Thursday, 7 November 2019

Matokeo ya UEFA Champions League Jana November 6




Share:

Kamati Kuu CHADEMA Kukutana kwa Dharura Leo Alhamisi November 7

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeitisha kikao cha dharura cha Kamati Kuu leo Alhamisi Novemba 7, 2019 kutoa msimamo kuhusu mchakato wa uchaguzi wa Serikali za mitaa.

Kuanzia Jumanne Novemba 4, 2019 Chadema kimekumbana na kilio cha wagombea wake wengi kuenguliwa katika mchakato wa uchaguzi  wa Serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 24, 2019.



Share:

CHADEMA Walimwa Barua Nyingine na Msajili wa Vyama vya Siasa

Msajili wa vyama vya siasa nchini Tanzania amekiandikia barua Chadema kukitaka kuwasilisha ratiba ya mkutano mkuu wa kuchagua viongozi wa kitaifa wa chama hicho kabla ya Novemba 11, 2019.

Barua hiyo imetolewa  Jumatano Novemba 6, 2019 na naibu msajili wa vyama vya siasa, Sisty Nyahoza kwa niaba ya msajili wa vyama vya siasa, Jaji Francis Mutungi.

Oktoba Mosi, 2019 chama hicho kikuu cha upinzani  nchini Tanzania kiliandikiwa barua na ofisi hiyo wajieleze kwanini wasichukuliwe hatua kwa madai ya kukiuka Sheria ya Vyama vya Siasa kwa kuchelewa kufanya uchaguzi mkuu wa chama hicho.




Share:

Jeshi La Polisi Kanda Maalumu ya Dar Lafanikiwa Kumuua Jambazi Sugu

Polisi kanda Maalumu ya Dar es Salaam, wamefanikiwa kumuua jambazi maarufu aliyekuwa akitafutwa kwa muda mrefu anayejulikana kwa jina la Kambale, usiku wa kuamkia  Novemba 6, 2019, eneo la Ukonga Mazizini, jijini humo na kumkuta na silaha moja aina ya Bastola.
 
Taarifa hiyo imetolewa  Novemba 6, 2019, na Kamanda wa kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa imesema kuwa, jambazi huyo alikuwa ni maarufu sana kutokana na matukio yake ya utekaji wa bodaboda na kuwaua watu.

"Katika juhudi zetu za kupambana na uhalifu, tumeua jambazi maarufu sana alikuwa anaitwa kambale, ametesa sana kule Ukonga - Mazizini na Kinyerezi, amekuwa anateka watu na kuwaua bodaboda na kufanya chochote anachotaka na jina la Kambale lilikuwa na maana ya kila akitaka kukamatwa anateleza", amesema SACP Mambosasa.

Akizungumzia hali ya usalama ndani ya Jiji hilo, Mambosasa amesema kuwa bado wanaendelea kuwasaka wale wote, wanaotaka kuleta taswira tofauti ili kabla hawajatimiza lengo lao wawafikie na Jiji liendelee kuwa salama.


Share:

Matokeo ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Jana November 6




Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Novemba 7

Mengine Yatawekwa muda si mrefu, Endelea kutembelea ukurasa huu


Share:

Kalemani: Tanzania Ina Akiba Ya Gesi Futi Za Ujazo Trilioni 57.54.

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
SERIKALI kupitia Wizara ya nishati imesema Tanzania ina akiba ya gesi futi za ujazo trilioni 57.54 huku matumizi ya rasilimali hiyo kwa sasa ni futi za ujazo trilioni 0.5 tu.

Kutokana na hayo imesema itashirikiana kwa ukaribu zaidi na asasi za kiraia kuhakikisha wanaleta maendeleo ya uchumi wa viwanda kwa kutumia rasilimali gesi.
 
Hayo yamebainishwa    Nov.6,2019  na waziri wa nishati Medardi  Kalemani wakati akitoa taarifa ya nishati  kwenye jukwaa la tisa la wadau wa sekta ya uziduaji wa mafuta ,  gasi  na madini Katika wiki ya AZAKI inayoendelea Jijini hapa.

Waziri Kalemani amesema matarajio ya serikali  ni  kuhakikisha rasilimali hiyo inashiriki kikamilifu kwenye uchumi wa viwanda na kuchochea maendeleo ya taifa na wananchi wake.

Pamoja na hayo amesema ,jitihada za Serikali zinaendelea Katika kuhundua mafuta kwa manufaa ya watanzania .

Aidha Mhe.Kaleman ame sisitiza masuala ya uwazi,uwajibikaji na ufuatiliaji wa uhakika  Katika masuala ya gesi unapaswa kupewa kipaumbele kwa kuzingatia teknolojia na ubunifu kwa uchumi wa viwanda.
 
Kwa upande wake Naibu waziri wa madini  Stanslaus Nyongo akizungumza katika jukwaa hilo alisema tangu serikali kufungua masoko ya madini katika maeneo mbalimbali nchini mchango wa sekta hiyo kwenye pato la taifa umeongezeka maradufu  huku asilimia 97% ya Watanzania mgodi wa Geita GGM wameajiriwa.

Aidha amesema ,Licha ya mafanikio hayo  vitendo vya ulanguzi kwa wachimbaji na utapeli wa watu kuuziwa madini bandia vimetoweka kabisa kutokana na umakini unayofanywa na Serikali.

Pamoja na hayo alisema ,Katika kuhakikisha ulinzi Katika sekta ya madini ,Serikali iliwakamata wanunuzi tisa wa madini ya dhahabu ambao walikiuka Sheria ya ununuzi.

Hata hivyo amebainisha kwamba,kwa Sasa Serikali kwa kushirikiana na Serikali za mitaa inatupia jicho kwa wachimbaji wadogo ili kuwawezesha ajira na kusaidia kuongeza pato la Taifa.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri huyo alisema  Serikali inapambana kuondoa vikwazo kwa wanawake Katika sekta ya madini  .

Amesema wanawake wamekuwa wakikumbana na vikwazo kwa kuchimba dhahabu  kwa kubahatisha kwa kuwa hawana taarifa sahihi za kijiolojia.

"Kupitia Shirika letu la stamiko Serikali inaendeleza huduma kwa kutoa elimu kwa wachimbaji wanawake kuhusu madini juu ya utafiti,uchenjuaji  na uzalishaji,"alisema.
 
Awali akizungumzia umuhimu wa jukwaa hilo mkurugenzi mtendaji wa Haki Rasilimali Rachel Chagonja amesema jukwaa hilo limelenga kujadili kwa pamoja ubia kati ya serikali wadau na wananchi kuhusu ushiriki kwenye sekta ya mafuta gesi na madini kwa maendeleo ya taifa na wananchi wake.

Amesema ,sekta hiyo inakabiliwa na mfumo dume kutokana na kukosekana uwiano sawa wa kijinsia huku wanawake wakinyanyasika na kudharauliwa hasa katika maeneo ya migodini na kuiomba Serikali kuwashirikisha zaidi wanawake Katika uchumi was viwanda.

Mwenyekiti wa bodi kutoka Haki Rasilimali  Bw.Donald Kasongi amesema asasi ya Haki Rasilimali inahakikisha inaboresha kipato kwa wananchi kutokana na Rasilimali zilizopo nchini.


Share:

Wednesday, 6 November 2019

Kamati za Rufaa Tendeni Haki kwa Wagombea

Nteghenjwa Hosseah, Manyara
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amezitaka Kamati ya Rufaa za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kutenda haki wa wagombea wote watakaowasilisha malalamiko yao kuhusu uteuzi.

Waziri Jafo ameyasema hayo wakati akizungumza na Kamati ya Rufaa pamoja na viongozi wa Mkoa wa Manyara katika ziara yake Mkoani humo kuangalia maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, 2019, Tarehe 6/11/2019.

Amesema tunataka haya malalamiko yanayoendelea huko nje hivi sasa yaishe na kuisha kwake ni ninyi wajumbe wa Kamati  hii kufanya kazi yake kwa umakini na uadilifu mkubwa ili kuhakikisha haki inatendeka.

“Tunategemea sana Kamati hizi za Rufaa zilizoundwa katika kila Wilaya Nchini kote, katika kutenda haki na kuweka mambo yote sawa ili  kila mtu awe na amani na tukamilishe zoezi la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa” alisema Jafo.

Aliongeza kuwa katika mchakato huu musimuonee aibu yeyote na wala msimuonee au kumpendelea mtu katendeni haki kwa watu watakaoleta  malalamiko yao kwenu ili kila mtu afurahie Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na ukamalike kwa amani

Ndio maana mmechaguliwa kutoka Taasisi za Ummambalimbali na  hamkutoka katika ofisi moja kila mmoja wenu katoka kwenye Taasisi yake hii itasaidia kupunguza mgongano wa maslahi kwa kuwa ninyi wengi hamfanyi kazi katika Serikali za Mitaa.

“Pimeni malalamiko kwa weledi wenu na kufuata Kanuni toeni maamuzi stahiki, inawezekana kabisa kwa Kamati ya Rufaa ikamrudisha mtu kwenye nafasi yake mbayo aliyeunguliwa hapo awali mkiona anastahili kwa mujibu wa vielelezo alivyowasilisha mrejesheni hiyo ndio kazi yenu kubwa katika kamati hii” Alisema Jafo.

Aliongeza kuwa wagombea wote ambao kuna baadhi ya vitu wanaona havikwenda sawa huu ndio wakati sasa wa kuviwasilisha kwenu ili muweze kuhakiki na kufanya maamuzi ya busara yanayofuata utaratibu, sheria na maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni Uchaguzi wa Wananchi, ni vyema michakato yote ikafanyika kwa haki kwenye ngazi zote haswa hii ya kugombea nafasi za uongozi haki inatakiwa kuonekana imetendeka hivyo  Kamati ya Rufaa nawaelekeza fanyeni kazi hii kwa haki, mkijiamini na kutoa maamuzi yatakayomaliza malalamiko ya wagombea alimalizia Jafo.


Share:

Wito Wa Wadau Kutoa Maoni Juu Ya Muswada Na Maazimio Kabla Haijaridhiwa Na Bunge




Share:

KARIBU INVO ENTERPRISES KWA HUDUMA ZA USAFI WANYUMBANI,OFISINI,HOTELINI,KANISANI ..N.K

Share:

WAZIRI MKUU AWASHUKURU WALIOJITOKEZA KWENYE MAZISHI YA KAKA YAKE


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewashukuru watu wote waliojitokeza katika mazishi ya kaka yake Mzee Bakari Majaliwa (78), aliyefariki juzi (Jumatatu, Novemba 04, 2019) nyumbani kwake katika kijiji cha Chimbila ‘B’wilayani Ruangwa, Lindi.


Ametoa shukrani hizo leo (Jumatano, Novemba 06, 2019) wakati wa ibada ya mazishi iliyofanyika kijijini Nandagala wilayani Ruangwa na amesema kwamba hayo ni mapenzi ya Mwenyezi Mungu na kila mtu atapita kwenye njia hiyo.

“Tulikuwa 12 na sasa tumebaki watano, wanaume wawili na wanawake watatu. Msiba huu kwetu ni mkubwa umepunguza idadi ya watoto wa Mzee Majaliwa lakini hatuna namna ni mapenzi ya Mwenyezi Mungu, wajibu wetu ni kuendelea kumuombea. Nawashukuru wote mlioacha shughuli zenu na kutukimbilia, familia imethamini sana ujio wenu jambao hili limetokea ghafla.”

Waziri Mkuu pia amemshukuru Rais Dkt. John Magufuli kwa salamu za pole alizozitoa. “Jambo hili pia limemgusa Mheshimiwa Rais wetu ambaye ametutaka tuwe watulivu katika kipindi hiki kigumu na kwamba kila mmoja kwa dhehebu lake aendelee kumuombea marehemu ili Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema.”

Amesema alipata taarifa za msiba huo wakati akijiandaa kwenda wilayani Ruangwa kwa ajili ya kushiriki mazishi yamwanasiasa mkongwe na Mwenyekiti wa zamani wa CCM wa Wilaya ya Ruangwa, Bw. Kaspar Selemani Mmuya.

Kwa upande wake, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Generali, Venance Mabeyo akitoa salamu za pole kwa niaba ya Maafisa na Askari wa Vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama amesema anajua uzito wa msiba pamoja na majonzi waliyonayo kwa kuondokewa na mpendwa wao na kwamba wamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwa ndiye anayetoa na anayetwaa. “Hakuna namna ya kurekebisha maamuzi ya Mwenyezi Mungu, tuendelee kumsindikiza kaka yetu kwa sala Mwenyezi Mungu ampokee kwa amani.”

Naye, Mwakilishi wa Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Othman Kaporo amesema amewataka wananchi wajiandae na kifo kwa kufanya ibada. “Ni kawaida kwa binadamu kujisahau lakini Mwenyezi Mungu ametuwekea vitu vya kutukumbusha juu ya uwepo wake ikiwemo kifo, hivyo tuyatekeleze yale yalikuwa ya wajibu kuyatekeleza.”

 (mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,


Share:

MWENYEKITI AUAWA AKITATUA MGOGORO WA ARDHI KIJIJINI

Mwenyekiti wa Kamati ya Mazingira wilayani Kiteto mkoani Manyara, Engerusi Mikonde (59), ameuawa katika shamba moja akiwa kwenye harakati za kutatua mgogoro wa ardhi ambao unadaiwa kuwa ungeleta madhara kati ya wakulima hao.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Augostino Senga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo akisema uchunguzi unaendelea na kwamba mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya wilaya Kiteto.

Mmoja ya wakazi walioshuhudia tukio hilo Daiomoni Nzungu, amesema Mikonde akiwa na kamati ya mazingira kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wa wakulima Kijijini hapo, alishambuliwa kwa marungu na mapanga hadi alipokutwa na umauti.

Baadhi ya wananchi wamelitaka jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa kina juu ya tukio hilo wakisema kuwa suluhu ya sakata hilo ni kupatikana kwa taarifa ya kina ili sheria ifuate mkondo wake kwa waliohusika.

Migogoro mingi ya wakulima na wafugaji wilayani Kiteto huanza kipindi ambacho wakulima wanaandaa mashamba huku wafugaji wakihitaji maeneo kwaajili ya shughuli za kufugia mifugo yao.
CHANZO - MTANZANIA
Share:

TIGO INAVYOREJESHA TABASAMU KWA WAGONJWA WA MGUU KIFUNDO

Mkurugenzi mtendaji (Tigo) Bw. Simon Karikari akimkabidhi mfano wa hundi ya Mil 110/- Ofisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Brenda Msangi.Hafla ya makabidhiano yalifanyika katika wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika hospitali ya CCBRT
****

Siku zote ni furaha pale mwanamke anapopata mtoto ambaye alimtarajia kwa takribani miezi tisa ya ujauzito.Hii ilidhihirika kwa Salma Hajj (29) baada ya kujifungua salama mtoto wake wa kwanza wa kiume miezi kumi iliyopita.

Hatahivyo, furaha ya Salma haikudumu.Baada ya muda mfupi, Salma ambaye ni mkazi wa Buza jijini Dar es Salaam furaha yake ilitokweka baada ya kugundua kuwa mwanae wa huyo alikuwa na tatizo la miguu kujikunja pasipo kujua ni nini tatizo.

Tatizo hilo linajulikana kama ‘mguu kifundo’ au kwa kiingereza linafahamika kama ‘Clubfoot’ ambalo kisayansi linalotokea hata kabla ya mtoto kuzaliwa.

Kila mwaka zaidi ya watoto 100,000 duniani huzaliwa na ugonjwa huu ambao humfanya mtoto kushindwa kutembea kwa kutumia unyayo na badala yake hutumia kifundo cha mguu.

Kwa Tanzania,inakadiriwa kuwa karibuni watoto 2,800 wanazaliwa na ugonjwa huu kila mwaka.Kati yao asilimia 50 wana athirika mguu mmoja huku waliobaki wakiathirwa miguu yote miwili.
Asilimia 80 ya wagonjwa wasiopata matibabu yake wanapatikana kwenye nchi zinazoendelea, ikiwamo Tanzania.Kama ugonjwa huu usipotibika unaweza kusababisha maumivu makali wakati wa kutembea na hatimaye husababisha ulemavu wa muda mrefu.

“Kiukweli ulikuwa ni wakati mgumu sana kwangu.Nilijisikia vibaya kwamba mwanangu hataweza kutembea vizuri na hatahivyo sikujua anasumbuliwa na tatizo gani kwa kipindi kile,” anasema Salma.

“Nilihisi kama ilikuwa mwisho wa dunia kwangu na mwanangu; nilijiuliza maswali mengi bila majibu kwamba atawezaje kutembea? ataonekanaje kwa watu? atasoma katika shule gani? nilichanganyikiwa sana,” anasema Salma.

Mmoja wa mtoa huduma (nesi) alimjulisha kuwa tatizo hilo linaweza kutibika katika Hospitali ya CCBRT iliyoko Msasani jijini Dar es Salaam bila malipo.Kilichofuata ilikuwa ni kutembelea hospitalini hapo ambapo madaktari walianza kutoa matibabu kwa mtoto wake kwa miezi michache tu.

Kwa mujibu wa daktari wa mifupa (Orthopedic) wa CCBRT, Dk. Zainab Ilonga, anasema chanzo cha ugonjwa huo bado hakijulikani.

Anasema hadi sasa sababu yake bado haijathibitika lakini wanaamini kuwa moja ya sababu ni matumizi ya pombe na matumizi mabaya ya madawa wakati wa ujazuzito au urithi wa vinasaba (genetic) na kwamba tafiti zaidi zitasaidia kutambua chanzo halisi cha tatizo hilo.

“Kuna njia mbili za kutibu ugonjwa huu wa mguu kifundo;moja ni kutumia njia ya Ponseti ambayo haihitaji kufanya upasuaji na nyingine ya kufanya upasuaji,” Dk Ilonga anasema na kuongeza 

“Kwa Tanzania tunatibu watoto takribani 400 kwa mwaka sawa na asilimia 25 ya wagonjwa wote na hii inatokana na baadhi ya wazazi kuwanawaficha watoto wenye tatizo hili.”

Ignacio V. Ponseti ni njia ambayo imekuwa ikitumia kutibu mguu kifundo tangu miaka ya 1940.Moja ya kanuni ya njia hii ni kwamba tishu za mtoto ikiwamo tendoni, ligamenti na maungio yake yapo katika hatua ya ukuaji hivyo kufanya mguu kuungana baada ya kila wiki moja.

Kwa kutumia njia hii ndani ya wiki kadhaa hali ya mgonjwa inaweza kubadilika na kufanikisha kurekebisha mguu bila uhitaji wa kufanya upasuaji.

Mtoto wa Salma alipitia hatua hiyo maarufu kama ‘gentle bone manipulations’ na ufuatiliaji (castings) ili kujua mabadiliko ya kibaolojia hasa misuli yake, maungio na tishu kwa lengo la kutibu tatizo alilokuwa nalo. 

“Kuna wakati alikuwa anapitia wakati mgumu kwani alikuwa analia sana jambo lililonifanya na mimi kulia.Nilikuwa na wasiwasi juu ya maisha ya mwanangu siku za mbeleni,” anasema kwa huzuni.

“Nawashukuru sana Tigo na madaktari wa CCBRT kwa msaada wao mkubwa kwasababu saizi mtoto wangu ana miezi kumi na amepona kabisa,” anasema Salma huku akiwa na uso wa furaha.

Afisa wa Uwajibikaji kwa Jamii wa Tigo, Halima Okash anasema 

“Tuliona kuna umuhimu wa kusaidia wahitaji hawa kwa sababu CCBRT inahudumia jamii yenye uhitaji na wasiojiweza katika kuwasaidia kupata huduma za matibabu.Tumeunga mkono jitihada hizi zinazofanywa na CCBRT kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapata nafasi ya kutibiwa kwa gharama ndogo au bure kabisa,” anasema Okash.

Kupitia huduma za upasuaji kutoka hospitali ya CCBRT jumla ya watoto 1,509 wamenufaika katika kipindi cha miaka sita iliyopita. 

“Haya ni mafanikio yanayotufanya sisi Tigo kujisikia faraja kwa kiasi kikubwa kwani kwa kutoa matibabu kwa watu wenye ulemavu,Tigo na CCBRT tunaleta matokeo chanya kwa maisha ya mtu mmoja mmoja, familia na jamii ya Tanzania kwa ujumla,” anasema Okash.

Tangu mwaka 2013, Tigo iliingia ubia na hospitali ya CCBRT kutoa matibabu kwa wagonjwa wa midomo sungura, kwa kutumia njia ya jumbe (SMS) zinazotumwa kwa wagonjwa wa CCBRT kuwakumumbusha kufuatilia matibabu na kutoa uelewa kuhusu huduma kwa umma.

Kupitia mpango huu, wagonjwa wanaweza kupata jumbe za matibabu kwa siku nne na siku moja kabla ya siku ya matibabu na hii imeisaidia CCBRT kupunguza idadi ya wagonjwa wanaokatisha matibabu.

Kwa msaada wa Sh110, 0000,000 kwa mwaka kutoka Tigo, CCBRT inaweza kutoa huduma za matibabu kwa njia Ponseti (bila upasuaji) kwa wagonjwa wapya zaidi ya 400 na wengine wanaoendelea na matibabu hospitalini hapo.

Share:

Sekta Ya Ngozi, Nyama Na Maziwa Zaundiwa Kozi Fupi Vyuoni

Na. Edward Kondela
Serikali imewataka wadau kwenye sekta ya ngozi, nyama na maziwa wanaoandaa mitaala kwa ajili ya vyuo kufundisha kozi fupi katika sekta hizo ngazi ya cheti na diploma kupitisha mitaala bora itakayohakikisha wanafunzi watakaohitimu mafunzo wanaleta matokeo chanya katika sekta hizo kwa wananchi na taifa kwa ujumla.

Akizungumza Jijini Dodoma wakati akifungua kikao kilichowahusisha wadau katika sekta za ngozi, nyama na maziwa kutoka serikalini na taasisi binafsi Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel amesema ili kupata malighafi bora zinazotokana na sekta ya ngozi, nyama na maziwa ni lazima wataalam ambao wamesomea sekta hizo ngazi ya cheti na diploma wawekewe mazingira ya kuhakikisha wanatumia utaalam watakaoupata kupitia vyuo mbalimbali baada ya kupitishwa kwa mitaala hiyo ili iwe na tija kwa taifa.

“Mitaala mnayokwenda kupitia na kuzungumzia lazima ijibu mahitaji ya wadau katika sekta tatu yaani ngozi, nyama na maziwa isiwe kuwa na cheti baada ya kuhitimu mafunzo ngazi ya cheti au diploma hawa wataalamu wa ngazi ya kati ndiyo wanaotegemewa kwenda kufanya kazi za vitendo, hakikisheni mnapata mitaala ambayo itakuwa na manufaa.” Amesema Prof. Gabriel

Aidha Prof. Gabriel amewataka wadau hao kubainisha njia bora za kufundishia mara baada ya kupitishwa kwa mitaala hiyo ili kuhakikisha wanafunzi watakaodahiliwa wanaelewa vizuri pamoja na kuwa na utaratibu mzuri wa kuwapata watu ambao wanafundishika na wawe tayari kupokea mafunzo hayo.

Akibainisha juu ya jamii kuwa na ufugaji wenye tija, katibu mkuu huyo amewaasa wadau wa mifugo wajenge utamaduni wa kuwatumia wataalam hususan wa ngazi ya kati ili waweze kufuga kisasa na kunufaika kupitia mifugo yao badala ya kufuga kwa mazoea na hatimaye kupata hasara.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Utafiti, Ugani na Mafunzo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Angello Mwilawa amesema mjadala wa kuandaa mitaala kwa ajili ya kufundisha vyuoni kozi fupi katika ngazi ya cheti na diploma kwenye kwenye sekta ya ngozi, nyama na maziwa umetoka kwa wadau, hivyo wizara ikashirikisha taasisi mbalimbali likiwemo Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ili kukamilisha mitaala hiyo.

Dkt. Mwilawa amefafanua kuwa mara baada ya kukamilika kwa taratibu za kuandaa mitaala hiyo vyuo vya serikali kwa kushirikiana na binafsi vitaanza kutekeleza kwa kutoa mafunzo ya tasnia ya ngozi, nyama na maziwa katika ngazi ya cheti na diploma.

Akielezea umuhimu wa serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuandaa mitaala hiyo, Katibu wa Chama cha Wafugaji Tanzania Bw. Magembe Makoye ameipongeza Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kuhakikisha sekta ya mifugo inasimamiwa vyema kupitia mambo ya kisera na kisheria ambayo ndiyo yamekuwa yakisimamia pamoja na kutunga kanuni mpya zenye lengo la kuhakikisha sekta ya mifugo inathaminiwa zaidi.

Bw. Makoye amesema sekta ya mifugo ambayo inaajiri watu wengi kote nchini kupitia mafunzo yatakayoanza kutolewa vyuoni mara baada ya kupitishwa kwa mitaala hiyo kutachangia kwa kiasi kikubwa kuongeza thamani ya sekta ya ngozi, nyama na maziwa kwa kuwa wafugaji sasa wataongezewa taarifa na maarifa kupitia kwa wataalamu watakaohitimu mafunzo hayo.

Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya ngozi, nyama na maziwa pamoja na taasisi mbalimbali likiwemo Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) inapitia mitaala kwa ajili ya kuanzishwa kwa kozi fupi ngazi ya cheti na diploma katika sekta hizo kwenye vyuo vya serikali na binafsi ili kuyaongezea thamani zaidi mazao ya ngozi, nyama na maziwa kwa kuwa na waatalamu wengi zaidi ngazi ya kati walipobobea katika sekta za ngozi, nyama na maziwa.


Share:

Serikali Yapiga Marufuku Walengwa Wa Tasaf Kulazimishwa Kuchangia Bima Za Afya Na Michango Ya Kijamii

Na. Aaron Mrikaria-Dodoma
Serikali imewaagiza Viongozi wa Vijiji kutowalazimisha walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kukatwa ruzuku kwa ajili ya kuchangia bima za afya na michango mbalimbali ya kijamii kwani ruzuku hiyo hutolewa na Serikali kwa ajili ya kuziwezesha kaya maskini kujikwamua kiuchumi.

Agizo hilo limetolewa Bungeni leo na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Kapt.

(Mst) Mhe. George H. Mkuchika (Mb), wakati akijibu swali la Mbunge wa Bahi, Mhe. Omary Ahmed Badwel aliyetaka kujua Utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika vijiji vyote nchini.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema, ruzuku inayotolewa na Serikali kwa walengwa ni kwa ajili ya kuwawezesha kupata mahitaji ya msingi kama vile chakula, gharama za elimu na Afya na kuwekeza katika kuanzisha miradi itakayowaongezea kipato na hatimaye kujikwamua na umaskini, hivyo ni maamuzi ya kaya husika kupanga matumizi ya ruzuku wanayoipata.

“Katika baadhi ya maeneo, Viongozi wa Vijiji wamekuwa wakiwalazimisha walengwa kukatwa ruzuku ili kulipia bima za afya na michango mbalimbali jambo ambalo si sahihi na halikubaliki”, Mhe. Dkt. Mwanjelwa amefafanua.

Aidha, Dkt. Mwanjelwa ameelekeza walengwa kutokatwa ruzuku moja kwa moja bila ridhaa yao bali wapewe stahiki zao na kama kuna michango ya shughuli za maendeleo ya kijiji inapaswa kutozwa kwa wananchi wote wa kijiji husika.

Dkt. Mwanjelwa amewataka viongozi wote waliokuwa wanatoa amri ya kukatwa kwa ruzuku za walengwa wa TASAF moja kwa moja bila ridhaa yao, waache mara moja kwani ni kinyume cha utaratibu na iwapo wataendelea, Serikali itawachukulia hatua za kali za kinidhamu na kisheria.

Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini tangu uanze kutekelezwa na Serikali mwaka 2013 umezinufaisha kaya maskini kwa asilimia 70, na hivi sasa Serikali inajiandaa kuanza utekelezaji wa Awamu ya Tatu sehemu ya pili mwishoni mwa mwaka huu baada ya Serikali kupata fedha lengo likiwa ni kuzifikia kaya zote maskini nchini


Share:

Serikali Yasema Haitaingilia Kupanga Bei Msimu Ujao Wa Pamba

Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema kuelekea msimu ujao wa pamba serikali itajitahidi kupunguza gharama na kwamba haitaingilia kupanga bei bali watatafuta njia nyingine za kumlinda mkulima na kuhakikisha hapati hasara.

Ametoa kauli hiyo bungeni leo Jumatano Novemba 6, alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Busega (CCM), Dk. Raphael Chegeni aliyetaka kupata tamko la serikali kuhusu wakulima wa pamba ambao waliuza pamba tangu Mei mwaka huu lakini hawajalipwa fedha zao.

“Wakulima wa pamba ambao mwaka hadi mwaka wamekuwa wakifanya kazi ya kulima wamekuwa wakipata hasara kwa mfano leo hii wakulima wa Mkoa wa Simiyu hasa wa Wilaya ya Busega wameuza pamba tangu mwezi Mei mpaka leo hawajaliwa fedha zao sasa hauoni kwamba hii ni kuwakatisha tamaa wakulima wasiweze kufanya kilimo kizuri zaidi na nini tamkola serikali juu ya hili,” amehoji.

“Ninakiri kuwa baadhi ya wakulima wa pamba hawajalipwa fedha zao, kwa mwaka huu mpaka sasa hivi jumla ya bilioni 417 zimeshalipwa kwa wakulima wa nchi nzima, ambao hawajalipwa wanadai bilioni 50 kufikia sasa hivi na sababu ya msingi ni lazima tufahamu kwamba asilimia zaidi ya 80 ya pamba inakwenda nje ya nchi, wanunuzi wetu wanakabiliwa na mtikisiko wa bei ambao umewakabili katika soko la dunia na sisi kama nchi tulitoa maelekezo ya bei ya kununulia na haya yalikuwa maamuzi ya serikali kwaajili ya kumlinda mkulima asipate hasara.

“Pamba yote iliyokuwa kwa wakulima imeshakusanywa sasa hivi kilichobaki mikononi mwa wakulima ni tani 5,000 tu ambayo tunaamini msimu unapoanza pamba yote ya wakulima itakuwa imeondoka, tunajitahidi kupunguza gharama msimu huu unaokuja na hatutaingilia kupanga bei, jukumu letu litakuwa ni kuhakikisha mkulima hapati hasara kwa kutafuta njia nyingine za kumlinda kuliko kumuathiri mnunuzi,” amesema Bashe.


Share:

Waziri wa Nishati, Medard Kalemani Atoa ONYO Kwa mameneja na wakandarasi wanaotoza Wananchi Gharama ya nguzo za umeme

Waziri wa Nishati, Medard Kalemani ametoa onyo kwa mameneja na wakandarasi wanaotoza nguzo za umeme wananchi na kuwataka waachane na tabia hiyo mara moja kwakua serikali imegharimia nguzo hizo kwa asilimia 100.

Waziri Kalemani ametoa kauli hiyo bungeni leo Jumatano Novemba 6, katika kipindi cha maswali na majibu alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Halima Bulembo aliyetaka kujua serikali inazungumzia vipi kadhia ya kulipishwa nguzo za umeme ambayo wananchi wa Mkoa wa Kagera wamekuwa wakikumbana nayo

Akijibu hoja hiyo Waziri Kalemani amesema serikali haitaendeleakufumbia macho suala hilo na kwamba yeyote atakaekamatwa atachukuliwa hatua za kisheria bila kujali cheo chake.

“Yapo maeneo bado wakandarasi na mameneja wa Tanesco wanaendelea kutoza nguzo wateja, ninaomba nitoe tamko kali sana kwamba ni marufuku kutoza nguzo kwa wateja wote, awe mkandarasi, Meneja wa Tanesco au kibarua na hii ni kwasababu serikali imegharamia kwa asilimia 100,” amesema Dk. Kalemani.

Aidha amesema serikali imekuwa ikipeleka umeme katika maeneo yote hasa vijijini lakini baadhi ya taasisi zimekuwa hazilipiwi na hivyo amewataka wamiliki wa taasisi hizo kuhakikisha wanalipa kiasi cha Sh 27,000 ili taasisi zote zipelekewe umeme.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger