Sunday, 10 November 2019

Dkt. Ndugulile: Ukatili Wa Kijinsia Ni Ujambazi Mpya

Na Mwandishi Wetu Dodoma
Naibu Waziri wa Afya Maeandeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amesema Mwaka 2017 Tanzania ilikuwa na matukio ya vitendo vya ukatili wa kijinsia takribani 41elfu na kati ya vitendo hivyo ukatili dhidi ya watoto pekee ni 13 elfu.

Naibu Waziri Ndugulile amesema hayo wakati akizungumza na vyombo vya habari wakati wa Semina ya wabunge wa Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuhusu Mkakati wa Taifa wa Kutokomeza Vitendo vya Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto Jijini Dodoma.

Aidha Naibu Waziri Ndugulile ameifananisha changamoto ya vitendo vya ukatili Nchini kuwa ni ujambazi mpya unaozidi kuwakumba wanawake na watoto kutokana na vitendo hivyo kuendelea kutokea katika maeneo mbalimbali hapa Nchini.

Dkt. Ndugulile amesema unapoongelea ukatili wa kijinsia unazungumzia maeneo makubwa matatu ambayo ni ukatili wa kimwili, kisaikolojia na ukatili wa kiakili na kuongeza kuwa changamoto ya ukatili wa kijinsia imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka.

Ameyataja matendo hayo yanayozidi kuongezeka kuwa ni mimba na ndoa za utotoni, ubakaji na ulawiti dhidi ya wanawake na watoto ndio maana ili kukabiliana na vitendo hivyo serikali tangu mwaka 2016 ilianzisha Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Vitendo vya Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto.

Dkt. Ndugulile ameongeza kuwa juhudi za Serikali katika utoaji elimu bure hapa nchini umepunguza suala la mimba na ndoa za utotoni kwa kuwa mtoto wa kike anapozidi kukaa shuleni ndivyo uwezekano wa mimba za mapema unapozidi kuwa mdogo.

Wakati huo huo Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe. Peter Serukamba amewambia wajumbe wa Kamati hiyo na Wizara kuwa jamii bado ina mila potofu zinazoendeleza vitendo vya ukatili kama vile ukeketeji na kuwataka Wabunge kuelimisha Jamii dhidi ya Vitendo hivyo.

Aidha Mhe. Serukamba amelitaja suala la elimu kwa umma kuhusu utokomezaji wa vitendo vya ukatili kupewa kipaumbelae huku akisifu mpango wa Serikali wa kutokomeza umasikini kwa kiwango cha kaya kupitia TASAF na kuongeza kuwa umasikini pia ni chanzo cha ukatili dhidi ya wawanawake na watoto.

Naye Mshauri Mbobezi wa Sera na Mipango kutoka Shirika la Wanawake la Umoja wa Mataifa Tanzania Bi. Usu Malya amesema shirika lake litaendelea kushirikiana na Wizara ya Afya Idara Kuu Maeandeleo ya Jamii kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto hapa nchini.

Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto ulianza tangu mwaka 2016 na umewezesha kuwa na mtazamo wa pamoja katika utekelezaji wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto na kuondoa mwingiliano, upotevu wa rasilimali watu, fedha na muda unaotumika katika kushgulikia suala moja.


Share:

Serikali Yakamata Pombe Kali Imetelekezwa Porini Kukwepa Kodi Shinyanga

Serikali mkoani Shinyanga imekamata pombe kali aina ya Shujaa, ambayo ilikuwa imetelekezwa porini eneo la Lubaga manispaa ya Shinyanga, ikiwa ndani ya gari aina ya Roli lenye namba za usajili T 391 AES, kwa madai ya kukwepa kulipa kodi.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari Novemba 9, 2019 Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akiwa kwenye kituo cha Polisi wilaya ya Shinyanga, eneo ambalo gari hilo limewekwa chini ya ulinzi, amesema kuwa serikali itawashughulikia wawekezaji wote ambao wanatabia ya kukwepa kulipa kodi ya serikali.

Telack ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Shinyanga, amesema Serikali inahitaji sana wawekezaji hapa nchini ili kukuza uchumi wa taifa, lakini siyo wawekezaji wa kukwepa kodi na kufanya biashara kiujanja ujanja.

“Pombe hii kali ya Shujaa Katoni 1,490 tumeikamata ikiwa imefichwa porini eneo la Lubaga manispaa ya Shinyanga, ikiwa ndani ya gari hili ambalo mnaliona hapa, na wamiliki wa kiwanda hiki wamekuwa na tabia ya kukwepa kulipa kodi na siyo mara ya kwanza kukamatwa,”amesema Telack.

“Hivyo naagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Kesho wafike hapa, ili kufanya tathmini ya kujua kiasi gani cha kodi ambacho watu hawa wanapaswa kulipa, ili Serikali iweze kukusanya mapato na kupata fedha za kutekeleza maendeleo kwa wananchi,”ameongeza.

Pia ameonya baadhi ya Askari Polisi kushirikiana na waharifu hao wa kiwanda cha Shujaa, na kuwapa mbinu za kukimbia ili kukwepa mkono wa Serikali, na kumuagiza Kamanda wa Jeshi hilo mkoani Shinyanga, kuwa ndani ya siku nne, wamiliki wa kiwanda hicho wawe wameshakamatwa.

Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Richard Abwao, alithibitisha kukamata Pombe hiyo ya Shujaa, na kuahidi kutekeleza maagizo hayo ya mkuu wa mkoa, huku akitoa wito kwa wamiliki hao wa kiwanda cha Shujaa wajisalimishe wenyewe kwa usalama wao kwani watakamatwa tu popote pale walipo.

Picha na Marco Maduhu- Malunde 1


Share:

Serikali Kumega ekari 3000 kutoka kwenye shamba la Karamagi Kilosa

Na Farida Saidy- Morogoro.
Serikali ya awamu ya tano kupitia Wizara ya Ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi imeagiza mmiliki wa shamba la Farm Africa maarufu kama shamba la Karamagi lililopo katika Halmashauri ya Wilaya Kilosa Mkoani Morogoro kutoa ekari 3000 kutoka kwenye shamba hilo ili zimilikishwe kwa wananchi wenye uhitaji wa ardhi kwa shughuli za kiuchumi.

Agizo hilo la Serikali limetolewa Novemba 8 mwaka huu na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi alipotembelea shamba hilo lenye ukubwa wa ekari elfu 13 ambapo hakuridhishwa na kasi ya uendelezaji wa eneo hilo tangu Mmiliki wa shamba hilo alipomilikishwa.

“Kwa taarifa zilizopo bwana Karamagi alimilikishwa shamba hili tangu mwaka 2012, hivyo alipaswa kila mwaka kuliendeleza shamba lake japo kwa kiwango cha moja ya nane (1/8), hii ina maana hadi kufikia mwaka huu ambapo umiliki wake umetimiza miaka minane alipaswa kukamilisha uendelezaji wa eneo hili” alisema Waziri Lukuvi,

“Kutokana na hali hii nikuagize Mkuu wa Wilaya umfikishie taarifa bwana Karamagi kwamba mimi kama Waziri wa Ardhi namuagiza atoe ekari 3000 kutoka kwenye shamba hili ili zimilikishwe kwa wananchi ili waziendeleze kwa shughuli za kilimo”, alisisitiza Waziri Lukuvi.

Sambamba na agizo hilo, Waziri Lukuvi alibainisha kuwa 2012, ni ekari 2000 pekee ndizo zilizoendelezwa kwa kupanda mazao kati ya ekari 13,000 za licha ya kipindi cha miaka minane kupita tangu mmiliki huyo alipopata uhalali wa eneo hilo mnamo mwaka shamba hilo wakati alitakiwa awe ameendeleza shamba lote kwa kipindi hicho.

Awali, kabla ya kutoa uamuzi wa kumega sehemu ya shamba hilo ekari 3000, Mhe. Lukuvi alisikiliza kero za wananchi wanaoishi jirani na shamba hilo ambao wengi walimuomba kuwasaidia kupata maeneo kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kiuchumi ikiwemo kilimo wakitaja shamba hilo kuwa ni sababu kubwa ya kuwakosesha maeneo ya kulima
Akiongea na viongozi wa Wilaya ya Kilosa katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo, Mhe.Lukuvi alibainisha kwamba Serikali tayari imejiridhisha kuwepo uhalali wa kufutwa mashamba 48 yaliyopo katika Halmashauri hiyo ambayo hayajaendelezwa ili yagawiwe kwa wananchi wa Wilaya hiyo kwa ajili ya kuyaendeleza.

Aidha, amewataka viongozi wa Halmshauri hiyo kufuatilia mashamba mengine 24 ambayo yameonekana kutoendelezwa ili waandike ilani kwa ajili ya kuomba kufutwa na kugawiwa wananchi wenye uhitaji.

Katika hatua nyingine Waziri Lukuvi amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Adam Mgoyi kuhakikisha suala la udalali na ukodishaji wa ardhi unaofanywa na baadhi ya viongozi wa Wilaya hiyo na kuwakosesha wananchi maeneo ya kilimo unakoma mara moja kwani suala hilo linapelekea kuibuka kwa migogoro ya ardhi Wilayani humo.

Sambamba na hayo Waziri Lukuvi amewaagiza wataalamu wa ardhi kuepuka kubadilisha hati za umiliki wa ardhi kwa wananchi watakaogawiwa maeneo yanayotokana na mashamba yaliyofutwa huku akiwataka wananchi kutouza maeneo watakayopewa kwani hiyo ni huruma ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli.
Akiendelea kutoa maagizo mbalimbali, Waziri Lukuvi amewataka wafugaji wote waliomilikishwa ardhi kihalali Wilayani Kilosa kuweka uzio katika maeneo yao ili kuzuia mifugo isitoke katika maeneo yao na kuingia katika maeneo ya wakulima ili kuepuka migogoro ya Mara kwa mara.

Amesema wakati umefika sasa kwa wafugaji kuacha ufugaji wa kizamani badala yake watumie maeneo hayo kufuga mifugo yao kisasa ndani ya eneo lenye uzio ili mifugo yao iwe na tija zaidi kwao ukilinganisha na ilivyo sasa.
Waziri Lukuvi yupo Mkoani Morogoro kwa ziara ya kikazi ya siku mbili ikiwa na lengo la kupata maoni na mapendekezo juu ya kazi ya awali iliyofanywa na tume ya uhakiki wa mashamba yasiyoendelezwa huku akishangazwa na upendeleo ulioonyeshwa katika kuyabakiza mashamba 24 ambayo yameonekana bado hayajaendelezwa.


Share:

Mawaziri Wa Mambo Ya Nje Wa Nchi NORDIC Na Afrika Watembelea Mradi Wa SGR

Mawaziri wa Mambo ya nje kutoka nchi za Nordic na Afrika watembelea Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa – SGR kipande cha Dar es Salaam – Morogoro, kuanzia Stesheni ya Dar es Salaam hadi Vingunguti jijini Dar es Salaam Novemba 09, 2019.

Lengo la ziara hiyo ni kuona hatua kubwa ambayo serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepiga katika kuboresha miundombinu ya usafirishaji ukizingatia miundombinu ni moja kati ya vitu muhimu katika kuimarisha uhusiano na ushirikiano baina ya nchi za Nordic na Afrika.

Mawaziri hao walipata fursa ya kuona maendeleo ya ujenzi wa stesheni ya reli ya kisasa inayojengwa eneo la stesheni jijini Dar es Salaam, daraja la treni lenye urefu wa KM 2.5 pamoja na maendeleo ya Mradi kwa ujumla kipande cha Dar es Salaam – Morogoro ambao umefikia zaidi ya 70%.

Miongoni mwa Mawaziri waliopata fursa ya kutembelea mradi ni kutoka nchini Egypt, Nigeria, Angola pamoja na Niger. Ziara hii ni matunda ya mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya nje kutoka nchi za Nordic na Afrika uliojadili mambo kadhaa kuhusu kuboresha uhusiano na ushirikiano uliopo kati ya nchi za Afrika na nchi za Nordic uliofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Mwl. J.K Nyerere jijini Dar es salaam.

Aidha Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania Ndugu Masanja Kungu Kadogosa amewashukuru Mawaziri hao kwa kuchagu kutembelea mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa kwa kuwa ipo Miradi mingi ya kimkakati.

Naye Waziri wa Mambo ya Nje nchini Nigeria Mhe. Zubairu Dada amesema kuwa amefurahishwa na emeipongeza Tanzania kwa kutumia fedha zake za ndani kujenga reli ya kiwango cha kimataifa kuanzia Dar es Salaam hadi Makutupora Singida. Ameongeza kuwa Afrika haiwezi kuendelea kusubiri maendeleo hivyo jitihada za haraka zinatakiwa kufanywa ili kuhakikisha miradi ya miundominu inakamilika haraka ili watu wapate huduma.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili November 10




Share:

Saturday, 9 November 2019

Administrative Assistant Job at U.S. Embassy

Job Opport at U.S. Embassy, Administrative Assistant Administrative Assistant OSC  U.S. MISSION DAR ES SALAAM VACANCY ANNOUNCEMENT The U.S. Mission in Dar es Salaam is seeking eligible and qualified applicants for the position below. Position Title:  Administrative Assistant OSC Vacancy Number:  DaresSalaam-2019-041 A copy of the complete position description listing all duties, responsibilities and qualifications required is available at:… Read More »

The post Administrative Assistant Job at U.S. Embassy appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

CHAUMMA NAO WATANGAZA KUTOSHIRIKI UCHAGUZI ...HASHIM RUNGWE ASEMA ' UCHAGUZI UMETAYARISHWA KWA HILA'



CHAMA cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), kimetangaza kutoshiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. 

Uamuzi huo umetangazwa leo tarehe 9 Novemba 2019 na Hashim Rungwe, Mwenyekiti wa CHAUMMA Taifa, wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam. 

Rungwe ameeleza kuwa, wamejitoa katika uchaguzi huo kwa kuwa mchakato wake ulikuwa na hila, kwa wagombea wa vyama vya upinzani.

“Tunashindwa, tunaona kwamba huu uchaguzi umetayarishwa kwa hila, kwamba wananchi wasishiriki. Tunaona kwamba uchaguzi huu umefanywa hila. Na sisi pia tunaamua hatutashiriki uchaguzi huu. Tunaomba wagombea wetu popote walipo wasishiriki,” ametangaza Rungwe.

Rungwe amesema wamefikia hatua hiyo, baada ya kuona jitihada zao za kutafuta suluhu kuhusu hujuma hizo, kugonga mwamba.

“Wanachama wote wafahamu huu uchaguzi una hila, tumekata rufaa lakini haijasaidia chochote. Kama wao ndio wanataka hivi, kwamba wale wana nguvu, wana dola, sisi hatuko tayari kupigana,” amesema Rungwe na kuongeza;

“Watanzania hatuko tayari kupigana. Hatuna tabia hiyo. Unatuzuia hatufanyi siasa. Sasa uchaguzi halali umeutangaza tumekuja kuchukua fomu, matatizo tunasumbuliwa, tumezirudisha zimekataliwa, tufanye nini.”

Rungwe amesema wananchi ambao ndio wapiga kura, wataamua la kufanya kuhusu uchaguzi.

Rungwe amesema CHAUMMA kilisimamisha wagombea zaidi ya 250, ambapo jiji la Dar es Salaam kilisimamisha wagombea 5, Morogoro (38), Iringa (30), Njombe (20) Tabora (38), Kigoma (10), Mwanza (25), Mara (40), Mtwara (7), Tanga 10 na Shinyanga (6).

CHAUMMA kinakuwa chama cha tatu kuususia uchaguzi huo, baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na ACT- Wazalendo, kutangaza kujiondoa.
Share:

Consultant – Gender Assessment Job at FAO

VACANCY ANNOUNCEMENT FOR Consultant – Gender Assessment BACKGROUND FAO’s Policy on Gender Equality established the preparation of a Country Gender Assessment as a minimum requirement for country level planning and programming in particular for the formulation of the Country Programming Framework (CPF). The rationale behind this requirement is that it is fundamental for FAO to have up-to-date objective… Read More »

The post Consultant – Gender Assessment Job at FAO appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Maswali 15 Yanayoulizwa Mara kwa Mara Kwenye Usaili ( Interviews ) na Namna ya Kuyajibu

Usail wa ajira (interviews) husababisha hofu na msongo wa mawazo kwa vijana wengi kabla au baada ya kutoka chumba cha usaili.

Tatizo hilo hutokana na hofu inayojenga wakati wa kujibu maswali unayoulizwa  na watu ambao wamekuzunguka wakati wa kufanyiwa usaili.

Njia moja ya kuzuia hii kutokea ni kufuatilia mfumo wa kujibu maswali.

Ifuatayo ni orodha yetu ya maswali 15 yanayoulizwa mara kwa mara kwenye interviews( Usaili) na namna ya kuyajibu;

▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬ 

1.Jitambulishe(Wewe ni Nani?)
Mara nyingi hili ni swali ambalo mtahiniwa huulizwa mara tu aingiapo kwenye chumba cha usaili. Kwa bahati mbaya watahiniwa wengi hudhani kuwa waajiri hutamani kujua majina yao. Hapana, majina yako wanayafahamu na pengine hata taarifa za ziada. Katika swali hili waajiri uhitaji kujua sifa zako zihusianazo na ajira zitakazo dhihirisha kuwa wewe ni mtu sahihi.

Mfano mtu anaweza kujibu hivi, “Jina langu ni Mti Mkavu, ni Mhitimu wa Shahada ya Masoko ya Chuo Kikuu Dodoma. Ni mtu makini, mbunifu, mchapa kazi na ninayependa watu. Pamoja na hayo ninao ujuzi usio na shaka kwenye masuala ya mawasiliano. Uwezo wangu unadhihirishwa na mrejesho ambao huwa na upata kwa kila mtu ninaye fanya naye kazi”.

Katika swali hili ni muhimu kujua kuwa halihitaji wewe kuzungumzia mambo yasiyo husiana na kazi na ajira. Kwenu mpo wa ngapi,jina la mama yako, mkoa unaotoka, kabila, kazi ya baba au mama yako havihitajiki katika taarifa unazotakiwa. 


2.Kwanini upewe ajira kwetu? | au unaweza ukaulizwa Kwa nini unahisi wewe ni mtu sahihi kwa kazi hii na siyo mwingine?

Kumbuka kuwa usaili wa kazi unahusisha ushindani hivyo swali hili linataka uoneshe utofauti ulionao. Katika kujibu swali hili zingatia mahitaji ya kazi husika kujenga hoja kwani hata kama una utofauti wa aina gani kama hautasaidia katika kufikia  malengo ya taasisi bado itakuwa ni kazi bure.

Mfano, “ Siyo kwamba mimi ni mchapakazi na mbobezi katika uhasibu pekee lakini pia ni mtu ambaye ninaweza kufanya shughuli zangu bila kusimamiwa. Mimi ni mtu wa matokeo hivyo kwa kila ambacho hufanya hulenga kutimiza malengo kwa wakati na kufikia viwango stahiki. 


"Ubora wangu unathibitishwa na tuzo kadhaa nilizowahi kupata ikiwemo mfanyakazi bora wa mwezi mara nne nilipokuwa nikifanya kazi na na Magogo Media. Hii inathibitisha kuwa mkinipa fursa hii hamtakuwa mnajaribu bali mtakuwa mnafanya maamuzi sahihi”.

3.Unajua nini kuhusu sisi?
Siku zote maandalizi ya usaili yanaenda sambamba na kutafuta taarifa sahihi za taasisi husika. Hivyo ni vyema kuhakikisha kuwa taarifa unazotoa hapa ni sahihi na muhimu katika kudhirisha kuwa ulishafanya utafiti wa kutosha kuhusu taasisi husika.

Mfano, “ Benki yenu ilianzishwa mwaka 1987 ina maono ya kuwa benki bora kuliko zote nchini kwa kutoa huduma za kifedha zinazo aminika na kufikia maeneo mengi nchini. Kwa sasa benki yenu ina matawi 700 na ATMs 500 huku ikiwa na mpango wa kufungua matawi mengine Kigoma hivi karibuni. 


Endapo mtanipa fursa ya kufanya kazi na nyinyi nitahakikisha natumia vyema uwezo wangu katika masuala ya masoko ili kuongeza wateja na kuhaikisha huduma bora mnayotoa inafahamika kwa watu wengi.”

4. Ni vitu gani unavyojivunia?
Katika swali hili waajiri huhitaji kujua mambo kadhaa ambayo unayaona kama mtaji mkubwa katika utendaji kazi. Ni vyema kukumbuka kuwa mambo utakayo yataja hapa ni yale yenye umuhimu katika kuongeza ufanisi au ubora katika kazi husika kwani kila kazi inamahitaji yake ya tofauti na kazi nyingine.

Kwa mfano, “mambo makuu mawili ninayojivunia ni ujuzi na uwezo katika huduma kwa wateja na kujisimamia katika majukumu yangu. Kila ninapowahudumia wateja huwa napokea mrejesho chanya juu ya namna wanavyoridhishwa na huduma yangu hivyo kutamani kuhudumiwa nami tena.


Hii hunifanya nijione kuwa mtu muhimu sana katika taasisi yoyote ninayofanya nayo kazi. Pia, uwezo wangu katika kufanya shughuli bila kusimamiwa au chini ya usimamizi mdogo unanifanya niwe mtu wa kuaminiwa na kutegemewa katika kufanya shughuli zangu.Haya ni baadhi ya mambo mengi yanayonifanya mimi kuwa mtu wa tofauti. Nina amini hamtaacha fursa ya kufanya kazi nami”
 

5.Udhaifu wako ni upi?
Hili ni moja ya maswali ambayo watainiwa wengi huyachukia na kuyaona kama yana lengo la kuwatafutia sababu za kuwanyima kazi. Wengine kwa lengo la kuonesha ukamilifu huthubu kusema kuwa hawana udhaifu wowote-usithubutu kusema hivyo. Kila mtu ana udhaifu wake kwani hakuna aliye mkamilifu.

Suala la msingi ni kujua namna ya kujibu suali hili. Mambo ya kuzingatia ni pamoja na kuchagua udhaifu ambao hauta athiri utendaji wako na pili hakikisha udhaifu huo unahusiana na ujuzi na sio tabia. 


Ujuzi ni rahisi kuutafuata lakini kubadilisha tabia ni ngumu zaidi hivyo usiseme kuwa wewe ni mvivu,mdokozi, na mengineyo ya kitabia. Na unapotaja udhaifu wowote kumbuka kuonesha jitihada ambazo umeshazifanya ili kudhibiti udhaifu huo.

Kwa mfano, kwa kazi ya uhasibu mtu anaweza sema, “Udhaifu nilio nao ni masuala ya ‘graphic designing’ niligundua hili nilipohitaji kuandaa tangazo kwa ajili ya ofisi niliyokuwa nikifanya nayo kazi. Hata hivyo, nimeanza kujifunza mwenyewe kupitia mtandao wa internet na naona napata mabadiliko chanya kila leo”.

Kwa jibu hili ni dhahiri kabisa graphic designing siyo mahitaji muhimu ya kazi ya uhasibu hivyo haita athiti utendaji wa kazi.


6. Kwa nini uliacha kazi yako ya mwanzo?
Hapa unahitajikua makini sana, kumbuka na epuka kuzungumza vibaya kuhusu muajiri yeyote kabla au sasa au uwezo wa muajiri. 


Hapa unaweza ukawajibu tu kwamba;" Kwa sababu ya kuboresha na kuongeza ujuzi, pia natafuta fursa bora zaidi."

7.Unatarajia kupata nini kutokana na kufanya kazi hapa? au unaweza ukaulizwa | Baada ya miaka mitatu wewe mwenyewe utakua wapi?
Ongelea unachotumaini kutimiza ila kuwa mkweli. Pia usiongee kwa ujumla. Chagua kitu maalum ambalo ni muhimu kwa kampuni alafu ilenge. Ila, uwe wazi kwa kusema itachukua muda kujifunza zaidi kuhusu kampuni ili kufanikiwa zaidi.

Kwa mfano; “Nikiwa mwalimu wa kiingereza, lengo langu ni kuongeza asilimia ya wanafunzi wanaofaulu mtihani wa taifa kuwa 85% ya darasa yangu. Najua itachukua muda kujua vizuri changamoto za wanafunzi ila, naamini nitafanikiwa”


Ni vizuri kusema kwamba unatumaini kuona uwajibikaji zaidi  katika kampuni hiyo na kuongeza thamani katika kampuni kwa mchango wako. 

8.Kwanini umekaa muda mrefu bila kupata ajira?

Wajibu kwamba; "Nilikuwa najiendeleza katika taaluma yangu "


9. Eleza namna unavyoweza kujisimamia mwenyewe
Wajibu kwamba: Nitakuwa nafanya kazi niliyopewa nikishirkiana na wasimamizi wangu na viongozi juu ya namna ya kumaliza kazi kabla ya muda uliopangwa.


10. Kitu gani kinakukera miongoni mwa wafanyakazi wenzako?

Wajibu kwamba; "Naamini katika kufanya kazi kwa pamoja. Hata kama nikikerwa na kitu chochote, huwa najaribu kuepuka isipokuwa kama ni kitu cha binafsi."

11.Unategemea kufanya kazi kwa muda gani kama ukipewa ajira?

Wajibu:Kwa muda mrefu kama nitaendelea kuongeza kitu katika taaluma yangu.

12:Je, mwenyewe unajiona kufanikiwa?

Wajibu: Ndio, ukiachana na uwezo wa taaluma yangu, nadhani nimepata watu sahihi wa kufanya nao kazi.

13. Uwezo wako ni upi katika kazi?
Wajibu: Mimi huwa naelewa na kufundishika kwa haraka na ni mchapakazi wa kweli.

14,Unapenda nafasi au cheo gani katika timu unayofanya nayo kazi?
Wajibu: Haijalishi hadi nitakapojifunza kitu kipya kwa kila mradi au kazi.

15.Je, unaswali lolote kwetu? 

Mwishoni wa interview, ni kawaida kwa mwajiri kuuliza kama una maswali kwao. Ukipewa nafasi hii, usiulizie mshaara na faida zingine. Badala yake, uliza:
  1.     Maadili ya kampuni
  2.     Aina ya uongozi
  3.     Wafanyakazi wenzako
  4.     Chochote ambacho hukuelewa kuhusu kazi hiyo.
  5.     Watakupa jibu baada ya muda gani?
==>>USIFANYE HAYA MAKOSA KATIKA SWALI HILO:
- Je, kuna fursa ya kukua / kupandishwa ngazi?
- Nitapata siku ngapi za likizo?

- waajiliwa wanafaidika vipi na kampuni hii. 

==>Tiba bora ya msongo wa interview ni kujiandaa
Ingawa interview inaweza ikakupa misongo mingi, ukijiandaa vizuri Utashangazwa na mafanikio yako.

Interview ni nafasi yako ya mwisho kumvutia mwajiri, na vidokezo vilivyoelezwa hapo juu vitakusaidia na hilo.

Kumbuka, hamna haja ya kuwa na wasiwasi ukiwa umejiandaa. 


Nakutakia Mafanikio mema kwenye Interview
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬

👉Sasa, kwa kuwa umeshajua jinsi ya kujibu vizuri maswali ya Interview, anza kutafuta kazi unayoitaka kwa kubofya hapo chini. 


Hilo ni Jukwaa Maalumu la Ajira zote za Serikali, Makampuni Binafsi n.k. Kuna Nafasi za Kazi zaidi ya 7000 kwa ajili yako.

👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
http://ajirazote.com/jobs


▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬


Share:

DAKTARI AIBUKA NA BIBLIA YA SEHEMU ZA SIRI ZA MWANAMKE...ZIJUE SIRI 5 ZA SEHEMU ZA SIRI

Kuna imani potofu kwenye mitandao ya kijamii kuhusu sehemu za siri za wanawake, mwanamke mmoja ameamua kujitoa kuelezea masuala hayo.

Dr Jen Gunter amekua daktari wa kina mama huko Marekani na Canada kwa miaka 25. Ametoa kitabu hivi karibu kinachoitwa biblia ya sehemu za siri za wanawake.

Kutokana na mijadala mbalimbali kuhusu sehemu za siri za wanawake, kuna mambo makuu matano ambayo mwanamke anapaswa kujua.

1- Sehemu za siri zinajisafisha zenyewe

Idadi kubwa ya wanawake, wana imani kuwa wakitumia bidhaa mbalimbali za urembo, kama sabuni basi ndio watajisafisha vizuri sehemu za siri. lakini Dr Gunter anasema kuwa hakuna haja ya kutumia chochote kusafisha sehemu ya siri, kwa sababu kunajisafisha yenyewe

''Ni sehemu inayojisafisha yenyewe'' anasema Dr Gunter

Pia anaonya juu ya kutumia manukato sehemu za siri, anasema kuwa ni kama sigara ilivyo hatari kwa mapafu ya binadamu.

''Hata maji wakati mwingine huweza kuharibu jinsi ya ufanyaji kazi wa sehemu za siri, pia inaweza kusababisha kuambukizwa kwa haraka kwa magonjwa ya ngono, kujifusha pia kuna madhara yake kwani unaweza kujichoma na mvuke.

''Sehemu ya nje inaweza kusafishwa na maji kwa utaratibu'' anasema Dr Gunter

Sabuni huweza kusababisha asidi kwenye sehemu za siri, na ikifika umri wa kukoma kwa hedhi basi inashauriwa kutumia mafuta kama ya mzaituni ama ya nazi.

Seli za kwenye sehemu za siri hujitengeneza kila baada ya saa 96, tofauti na eneo lolote la ngozi, sehemu za siri hujirekebisha haraka zaidi.

2 -Ni muhimu kujua sehemu za siri kuanzia sehemu ya nje (Vulva)

Sehemu ya siri imegawanyika sehemu ya ndani na nje, sehemu ya nje ndio sehemu ambayo itakugusa kwenye nguo yako ya ndani, Dr. Gunter anasema kuwa ni muhimu sana kujua kutofautisha maeneo hayo.

''Huwezi kutaja maneno haya ya sehemu za siri kwa uwazi kwasababu tu ni jambo la aibu, hii si sahihi''

Anasisitiza kuwa kutumia maneno ya sehemu za siri si suala la aibu, na inaweza kuleta madhara kwa mwanamke pale ambapo atashindwa kueleza kwa usahihi ni sehemu gani za sehemu za siri anaumwa.

3 - Sehemu za siri za mwanamke ni kama bustani

Sehemu za siri zina jeshi kubwa la bakteria wazuri ambao wanasaidia kufanya kuwe na afya.

Bakteria wazuri wanatengeneza ute ambao una asidi kidogo ambazo zinaondoa bakteria wabaya, na hufanya kuweka unyevunyevu wakati wote.

Sababu hii inatakiwa kusiwekwe wala kupanguswa kwa kitu chochote ndani ya sehemu za siri ili kuhakikisha bakteria wazuri wabaki na kuwazuia bakteria wabaya kutokuchukua nafasi.

Dr Gunter anasema baadhi ya wanawake wamekua wakikausha sehemu za siri kwa kutumia kifaa cha kukaushia nywele, hawatakiwi kufanya hivyo, eneo hilo linatakiwa linabaki na unyevunyevu wakati wote.

4 - Nywele za sehemu za siri zipo hapo kwasababu.

Gunter anasema kuwa imekua ni utamaduni kwa wanawake kunyoa sehemu za siri na kubakiza upara kabisa, hii inaweza kusababisha kushambuliwa kwa urahisi na bakteria.

''Unavyonyoa sehemu za siri, unasababisha usumbufu kwenye ngozi, anasema Dr Gunter, tumeona watu wanajikata, na maambukizi pia''

Kama unataka kunyoa, unapaswa kutumia wembe safi, mpya, na unyoe namna ambayo nywele zimeota, ili kuepusha nywele kuota vibaya.

Lakini pia nywele zinatakiwa zibaki kwa sababu kwa namna moja ama nyingine husababisha athari kwa masuala ya ngono.

''Nywele zina maana yake, na ni sehemu muhimu kati ya ngozi na sehemu za siri'' anasema Dr Gunter.

5 - Umri unavyoenda unaathiri na sehemu za siri.

Baada ya miaka kadhaa ya kupata hedhi, wakati mwingine watoto, mayai ya uzazi huacha kuzalishwa na hedhi pia inakoma. Idadi ya homoni inayofanya mwili wa mwanamke uzalishe zinapungua sana, hii inaleta athari kwa sehemu za siri.

Tishu ambazo zinaleta unyevunyevu kwenye sehemu za siri zinapungua na kusababisha kubaki kukavu, na husababisha maumivu wakati wa tendo la ndoa,

Hii inaweza kuleta msongo wa mawazo kwa baadhi ya wanawake, lakini Dr Gunter anasema kuwa wanaweza kupata msaada kwa kutumia vilainishi ambavyo huuzwa kwenye maduka ya dawa.

''Sio lazima upate shida unaweza kutumia vilainishi'' anasema Gunter.
Chanzo - BBC
Share:

DC Chongolo Atekeleza Agizo La Rais Jpm La Kusimamia Kurudishwa Kwa Nyumba Ya Bibi Mwenye Miaka Zaidi Ya 80.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo ametekeleza agizo la Rais Dk. John Pombe Magufuli la kusimamia kurudishwa kwa nyumba ya Bi Amina Muhenga mwenye miaka zaidi ya 80 aliyozurumiwa kwa kipindi cha miaka zaidi ya 30 iliyopita.

Rais Dk. Magufuli alitoa agizo hilo zaidi ya miezi miwili iliyopita alipokuwa kwenye ibada ya jumapili katika kanisa la mtakatifu Petro ambapo Bi Amina alimfuata na kumueleza malalamiko yake kuhusiana na nyumba yake kuchukuliwa na mtu mwingine kinyume cha taratibu na hivyo kumsababishia kukosa makazi maalumu ya kuishi.

Mhe. Chongolo alieleza kuwa baada ya Rais kutoa maagizo hayo, kwakuwa ni waisaidizi wake ,walilifanyia kazi na hivyo kufanikisha kumrudishia Bi Amina nyumba yake pamoja na hati huku utaratibu mwingine ukiendelea kufanyika.

“Baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa Bibi, Mhe rais  kwakuwa sisi ni wasaidizi wake, alituagiza kulifanyia kazi na leo hii tumehitimisha kwa kumkabidhi hati za umiliki wa nyumba yake, na mambo mengine tunaendelea kuyakamilisha, kuanzia sasa bibi anarudi kwenye nyumba yake.” Amessema Mhe. Chongolo.

Aidha Mhe. Chongolo ameonyesha masikitiko yake ya baadhi ya wananchi wanaoishi katika Wilaya ya Kinondoni kuishi kwa ujanja ujanja na kusema kuwa kunaidadi kubwa ya watu wanaoishi kwenye mfumo huo na hivyo kutoa onyo la kuwataka kuacha mara moja tabia hiyo.

Amesema imekuwa ni jambo la kawaida kwa wananchi hao kwani kila siku ofisi yake imekuwa ikipokea malalamiko yanayohusiana na kuzurumiwa kwa nyumba zao kwakutumia kigezo cha hukumu ya Mahakama na hivyo kuacha watu wakiteseka.

Ameongeza kuwa,wakitoka Mahakamani wanakuja kuwatoa watu wenye haki, sijui niseme nini ila ukiangalia kunahali ya rushwa, ambayo imekuwa ikiwatesa sana baadhi ya wananchi, kazi yetu sisi ni kusimamia haki,nitahakikisha haki inasimamiwa na inatolewa kwa mwenye haki” amesema Mhe. Chongolo.

Kwa upande wake Bi Amina amemshukuru rais Magufuli kwa kumsaidia kupata nyumba yake, na hivyo kusema kuwa anamuombea kwa mungu aendelee kuwatumikia wanyonge.


Share:

Jobs Opportunities at Management and Development for Health (MDH)

Jobs Opportunities at Management and Development for Health (MDH) Management and Development for Health (MDH) is a non-profit, non-governmental organization whose primary aim is to contribute to address public health priorities of Tanzania and world at large. The priorities include: HIV/AIDS, Tuberculosis, Malaria; Reproductive, Maternal, New-born and Child health (RMNCH), Nutrition; Non-Communicable Diseases of public health significance; as… Read More »

The post Jobs Opportunities at Management and Development for Health (MDH) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Nafasi za kazi Ardhi University, November 2019

ARDHI UNIVERSITY  Employment Opportunities  Ardhi University has vacant positions in the Academic cadres as indicated below. The University subscribes to the policy of an equal opportunity employer and therefore invites applications from candidates who are interested to work in a thriving University environment and have the requisite skills, qualifications and experience for various positions as indicated below;  A:… Read More »

The post Nafasi za kazi Ardhi University, November 2019 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Managing Director Job at NJUWASA

Job Opportunity at NJUWASA, Managing Director TITLE: MANAGING DIRECTOR Njombe Urban Water Supply and Sanitation Authority (NJUWASA) is an autonomous entity charged with the overall operations and management of water supply and sanitation services in Njombe Township. NJUWASA was established under the auspices of The Water Supply and Sanitation Act No 12 of 2009, It has mandate to Supply… Read More »

The post Managing Director Job at NJUWASA appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

MEDICAL DOCTOR II at Songambele Hospital

Job Summary The Medical Doctor will be responsible for the provision of quality health care assistance for patients within the health center. Minimum Qualification: Bachelor Experience Level: Management level Experience Length: 1 year Job Description Job Description:MEDICAL DOCTOR II – 2 POSTS DUTIES AND RESPONSIBILITIES 1. Attending in and out patients. 2. Attending emergency medical duties. 3. Carrying out investigations of… Read More »

The post MEDICAL DOCTOR II at Songambele Hospital appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Audit Senior at INNOVEX

Job Opportunity at INNOVEX, Audit Senior Audit Senior  INNOVEX is a professional services firm providing advisory and assurance services in Africa. The firm is inviting job applications from individuals that are performance driven and interested in building a professional services career as detailed below. The current vacant positions are based in Par es Salaam. Audit Senior An Audit… Read More »

The post Audit Senior at INNOVEX appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Audit Manager at INNOVEX

Job Opportunity at INNOVEX, Audit Manager Audit Manager   INNOVEX is a professional services firm providing advisory and assurance services in Africa. The firm is inviting job applications from individuals that are performance driven and interested in building a professional services career as detailed below. The current vacant positions are based in Par es Salaam. Audit Manager The Audit… Read More »

The post Audit Manager at INNOVEX appeared first on Udahiliportal.com.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger