Saturday, 9 May 2020

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi May 09



















Share:

Friday, 8 May 2020

RAIS MAGUFULI AMEFANYA UTEUZI MWINGINE LEO MEI 8




Share:

Picha : MBUNGE AZZA HILAL AKABIDHI GARI LA WAGONJWA KITUO CHA AFYA TINDE...FEDHA UJENZI WODI YA WAZAZI ZAHANATI YA MWANANYUDA NA LYABUKANDE


Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad ( CCM) amekabidhi gari la kubebea Wagonjwa ‘ Ambulance’ lililotolewa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto katika Kituo cha Afya Tinde kilichopo katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Mhe. Azza Hilal Hamad amekabidhi gari hilo leo Ijumaa Mei 8,2020 kwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko katika Kituo cha Afya Tinde kilichokuwa kinakabiliwa na ubovu wa gari ambalo lilikuwa linagharimu shilingi milioni 5 kila mwezi kwa ajili ya matengenezo.

Akizungumza wakati kukabidhi gari hilo,Mhe. Azza aliishukuru Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuendelea kuboresha huduma za afya ili wananchi wapate huduma bora za afya.

“Mwezi Julai mwaka 2018 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika ziara yake mkoani Shinyanga alitembelea kituo cha afya Tinde akajionea hali yake. Tukiwa tunaendelea na Ziara katika Halmashauri nilimuomba atusaidie gari la wagonjwa kwa ajili ya Ushetu lakini katika kujibu Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliahidi serikali italeta magari kwa ajili ya Ushetu na Tinde na leo ninakabidhi gari hili katika kituo hiki cha Tinde”,alieleza Mhe. Azza.

Mbunge huyo pia ametoa shilingi Milioni 1 kwa ajili kuchangia ujenzi wa Uzio wa Kituo cha Afya Tinde pamoja shilingi 2,500,000/= kusaidia ujenzi wa wodi ya wazazi katika Zahanati Lyabukande pamoja shilingi 2500,000/= kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya wazazi zahanati ya Mwamanyuda.

Mganga Mfawidhi Kituo cha Afya Tinde, Dkt. Greyson Matogo alisema kituo hicho kinakabiliwa na upungufu wa watumishi wa afya na kwamba gari la wagonjwa lililopo ni bovu na mara kwa mara limekuwa likiharibika na kujikuta wakitumia shilingi milioni 5 kwa ajili ya matengenezo kila mwezi.

Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko alimshukuru Mbunge Azza Hilal kwa namna anavyotolea kusaidia wananchi ndani na nje ya Chama Cha Mapinduzi.

Kuhusu changamoto ya upungufu wa watumishi wa afya, Mkuu huyo wa wilaya alisema serikali italeta watumishi wawili katika kituo cha afya Tinde, Samuye wawili na Kambarage mmoja.

Mboneko aliwataka wananchi kuendelea kuchangia miradi ya maendeleo ikiwemo kuchangia uzio wa kituo cha afya Tinde huku akiwahakikishia kuwa serikali itaendelea kuboresha huduma za afya kwani Rais Magufuli anapenda kuona wananchi wanapata huduma bora za afya.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
 Gari la kubebea Wagonjwa ‘Ambulance’ lililokabidhiwa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad ( CCM) kwa ajili ya Kituo cha Afya Tinde kilichopo katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kufanya ziara katika kituo cha Tinde Mwaka 2018. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad ( CCM) akizungumza wakati wa kukabidhi gari la kubebea Wagonjwa ‘ Ambulance’ lililotolewa na Serikali katika Kituo cha Afya Tinde kilichopo katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko kadi ya gari la kubebea Wagonjwa ‘ Ambulance’ lililotolewa na serikali kwa ajili ya Kituo cha Afya Tinde kilichopo katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko funguo ya gari la kubebea Wagonjwa ‘ Ambulance’ lililotolewa na serikali kwa ajili ya Kituo cha Afya Tinde kilichopo katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akionesha funguo ya gari la kubebea Wagonjwa ‘ Ambulance’ lililotolewa na serikali kwa ajili ya Kituo cha Afya Tinde kilichopo katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. Kulia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM).
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akiwa ndani ya gari la kubebea Wagonjwa ‘ Ambulance’ lililotolewa na serikali kwa ajili ya Kituo cha Afya Tinde kilichopo katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akiendesha gari la kubebea Wagonjwa ‘ Ambulance’ lililotolewa na serikali kwa ajili ya Kituo cha Afya Tinde kilichopo katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akishuka ndani ya gari la kubebea Wagonjwa ‘ Ambulance’ lililotolewa na serikali kwa ajili ya Kituo cha Afya Tinde kilichopo katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza baada ya kukabidhiwa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad gari la wagonjwa kwa ajili ya kituo cha afya Tinde.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akimkabidhi Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Mhe. Hoja Mahiba funguo za gari la wagonjwa katika kituo cha afya Tinde.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akikabidhi kadi ya gari la wagonjwa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Mhe. Hoja Mahiba na Kaimu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Nicodemus Simon.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Mhe. Hoja Mahiba akikabidhi kadi kwa Mganga Mfawidhi kituo cha afya Tinde Dkt. Dkt. Greyson Matogo  na Kaimu Mganga Mkuu wilaya ya Shinyanga Dkt. Fidelis Mushi.
Viongozi mbalimbali wa serikali na CCM wakipiga picha ya pamoja.
Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad ( CCM) akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko shilingi 1,000,000/= alizotoa kuchangia ujenzi wa uzio katika kituo cha Afya Tinde pamoja na shilingi 100,000/= iliyotolewa na Paroko wa Parokia ya Usanda, Padri Josephat Mahalu kusaidia ujenzi wa uzio huo. Mhe. Azza pia amechangia shilingi 2,500,000/= kusaidia ujenzi wa wodi ya wazazi katika Zahanati Lyabukande shilingi 2500,000/= kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya wazazi zahanati ya Mwamanyuda.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Hoja Mahiba shilingi Milioni 1.1 zilizotolewa na Mbunge Azza Hilal na  Paroko wa Parokia ya Usanda, Padri Josephat Mahalu kusaidia ujenzi wa uzio wa kituo cha afya Tinde.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Share:

DOWNLOAD - PAKUA APP YA MALUNDE 1 BLOG ...TUKUTUMIE HABARI ZOTE BURE KWENYE SIMU YAKO

Kuwa wa Kwanza kupata habari na matukio yanayojiri Tanzania na dunia kwa ujumla kwa kupakua/ kudownload App ya Malunde 1 blog tukuhabarishe masaa 24.


Tembea na dunia kiganjani mwako sasa.

Pakua App mpya ya Malunde 1 blog imeboreshwa zaidi ili kukidhi mahitaji ya wasomaji wetu. Hii ndiyo mpya kabisa,ina alama hii ↡↡
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Ni rahisi sana : Ingia Play store kisha Andika Malunde 1 blog halafu bonyeza Install

https://bit.ly/2Qb7qyF

Tafadhali fuata maelekezo hapo juu... Usikubali kukosa habari kizembe..Pakua app yetu Mpya ya Malunde1 blog Sasa
Share:

Tumefanya Maboresho Kwenye App Yetu ya Mpekuzi Ili Kukuwezesha Kupata Habari zetu Haraka hasa Wakati huu wa janga la Corona

Tumefanya maboresho katika App yetu ya MPEKUZI ili kuendana na changamoto ya sasa ya janga la Corona inayoikumba dunia Nzima

Usikubali kupitwa na taarifa muhimu zinazoendelea hapa nchini na Duniani  kwa Ujumla . Tumejipanga vizuri sana kukupatia taarifa sahihi na kwa wakati.

👉1. Tumebadili muonekano na kuufanya kuwa mzuri zaidi
👉2. Kila habari tunayoweka kuanzia sasa utapata notification kwenye simu yako 
👉3. Habari zote kwa sasa zinafika kwa haraka kwenye simu yako kuliko ilivyokuwa hapo awali

KUMBUKA: App yetu ni BURE. Unachotakiwa kukifanya ni kuingia Playstore na kupakua MPEKUZI APP

Kama tayari unayo, basi Ingia Playstore kwa ajili ya kupata UPDATE hii ya Toleo Jipya

Tumekurahisishia, Unaweza pia ...<<KU BOFYA HAPA>> Kupata toleo hili Bure Kabisa


Share:

Picha : WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA TANZANIA ATUA MADAGASCAR KUCHUKUA DAWA YA CORONA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi wa kulia akiwa amebeba dawa ya kutibu ugonjwa wa virusi vya corona
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi wa kulia akinywa dawa ya kutibu ugonjwa wa virusi vya corona
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Madagascar Mhe. Tehindrazanarivelo Djacoba As Oliva mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Antananarivo kwa ajili ya kupokea msaada wa dawa ya kutibu na kukinga ugonjwa wa COVID-19 unaosababishwa na Virusi vya Corona uliotolewa kwa Tanzania na Nchi ya Madagascar.
Share:

Picha : WORLD VISION TANZANIA YATOA MSAADA WA VIFAA TIBA NA KINGA CORONA KWA WATOA HUDUMA ZA AFYA SHINYANGA

Shirika la World Vision Tanzania limetoa msaada wa vifaa tiba na kinga vyenye thamani ya shilingi milioni 29 kwa ajili ya kusaidia watumishi wa sekta ya afya katika mkoa wa Shinyanga kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona ‘Covid 19’ wanapohudumia wagonjwa.

Vifaa hivyo vimekabidhiwa leo Ijumaa Mei 8, 2020 na Meneja wa World Vision Tanzania Kanda ya Ziwa John Massenza kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga.

Massenza alisema wao kama wadau wa sekta ya afya wanaofanya kazi zao katika wilaya ya Shinyanga,Kahama na Kishapu jukumu lao kubwa sasa ni kushirikiana na serikali kupambana na janga la COVID -19 kwa kusaidia kuimarisha au kuboresha mifumo ya afya.

“Shirika la World Vision Tanzania Kanda ya Ziwa tumeleta vifaa vya kujikinga na COVID – 19 ambavyo vimenunuliwa kutoka MSD lakini Magauni yamenunuliwa kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kusaidia watumishi wa sekta ya afya katika mkoa mzima wa Shinyanga”,alisema Massenza.

Alivitaja vifaa hivyo kuwa Vipaza sauti 243 ‘Megaphones’ kwa ajili ya watoa huduma ngazi ya jamii kutoa elimu ya Corona vijijini, Barakoa ‘ Surgical masks’ pea 1000, Vitakasa mikono ‘ Sanitizers’ lita 300, Magauni maalumu ya kujikinga‘ Personal Protective Equipments – PPE Gouwns’ 60, Gloves boksi 1000 vyote vikiwa na thamani ya shilingi 29,013,000/=.

Alisema mbali na kuchangia vifaa tiba na vifaa kinga, pia wametoa mafunzo kuhusu ugonjwa wa Corona kwa watoa huduma ngazi ya jamii 117,watoa huduma 132 kwenye vituo vya afya na madiwani 47 wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

“Kwa ujumla mchango wetu World Vision Tanzania katika mkoa wa Shinyanga mpaka sasa umegharimu shilingi 100,083,500/=,na tutaendelea kutoa mchango mpaka tutakapofanikiwa kumaliza tatizo hili la COVID 19”,alisema.

“Tunaishukuru serikali kwa ushirikiano inaotupatia katika mapambano dhidi ya COVID -19”,aliongeza Massenza.

Akipokea vifaa hivyo Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack alilishukuru Shirika la World Vision kwa mchango huo wa vifaa tiba akibainisha kuwa vitawasaidia watoa huduma za afya kuwa na amani wakati wa kwenda kuhudumia wagonjwa kwa sababu watakuwa na uhakika kuwa na wao wamejikinga dhidi ya maambukizi ya COVID – 19.

“Mimi niwashukuru sana World Vision, tuko pamoja na tutaendelea kushirikiana na naomba muendelee msichoke kutoa mchango kwa sababu ugonjwa huu siyo wa mtu hakuna anayenyoshewa kidole kuwa huyu atapata. Tunakijikinga sote, tunajikinga sisi ili pia tusiambukize na wengine lakini na wale tunaowakinga wakiweza kujikinga na sisi hatuwezi kuambukizwa",alisema Mhe. Telack. 

Mkuu huyo wa mkoa alitumia fursa hiyo kuwashukuru wadau wote wanaoendelea kushirikiana na serikali kukabiliana na ugonjwa wa Corona.

Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile alisema mchango huo wa vifaa utaongeza ari,nguvu na moyo kwa watumishi wa afya kuhakikisha kuwa wanatoa huduma stahiki kwa wagonjwa bila kusita,bila hofu wala mashaka.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Kushoto ni Meneja wa World Vision Tanzania Kanda ya Ziwa John Massenza akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack  gauni maalumu la kujikinga na maambukizi ya COVID -19' PPE Gouwns' ambalo ni sehemu ya magauni 60 yaliyolewa kwa ajili ya kusaidia watumishi wa sekta ya afya katika mkoa wa Shinyanga kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona ‘Covid 19’ wanapohudumia wagonjwa leo Ijumaa Mei 8,2020 katika Hospitali ya Rufaa mkoa wa Shinyanga. Kulia ni Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack  akiangalia gauni maalumu la kujikinga na maambukizi ya COVID -19' PPE Gouwns' ambalo ni sehemu ya magauni 60 yaliyolewa na Shirika la World Vision Tanzania kwa ajili ya kusaidia watumishi wa sekta ya afya katika mkoa wa Shinyanga kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona ‘Covid 19’ wanapohudumia wagonjwa.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack  akikagua gauni maalumu la kujikinga na maambukizi ya COVID -19' PPE Gouwns' ambalo ni sehemu ya magauni 60 yaliyolewa na Shirika la World Vision Tanzania kwa ajili ya kusaidia watumishi wa sekta ya afya katika mkoa wa Shinyanga kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona ‘Covid 19’ wanapohudumia wagonjwa.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akikagua vazi maalumu la kujikinga na maambukizi ya COVID -19' ambalo ni sehemu ya magauni 60 yaliyolewa na Shirika la World Vision Tanzania kwa ajili ya kusaidia watumishi wa sekta ya afya katika mkoa wa Shinyanga kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona ‘Covid 19’ wanapohudumia wagonjwa.
Kushoto ni Meneja wa World Vision Tanzania Kanda ya Ziwa John Massenza akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack Kipaza sauti na Gloves.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akiangalia moja Sanitizer ambayo ni sehemu ya lita 200 zilizotolewa na Shirika la World Vision Tanzania kwa ajili ya kusaidia watumishi wa sekta ya afya katika mkoa wa Shinyanga kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona ‘Covid 19’ wanapohudumia wagonjwa.
 Kulia ni Meneja wa World Vision Tanzania Kanda ya Ziwa John Massenza akizungumza wakati wa kukabidhi msaada wa vifaa tiba na kinga vyenye thamani ya shilingi milioni 29 kwa ajili ya kusaidia watumishi wa sekta ya afya katika mkoa wa Shinyanga kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona ‘Covid 19’ wanapohudumia wagonjwa.
Meneja wa World Vision Tanzania Kanda ya Ziwa John Massenza akielezea namna wanavyoshirikiana na serikali katika mapambano dhidi ya Virusi vya Corona.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akilishukuru Shirika la World Vision kwa mchango wa vifaa tiba na kueleza kuwa vitawasaidia watoa huduma za afya kuwa na amani wakati wa kwenda kuhudumia wagonjwa kwa sababu watakuwa na uhakika kuwa na wao wamejikinga dhidi ya maambukizi ya COVID – 19.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akiwashukuru wadau wanaoshirikiana na serikali katika mapambano dhidi ya Virusi vya Corona.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akiwasisitiza watumishi wa afya na wananchi kuendelea kuchukua tahadhari kuhusu ugonjwa wa Corona.
Watumishi wa afya katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga wakifuatilia zoezi la kukabidhi vifaa tiba na kinga vilivyotolewa na Shirika la World Vision Tanzania.
Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile akilishukuru Shirika la World Vision Tanzania kwa mchango wa vifaa tiba na kinga ambapo alisema mchango huo wa vifaa utaongeza ari,nguvu na moyo kwa watumishi wa afya kuhakikisha kuwa wanatoa huduma stahiki kwa wagonjwa bila kusita,bila hofu wala mashaka.
 Sehemu ya vifaa tiba na kinga vyenye thamani ya shilingi milioni 29 vilivyotolewa na Shirika la World Vision Tanzania limetoa kwa ajili ya kusaidia watumishi wa sekta ya afya katika mkoa wa Shinyanga kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona ‘Covid 19’ wanapohudumia wagonjwa.
 Sehemu ya vifaa tiba na kinga vyenye thamani ya shilingi milioni 29 vilivyotolewa na Shirika la World Vision Tanzania limetoa kwa ajili ya kusaidia watumishi wa sekta ya afya katika mkoa wa Shinyanga kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona ‘Covid 19’ wanapohudumia wagonjwa.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Share:

Serikali Yataja Sababu za Kuchelewa Kutoa Taarifa Za Mwenendo wa Wagonjwa Wa Corona Nchini

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema sababu ya kutotangaza mwenendo wa ugonjwa wa Corona ni kutokana na maboresho yanayofanyika kwenye Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii, ambapo kuna marekebisho yanafanyika na ndani ya siku chache marekebisho yatakamilika na watatoa taarifa.

Aidha Waziri Ummy amesisitiza kuwa vifo vinavyotokana na Corona vipo na kesi za maambukizi zipo, hivyo wananchi wanatakiwa waendelee kuchukua tahadhari ili kuepuka kuambukizwa huku akiwataka kufuata taarifa sahihi na kuacha kujawa na hofu.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger