Thursday, 9 January 2020

Ijue Sayansi ya Kusimama na Kusinyaa kwa Maumbile ya Kiume ( Sayansi ya Nguvu za Kiume)


Ukosefu  na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume, ni tatizo linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume duniani.

Tatizo  la  ukosefu/upungufu  wa  nguvu  za  kiume ni  nini  ?
Ukosefu  ama  upungufu  wa  nguvu za  kiume  ni  ile  hali  ya  mwanaume  kutokuwa  na  uwezo  wa kufanya  tendo  la  ndoa  kwa  ukamilifu


Hatua  mbili  Muhimu 
Ili  mwanaume   aweze  kufanya  tendo  la  ndoa  na  andelee  kufanya  tendo  la  ndoa, ni  lazima  maumbile yake ya kiume yapitie  hatua  kuu  mbili  kama  ifuatavyo :

Hatua  ya  kwanza, ni  lazima  yaweze  kusimama  barabara  na  kuwa  magumu  kama  msumari.

Na  hatua  ya  pili  ni  lazima, yaendelee  kusimama  kwa  muda  mrefu  wakati  wa  tendo  la  ndoa.  Hatua  zote  mbili  zinapo  kamilika, ndipo  tunapo  pata  kitu  kinaitwa  STRONGER  AND  LONGER  ERECTION

Endelea na Makala hii kwa <<Kubofya Hapa>.


Share:

Prof. Kabudi akutana na kufanya mazungumzo na mwakilishi wa UNICEF

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF) nchini Tanzania, Bi. Shalini Bahuguna katika ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Waziri Kabudi amemweleza Bi. Shalini Bahuguna kuwa UNICEF imekuwa na mchango mkubwa sana kwa kuiunga mkono Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kukuza, kulinda na kutimiza haki za watoto.

“Kwa ujumla UNICEF imekuwa ikisaidia Tanzania kufanikisha agenda zake za maendeleo endelevu ya kulinda, kukuza na kutunza haki za watoto…..na tunaamini watoto hawa ni taifa la kesho”. Amesema Prof. Kabudi.

Waziri Kabudi amemueleza Bi. Bahuguna kuwa tangu mwaka 2016 Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na UNICEF, imefanikiwa kuboresha sekta za elimu na afya ikiwa ni pamoja na kuboresha mazingira ya upatikanaji wa huduma bora za kijamii, kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi na kuboresha huduma za maji katika mikoa mbalimbali ikiwemo, Dar es Salaam, Mbeya, Iringa, Kigoma, Njombe na Songwe.

Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF) nchini, Bi. Bahuguna amesema kuwa UNICEF itaendelea kushirikiana na Serikali ili kuhakikisha kuwa Tanzania inaendelea
kulinda haki za watoto.

“Haki za watoto katika taifa ni jambo muhimu sana, hivyo UNICEF itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania kuhakikisha kuwa haki za watoto zinalindwa pamoja na kupatiwa mahitaji muhimu”. Amesema Bi. Bahuguna.


Share:

Waziri Mhagama Aridhishwa Na Hatua Za Ujenzi Wa Jengo La NEC Dodoma

NA.MWANDISHI WETU
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama ametembelea na kukagua hatua ya ujenzi wa jengo la Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi zilizopo eneo la Njedenwa Jijini Dodoma na kusema ameridhishwa na hatua iliyofikiwa.

Alikagua mradi huo, Januari 07, 2020 ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Mhe. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliyoyatoa Novemba 18, 2019 alipotembelea na kukagua mradi huo na kutoridhishwa na kasi ya ujenzi na kutoa maagizo hayo baada ya TBA kusimamisha zoezi la ujenzi kwa ongezeko la gharama za  kutoka bilioni 13 hadi bilioni  32 na hivyo kumtaka Waziri Mhagama kufuatilia.

Ziara ya Waziri Mhagama imebaini maendeleo mazuri ya ujenzi na kufikia hatua ya asilimia 75 baada ya Tume hiyo kuingia mkataba SUMA JKT kuwapongeza wakandarasi kwa hatua hiyo wanayoendelea nayo.

“Kwa kipindi chote ambacho SUMA JKT imeendeela na kazi ya ujenzi wa jengo hili hali inaridhisha na ni vyema kuhakikisha mnaendana na kasi inayotakiwa kwa kuzingatia gharama zilizokubalika za bilioni 16,”Alisistiza Waziri Mhagama

Alieleza kuwa ujenzi wa majengo ya Serikali ni moja ya hatua za kuhakikisha zoezi la kuhamisha watumishi Dodoma linafanikiwa kwa kuendelea kuweka miundombinu rafiki ya ofisi zao.

“Mpaka sasa tayari watumishi wapatao 14868 wameshahamia hapa Dodoma hivyo tutaendelea kuandaa mazingira ikiwemo ujenzi wa ofisi hizo kwa kuzingatia kazi ya Uratibu huo ipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu,”alisema Mhagama

Alifafanua kuwa, kukamilika kwa jengo hilo kutasaidia kuhakikisha watumishi wa ofisi hiyo wanatoa huduma vizuri kwa kuzingatia mwaka 2020 ni mwaka wa uchaguzi mkuu ambapo itasadia utendaji wa kazi.

Waziri Mhagama ameendelea kueleza kuwa   , miongoni mwa majukumu ya Ofisi yake ni kuhakikisha inaratibu shughuli zote za kuhamisha watumishi wa Serikali na kuweka mazingira mazuri ya ofisi zao ili kuendelea kuitumikia nchi kwa weledi na kujiletea maendeleo yao kwa kutoa wa huduma bora zinazostahili.

Kwa upande wake mmoja wa wasimamizi wa ujenzi wa majengo hayo Mhandisi Michael Mussa alieleza kuwa, wataendelea kufanya kazi kwa viwango vinavyotakiwa ili kuwa na majengo yenye ubora kwa kuzingatia gharama zilizofikiwa kwenye mkataba wa ujenzi huo.

“Tumefarijika kwa ujio wa Mhe. Waziri na tunaahidi tutajenga kwa kipindi kilichopangwa kwa kuzingatia gharama zilizopo kwenye mkataba wa ujenzi huu,”alieleza Mhandisi Michael.

=MWISHO=


Share:

RPC ataja chanzo mlipuko wa moto Kigamboni

Kamanda wa Polisi Temeke, Amon Kakwale, amesema chanzo cha moto uliotokea usiku wa kuamkia leo katika matanki ya mafuta ya kampuni ya Lake Oil, eneo la Kigamboni, umesababishwa na hitilafu ya mota inayosukuma mafuta kutoka chini na kupandisha juu, iliyopelekea cheche na kuleta mlipuko.

Kamanda Kakwale amesema licha ya kufanikiwa kuuzima moto huo, Askari mmoja wa Jeshi la Zimamoto alipata mshituko baada ya kuingia kwenye chemba moto ulikoanzia na kuuzima.

"Mota ilipata hitilafu za kiufundi ambayo ilizalisha cheche za moto kutoka kwenye chemba ndogo ya chini, madhara yaliyotokea ni mwenzetu wa uokoaji mmoja, moshi ulimuingia kwenye kinywa na kupata mshituko kidogo" amesema Kamanda Kakwale.

Aidha Kamanda Kakwale ameongeza kuwa hadi sasa bado uongozi wa kampuni ya mafuta ya Lake Oil, haijawapelekea ripoti kamili inayoonesha ni athari kiasi gani imetokea.


Share:

Maafisa Tarafa Nchini Watakiwa Kushiriki Vikao Vya Kamati Za Kudumu Na Baraza La Madiwani Ili Kusimamia Vyema Shughuli Za Maendeleo

Na Happiness Shayo, Iramba-Singida
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) amewataka Maafisa Tarafa nchini kushiriki vikao vya Kamati za Kudumu na Baraza la Madiwani ili kurahisisha utendaji kazi hasa katika usimamizi wa  shughuli za maendeleo katika maeneo yao ya kazi.

Agizo hilo amelitoa wakati wa kikao kazi na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji, kabla ya kutembelea  wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika halmashauri hiyo.

“Kwa mujibu wa Mwongozo wa Uwajibikaji wa Makatibu Tarafa katika Wilaya na Halmashauri za Serikali za Mitaa wa mwaka 2003 ni haki ya msingi kwa Afisa Tarafa kuhudhuria vikao vya Kamati za Kudumu na Baraza la Madiwani vya Halmashauri ili kutoa ushauri  pamoja na taarifa za utekelezaji wa shughuli zilizofanyika katika eneo lake” Dkt. Mwanjelwa amefafanua.

Dkt. Mwanjelwa amesema kuwa Maafisa Tarafa wasipopewa nafasi za kushiriki katika vikao vya Kamati za Kudumu na Baraza la Madiwani, hoja za msingi za kimaendeleo hazitawasilishwa hivyo maendeleo yatakwamishwa katika halmashauri wanazozihudumia.

Dkt. Mwanjelwa ameweka bayana kuwa ni muhimu Maafisa Tarafa, Makatibu Tawala na Wakurugenzi wa Halmashauri wakafanya kazi kwa kushirikiana ili kuongeza ufanisi katika shughuli za maendeleo.

Aidha, Mhe. Dkt. Mwanjelwa amewataka Watendaji wa Halmashauri kujenga utaratibu wa kufanya vikao na watumishi ili kusikiliza kero zao na kuzitatua.

“Hakikisheni mnatenga muda wa kuongea na Watumishi walio chini yenu ili kuwaelimisha kuhusu nyaraka mbalimbali za kiutumishi pamoja na kusikiliza kero na maoni yao na kuyafanyia kazi” Dkt. Mwanjelwa amesisitiza.

Mhe.Dkt. Mwanjelwa yupo katika ziara ya kikazi Mkoani Singida kwa lengo la kukagua utekelezaji wa shughuli za TASAF


Share:

Iran Yagoma Kuipa Marekani "Black Box" Ya Ndege ya Ukraine Iliyoanguka Jana

Iran imesema kuwa haitakabidhi kisanduku cha kunakili safari ya ndege ama ''Black box'' ya ndege ya Ukraine iliyopata ajali na kuua watu 176, kwa kiwanda kilichotengeneza ndege hiyo au kwa Marekani.

Ndege hiyo ya Ukraine aina ya Boeing 737-800 ilianguka muda mfupi baada ya kuanza safari yake kutokea uwanja wa ndege wa Tehran, na hakuna mtu aliyenusurika katika ajali hiyo.

Kwa mujibu wa sheria za anga za kimataifa , Iran ina haki ya kufanya uchunguzi kuhusu ajali hiyo.

Lakini watengenezaji wa ndege hiyo kwa ushirikiano na wataalamu kutoka nchi kadhaa wanaweza kuchunguza kisanduku hicho.

Ajali hiyo imetokea wakati ambapo kuna mvutano mkubwa kati ya Marekani na Iran, muda mfupi baada ya Iran kushambulia kwa makombora kambi mbili za kijeshi za Marekani zilizopo Iraq.

Aidha hakuna ushahidi kuwa matukio haya mawili yanahusiana na kuanguka kwa ndege hiyo.

Kwa kawaida, bodi ya Marekani ya usafirishaji salama ina jukumu la kuchunguza masuala yeyote ya kimataifa yanayohusisha ndege aina ya Boeing iliyotengenezwa Marekani kwa idhini ya sheria za nchi husika.

Kiongozi wa shirika la anga Iran Ali Abedzadeh alinukuliwa katika vyombo vya habari nchini humo akisema:"Hatutawapa kisanduku cheusi kampuni iliyotengeneza ndege hiyo au Wamarekani"

"Tukio hilo litachunguzwa na shirika la anga la Iran lakini Ukraine itaruhusiwa kuwepo katika uchunguzi huo" 


Share:

Taarifa Kwa Umma: Uwepo Wa Matapeli Katika Utoaji Wa Huduma Za Fedha.




Share:

Marekani Yasema Iko Tayari Kufanya Mazungumzo na Iran Bila Masharti Yoyote

Serikali ya Marekani imetangaza kuwa, iko tayari kufanya mazungumzo na Iran bila masharti yoyote.

Shirika la Habari la Reuters limeripoti kuwa,  balozi na mwakilishi wa kudumu wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Kelly Craft  ametangaza katika umoja huo kwamba, nchi yake ipo tayari kuanza mazungumzo na Iran bila masharti yoyote.

Hayo yanajiri katika hali ambayo, Rais wa Marekani Donald akizungumza jana katika hotuba yake kuhusiana na mashambulio ya makombora ya Iran dhidi ya kambi za kijeshi za nchi hiyo nchini Iraq alidai kuwa, hakuna raia wa Iraq au Marekani aliyeuawa katika shambulio hilo japo kambi hizo ziliharibiwa kidogo. 

Trump alidai kwamba, Iran inaonekana kurudi nyuma, hatua ambayo ni nzuri kwa pande zote husika. Hata hivyo alisema kuwa, ataongeza vikwazo dhidi ya Iran.

Wakati Rais Trump akidai kwamba, hakuna mwanajeshi wa Marekani aliyejeruhiwa au kuuawa katika shambulio hilo, vyombo vya Iran jana vilisema kuwa Wanajeshi 80 wa Marekani  waliuawa japo havikutoa uthibitisho wowote


Share:

MVULANA WA MIAKA 10 AJITAHIRI KWA KISU AKIOGOPA KUCHEKWA NA WENZIE


Mvulana wa miaka 10 mkazi wa kijiji ya Itare nchini Kenya amejitahiri kwa kutumia kisu cha jikoni baada ya wazazi wake kushindwa kulipia gharama ya Ksh 1000/- ya kupewa huduma hiyo hospitali.

Mtoto huyo wa darasa la pili ameeleza chombo cha habari kimoja nchini humo kuwa alilazimika kufanya hivyo kwa kuhofia unyanyapaa atakaofanyiwa na wenzake ambao wao walifanyiwa toraha kipindi cha likizo ya mwezi Desemba.

Inaelezwa kuwa hali ya mtoto huyo kiafya sio nzuri tangu alipojifanyia kitendo hicho mwezi mmoja uliopita na awali alipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Kisii lakini wazazi wake walimrudisha nyumbani kwa kushindwa kumudu gharama za matibabu.

Mwanaharakati wilayani Kisii, Samwel Momanyi ameomba serikali iingilie kati na kumsaidia mtoto huyo kupata matibabu kwani anapata maumivu makali sana hususani akijisaidia haja ndogo.

Mvulana huyo ameshindwa kuanza masomo shule zilivyofunguliwa  siku ya Jumatatu Januari 6,2020 kutokana na afya yake kutoimarika.
Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi January 9





















Share:

Wednesday, 8 January 2020

Israel Yatoa Onyo Kama Itashambuliwa na Iran

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameonya kwamba nchi yake italipiza kisasi kwa yoyote atakayewashambulia, huku akirejelea matamshi yake ya kuiunga mkono hatua ya Marekani ya kumuua mkuu wa kikosi maalumu cha Iran Jenerali Qassemi Soleimani wiki iliyopita. 

Amesema mjini Jerusalem kwamba yoyote atakayewashambulia atakabiliwa na hatua kali ya kulipiza kisasi na kuongeza kuwa Israel inasimama kikamilifu na uamuzi wa rais wa Marekani Donald Trump na kuongeza kuwa anahitaji kupongezwa kwa kuchukua hatua hiyo kwa utaratibu, ujasiri na umadhubuti.


Share:

Iran Yasema Mashambulizi Ya Leo Dhidi Ya Marekani Ni Kama Makofi ya Uso Tu

Kiongozi mkuu wa  Iran, Ayatollah Ali Khamenei amesema hii leo kwamba shambulizi la makombora kwenye kambi za kijeshi zinazotumiwa na Marekani nchini Iraq ni kofi la uso kwa taifa hilo na  amesisitiza hatua hiyo ya kijeshi haitoshi. 

Ayatollah amelihutubia taifa masaa kadhaa baada ya kushambulia kambi hizo za kijeshi.

Shambulizi hili ni la kisasi dhidi ya mauaji ya jenerali wa kikosi maalumu cha Quds cha Iran, Qassemi Soleimani aliyeuliwa na Marekani mjini Baghdad Ijumaa iliyopita. 

Khamenei amesema uwepo usio halali wa Marekani kwenye ukanda huo unatakiwa kumalizwa akisema umesababisha vita, mgawanyiko na uharibifu. 

Waziri wa mambo ya nje wa Iran Mohamad Zarif amesema shambulizi hilo ni sawa na hatua za kujilinda huku rais wa halmashauri ya Ulaya Ursula von der Leyen akitoa mwito wa kufanyika makubaliano ya kidiplomasia.


Share:

Watoto 404 Wafanyiwa Ukatili Wa Kingono Iringa

Na Mwandishi Wetu Iringa
Mkoa wa Iringa kwa kipindi cha Januari mpaka Novemba 2019 umekuwa na matukio takribani 404 ya vitendo ya ukatili wa kingono kwa watoto ikiwa ni tatizo kubwa linalowakabili watoto katika malezi na makuzi yao nchini.

Hayo yamebainika mkoani Iringa wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Afya, Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile alipotembelea vikundi vya malezi kwa watoto katika kijiji cha Kising’a kilichopo Wilaya ya iirnga mkoani Iringa.

Akitoa taarifa hiyo Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Saida Mgeni amesema kuwa mkoa wa Iringa unakabiliwa na matatizo mbalimbali na umekuwa ukiongoza katika masuala mabalimbali yasiyofaaa katika jamii ikiwemo vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Ameongeza kuwa Serikali ya mkoa wa Iringa imejipanga katika kuhakikisha inapambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto mkoani humo kwa kuhakikisha inaratibu utoaji wa elimu kwa wananchi juu ya madhara ya vitendo hivyo kwa wanawake na watoto.

Akizungumza katika ziara hiyo Naibu Waziri wa Afya, Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amesema kuwa Serikali haijalala wala kufumbia macho suala la vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto bali inachukua hatua kali kwa wahusika wa vitendo hivyo wanaobainika.

Dkt. Ndugulile amezitaka Kamati za malezi ya mtoto mkoani Iringa na nchi nzima kuhakikisha wanatoa taarifa za vitendo vya kikatili dhidi ya wanawake na watoto kwa kuhakikisha hawawafichi watuhumiwa na hawamalizani kifamilia kesi za ukatil wa kijinsia.

Ameongeza kuwa ni jambo la aibu kwa Tanzania ya viwanda kuwa na vitendo vya kikatili kutokea katika jamii zetu kwani ni kikwazo kikubwa katika kuhakikisha jamii inajiletea maendeleo yao na taifa kwa ujumla.

“Mkiona wanajamii miongoni mwenu wanataka kumalizana katika kesi za vitendo vya ukatili wa kijinsia toeni taarifa ili tukomehse vitendo hivi visiendelee nchini” alisema Dkt. Ndugulile

Dkt. Ndugulile amewataka wazazi na walezi nchini kuhakikisha wanakaa na kuzungumza na watoto wao na sio kuwapiga na kuwapa adhabu zinatazosababisha kupata ukatili wa kisaikilojia ambao ni hatari kwa malezi na makuzi yao na kuhakikisha watoto hao wanapata haki zao za msingi zilizopo kisheria.


Share:

Nafasi 100 za Kazi CRDB Bank | Direct Sales Executive (DSE)

CRDB Bank PLC is looking for suitable people to fill vacant positions of Direct Sales Executive (DSE) – (1 year contract- 100 positions) in the Department of Retail Banking in different zones.

Job Purpose:

Translation and execution of retail sales agenda to ensure all set goals are met within agreed time. This is a sales target role based; in which the DSE is required to ensure door-to-door sales activities to meet the set sales target. The main agenda is to open new accounts, attract more deposits and promote usage.

==> BOFYA HAPA KUJUA ZAIDI


Share:

ELIMU JUU SEKTA YA MADINI INATAKIWA MOROGORO


 Waziri wa Madini Doto Biteko kushoto akizungumza kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga  Loata Sanare



Waziri wa Madini Doto Biteko katikati akizungumza, kushoto ni Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Sanare wakiwa kwenye kikao.


 Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akizungumza




Na Tito Mselem Dodoma


Waziri Biteko ameagiza uongozi wa Mkoawa Morogoro kwa kushirikiana na Wizara ya Madini kuandaa maonesho ya madini kwalengo la kuelimisha Umma kwa watu wa Morogoro na mikoa jirani juu yaSheria, Kanuni na fursa zilizopo katika Sekta ya Madini.

Hayo yamebainishwa leo January 08, 2020 na Waziri wa Madini Doto Biteko alipofanya kikao na MkuuwaMkoawa Morogoro, LoataSanare, kilichofanyika katika ukumbi wa WizarayaMadini, Mtumba Jijini Dodoma.

“Nichukue fursa hii kuwaelekeza wataalamu wote wa Wizara ya Madini na Taasisi zake kuhakikisha wanashirikiana naMkoa wa Morogoro kuzitangaza fursa zinazopatikana katika Sekta ya Madini Mkoani Morogoro kwa kutumia njia mbalimbali ikiwemo kuandaa maonesho yatakayopelekea kuelimika kwa wananchi wa Mkoa huo,” alisema Waziri Biteko.

Aidha, Waziri Biteko amesisitiza ushirikiano katika kusimamia Sekta ya Madini kati yaWizara na Mkoa wa Morogoro na kumpongeza Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Morogoro Emmanuel Shija kwa kazi nzuri anazozifanya katika ukusanyaji wa mapato ya serikali.

Waziri Biteko amesema maendeleo ya Sekta ya Madini katika Mkoa wa Morogoro yatatokana na wachimbaji wenyewe, hivyo Wizara na Mkoa inapaswa kuwalinda nakuwalea wachimbaji na wadau wote wa madini mkoanihumo.

Akizungumzia changamoto inayowakabili wananchi wa Morogoro Biteko alisema ni pamoja na uelewa mdogo walionao juu ya masuala yanayohusiana na Sekta ya Madini kuwa ni kikwazo katika kupelekea maendeleo Mkoani humo.

Kwa upande wake,Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, ameonesha kufurahishwa na kitendo cha Mkoa wa Morogoro kuonesha mafanikio makubwa katika makusanyo ya mapato ya serikali kutoka shilingi 811,714,294.12 kwa mwaka 2017/2018 mpaka kufikia 1,031,865,068.41 kwamwaka 2018/2019.

“Madini ya Ujenzi, Vito na Dhahabu tukiyasimamia vizuri hakika yatatuingizia fedha nyingi watu wa Morogoro, hivyo nikuombe Mkuu wa Mkoa ukalifanyie kazi hilo, pia sisi kama Wizara ya Madini tutashirikana na Mkoawa Morogoro kuhakikisha wawekezaji wanakuja kuwekeza katika Sekta ya Madini Mkoani Morogoro,”alisemaNyongo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Loata Sanare, amemuomba Waziri kupatiwa ushirikiano katika kuitangaza Morogoro kuwani Mkoa wa Madini na sio kilimo peke yake.

Pia Sanare, amesema, Mkoawa Morogoro una mpango wakufufua viwanda vya Ceramics vilivyokuwepo ili kuongeza matumizi ya madini ya viwandani yanayopatikana katika Mkoa huo kwa wingi na kuendeleza uhamasishaji wa uanzishwaji wa viwanda vipya vya Ceramics.

Wakatihuohuo, AfisaMadiniMkaziwaMkoawa Morogoro, Emmanuel Shija,amesema Mkoawa Morogoro una Jumlaya leseni 3082 za wachimbaji wa dogo kati yake ni leseni 250 tu ndizo zinafanya kazi ya uzalishaji, hivyo Ofisi ya Madini inaendelea na zoezi la kufuta leseni zote zenye makosa.

“Mwaka 2019 jumlayaleseni 223 zilifutwa na jumla ya hati za makosa kwa leseni 836 zimetolewa, leseni hizo ziko kwenye utaratibu wa kufutwa ndani ya mwaka huu wa fedha endapo wamiliki wa leseni hizo hawatarekebisha makosa yao kama Sheria inavyoelekeza,” alisemaShija.

Kikao hicho kilicho lenga kujadili changamoto na maendeleo ya Sekta ya Madini kwaMkoa wa Morogoro ikiwa ni pamoja na kuangalia fursa zilizopo katika Sekta ya Madini katika kuharakisha maendeleo ya mkoa huo.

Ambacho kilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Wizara ya Madini na Taasisi zilizo chini ya Wizara akiwepo Naibu Waziri waMadini, StanslausNyongo, Mtendaji Mkuu wa Tume ya Madini Prof. ShukraniManya, Mkurugenzi Taasisi ya Jiolojia na Utafiti Tanzania Dkt Musa Budeba, Kamishna wa Madini Mhandisi David Mulabwa, Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara ya Madini Edwin Egenge, Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Madini Augustine Ollal na wengine.
Share:

Nafasi za Kazi Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka-DART

Mtendaji  Mkuu  wa  Wakala  wa  Mabasi  Yaendayo  Haraka,  anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa watanzania wenye sifa na uwezo kujaza nafasi wazi mbili (2)kwa kazi ya Derevakama zilivyobainishwa katika tangazo hili.

1.0.DEREVA (2)
1.1.SIFA ZA MUOMBAJI.
I.Cheti cha Mtihani wa Kidatocha IV, 
II.Leseni ya daraja ”C1’’au “E” ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda wa mwaka mmoja bila kusababisha ajali,
III.mafunzo  ya  msingi  ya  uendeshaji  magari  (Basic  Driving  Course) yanayotolewa na Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) au chuo cha Usafirishaji (NIT). IV.Waombaji   wenye   Cheti   cha   Majaribio   ya   Ufundi   Daraja   la   II watafikiriwa kwanza.
 
1.2.MAJUKUMU YA KAZI.
II.Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari,
III.Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenyesafari za kikazi,
IV.Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari,
V.Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali,
VI.Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari,
VII.Kufanya usafi wa gari, na
VIII.Kufanya kazi nyingine kadri anavyoelekeza na Msimamizi wake

Kutuma Maombi <<BOFYA HAPA>>


Share:

USAFIRISHAJI WA MIZIGO KWA NJIA YA RELI WAREJEA MKOANI TANGA

 Meneja wa Shirika la Reli Kanda ya Kaskazini (TRC) Ramadhani Ebrahim Gombo akizungumza na waandishi wa habari Jijini Tanga kuhusu kurejea kwa treni ya mizigo
 MBUNGE wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajab akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea eneo la reli ambalo liliathirika kwa kusombwa na maji Muheza ambalo kwa sasa limekarabatiwa na kuanza kupitisha treni
 MBUNGE wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajab akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea eneo la reli ambalo liliathirika kwa kusombwa na maji Muheza ambalo kwa sasa limekarabatiwa na kuanza kupitisha treni

 MBUNGE wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajab katikati aliyevaa tisheti ya mistari nyeupe akiangalia ukarabati huo ukiwa unamalizika kuendelea eneo la Muheza ambapo kwa sasa Reli zimeanza kupita
 Mafundi wa shirika la Reli mkoa wa Tanga wakiendelea na ukarabati huo
  Greda likiendea na kazi eneo la reli Muheza kama lilivyokutwa
 Greda likiendea na kazi eneo la reli Muheza kama lilivyokutwa

HATIMAYE usafirishaji wa mizigo kwa njia ya reli kutoka mkoa wa Tanga kwenye mikoa ya Kanda ya Kaskazini umerejea kwenye hali yake ya kawaida baada ya kukwama kwa kipindi cha miezi mitatu


Hatua hiyo inatokana na daraja kubwa lililopo eneo la Muheza kusombwa na maji mwishoni mwa mwaka jana wakati wa mvua kubwa zilizokuwa zikinyesha hapa nchini na hivyo kuleta athari kubwa.

Hayo yalisemwa jana na Meneja wa Shirika la Reli Kanda ya Kaskazini (TRC) Ramadhani Ebrahim Gombo wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema usafiri huo umerejea baada ya kufanyia matengenezo makubwa kwenye eneo hilo.

Alisema kwamba baada ya daraja kubwa la reli lililopo eneo la Muheza kukatika lilishindwa kutumika na hivyo wafanyabiashara kushindwa kuitumia kwa ajili ya kusafirishia bidhaa zao na hivyo kusimama kwa muda.

“Daraja la Muheza lilisombwa na Maji Octoba 10 mwaka jana na ulazimika kuanza kunyia ukarabati kuanzia mwezi wa 11 tulianza kurekebisha kwa kuondoa maji eneo hilo kuwawezesha wananchi kuendelea na shughuli zao”Alisema

“Lakini baada ya hapo tulihamia maeneo mengine Korogwe,Mnyuzi, Gendagenda kwani maeneo mengi yaliathirika na tulivyomaliza maeneo hayo 23 Novemba 2019 ndipo tuliporudi hapa muheza mpaka Januari mwaka huu tulipomaliza daraja hilo na kwa sasa treni zinatembea na usafirishaji mizigo umerudi kwenye hali yake ya kawaida”Alisema

Alisema kwa sasa treni inaendelea vizuri na usafirishaji wa mizigo umerudi kwenye hali yake ya kawaida huku akielezwa kwamba wamepata hasara kubwa kwani treni za mizigo hazikufanya kazi ya kusafirisha mizigo na mzigo wa mingi wanategemea kutoka Bohari ya Mafuta mkoani Tanga (GBP) na Saruji kwenda mikoa ya Kilimanjaro, Dar na mikoa mingine Kanda ya Ziwa wamepata hasara kubwa kwa kusombwa daraja la muheza.

Hata hivyo Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu ambaye alitembelea eneo la reli wilayani Muheza ambalo lililikuwa limeathirika na mvua kubwa na kupelekea usafiri huo kusitishwa.

Alisema kwamba athari ambazo zimetokea kutokana na kusitishwa usafiri huo ni kubwa kwa sababu daraja hilo la reli na maeneo yote yalijaa maji na mawasiliana ya reli dar kwenda Tanga kukatika.

Aidha alisema lakini sasa shirika la reli wamefanya kazi nzuri sana kwa kipindi kifupi wamekuwa wakifanya kazi kwa usiku na mchana kuhakikisha inafanya kazi.

Mbunge huyo alisema kwamba kuanzia juzi wananchi wa Muheza wamejisikia furaha kubwa baada ya kuanza kuona reli inapita licha ya kupatikana kwa hasara kutokana na huduma hiyo kusitizwa kutokana na mvua kubwa zilizokuwa zikinyesha mwaka jana na kuleta athari hiyo.

“Kama juzi juzi mmesikia reli inapita kwenda Moshi lakini pia ilikuwa ipite na hapo Muheza kwenda Tanga lakini kutokana na tatizo hilo imeshindwa kufika huku lakini naamini serikali itaanzisha usafiri wa kuelekea mkoani Tanga kwa sasa baada ya matengenezo “Alisema
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger