Friday, 8 May 2020

Tumefanya Maboresho Kwenye App Yetu ya Mpekuzi Ili Kukuwezesha Kupata Habari zetu Haraka hasa Wakati huu wa janga la Corona

Tumefanya maboresho katika App yetu ya MPEKUZI ili kuendana na changamoto ya sasa ya janga la Corona inayoikumba dunia Nzima

Usikubali kupitwa na taarifa muhimu zinazoendelea hapa nchini na Duniani  kwa Ujumla . Tumejipanga vizuri sana kukupatia taarifa sahihi na kwa wakati.

πŸ‘‰1. Tumebadili muonekano na kuufanya kuwa mzuri zaidi
πŸ‘‰2. Kila habari tunayoweka kuanzia sasa utapata notification kwenye simu yako 
πŸ‘‰3. Habari zote kwa sasa zinafika kwa haraka kwenye simu yako kuliko ilivyokuwa hapo awali

KUMBUKA: App yetu ni BURE. Unachotakiwa kukifanya ni kuingia Playstore na kupakua MPEKUZI APP

Kama tayari unayo, basi Ingia Playstore kwa ajili ya kupata UPDATE hii ya Toleo Jipya

Tumekurahisishia, Unaweza pia ...<<KU BOFYA HAPA>> Kupata toleo hili Bure Kabisa


Share:

Picha : WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA TANZANIA ATUA MADAGASCAR KUCHUKUA DAWA YA CORONA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi wa kulia akiwa amebeba dawa ya kutibu ugonjwa wa virusi vya corona
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi wa kulia akinywa dawa ya kutibu ugonjwa wa virusi vya corona
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Madagascar Mhe. Tehindrazanarivelo Djacoba As Oliva mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Antananarivo kwa ajili ya kupokea msaada wa dawa ya kutibu na kukinga ugonjwa wa COVID-19 unaosababishwa na Virusi vya Corona uliotolewa kwa Tanzania na Nchi ya Madagascar.
Share:

Picha : WORLD VISION TANZANIA YATOA MSAADA WA VIFAA TIBA NA KINGA CORONA KWA WATOA HUDUMA ZA AFYA SHINYANGA

Shirika la World Vision Tanzania limetoa msaada wa vifaa tiba na kinga vyenye thamani ya shilingi milioni 29 kwa ajili ya kusaidia watumishi wa sekta ya afya katika mkoa wa Shinyanga kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona ‘Covid 19’ wanapohudumia wagonjwa.

Vifaa hivyo vimekabidhiwa leo Ijumaa Mei 8, 2020 na Meneja wa World Vision Tanzania Kanda ya Ziwa John Massenza kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga.

Massenza alisema wao kama wadau wa sekta ya afya wanaofanya kazi zao katika wilaya ya Shinyanga,Kahama na Kishapu jukumu lao kubwa sasa ni kushirikiana na serikali kupambana na janga la COVID -19 kwa kusaidia kuimarisha au kuboresha mifumo ya afya.

“Shirika la World Vision Tanzania Kanda ya Ziwa tumeleta vifaa vya kujikinga na COVID – 19 ambavyo vimenunuliwa kutoka MSD lakini Magauni yamenunuliwa kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kusaidia watumishi wa sekta ya afya katika mkoa mzima wa Shinyanga”,alisema Massenza.

Alivitaja vifaa hivyo kuwa Vipaza sauti 243 ‘Megaphones’ kwa ajili ya watoa huduma ngazi ya jamii kutoa elimu ya Corona vijijini, Barakoa ‘ Surgical masks’ pea 1000, Vitakasa mikono ‘ Sanitizers’ lita 300, Magauni maalumu ya kujikinga‘ Personal Protective Equipments – PPE Gouwns’ 60, Gloves boksi 1000 vyote vikiwa na thamani ya shilingi 29,013,000/=.

Alisema mbali na kuchangia vifaa tiba na vifaa kinga, pia wametoa mafunzo kuhusu ugonjwa wa Corona kwa watoa huduma ngazi ya jamii 117,watoa huduma 132 kwenye vituo vya afya na madiwani 47 wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

“Kwa ujumla mchango wetu World Vision Tanzania katika mkoa wa Shinyanga mpaka sasa umegharimu shilingi 100,083,500/=,na tutaendelea kutoa mchango mpaka tutakapofanikiwa kumaliza tatizo hili la COVID 19”,alisema.

“Tunaishukuru serikali kwa ushirikiano inaotupatia katika mapambano dhidi ya COVID -19”,aliongeza Massenza.

Akipokea vifaa hivyo Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack alilishukuru Shirika la World Vision kwa mchango huo wa vifaa tiba akibainisha kuwa vitawasaidia watoa huduma za afya kuwa na amani wakati wa kwenda kuhudumia wagonjwa kwa sababu watakuwa na uhakika kuwa na wao wamejikinga dhidi ya maambukizi ya COVID – 19.

“Mimi niwashukuru sana World Vision, tuko pamoja na tutaendelea kushirikiana na naomba muendelee msichoke kutoa mchango kwa sababu ugonjwa huu siyo wa mtu hakuna anayenyoshewa kidole kuwa huyu atapata. Tunakijikinga sote, tunajikinga sisi ili pia tusiambukize na wengine lakini na wale tunaowakinga wakiweza kujikinga na sisi hatuwezi kuambukizwa",alisema Mhe. Telack. 

Mkuu huyo wa mkoa alitumia fursa hiyo kuwashukuru wadau wote wanaoendelea kushirikiana na serikali kukabiliana na ugonjwa wa Corona.

Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile alisema mchango huo wa vifaa utaongeza ari,nguvu na moyo kwa watumishi wa afya kuhakikisha kuwa wanatoa huduma stahiki kwa wagonjwa bila kusita,bila hofu wala mashaka.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Kushoto ni Meneja wa World Vision Tanzania Kanda ya Ziwa John Massenza akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack  gauni maalumu la kujikinga na maambukizi ya COVID -19' PPE Gouwns' ambalo ni sehemu ya magauni 60 yaliyolewa kwa ajili ya kusaidia watumishi wa sekta ya afya katika mkoa wa Shinyanga kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona ‘Covid 19’ wanapohudumia wagonjwa leo Ijumaa Mei 8,2020 katika Hospitali ya Rufaa mkoa wa Shinyanga. Kulia ni Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack  akiangalia gauni maalumu la kujikinga na maambukizi ya COVID -19' PPE Gouwns' ambalo ni sehemu ya magauni 60 yaliyolewa na Shirika la World Vision Tanzania kwa ajili ya kusaidia watumishi wa sekta ya afya katika mkoa wa Shinyanga kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona ‘Covid 19’ wanapohudumia wagonjwa.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack  akikagua gauni maalumu la kujikinga na maambukizi ya COVID -19' PPE Gouwns' ambalo ni sehemu ya magauni 60 yaliyolewa na Shirika la World Vision Tanzania kwa ajili ya kusaidia watumishi wa sekta ya afya katika mkoa wa Shinyanga kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona ‘Covid 19’ wanapohudumia wagonjwa.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akikagua vazi maalumu la kujikinga na maambukizi ya COVID -19' ambalo ni sehemu ya magauni 60 yaliyolewa na Shirika la World Vision Tanzania kwa ajili ya kusaidia watumishi wa sekta ya afya katika mkoa wa Shinyanga kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona ‘Covid 19’ wanapohudumia wagonjwa.
Kushoto ni Meneja wa World Vision Tanzania Kanda ya Ziwa John Massenza akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack Kipaza sauti na Gloves.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akiangalia moja Sanitizer ambayo ni sehemu ya lita 200 zilizotolewa na Shirika la World Vision Tanzania kwa ajili ya kusaidia watumishi wa sekta ya afya katika mkoa wa Shinyanga kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona ‘Covid 19’ wanapohudumia wagonjwa.
 Kulia ni Meneja wa World Vision Tanzania Kanda ya Ziwa John Massenza akizungumza wakati wa kukabidhi msaada wa vifaa tiba na kinga vyenye thamani ya shilingi milioni 29 kwa ajili ya kusaidia watumishi wa sekta ya afya katika mkoa wa Shinyanga kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona ‘Covid 19’ wanapohudumia wagonjwa.
Meneja wa World Vision Tanzania Kanda ya Ziwa John Massenza akielezea namna wanavyoshirikiana na serikali katika mapambano dhidi ya Virusi vya Corona.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akilishukuru Shirika la World Vision kwa mchango wa vifaa tiba na kueleza kuwa vitawasaidia watoa huduma za afya kuwa na amani wakati wa kwenda kuhudumia wagonjwa kwa sababu watakuwa na uhakika kuwa na wao wamejikinga dhidi ya maambukizi ya COVID – 19.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akiwashukuru wadau wanaoshirikiana na serikali katika mapambano dhidi ya Virusi vya Corona.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akiwasisitiza watumishi wa afya na wananchi kuendelea kuchukua tahadhari kuhusu ugonjwa wa Corona.
Watumishi wa afya katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga wakifuatilia zoezi la kukabidhi vifaa tiba na kinga vilivyotolewa na Shirika la World Vision Tanzania.
Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile akilishukuru Shirika la World Vision Tanzania kwa mchango wa vifaa tiba na kinga ambapo alisema mchango huo wa vifaa utaongeza ari,nguvu na moyo kwa watumishi wa afya kuhakikisha kuwa wanatoa huduma stahiki kwa wagonjwa bila kusita,bila hofu wala mashaka.
 Sehemu ya vifaa tiba na kinga vyenye thamani ya shilingi milioni 29 vilivyotolewa na Shirika la World Vision Tanzania limetoa kwa ajili ya kusaidia watumishi wa sekta ya afya katika mkoa wa Shinyanga kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona ‘Covid 19’ wanapohudumia wagonjwa.
 Sehemu ya vifaa tiba na kinga vyenye thamani ya shilingi milioni 29 vilivyotolewa na Shirika la World Vision Tanzania limetoa kwa ajili ya kusaidia watumishi wa sekta ya afya katika mkoa wa Shinyanga kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona ‘Covid 19’ wanapohudumia wagonjwa.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Share:

Serikali Yataja Sababu za Kuchelewa Kutoa Taarifa Za Mwenendo wa Wagonjwa Wa Corona Nchini

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema sababu ya kutotangaza mwenendo wa ugonjwa wa Corona ni kutokana na maboresho yanayofanyika kwenye Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii, ambapo kuna marekebisho yanafanyika na ndani ya siku chache marekebisho yatakamilika na watatoa taarifa.

Aidha Waziri Ummy amesisitiza kuwa vifo vinavyotokana na Corona vipo na kesi za maambukizi zipo, hivyo wananchi wanatakiwa waendelee kuchukua tahadhari ili kuepuka kuambukizwa huku akiwataka kufuata taarifa sahihi na kuacha kujawa na hofu.


Share:

Corona Yashusha Mapato Sekta Ya Utalii Tanzania

Kutokana na virusi vya corona vinavyoendelea kuisumbua dunia, Wizara ya Utalii na Maliasili imesema mapato katika sekta hiyo yameshuka kutoka Sh trilioni 2.6 zilizotarajiwa kukusanywa 
 
Pia taasisi zilizokadiriwa kukusanya zaidi ya Sh bilioni 132.1 zinatarajia kukusanya Sh bilioni 33.5 ikiwa ni anguko la asilimia 75.

Vilevile, Serikali imesema kama hali haitatulia hadi Oktoba, ajira za moja kwa moja katika sekta ya utalii zitashuka kutoka 623,000 hadi kufikia 146,000 na watalii watashuka kutoka 1,867,000 waliotarajiwa hadi 437,000.

Kauli hiyo ilitolewa bungeni jana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla wakati akiwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2020/21.

Dk. Kigwangalla alisema sekta ya utalii imeathirika kwa kiwango kikubwa kutokana na corona.
 
Alisema wizara ilifanya tathmini ya awali (rapid assessment) iliyojikita katika kipindi cha tangu ugonjwa huo uanze hadi Aprili 6, mwaka huu.

Dk. Kigwangalla alisema tathmini hiyo ilibaini kuwa madhara makubwa ya corona katika sekta ya utalii yalianza kuonekana mwanzoni mwa Machi, tofauti na Februari na Januari, mwaka huu ambapo hali ilikuwa shwari. Alisema tathmini ilibaini mashirika 13 ya ndege yalisitisha safari za kuja nchini tangu Machi 25, mwaka huu hivyo kuondoa uwezekano wa kuendelea kupata watalii kutoka nje ya nchi.

Dk. Kigwangalla alisema mashirika yaliyositisha safari zake ni pamoja ni Emirates, Swiss, Oman Air, Turkish, Egyptian Air, South African Airways, Rwandair, Qatar, Kenya Airways, Uganda Airlines, Fly Dubai na KLM

Alisema NCAA ilikadiria kukusanya Sh bilioni 162.7, kwa sasa itakusanya Sh bilioni 58, TFS ilikadiria Sh bilioni 153.6, sasa ni Sh bilioni 121 na Tawa ilikadiria Sh bilioni 58.1 sasa ni Sh bilioni 22.


Share:

Rais wa Marekani Donald Trump na Makamu Wake Wapimwa Tena Corona Baada ya Mwanajeshi wa IKULU Kukutwa na Virusi Hivyo

Rais wa Marekani Donald Trump na Makamu wake wa Rais Mike Pence wamelazimika kupima tena corona baada ya Mwanajeshi anayefanya kazi Ikulu kubainika ana corona, Trump na Pence wote ni wazima, hawajakutwa na virusi hivyo.

"Tuna vipimo bora kuliko Nchi zote Duniani, nimepima jana na leo pia na sina corona, kupima sio kitu kigumu, imenishangaza kuona Mtu wangu wa karibu ana corona namfahamu ni Mtu mzuri, ila ndio hivyo wasiwasi umetanda kila kona unaweza kukutana na Mtu ni mzima, kesho ukasikia tayari ana corona”-  Amesema Trump

Hadi mapema leo hii vifo vitokanavyo na Virusi vya corona Nchini Marekani vimefikia 76,938 na visa 1,292,623 ikiwa ndiyo Nchi inayoongoza Duniani kwa wagonjwa na vifo.

Hispania visa 256,855 na vifo 26,070, Italia visa 215,858 na vifo 29,958, Uingereza visa 206,715 na vifo 30,615 ikiwa ndiyo Nchi inayoongoza kwa vifo vya corona kwa Bara la Ulaya.


Share:

DC Jokate Mwegelo Kasema Kisarawe Imeanza Kuzalisha PPE, barakoa na vitakasa mikono Kwa Ajili Ya Kukabiliana na Corona

Hospitali Ya Wilaya Ya Kisarawe katika kuwalinda wahudumu  wote wa afya waliomstari wa mbele katika mapambano ya Virusi vya Corona,  imeanza kuzalisha PPE 


Pamoja na hayo pia imeanza kuzalisha barakoa na vitakasa mikono vyote tayari vinapatikana kwenye famasia/pharmacy  wilayani humo.

Hayo yameelezwa Leo Ijumaa May 08, 2020 na Mkuu wa Wilaya hiyo, Jokate Mwegelo kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Akizungumzia ubora wa vazi hilo ambalo linafanana na lile linalozalishwa Muhimbili, Jokate ameandika; "Kuhusiana na ubora wa vazi letu la PPE; Quality ni kama ile ya Muhimbili kwa maana ya material iliyotumika lakini kwa maana ya uimara yetu imeongezwa uimara wa ndani kuzuia isichanike/kutatuka haraka wakati wa kuitumia."


Share:

Dereva mwingine wa Lori kutoka Tanzania akutwa na corona Uganda

Wizara ya Afya Uganda imesema Dereva mwingine wa Lori kutoka Tanzania (32) amebainika kuwa na corona na kufanya maambukizi ya corona Uganda kufikia 101 kutoka 100.

 Dereva huyo aliingia Uganda kupitia mpaka wa Mutukula, waliopona corona Uganda wamesalia 55 na hakuna kifo.


Share:

Cecil Mwambe Adai Sasa Amerejea Bungeni Rasmi Baada Ya Kuitwa na Spika.....Bunge Likiisha Ataiacha CHADEMA Na Kurudi CCM

Mbunge wa Ndanda kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Cecil Mwambe, amesema kuwa kwa sasa amerejea Bungeni rasmi kumalizia muda wake wa Ubunge kwa kipindi kilichobaki na kwamba yeye ni mwanachama halali wa CCM, hivyo uchaguzi ujao atagombea kupitia tiketi ya CCM.

Mwambe ameyabainisha hayo leo Mei, 8, 2020, wakati akizungumza na Kituo cha  EATV na kuongeza kuwa yeye ni kiongozi mtiifu hivyo aliona ni vyema kuitikia wito wa Spika Ndugai, na kwamba leo atakaa bungeni upande wa Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni Wilfred Lwakatare kwa kuwa ndiye anayemtambua kwa sasa.

"Nimefika Dodoma kama ambavyo nilisema, nimekutana na Mh Spika hivyo ninatakiwa kuendelea na shughuli zangu za Kibunge, mimi nitaendelea kuwa Mbunge wa CHADEMA na mchana huu nitahudhuria vikao vya Bunge, nilijiuzulu uanachama na nikaacha kila kitu hivyo Mh Spika amenitaka nimalizie kipindi kilichosalia" amesema Mbunge Mwambe.

Akizungumzia suala la kulipwa mishahara na posho zingine ilihali yeye si Mbunge, Mwambe amesema kuwa, "Mimi nasema kwamba Spika alikuwa halipi mshahara kwa Mbunge hewa, mimi nimelipwa mshahara wangu wa mwisho ni wa Februari 15, ambao nililipwa Machi na nilipewa nusu sababu ndiyo nilioufanyia kazi".


Share:

Marekani Yaondoa Mifumo Yake Ya Makombora Saud Arabia

Marekani imeanza kuondoa katika ardhi ya Saudi Arabia mifumo yake ya makombora ya Patriot na zana zingine za kijeshi, ikiwa ni sehemu ya mkakati mpana wa kupunguza uungaji mkono wake wa kijeshi kwa utawala huo wa kifalme.

Katika ripoti ya jana Alhamisi, jarida la The Wall Street Journal lilinukuu maafisa wa serikali ya Washington ambao hawakutaka kutaja majina yao waliosema kuwa, mifumo minne ya makombora ya ardhini hadi angani ya Patriot, zana nyinginezo za kijeshi pamoja na maafisa wa kijeshi wa Marekani wataondolewa kutoka kwenye vituo vya mafuta vya Saudia.

Kadhalika maafisa hao wamesema Marekani inatazamiwa kupunguza vikosi vyake vya baharini katika Ghuba ya Uajemi karibuni hivi, na kwamba tayari ndege mbili za kivita za US zimeshaondolewa katika eneo hili.

Zana hizo za kijeshi za Marekani zilipelekwa Saudia mwezi Septemba mwaka jana, baada ya kujiri wimbi la mashambulizi ya makombora dhidi ya vituo vya mafuta vya Riyadh pamoja na hofu ya kuibuka vita iliyokuwepo kati ya Marekani na Iran

Mapema mwezi uliopita wa Aprili, Rais Donald Trump alitishia kwamba, Washington itasitisha uungaji mkono wake wa kijeshi kwa Saudia, iwapo utawala huo wa kifalme hautasitisha mvutano baina yake na Russia juu ya bei ya mafuta.

Trump alitoa vitisho hivyo katika mazungumzo ya simu na Mohammad bin Salman, mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia, ambapo alisema kuwa Marekani haitakuwa na budi ila kuanza kuondoa vikosi vyake Saudia iwapo utawala wa Riyadh hautapunguza kiwango cha mafuta unachozalisha.


Share:

TAKUKURU Manyara yampiga miaka saba jela Mhasibu wa Halmashauri,wengine wapewa onyo kali.

Na John Walter- Manyara.
Mahakama  kuu ya Tanzania kanda ya Arusha imemhukumu kifungo cha miaka 7 gerezeni  aliyekuwa Mhasibu wa Halmashauri ya wilaya Simanjiro Mkoani Manyara, Peter John Mollel kwa makosa ya wizi akiwa mtumishi wa umma.

 Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo Mei 8, 2020, kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Manyara,Holle Makungu  amesema kwamba hukumu hiyo ilitolewa mei 7 mwaka huu (2020) na Naibu Msajili wa mahakama kuu ya kanda ya Arusha,John Mkwabi.

Kamanda huyo wa TAKUKURU alisema kwamba pamoja na adhabu hiyo iliyotokana na makosa 11 ya wizi yaliyofanywa na mshatakiwa akiwa mtumishi wa umma, Hakimu Mkwabi pia alitoa adhabu ya kulipa faini ya shilingi milioni  4,000,000  kwa  kila kosa  kwa  makosa 9 ya matumizi ya nyaraka  kumdanganya mwajiri, sawa na shilingi milioni 36,000,000  au kifungo cha miaka mitatu jela.

Hakimu Mkwabi pia alimhukumu mshtakiwa huyo kifungo cha mwaka mmoja gerezani bila faini kwa makosa mawili ya matumizi mabaya ya madaraka kinyume cha kifungu cha 31 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11/2007.

Adhabu hiyo iliotolewa mei 7 mwaka huu na hakimu Mkwabi,  katika kesi ya jinai Namba CC.48/2016 aliyokuwa akiisikiliza katika mahakama ya Wilaya ya Simanjiro -Orkesumeti Mkoani Manyara.

Makungu alisema mwingine aliyetiwa hatiani katika kesi hiyo na kupewa adhabu sawasawa na mshtakiwa wa kwanza ni mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo  Ester Melkior ambaye alikuwa mhasibu msaidizi katika Halmashauri hiyo ambapo washtakiwa wote wawili wamepelekwa Gerezani kuanza kutumikia kifungo.

Awali  waendesha mshataka wa TAKUKURU Isdory Kyando akisaidiwa na Adamu Kilongozi waliwafikisha washtakiwa hao mahakamani hapo na kuwasomea jumla ya makosa (24),katika makosa hayo (10) yalihusu kutumia nyaraka za kumdanganya mwajiri kinyume cha cha kifungo cha 22 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa  namba 11/2007.

"makosa mawili yalihusu matumizi mabaya ya madaraka kifungu cha 31 sheria ya kuzia na kupambana na rushwa namba 11/2007 na makosa 12 yalihusu  wizi uliofanywa na washatakiwa wakiwa watumishi wa umma kinyume na vifungu vya 258 na 270 vya sheria ya kanuni ya adhabu"Alisema Makungu

Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Manyara Holle Makungu aliendela kueleza kwamba, waendesha mashata hao waliwasilisha ushahidi usioacha shaka mahakamani hapo kuonyesha kwamba kati ya mwaka 2008 na 2010 mshatakiwa wa kwanza kwa nafasi yake ya mweka hazina wa Halmashauri alikuwa ndiye muidhinishaji wa nyaraka hizo na mshatakiwa wa pili kwa nafasi yake ya mhasibu Msaidizi ndiye aliyeandaa nyaraka hizo.

"Kwa pamoja walishirikiana kuzidisha orodha ya walipwaji na kiasi cha mishahara ambacho walipaswa kulipwa kwenye hati za malipo kisha kuziwasilisha nyaraka hizo benki kwa ajili ya malipo ambapo fedha hizo zilizokuwa zikizidi zilikuwa zinaingizwa kwenye akaunti za benki za washtakiwa na kisha washtakiwa hao kuzitumia kwa manufaa yao,hivyo jumla ya fedha walizojipatia kutokana na udanganyifu huo ni sh.Mil.34,520,000 "alisema Makungu.

Aidha alisema  kabla ya adhabu hiyo kutolewa na Hakimu Mkwabi,wakili wa utetezi Justus IIyarugo aliiomba mahakama iwapunguzie adhabu washtakiwa kwa kuwa mshtakiwa Peter John Mollel ni baba mwenye familia inayomtegemea, pia wakili huyo aliiomba mahakama imuonee huruma na kumpunguzia adhabu mshtakiwa wa pili Esta Melkior kwa kuwa ni mama  mwenye mtoto mmoja ,hana mume pia ni mlezi wa mama yake mzazi.

Alisema  Holle Makungu kwamba kwa upande wa waendesha mashtaka wa TAKUKURU waliiomba mahakama itoe adhabu kali kwa washtakiwa  kwa kuwa makosa waliyoyatenda ya rushwa na wizi wakiwa watumishi wa umma ni kati ya makosa mabaya na ndiyo maana bunge la Tanzania liliweka adhabu kali kwa makosa hayo ili iwe fundisho kwa watumishi wa umma wenye fikira za wizi na rushwa katika utumishi wa umma.

Hata hivyo Hakimu wa Mahakama hiyo ya Tanzania kanda ya Arusha John Mkwabi baada ya kusikiliza na kuzingatia hoja zilizotolewa na upande wa mashtaka na upande wa utetezi aliweza kutoka adhabu kwa mjibu wa sheria kulingana na makosa ambayo washtakiwa waliyatenda .

Hata hivyo, Mkuu wa Takukuru mkoa wa Manyara,Holle Makungu alitoa wito kwa watumishi wa umma kuridhika na vipato vya haki wanayolipwa na Serikali na kwa wale ambao wanafikra za kufanya wizi wakiwa watumishi wa umma ,ubadhirifu,ufisadi na rushwa hawatakuwa salama .



Share:

Tangazo la kuitwa kazini Madaktari nafasi 610.






Share:

Wabunge waliopo Dar es Salaam watakiwa kuripoti Polisi.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar, limesema baada ya RC Makonda kutoa saa 24 kwa Wabunge walioko jijini humo kurejea Bungeni, limewataka wale ambao bado hawajaondoka, kuripoti kwa hiyari yao katika ofisi ya Upelelezi, Kanda Maalum kwa mahojiano


Share:

World Vision Yatoa Vifaa Vya Kujikinga Na Covid-19 Vya Milioni 17 Kwa Mkoa Wa Tabora

NA TIGANYA VINCENT
SHIRIKA la World Vision Tanzania limekabidhi vifaa vya thamani ya shilingi milioni 17.1 vya kudhibiti virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wahoma kali ya mapafu ya Covid -19 kwa Mkoa wa Tabora

Msaada huo umekabidhiwa jana mjini Nzega na Meneja wa Kanda wa Shirika World Vision John Masenza kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri.

Alitaja msaada huo unajumuisha glovu boksi 990, magauni ya wahudumu wa afya ya kuwafaa wakati wa kuwahudumia wagonjwa 80 , lita 290 ya vitakasa mikono na vipasa saui kwa ajili ya utoaji wa elimu kujikinga na corona 22.

Masenza alisema msaada huo utagawanywa kwa Halmashauri zote nane za Mkoa wa Tabora ili ziwaweze watoa huduma kusaidia katika mapambano dhidi ya Covid-19.

Alisema msaada mwingine ambao ni barakoa kwa ajili ya huduma za upasuaji ziko njia na zitarajiwa kuwakabidhiwa baada ya kuwasili.

Akipokea msaada huo Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mwanri alilishukuru shirika la World Vision kwa kuunga mkono juhudi za Serikali za kukabiliana na kudhibiti ugonjwa wa Covid -19.

Alisema msaada huo umekuja wakati muhimu ambapo Taifa liko katika vita ya kudhibiti ugonjwa wa Covid- 19 usiendelee kusambaa.

Mkuu huyo wa Mkoa alisema wadau wote Mkoani humo wanapaswa kuungana katika vita ili hatimaye waweze kuushinda ugonjwa wa Covid-19.

Alisema msaada huo walioupokea baada ya kudhibitishwa na wataalamu wa sekta ya afya kuwa ziko vizuri zitagawanywa katika Wilaya zote za Mkoa wa Tabora kwa ajili ya kuwasaidia watoa huduma za afya ambao wanasaidia kukabiliana na ugonjwa wa Covid-19 na watu wengine ambao hajiwezi.

Mkuu huyo wa Mkoa alitoa wito kwa wadau wengine wanaoendesha shughuli zao ikiwemo za biashara na kutoa huduma mbalimbali kuendelea kushirikiana na Serikali katika mapambano dhidi ya janga la Corona.

Mwisho


Share:

KASHUWASA Waiunga Mkono Serikali Katika Mapambano Dhidi Ya Covid 19

SALVATORY NTANDU
Katika jitihada za kuunga mkono Serikali katika mapambano dhindi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu  inayosababishwa na virusi vya Corona Mamlaka ya Maji Kahama na Shinyanga (KASHUWASA) imekabidhi vifaa vya kunawia mikono  kwa Mkuu wa wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Anamringi Macha ili viweze kusaidia katika mapambano ya dhidi ya COVID 19.

Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi  vifaa hivyo iliyofanyika Mei 7 mwaka huu katika Mjini Kahama Mkurugenzi wa KASHUWASA, Joshua Mageyekwa amesema vifaa hivyo vitatumika  kuwasaidia wananachi hasa kwenye sehemu yenye mikusanyiko mikubwa kama vile kwenye masoko minada na hospitali.

“Bodi ya wakurugezi ya KASHUWASA ilikubaliana kugawa vifaa vya kunawia mikono katika maeneo yote ambayo sisi tunatoa huduma ambapo leo katika wilaya ya kahama tunatoa mapipa 15 yenye ujazo wa lita 210 ili kuisaidia jamii katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa COVID 19,”alisema Mageyekwa.

Aliongeza kuwa KASHUWASA itaendelea kushirikiana na serikali katika janga hili ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma stahiki ambazo zitawawezesha kuchukua tahadhari sambamba na kuwakinga wengine kwa kuzingatia maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa afya.

Awali akipokea vifa hivyo mkuu wa wilaya hiyo Anamringi Macha amesema msaada huo umekuja katika muda muafaka na atahakikisha  mapipa hayo yanawekwa katika maeneo yote ya umma yenye mikusanyiko mikubwa ya watu katika halmashauri tatu za Ushetu,Mji na Msalala.

“Nitoe shukurani zangu kwenu KASHUWASA kwa msaada wenu kwa wananchi wa wilaya ya kahama,awali tulianza kutumia ndoo ndogo kwaajili ya kunawia mikono lakini hivi sasa nyinyi mmetupatia mapipa makubwa tutahakikisha yanatumika katika maeneo yote ya umma,”alisema Macha.

Macha amewaomba wafanyabiashara na watoa huduma wengine katika maeneo yao kuhakikisha wanalinda afya za wateja wao kwa kuhakikisha wanachukua tahadhari kwa kunawa mikono kwa maji safi na salama ili kujikinga na Janga la ugonjwa wa COVID 19.

“Kama hakuna wateja hakuna biashara ni wajibu wenu wafanyabiashara kuhakikisha mnaweka mazingira rafiki ili kuendeleza biashara zenu,wamiliki wa baa na watoa huduma za usafiri himizeni wateja wenu wanawe mikono kabla ya kupata huduma au kuingia kwenye basi,”alisema Macha.

Sambamba na hilo Macha alisema kuwa mwitikio wa wananchi katika unawaji wa mikono katika maeneo mbalimbali umekuwa mkubwa ikilinganishwa na hapo awali ambapo hivi sasa elimu juu ya kujikinga na ugonjwa huu imeanza kueleweka kwani katika maeneo mengi huwezi kupata huduma bila kunawa mikono au kuvaa barakoa.

Mwisho.


Share:

Halmashauri ya mji wa Kahama Yatoa Msaada Kwa Waumini Wa Kiislamu Kahama

SALVATORY NTANDU
Halmashauri ya mji wa Kahama mkoani Shinyanga imetoa msaada wa vitu mbalimbali kwa baraza la waislam Tanzania (BAKWATA) wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 5.3 kwa  waumini wa dini ya kiislam wilayani  Kahama ambao utatumika katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Akikabidhi msaada huo leo  kwa Shekhe wa wilaya ya Kahama, Alhaj Omary Damka, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Anderson Msumba amesema msaada huo unalenga kuwauga mkono waumini hao katika mwezi huu maalumu wa toba.

“Halmashauri ya Mji kahama imetoa Michele, kg 1000, unga wa ngano kg 100,  Sukari Kg 200, mafuta ya kula Lita 200, Maharage kg 442 na tambi boksi 40,tunaomba msaada wetu upokelewe,sisi tumetoa kiasi hiki kidogo tunaimani kitawasaidia,”alisema Msumba.

Msumba aliongeza kuwa Halmashauri inatambua mchango wa viongozi wa dini na itaendelea kushirikiana nao katika Nyanja mabalimbali ili kuhakikisha jamii inakuwa na hofu ya Mungu na kutenda matendo Mema.

“Viongozi wa dini tunathamini uwepo wao hasa katika kipindi hiki cha Janga la Ugonjwa wa Covid 19 wamekuwa mstari wa mbele kwa kuiombea Halmashauri yetu na taifa kwa Ujumla ambapo waumini katika nyumba za ibada wanaendelea kuhimizwa kuhusiana na namna ya kuchukua tahadhari,”alisema Msumba.

Akipokea Msaada huo Shekhe wa wilaya ya Kahama Alhaj Omary Damka ameishukuru Halmashauri ya Mji kahama kwa msaada huo ambao umekuja katika kipindi muhimu cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambapo kuna wahitaji wengi katika jamii hususani kundi la wazee wasiojiweza na watoto yatima.
 
“Msaada huu tutawapatia watoto yatima,Wazee wasiojiweza sambamba na wahitaji wengine tunawashukuru kwa moyo wenu mzuri wa kutushika mkono katika kipindi hiki cha toba hakika mmefanya jambo jema la kumpenda Mwenyezi Mungu,”alisema Damka.

Sambamba na hilo Damka amewataka waumini wa kiislamu kuendelea kuchukua tadhari dhidi ya Ugonjwa wa Covid 19  kwa kuzingatia maelekezo yanayotolewa na serikali ikiwa ni pamoja na kunawa mikono na sabuni,kuvaa barakoa na kutokwenda kwenye mikusanyiko isiyokuwa na tija.

Mwisho.



Share:

Watuhumiwa Wa Ujambazi Wakamatwa Wakiwa Njiani Kwenda Kufanya Uhalifu Mkoani Arusha

Na Ahmed Mahmoud ,Arusha
Jeshi la polisi mkoa wa Arusha baada ya kupata taaarifa fiche limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wanne wa ujambazi akiwemo Mganga wa Kienyeji  wakiwa na silaha mbili za Moto kwa ajili ya kuja kufanya matukio ya kiuhalifu mkoani hapa.

Akizungumza na vyombo vya habari mkoani hapa kamanda wa polisi Jonathan Shana amesema jeshi limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa ambao ni Steven Godfrey (32) mkazi wa Tabata, Yunusi Hamed (37)mkazi wa Tanga, Said Hamisi(38) mkoa Dar es salaam na mwingine Msafiri Yohana (22) mkazi wa mwanza.

Mnamo tarehe 6 mwezi wa tano mwaka huu majira ya saa nne usiku huku maeneo ya daraja la Nduruma Kata ya Baraa Halmashauri ya jiji la Arusha jeshi letu lilifanikiwa kuwakamata watuhumiwa wanne wa Ujambazi waliokutwa na bunduki moja na Bastola moja zenye jumla ya Risasi 12 .

Alisema mnamo majira ya saa nne baada ya kupata taarifa fiche ambapo tuliweka mtego maeneo ya daraja la mto turuma ndipo tulipowaona watuhumiwa hao waliotekea Dar es salaam kuja Arusha kwa kutumia gari aina ya Toyota crown, lenye namba la usajiri T. 777 DSJ ndipo walipolisimamisha gari hilo lakini walikaidi amri.

Hata hivyo askari walichukua uamuzi wa kufyatua risasi hewani kwa lengo la kuwataadharisha lakini waliendelea kukaidi amri hiyo, ndipo Askari walipoamua kufyatua risasi kwa kulenga matairi ya gari hilo hali iliyosababisha kufanikisha ukamataji wa watuhumiwa hao huku mmoja wao aitwaye Msafiri Yohana akiwa amejeruhiwa kwa risasi katika viganja vyake vya mikono.

Aidha kwa mujibu wa Kamanda Shana katika upekuzi wa gari hilo kulikutwa na aina za  silaha mbili Shortgun (1) na bastola 1 zenye risasi nne za bunduki aina ya Shortgun na risasi nane za bastola zilizokuwa kwenye magazine pamoja na mikasi mitatu ya kukatia vyuma, nondo mbili, gundi na madawa mbalimbali ya mitishamba.

Alieleza Kamanda katika mahojiano na watuhumiwa hao wamekiri kuja Arusha kwa lengo la kufanya uhalifu na watuhumiwa hao watafikishwa mahakani pindi upelelezi utakapokamilika, ambapo akatoa wito kwa watu wote wenye nia ya kufanya uhalifu awatafanikiwa kuingia lakini watatoka majivu.

Pia niwaombe wananchi waendelee kutoa taarifa sahihi za uhalifu na wahalifu kwa jeshi hilo ili waweze kuzifanyia kazi hali itakayosaidia kuimarisha utulivu, amani na usalama tulivu uliyopo.

Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha alilipongeza jeshi hilo kwa kufanya kazi zake kwa weledi na kuwataka wananchi kufuata Maelekezo ya kutii sheria bila shuruti na wanaoshindwa mmekuwa mkiwashurutisha kama hawa

Alisema kuwa kila wakati jeshi hilo limekuwa likiwataka wananchi kutiii sheria bila shuruti na wanaokaidi mmekuwa mkiwashurutisha leo mmenyesha mfano mmekamata majambazi wametii sheria na hawakuu wawa na matokeo yake ni tofauti na huko nyuma wengi walikuwa wakikaidi na kujikuta wakiuwawa. 




Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger