Thursday, 7 May 2020

Naibu Waziri Wa Afya Afya Dr Ndugulile aagiza NIMR kufanya utafiti kuhusu Corona

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeitaka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kufanya utafiti kuhusu ugonjwa wa Corona (Covid-19) kwa kuwa kuna tofauti kubwa ya dalili zilizojitokeza kwa wagonjwa hapa nchini ukilinganisha na wagonjwa waliopo nje ya  nchi.

Agizo hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile wakati alipokutana na watafiti wa taasisi hiyo wakati  wakijadili maambukizi ya ugonjwa wa Corona na aina ya matibabu ambayo wagonjwa wanatakiwa kupatiwa hasa baada ya kubainika kuwa dalili za ugonjwa huo zinatofautiana na dalili za wagonjwa wa mataifa mengine.

Pia, amesema kupitia utafiti huo wanataka kujua aina za matibabu ambayo wagonjwa wanatakiwa kupatiwa ili kuhakikisha ugonjwa wa Covid-19 unadhibitiwa hapa nchini.

Naye Mkurugenzi Mkuu  wa NIMR, Prof. Yunus Mgaya amesema mapambano dhidi ya ugonjwa Covid-19  ni vita ambayo inapaswa kufanyiwa utafiti ambao utasaidia kupatikana kwa njia sahihi za kukabiliana na maambukizi ya ugponjwa huo.


Share:

EWURA yatakiwa kudhibiti changamoto zinazoikabili Sekta ya Maji.




Share:

AWESO AITKA EWURA KUTOWABAMBIKIA WANANCHI ANKARA KIHOLELA


Naibu Waziri wa Maji, Juma Aweso wakati akizungumza leo jijini Dodoma na Menejimenti ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kuhusu malalamiko ya wateja wa maji nchini kuhusu Ankara za Maji
Naibu Waziri wa Maji.Juma Aweso wakati akisisitiza jambo wakati akizungumza na Menejimenti ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kuhusu malalamiko ya wateja wa maji nchini kuhusu Ankara za Maji
Kaimu Mkurugenzi Mkuu EWURA,akizungumza wakati Naibu Waziri wa Maji,Juma Aweso alipokutana na Menejimenti ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kuhusu malalamiko ya wateja wa maji nchini kuhusu Ankara za Maji

Mkurugenzi wa Udhibiti Uchumi Bw.Nzinyangwa Mchany akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa maji, Juma Aweso (hayupo pichani) alipokutana na Menejimenti ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kuhusu malalamiko ya wateja wa maji nchini kuhusu Ankara za Maji
.....................................................................................
Na. Mwandishi Wetu, Dodoma
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetakiwa kuhakikisha inadhibiti bei za Ankara maji nchini zinazopandishwa kiholela na kubambikiwa Ankara kwa wananchi zinazofanywa na mamlaka za maji nchini bila kupata kibali kutoka EWURA na kutoa elimu kwa wananchi.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dodoma na Naibu Waziri wa maji,Juma Aweso wakati akizungumza na Menejimenti ya EWURA kuhusu malalamiko ya wateja wa maji nchini kuhusu Ankara za Maji.

Aweso ameitaka EWURA kuwarejeshea huduma za maji wateja wote nchini waliokatiwa maji kwa makubaliano ili waweze kupata huduma hiyo katika kipindi hiki cha kupambana dhidi ya ugonjwa wa Homa ya mapafu inayosababishwa na Virusi vya Corona(COVID 19).

"Taifa liko katika mapambano na vita dhidi ya Corona, ugonjwa unaua kama yanavyouwa magonjwa mengine kikubwa ni kuchukua tahadhari na kuzingatia maelekezo yanayotolewa na wataalam, silaha pekee ya kukabiliana nayo ni maji tiririka na sabuni, sasa tunaagiza warejesheeni wananchi maji, mliowakatia kwa kuweka utaratibu mzuri wa kulipa madeni yao,"Am.Aweso

Aidha Mhe.Aweso amesema licha ya Mambo mazuri na kazi kubwa inayofanywa na EWURA ila bado kuna matatizo na changamoto ambazo zinahitaji kupatiwa ufumbuzi wa kina ili kutoa huduma Bora kwa wananchi na hasa masikini.
"Mnafanya kazi nzuri lakini nataka nisiwapake mafuta maana haitawasaidia nawaeleza ukweli kuna malalamiko makubwa, Hali inayosababishwa ninyi muonekane kama taasisi ya kutoa tunzo na kushindwa kushughulikia na kero hizo,"Amesema Naibu Waziri Aweso

Aidha amebainisha kuwa, zipo mamlaka ambazo ni vinara kwa kuwabambikia na kuwapandishia wananchi bei za maji kiholela, akiwataka EWURA kuhakikisha wanafikisha ripoti ya mamlaka za aina hiyo wizarani ili ziweze kuchukuliwa hatua stahiki maana wizara ndio yenye kauli ya mwisho.

Pia Aweso amesema kuwa changamoto kubwa ni elimu, EWURA hawajafanya kazi ya kutoa elimu kwa watumiaji wa maji, juu ya wajibu na haki yao pia kwa mtoa huduma Jambo ambalo litazaidia kuondoa malalamiko tofauti na hivi sasa ambapo wananchi wanapata haki ya kutumiwa Ankara kwa njia ya simu bila ushirikishwaji.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Maji na Usafi wa Mazingira, Titus Safari, amesema kuwa EWURA, imefanikiwa kutoa jumla ya leseni 119 katika kipindi cha Juni 2019.

Safari amesema kuwa EWURA imekuwa ikifanya ukaguzi kwa mamalaka za maji nchini zisizopungua 50, na kutoa maelekezo ya kuboresha na kuongeza ufanisi katika kutoa huduma Bora kwa wananchi.
Share:

CCM UBUNGO YAMPONGEZA DC MAKORI KWA UTENDAJI


 Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makori, (kushoto) akiwasilisha taarifa yake mbele ya Kamati ya Siasa Wilaya ya Ubungo, katikati ni Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya  ya Ubungo, Lucas Mgonja pamoja na Katibu wa wilaya hiyo, Chifu Silvester Yaredi

Wajumbe wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Ubungo, wakijadili taarifa ya utendaji ya Mkuu wa Wilaya

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM
 
KAMATI ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Ubungo, chini ya mwenyekiti wake Lucas Mgonja, imempongeza Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makori kwa utendaji wake ikiwamo vita dhidi ya ugonjwa wa corona wilayani humo.

Taarifa ilitolewa leo na Katibu wa Siasa ya Uenezi, Wilaya ya Ubungo, Mbaruku Masudi, imeeleza kuwa katika kikao hicho pamoja na mambo kilipokea taarifa ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makori  ikiwamo hali ya ugonjwa wa corona, ujenzi wa vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo kwa shule za msingi na sekondari wilayani Ubungo.


“Jana tarehe 6/05/2020  Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Ubungo ilikuwa na kikao chake cha kwanza cha kawaida kwa mwaka 2020.

“Katika Kikao hicho pamoja na mambo mengine kilipokea taarifa kutoka kwa Kamisaa wa chama Mkuu wa Wilaya Kisare Makori ikiwamo taarifa ya hali ya ugonjwa wa corona katika wilaya yetu (Ubungo) na jitihada zinazofanyika.

“Ujenzi wa vyumba vya madarasa, ofisi za walimu, matundu ya vyoo na ununuzi wa viti, meza na madawati. Pia kikao kilijadili hali ya uharibifu wa miundombinu ya barabara nahatua zilizochukuliwa hasa katika kipindi hicho cha mvua,” amesema Mbaruku

Katibu huyo Mwenezi wa Wilaya ya Ubungo, amesema kuwa pamoja na hali hiyo pia walipokea taarifa ya kutoka kwa DC Makori kuhusu kupatikana kwa eneo la ujenzi wa mahakama ya wilaya, polisi, Zimamoto na Uokoaji pamoja na ujenzi wa ofisi ya Katibu Tarafa Kibamba eneo lenye ukubwa wa takribani ekari 11.9.

“Pia Kamati ya Siasa ya Wilaya chini ya Mwenyekiti Mgonja ilipokea taarifa kuhusu suala la bei elekezi ya sukari na hatua zilizochukuliwa,” amesema

Kutokana na hali hiyo amesema kuwa CCM Wilaya ya Ubungo, kimeipongeza Serikali ngazi ya wilaya na kuishauri kuongeza jitihada katika kutoa elimu kuhusu kingi dhidi ya ugonjwa wa corona ikiwamo kujilinda na janga hilo.

Pamoja na hali hiyo Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ubungo, Lucas Mgonja, alitoa wito kwa wana CCM kuendelea kushirikiana na Serikali katika kipindi hiki ili kuhakikisha maelekezo yote muhimu yanatolewa yanazingatiwa.
Share:

Trump atumia veto kuukataa muswada wa Kongresi uliompunguzia mamlaka ya kuanzisha vita dhidi ya Iran

Rais Donald Trump wa Marekani ametumia mamlaka yake ya veto kuukataa muswada uliopitishwa na Kongresi, ambao umetaka mamlaka aliyopewa ya kuchukua hatua ya kijeshi dhidi ya Iran yapunguzwe.

Kufuatia hatua hiyo ya Trump, muswada huo sasa unahitaji theluthi mbili za kura za uungaji mkono za bunge hilo la Marekani ili uweze kuwa sheria moja kwa moja bila kuhitaji kusainiwa na rais wa nchi hiyo.

Tarehe 14 ya mwezi uliopita wa Aprili, Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani, Nancy Pelosi alisaini azimio la kupunguza mamlaka ya rais wa nchi hiyo ya kuanzisha vita dhidi ya Iran ambalo lilipitishwa na baraza hilo mwezi Machi.

Vitisho vya kuanzisha vita dhidi ya Iran ambavyo Rais wa Marekani Donald Trump alivitoa baada ya mauaji ya Kamanda wa Jeshi la Iran,  Qassem Soleimani na watu alioandamana nao yaliyofanywa na jeshi  la Marekani, vilizidi kulitia wasiwasi bunge la nchi hiyo na kuwafanya wabunge wa chama cha Democrat wachukue hatua ili kupunguza mamlaka ya Trump yanayohusiana na kuanzisha vita dhidi ya Iran.

-Parstoday


Share:

Trump Aendelea Kuishambulia China Kuhusu Virusi Vya Cona......Waliofariki Kwa Virusi Hivyo Marekani Wafika 74,809

Kwa mara nyingine rais wa Marekani Donald Trump ameishambulia China kwa jinsi ilivyoshughulikia mlipuko wa virusi vya corona huku akisema janga hilo limekuwa na madhara makubwa kwa Marekani.

Rais Trump amewaambia waandishi habari mjini Washington kuwa ugonjwa wa COVID-19 umeiathrii Marekani  kwa kiwango kikubwa kuliko mashambulizi ya mabomu dhidi ya kambi ya kijeshi ya Pearl Harbor ya mwaka 1941 au tukio la kigaidi la Septemba 11.

Hayo ni moja ya matukio makubwa kabisa na yaliyosababisha athari pana katika historia ya Marekani.

Mashambulizi ya Japan kwenye kambi ya Pearl Harbor iliyokuwepo Hawaii  yaliilazimisha Marekani kuingia katika vita kuu ya pili ya dunia huku mkasa wa Septemba 11 uliwauwa wamarekani zaidi ya 3,000 na kuisukuma Washington kuanzisha operesheni dhidi ya ugaidi nchini Iraq, Afghanistan na kwingineno.

Trump ameilaumu China akisema virusi vya corona visingesababisha athari kubwa iwapo Beijing ingefanikiwa kuvidhibiti kikamilifu vilipozuka mwishoni mwa mwaka uliopita.

Huo ni mfululizo wa lawama za Marekani kwa China kuhusu virusi vya corona na katika siku za karibuni rais Trump na viongozi wake waandamizi wamesema wana ushahidi kuwa virusi vya corona vilizuka kutoka maabara moja mjini Wuhan nchini China.

Madai hayo yamepingwa vikali na China na wanasayansi bado wanaamini virusi hivyo vialinzia kwa wanyama kabla ya kuingia kwa binadamu hususan kupitia soko la nyamapori la mjini Wuhan.

Hadi sasa zaidi ya watu 74,809 wamekufa nchini Marekani kutokana na ugonjwa wa COVID-19 na mkuu wa zamani wa taasisi ya kuzuia magonjwa nchini humo amebashiri idadi ya vifo inaweza kufikia 100,000 mwishoni mwa mwezi Mei.


Share:

Mafuriko Yaua Watu 194 Nchini Kenya

Mvua kubwa zilizonyesha nchini Kenya zimeua  watu 194, kwa mujibu wa maafisa wakinukuliwa na vyombo vya habari nchini humo. 

Kwa mujibu wa  gazeti la kila siku la Daily Nation, watu 194 wamefariki dunia kote nchini kutokana na mvua kubwa zinazonyesha na kusababisha mafuriko.

Mamlaka nchini Kenya imewataka watu wanaoishi katika maeneo yanayokumbwa na mafuriko, kama vile kando ya mito, kuondoka haraka maeneo hayo.

Gazeti la Daily Nation limemnukuu  Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Fred Matiangi akisema kwamba viongozi wako tayari kuwatoa  "kwa nguvu" watu walio katika hatari .

"Hatuna chaguo jingine. Tutahamisha watu kwa nguvu, hata ikiwa tutawasafirisha wenyewe kwa malori, tutafanya hivyo," afisa mmoja ameliambia Gazeti la kila siku la Standard Digital.

Kwa wale ambao hawajui wapi pa kwenda, mamlaka imetenga shule zilizofungwa kwa sababu ya marufuku ya watu kutotembea kutokana na janga la Corona. Shule hizi zitatumiwa kama hifadhi kwa muda kwa familia zilizohamishwa.

Mamlaka pia inasema serikali itatoa msaada wa chakula, maji na fedha kupitia simu kwa familia zilizohamishwa.


Share:

Spika Ndugai Aigomea Barua Ya CHADEMA ya kutomtambua Cecili Mwambe kama Mbunge

Spika Job Ndugai  jana alisoma barua ya Katibu wa Chadema, John Mnyika, iliyotaka bunge kutomtambua Cecili Mwambe kama Mbunge na kumlipa stahiki zake.

“Barua yenyewe ni fupi ngoja niwasomee, anasema Ceceli Mwambe, alikuwa mbunge wa jimbo la Ndanda aliyedhaminiwa na Chadema na Februari mwaka huu alitangaza kupitia vyombo vya habari amehama chama hicho,”alisema na kuongeza:

“Kwa mujibu wa ibara ya 7(f) ya Katiba amekoma kuwa mbunge na ameacha kiti chake katika bunge, kwahiyo bunge lisiendelee kumpatia stahiki zozote.”

Spika alisema anamshangaa Mnyika kwa kuwa maneno anayosema alipaswa aambatanishe na barua ya Mwambe inayothibitisha anayosema Mnyika na hajafanya hivyo.

“Pili sina barua ya Mwambe kusema kaacha ubunge kwa hiyari yake mwenyewe, na kama ni chama hiki kimechukua hatua sina viambatanisho vinavyoonyesha vikao halali vilivyofanya maamuzi haya, kwahiyo hii barua haina maana, haina mantiki,”alisema.

“Nawaambia wabunge wote ikiwamo wa Chadema mnaotishwatishwa huko kuwa mnaye Spika imara atawalinda mwanzo mwisho, habari ya ukandamizaji na ubabaishaji hauna nafasi, fanyeni kazi zenu kwa kujiamini, mmeaminiwa na wananchi,”amesisitiza


Share:

Spika Ndugai Awataka CHADEMA Wajiandae Kulipa gharama za kesi iliyofunguliwa na Tundu Lissu

Spika wa Bunge ,Job Ndugai amekitaka Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) kujiandaa kulipa gharama za kesi iliyofunguliwa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho,Tundu Lissu.

Spika Ndugai amesema amepewa nakala ya hukumu kutoka Mahakama Kuu iliyotupilia mbali rufaa yake namba 42 ya mwaka 2019 iliyowashitaki yeye (Spika ) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhusu ubunge wa Singida Mashariki.

“Nimepata nakala ya hukumu Spika na Mwanasheria Mkuu wa Serikali walikuwa wameshitakiwa na bwana Tundu Lissu katika shauri la Mahakama Kuu namba 42 la mwaka 2019 ya kwamba Mahakama imetupilia mbali madai hayo tena kwa gharama kwa hio wajiandae kulipa ” amesema Spika Ndugai

Lissu alifungua kesi hiyo akipinga kuvuliwa ubunge wake wa Singida Mashariki ambalo kwa sasa linaongozwa na Miraji Mtaturu kutoka Chama cha Mapinduzi.


Share:

Video Mpya : MAMA USHAURI 'FULL MELODY CLASSIC' - CORONA


Msanii Maarufu wa Nyimbo za Asili Mama Ushauri ' Full Melody Classic' kutoka Tinde Shinyanga anakualika tazama video ya wimbo wake mpya unaitwa Corona...
Tazama hapa chini

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMIS MEI 7,2020




























Share:

Wimbo Mpya : JANE MBESHI - CORONA


Msanii wa Nyimbo za Asili Jane Mbeshi ameachia wimbo mpya unaitwa Corona..
Usikilize hapa chini

Share:

Wednesday, 6 May 2020

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU RATIBA YA MKUTANO WA KUMI NA TISA WA BUNGE LA TANZANIA





Share:

SANAMU LA MWALIMU NYERERE KUJENGWA MAKAO MAKUU YA AU,ADDIS ABABA

Na Shamimu Nyaki – WHUSM

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inaratibu ujenzi wa  Sanamu ya Mwalimu  Julius Kamabarage Nyerere katika viwanja vya jengo la Amani na Ulinzi la Julius Nyerere lililopo katika Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) Jijini Addis Ababa, Ethiopia.

Akizungumza wakati wa uwasilishaji wa Hutoba ya Makadirio ya Bajeti kwa mwaka 2020/2021 Bungeni Jijini Dodoma, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa ujenzi wa sanamu hiyo ni utekelezaji wa Azimio la Mkutano wa 35 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika Jijini Harare, Zimbabwe mwaka 2015.

 “Ujenzi wa Sanamu ya Mwalimu Julius Nyerere katika Umoja wa Afrika (AU) ni makubaliano ya mkutano wa wakuu wa nchi wa SADC ambao walikuabaliana kuwa ujenzi huo lengo lake ni kutambua na kuenzi mchango wa waanzilishi wa SADC katika kulikomboa Bara la Afrika” alisema Dkt. Mwakyembe.

Dkt. Mwakyembe ameongeza kuwa ujenzi wa Sanamu hiyo utatumia malighafi ya Shaba nyeusi (bronze statue) ambapo ameeleza kuwa Kamati ya Kitaifa ya Uratibu na Kamati ya Ujenzi wa Sanamu za Kuwaenzi Waasisi wa Taifa kama inavyotakiwa katika sheria ya Kuwaenzi Waasisi wa Taifa ya mwaka 2004 zimeshaundwa na kuanza kazi tangu 2018.

Kwa upande wake Meneja Mradi wa mradi huo Dkt. Emmanuel Ishengoma ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi  wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa katika Wizara ya Habari, Utaaduni, Sanaa na Michezo amesema kuwa hatua za awali za ujenzi wa Sanamu hiyo tayari zimeanza na mradi unatekelezwa na Kampuni ya SAMCRO ya nchini Afrika Kusini chini ya usimamizi wa SADC na Tanzania na utagharimu takriban Dola za Marekani 267,992.60 ambazo ni sawa na takriban Shilingi 615,000,000 ambazo zitatolewa na SADC na gharama za usimamizi kutolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

Dkt. Ishengoma ameongeza kuwa mradi huo unatarajiwa kukamilika mwezi Oktoba mwaka huu ambapo Sehemu kubwa ya kazi hiyo itafanyika nchini Afrika Kusini na ikiishakamilika na kuridhiwa na Tanzania pamoja na SADC itasafirishwa na kusimikwa katika Makao Makuu ya AU huko Addis Ababa Ethiopia. 

Ujenzi wa Sanamu hiyo umetokana na wazo alilolitoa Rais wa zamani wa Zimbabwe Hayati Robert Mugabe katika Mkutano wa 35 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC kuhusu mkakati wa kuwaenzi viongozi waanzilishi wa SADC ambao walishiriki katika kulikomboa Bara la Afrika.

….MWISHO…





Share:

KAMPUNI YA JAMBO YAKANUSHA TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI LINALOSAMBAZWA MTANDAONI




Share:

Breaking : MBUNGE WA KISHAPU AKAMATWA KWA TUHUMA ZA KUKUTWA NA SILAHA 10 NA NYAMA 'UWINDAJI HARAMU'


Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga linamshikilia Mbunge wa Jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Suleiman Masoud Suleiman maarufu Suleiman Nchambi (CCM) kwa tuhuma za kupatikana na silaha 10, risasi 536 na nyama zinazodhaniwa kuwa ni za wanyawapori kinyume cha sheria.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Jumatano Mei 6,2020, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba amesema tukio hilo limetokea Mei 3,2020 majira ya saa sita kasoro usiku katika mtaa wa Lubaga kata ya Lubaga Manispaa ya Shinyanga. 

“Mei 3,2020 majira ya sita kasoro usiku Kikosi kazi cha askari wa upelelezi kikiongozwa na Kaimu Mkuu wa upelelezi wa Makosa ya Jinai mkoa wa Shinyanga SP Davis Msangi kwa kushirikiana na Afisa wa Wanyamapori mkoa wa Shinyanga Perfect Mbwambo walifanya upekuzi kwenye makazi ya Mbunge wa Jimbo la Kishapu baada ya kupata taarifa za kiintelejensia kuwa Mheshimiwa huyo alikuwa akifanya uwindaji haramu kwenye eneo la Negezi wilayani Kishapu akiwa na gari yenye namba za ujasili T760 DSD Nissan Hard Body”,ameeleza Kamanda Magiligimba. 

“Katika upekuzi huo walifanikiwa kukamata nyama iliyodhaniwa kuwa ni wanyamapori yenye uzito wa kilogramu 35 zikiwa zimehifadhiwa kwenye jokofu lililokuwa jikoni,jingine sehemu ya mazoezi na nyama nyingine ilikutwa kwenye gari hilo likiwa limeegeshwa nyumbani kwake ndani ya uzio wa nyumba hiyo”,amesema Kamanda Magiligimba. 

“Katika gari hilo kulikutwa silaha moja aina ya shortgunWakati askari hao wakiendelea na upekuzi ndani ya chumba chake cha kulala zilipatikana silaha zingine za aina mbalimbali na kufanya jumla ya silaha zilizokamatwa kuwa 16 ambazo ni Airgun 3, Shortgun 3,Rifle 8, Pistol 1 na Mark IV 1 pamoja na risasi 536 zikiwa kwenye kabati la nguo",anaeleza Kamanda. 

“Baada ya uchunguzi wa awali iligundulika kuwa silaha 10 ambazo ni Airgun 2, Rifle 5, Shortgun 2 na Mark IV 1 kati ya 16 anazimiliki isivyo halali”,ameeleza Kamanda Magiligimba. 

Kamanda Magiligimba amesema nyama hizo zimepelekwa maabara ya mkemia mkuu wa Serikali kwa uchunguzi zaidi na gari husika limekamatwa. 

“Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika. Natoa onyo kali kwa yeyote atakayejihusisha na vitendo vya kumiliki silaha isivyo kihalali hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake”,amesema Kamanda Magiligimba.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu kukamatwa kwa Mbunge wa Jimbo la Kishapu Suleiman Masoud Suleiman
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha kwa waandishi wa habari silaha alizokamatwa nazo mbunge wa Jimbo la Kishapu Suleiman Masoud Suleiman
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha kwa waandishi wa habari silaha alizokamatwa nazo mbunge wa Jimbo la Kishapu Suleiman Masoud Suleiman
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha kwa waandishi wa habari risasi alizokamatwa nazo mbunge wa Jimbo la Kishapu Suleiman Masoud Suleiman


Share:

SSA – Logistics Officer for COVID-19 (2 Posts)  at WHO Tanzania, May 2020

SSA – Logistics Officer for COVID-19 (2 Posts) RATIONALE Purpose of the SSA: Background The United Republic of Tanzania is one of the countries experiencing increased COVID-19 transmission. To date, more than 16 regions in the country are reporting cases. Most of the regions have designated/repurposed isolation and treatment facilities ready to receive COVID-19 patients. WHO is providing financial… Read More »

The post SSA – Logistics Officer for COVID-19 (2 Posts)  at WHO Tanzania, May 2020 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger