. Amina Abdalla aliipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kwa kusimamia utekelezaji wa mradi huo kwa kuwa umeondoa kero kwa akina mama wa vijiji hivyo waliokuwa wakisafiri umbali mrefu kutafuta huduma ya maji.
Bi. Rehema Mussa Mkazi wa Kijiji cha Mpekenyera alisema kwa kipindi cha nyuma hali ya upatikanaji wa huduma ya maji katika vijiji hivyo haikuwa ya kuridhisha, hususani wakati wa kipindi cha kiangazi na kuwalazimu wananchi wengi kutembea umbali wa kilometa 3 kufuata huduma ya maji katika vyanzo visivyo rasmi huku wakitembea na watoto migongoni.
‘Utekelezaji wa mradi huu ni mkombozi mkubwa sana kwetu wananchi wa Naunambe na Mpekenyera kwani kwa sasa shida ya maji imeisha, tunaipongeza Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli pamoja na juhudi kubwa zinazofanywa na Mbunge wetu wa Ruangwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa’’ alisema Rehema.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Andrea Chezue alisema hali ya upatikanaji wa maji katika Wilaya hiyo umefikia asilimia 55 huku kukisaliwa na maeneo machache ambayo yanakosa huduma ya maji ambapo Ofisi yake imekuwa ikiendelea na jitihada mbalimbali za kuhakikisha huduma ya maji inafikia walau asilimia 70 ifikapo mwishoni mwaka 2020.
‘Halmashauri ya Ruangwa inaendelea kutekeleza miradi mikubwa ya maji katika vijiji mbalimbali ikiwemo mradi wa maji wa Naunambe-Mpekenyera wananchi wanapata maji na wanafurahia huduma inayotolewa kwa mwaka 2019 pekee tulipata miradi minne ikiwemo mradi wa maji Kitandi na tayari tumeanza kufanya mawasiliano na Halmashauri ya Mtama kuhakikisha kuwa maji yanafikishwa katika vijiji jirani ikiwemo vijiji vya Nangumbu A na B’’ alisema Chezue.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maji Kata ya Mandawa Rashid Mshamu anasema mradi wa maji mandawa unahuhudumia jumla ya vijiji 5 vya Nahanga, Chikundi, Mandawa Chini, Mchichili na Mtondo unaogharimu kiasi cha Tsh. Bilioni 1.7 zilizotolewa na Serikali, ambapo mradi huo unawanufaisha jumla ya watu 13,756.
Anaongeza kuwa mradi huo ulioasisiwa mwaka 1975 ulikuwa na miundombinu chakavu na kusababisha kero kubwa kwa wananchi hususani wazee, wanawake na watoto ambapo walikuwa wanahangaika, ambapo Serikali iliamua kuufua mradi huo katika bajeti ya mwaka 2014/15.
Anasema kuwa kwa sasa mradi huo unaendelea vyema na huduma ya maji ni ya uhakika na wananchi wa vijiji hivyo wanalazimika kuchangia kiasi cha Tsh. 50 inayopelekwa katika mfuko wa maji wa kijiji hicho na kutumika kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya mradi.
Miradi mingine ya maji inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa ni pamoja na mradi wa maji Nanganga, mradi wa maji Likunja, mradi wa maji Namahema, mradi wa maji Chenjele, ambapo katika maeneo yote hali ya upatikanaji wa maji ni ya kurithisha.
Miradi mingine ni pamoja na ujenzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Mibure, Namakuku na Namahema ambao tayari umekamilika na jumla ya watu 6,133 wananufaika, ambapo kiasi cha Tsh. Milioni 631,593,444.50 zimetumika.
Serikali imewekeza katika miradi ya maji mikubwa na midogo ili kufikisha huduma ya maji kwa wananchi, ambapo uwekezaji huo umeleta mabadiliko makubwa katika sekta mbalimbali nchini na maisha ya wananchi kwa ujumla.
Ili kuleta matokeo tarajiwa utekelezaji wa ujenzi wa miradi ya maji hapa nchini unahusisha ushirikiano baina ya serikali na sekta binafsi na pia wadau wa maendeleo kutokana na ukweli kuwa Serikali imeweka lengo la kufakisha huduma ya maji kwa asilimia 85 kwa upande wa wananchi.
MWISHO
VIDEO: Tigo yaongeza tahadhari kwa wateja wanaotembelea Banda lao SabaSaba
Waziri Mkuu:Tutaendelea Kudhibiti Matumizi Ya Fedha Za Umma
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli itaendelea kudhibiti matumizi ya fedha za umma ili iweze kuendelea na ujenzi wa miradi ya kimkakati zikiwemo bandari kwa lengo la kuboresha maendeleo ya wananchi wake.
Pia, Waziri Mkuu amesema changamoto ya usafirishaji wa mizigo na abiria kati ya Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) itakuwa historia baada ya kuboreshwa na kujengwa kwa miundombinu ya bandari katika wa Ziwa Tanganyika ukiwemo upanuzi wa bandari ya Kasanga.
Waziri Mkuu aliyasema hayo jana jioni (Jumapili, Julai 05, 2020) alipozungumza na wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa upanuzi wa Bandari ya Kasanga iliyoko wilaya ya Kalambo akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Rukwa. Mradi huo unagharimu zaidi ya sh. bilioni 4.7.
Alisema upanuzi wa bandari hiyo utawezesha mizigo inayotoka nchini kwenda Congo kufika kwa wakati kwa sababu itasafirishwa moja kwa moja bila kupitia katika nchi nyingine kama ilivyo sasa, ambapo madereva wanalazimika kupita kwenye Mataifa mengine na kutumia muda mrefu.
“Mradi huu ukikamilika utaongeza pato la mwananchi mmoja mmoja pamoja na Taifa kwa ujumla. Rais Dkt. Magufuli amedhamiria kuboresha maendeleo ya wananchi nchi nzima ikiwemo na wilaya hii ya Kalambo. Ujenzi wa miradi hii unatoa fursa za ajira kwa wananchi, hivyo zichangamkieni.”
Vilevile, Waziri Mkuu alisema mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa bado yanaendelea nchini, hivyo mtu yeyote atakayebainika anajihusisha na masuala hayo atafutwe popote alipo akamatwe na achukuliwe hatua za kisheria kwa sababu rushwa ni adui wa haki.
Pia, Waziri Mkuu aliendelea kuwakumbusha watendaji ndani ya Serikali wahakikishe wananchi wanapofika katika maeneo yao ya kazi wawapokee, wawasikilize na kuwahudumia bila ya ubaguzi. “Hatuangalii sura wala kabila yeyote atakayekanyaga kwenye maeneo yenu ahudumiwe ipasavyo.”
Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe alisema Tanzania na Congo zimeungana kwa Ziwa Tanganyika, usafiri wa barabara uliokuwa unatumika awali uliyalazimu maroli ya mizigo kupitia nchini nyingine na kuchelewa kufika.
Alisema kukamilika kwa upanuzi wa bandari hiyo pamoja na ujenzi wa barabara kwa kiwago cha lami kutoka Sumbawanga hadi Kasanga kutarahisisha usafirishaji wa abiria na mizigo kwa kutumia bandari hiyo kuingia nchini Congo moja kwa moja bila kupita kwenye nchi juirani.
Waziri Kamwelwe alisema kuwa awali kulikuwa na changamoto ya barabara hali iliyosababisha meli kufika kwenye Bandari ya Kasanga na kulazimika kusibiri mizigo ambayo ilikuwa ikichelewa kufika kutokana na ubovu wa barabara na sasa tayari Serikali imeitatua kwa kuijenga kwa kiwango cha lami.
Awali, akitoa taarifa ya maendeleo ya mradi huo, Kaimu Katibu Mkuu wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Uchukuzi, Mhandisi Thomas Ngulima alisema mradi huo umeanzishwa ili kuongeza ushindani na tija katika shughuli za kibandari kusini mwa Ziwa Tanganyika.
Alisema mradi huo unahusisha upanuzi mkubwa wa gati ilililopo sasa lenye urefu wa mita 20 lifikie mita 120, ambazo zitawezesha kuhudumia meli mbili hadi sita kwa wakati. Kazi nyingine ni ujenzi wa miundombinu ya bandari ikiwemo jengo la kupumzikia abiria, mgahawa na nyumba za watumishi.
Mhandisi Ngulima alisema mradi huo unaojengwa na kampuni ya Inter-Consult Limited umefikia asilimia 70 na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Septemba, 2020 na kwamba utafungua na kuboresha njia ya biashara ya mazao ya chakula katika nchi za DRC, Burudi na Zambia.
Aliongeza kuwa, ujenzi wa barabara ya kimkakati inayoanzia Manispaa ya Sumbawanga hadi Kasanga (km 107), pamoja na upanuzi wa bandari unaoendelea, utawezesha mtiririko wa shehena za saruji, makaa ya mawe, chokaa na sabuni kuongezeka hivyo kukuza uchumi wa wananchi na Taifa.
VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA WATAKIWA KUWACHUJA WAGOMBEA, MAGUFULI AMWAGIWA SIFA
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uimarishaji wa Maadili na Usaidizi Katika Utumishi wa Umma na wa Binafsi (WoLaOTa) Samwel Olesaitabau akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi wa taasisi hiyo iliyofanyika mkoani Singida jana.
Waandishi wa habari wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa taasisi hiyo.
Na Dotto Mwaibale, Singida
VIONGOZI wa vyama vya kisiasa wametakiwa kuhakikisha wote wanaoomba nafasi ya uongozi wanachujwa ipasavyo ili kusaidia kupunguza viongozi wala rushwa nchini.
Ombi hilo limetolewa na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uimarishaji wa Maadili na Usaidizi Katika Utumishi wa Umma na wa Binafsi (WoLaOTa) Samwel Olesaitabau wakati wa hafla ya uzinduzi wa taasisi hiyo iliyofanyika mkoani hapa jana.
Katika hatua nyingine Olesaitabau amewaomba viongozi wa dini kote nchini kutenga muda katika ibada zao hata kwa dakika tano kuiombea Nchi na Uchaguzi Mkuu wa 2020 hata kwa wale wasio na dini rasmi wanaoabudu mawe au milima nao wafanye hivyo.
"Mwaka huu kuna uchaguzi na niwaombe sana viongozi wote wa vyama vya kisiasa kikiwemo chama Tawala cha CCM kuhakikisha wote wanaoomba uongozi wamechujwa ipasavyo na wasiwe na huruma na wakifanya hivyo basi kwa vyovyote vile tutapunguza viongozi wala rushwa Serikalini" alisema Olesaitabau.
Akizungumzia kusudi la kuanzisha taasisi hiyo alisema ni kusaidia uongozi wa nchi yetu kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli kama aalivyoonesha Rais John Magufuli.
Aidha Olesaitabau alisema dira ya taasisi hiyo ya kipekee hapa nchini ni utoaji wa elimu ya kuimarisha maadili kwa waajiri, na watumishi wa sekta za umma na binafsi Tanzania Bara ili watumie Ueledi na Taaluma zao kwa kuleta matokeo chanya.
Olesaitabau akizungumzia baadhi ya sifa kati ya 35 alizoziona za utendaji kazi wa Rais Dkt. John Magufuli alisema ni kiongozi ambaye ana uwezo wa kuamua jambo na kulisimamia kuanzia mwanzo hadi mwisho na kuwa hayumbishwi na kelele ama za ndani ya nchi au hata nje kwa jambo ambalo amelianzisha kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.
Alitaja sifa nyingine kuwa anaichukia rushwa na anapenda kila mtu afanye kazi ya kujipatia kipato kwa jasho lake mwenyewe bila ya kumdhulumu mwingine na kuwa ana uwezo wa kuweka kumbukumbu/ takwimu kiusahihi katika kichwa chake kwa muda mrefu bila ya kusahau.