Sunday, 10 May 2020

ZOEZI LA ULIPAJI FIDIA MRADI WA LNG LINDI LASHIKA KASI



Eneo ambalo kiwanda cha LNG kinatarajiwa kujengwa katika kijiji cha Likong’o katika Manispaa ya Lindi 
**
Serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) imeanza kutekeleza zoezi la ulipaji fidia kwa wananchi ambao wanaguswa na mradi wa uchakataji na usindikaji wa gesi asilia (LNG) Mkoani Lindi. 


Mradi huo ambao unagusa Mitaa mitatu ya Likong’o, Masasi ya Leo na Mto Mkavu unachukua eneo lenye ukubwa wa hekta 2,071.7, ambapo Serikali imetoa kiasi cha Shilingi Bilioni 5.2 kwa ajili ya kufidia wanachi 693 ambao wanaguswa na mradi huo. 
Akizungumzia mradi huo, Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mh. Godfrey Zambi alisema, “mchakato wa kuwafidia waathirika wa mradi wa LNG umechukua muda mrefu sana na nimekuwa nikijibu maswali mengi sana kutoka kwa wananchi hao. 

Hatimaye Serikali imeidhinisha kiasi cha Shilingi Bilioni 5.2 kufidia wananchi wanaoguswa na mradi huu muhimu. Napenda kutumia fursa hii kuishukuru Serikali pamoja na Shirika letu la TPDC kufikia hatua hii muhimu.” 
Wananchi watakaopisha mradi wa LNG eneo la Likong’o, Manispaa ya Lindi wakifuatilia na kusmsikiliza kwa makini Afisa Maendeleo ya Jamii Ndugu Oscar Mwakasege kutoka TPDC, alipokuwa akiwasilisha mada ya utatuzi wa migogoro ya wananchi katika mradi huo


Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mh. Godfrey Zambi akitoa maelezo ya mradi wa LNG mbele ya Waandishi wa Habari Ofisini kwake.



 **
Katika hatua nyingine, Meneja mradi wa LNG kutoka TPDC, Mhandisi Fedister Agrey aliwahakikishia wananchi na vyombo vya habari kwamba, “mradi upo na ndiyo maana kikosi kazi kutoka TPDC, Benki ya NMB pamoja na Taasisi zingine za Serikali wapo hapa.” 

“Zoezi hili linatekelezwa katika hatua mbili, hatua ya kwanza inahusisha utoaji wa elimu ya fidia, matumizi sahihi ya fedha, sharia na utatuzi wa migogoro kwa waathirika wote wa mradi. 

Na hatua ya pili itahusisha zoezi la ulipaji fidia kwa wananchi husika” alisisitiza Mhandisi Fedister. Wananchi watakaopisha mradi wa LNG eneo la Likong’o, Manispaa ya Lindi wakifuatilia na kusmsikiliza kwa makini Afisa Maendeleo ya Jamii Ndugu Oscar Mwakasege kutoka TPDC, alipokuwa akiwasilisha mada ya utatuzi wa migogoro ya wananchi katika mradi huo.

Akiongea kwa niaba ya wananchi, Mwenyekiti wa Mtaa wa Masasi ya leo Bwana Saidi Ismail Lihoka alisema, “Tunaipongeza Serikali na Shirika la TPDC kwa kutimiza ahadi yao ya kulipa fidia wananchi watakaopisha mradi wa LNG. 



Pia, nitumie fursa hii kuwaasa wananchi wenzangu kwamba, wawe watulivu na wafuate utaratibu uliopangwa na TPDC katika kufanikisha zoezi hili.” Mhandisi wa Petroli Kutoka TPDC Ndugu Felix Nanguka akitoa mada ya masuala ya fidia kwa waathirika wa mradi wa LNG katika Mtaa wa Likong’o, Manispaa ya Lindi Mnamo Desemba, 2015 Serikali ilitwaa ardhi ya iliyokuwa shamba la mkonge na kuipatia TPDC hati ya umiliki wa eneo hilo kwa ajili ya kuendeleza mradi wa LNG.



Aidha, uthamini wa ardhi ya mradi ulifanyika mwaka 2015 na kufanyiwa marekebisho madogo mwezi Aprili 2017, ili kufidia eneo la ardhi ambalo lilikuwa linamilikiwa na wananchi pamoja na maendelezo yaliyofanywa na wananchi katika eneo ambalo limetwaaliwa na Serikali. 

Mradi huu ni mkubwa na wa aina yake kwa Tanzania, ambao Serikali inajipanga vyema ili kuhakikisha maslahi mapana yanapatikana kwa Watanzania. 

Lengo la mradi huu ni kuiwezesha Tanzania kuzalisha gesi nyingi iliyogundulika baharini na kuuza rasilimali hii katika soko la Dunia, pamoja na kuwezesha upatikanaji wa gesi ya kutosha katika soko la ndani kwa ajili ya kuzalisha nishati ya umeme na matumizi mbalimbali ya viwandani na majumbani.
Share:

KABUDI : DAWA YA CORONA TULIYOICHUKUA MADAGASCAR NI KWA AJILI YA UTAFITI KWANZA KABLA YA KUANZA KUTUMIWA


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi akizungumza na waandishi wa habari katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha JNICC jijini Dar leo, mara Baada ya kurejea kutoka nchini Madagascar kuchukua dawa ya virusi vya Corona, ii kupambana na maradhi hayo ya COVID – 19 ambapo itafanyiwa utafiti kabla ya kuanza kutumiwa.

 *****
Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, imesema kuwa dawa ambayo nchi ya Madagascar imeitoa kama msaada wa Serikali ya Tanzania ni kwa ajili ya utafiti kwanza kabla ya kuanza kutumiwa na walengwa. 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) amewaambia waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuwa dawa hiyo inayojulikana kaitaalamu kama "COVIDORGANICS" siyo kwa ajili ya kugawa kwa wananchi, bali ni kwa ajili ya utafiti na mara baada ya utafiti kukamilika wataalamu wa afya watatoa maelekezo ya jinsi ya utumiaji wa dawa hiyo.

Aidha, Profesa Kabudi anesema kwamba dawa hiyo imegawanyika katika makundi mawili ambapo kundi la kwanza la dawa ni kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya COVID 19 kwa wale ambao hawajaambukizwa ugonjwa wa Corona. Kundi la pili ni kwa ajili ya matibabu kwa wananchi ambao tayari wameathirika na COVID 19.

"Dawa hii tuliyokuja nayo jana kutoka Madagascar mara baada ya utafiti kukamilika na kupata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa wataalamu wetu wa afya itatumika kukinga wananchi ambao hawajaathirika na kutibu wale walioathirika," Prof. Kabudi

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa serikali Prof. Abel Makubi amesema kuwa mara baada ya kupokea dawa hiyo kazi ya kwanza ya ni kuanza utafiti ambao utaonesha kama dawa hiyo ni salama na haina madara kwa wananchi na pili utafiti wa kuangalia ubora wa kutibu au kupunguza makali ya COVID 19.

"Mara baada ya utafiti wa dawa hii kukamilika itatumika katika makundi matatu ambayo kundi la kwanza ni wagonjwa kutumia dawa ya kawaida, kundi la pili watapata dawa ya kawaida na hii iliyotoka Madagascar na kundi la tatu wagonjwa watatumia dawa ya kawaida na ile inayozalishwa na Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (Nimr)," Amesema Prof. Makubi

Prof. Makubi pamoja na mambo mengine ametoa wito kwa watanzania kuchukua tahadhari katika kujikinga na ugonjwa wa COVID 19 na wasibweteke na lolote.

Nae Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Prof. Yunus Mgaya amesema kuwa wamejipanga kushirikiana na taasisi nyingine za Serikali hasa Ofisi ya Mkemia Mkuu katika kuhakikisha inafanya utafiti wa kina juu ya matumizi ya dawa hiyo.

"NIMR inafanya tafiti mbalimbali za kupambana na ugonjwa huu wa COVID 19 na itaendelea kufanya tafiti hizo ili kuwasaidia watanzania," amesema Prof. Mgaya

Kwa upande wake Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko amesema kuwa Ofisi ya Mkemia Mkuu inalo jukumu la kuchunguza dawa au sumu zozote kwenye sampuli, kukadiria kwa usahihi kiasi cha dawa, umetaboli au sumu.

Dkt. Mafumiko ameongeza kuwa, kupitia utafiti wa dawa hiyo, ofissi yake kwa kushirikiana na wataalamu wa afya watatafsiri matokeo ya uchunguzi katika dawa hiyo kutoa maelekezo sahihi juu ya matumizi yake kwa mwananchi.

Mkutano huu ulihudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb), Mganga Mkuu wa serikali Prof. Abel Makubi, Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (Nimr) Prof. Yunus Mgaya, Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Tiba za Asili Dkt. Paul Mkama.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani) dawa ambayo imetolewa na Madagascar leo Jijini Dae es Salaam 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani) dawa ambayo imetolewa na Madagascar leo Jijini Dae es Salaam
Mganga Mkuu wa serikali Prof. Abel Makubi akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano uliofanyika leo Jijini Dae es Salaam
Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Prof. Yunus Mgaya akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano uliofanyika leo Jijini Dae es Salaam
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano .
Mkuu wa Kitengo cha Tiba za Asili Dkt. Paul Mkama akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati mkutano ukiendelea .
Share:

Ofisi Za Ardhi Kila Mkoa Zaanza Rasmi

Na Munir Shemweta, WANMM DODOMA
Ofisi za Ardhi za mikoa kuanza rasmi kufanya kazi katika mikoa 26 ya Tanzania Bara mwezi huu wa Mei 2020 ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli kuitaka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuondoa kero na mzigo wa gharama kwa wananchi katika masuala ya ardhi.

Uanzishaji ofisi hizo ni usogezaji huduma za sekta ya ardhi karibu na wananchi sambamba na kuwapunguzia gharama za kufuata huduma hiyo umbali mrefu ambapo huduma za ardhi awali zilikuwa zikitolewa kwenye ofisi za Ardhi za Kanda na Makao Makuu.

Akizungumza leo tarehe 10 Mei 2020 jijini Dodoma kabla ya kuwasilisha Makadirio ya Hotuba yake hapo kesho tarehe 11 Mei 2020, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi alisema Wizara ya Ardhi imeanzisha ofisi za ardhi katika kila Mkoa ili kutoa huduma zote zilizokuwa zinatolewa kwenye ofisi za Kanda au Makao Makuu.

Alisema, kuanzia sasa wananchi watapata huduma zote ndani ya mikoa yao na kubainisha kuwa wananchi wa mikoa ya Kigoma na Katavi hawataenda tena Tabora kuchukua hati kama walivyokuwa wakifanya awali huku wale wa Tanga, Manyara na Arusha wakipata huduma katika mikoa yao badala ya kwenda Moshi na wale wa mikoa ya Iringa, Njombe, na Rukwa wakisalia mikoa husika badala ya kwenda Mbeya.

Aidha, wananchi wa mikoa ya Ruvuma na Lindi sasa hawataenda mkoa wa Mtwara kupata huduma za ardhi na wananchi wa Kagera na Geita nao hawatalazimika kwenda Mwanza  huku wananchi wa mikoa ya Mara na Shinyanga wakisalia mikoa yao kupata huduma za ardhi ambapo sasa hawataenda Simiyu na wale wa Singida na Morogoro wakiepuka kwenda mkoa wa Dodoma kuchukua hati.

Kwa mujibu wa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi,  Nyaraka zote,  watumishi pamoja na vitendea kazi tayari vipo mikoani na kubainisha kuwa, sasa Taasisi kama mabenki zitaweza kukopesha kwa kasi kwa kuwa dhamana za wakopeshwaji yaani Hati zipo mikoani na Masjala za Hati zimerudishwa kila mkoa.

Waziri huyo mwenye dhamana ya Ardhi alisema, Wasajili wa hati wa mikoa watatoa hati kwa wananchi kupitia ofisi za Ardhi za Wilaya na siyo wananchi kufuata hati kwenye kanda au mkoani na kuongeza kuwa, vifaa mbalimbali vya upimaji vimenunuliwa na kusambazwa ofisi hizo za mikoa ili Halmashauri za Wilaya ziweze kuazima na kupima maeneo yao bila gharama za kuvikodisha.

‘’Tumeanza mkakati wa kununua vifaa kwa kila Wilaya.  Uanzishwaji wa ofisi hizi ni utekelezaji wa maagizo ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli aliyetutaka Wizara tuondoe kero na mzigo wa gharama kwa wananchi na wadau mbalimbali wa ardhi’’ alisema Lukuvi.


Share:

Rais wa Marekani Donald Trump na Makamu Wake Huenda Wakapimwa Tena Corona Baada ya Mtumishi Mwingine Wa IKULU Kukutwa na Virusi Vya Corona

Marekani imesema huenda Rais Trump na Makamu wake Mike Pence wakalazimika kupima tena corona kwa mara ya tatu mfululizo kufuatia Mfanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Katibu wa Habari) kuugua corona, juzi Viongozi hao walipimwa corona baada ya Mfanyakazi wa Ikulu kuugua corona.

Trump mwenyewe ndiye  aliyetangaza siku ya Ijumaa wakati wa mkutano na wabunge na maseneta kutoka chama cha Republican kwamba Katie Miller, mke wa mshauri wake wa katika masuala ya uhamiaji, Stephen Miller, ambaye pia ni Msemaji wa Makamu wa rais wa Marekani Mike Pence ameathirika. 

Kutangazwa kwa kesi hii ya pili kwa siku mbili katika Ikulu ya White House kumezua hofu kwa afya ya rais na makamu wa rais, ambao wote wawili walianza tena shughuli zao na safari zao, wakati vifo vya watu waliofariki kwa Covid-19 vimezidi 80,000.


Share:

195 Jobs - Tume ya Utumishi wa Mahakama (Judiciary of Tanzania )

195 Jobs Judiciary of Tanzania (Tume ya Utumishi wa Mahakama)

The Constitution of the United Republic of Tanzania, 1977 vests the authority and responsibility to administer justice in the Judiciary of Tanzania. The Judiciary has its foundation on Article 107A (1) and 107B of the Constitution and states clearly about the Independence of the Judiciary in the United Republic of Tanzania. Now the strategic plan for Judicial Independence is focused in both form and content.

Applications should be submitted latest by May 21, 2020

CLICK HERE TO APPLY


Share:

9 Job Opportunities at National Audit Office, ICT Officer (Information System Auditors)

ICT OFFICER II (INFORMATION SYSTEM AUDITOR) GRADE II – 9 POST

POST CATEGORY(S) IT AND TELECOMS
EMPLOYER NATIONAL AUDIT OFFICE (NAOT)
APPLICATION TIMELINE: 2020-05-07 2020-05-21

DUTIES AND RESPONSIBILITIES

i.To Prepare annual risk based IS audit plans and coordinate their implementations;

ii.To Develop an IS audit strategy to cover all areas under audit, define scope, plan resources, nature, timing, and extent of the audit in accordance to ISACA, ISSAI and INTOSAI standards;

iii.To Perform general and application control reviews for simple to complex computer information systems to ensure valid, reliable, timely, and secure input, processing, and output;

iv.To Perform reviews of clients’ information controls to include system development standards, operating procedures, system security, programming controls, communication controls, backup and disaster recovery, and system maintenance;

v.To Perform reviews of internal control procedures and security for systems under development and/or enhancements to the existing systems;

vi.To Assist financial auditors in extraction of data from various computer systems and perform data analysis based on the audit objectives;

vii.To Provide assurance services to financial auditors on the effectiveness of automated controls in application systems that have impact on financial statements;

viii.To Communicate audit results to audit clients and ensure positive management commitment to implement the given recommendations;

ix.Adequate and timely maintenance of IS audit supporting evidence in Teammate Audit Management System;

x.To Prepare and present IS audit reports and other technical information to relevant parties;

xi.To Follow up on audit findings and assess implementation of audit recommendations to audited entities;

xii.To Prepare a database of all IT systems in the government sector which will be updated on continuous basis and will form the information system (IS) Audit universe and basis for IS audit; and

xiii.To perform any other related duties assigned by the Supervisor.

QUALIFICATION AND EXPERIENCE
Bachelor Degree either in Computer Science, Information Technology, Computer Engineering or equivalent qualifications. Having CISA certification will be an added advantage.

REMUNERATION TGS E

Deadline for receiving applications is  21 May 2020

CLICK HERE TO APPLY


Share:

WAZIRI DKT KALEMANI ATAKA WANAOIBA UMEME WAKAMATWE NA KUWEKWA KOROKORONI

 WAZIRI wa Nishati Dkt Medard Kalemani katika akikata upete kuashiriki kuwasha umeme kwenye Kijiji cha Kwasunga wilayani Korogwe wakati wa ziara yake katika wilaya za Lushoto,Handeni na Korogwe mkoani Tanga iliyokuwa inalenga kutembelea kwenye maeneo yanayofanyiwa kazi na wakandarasi kupitia mradi wa Rea awamu ya tatu unaoendelea ambao unatarajiwa kukamilika mwezi June mwaka huu kulia ni Meneja wa Tanesco wilaya ya Korogwe Mhandisi Peter Kanuti Magari
 WAZIRI wa Nishati Dkt Medard Kalemani kushoto akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kweisasu Kata ya Sindeni wilayani Handeni mara baada ya kuwasha umeme katika eneo la Shule ya Msingi Kweisasu wakati wa ziara yake kulia ni Mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe
 WAZIRI wa Nishati Dkt Medard Kalemani akiwasha umeme kwenye moja ya nyumba zilizopo kwenye Kijiji cha Kwasunga wilayani Korogwe wakati wa ziara yake kushoto anayeshuhudia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Korogwe Rahel Mhando kulia ni mzee mwenye nyumba hiyo
 WAZIRI wa Nishati Dkt Medard Kalemani kushoto akizungumza na mzee wa nyumba aliyowasha umeme kwenye Kijiji cha Kwasunga wilayani Korogwe wakati wa ziara yake
 WAZIRI wa Nishati Dkt Medard Kalemani akisisitiza jambo kwa Meneja wa Tanesco wa Kanda ya Kaskazini Mhandisi Gaspar Msigwa kushoto na kulia anayefuatilia kwa umakini ni Meneja wa Tanesco Mkoa wa Tanga Mhandisi Julius Sabu wakati alipowasilia eneo la Mkata wilayani Handeni kwa ajili ya kuanza ziara yake mkoani hapa
 WAZIRI wa Nishati Dkt Medard Kalemani katikati akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Tanesco wilaya ya Korogwe Mhandisi Peter Kanuti Magari kuhusu namna kituo cha Umeme Kilole kinavyofanya kazi wakati wa ziara yake ya kushtukiza kwenye kituo hicho kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Korogwe Rahel Mhando

WAZIRI wa Nishati Dkt Medard Kalemani kushoto akisisitiza jambo kwa Meneja wa Tanesco wilaya ya Korogwe Mhandisi Peter Kanuti Magari wakati alipotembelea kituo cha Umeme cha Kilole wilayani Korogwe wakati wa ziara yake
 
WAZIRI wa Nishati Dkt Medard Kalemani ameagiza watu ambao watakaobainika kuhujumu miundombinu ya umeme kwenye maeneo mbalimbali nchini kwa kuiba umeme au vifaa vyake wakamatwe na kuwekwa korokoroni ili waendelee na utaratibu wa kisheria kusudi watu wengine wenye nia mbaya wajifunze na kuachana na vitendo hivyo.

Dkt Kalemani aliyasema hayo wakati wa ziara yake katika wilaya za Lushoto,Handeni na Korogwe mkoani Tanga iliyokuwa inalenga kutembelea kwenye maeneo yanayofanyiwa kazi na wakandarasi kupitia mradi wa Rea awamu ya tatu unaoendelea ambao unatarajiwa kukamilika mwezi June mwaka huu.

Kauli ya Waziri huyo inatokana na Taarifa aliyopatiwa na Katibu Tawala wa wilaya ya Korogwe Rahel Mhando wakati alipofika kuwasha umeme kwenye Kijiji cha Kwasunga wilayani humo ambapo alielezwa namna wizi wa umeme ulivyokithiri kwenye wilaya hiyo.

Licha ya kuwasha umeme kwenye baadhi ya vijiji kwenye wilaya ya Handeni,Korogwe na Lushoto pia alifanya ufuatiliaji huo ili waweze kukamilisha kazi yao ndani ya muda huo na amekwisha kutoa maelekezo kwa nchi nzima kwa wakandarasi wote wanaoendelea kwa wale ambao watashindwa kumaliza kazi zao kwa mujibu wa mkataba wake ambao unaishia mwezi June mwaka huu.

Maelekezo hayo ni kwa wanaowasimamia wahandisi wote waanze kuwakata malipo yao ya mishahara kwenye mikataba hiyo ambayo ni kwa mujibu wa mikataba ya malipo hayo huku akiagiza ikikatwa wasikae nayo wairejeshwe kwa katibu mkuu hazina ambaye ni mlipaji mkuu wa serikali ili fedha hizo zitumike kwa ajili ya kuwaweka wakandarasi wengine ambao wataweza kumaliza kazi hizo.

“Ndugu zangu ikibainika mtanzania amefanya hujuma ya kuiba umeme au vifaa vyake mtu wa namna hiyo ni mhujumu achukuliwe hatua na viongozi wa maeneo husika wala suala hilo sio la kumsubiri mweneja wa mkoa aje ajiridhishe tunaomba ma DC msisite kutoa taarifa…

“Lakini kwa wasiokuwa na nia njema ya miumbonu ya umeme wakamateni na wawekeni Korokoroni na muendelee na utararibu wea kishereia kusudu watu wengine wenye nia mbaya wajifunze kutoka kwenye tabia hizo ambazo sio nzuri kwa ustawi wa shirika letu kwani wanakuwa wakirudisha nyuma juhudi kubwa tunazozifanya “Alisema

Aidha Waziri Dkt Kalemani alisema wakati mwengine kunapotokea wizi mameneja nao wanakuwa sehemu ya wizi huo kama sio wao ni vibarua wao kwa sababu haiwezekani mtu ambaye haujui umeme anafungua transfoma na kuiba umeme bila kujua taalumu ya umeme halafu anaiba vifaa bila kuuungua lakini hatama kama sio mtaalamu wa tanesco ni mtu aliyewahi kufanya kazi nanyi

“Nikisiria transfoma imeibiwa mahali mtu wa kwanza kumchukulia hatua ni meneje wa eneo husika kwa sababu yeye ndio mwenye jukumu la kusimamia wataalamu wake anaowapa kazi lakini pia acheni kuwapa kazi vishoka kwani mnapowapa kazi matokeao yake ndio hayo”Alisema Waziri Dkt Kalemani.

Akizungumzia suala tatizo hilo mbele ya Waziri wa Nishati, Katibu Tawala wa wilaya hiyo Rahel Mhando alimueleza kwamba kumekuwa na tatizo la wizi wa umeme hilo tatizo bado lipo Korogwe ni kubwa huku akieleza kwamba wameweka mikakati mbalimbali kama wilaya ya kuweza kukabiliana nalo

“Mh Waziri amekwisha kutoa maelekezo na sisi kama wilaya tumepokea maelekezo hayo na labda nisema kwamba kwa yoyote tutakayembaini anaiba umeme huo ni hujumu uchumi atachukuliwa hatua kali na hatutawatamfumbia macho hilo hazungumzia waziri tu bali hata Rais Dkt John Magufuli kila siku amekuwa aksisitiza wizi wa miundombi ya umeme na kubuka umeme hilo wataendelea kulifanyia kazi”Alisema

Hata hivyo Katibu Tawala huyo alimshukuru Waziri kwa kufika kwenye kijiji cha Kwasunga kuwawashia umeme ambacho kina kaya 204 ambazo zimekwisha kupata umeme lakini kwa furaha wanamshukuru kwani mbali na vijiji vya awali zimeongezwa vijiji tisa kwenye Jimbo la Korogwe Vijiji.

“Sisi kama wilaya tunashukuru kwa sababu mmeendelea kutuongezea ukubwa upatikana umeme Korogwe kwani tuna kituo cha kilole ambacho waziri ametembelea kuna megawatts 5 zitaenda kuongezeka hivyo kitaongeza wigo mkubwa kwenye matumizi ya umeme”Alisema Das Rahel.
Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumapili May 10
















Share:

WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA YAENDELEA KUHAMASISHA WAZALISHAJI KUTENGENEZA VIFAA KINGA DHIDI YA COVID - 19


Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stella Manyanya akizungumza katika hafla ya kukabidhi malighafi (Ethanol) kwa ajili ya kutengenezea vitakasa mikono katika kiwanda cha Consumer's Choice Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stella Manyanya akimsikiliza Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Consumer's Choice limited Bi.Frida Mlingi (katikati) katika hafla ya kukabidhi malighafi (Ethanol) kwa ajili ya kutengenezea vitakasa mikono katika kiwanda cha Consumer's Choice Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Consumer's Choice limited Bi.Frida Mlingi akieleza namna walivyotumia ethanol kutengeneza product mbalimbali ikiwemo mafuta kwaajili ya jiko la kisasa la kupikia.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stella Manyanya (Kushoto)akikabidhi ethanol kwa wizara ya afya katika hafla ya kukabidhi malighafi (Ethanol) kwa ajili ya kutengenezea vitakasa mikono katika kiwanda cha Consumer's Choice Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stella Manyanya (Kulia)akikabidhi ethanol Shirika la Viwanda Vidogo SIDO katika hafla ya kukabidhi malighafi (Ethanol) kwa ajili ya kutengenezea vitakasa mikono katika kiwanda cha Consumer's Choice Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stella Manyanya (Kushoto)akikabidhi ethanol kwa Shirika la Utafiti wa Maendeleo ya Viwanda nchini (TIRDO) katika hafla ya kukabidhi malighafi (Ethanol) kwa ajili ya kutengenezea vitakasa mikono katika kiwanda cha Consumer's Choice Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stella Manyanya akishuhudia shughuli ya utengenezaji vitaka mikono ukiendelea katika hafla ya kukabidhi malighafi (Ethanol) kwa ajili ya kutengenezea vitakasa mikono katika kiwanda cha Consumer's Choice Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stella Manyanya akinawa mikono kwenye maji tiririka na sabuni katika hafla ya kukabidhi malighafi (Ethanol) kwa ajili ya kutengenezea vitakasa mikono katika kiwanda cha Consumer's Choice Jijini Dar es Salaam.

********************************
NA EMMANUEL MBATILO
Shirika la Viwanda Vidogo SIDO pamoja na Shirika la Utafiti wa Maendeleo ya Viwanda nchini (TIRDO) wametakiwa kutumia malighafi (ethanol) vizuri kuokoa maisha ya watanzania kwa kuzalisha vitakasa mikono vyenye bei nafuu.

Ameyasema hayo leo Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stella Manyanya katika hafla ya kukabidhi malighafi (Ethanol) kwa ajili ya kutengenezea vitakasa mikono katika kiwanda cha Consumer's Choice Jijini Dar es Salaam.

Aidha Mhe.Stella ametoa wito kwa wenye viwanda vya kutengeneza vifaa kinga nchini kuongeza bidii katika uzalishaji ili kuwezesha maeneo yote ya nchi kupata vifaa hivyo kwa urahisi na kwa bei nafuu.

"Nimefarijika kuona kuwa kiwanda cha Consumer’s Choice pamoja na kuchangia usafirishaji wa mali ghafi hii pia mmejikita katika kutengeneza vitakasa mikono, nawasihi wadau wengine wenye viwanda vyenye mifumo inayoweza kutengeneza vitakasa mikono tuweke nguvu kwenye uzalishaji wa vifaa hivi kwa wingi ili kusaidia mapambano haya". Amesema Mhe.Stella.

Nae Mkurugenzi wa biashara Kilombero Sugar Company Limited Bw.Fimbo Butallah amesema kuwa wao kama kampuni wamekuwa na kiwanda pia cha kutengeneza ethanol hivyo wameona nao washirikiane na serikali katika mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona wametoa lita 30,000 za ethanol bure kwa serikali ili iweze kuzalisha vitakasa mikono na kuvigawa kwa watanzania kwa urahisi na kwa bei iliyo na nafuu.

"Wenzetu wa Consumer's Choice kwasababu wapo kwenye viwanda wao waliomba kuisaidia serikali wakaisomba ethanol yote kutoka kiwandani mpaka hapa Dar es Salaam lakini pia wakaenda hatua moja zaidi wakaanza kuengeneza vitaksa mikono kwaajili ya serikali". Amesema Bw.Fimbo.

Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Consumer's Choice limited Bi.Frida Mlingi amesema kuwa kutokana na kikao kilichoitishwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Innocent Bashungwa na kuhudhuriwa na wazalishaji wa malighafi zinazotumika kutengenezea vitakasa mikono (hand Sanitizer), kampuni hiyo kwa kuona umuhimu kwenye mapambano ya vita dhidi ya Corona, waliahidi kusafirisha lita 30,000 za ethanol zilizotolewa na kiwanda cha Kilombero Sugar Company Limited.

Hata hivyo Bi.frida amesema kuwa pamoja na ahadi hiyo kampuni hiyo iliamua kubadili 75% ya Ethanol iliyokuwa itumike kwa kutengenezea vilevi itumike kutengenezea vitakasa mikono (hand Sanitizer) na 25% pekee ndo itumike kutengenezea vilevi, dhumuni kubwa likiwa ni kushirikiana na serikali katika mapambana dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona.

"Kwa kushirikiana na kampuni ya kuzalisha products za usafi (G&Co. Cleaning & Sanitation Limited) tumefanikiwa pia kutengeneza vitakasa mikono lita 11,000 zilizotokana na lita 8,000 za ethanol kati ya lita 20,000 walizopewa wizara ya afya". Amesema Bi.Frida.

Pamoja na hayo Bi.Frida amesema kuwa wapo tayari kushirikiana na serikali katika mapambano haya kwa kutoa kipaumbele kwenye vifaa kinga ili kufanikisha mapambano haya.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kiwanda cha kuzalisha product za usafi (G&Co. Cleaning & Sanitation Limited Mhandisi Aswile Simon amesema kuwa wametengeneza vitakasa mikono 11,000 na kuzigawa kwa wizara ya Afya kwa kushirikiana na kampuni ya Consumer Choice na lengo lao ni kushirikiana na serikali kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona.

Mwakilishi wa Wizara ya Afya ofisi ya mganga Mkuu wa Serikali Bi.Neema Nagu amesema kuwa tokea maambukizi ya Corona kuwepo hapa nchini wizara imekuwa ikifanya kazi kila kukicha ili kuahikikisha inalinda afya za watanzania.

Vilevile Bi.Neema ameyashukuru makampuni yanayojitahidi kushirikiana na serikali kupambana dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona.


Share:

Saturday, 9 May 2020

Video Mpya : NTEMI 'NG'WANA KANG'WA' - HAPPY BIRTHDAY

Msanii wa Nyimbo za asili Ntemi 'Ng'wana Kang'wa anakualika kutazama video ya wimbo wake mpya unaitwa Happy Birthday..itazame hapa mtu wangu

Share:

Video Mpya : SUPER NYANKOLE - CORONA


Nakualika kutazama video mpya ya Msanii wa Nyimbo za Asili Super Nyankole inaitwa Corona... Wimbo wa Corona ameuimba kwa Lugha ya Kiswahili na Kisukuma..
Tazama video hii hapa chini

Share:

Waziri wa Ujenzi Isack Kamwelwe azindua huduma ya Tiketi Mtandao kwa ajili ya Wananchi kununua tiketi za mabasi kupitia simu zao za mkononi

Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Isack Kamwelwe amezindua majaribio ya awali ya mfumo wa ukataji tiketi za mabasi kwa njia ya mtandao nchini utakao simamiwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Aridhini (LATRA) .

Waziri Kamwelwe amezindua mfumo huo jijini Dar Es salaam ambapo amesema kuwa mfumo huo uliotengenezwa na Kituo cha Taifa cha Kutunza Taarifa (NIDC) utasaidia kupunguza msongamano katika vituo na kurahisisha huduma ya ukataji tiketi kwa wasafiri.

“Mfumo huu wa tiketi mtandao utatatua changamaoto za muda mrefu katika sekta ya usafiri, kwani utakuwa na taarifa zote muhimu ambazo zinaweza kutumiwa na taasisi kama Jeshi la Polisi, Uhamiaji na Mamlaka ya mapato Tanzania(TRA) ambazo zinahusika na takwimu, sera na utafiti” Amesema Waziri Kamwelwe

Waziri Kamwelwe amesema kuwa mfumo huo unafaida kwa wamiliki wa mabasi na watumiaji wa usafiri, ambapo utaondoa upotevu wa mapato kwa wamiliki yaliyokuwa yanapotea kwenye mikono ya wapiga debe.

Waziri amesema mfumo huo upo tayari kutumika kwa majaribio hadi mwisho wa mwezi juni 2020 kwa usafiri wa mabasi ya masafa marefu na ifikapo septemba 2020 utekelezaji wa mfumo huo utaanza kwenye mabasi ya mjini.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa LATRA Gilliard Ngewe, amesema kuwa matumizi ya tiketi mtandao yataleta mabadiliko makubwa katika sekta ya usafirishaji nchini kwani watoa huduma na mawakala hawataweza kuwadanganya wamiliki wa mabasi kwani taarifa zitakuwepo kwenye mfumo.

“Suala la kumfungia tajiri hesabu halitakuwepo kwani tajiri atajifungia hesabu yeye mwenyewe”Amesema Ngewe

Amesma kuwa matumizi ya tiketi mtandao yataondoa orodha ya abiria iliyokuwa inapigwa muhuri na Jeshi la Polisi kwani orodha hiyo itapatikana kwa njia ya mtandao.

Ameongeza kuwa suala la abiria kulanguliwa nauli kila ifikapo kipindi cha mwisho wa mwaka limekwihsa kwani abiria anaweza kukata tiketi kwa kutumia simu yake ya mkoni bila kufika kituo cha mabasi.

Ngewe amesema kuwa LATRA imejipanga kusimamia mfumo huo kikamilifu kwani kutakuwa na kituo maalum cha kutoa huduma kwa wateja ambapo wataweza kupiga simu na kupatiwa huduma kwa saa 24 kwa kupiga namba 0800110150.


Share:

Kamati Kuu CHADEMA Yafanya Vikao vyake kwa Njia ya Mtandao

Kamati Kuu ya CHADEMA leo May 09,2020 ikiongozwa na Mwenyekiti wa Chama Taifa,Freeman Mbowe, imeanza vikao vyake vya ki-digitali (CHADEMA Digital), vikao vitajadili agenda mbalimbali ikiwemo hali ya corona na Siasa nchini na kufikia maazimio ambayo yatatolewa kwa umma baada ya vikao kukamilika.




Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger