Tuesday, 9 June 2020

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO JUNI 10,2020... HABARI KUBWA MBOWE KUPIGWA


Magazetini leo Jumatano Juni 10,2020

Share:

MOTISHA YA MBUNGE ILIVYOCHOCHEA UFAULU SEKONDARI ZA MADABA



Mbunge jimbo la Madaba Mhe. Joseph Mhagama  akikagua ujenzi wa darasa Ifinga
Mwanafunzi shule ya secondary Wino Gaston Ndimbo akielekeza namna ya kuchanganya kemikali mbele ya Mbunge wa jimbo la Madaba Joseph Mhagama (wa kwanza kushoto)wakati alipotembelea shuleni hapo
Mwananchi akimshukuru mgeni rasmi Mbunge wa jimbo la Madaba Joseph Kizito Mhagama wakati wa mahafali ya shule ya sekondari Magingo.

****
Motisha inayotolewa kwa Walimu na wanafunzi  imekuwa chachu ya maendeleo ya elimu katika Jimbo la Madaba hapa mkoani Ruvuma; na hali hii imeongeza ufaulu  na kutuinua kimkoa na kitaifa.

Anasema Ofisa Elimu (Sekondari) wa Halmashauri ya Madaba, Michael Hadu, anapozungumzia kiwango cha ufaulu katika shule za halmashauri hiyo iliyo katika Jimbo la Madaba mkoani Ruvuma.

“Tangu Mbunge wa Jimbo hili (Joseph Mhagama) aanze kutoa motisha kwa walimu na wanafunzi wa shule za sekondari ili kuhamasisha na kuchochea ari ya walimu kufundisha na wanafunzi kujifunza sambamba na kusaidia wananchi kujenga mabweni na vyumba vya madarasa, kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi  wa shule za sekondari na msingi katika jimbo hili kimepaa,” anasema Ofisa Elimu huyo.

Hadu anaongeza: “Ndiyo maana maana unaona tangu mbunge alipoanza kuweka msukumo huu kwa manufaa ya watoto wa halmashauri na jimbo hili, sambamba na kuhakikisha kunakuwapo ongezeko la viti, meza, vitabu na vifaa vingine vya kufundishia na kujifunzia, shule wanafunzi wameongeza ufaulu sana.”

Anatoa mfano akisema ufaulu wa wanafunzi katika Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Pili umepanda kutoka nafasi ya 104 mwaka 2018 hadi nafasi ya 24 mwaka 2019 na kushika nafasi ya kwanza kimkoa.

Katika kuelezea matunda ya kujitoa na kuwajibika kwa mbunge huyo wa Madaba kwa wnaanchi wake, Ofisa Elimu huyo anasema hata katika mtihani wa taifa wa kidato cha nne, halmashauri ya madaba imefanya vizuri na kushika nafasi ya 23 kitaifa mwaka 2019  huku ikiwa ya kwanza kimkoa.

“Haya ni mafanikio ya kutoka nafasi ya 121 kitaifa mwaka 2018  na hii yote imechangiwa na juhudi za Mbunge (Mhagama) kupita na kuzungumza na walimu, kusikiliza kero zao na kuwatia moyo huku akiwasisiza kuwafundisha watoto kwa upendo na kufanya kazi kwa bidii...” anasema na kuongeza: “Kweli walimu walimwelewa vizuri; wakabadilika na sasa wanafundisha kwa bidii ndiyo maana ufaulu unazidi kupanda siku hadi siku.”

“Siyo siri, Ofisi ya Mbunge imekuwa  na mchango mkubwa kwa Idara ya Elimu katika jimbo na halmashauri hii.”

“Mheshimiwa Joseph Mhagama amesaidia sana hata kufuatilia na kutuletea Sh milioni 240 kwa ajili ya ujenzi wa maabara na amekuwa karibu sana na walimu na ofisi yake imekuwa ikitoa sukari ya mwaka mzima kwa ajili ya walimu,” anafahamisha.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa makala haya, tangu mwaka 2017, mbunge huyo wa Jimbo la Madaba amekuwa akitoa Sh 500,000 kwa kila shule kwa ajili ya chai kuwasaidia walimu kupata chai shuleni na hivyo, kuokoa muda.

“Hata kile kitendo chake cha kusikiliza shida binafsi za walimu na kuwasaidia hata kwa kutoa fedha zake binafsi mwalimu anapokuwa na shida, kimewatia moyo sana walimu ndiyo maana wanasema ni mlezi mzuri kwa walimu na wanafunzi,” anasema Ofisa Elimu huyo

“Mbunge huyu ni msaada mkubwa maana amesaidia sana kuinua elimu hata ‘form six’ (kidato cha Sita) mwaka 2019 katika Shule ya sekondari ya Madaba, wanafunzi 23 wamepata  daraja la kwanza, hivyo tumeshika nafasi ya 7 kati ya shule 26 za Mkoa wa Ruvuma”

“Nayo Sekondari ya Wilma imeshika nafasi ya 8, hivyo tumeingiza shule zetu mbili za ‘A Level’ katika kumi bora kitu ambacho hakijawahi kutokea na hii ni kutokana na ufatiliaji mzuri wa wataalamu kwa kushirikiana na Mbunge wa Madaba ambaye alizungumza na walimu na kuwazawadia Sh 200,000,” anasema.

Mmoja wa wanawake ambaye ni ofisa katika Halmashauri ya Madaba aliyekataa jina na idara yake kutajwa gazetini, anasema anaijua miradi mingi ya elimu iliyowezeshwa na Mbunge huyo ukiwamo ujenzi wa hosteli na vyoo vya  wanafunzi wa kike katika shule mbalimbali.

Anazitaja baadhi ya shule hizo kuwa ni pamoja na sekondari za Nguluma na Lipupuma alipokarabati jengo la utawala na na kukarabati choo cha wasichana katika Shule ya Sekondari ya Magingo na kuweka umeme katika madarasa ikisemekana pia kuwa, ametumia Sh 7,000,000 kuezeka madarasa katika shule ya Mateteleka.

Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mahanje, Makoye Richard, anasema motisha kwa walimu zimeongeza ari ya ufundishaji kwa walimu na kuongeza ufaulu  shuleni kwake.

Makoye anasema: “Ufaulu wa   daraja la kwanza na la pili ulikuwa ndoto kwa shule yetu, lakini tunashukuru maana kwa mara ya kwanza, wanafunzi 48 waliofanya mtihani wa taifa wa kidato cha nne  mmoja alipata  daraja la kwanza na wanafunzi sita wakapata ‘division two’ wanafunzi 14 walipata ‘division three’ na  wanafunzi 26 wakapata ‘division four.” 4.

Anaupongeza ushirikiano uliopo baina ya wazazi, walimu na mbunge wao akisema umewafanya vijana kuongeza bidii na umakini kiasi kwamba, sasa karibu nusu ya darasa wanafaulu na kujiunga na kidato cha tano. Hata wengine wanaobaki, nao wanaenda katika vyuo.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Shule huyo, ufaulu huo umechangiwa kwa kiasi kikubwa na juhudi za Mbunge Mhagama kutembelea shule mbalimbali na kuzungumza na walimu na wanafunzi. Anasema: “Hapa kwetu kwa mwaka anaweza kuja mara mbili hadi tatu.”

Makoye anafahamisha kuwa, Mbunge huyo amekuwa akitoa motisha kwa walimu wanaofanya vizuri na wanafunzi hata Sh 300,000 kwa kila mmoja sambamba na vifaa vya kujifunzia na kufundishia.

“Hapa shuleni, amewasupport wanafunzi wa kike kwa kuhakikisha wanapata pedi, hivyo wawanafunzi hao kuongeza mahudhurio katika vipindi vyote vya masomo hata wakati wakiwa kwenye hedhi. Hali hii inawafanya waongeze umakini na ufaulu katika masomo...” anasema

Daud Mgaya Mwanafunzi wa kidato cha nne Mahanje sekondari anasema, mbunge amefanya kazi kubwa kuwajenga kisaikolojia na kuwatia matumaini pale wanapopitia wakati mgumu wakiwa shule kwa kuwapa motisha hivyo kuwafanya wasome kwa bidii zaidi hali iliyoongeza ufauhulu.

“Tunamshukuru sana Mbunge kwa kujitoa kwake kwetu na kwa walimu kwani mara kwa mara amekuwa bega kwa bega na sisi na ametusupport sana kwenye miradi midogo midogo ya hapa shuleni zikiwemo club za wanafunzi,” anasema Mgaya

Mzazi na mkazi wa Kijiji cha Mateteleka anasema, Allan Mwenda, anasema amekuwa akivutiwa na jitihada zinazofanywa na Mbunge Mhagama katika suala la elimu ya watoto wao.

“Amejitoa kwa hali na mali kuwasaidia watoto wa wanyonge. Binafsi huwa najivunia sana mtu anayependa elimu na huyu Mbunge ni miongoni mwa viongozi wanaopenda sana elimu ndiyo maana ameweza kutambua mchango wa walimu na kuwasaidia kwa kuwapa zawadi na kuwachangia sukari kwa mwaka mzima; ni viongozi wachache sana wenye upendo kama huo. Tunamwombea kwa Mungu aendelee kutusaidia wananchi wa Madaba,” anasema Mwenda.

Alipoulizwa anavyochangia kuinua kiwango cha elimu jimboni Madaba, mbunge huyo anasema amekuwa na utaratibu wa kutoa motisha na hamasa kwa walimu na wanafunzi wa sekondari kwa kuwatembelea kila mwaka, kuzungumza nao, kushiriki nao chakula, na kuwapa zawadi.

“Katika kipindi hicho, nimetumiatakriban Sh 11,700,000 kama zawadi kwa wanafunzi wanaofanya vizuri na chai ya walimu wetu wa Sekondari katika shule zetu zote”

Anasema:“Kwa mfano, kutokana na kufanya vizuri, wanafunzi Sekondari ya Wino walipewa zawadi ya TV ya Sh 1,000,000 wanayotumia kupata habari na burudani mbalimbali.”

Mintarafu motisha kwa walimu, wanafunzi na wafanyakazi katika Shule ya Sekondari ya Wilma anasema zilitumika Sh 1,200,000. 

“Jitihada hizi zimechangia sana kuongezeka kwa ufaulu kwa watoto wetu ambapo katika matokeo ya Kidato cha Nne 2019 Madaba imeshika nafasi ya kwanza  kimkoa na nafasi ya 24 kitaifa; asante sana walimu, wanafunzi na wazazi!  Jumla Sh. 13,550,000 zimetumika kulipa motisha”.anasema Mhagama.

Kuhusu maendeleo ya elimu kwa shule za msingi anasema: “Kama mbunge wao, pia nimekuwa na utaratibu kama huo wa kuhamasisha na kutoa motisha kwa walimu na wanafunzi wa shule zetu za msingi kwa kuwatembelea kila mwaka, kuzungumza nao, na kuwapa zawadi.”

“ Katika kipindi hiki, takriban Sh 3,700,000 zimetumika kama zawadi kwa walimu, na ununuzi wa chaki kwa shule zote. Mpaka sasa bado chaki zinasambazwa.  Jitihada hizi zinachangia sana kuongezeka kwa ufaulu,“ anasema Mhagama. 

Anasema ukamilishaji wa maabara moja katika Shule ya Sekondari ya  Wino umegharimu  Sh 4,505,500  na kazi inaendelea  na kadhgalika, ukarabati wa vyoo katika Shule ya Sekondari Ifinga ulifanyika na kukamilika kwa Sh. 1,000,000 kutoka Mfuko wa Jimbo 2019/20.

Anasema mbali na ujenzi wa madarasa mawili na ofisi ya walimu katika Sekondari ya Wino zilipotumika takriban Sh 30,000,000, pia kumekuwa na usambazaji wa madawati katika shule za msingi na sekondari kupitia mfuko maalum wa Bunge.

“Serikali imetuletea madawati 251 yaliyosambazwa katika shule zetu wa msingi na chache za sekondari... Gharama za kusafirishia madawati hayo takriban Sh 534,000 zilitolewa na mbunge,” anasema Mhagama.

Uchunguzi umebaini kuwa Mhagama pia amesaidia kupatikana kwa fedha za miradi mbalimbali ikiwemo ya ujenzi wa madarasa, nyumba za walimu, ofisi na vyoo. Katika Shule ya Msingi Matetereka, wamefanikiwa kukamilisha ujenzi wa madarasa mawili yaliyogharimu  Sh 25,500,000.

Imebainika pia kuwa, katika kutatua changamoto ya ukosefu wa mabweni katika Shule ya Sekondari Mahanje iliyowaathiri zaidi kimasomo wanafunzi wa kike,  alitafuta na kupata Sh 196,600,000 (P4R 2017/18 awamu ya kwanza).mradi wa kulipa kulingana na matokeo.

“Kwa kushirikiana na wananchi, tumejenga mabweni makubwa mawili moja la wanafunzi wa kike na moja la wavulana,” kinasema chanzo kimoja jimboni humo na kufafanua kuwa, kila bweni lina vyumba 20 vyenye vitanda 4 kila chumba.

 Mikakati yake ni kuendelea kutoa motisha zaidi kwa walimu na wanafunzi na kusaidia vifaa vya kufundishia na kujifunzia ili kupunguza kero zinazowatatiza walimu

Anawashauri wadau wa Elimu halmashauri ya Madaba kuendelea kusaidia elimu ilikuweza kupandisha ufaulu katika Halmashauri hiyo.
Share:

Ugonjwa Wa Corona Unaelekea Kuisha Nchini-Waziri Ummy

Na WAJMW-DOM
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema ugonjwa wa Corona unaelekea kuisha nchini ambapo mikoa zaidi ya 15 haijaripoti mgonjwa yeyote wa Corona kwa zaidi ya wiki.

Waziri Ummy amesema hayo leo wakati alipotembelea kituo cha afya cha Mkonze kilichotengwa kwa ajili ya kuwahudumia watu waliopata maambukizi ya ugonjwa wa Corona jijini Dodoma na kukuta vitanda vikiwa tupu bila kuwa na mgonjwa yeyote kwa zaidi ya wiki.

Waziri Ummy amesema kupitia Waganga wakuu wa Mikoa 15 nchini wamethibitisha kutokua na mgonjwa wa Corona na Mikoa mingine yenye wagonjwa imeripoti kuwa wagonjwa hao wanaendelea vizuri.

Aidha, Waziri Ummy amewashukuru watoa huduma za afya wa kituo cha Mkonze kwa kazi nzuri walioifanya ya kuwahudumia wagonjwa na kuchukua tahadhari zilizosaidia wahudumu hao kutopata maambukizi ya Corona.

Pamoja na hayo Waziri Ummy amesema licha ya ugonjwa wa Corona kuelekea kumalizika nchini, amewataka wananchi kutobweteka na kuendelea kuchukua tahadhari kwa kuzingatia maelekezo yanayotolewa na wataalam wa afya ikiwemo kunawa mikono mara kwa mara kwa sabuni na maji tiririka pamoja na kuvaa barakoa za vitambaa wanapokua kwenye mikusanyiko


Share:

BREAKING NEWS: Rais wa Burundi aliyemaliza muda wake, Pierre Nkurunziza afariki dunia.

Aliyekua Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amefariki dunia  kwa mshtuko wa Moyo

Serikali ya Burundi imetangaza hayo leo kupitia ukurasa wake rasmi wa Twitter.

Ujumbe kwenye ukurasa huo umeeleza kuwa serikali ya Burundi inatangaza kwa masikitiko makubwa kifo cha Rais Nkurunziza na kuongeza kuwa amefariki kutokana na tatizo la moyo.


Nkurunziza alizaliwa Desemba 18, 1963, ambapo alikuwa Mwenyekiti wa chama tawala cha CNDD-FDD, hadi alipochaguliwa kama Rais wa Burundi mwaka 2005.



Share:

Breaking : RAIS WA BURUNDI PIERRE NKURUNZIZA AFARIKI DUNIA



Rais wa Burundi aliyemaliza muda wake Pierre Nkurunziza (55) amefariki dunia leo Jumanne Juni 9,2020 akisumbuliwa na Ugonjwa wa Moyo.


Burundi President Pierre Nkurunziza don die at di age of 55 of heart attack according to goment sources.
We eye still dey dis tori wey just land and we go bring una more as e dey comot. Make una load di page again to see di full tori.
Share:

Freeman Mbowe Ahamishiwa Dar Es Salaam Kwa Ajili Ya Matibabu Zaidi

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amewahamishiwa jijini Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu zaidi baada ya kushambuliwa usiku wa kuamkia leo jijini Dodoma.

Mnadhimu wa Kambia Rasmi ya Upinzani Bungeni, Esther Bulaya amesema baadae wataeleza ni hospitali gani kiongozi huyo ambaye pia ni Mbunge wa Hai anapelekwa.

Kiongozi huyo alishambuliwa usiku wa kumkia leo wakati akirejea nyumbani kwake majira ya saa sita usiku, na miongoni mwa maeneo aliyoumia ni pamoja na mguu wa kulia.

Viongozi mbalimbali wamefika kumjulia hali Mbowe ambao ni pamoja na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge, Job Ndugai, Naibu Spika, Tulia Ackson


Share:

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Amjulia Hali Freeman Mbowe

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Juni 9, 2020 amemtembelea na kumjulia hali Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe ambaye amelazwa katika hospitali ya Ntyuka jijini Dodoma kwa matibabu.

Waziri Mkuu amemuombea kiongozi huyo uponyaji wa haraka wa majeraha aliyoyapata baada ya kuvamiwa na watu ambao bado hawajajulikana wakati akiingia nyumbani kwake jijini Dodoma usiku wa kuamkia leo Juni 9, 2020.

“Nimepokea kwa masikitiko makubwa  taarifa za tukio la kuvamiwa kwa Mheshimiwa Mbowe na watu ambao bado hawajajulikana, namuomba Mwenyezi Mungu amjalie  apone haraka ili aweze kurejea katika majukumu yake.”

Baadhi ya wabunge wa Upinzani waliokuwepo hospitalini hapo na ambao walimpokea Waziri Mkuu ni Mbunge wa Bunda, Esther Bulaya, Mbunge Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa, Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi na Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema.

Mwisho.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU


Share:

HALMASHAURI YAPEWA JUKUMU UKAMILISHAJI MIRADI MAENDELEO



Madiwani wa manispaa ya Shinyanga wameutaka uongozi wa manispaa hiyo kukamilisha miradi yote ya maendeleo, ambayo haijakamilika iliyoanzishwa ndani ya miaka mitano na madiwani hao ili ikamilike na kuanza kutoa huduma kwa jamii.


Hayo yamebainishwa leo Juni 9, 2020 kwenye Baraza maalumu la madiwani wa manispaa hiyo ambalo ni la mwisho, kuwa kuna miradi mingi ya maendeleo ambayo ilianzishwa kipindi cha utawala wa madiwani hao tangu mwaka 2015, ambayo mingine bado haijamalizika kujengwa.

Baadhi ya Madiwani hao akiwemo David Nkulila wa Ndembezi, walisema ndani ya utawala wao wa miaka mitano, kuna miradi mingi ya maendeleo ambayo wameianzisha, ikiwamo ya ujenzi wa maboma ya zahanati, madarasa, mabweni, vyoo vya shule, bararaba, machinjio, dampo, ambapo mengine haijakamilika.

“Sisi madiwani tunamaliza muda wetu wa kutumikia wananchi katika manispaa hii ya Shinyanga, lakini kuna miradi ya maendeleo ambayo tuliianzisha ndani ya utawala wetu wa miaka mitano tangu 2015, ambapo mingine haijakamilika kujengwa, hivyo jukumu hili tunaliacha kwa menejimenti ya manispaa kuikamilisha,” walisema madiwani kwa nyakati tofauti

Naye Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, alisisitiza uongozi huo wa manispaa ya Shinyanga, wazungukie miradi yote ya maendeleo iliyotekelezwa na kuibaini ile ambayo haijakamilika, ili wapate kutengewa fedha kupitia makusanyo ya ndani na kuikamilisha haraka.

Katika hatua nyingine Mboneko aliwataka madiwani watakaorudi kugombea, wakafanye siasa za kistaarabu, ikiwa Serikali imejipanga vyema kuhakikisha uchaguzi huo mkuu utafanyika kwa amani na utulivu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Geofrey Magulumbi, alisema maelekezo yote yaliyotolewa watayafanyia kazi, kwa ajili ya mustakabali wa maendeleo ya manispaa hiyo.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza kwenye baraza la madiwani wa Manispaa ya Shinyanga. Picha zote na Marco Maduhu

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Stephen Masele, akizungumza kwenye baraza hilo.

Mstahiki Meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Mkadam akizungumza kwenye kikao cha baraza hilo.

Naibu Meya wa manispaa ya Shinyanga John Peter Kisandu, akizungumza kwenye kikao cha baraza hilo la madiwani.


Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi, akizungumza kwenye baraza hilo na kuahidi kuyafanyia kazi maelekezo yote yaliyotolewa.

Madiwani wa manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye baraza lao la mwisho.

Diwani wa vitimaalum Mariam Nyangaka, akizungumza kwenye baraza hilo.

Diwani wa Ngokolo Emmanuel Ntobi, akizungumza kwenye baraza hilo.

Diwani wa Ndembezi David Nkulila, akizungumza kwenye baraza hilo.

Diwani wa Ndala, Wiliamu Shayo akizungumza kwenye baraza.

Watendaji wa kata manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye baraza la madiwani wakifuatilia baraza hilo.

Watendaji wa manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye baraza la madiwani wakifuatilia baraza hilo.

Picha zote na Marco Maduhu
Share:

DC MBOGWE AWASHUKIA WATENDAJI WANAOKWAMISHA MAENDELEO YA WANANCHI

Na Mohab Dominick - Mbogwe
SERIKALI Wilayani Mbogwe Mkoani Geita imewataka watendaji wa halmashauri hiyo pamoja na viongozi wengine katika chama kutowakatisha tamaa wananchi wenye wanaojitolea nguvu zao katika zoezi la utekelezaji wa shughuli za maendeleo.

Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe Martha Mkupasi aliyasema hayo juzi wakati akizungumza na kamati ya shule ya msingi Kanegere iliyopo Kata ya Bukandwe wilayani Mbogwe alipoongozana na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo kujionea utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa vyoo 18 katika shule ya msingi Kanegere iliyopo Kata ya Bukandwe. 

Katika shule hiyo Mkupasi alisema kuwa mradi huo unatekelezwa kwa gharama ya shilingi Milioni 27. 9 huku akisisitiza kuwa serikali yake imepokea fedha kiasi cha shilingi Milioni 175 ambazo kwa sasa zinatekeleza mradi mkubwa wa vyoo 177 kwenye shule 7za msingi ikiwemo shule ya msingi Kanegele iliyotengewa Milioni 27.9 kwaajili ya ujenzi wa vyoo 18.

“Namshukuru Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli kusikia kilio chetu na kutupa fedha za ruzuku kutoka serikali kuu, Milioni 175 siyo nawaagiza watendaji wa Halmashauri fedha hizo zitumike kama ilivyopangwa asitokee mjanja mmoja akakwamisha shughuli nzima naamini mradi huu utakwenda hadi miezi miwili,” alisema Mkupasi na kuongeza.

“Ndugu zangu wananchi vyoo vya kisasa vinajengwa katika shule zenu naamini suala la kujisaidia vichakani halitakuwepo tena, licha ya shule ya msingi Kanegere kuanza kuchimbwa mashimo kwaajili matundu ya vyoo, kwa sasa kuna hatua nzuri kutokana na ushirikiano mzuri na wananchi wanaojitolea nguvu zao,” alisema Martha mkupasi mkuu wa Wilaya ya Mbogwe.

Aliwahakikishia wananchi wake kuwa mradi wa vyoo vya kisasa katika wilaya hiyo utakuwa wa mfano hapa nchini huku akitamba kuwa halmashauri zingine pindi mradi huo utakapokamilika watatua kuja kujifunza na kutumia fursa hiyo kuwaomba wananchi waendelee kuunga mkono juhudi za serikali kwa kuhamasika kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo.

“Licha ya fedha za Ruzuku Milioni 175 kutoka serikali kuu pia katika mwaka wa fedha ujao serikali kupitia Halmashauri ya Mbogwe imetenga zaidi ya shilingi Milion 200 kwaajili ya ujenzi wa vyoo ili kukabiliana na upungufu",alisema.

Nae afisa elimu takwimu na vifaa wa wilaya ya Mbogwe mkoani Geita, Frolence Leodigard akizungumza mbele ya mkuu wa wilaya kwa niaba ya afisa elimu msingi Wilaya Peter Buvuva alisema kuwa shule ya msingi Kanegere ni kati ya shule saba zinazonufaika na mradi huo na imetengewa kiasi cha shilingi Milioni 27.9 ili kutekeleza ujenzi wa vyoo vya kisasa.

“Kwa wilaya nzima upungufu wa matundu ya vyoo ni 3178, vilivyopo ni 815 na katika shule hii ya Kanegere ina jumla ya wanafunzi 1,147 wasichana ni 585 na wavulana wakiwa 562 kwa hiyoa matundu 16 ya vyoo yaliyopo shuleni hapo hayatoshelezi idadi hiyo, mahitaji ni matundu 51, yaliyopo ni 11,” alisema Leodigard.

Akizungumzia mradi huo afisa mtendaji wa Kata ya Bukandwe Muberwa Bakalemwa alimweleza mkuu huyo wa wilaya kuwa wananchi wa eneo hilo wamepokea mradi huo kwa shangwe kubwa huku akibainisha kuwa kutokana na wananchi kufuata mchanga umbali mrefu waliruhusiwa na wakala wa huduma za misitu Tanzania TFS wilaya ya Mbogwe kuzoa katika moja ya hifadhi baada ya kuwaandikia barua.

“Sisi kamati ya shule ya msingi Kanegere tulihamasisha wazazi na wananchi wengine kujitolea nguvu zao ambapo kupitia vitongoji vyao na kijiji kwaujumla wananchi waliguswa na hali ya uhaba wa vyoo na sasa wamejitolea kuchimba mashimo kwaajili ya matundu ya vyoo ikiwemo kusomba mchanga makarai matatu kila mwananchi pamoja na mawe ambayo kwa sasa yapo ya kutosha,” alisema Samweli Shitungulu mwenyekiti kamati ya shule.

Mkuu wa wilaya ya Mbogwe mkoani Geita, Martha Mkupasi aliyeongozana na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo kujionea utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa matundu vyoo 18 katika shule ya msingi kanegere iliyopo Kata ya Bukandwe.


 Wananchi wa Kata ya Bukandwe wakijitolea nguvu zao katika kushiriki ujenzi wa vyoo hivyo  ili kukabiliana na uhaba uliopo katika shule hiyo ambayo ni miongoni mwa shule saba inayonufaika na mradi wa Milioni 175 kutoka serikali kuu huku shule hiyo ikitengewa shilingi Milioni 27.9 kwaajili ya utekelezaji wa mradi huo wa vyoo vya kisasa,  na vyoo vinavyoonekana ni vya zamani.









Share:

Developer Internship Opportunities- Internship program at Smart Lab Tanzania

Developer Interns- Internship program at Smart Lab Tanzania Smart Lab is an innovation platform that links learning institutions with corporate partners to empower groundbreaking solutions that will impact African communities. Are you a fresh graduate with a degree in computer science/engineering, aspiring to become a great developer? Smart Lab is looking for you, join a diverse team of… Read More »

The post Developer Internship Opportunities- Internship program at Smart Lab Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

PICHA: Spika Ndugai Awasili Hospitali Kumjulia Hali Freeman Mbowe

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amefika Hospitalini Dodoma kumjulia hali Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe aliyelazwa hapo baada ya kushambuliwa usiku wa kumkia leo na watu wasiojulikana.



Share:

Billing Administrator: Postpaid Billing Job vacancy at Vodacom Tanzania

Billing Administrator: Postpaid Billing Job vacancy at Vodacom Tanzania Posting Country: Tanzania, United Republic of Date Posted: 08-Jun-2020 Full Time / Part Time: Full Time Contract Type: Permanent Joining Vodacom is more than a job, what we do matters. We don’t just carry minutes, texts and data – we carry people’s lives. And that’s a huge responsibility. If… Read More »

The post Billing Administrator: Postpaid Billing Job vacancy at Vodacom Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Head Of Marketing at DKT Tanzania Dar es Salaam, Tanzania

Position description The Head of Marketing will be in charge of all DKT Tanzania Marketing activities incorporating all product lines. He/she will be responsible for developing the marketing strategy with his/her team to ensure targets are met and surpassed via a winning strategy that creates even greater health impact. The primary purpose of the position is to accelerate… Read More »

The post Head Of Marketing at DKT Tanzania Dar es Salaam, Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Program Support Specialist – Health (Arusha City) at Compassion International Arusha, Tanzania

Program Support Specialist – Health (Arusha City) at Compassion International Arusha, Tanzania Overview The role of Program Health Support Specialist will provide subject matter expertise regarding the health of all program beneficiaries (pregnancy through youth).  This role will collaborate with other Support Specialists, Program Trainers and Partnership Facilitators to ensure staff and Implementing Church Partners are adequately informed… Read More »

The post Program Support Specialist – Health (Arusha City) at Compassion International Arusha, Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

PICHA: Naibu Spika Dkt Tulia Ackson Akiwasili Hospitali Kumjulia Hali Freeman Mbowe Aliyevamiwa na Kuvunjwa Mguu Dodoma

Naibu Spika, Dkt Tulia Ackson akiwasili katika Hospitali ya DCMC Ntyuka kumjulia hali M/Kiti wa Chadema na Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe aliyelazwa katika hospitali hiyo akipatiwa matibabu baada ya kuvamiwa na kujeruhiwa na watu wasiojulikana.

*****

Naibu Spika, Dk.Tulia Ackson  amemjulia hali Mwenyekiti Chadema, Freeman Mbowe katika Hospitali ya Ntyuka, Dodoma anakopatiwa matibabu  baada ya kuvamiwa na watu wasiojulikana na kisha kujeruhiwa na kuvunjwa mguu mmoja na kusema kuwa amemuona akiwa na majeraha mguuni na kwamba wanasubiri taarifa ya daktari ili kujua ameumia kwa kiasi gani.

"Ana maumivu ya mguu, mimi nimemuona ila bado wanaendelea kufanya uchunguzi na vipimo vingine, niwatoe hofu watanzania kwamba yupo anaendelea kupata huduma"- Amesema Naibu Spika Baada ya kumtembelea Mbowe 


Share:

PICHA: Freeman Mbowe Akiwa Amelazwa Baada Ya Kushambuliwa na Kuvunjwa Mguu Dodoma Leo

Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe akiwa amelazwa katika hospitali ya DCMCT Ntyuka mkoani Dodoma kwa matibabu baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana na kuvunjwa mguu.




Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger