Sunday, 5 January 2020

Marekani yajiandaa na shambulizi la kulipiza kisasi kutoka Iran... Wanajeshi Wengine 3500 Kutumwa Mashariki ya Kati

Marekani kwa sasa inajiandaa na shambulizi la kulipiza kisasi kutoka Iran baada ya shambulizi lake la anga kumuua kamanda mkuu wa Iran, hatua ambayo imetia wasiwasi nchi zote duniani na hata kutiliwa shaka na baadhi ya wabunge wa Marekani.

Shambulizi la anga la Marekani Alhamis lilimuua Meja Jenerali Qassem Soleiman, mkuu wa kikosi cha Quds, pamoja na kamanda wa wanamgambo wa Iraq, karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad, na kuchochea vitisho vikali vya kulipiza kisasi kutoka kwa Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei.

Ikijibu tishio hilo linalozidi kuongezeka dhidi ya wafanyakazi na vituo vya Marekani katika Mashariki ya Kati, wizara ya ulinzi ya Marekani imetoa taarifa ikisema itasambaza kikosi huko Kuwait kama hatua ya tahadhari na sahihi, bila kutaja idadi ya wanajeshi. 


Hata hivyo vyombo vya habari vya Marekani jana vilitangaza kuwa nchi hiyo itatuma zaidi ya askari 3,500 wikiendi hii. Na askari wengine wa ziada kutoka divisheni ya 82 ya askari wa parashuti watapelekwa Iraq, Kuwait na sehemu nyingine za kanda hiyo.


Share:

Mangula Atoa Onyo kwa Wanaokiuka Kanuni za Uchaguzi CCM 2020

Makamu mwenyekiti wa CCM Tanzania bara Philipo Mangula ametoa onyo na kuahidi kuanza kuwachukulia hatua kali za kimaadili kupitia kamati za ngazi tofauti za siasa ndani ya chama wanasiasa wote ambao wameanza kupita kwa wananchi na kutangaza nia ya kugombea nafasi mbalimbali jambo ambalo kinyume na kalenda ya chama.

Mangula ametoa katazo hilo katika kikao cha halmashauri kuu ya chama wilaya ya Wanging’ombe ambacho kimeketi kwa lengo la kupokea ripoti ya utekelezaji wa ilani ya Chama kwa mbunge na mkuu wa wilaya hiyo katika kipindi cha 2015 -2020 ambapo anasema kufanya hivyo kunakiuka misingi na maadili ya chama na kuathiri utendaji wa viongozi waliopo madarakani na kupiga marufuku kutoa zawadi ama msaada wa aina yeyote bila mawasiliano na mwakilishi.

Awali wakiwasilisha ripoti ya utekelezaji mbunge wa jimbo la Wanging’ombe mhandisi Gerson Lwenge na mkuu wa wilaya hiyo Comrade Ally Kassinge wamesema licha ya uchanga wa wilaya hiyo lakini katika kipindi cha miaka mitano wamefanya mabadiliko makubwa katika sekta ya elimu,umeme,viwanda ,miundombinu na uchukuzi na kuahidi kuendelea kuchapa kazi.

Nao baadhi ya wajumbe akiwemo Juma Nambaila na Paulina Samatta  wanakiri kuridhishwa na utendaji wa viongozi hao huku wakiwataka mwaka huu kuelekeza nguvu katika kusogeza nishati ya umeme na utatuzi wa migogoro ambao umekithiri katika wilaya hiyo.
 
Katika kikao hicho nae katibu wa siasa na uenezi wa chama hicho mkoa wa Njombe  Erasto Ngole anatumia fursa hiyo kuwataka wananchi kujitokeza kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura ambalo limeanza kufanyika tangu januari mosi na kuhitimishwa januari 7.


Share:

BENKI YA TPB YATOA ELIMU KWA WALIMU WASTAAFU WILAYANI KAHAMA



Benki ya TPB  imetoa elimu kwa walimu wastaafu wilayani kahama kuhusu maboresho ya huduma zao lakini namna gani mzee anapaswa kuwekeza na kuwa na matumizi bora ya pesheni yake.

Akizungumza katika mkutano huo Januari 4,2020  Meneja wa Benki ya TPB mkoa wa Shinyanga Jumanne Wagana
aliwapa wazee Elimu  ya BIMA ya Maisha ya Tsh 1000/=, Biashara ya akaunti ya Amana kwa muda maalumu inayokupa faida mpaka 12%,  jinsi ya kupata mitaji kupitia mikopo ya riba nafuu ya wastaafu, mikopo ya kilimo, mikopo ya biashara n.k.

 Katika mkutano huo ambao ulifadhiliwa na Benki ya TPB wastaafu mbalimbali walitoa shukrani zao za dhati kwa Benki ya Serikali ya TPB kwa kuwajali na kuwawezesha wafikie malengo yao ambayo walikuwa hawajakamilisha wakati wanastaafu. 

Naye Kaimu Meneja wa tawi la Kahama  Patrice Garani  akichangia amewaomba wazee wasiogope kukopa kwani mikopo ya TPB ina Bima.
Meneja wa TPB Mkoa wa Shinyanga Ndg Jumanne Wagana akitoa Elimu kwa Waalimu Wastaafu wilayani ya Kahama.
Walimu Wastaafu wakifuatilia kwa umakini Wawezeshaji kutoka Benki ya TPB wakitoa elimu ya fedha, mikopo na ujasiriamali.
Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili January 5















Share:

Saturday, 4 January 2020

Ajira Mpya Tanzania | Latest Jobs in Tanzania January 2020

Share:

Waziri Mkuu: Mradi Wa Hoteli Ni Muhimu Kwa Utalii

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema mradi wa ujenzi wa hoteli ya Golden Tulip Airport Zanzibar ni muhimu katika kuimarisha sekta ya utalii na huduma   za malazi kwa wageni wanaotumia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume.

Amesema mradi huo unakwenda sambamba na juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar za kuimarisha uwanja wake wa ndege ili kuongeza uwezo wake katika kutoa huduma bora kwa abiria na wafanyakazi wa mashirika ya ndege ya ndani na nje ya nchi.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumamosi, Januari 4, 2020), wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa hoteli hiyo. Miongoni mwa watakaonufaika na mradi huo ni pamoja na wasafiri wanaopita Zanzibar kwa ajili ya kuunganisha ndege na baadaye kuendelea na safari.

Waziri Mkuu ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa Hoteli ya Golden Tulip Airport Zanzibar inayojengwa katika eneo la uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya miaka 56 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yam waka 1964.

Ujenzi wa hoteli hiyo unatarajiwa kugharimu Dola za Marekani milioni 8.5. sawa na sh. bilioni 19.55. “Ama kwa hakika uwekezaji huu ni mkubwa na naamini wawekezaji hawa wengeliamua kuwekeza katika nchi nyingine yoyote, nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wangelipokelewa kwa mikono miwili.” 

“Hata hivyo, mazingira mazuri ya uwekezaji hapa Zanzibar na uzalendo alionao Mhe. Mohamed Raza, Mwenyekiti wa ‘Royal suites group of companies’ vilipelekea ushawishi mkubwa wa hoteli ya aina hii kujengwa hapa Zanzibar.”

Waziri Mkuu amesema kuwa “Nyote mtakubaliana nami kuwa viwanja vingi vya ndege vilivyopo kwenye ukanda huu wa Afrika Mashariki, havina hoteli kubwa na za kisasa zilizopo karibu na viwanja hivyo. Uamuzi wa kujenga mradi huu ni sahihi, kwani Zanzibar na Tanzania kwa ujumla ni mahali salama na wezeshi kwa biashara na uwekezaji.”

Amesema kwa upande mwingine, Serikali zinaendelea kuimarisha amani na utulivu, miundombinu wezeshi ya kiuchumi, huduma za fedha na mifumo ya kodi ili kuvutia uwekezaji. “Mambo haya ni muhimu sana katika kuvutia wawekezaji katika sekta mbalimbali kwa pande zote mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.”

Hivyo, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kutoa pongezi za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein kwa juhudi wanazoendelea kuzifanya za kushajiisha uwekezaji. “Tunawashukuru sana.”

Amesema kwa upande wa Zanzibar, katika kipindi hiki cha miaka tisa ya Awamu ya Saba, ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, jumla ya miradi ya uwekezaji 304 yenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 3.74 imeidhinishwa na mingine iko katika hatua mbalimbali za utekelezaji.

Utekelezwaji wa miradi hiyo, umetoa mchango mkubwa katika kukuza ajira, teknolojia, kuongeza mapato ya Serikali na kuimarisha ustawi wa Wananchi wetu. “Hivyo, nawapongeza wawekezaji wetu wote waliowekeza na wanaoendelea kuwekeza hapa nchini. Wawekezaji hawa wameonesha imani na upendo mkubwa kwetu, nasi tunaahidi kufanya nao kazi kwa ushirikiano makubwa.”

Kwa upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Mohammed Ramia amesema mradi huo ni muhimu kwa kuwa utakapokamilika utaenda kuongeza mapato ya Serikali.

Amesema hoteli hiyo ni ya kwanza kwa Zanzibar kwa sababu mbali ya kuwa na ukumbi wa watu mashuhuri (VIP Business Lounge) ambao wageni wake watakuwa na uwezo wa kukamilisha taratibu za abiria wa ndege (check in) na taratibu za uhamiaji moja kwa moja kutoka katika ukumbi huo.

Awali, Afisa Mtendaji Mkuu  wa Royal Group of Companies,  Bw. Hassan Mohammed Raza alisema ujenzi wa hoteli hiyo yenye vyumba 61, kumbi tatu za mikutano zenye uwezo uwezo wa kuchukua watu 600 ina hadhi ya nyota nne, ulianza februari 2019 na unatarajiwa kukamilika Septemba mwaka huu.

Alisema nembo ya Golden Tulip ni sehemu moja ya kampuni ya pili kwa ukubwa duniani kwa upande wa hoteli ukiwa chini ya mwavuli wa Louvre Hoteli ambayo inamilikiwa na Shanghai Municipal Council. Mtandao huo una hoteli zaidi ya 8,000 duniani, hivyo hoteli yao italazimika kufuata na kutimiza vigezo bora vya hoteli katika sekta ya hoteli duniani.

(mwisho)
IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU


Share:

Maelfu wakusanyika kwa Maombolezo ya Kamanda wa jeshi la Iran Qasem Soleimani

Maelfu ya waombolezaji wamekusanyika leo Jumamosi mjini Baghdad  kushiriki maandamano ya mazishi ya kamanda wa jeshi la Iran Qasem Soleimani, aliyeuawa katika shambulio la angani lililotekelezwa na Marekani siku ya Ijumaa.

Wengi wa waombolezaji walivalia nguo nyeusi na kubeba bendera za Iraq pamoja na bendera za wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran ambao ni watiifu kwa jenerali Soleimani. 

Soleimani alikuwa kiungo muhimu katika oparesheni ya Iran Mashariki ya kati na taifa hilo limeapa "kulipiza kisasi" mauaji yake.

Waandamanaji walianza kukusanyika mjini Baghdad mapema asubuhi ya Jumamosi wakipeperusha bendera ya Iraq naya waasi wakiimba "kifo kwa Amerika".

Waandamanaji walizunguka barabara za mji huo wakibeba mababgu yaliyo na picha ya Soleimani huku wengine wakiwa na mabangu yaliyo na picha ya kiongozi mkuu wa kidini wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei.

Soma hii: Nafasi Mpya za Kazi Tanzania-January 2020

Ripoti zinasema mwili ya raia huyo wa Iran aliyeuawa katika shambulio hilo utasafirishwa nchini humo Jumamosi jioni, ambako siku tatu ya maombolezo imetangazwa kwa heshima ya jenerali.

Mazishi yake yatafanyika siku ya Jumanne nyumbani kwake Kerman eneo la kati la Iran.


Share:

Uingereza yatoa tahadhari kwa raia wake kutosafiri Iraq na Iran

Serikali ya uingereza hii leo imetoa onyo kwa raia wake kutosafiri kuelekea Iraq au kufanya safari za aina yoyote kuelekea Iran kufuatia kuuwawa kwa Qassem Soleimani, Kamanda wa kijeshi wa ngazi ya juu wa Iran. 

Ofisi ya Wizara ya mambo ya kigeni imesema kufuatia mvutano wa kikanda unaozidi kupamba moto, hivi sasa imewashauri raia wake kutosafiri kuelekea katika maeneo hayo isipokuwa tu eneo la Kurdistan.

Soma na hii:  Latest Jobs Today  in Tanzania January 2020

Waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza Dominic Raab amesema ni vizuri raia wa taifa hilo kufikiria kwa makini iwapo ni salama kwao kusafiri kuelekea Iran kwa sasa.


Share:

Serikali yajipanga kutumia Filamu kutangaza Vivutio vya Utalii Kimataifa

Na Anitha Jonas – WHUSM,Dar es Salaam.
Viongozi wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo na Wizara ya Maliasili na Utalii wapanga mkakati wa kutumia sekta ya filamu kuwavutia watengenezaji wa filamu kutoka nje kutumia vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania.
 
Kikao cha kupanga mkakati huo kimefanyika leo jijini  Dar es Salaam baina ya wizara hizo ambapo walijadili namna ya kuboresha mazingira ya katika utoaji wa huduma za waandaji wa filamu kutoka nje ya nchi na kuwavutia kuja kwa wingi kutumia vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini kufanya kazi zao.
 
Akizungumza katika kikao hicho Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo alisema katika kudumisha mahusiano ya wizara hizo mbili ambazo zinamwingiliano kutokana na majukumu yake wizara  itaangalia maslahi mapana ya usalama wa taifa katika kuboresha mazingira ya uandaaji wa filamu za wadau kutoka nje ya nchi.
 
“Tumeunda timu kutoka pande zote mbili ambayo itaenda kuangalia  namna ya kuboresha mazingira yatakayowavutia waandaji  wa filamu na makala kutoka nje ya nchi kuja kwa wingi zaidi kufanya kazi zao katika vivutio vyetu, na watakapomaliza  kazi hiyo wataleta ushauri wao, lengo ni kuhakikisha nchi inafanikiwa kukuza uchumi,’’ alisema Dkt.Possi.

Soma Hii: Latest Jobs  in Tanzania January 2020
 
Pamoja na hayo Dkt.Possi alisema  kuwa katika kikao hicho walijadili  kuweka msisitizo pia kuhusu kuhakikisha utoaji wa vibali kwa waandaji wa flamu za nje unakuwa wa haraka na suala hilo limezingatiwa kwa maslahi ya Taifa .
 
Kwa upande wa Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Prof.Adolf Mkenda alisema nchi inavivutio vingi vizuri na baadhi ni vipya hivyo kwa kutumia sekta ya filamu inaweza kutangaza vivutio hivyo kwa wingi pasipo gharama kwani gharama ya kutangaza  vivutio ni kubwa.
 
“Tunaangalia namna yakukuza utalii kupitia filamu sababu ni moja ya njia rahisi ya kutangaza vivutio vya utalii  ni filamu,mfano wa Filamu ya ‘Serengeti  Shall Never Die’ ilifanya vizuri katika kutangaza mbuga ya Serengeti  pia ilisaidia  kuongeza idadi ya  watalii katika mbuga hiyo, hivyo tumeona tuangalie namna ya kuboresha mazingira ya kuwavutia waandaaji hao wa filamu kuja kufanya kazi zao katika vivutio vyetu kama Katavi,Gombe,Burigi,Rubondo na vinginevyo,’’alisema Prof.Mkenda.
 
Aidha, Katibu Mkuu huyo wa  Wizara ya Maliasili na Utalii aliendelea kusema kwa sasa vivutio vinavyofanya vizuri katika utalii ni Serengeti, Ngorongoro ,Kilimanjaro,Manyara , Tarangire na Mikumi  na Tanzania inavivutio vingi sana hivyo tukitumia fursa ya waandaji wa filamu wa nje ya nchi itasaidia kuongeza utalii wa vivutio ambavyo bado havijapata umaarufu.
 
Halikadhalika nae Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi.Joyce Fisoo alitoa ombi kwa Wizara ya Maliasili na Utalii  kusaidia kutoa ufadhili wa masomo kwa wataalamu wa uandaaji wa kazi za filamu nchini kwani kwa sasa kuna  upungufu  wataalam hao na hii ni changamoto kwa waandaji  wa filamu hizo wanapokuja nchini na kuhitaji wataalamu hao kutoka nchini.
 
“Katika  kuboresha  sekta ya uandaaji wa filamu za kisasa na zenye ubora  ningeiomba    Wizara ya  Maliasili na Utalii kutoa ufadhiili wa masomo  ya uandaaji wa kazi za filamu kwa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC)  kwani kutasaidia kuboresha  vipindi vya kutangaza  vivutio vilivyopo nchini kupitia Safari Chaneli  ambayo ni chaneli ya kutangaza utalii”alisema Bibi.Fisoo.
 
Hatahivyo nae Kaimu Kaimu Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Dkt.Kiagho Kilonzo alisema ofisi yake imeandaa kikao na wadau wanaleta watengenezaji wa filamu kutoka nje ya nchi  kwa lengo la kuzungumza nao na kufahamu  ni changamoto gani wanazoziona katika kuwavutia watengenezaji hao wa filamu kuja kufanya kazi nchini nini kifanyike ili kuboresha na kufikia malengo ya kutangaza utalii wa vivutio vilivyopo nchini.


Share:

Project Officer-GFD at DRC Nduta

Project Officer-GFD Job Opportunity at DRC Nduta Project Officer-GFD Job description Job title: Project Officer – GFD Employment category: Grade D, level 1 Reporting to: GFD Project Manager Technical line manager: Area manager Direct reports: – Unit/department: GFD Location: Kibondo (Nduta/Mtendeli) Authorization level: – Overall purpose of the role: The Project officer- GFD will work with the Program… Read More »

The post Project Officer-GFD at DRC Nduta appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Information Management Assistant-Inter Agency at DRC

Information Management Assistant-Inter Agency Job Opportunity at DRC Information Management Assistant-Inter Agency Job description Job title: Information Management Assistant- Inter- Agency help desk, GFD Employment category: Grade E, level 1 Reporting to: GFD Project Manager Technical line manager: Area manager Direct reports: – Unit/department: GFD Location: Kibondo (Nduta/Mtendeli) Authorization level: – Overall purpose of the role: The information… Read More »

The post Information Management Assistant-Inter Agency at DRC appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

4 Job Opportunities at 361 Degrees Africa Ltd

OVERVIEW 361 Degrees Africa Ltd is an all-inclusive creative and communication agency that provides a one stop shop service catering for your Events, Media, Public Relations, Fabrication, Publishing, B2B Consultation, Marketing and Advertising needs by providing a creative, concise, customized and cost-effective solutions. Our Vision To be the country leader in providing creative, concise, customized and cost-effective event… Read More »

The post 4 Job Opportunities at 361 Degrees Africa Ltd appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Administration Officer (2 Post) at Good Neighbors Tanzania

Administration Officer (2 Post) Job Opportunity at Good Neighbors Tanzania Position: Administration Officer (2 Post) Reports to: Assistant Manager Location: Nambinzo Field Office (NFO), Isenzanya Village, Mbozi District, at Songwe Region. Contract Duration: One year (Contract renewable subject to fund availability and employee performance). The Administrative Officer is largely responsible for providing administrative support to Nambinzo Field Office… Read More »

The post Administration Officer (2 Post) at Good Neighbors Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Personal Secretary II at BUWASA

Personal Secretary II at Job Opportunities BUWASA BUWASA is an autonomous entity which is responsible for supplying clean and safe water as well as provision of sanitation services for Bukoba Municipality. The Authority is looking for competent, dynamic, energetic, committed, experienced and well qualified Tanzanian who is capable of embracing and driving change in BUWASA to fill the… Read More »

The post Personal Secretary II at BUWASA appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Program Coordinator at Care Tanzania

Program Coordinator Job Opportunity at Care Tanzania Job Title: Program Coordinator CARE Tanzania seeks to recruit self-motivated, results driven, dynamic, suitably qualified, competent and dedicated Tanzanian to fill a vacant position as mentioned hereunder: Program Coordinator for Ardhi Yetu Program (AYPII) based in Dar es Salaam Job Summary The Program Coordinator (PC) for Civil Society Land Rights Program… Read More »

The post Program Coordinator at Care Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Jobs at African Underground Mining Services

Jobs Opportunities at African Underground Mining Services African Underground Mining Services (AUMS) is an international leader in mechanised hard rock underground mining. AUMS is part of Perenti (Formerly the Ausdrill Group), an ASX 200 company and Australia’s second largest integrated mining services provider. We are a global leader in hard rock underground mining; together with Barminco we operate… Read More »

The post Jobs at African Underground Mining Services appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Monitoring Assistant (Agriculture/Nutrition) G4 at WFP

Monitoring Assistant (Agriculture/Nutrition) G4 Job Opportunity at WFP Monitoring Assistant (Agriculture/Nutrition) G4 Equivalent – Service Contract Appointment (111643) Requisition # 111643 – Posted 02/01/2020 – Short Term-SC WFP – Africa, Central & Eastern – Tanzania, United Republic of – Dodoma – Working Job Language (1) – PROGRAMME & POLICY WFP seeks candidates of the highest integrity and professionalism… Read More »

The post Monitoring Assistant (Agriculture/Nutrition) G4 at WFP appeared first on Udahiliportal.com.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger