Friday, 15 May 2020

Waziri Mkuu Akagua Ujenzi Wa Reli Ya Kisasa (SGR)....Asema Nguzo Za Umeme 154 Kati Ya 160 Zimeshasimikwa

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) na kusema kuwa mradi huo umesaidia kupungua tatizo la ajira kwa kuajiri wafanyakazi 18,700.

“Kukamilika kwa awamu ya kwanza ya mradi huu, kumesaidia kupunguza ukosefu wa ajira kwa kutoa ajira 7,400 kwa kipande cha Dar hadi Morogoro. Kipande cha Morogoro hadi Singida kimetoa ajira 6,300 wakati mradi wa umeme kutoka Bwawa la Mwalimu Nyerere nao pia umetoa ajira 5,000,” amesema Waziri Mkuu

Waziri Mkuu amesema hayo jana (Alhamisi, Mei 14, 2020) baada ya kutembelea mradi huo na kuzungumza na wananchi aliowakuta kwenye stesheni ya Soga, iliyoko wilayani Kibaha, mkoani Pwani.

Amesema faida nyingine ya mradi huo katika awamu yake ya kwanza, ni kupunguzwa kwa muda wa safari kati ya Dar es Salaam na Morogoro. Amewataka wananchi hao wawe walinzi wa mradi huo kwa sababu utakapokamilika utawanufaisha na wao pia.

Reli hiyo itakuwa na vituo sita vya Dar es Salaam, Pugu, Soga, Ruvu, Ngerengere na Morogoro, huku vituo vya Dar es Salaam na Morogoro vikiwa ndiyo vituo vikuu. “Kwenye vituo vya kushusha abiria vya reli hii, kutakuwa na huduma za kibenki na maduka, kwa hiyo wananchi hata kama hamsafiri, mtaweza kupata huduma na mahitaji yenu kutokea hapo,” amesema.

Akielezea maendeleo ya mradi huo unaojengwa kwa awamu mbili, Waziri Mkuu amesema Serikali iliweka malengo ya kukamilisha mradi huo kwa wakati na ndiyo maana aliamua kwenda kuukagua.

“Katika awamu ya kwanza, ambayo inatoka Dar es Salaam hadi Morogoro (km. 300), mradi huu umekamilika kwa asilimia 77.91. Hii maana yake ni kwamba wamemaliza kazi hii kwa zaidi ya robotatu. Wametengeneza njia na kulaza mataruma na mimi nimekuja na hii treni maalum kwa karibu kilometa 20,” amesema huku akishangiliwa na wananchi hao.

“Rais wetu, Dkt. John Pombe Magufuli alianzisha mradi huu na kuwaahidi Watanzania kwamba tunaweza kuujenga kwa fedha zetu. Vilevile, mradi huu ni utekelezaji wa agizo la Ilani ya CCM ambalo linaitaka Serikali ya awamu ya tano, iimarishe usafiri wa reli nchini.”

Amesema katika kutekeleza agizo hilo, Serikali ya awamu ya tano, mbali ya kujenga reli hiyo ya kisasa, imefanikiwa pia kufufua reli ya kutoka Dar – Tanga – Moshi ambayo ilikuwa haitumiki kwa zaidi ya miaka 20. Huduma ya mizigo katika reli hiyo ilikuwa haifanyi kazi kwa miaka 12 na huduma ya kusafirisha abiria ilisitishwa tangu mwaka 1994.

Akielezea kuhusu awamu ya pili ya ujenzi wa mradi huo, Waziri Mkuu amesema ujenzi wa reli kutoka Morogoro hadi Makutupora, Dodoma (km. 422) ulianza mwaka jana mwishoni na sasa hivi umefikia asilimia 30 ya kazi, ambapo wanatarajia kuukamilisha ifikapo Juni, 2021.

Waziri Mkuu amesema sambamba na ujenzi wa reli hiyo, umeme pia umeanza kuwekwa ambapo nguzo 154 kati ya 160 zinazotakiwa kuwepo zimeshasimikwa. “Tumeweka miundombinu ya umeme kutoka Bwawa la Mwalimu Nyerere, kutoka Kidatu na Kinyerezi. Nia yetu ya kupata umeme kutoka vyanzo vyote vitatu, ni kuhakikisha kuwa umeme upo saa zote.”

“Tuna uhakika wa kutumia umeme wa Kinyerezi na Kidatu au Kidatu na Mwalimu Nyerere au Mwalimu Nyerere na Kinyerezi na hata umeme ukikatika kabisa, mabehewa yetu yana uwezo wa kutunza umeme kwa dakika 45, na katika muda huo, ni lazima tutakuwa tumerejesha umeme kutoka chanzo kimojawapo,” amesema.

Waziri Mkuu amesema kuwa ameridhishwa na ujenzi wa reli hiyo na akawapongeza mafundi wa kampuni ya Yapi Merkezi ya Uturuki ambayo inajenga reli hiyo. “Kampuni ya Yapi Merkezi imefanya kazi kama walivyosaini kwenye mkataba na Serikali, na ninaamini watakamilisha kazi kabla ya muda,” amesema.

(mwisho)
IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU


Share:

Serikali Yaridhishwa Na Utendaji Kazi Wa Bodi Za Parole Nchini

Na ASP. Lucas Mboje, Dodoma
SERIKALI imeridhishwa na kiwango cha kazi zinazofanywa na Bodi ya Taifa ya Parole pamoja na Bodi za Parole mikoa katika utekelezaji wa Sheria ya Bodi ya Parole nchini licha uwepo wa changamoto mbalimbali.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe. Hamad Masauni(Mb)katika hafla ya uzinduzi rasmi wa Bodi ya Taifa ya Parole iliyofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango, jana Mei 14, 2020 jijini Dodoma ambapo amewataka kutekeleza wajibu wao ipasavyo kama Rais Dkt. John Pombe Magufuli alivyowaamini na kuwapa jukumu hilo.

“Serikali inaridhishwa sana na kiwango cha kazi mnazozifanya kikamilifu katika urekebishaji wa wahalifu kwa kuwapa wafungwa fursa ya kutumikia sehemu ya adhabu zao wakiwa nje ya magereza kwa usimamizi wa jamii nzima. Hongereni sana”, amesema Naibu Waziri Masauni.

Waziri Masauni amesema kuwa ustarabu wa nchi zote duniani hupimwa kwa kuzingatia namna zinavyoshughulikia uhifadhi salama na urekebishaji wa wahalifu katika magereza.

Aidha, ameongeza kuwa nyenzo kubwa ya msingi zitakazowawezesha wajumbe wa Bodi hiyo ni kujenga uewelewa wa mpango wa Parole , uelewa wa dhana na filosofia yake na umhimu wake katika jamii.

“ Ni muhimu sana ninyi wajumbe wa bodi hii ya Taifa Parole kuielewa sheria yenyewe na taratibu zake kiutekelezaji, dhana yenyewe, filosofia ya mpango wa Parole na manufaa yake katika jamii”, amesisitiza Naibu Waziri Masauni.

Wakati huo huo, Naibu Waziri Masauni amewaasa wafungwa wote wa Parole nchini ambao wamenufaika na utaratibu huo kuwa na nidhamu na washirikiane vema na jamii inayowazunguka ili kudhihirisha kwamba wamebadilika tabia na kuaacha uhalifu.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa Parole, Dkt. Augustino Mrema amesema kuwa atahakikisha kuwa anafanya kazi kwa weledi mkubwa huku akishirikiana na wajumbe wote na atahakikisha bodi hiyo inasonga mbele na si kurudi nyuma. Aidha, ametoa shukrani za dhati kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kumteua kuwa Mwenyekiti wa bodi hiyo.

“Napenda nitoe shukrani zangu za kipekee kwa Rais Magufuli kwa kuniteua kwa mara nyingine kuiongoza bodi hii, kuteuliwa kwangu ni ishara ya imani katika kulibeba jukumu hili la kijamii”, amesema Mwenyekiti Parole Taifa, Dkt. Mrema.

Kwa upande wake, Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Suleiman Mzee ambaye pia ni Katibu wa Bodi ya Taifa Parole amempongeza Mhe. Dkt. Augustino Mrema kwa kuteuliwa tena  kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa Parole pamoja na wajumbe wote na kuongeza kuwa hiyo inadhihirisha imani kubwa ya Serikali katika kubeba dhamana hiyo.

Kamishna Jenerali Mzee amesema kuwa tangu bodi hiyo ya Parole Taifa ianze kutekeleza Sheria ya Parole nchini mpaka sasa wamefanikiwa kujadili wafungwa 6,237, wafungwa walionufaika kwa Parole ni 5,535, na wafungwa waliokataliwa kwa sababu mbalimbali 702.  Aidha, mpaka sasa ni wafungwa 25 tu ndio waliokiuka masharti ya Parole na kurudishwa magerezani.

“Mhe. Naibu Waziri mpaka sasa jumla ya vikao 41 vimeshafanyika tangu ianzishwe Sheria ya Bodi za Parole nchini na imewezesha kujadili wafungwa hawa walionufaika na wale ambao hawakunufaika”, amesema Kamishna Jenerali Mzee.

Bodi ya Taifa Parole ni tasnia muhimu sana katika urekebishaji wa wahalifu kwa kuishirikisha jamii. Tangu kuanzishwa kwa bodi hiyo mwaka 1994 mafanikio makubwa yameonekana kutokana na baadhi ya wafungwa kuachiliwa kupitia utaratibu huu hivyo kupunguza sehemu ya changamoto ya msongamano magerezani.


Share:

Wagonjwa Wa Corona Uganda Wafika 160...Ni Baada Ya Wengine 21 Kuongezeka

Uganda imethibitisha wagonjwa wapya 21 wa homa ya COVID19 na kufanya idadi ya maambukizi kuwa 160.

21 hao wamebainika baada ya kufanyika vipimo kwa sampuli 1593 za madereva katika mipaka ya Mtukula ,Busia ,Malaba na Elegu.

Wizara ya Afya nchini humo imesema, kati ya hao Wakenya ni 08, Waganda ni 05, Watanzania ni 07 na Mmoja ni Raia wa Sudani



Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa May 15



















Share:

Tumefanya Maboresho Kwenye App Yetu ya Mpekuzi Ili Kukuwezesha Kupata Habari zetu Haraka hasa Wakati huu wa janga la Corona

Tumefanya maboresho katika App yetu ya MPEKUZI ili kuendana na changamoto ya sasa ya janga la Corona inayoikumba dunia Nzima

Usikubali kupitwa na taarifa muhimu zinazoendelea hapa nchini na Duniani  kwa Ujumla . Tumejipanga vizuri sana kukupatia taarifa sahihi na kwa wakati.

👉1. Tumebadili muonekano na kuufanya kuwa mzuri zaidi
👉2. Kila habari tunayoweka kuanzia sasa utapata notification kwenye simu yako 
👉3. Habari zote kwa sasa zinafika kwa haraka kwenye simu yako kuliko ilivyokuwa hapo awali

KUMBUKA: App yetu ni BURE. Unachotakiwa kukifanya ni kuingia Playstore na kupakua MPEKUZI APP

Kama tayari unayo, basi Ingia Playstore kwa ajili ya kupata UPDATE hii ya Toleo Jipya

Tumekurahisishia, Unaweza pia ...<<KU BOFYA HAPA>> Kupata toleo hili Bure Kabisa


Share:

Thursday, 14 May 2020

UDSM-CALL FOR PROPOSALS FOR COMPETITIVE RESEARCH AND INNOVATION GRANTS FOR YEAR 2020-2021

The University of Dar es Salaam has a noble obligation to contribute to the national development through teaching, research, innovation and public services. Guided by its grand Vision 2061, the University seeks to become a leading center of intellectual wealth spearheading the quest for sustainable and inclusive development. This Vision is coupled with an aspiration of becoming a… Read More »

The post UDSM-CALL FOR PROPOSALS FOR COMPETITIVE RESEARCH AND INNOVATION GRANTS FOR YEAR 2020-2021 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Jeshi La Polisi Dodoma Lakamata Magari 6 Ya Wizi......latangaza Dau La Milioni Moja Kwa Mtu Atakayesaidia Kutoa Taarifa Za Wizi Wa Magari

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Jeshi la Polisi mkoani Dodoma linayashikilia magari sita  yanayodhaniwa kuwa ya wizi .

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Mei,14,2020 jijini Dodoma Kamanda wa Polisi mkoani hapa SACP Gilles Muroto amesema  mnamo tarehe 10/05/2020 majira ya saa 10  kijiji cha Mbande  ,kata ya Sejeli ,wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma   barabara kuu ya Morogoro –Dodoma , lilikamatwa gari Na.T.936 Toyota Land Cruiser VX Rangi nyeupe ,Chassis Na.HDJ800003615 na Engine Na.1HZ80-0019603.

Kamanda Muroto amebainisha kuwa katika uchunguzi wa awali gari limegundulika kutofautiana na taarifa zilizopo kwenye kadi inayoonesha Chassis Na.HZJ800019603  na Engine Namba 0111948  tofauti kabisa na uhalisia  na kutiliwa mashaka kuwa ni mali ya wizi.

Dereva Ramadhan Zaniel Sekiondo [31] mkazi wa Magomeni Mikumi Dar E s Salaam   alikuwa akilipeleka mkoani Tabora  kwa mtu asiyemfahamu akitokea Dar Es Salaam  baada ya kukabidhiwa na mtu asiyemfahamu  anayeishi  jiji Dar Es Salaam .

Katika tukio la pili Kamanda Muroto amefafanua kuwa mnamo  tarehe 11/5/2020 eneo la Area A  kata ya Kizota jijini Dodoma yalikamatwa magari mawili yaliyokuwa yamehifadhiwa kwa kufungiwa ndani ya nyumba yasiyo na Namba za usajili yakitumia Namba ya Chassis ambayo ni Toyota HARRIER Chassis Na.MCU310001691,Engine Na.1MZ1589700 na Toyota IST Chassis Na.NCP600209833 Engine Na.2MZ3578179.

Katika uchunguzi wa awali imegundulika kuwa hayana kumbukumbu zozote  na yaliingia nchini bila Uhalali huku  uchunguzi zaidi ukiendelea kwa kushirikiana na Interpol  na mtuhumiwa Omari Chilipachi [29] mkazi wa Sinza DSM anahojiwa na jeshi la Polisi.

Aidha,siku hiyohiyo,  Eneo la  Area A  Kata ya Kizota jijini hapa lilikamatwa gari aina ya Land Rover Discovery  lenye namba za usajili wanchi ya Afrika kusini  namba SJV576 GP  Chassis Na.SALLAAA135A339616 ambazo zinatofautiana na  zilizopo katika gari  049053121030305071757 ambalo halipo kwenye mfumo wa usajili wa magari  na mtuhumiwa Jamal Swalehe Rasidi [28] mkazi wa Area A anaendelea kuhojiwa na jeshi la polisi.

Katika tukio jingine,Kamanda Muroto amesema mnamo tarehe 12/5/2020  eneo la Nzunguni jijini Dodoma lilikamatwa  gari aina ya Toyota Alphard lenye kadi Na.384 DMU lenye  Chassis Na. ANH100038956 Engine Na.2AZ1184313   ambapo katika uchunguzi wa awali ulibaniwa kuwa  chassis ANH100030547 na Engine ZNZ 0860988  halisi kwenye gari zinatofautiana na lililetwa Dodoma kwa matengenezo kutoka Mbeya  na Mtuhuiwa Gofrey Amos Sanga[37] mkazi wa Nzunguni anaendelea kuhojiwa.

Mnamo tarehe 13/5/2020  stand ya Daladala Sabasaba jijini Dodoma lilikamatwa gari  Na.T.589 BAD aina ya Toyota Hiace yenye  Chassis  LH1741000724,Engine  5L5091996  na baada ya ukaguzi wa awali liligundulika kutofautiana na namba halisi  ambazo ni chassis LH12330013812 na Engine 3L4538966.

Hata hivyo kamanda Muroto amesema wilayani Kondoa na Dodoma katika mwendelezo wa msako wa wezi wa pikipiki walikamatwa watuhumiwa wawili wa wizi wa pikipiki .

Pia,Kamanda Muroto amebainisha kuwa mnamo tarehe 13/5/2020  eneo la Medeli kata ya Tabuka Reli jijini Dodoma  alikamatwa Shaban Nyamhanga Wisandala [32] mkazi wa Medeli akijifanya afisa usalama wa taifa  na kuwatapeli watu  pamoja na kuwafanyia vitishio.

Jeshi la Polisi mkoani Dodoma limetoa dau la Tsh.milioni moja kwa mtu atakayesaidia kutoa taarifa ya wizi wa magari.


Share:

Kijana Atiwa Mbaroni Baada Ya Kutumia sare za JWTZ alizomwibia Baba Mkwe Wake Na Kuzitumia Kutapeli Watu

Jeshi la Polisi mkoani Kagera linamshikilia kinyozi wa Arusha, anayedaiwa kuiba na kuvaa sare za Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) za baba mkwe wake na kuzitumia mkoani hapa kutapeli vijana kuwa anaratibu uandikishaji kwa wanaohitaji kujiunga na jeshi hilo.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera, Revocatus Malimi amemtaja mtuhumiwa kuwa ni Mrisho Ibrahim (34) mkulima na kinyozi, mkazi wa Mtaa wa Kimandolu jijini Arusha.

Alisema Ibrahim ambaye alikwenda mkoani Kagera kwa lengo la kumtembelea rafiki yake wa kike, alikamatwa Mei 5, mwaka huu Kamachumu wilayani Muleba akiwa na sare kamili baada ya kujitambulisha kwa uongo kuwa ni mwajiriwa na askari wa JWTZ mwenye cheo cha Private kikosi cha Mizinga Arusha.

“Baada ya kufika mkoani Kagera na kumkosa mpenzi wake ambaye alikuwa amehama nyumba, aliishiwa fedha ndipo akaamua kutumia sare hizo kufanya utapeli.

“Mtuhumiwa huyo alikamatwa akiwa kwenye nyumba ya kulala wageni ya Ruto, ambako alipangishiwa na mwenyeji wake ambaye ni askari mgambo aliyemtaja kwa jina moja la Rweyemamu,” alidai Kamanda Malimi.

Alidai kuwa katika mahojihano mtuhumiwa alikiri kuwa si mwajiriwa wa JWTZ na kwamba sare hizo ni mali ya baba mkwe wake ambaye ni askari wa jeshi hilo.

Kamanda Malimi alidai kuwa Ibrahim alisema kwamba alizichukua sare hizo baada ya kukabidhiwa jukumu la kuwa mwangalizi wa makazi ya baba mkwe ambayo yapo Arusha Kimandolu.

“Aliamua kuvaa sare hizo na kuja nazo hadi Muleba Kagera ambako alimfuata rafiki yake wa kike (mchepuko), lakini akamkosa baada ya kuwa amehama, ndipo kutokana na kukosa fedha akamuona huyo askari mgambo na kumdanganya kama anataka kazi ya JWTZ atafute pesa na hata kama kuna vijana wengine apelekewe wakiwa na fedha.

“Hadi anakamatwa alikuwa anatafutiwa vijana hao. Hivyo tunaendelea na upelelezi, ushahidi ukikamilika atafikishwa mahakamani,” alisema Kamanda Malimi.


Share:

Job Opportunity at EWURA, Senior Electricity Inspector

Senior Electricity Inspector
The Energy and Water Utilities Regulatory Authority (EWURA) is an independent, world class regulatory authority responsible for licensing, tariff setting and quality of sendee regulation of the electricity, water, petroleum and natural gas sectors. EWURA has the following vacancies for which suitably qualified Tanzanian are invited to apply.

THE ELECTRICITY DIVISION
Post Title: Senior Electricity Inspector – 1 post
Duty Station: EWURA Lake Zone Office
Reports to: Zonal Manager
Senior Electricity Inspector will be responsible for a day to day Electricity Inspection activities to ensure the complience to the applicable standards and good industry practice.

Main Duties and Responsibilities:
  1. To participate in coordination of the process of overseeing effective and efficient application of provisions of the Electricity Act in  order to ensure environmental and safety aspects of electricity sector are in conformity with provision of the Act and good industry practices.
  2.  To inspect electrical installations in buildings and any other electricity supply infrastructure to ensure compliance with applicable industry standards.
  3. To review performance and ethics of Electrical Installation Licensees to identify malpractices in electrical installation activities.
  4. To inspect various premises under construction and submit inspection report for further recommendations to responsible authorities for
  5. To participate in dispute resolutions of various customers’ complaints.
  6.  To inspect premises damaged by electrical accidents.
  7.  To respond to any reported electrical emergency event.
  8. To conduct pre and post installation inspections of standby and own uses generators.
  9. To participate in pre licensing inspection of electrical facilities undertaken by the Directorate.
  10. To assist in coordinating and preparation of the Annual Directorate report and Annual Sector report.
  11.  To undertake any other duties as assigned by superiors.
Minimum Academic Qualifications and Experience

The ideal candidate for this position should have the following qualifications and experience;
  1.  University Degree in Electrical Engineering.
  2. Possession of Master degree qualifications in the relevant field will be an added advantage.
  3. Registration with Engineers Registration Board as a professional engineer (ERB) is a must.
  4. Knowledge and Competence in Information and Communications Technology (ICT) application
  5.  Possession of at least five (4) years working experience in relevant field.
Tenure and Remuneration

A competitive salary will be offered to the right candidates for the posts.
EWURA is an equal opportunity employer.
Staff will be employed on permanent and pensionable terms.

Mode of Application

Application letter with Curriculum Vitae (CV) including e-mail address or day time contact telephone number, together with photocopies of certificates and transcripts (certificates from Foreign Universities should be verified by The Tanzania Commission for Universities (TCU), Birth certificate, one passport size photo and names and contacts of three referees should be addressed to reach the under-mentioned by 22nd May 2020

Only short-listed candidates meeting the above criteria will be invited for interview. Lobbying and canvassing for employment will not be entertained and may work to the candidate’s disadvantage.

Application letter should be addressed to:

The Director General,
Energy and Water Utilities Regulatory Authority (EWURA)
4th Floor, LAPF House Makole Road,
P.0 Box 2857
DODOMA


Share:

Job Opportunity at EWURA, Office Attendant

Office Attendant at EWURA 
The Energy and Water Utilities Regulatory Authority (EWURA) is an independent, world class regulatory authority responsible for licensing, tariff setting and quality of sendee regulation of the electricity, water, petroleum and natural gas sectors. EWURA has the following vacancies for which suitably qualified Tanzanian are invited to apply.

CORPORATE AFFAIRS DIVISION
Post Title: Office Attendant – 1 Post
Duty Station: EWURA Eastern Zone Office
Reports to: Stores cum Assistant Administrative Officer
Office Attendant will be responsible for assisting the day to day administrative and clerical work of the Authority.

Duties and Responsibilities:
  1. To move/run mails, other correspondences goods and supplies within the Authority.
  2. To move/run mails and other correspondences outside the Authority.
  3. To provide general administrative assistance.
  4.  To provide cleaning to the Authority’s offices.
  5. To undertake any other duties as assigned by the supervisor.
Academic Qualifications and Experience
The ideal candidate for this position should have the following qualifications and experience.

    Form IV certificate with pass grade in English.
    Possession of a certificate in office management will be an added advantage.
    No prior work experience is required but Possession of work experience in related field will be an added advantage.

Personal Attributes
In addition to the above skills and qualifications, applicants for the above positions are required to have the following attributes:

    A very high level of integrity, honesty and sense of responsibility;
    Ability to work under pressure and produce expected results;
    Ability to work in a dynamic team;
    Ability to self-manage, achieve results and meet deadlines; and
    Willingness to work beyond the call of duty.

Tenure and Remuneration
A competitive salary will be offered to the right candidates for the posts.
EWURA is an equal opportunity employer.
Staff will be employed on permanent and pensionable terms.

Mode of Application
Application letter with Curriculum Vitae (CV) including e-mail address or day time contact telephone number, together with photocopies of certificates and transcripts (certificates from Foreign Universities should be verified by The Tanzania Commission for Universities (TCU), Birth certificate, one passport size photo and names and contacts of three referees should be addressed to reach the under-mentioned by 22nd May 2020

Only short-listed candidates meeting the above criteria will be invited for interview. Lobbying and canvassing for employment will not be entertained and may work to the candidate’s disadvantage.

Application letter should be addressed to:

The Director General,
Energy and Water Utilities Regulatory Authority (EWURA)
4th Floor, LAPF House Makole Road,
P.0 Box 2857
DODOMA


Share:

Head, Financial Crime Compliance at Standard Chartered Bank

Head, Financial Crime Compliance  Job: Compliance Primary Location: Africa & Middle East-Tanzania-Dar es Salaam Schedule: Full-time Employee Status: Permanent About Standard Chartered  We are a leading international bank focused on helping people and companies prosper across Asia, Africa and the Middle East. To us, good performance is about much more than turning a profit.  It’s about showing how… Read More »

The post Head, Financial Crime Compliance at Standard Chartered Bank appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Office Attendant at EWURA

Office Attendant at EWURA   The Energy and Water Utilities Regulatory Authority (EWURA) is an independent, world class regulatory authority responsible for licensing, tariff setting and quality of sendee regulation of the electricity, water, petroleum and natural gas sectors. EWURA has the following vacancies for which suitably qualified Tanzanian are invited to apply. CORPORATE AFFAIRS DIVISION Post Title: Office… Read More »

The post Office Attendant at EWURA appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Kabudi Atoa Sababu Tanzania Kutohudhuria Mikutano ya EAC, SADC

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi ametoa sababu za Tanzania kutoshiriki kwenye mikutano ya kikanda ukiwemo mkutano wa Korido ya Kaskazini wa Jumuiya ya Afika  Mashariki unaohusisha nchi nne pamoja na mkutano wa SACU uliotishwa na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa.

Profesa Kabudi alitoa ufafanuzi huo jana Mei 13,2020 Bungeni Mjini Dodoma 
 
Profesa Kabudi alianza kwa kuelezea mkutano uliohusisha nchi nne ambazo zinaunda Korido ya Kaskazini ambapo alisisitiza mkutano huo haukuwa unaihusu Tanzania ingawa ilikuwa na taarifa za kufanyika kwake.

"Mkutano ambao umefanyika ni wa Korido ya Kaskazini na walitutaarifu na tulijua, kwanini walitutaarifu lakini kwanini tuhudhurie mkutano wa Korido ya kaskazini? Ni wa kwao , ule haukuwa mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

"Na sitaki kurudia aliyoyasema Rais mstaafu Jakaya Kikwete mwaka 2012, hayo yamepita tusiruhusu maadui zetu kutaka kuitingisha Jumuiya hii ya Afrika Mashariki. Wana yao na sisi tusiwe sehemu ya hayo, ndwele si sifa lakini Tanzania haijawahi kuacha kusimamia maslahi yake pamoja na udogo wa nchi hii kiuchumi.

"Nchi hii(Tanzania) imefanya mambo makubwa sana kwa hiyo nataka kuwahakikishia mkutano ule wa zile nchi nne ulikuwa ni mkutano wa majadiliano wa Korido ya kaskanini,lakini sisi na Rwanda tumekuwa na centre Corido , ndio maana sisi na Burundi hatukwenda, kwasababu Burundi ni Centre Corido.Kwanza utafanyikaje bila sisi kualikwa.Kwanza nilitaka hilo lieleweke na watu wasikuze,"alisema Profesa Kabudi wakati anatoa ufafanuzi.
 
Kuhusu mkutano ulioitishwa na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, Profesa Kabudi alisema kuwa Rais huyo hakuitisha mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC),kwani mikutano ya SADC inaitishwa na Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo kwa kushiriana na Mwenyekiti .

Alisema kuwa mkutano uliotishwa na Rais Ramaphosa ulikuwa ni mkutano wa nchi ambazo ni majirani wa Afrika Kusini(SACU)ambao wengi wao wako SACU ukiondoa Zimbabwe ingawa inapakaa na Afrika kusini, Msumbuji na Angola na ndio maana nchi nane hazikuhudhururia.

Profesa Kabudi alizitaja nchi ambazo hazikuhudhuria mkutano huo wa SACU ni Tanzania, Zambia, Malawi,Madagasca, Mauritius, Comoro na DRC


Share:

Senior Electricity Inspector at EWURA

Senior Electricity Inspector  The Energy and Water Utilities Regulatory Authority (EWURA) is an independent, world class regulatory authority responsible for licensing, tariff setting and quality of sendee regulation of the electricity, water, petroleum and natural gas sectors. EWURA has the following vacancies for which suitably qualified Tanzanian are invited to apply. THE ELECTRICITY DIVISION Post Title: Senior Electricity… Read More »

The post Senior Electricity Inspector at EWURA appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Waziri Kabudi Asema Zambia Haijafunga Mpaka Wake na Tanzania....."Hawajafunga Mpaka na Nina Barua Yao Wametuandikia"

Serikali imewatoa hofu Watanzania na kusema kwamba Zambia haijafunga mpaka wake na Tanzania. Imesisitiza kuwa uhusiano kati ya nchi hizo ni mzuri.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi, ametoa ufafanuzi huo jana Bungeni jijini Dodoma, wakati akihitimisha hoja za Wabunge waliojadili Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2020/2021.

" Nataka niwaambie Zambia haijafunga mpaka na Tanzania, narudia tena Zambia haijafunga mpaka na Tanzania ,haya si maneno yangu,ninayo barua kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje nchini Zambia Joseph Malanji ambaye Mungu amemjaalia kujua lugha nyingi.

"Kwa hapa Tanzania anazungumza kinyakyusa , Kinyiha, Kinyamwanga, na jana na leo tumezungumza kwa Kiswahili. Naomba nisome barua yake japo ni jambo ambalo si la kawaida , ameniandikia barua ambayo imefika leo baada ya kufanyika kwa mazungumzo,"alisema Profesa Kabudi na kisha kuisoma barua hiyo iliyoandikwa kwa lugha ya Kingereza. 


Profesa Kabudi alifafanua kwa mujibu wa barua hiyo ambayo imefafanua kwa kina kuwa Zambia haijafunga mpaka, imeeleza kuwa Kamati ya timu ya watalaamu kutoka Tanzania na Zambia watakutana kwa pamoja kuweka mambo sawa na kisha huduma kurejea kama kawaida.
 
Aidha, Waziri Kabudi, amesema, kamwe Tanzania haitaruhusu maadui kutaka kuivuruga Jumuiya ya Afrika Mashariki.


Share:

SHIRIKA LA SEMA LATOA MAFUNZO YA KUJIKINGA NA VIRUSI VYA CORONA KWA WASAIDIZI WA KISHERIA ILONGERO MKOANI SINGIDA

 Mtoto Samia Selemani akinawa mikono  wakati wa kampeni ya utoaji elimu ya namna ya kujikinga dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa corona Ilongero Wilaya ya Singida Vijijini mkoani Singida jana. 



Kampeni hiyo ilifanywa na Shirika lisilo la Kiserikali  la Sustanable Environment Management Action (SEMA) kwa kushirikiana na wadau kutoka Taasisi ya Empower Youth Prosperity  ( EYP) ya mkoani Mbeya kwa ufadhili wa Shirika la Stromme East Africa Foundation lenye Makao Makuu Kampala nchini  Uganda huku ufadhili mkuu wa mashirika hayo ukitolewa na Shirika la Stromme Foundation la Norway kupitia mradi wa uwezeshaji jamii kiuchumi unaowalenga vijana wa kiume, wa kike, watoto na wakina mama.
Mdau wa mapambano dhidi ya Corona kutoka Taasisi ya Empower Youth Prosperity  ( EYP) ya mkoani Mbeya, Amani Twaha akitoa elimu ya kujikinga dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa corona kwa Wasaidizi wa Kisheria wa Ilongero mkoani Singida ili nao wakatoe elimu hiyo kwa wananchi. 
Mdau wa mapambano dhidi ya Corona, Amani Twaha  akionesha namna  sahihi ya kunawa mikono.
 Msaidizi wa Kisheria, Salum Kaghondi wa Ilongero, akionesha namna ya kunawa mikono baada ya kupata elimu.


Wasaidizi wa Kisheria wa Ilongero mkoani Singida wakipata elimu ya kujikinga dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa corona.
 Kampeni ya utoaji elimu kwa njia ya mabango ikifanyika. 
 Afisa wa Shirika lisilo la Kiserikali  la Sustanable Environment Management Action (SEMA) la Mkoa wa Singida, Gerson Janga  akitoa elimu kwa mafundi baiskeli wa Ilongero jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa corona. .
 Afisa Mtendaji wa Ilongero, Mohammed Mambo akielezea mafanikio ya kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo.
 Mkazi wa  Ilongero, Sued Sued akizungumzia umuhimu wa Serikali kutoa idadi ya watu waliobainika kuwa na ugonjwa huo kama inavyofanywa na nchi nyingine.
  Mkazi wa  Ilongero, Hussein Ndeso akizungumzia ugonjwa huo ulivyobadilisha naamna ya kuswali.
 Mdau wa mapambano dhidi ya Corona kutoka Taasisi ya Empower Youth Prosperity  ( EYP) ya mkoani Mbeya, Ipyana Mwakyusa akitoa elimu ya kujikinga dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa corona kwa wakina mama katika Kituo cha Afya cha Ilongero.
 Afisa Tabibu wa Kituo cha Afya cha Ilongero, Grace Kishindo akielezea mafanikio ya kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo.
 Afisa Tabibu wa Kituo cha Afya cha Ilongero, Grace Kishindo (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Wadau wa mapambano dhidi ya Corona. Kutoka kulia ni Witness Anderson, Hashim Mtahyabarwa, Muuguzi wa kituo hicho cha Afya na Ipyana Mwakyusa  kutoka Taasisi ya Empower Youth Prosperity  ( EYP) ya mkoani Mbeya.
  Afisa Tabibu wa Kituo cha Afya cha Ilongero, Grace Kishindo (kulia) , akiwaelekeza jambo wafanyakazi wenzake.
 Kampeni wa njia ya mabango ikiendelea Stendi ya Mabasi ya Ilongero.
 Afisa wa Shirika lisilo la Kiserikali  la Sustanable Environment Management Action (SEMA) la Mkoa wa Singida, Daria John akitoa elimu kwa wananchi katika  Stendi ya Mabasi ya Ilongero.
  Afisa wa Shirika la SEMA, Veronica Peter akitoa elimu ya namna ya kujikinga dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa corona wa abiria waliokuwa ndani ya Noah katika  Stendi ya Mabasi ya Ilongero.

Mwanasheria wa Shirika la SEMA, Joseph Lakati, akitoa elimu  kwa njia ya bango.

Share:

Finance Team Leader at Hyatt

Finance Team Leader  Summary Person responsible for below Account payable Cost control General cashier Qualifications To be Successful in This Role, You Will Require to Have; Minimum of two years’ experience in the industry and previous experience at a 5 start hotel. Certificate or qualification in Finance and/or Accounting. CLICK HERE TO APPLY

The post Finance Team Leader at Hyatt appeared first on Udahiliportal.com.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger