Friday, 3 July 2020

Taarifa Kwa Umma Kutoka Mamlaka ya Mawasiliano -TCRA:Ufafanuzi wa URASIMISHAJI wa Laini za Ziada katika Mtandao Mmoja

1.0 UTANGULIZI
Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Usajili wa Laini za Simu) za mwaka 2020, yaani “The Electronic and Postal Communications (SIM Card Registration) Regulations, 2020”, zimeainisha katika Kanuni ya 18 kuwa:-

18 (1) Mtu anayehitaji kumiliki na kutumia laini ya simu ataruhusiwa kusajili:-

(a) Kama ni mtu binafsi

    Idadi ya laini moja kwa kila mtoa huduma za mawasiliano kwa ajili ya kupiga simu za sauti, kutuma ujumbe mfupi pamoja na matumizi ya data;
    Idadi ya laini zisizozidi nne kwa kila mtoa huduma za mawasiliano

kwa matumizi ya mawasiliano kati ya mashine na mashine; na

(b) Kama ni Kampuni au Taasisi

    Idadi ya laini zisizozidi thelathini kwa kila mtoa huduma za mawasiliano kwa ajili ya kupiga simu za sauti, kutuma ujumbe mfupi pamoja na matumizi ya data;
    Idadi ya laini zisizozidi hamsini kwa kila mtoa huduma za mawasiliano kwa matumizi ya mawasiliano kati ya mashine na mashine.

(2) Laini zilizosajiliwa kwa matumizi yaliyoainishwa kwenye Kanuni 18 (1) (a) hazipaswi kutumiwa kwa kubadilishana (interchangebly).

(3) Bila kujali Kanuni ya 18 (1), Mtu binafsi, Kampuni au Taasisi inaweza kuruhusiwa kusajili na kumiliki laini zaidi ya zilizoainishwa kwa kuomba na kupata idhini kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania

(4) Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya Kanuni hizi, atakuwa ametenda kosa la jinai.

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inapenda kuutaarifu umma kwamba zoezi la kuomba idhini ya umiliki wa laini za simu zaidi ya moja katika mtandao mmoja linaendelea. Tunawashauri wamiliki wa laini za mawasiliano ya simu kuendelea kuhakiki usajili wa laini zao zote wanazomiliki.

2.0 KUTHIBITISHA IDADI YA LAINI ZILIZOSAJILIWA KUTUMIA KITAMBULISHO CHA TAIFA (NIDA)

2.1 Kila mmiliki wa laini ya simu anatakiwa kupiga namba *106# na kuangalia usajili wa laini anazomiliki na endapo atakuta namba ambayo haitambui na imesajiliwa kwa kutumia namba ya kitambulisho chake cha Taifa anashauriwa kuwasiliana na mtoa huduma wake ili azifunge mara moja kuepusha matumizi mabaya na kumsababishia usumbufu usiokuwa wa lazima utakaojitokeza.

2.2 Kwa wale ambao kwa sasa wanamiliki laini zaidi ya moja katika mtandao mmoja, mwisho wa kuhakiki laini zao itakuwa tarehe 31 Julai 2020.

2.3 Utaratibu wa kuomba idhini ya kumiliki laini mpya za ziada katika mtandao mmoja unaendelea na mteja anaweza kupata huduma hii kupitia kwa wakala au kwenye ofisi za watoa huduma ambapo kwa kutumia njia za kielektroniki mtoa huduma atawasilisha maombi ya mteja wake TCRA kwa idhini ya kusajili na kumiliki laini za ziada; mteja atapokea majibu ya maombi yake ndani ya takribani dakika tano.

3.0 URASIMISHAJI WA LAINI ULIZOTHIBITISHA

3.1 Urasimishaji wa laini za ziada kwa sasa unaweza kufanyika kwa wakala au kwenye ofisi za watoa huduma ambapo kwa kutumia njia za kielektroniki ambapo mtoa huduma atawasilisha maombi yake ya idhini ya kurasimisha laini za ziada TCRA na kupokea majibu ndani ya takribani dakika tano; au

3.2 Kwa kupitia namba *106# ambapo wewe mwenyewe utaweza kuomba idhini ya kurasimisha kutoka TCRA kupitia simu yako. Huduma hii ya kurasimisha kwa njia ya simu yako itaanza kutumika rasmi Agosti 1, 2020.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu, 
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)




Share:

Breaking News : RAIS MAGUFULI ATEUA WAKUU WA MIKOA NA WAKUU WA WILAYA WAPYA... AGGREY MWANRI, KUPUMZIKA,ANDENGENYE ALAMBA KIGOMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo Ijumaa Julai 3,2020 amefanya uteuzi wa Wakuu wa mikoa wawili ambapo amemteua Dkt. Philemon Sengati kuwa mkuu wa mkoa wa Tabora kuchukua nafasi ya Bw. Aggrey Mwanri ambaye amestaafu huku akimteua Bw. Thobias Andengenye (aliyewahi kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji) kuwa Mkuu wa mkoa wa Kigoma kuchukua nafasi ya Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga ambaye amestaafu.

Rais Magufuli pia ameteua wakuu wa wilaya 9
1. Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza (SACP) Ismail Twahir Mlawa kuwa mkuu wa wilaya ya Kilombero kuchukua nafasi ya James Mugendi ambaye amestaafu.
2. Jamila Yusuph kuwa Mkuu wa wilaya ya Mpanda mkoani Katavi kuchukua nafasi ya Lilian Charles Matinga ambaye amestaafu.

3. Mhandisi Martine Ntemo kuwa mkuu wa wilaya ya Kibaha mkoani Pwani kuchukua nafasi ya Asumpter Nshunju Mshama ambaye amestaafu.

4. Salum Kali kuwa mkuu wa wilaya ya Magu mkoani Mwanza akichukua nafasi ya Dkt. Philemon Sengati ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa mkoa wa Tabora.

5. Wilson Samwel Shimo kuwa mkuu wa wilaya ya Nyang'wale mkoani Geita.

6. Kanali Mathias Kahabi kuwa Mkuu wa wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera kuchukua nafasi ya Saada Malunde ambaye amestaafu.

7. Abbas Kayanda kuwa mkuu wa wilaya ya Karatu mkoani Arusha kuchukua nafasi ya Theresia Jonathan Mahongo ambaye amestaafu.

8. Lazaro Jacob Twange kuwa mkuu wa wilaya ya Babati mkoani Manyara kuchukua nafasi ya Elizabeth Simon Kitundu ambaye amestaafu.


9. Toba Alnason Nguvila kuwa mkuu wa wilaya ya Handeni mkoani Tanga kuchukua nafasi ya Godwin Gondwe ambaye amehamishwa kituo cha kazi na kuwa mkuu wa wilaya ya Temeke mkoani Dar es salaam. Godwin Gondwe anachukua nafasi ya Felix Jackson ambaye amestaafu.


Share:

India yanunua ndege za kivita za Urusi

Wizara ya ulinzi ya India imetia saini jana kununua ndege 33 za kijeshi kutoka Urusi na 59 nyingine kuzifanya za kisasa zaidi zenye thamani ya dola bilioni 2.4, huku kukiwa na ongezeko la hali ya wasi wasi na nchi jirani ya China yenye silaha za kinyuklia. 

Ununuzi wa ndege chapa MiG-29 na 12 SU-30 MKI, pamoja na ukarabati wa ndege nyingine 59 chapa MiG-29, ilikuwa kuweka sawa uwezo wa jeshi la anga la India, wizara ya ulinzi imesema. 

Mifumo mipya na ya ziada ya makombora itakayotengenezwa nchini India pia imenunuliwa kwa vitengo vyote vitatu vya jeshi la India. 

Ongezeko la uwezo wa ulinzi nchini India ulichukuliwa kutokana na haja ya kuimarisha majeshi ya ulinzi ili kulinda mipaka ya nchi hiyo na wito wa waziri mkuu Narendra Modi wa India inayojitegemea, wizara hiyo imeongeza katika taarifa.


Share:

Tembelea banda la Tigo msimu huu wa Saba Saba 2020

Kampuni ya mawasiliano inayoongoza kwa kutoa huduma za kidigitali nchini, Tigo Tanzania inawakaribisha wadau na wateja wake pamoja na wananchi wote kwa ujumla katika banda lao lililopo viwanja vya maonesho ya biashara Sabasaba jijini Dar es Salaam ufurahie huduma mbali mbali na ofa kibao. Banda la Tigo lipo mkabala na banda la Wizara ya Viwanda na Biashara.



Share:

Breaking : MATATANI KWA KUNASWA NA DOTI 600 ZA VITENGE VYENYE NEMBO YA CCM...TAKUKURU SHINYANGA YATOA ONYO KALI

NB- Picha haihusiani na habari hapa chini

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Shinyanga inamshikilia Joseph Jonas Tasia mkazi wa Mwasele Mjini Shinyanga kwa kukutwa na doti 600 za vitenge vyenye namba ya Chama Cha Mapinduzi vinavyodaiwa kuwa vilikuwa vinaandaliwa kutumika katika kufanya ushawishi kwa wapiga kura. 

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo Julai 3,2020 na Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Shinyanga Hussein Mussa,mtuhumiwa alikamatwa na vitenge hivyo nyumbani kwake Juni 29,2020 majira ya saa tatu usiku katika mtaa wa Mwasele B. 

“Tukiwa tunaendelea na ufuatiliaji wa vitendo vya Rushwa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu wa viongozi, Juni 29,2020 majira ya saa tatu usiku nyumbani kwa Joseph Jonas Tasia tulikamata doti 600 za vitenge vyenye nembo ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na vya kawaida vikiwa vimehifadhiwa nyumbani kwake jambo ambalo linaashiria kuwa vilikuwa vinaandaliwa kutumika katika kufanya ushawishi kwa wapiga kura”,amesema Mkuu huyo wa TAKUKURU. 

Amesema uchunguzi wa TAKUKURU umebaini kuwa Joseph Jonas Tasia ambaye ni mfanyabiashara wa usafiri wa magari madogo TAXI hana duka na wala hafanyi biashara ya kuuza vitenge. 

“Katika mahojiano na maafisa wa TAKUKURU baada ya mtuhumiwa kukamatwa na mzigo huo ameshindwa kutoa maelezo yanayojitosheleza kuhusiana na vitenge hivyo na hata nyaraka za manunuzi ya mzigo huo alizowasilisha hazijitoshelezi na hivyo kuongeza mashaka juu ya uhalali wa vitenge hivyo”,ameongeza Mussa. 

Amesema uchunguzi wa kina unaendelea ili kubaini iwapo vitenge hivyo vilikuwa ni kwa ajili ya kuhusika na vitendo vya Rushwa katika uchaguzi ujao au ni kwa ajili ya kufanya biashara katika msimu huu wa kuelekea katika uchaguzi mkuu wa viongozi 2020. 

“TAKUKURU mkoa wa Shinyanga inawaonya watu wote wenye nia ya kutaka kutumia taarifa zozote za uchunguzi zinazofanyiwa kazi na ofisi ya TAKUKURU kwa nia ya kujinufaisha kisiasa na kwamba kitendo hicho ni kuingilia uchunguzi unaoendelea na ni kosa la jinai. Hivyo atakayefanya hivyo atachukuliwa hatua kali za kisheria”,amesema Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Shinyanga.
Share:

Ajali Mbaya ya Lori na Noah Yaua Watano Dodoma

Watu 5 wamefariki  na 2 kujeruhiwa baada ya gari dogo aina ya Noah lililokuwa likitokea Morogoro kwenda Dodoma kugongana na lori eneo la kibaigwa jijini Dodoma .

Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, Gilles Muroto amethibitisha.

Amesema ajali hiyo imesababishwa na uzembe wa dereva wa lori ambaye aliingia katikati ya barabara akitokea kwenye kituo cha mafuta bila kuangalia pande zote za barabara na kusababisha Noah kuingia uvunguni mwa lori.


Share:

Vijiji Vinavyochipukia Kuwa Miji Kutangazwa Maeneo Ya Mipango Miji

Na Munir Shemweta, WANMM KIGOMA
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amewataka Maafisa Mipango Miji nchini kuzisaidia wilaya kuhakikisha maeneo yote ya vijiji yanayochipukia kuwa miji anapelekewa ili ayatangaze kuwa maeneo ya Mipango Miji.

Lukuvi alisema hayo jana wakati akizindua ofisi ya ardhi mkoa wa Kigoma ikiwa ni mfululizo wa uzinduzi wa ofisi za ardhi katika mikoa mbalimbali nchini. Tayari ofisi za ardhi kwenye mikoa ya Tanga, Arusha, Manyara, Singida, Iringa, Njombe, Songwe, Rukwa, Katavi zimezinduliwa.

Alisema, wizara yake kwa sasa ina mpango wa kupima kila kipande cha ardhi nchi nzima sambamba na kuhakikisha maeneo yanapangwa ili kuepuka ujenzi holela.

 ‘’Maeneo yote ambayo vijiji vinachipukia nileteeni nitangaze kuwa maeneo ya mipango miji  na maafisa mipango miji mzisaidie wilaya katika hili’’ alisema Lukuvi

Kwa mujibu wa Waziri Lukuvi, baada ya maeneo hayo ya vijiji vinavyochipukia kutangazwa maeneo ya mipango miji wananchi wake hawatapewa tena hati za kimila na badala yake watapata hati za miaka 99 kama wanavyopata watu wanaoishi mijini.

Alisema, mpango wa kuyatangaza maeneo hayo ya vijiji inavyochipukia siyo lazima uanzie wizarani bali Maafisa Mipango Miji katika halmashauri za wilaya wanatakiwa kuyawahi mapema ili kuepuka ujenzi holela.

Akizungumzia utendaji kazi katika ofisi za ardhi za mikoa, Waziri Lukuvi alisema, ofisi hizo zimekamilikia kutokana na kuwa na wataalamu wa fani zote kama vile Upimaji, Uthamini, Mipango Miji pamoja na Usaji wa Hati na kubainisha kuwa vifaa vya kisasa vya upimaji navyo vimepelekwa kwenye ofisi hizo na sasa mwananchi halazimiki kufika Wizarani kwa kuwa huduma zote zinapatikana ofisi za mikoa.

Kuhusu upungufu wa watumishi wa sekta ya ardhi kwenye halmashauri za wilaya, Lukuvi alisema kuwa, baada ya kupeleka watumishi ngazi ya mkoa, zoezi linalofuata ni kuwapanga upya watumishi katika ngazi ya halmashauri kwa kuzingatia wataalam wa fani zote.

Akigeukia suala la utoaji hati miliki za ardhi nchini, Lukuvi ameagiza wananchi wote waliopimiwa ardhi kwenye mkoa wa Kigoma kwenda ofisi za halmashauri za wilaya kuomba kutengenezewa hati na kubainisha kuwa, atakayeshindwa baada ya siku tisini atapelekewa hati ya malipo na kudaiwa kuanzia tarehe aliyopimiwa kiwanja chake.

‘’kama hukwenda kujisalimisha kudai hati ya eneo lako lililowekewa mawe basi baada ya siku tisini utaletewa bili na utadaiwa kuanzia siku ambayo kiwanja chako kiliwekewa mawe, kama yaliwekwa mwaka 1986 basi utaanza kudaiwa kuanzia hapo’’ alisema Lukuvi

Kwa mujibu wa Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Kigoma Chediel Mrutu, mkoa huo una wamiliki wa viwanja 14,746 ambao hawajachukua hati zao pamoja na kukamilika taratibu zote za umilikishwaji ikiwemo kuwekewa alama jambo linaloikosesha serikali mapato sambamba na wamiliki wake kukosa fursa za kiuchumi zinazotokana na kuwa na hati miliki

‘’Usipokuwa na hati ya kiwanja hukopesheki, ongezeni thamani ya mitaji yenu na ardhi isiyopimwa inaitwa mitaji mifu na unapopima ardhi yako na kumilikishwa unakuwa na kinga ya kisheria ‘’ alisema Lukuvi.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emanuel Maganga aliielezea ardhi kama msingi wa haki na dhuluma yoyote inayofanyika inaweza kuleta vita kwa kuwa ardhi ina rasilimali mbalimbali. Kwa mujibu wa Brigedia Jenerali Mstaafu Maganga,  uanziushwaji ofisi za ardhi katika mkoa wa Kigoma utawezesha wana kigoma kuepukana na changamoto mbalimbali ikiwemo kusafiri hadi Tabora kuifuta huduma kwenye ofisi ya kanda.

Mapema Kamishna Msaidizi wa Ardhi Uratibu na Usimamizi kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Wilson Luge alisema, uanzishwaji ofisi za ardhi za mikoa unaenda sambamba na usambazaji vifaa vya kisasa kwenye ofisi hizo ili kuongeza kasi ya upangaji, upimaji na umilikshaji ambapo alibainisha kuwa ardhi inaweza kutumika kama sehemu ya mwananchi kujiongezea kipato.


Share:

Waliowauzia Wafugaji Ng’ombe Wasio Na Sifa Wasakwa

Na. Edward Kondela
Serikali imeagiza kutafutwa kwa watu waliohusika kuwauzia kwa njia ya mkopo wafugaji ng’ombe wa maziwa waliozaa tayari na kuwahadaa wafugaji kuwa ng’ombe hao hawana uzao wowote (mitamba) ili wawapatie wafugaji ng’ombe wenye sifa kama walivyokubaliana katika mikataba.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amesema hayo katika Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga, wakati akikabidhi lori moja la kukusanyia maziwa, keni za maziwa 250 pamoja na vifaa vingine vya kuboresha vituo vya kukusanyia maziwa wilayani humo kwa Chama Kikuu cha Ushirika cha Wafugaji wa Ng’ombe wa Maziwa Mkoa wa Tanga (TDCU) na kufafanua kuwa serikali imefanya kazi nzuri kuhakikisha wafugaji wanapata mikopo hiyo kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), hivyo lazima ihakikishe wafugaji hao wananufaika.

“Katika hatua ya upatikanaji wa ng’ombe mkajikuta mkaingia kwenye mitego ng’ombe ameshakuwa mkongwe halafu huku unaambiwa hana uzao wowote ilhali ng’ombe amezaa zaidi ya mara mbili, TDCU pamoja na vyama vya msingi hakikisheni wale waliowazuia ng’ombe wafugaji hawa wanafanya maboresho ili lengo la serikali liweze kukamilika najua mmeuziana baina yenu lakini hatuwezi kama serikali kukaa kimya lengo letu ni kuhakikisha mambo yanaenda katika unyoofu wake.”  Amesema Mhe. Ulega

Aidha Mhe. Ulega amefafanua kuwa endapo wafugaji hao wataendelea kuwa na ng’ombe hao watazidi kuwa masikini kwa kuwa watatumia nguvu kubwa kuwapatia malisho na dawa za mifugo ilhali ng’ombe hao wanatoa lita chache za maziwa tofauti na matarajio.

Katika upande mwingine, Naibu Waziri Ulega amewataka pia wafugaji wa ng’ombe wa maziwa Mkoani Tanga, kuwa waaminifu kwa kuhakikisha wanapeleka maziwa ya kutosha TDCU ili maziwa hayo yaweze kutosheleza mahitaji ya kiwanda cha kuchakata maziwa cha Tanga Fresh ambacho kinapokea maziwa kupitia chama hicho.

Aidha kuhusu bima ya mifugo Naibu Waziri Ulega amefafanua kuwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi imefanya kazi kubwa kwa kushirikiana na Shirika la Bima la Taifa (NIC) ambapo tayari sera ya bima ya mifugo ipo tayari na kwamba ipo katika hatua ya mwisho kuzinduliwa mwaka huu ili ianze kutumika na kuwanufaisha wafugaji pindi wanapopata majanga mbalimbali ya mifugo yao.

Naye Mratibu wa Miradi kutoka shirika la kimataifa la Heifer Bw. Mark Tsoxo akizungumza juu ya Mradi wa Usindikaji wa Maziwa Tanzania (TMPP) uliowezesha kupatika kwa lori la kukusanyia kwa TDCU lenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 170, amesema mradi huo unafadhili matenki 6 ya kuhifadhi maziwa yenye ujazo wa lita 24,000, kukarabati vituo 10, jenereta 7 na ufadhili wa malori 5 ya kubebea maziwa.

Bw. Tsoxo amefafanua kuwa kutokana na jitihada za mradi kwa kushirikiana na wasindikaji, ukusanyaji wa maziwa umeongezeka kwa zaidi ya lita 12,000 kwa siku kutoka kati ya mwezi Januari  lita 55,817 kwa siku hadi sasa lita 68,017 kwa siku.

Nao baadhi ya wafugaji waliopatiwa mikopo ya ng’ombe wa maziwa pamoja na ujenzi wa mabanda kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) wamefurahishwa na hatua hiyo huku wakiomba serikali na taasisi zingine kuwaboreshea zaidi mazingira ya ufugaji hapa nchini.

Kuhusu elimu juu ya ufugaji bora wa maziwa wafugaji hao wameiomba Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia wataalam wa wizara hiyo, mikoa na wilaya kuhakikisha wanawatembelea wafugaji mara kwa mara ili kuwapatia elimu bora ikiwemo ya kilimo cha malisho bora ya mifugo.

Mwisho.


Share:

Waziri Angela Kairuki Awataka Tpc Kuzalisha Sukari Ya Viwandani

Na Dixon Busagaga -Kilimanjaro .
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia uwekezaji, Angela Kairuki,ameutaka uongozi wa Kiwanda cha Sukari cha TPC, kilichopo Wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, kuangalia uwezekano wa kuanza uzalishaji wa Sukari ya viwandani, ili kuondoa adha ya kuagiza sukari hiyo nje ya nchini.

Kairuki alisema mpaka sasa hakuna mzalishaji wa sukari za viwandani nchini na kwamba serikali huagiza zaidi ya Tani 155,000,na kwamba endapo TPC wataanza uzalishaki huo, watasaidia upatikanaji wa sukari hiyo kwa urahisi.

"Niwashauri TPC, kuangalia ni namna gani,mnaweza kuzalisha sukari za viwandani, tukitambua bado hatuna mzalishaji hata mmoja hapa nchini, ambaye anazalisha sukari za viwandani,tunaagiza zaidi ya tani 155,000 za sukari hii, tunamini mkileta mitambo, mnaweza kuzalisha na kuweza kupata sukari hiyo hapa nchini"alisema Kairuki

Mbali na hilo Kairuki amewataka wawekezaji, kuendelea kutazama fursa za uwekezaji zilizopo nchini na kuwekeza katika nyanja mbalimbali, ili kufanikisha malengo ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya Viwanda.

Alisema bado kuna mahitaji makubwa ya bidhaa mbalimbali nchini, na bidhaa nyingine zinaagizwa nje ya nchi, hivyo ipo haja kwa wawekezaji kujitokeza na kuwekeza katika nyanja mbalimbali, hatua ambayo itapanua wigo wa ajira kwa watanzania na hata kuinua pato la taifa.

"Mahitaji bado ni makubwa nchini, kuna changamoto ya chupa za kioo,Chupa za Plastiki na bidhaa nyingi tunaagiza nje, sasa angalieni, mkiona kuna fursa, serikali tupo tayari kutoa ushirikiano, ili muweze kupanua wigo wa uwekezaji"alisema Kairuki.

Akizungumza Ofisa mtendaji utawala katika kiwanda cha TPC, Jaffari Ally,alisema mpaka sasa kiwanda hicho kina sukari zaidi ya tani 3,300 ambazo zipo kwenye Ghala, na kuwatoa hofu watanzania, kuwa hakuna tena upungufu wa sukari nchini.

"Tuwatake wasambazaji wakubwa na wauzaji wa rejareja wa sukari nchini, kuacha kuwalangua wananchi na kuhakikisha wanauza sukari kwa bei ya awali ya kabla ya kufungwa kwa msimu, maana kwa sasa sukari inayouzwa inazalishwa hapa nchini na hakuna inayoagizwa nje ya nchi"alisema.

Mwisho.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Uwekezaji Angellah Kairuki akizungumza na Menenjimenti ya Kiwanda cha Sukari -TPC kilichopo wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro (Hawapo pichani)  alipotembelea kiwanda hicho ikiwa ni sehemu ya ziara yake .
Afisa Mtendaji -Utawala wa Kiwanda cha Sukari cha TPC-Jafary Ally akielezea jambo mbele ya Waziri Kairuki alipotembelea kiwandani hapo .
Afisa Mtendaji -Utawala wa Kiwanda cha Sukari cha TPC-Jafary Ally  (Wa pili kutoka kulia) akimuongoza Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu-Uwekezaji Angella Kairuki kutembelea maeneo mbalimbali ya kiwanda hicho.
Sehemu ya Kiwanda cha Sukari cha TPC 
Waziri Kairuki akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi a kiwanda cha Sukari cha TPC namna ambavyo machine ya kuzalisha umeme kiwandani hapo inafanya kazi .
Waziri Kairuki na Viongozi wengine alioambatana nao wakishuka katika moja ya ngazi zilizopo kiwandani hapo .
Sehemu ya Mabehewa yanayotumika kusafirisha Miwa kutoka mashambani na kuifikisha katika eneo la kiwanda .
Waziri Kairuki akitizama namna ambavyo sukari inawekwa kwenye mifuko kabla ya kwenda kwa mtumiaji wa mwisho .
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Uwekezaji Angela Kairuki akitoka katika eneo la kiwanda hicho mara baada ya kujionea uzalishaji unavyofanyika katika kiwanda hicho .




Share:

Tanzania Kuna Fursa Ya Kubwa Ya Kuleta Mapinduzi Katika Tasnia Ya Mbolea – Katibu Mkuu Kilimo

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bwana Gerald Musabila Kusaya kusaya amesema Tanzania ina nafasi yakubwa ya kuleta mapinduzi makubwa katika Sekta ya Kilimo ikiwa kila Mdau kwenye mnyororo wa thamani atatimiza wajibu wake ipasavyo.

Katibu Mkuu Kusaya ameyasema hayo, jana tarehe 02/07/2020 wakati wa kikao maalum alichokiitisha ili kujadiliana na Wadau wa zao la chai pamoja na Wazalishaji wa mbolea maalum ya zao la chai; Inayoitwa Minjingu Chai katika Ukumbi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea (TFRA) Jengo la Kilimo I, Jijini, Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Kusaya amesema Mkulima anategemea maendeleo ya utafiti kwenye tasnia ya mbolea, anategemea ushauri mzuri wa Maafisa Ugani, anategemea kwa sehemu kubwa uzalishaji wa mbolea ambao utamuakikishia kupatikana kwa wakati na kwa bei nafuu lakini pia Mkulima anategemea Ushirika imara ili awe na uhakika wa kuuza mazao yake baada ya kuvuna.

Bwana Gerald Kusaya ameongeza kuwa pembejeo moja ya muhimu katika ukuaji wa Sekta ya Kilimo ni mbolea na kwamba mazingira ya Tanzania yanatoa fursa nyingi kwa viwanda vingi kuanzishwa licha ya kukiri kuwa kuna changamoto kadhaa ambazo Serikali imekuwa ikiendelea kuzitatua ili siku moja mazingira ya uwekezaji yawe mazuri kwa kiwangi kikubwa.

Bwana Gerald Kusaya ameongeza kuwa Serikali imeendelea kuweka jitihada na kuweka mazingira mazuri na wezeshi katika uwekezaji na ujenzi wa viwanda vya mbolea nchini. Aidha, sambamba na jitihada hizo, pia kuna fursa mbalimbali zinazohamasisha uwekezaji katika shughuli za uzalishaji wa mbolea nchini.

Amezitaja fursa hizo kuwa ni pamoja na: - Uwepo wa utashi wa kisiasa unaoruhusu uwekezaji katika tasnia ya mbolea.

“Tanzania ni kitovu cha usambazaji katika mataifa ya Jumuia ya Afica ‘SADC’ ambayo hayana bandari. Uwepo wa Wahandisi wa Kemikali “Chemical Engineers” wenye taaluma ya kuzalisha mbolea wa kutosha katika soko la ajira.” Amekaririwa Katibu Mkuu Kusaya.

Bwana Gerald Kusaya ametaja fursa nyingine ni pamoja na uwepo wa Vituo vya Utafiti wa mazao ya kilimo; Yanayotumia mbolea. Uwepo na nia ya makampuni binafsi yanayojihusisha na uwekezaji wa mbolea na visaidizi vyake. Kufunguliwa kwa mipaka ya kuuza mazao nje ya nchi inayohamasisha kuwepo kwa mahitaji makubwa ya mbolea na visaidizi vyake.

Katibu Mkuu Kusaya ameongeza kuwa kuwepo kwa soko kubwa la ndani na nje la mahitaji ya mbolea na visaidizi vyake. Uwepo wa Miundombinu kama nishati na barabara inayowezesha usafirishaji wa mbolea kutoka bandarini hadi kwa mkulima wa mwisho.

Uwepo wa malighafi za kuendeshea viwanda zinazotokana na mazao ya kilimo ambayo yanazalishwa kwa kutumia mbolea pamoja na uwepo wa viwanda vingi vinavyotumia malighafi za mazao ya kilimo; hivyo kufanya mahitaji ya mbolea kuongezeka.

Aidha Katibu Mkuu Bwana Gerald Kusaya amekiri kuwa tasnia ya mbolea inakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo; Gharama kubwa za uwekezaji na uzalishaji zinazofanya mbolea zinazozalishwa nchini kuwa na bei kubwa kuliko zinazoingia nchini.

Ameongeza kuwa kuwepo na mifumo ya kisheria yenye utata ambayo inamlazimisha mwekezaji kushughulikia masuala mengine ambayo yanaweza kufanywa na taasisi zingine.

Pamoja na kukosekana kwa ushirikiano “collaboration” na watengenezaji wa bidhaa saidizi kama kutengeneza vifungashio, kuweka maandishi kwenye mifuko.

“Changamoto tajwa hapo juu zinaweza kupatiwa ufumbuzi kwa kuundwa kwa jopo la kiwizara ili kuimarisha mahusiano na Ofisi ya Rais TAMISEMI na kuimarisha utekelezaji wa Sheria ya Mbolea Namba 9 ya Mwaka 2009 kuhusu usimamizi wa uwekezaji katika viwanda vya mbolea (Interministerial Commitee).” Amekaririwa Bwana Gerald Kusaya.

Katibu Mkuu Kusaya amesema Bodi ya TFRA inajukumu la kuboresha mazingira ya uwekezaji katika viwanda na kurekebisha sheria ya mbolea na miongozo inayohamasisha Wawekezaji waliopo kuzalisha kulingana na uwezo wa kiwanda.

“TFRA iendelee kusimamia na kuhakikisha kwamba viwanda vyote vya mbolea na visaidizi vyake nchini vinasajiliwa na kuwa na leseni hai muda wote.”

“TFRA iendelea kufuatilia na kutoa ushauri kwa wawekezaji wa viwanda vya mbolea kukamilisha nyaraka zote muhimu zinazotakiwa ili waweze kukidhi vigezo vya kuanzisha viwanda vya mbolea.”

“TFRA iendelee kushirikiana na Taasisi za utafiti na wadau wengine wa maendeleo katika kuelimisha umma juu ya umuhimu wa matumizi sahihi y mbolea.”

“TFRA iendelee kuhamasisha wadau mbalimbali wa kilimo kupitia vyombo vya habari na maonesho ya kilimo ili wawekeze katika tasnia ya mbolea.” Amekaririwa Katibu Mkuu akitoa maagizo hayo kwa Menejimenti na Watumishi wa Mamlaka ya Mbolea nchini (TFRA).

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bwana Gerald Kusaya yupo Jijini Dar es Salaam, ambapo tangu siku ya Jumanne tarehe 30 Juni, 2020 hadi Ijumaa tarehe 03 Julai, 2020 atakuwa akizitembela Taasisi za Wizara ya Kilimo, zilizopo Jijini, Dar es Salaama na baadae anataraji kuanza ziara ya kutembelea ili kujionea changamoto na maendeleo ya Sekta ya Kilimo mazao katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, ziara ambayo inataraji kuanza tarehe 08 Julai, 2020.


Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA JULAI 3,2020


Share:

Thursday, 2 July 2020

Job vacancies at Muhimbili National Hospital (MNH)

VACANCIES ANNOUNCEMENT-RE-ADVERTISED On behalf of Muhimbili National Hospital (MNH), Public Service Recruitment Secretariat invites dynamic and suitably qualified Tanzanians to fill 2 vacant posts mentioned below; 1.0 MUHIMBILI NATIONAL HOSPITAL (MNH) Muhimbili National Hospital (MNH) is a tertiary specialised and super specialist hospital in Tanzania organized into nine directorates with bed capacity of 2,178 out […]

The post Job vacancies at Muhimbili National Hospital (MNH) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Wanachama na Wafuasi wa Chama Cha ACT-Wazalendo Wamchangia 500,000 Maalim Seif Sharif Hamad ili Agombee Urais Zanzibar

Wanachama na Wafuasi wa Chama Cha ACT-Wazalendo wa Micheweni kisiwani Pemba wameamua kumchangia fedha Maalim Seif Sharif Hamad kuwania tena urais wa Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020.

Akizungumza kwa niaba ya Wanachama hao ambao wamemchangia Maalim Seif kiasi cha Sh. 500,000, Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Mkoa wa Micheweni kichama , Rashid Khalid amesema, wameamua kufanya hivyo kwakua kiongozi huyo ndiye pekee atakayeweza kutetea maslahi ya Wazanzibari .

Amesema kuwa, Wazanzibar wanahitaji muungano na kuwakomboa katika dimbwi la umasikini na ukosefu wa ajira ambavyo vyama vingine vimeshindwa kuwatimizia.

“Tumeamua kukuchangia fedha hizi ili zikusaidie katika kulipia ada ya uchukuaji wa fomu, sisi wanachama wa Micheweni tunaona wewe ndiye mtu pekee utakayeweza kutuokoa kutokana na madhila wanayotufanyia vyama vingine ,” amesema kiongozi huyo.

Baada ya kupokea fedha hizo, Maalim Seif amesema, kiasi hicho kitamsaidia kupunguza gharama za ada ya uchukuaji wa fomu ya kugombea urais wa Zanzibar ambayo ni shilingi milioni moja.

Pia amewashukuru wanachama hao na kusema kuwa uongozi wa Chama Cha ACT-Wazalendo kimejipanga vyema katika kuhakikisha kinapata ushindi ili kiweze kuwahudumia wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwa kuzingatia misingi ya haki na usawa kwa wananchi wote.

Julai 4, 2020 Maalim Seif anatarajia kuchukua fomu rasmi ya kuomba kuteuliwa na chama chake ili kugombea nafasi ya urais wa Zanzibar kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2020.


Share:

Majimbo manne ya uchaguzi Zanzibar Yafutwa

Tume ya Uchaguzi Zanzibar imefuta majimbo manne ya uchaguzi Zanzibar na kubakiza majimbo 50 badala ya majimbo 54 yaliokuwepo awali.

Jaji Mkuu Mstaafu, Hamid Mahmoud Hamid, Mwenyekiti wa ZEC ametangaza uamuzi huo leo tarehe Alhamisi tarehe 2 Julai 2020.

Baada ya mabadiliko hayo, kwa sasa Zanzibar ina majimbo 50 badala ya 54 ilivyokuwa awali, ambapo Unguja ina majimbo 32 na Pemba 18.


Share:

TCRA Yavipiga Faini Vyombo vya Habari Sita vya Utangazaji kwa kurusha maudhui katika muda ambao watoto hawapaswi kuangalia ama kusikiliza

Mamlaka  ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imevitoza faini ya Sh milioni 30 vyombo vya habari sita, kwa kukiuka kanuni na maadili ya utangazaji ikiwamo redio ya Clouds FM kuzungumzia supu ya pweza kuimarisha tendo la ndoa katika muda ambao wasikilizaji wanaweza kuwa watoto.

Mbali ya Clouds FM, vyombo vingine vilivyoadhibiwa ni East Africa Radio, na televisheni za Star, Sibuka, na Global Tv na Duma Tv.

Akisoma uamuzi huo jana jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA, Joseph Mapunda alisema vyombo hivyo vilikiuka kanuni za mawasiliano kwa nyakati tofauti.

Mapunda alisema redio ya Clouds FM kupitia kipindi chake cha Jahazi, walihamasisha vitendo vya ngono, kwa kutumia supu ya pweza katika kuimarisha tendo la ndoa kwa muda ambao wasikilizaji wanaweza kuwa watoto.

Alisema baada ya kusikiliza utetezi wao, wanatozwa faini ya Sh milioni saba na kupewa onyo kali baada ya kuwatia hatiani kwa kosa hilo.

Katika shauri lingine, kituo cha Duma TV kimetozwa faini ya Sh milioni saba na kufungiwa kuchapisha maudhui kwa muda wa mwezi mmoja ili wajipange na kuzifahamu kanuni na kuzingatia weledi na maadili ya utangazaji.

Mapunda alisema Duma ilikutwa na hatia ya kukiuka kanuni kwa kuchapisha na kutangaza maudhui yenye lugha isiyo na staha na iliyo na udhalilishaji wa kijinsia kwa wanaume na wanawake.

Alisema redio ya East Africa imetozwa faini ya Sh milioni tatu na kupewa onyo kali kwa kukiuka kanuni hiyo, kwa kurusha maudhui ya kukashifu utendaji wa serikali kupitia uteuzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na kutumia lugha ya kashfa dhidi ya utendaji wake.

Vilevile Global Tv imetozwa Sh milioni saba na kupewa onyo kali, baada ya kupatikana na hatia ya kuchapisha picha ya mnato na kutangaza maudhui yasiyokuwa na lugha ya staha na yenye kushabikia vitendo vya mahusiano ya kimapenzi ya jinsia moja.

Mapunda alisema maudhui hayo, yangeweza kuwaumiza na kuwakwaza waumini wa dhebebu la Anglikana na Watanzania kwa ujumla. Pia, alisema Sibuka Tv inatozwa faini ya Sh milioni tatu baada ya kupatikana na hatia ya kushabikia mauaji ya kutisha katika muda, ambao watoto wanaweza kuwa sehemu kubwa ya watazamaji.


Share:

PAKUA APP YA MALUNDE 1 BLOG ILI TUWE TUNAKUMIA HABARI NA MATUKIO MOJA KWA MOJA KWENYE SIMU YAKO

Kuwa wa Kwanza kupata habari na matukio yanayojiri Tanzania na dunia kwa ujumla kwa kupakua/ kudownload App ya Malunde 1 blog tukuhabarishe masaa 24.


Tembea na dunia kiganjani mwako sasa.

Pakua App mpya ya Malunde 1 blog imeboreshwa zaidi ili kukidhi mahitaji ya wasomaji wetu. Hii ndiyo mpya kabisa,ina alama hii ↡↡
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Ni rahisi sana : Ingia Play store kisha Andika Malunde 1 blog halafu bonyeza Install

https://bit.ly/2Qb7qyF

Tafadhali fuata maelekezo hapo juu... Usikubali kukosa habari kizembe..Pakua app yetu Mpya ya Malunde1 blog Sasa
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger