Tuesday, 12 May 2020
WALIOFARIKI KWA CORONA NCHINI MAREKANI WAFIKA 81,795
PAKUA APP YA MALUNDE 1 BLOG ...IMEBORESHWA KWA UBORA WA HALI YA JUU KUKUWEZESHA KUPATA HABARI ZOTE KWA WAKATI KIPINDI HIKI CHA CORONA
Pakua App mpya ya Malunde 1 blog imeboreshwa zaidi ili kukidhi mahitaji ya wasomaji wetu. Hii ndiyo mpya kabisa,ina alama hii ↡↡
FULL POWER, ZATI 50 NI KIBOKO YA TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA UUME MDOGO
Madereva Wa Tanzania Walalamika Zoezi La Upimaji Corona Mpaka wa Namanga Kwenda Kenya
Mbarali District Council Various Jobs (Watendaji)
Monday, 11 May 2020
41 New Government Jobs at MNH, TPRI, NAOT, STAMICO and SUA
The Public Service Recruitment Secretariat (PSRS) is a government organ with a status of independent Department established specifically to facilitate the recruitment process of employees to the Public Service. Public Service Recruitment Secretariat was established by the Public Service Act No. 8 0f 2002 as amended by Act No. 18 of 2007, section 29(1)
Public Service Recruitment Secretariat (PSRS) On behalf of the Muhimbili National Hospital (MNH), Tanzania Insurance RegulatoryAuthority (TIRA), Tanzania Tropical Seeds Research Institute (TPRI),The National AuditOffice of Tanzania (NAOT), The State Mining Corporation (STAMICO) and SokoineUniversity of Agriculture (SUA), Public Service Recruitment Secretariat invites qualifiedTanzanians to fill 41 vacant posts as mentioned in the PDF file attached;
Click link below to download the file:
Deadline for application is 21st May, 2020;
DOWNLOAD PDF FILE HERE
LHRC WACHANGIA VIFAA KINGA, MAPAMBANO DHIDI YA CORONA
CHADEMA YAWAFUTA UANACHAMA WABUNGE WANNE
Picha : SHIRIKA LA AGAPE LATOA MSAADA WA VIFAA KUKABILIANA NA CORONA VIJIJI VYA KATA YA MWAMALA SHINYANGA
Waziri Mkuu wa Uingereza alegeza vikwazo kwa mara ya kwanza nchini humo Tangu Janga La Corona Liikumbe Nchi Hiyo
Johnson amesema kuanzia leo, watu ambao walikuwa hawawezi kufanya kazi wakiwa nyumbani, wanaweza kurudi kazini.
Waziri Mkuu huyo pia amesema kuanzia Jumatano watu walio na jamaa zao majumbani wanaweza kutoka nje tena bora tu wadumishe kanuni za umbali wa mtu mmoja na mwingine.
Amesema kuanzia Juni mosi, serikali yake itatoa tangazo la iwapo maduka yataanza kufunguliwa taratibu na iwapo wanafunzi wa shule za msingi wataweza kurudi shule.
Johnson vile vile ametoa ruhusa ya watu kufanya mazoezi.
Uingereza imeshuhudia vifo vya watu 32, 0000 vilivyotokana na mamabukizi ya Corona, huku maelfu wakiambukizwa, ikiwa nchi ya pili baada ya Marekani duniani kuwa na idadi kubwa ya maambukizi.
Naibu Waziri wa Afya Dkt Faustine Ndugulile Akanusha Taarifa Kwamba Ni Mgonjwa
MBUNGE WA KISHAPU SULEIMAN NCHAMBI KUENDELEA KUSOTA RUMANDE..KESI YAKE YA UHUJUMU UCHUMI YAPIGWA KALENDA HADI MEI 25
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mbunge wa Jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga Suleiman Masoud Nchambi (CCM), imetajwa tena leo Jumatatu Mei 11,2020 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Shinyanga na kuahirishwa hadi Mei 25, 2020 itakapotajwa tena kwa ajili ya maombi ya dhamana.
Katika mashtaka 12 ya uhujumu uchumi anayokabiliwa nayo Mbunge huyo ni pamoja na shtaka la kwanza, tatu ambayo ni kupatikana na silaha, shtaka la pili ni kupatikana na risasi, la nne ni kumiliki silaha aina ya Riffle kinyume na sheria kwa mujibu wa Sheria ya kumiliki silaha Na. 2 ya mwaka 2015, shtaka la tano, sita, saba, nane na tisa ni kumiliki risasi bila kibali, shtaka la 10 ni kumiliki silaha bila kibali na 11 ni kumiliki risasi isivyo halali.
Mbunge huyo alipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza Mei 8, 2020 mahakamani hapo katika shauri la uhujumu uchumi namba 10 la mwaka 2020 na kusomewa mashitaka 12 ya uhujumu uchumi mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Ushindi Swalo.
Upande wa mshtakiwa ukiongozwa na Wakili Frank Mwalongo uliomba mteja wao apate dhamana lakini maombi yao yalishindikana baada ya upande wa Mashitaka ukiongozwa na Mkuu wa Mashtaka mkoa wa Shinyanga, Margareth Ndaweka kupinga na kueleza kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kutoa dhamana hiyo ambapo Hakimu Swalo alikubaliana na hoja hiyo na kuahirisha shauri hilo hadi Mei 25, mwaka huu ambapo litaletwa kwa ajili ya kutajwa tena na kushughulikia dhamana, ambapo mshtakiwa amerudishwa tena rumande.
Wakili wa mshtakiwa, Frank Mwalongo amewaeleza waandishi wa habari kuwa mteja wake amekosa dhamana kwa kuwa hati ya mashtaka haijataja thamani (kiasi) anachodaiwa kuhujumu mshtakiwa, hivyo haina mamlaka ya kutoa dhamana na kuwataka waombe mahakama kuu ambayo ina mamlaka ya kutoa dhamana hiyo.