Monday, 11 May 2020
Naibu Waziri wa Afya Dkt Faustine Ndugulile Akanusha Taarifa Kwamba Ni Mgonjwa
MBUNGE WA KISHAPU SULEIMAN NCHAMBI KUENDELEA KUSOTA RUMANDE..KESI YAKE YA UHUJUMU UCHUMI YAPIGWA KALENDA HADI MEI 25
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mbunge wa Jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga Suleiman Masoud Nchambi (CCM), imetajwa tena leo Jumatatu Mei 11,2020 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Shinyanga na kuahirishwa hadi Mei 25, 2020 itakapotajwa tena kwa ajili ya maombi ya dhamana.
Katika mashtaka 12 ya uhujumu uchumi anayokabiliwa nayo Mbunge huyo ni pamoja na shtaka la kwanza, tatu ambayo ni kupatikana na silaha, shtaka la pili ni kupatikana na risasi, la nne ni kumiliki silaha aina ya Riffle kinyume na sheria kwa mujibu wa Sheria ya kumiliki silaha Na. 2 ya mwaka 2015, shtaka la tano, sita, saba, nane na tisa ni kumiliki risasi bila kibali, shtaka la 10 ni kumiliki silaha bila kibali na 11 ni kumiliki risasi isivyo halali.
Mbunge huyo alipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza Mei 8, 2020 mahakamani hapo katika shauri la uhujumu uchumi namba 10 la mwaka 2020 na kusomewa mashitaka 12 ya uhujumu uchumi mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Ushindi Swalo.
Upande wa mshtakiwa ukiongozwa na Wakili Frank Mwalongo uliomba mteja wao apate dhamana lakini maombi yao yalishindikana baada ya upande wa Mashitaka ukiongozwa na Mkuu wa Mashtaka mkoa wa Shinyanga, Margareth Ndaweka kupinga na kueleza kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kutoa dhamana hiyo ambapo Hakimu Swalo alikubaliana na hoja hiyo na kuahirisha shauri hilo hadi Mei 25, mwaka huu ambapo litaletwa kwa ajili ya kutajwa tena na kushughulikia dhamana, ambapo mshtakiwa amerudishwa tena rumande.
Wakili wa mshtakiwa, Frank Mwalongo amewaeleza waandishi wa habari kuwa mteja wake amekosa dhamana kwa kuwa hati ya mashtaka haijataja thamani (kiasi) anachodaiwa kuhujumu mshtakiwa, hivyo haina mamlaka ya kutoa dhamana na kuwataka waombe mahakama kuu ambayo ina mamlaka ya kutoa dhamana hiyo.
Katibu baraza la ardhi Kiteto kizimbani kwa rushwa
Dawa ya Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) yatoa mwanga wa matumaini kwa wagonjwa wa corona
Wakusanyaji Mapato Mkoani Tabora Ambao Hawajapeleka Fedha Benki Kuchukuliwa Hatua
RAS Tabora Anzeni Kulima Mazao Mengine Kukabiliana Na Matatizo Ya Kushuka Kwa Uzalishaji Wa Zao La Tumbaku
Tumefanya Maboresho Kwenye App Yetu ya Mpekuzi Ili Kukuwezesha Kupata Habari zetu Haraka hasa Wakati huu wa janga la Corona
Sunday, 10 May 2020
Wagonjwa Wa Corona Nchini Kenya Wafika 672
Iran Yasema Iko Tayari Kubadilishana Wafungwa na Marekani
Kwa mujibu wa Idhaa ya Kishwahili DW, Rabiei amesisitiza kuwa Tehran iko tayari kubadilishana wafungwa na Marekani bila masharti yoyote.
Iwapo hilo litatokea, basi itakuwa ni mojawapo ya matukio machache ya ushirikiano kati ya Marekani na Iran, mataifa mawili ambayo yamekuwa kama mfano wa pamba na moto.
Uhusiano wa Marekani na Iran umezidi kuwa mbaya hasa baada ya Rais Donald Trump kuingia madarakani
Kumetolewa wito na nchi zote mbili kubadilishana wafungwa kutokana na janga la virusi vya Corona.
Katika eneo la Mashariki ya kati, Iran imeathirika pakubwa na janga hilo nayo Marekani ikiongoza kwa idadi ya vifo vinavyotokana na ugonjwa wa Covid 19 kote duniani.
Korea Kusini Yaamuru kufungwa kwa maeneo yote ya kuuza vileo na kumbi za starehe baada ya kuzuka visa vipya vya Corona
Mashambulizi makali ya waasi yaharibu Uwanja wa Ndege wa Tripoli Libya
-Parstoday
HAPPY MOTHER'S DAY!!
International Istqaama Muslim Commuty Yatoamsaada Kwa Wafungwa Kahama
Barabaraya Uyogo – Ulowa Katika Halmashauri Ya Ushetu Yapandishwa Hadhi
FULL POWER , ZAT 50 NI SULUHISHO LA KUDUMU TATIZO LA NGUVU ZA KIUME NA UUME MDOGO





























