Tuesday, 22 October 2019

Ofisa Takukuru atiwa mbaroni kwa madai ya kumuua Mkewe kwa Risasi

Ofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wilayani Tunduru, James Paulo (27), anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuua kwa kumpiga risasi mke wake.

Mtuhumiwa huyo anadaiwa kufanya kitendo hicho usiku wa kuamkia Oktoba 21, mwaka huu, baada ya kutokea ugomvi kati yao.

Kamanda Polisi Mkoa wa Ruvuma, Simon Maigwa, amethibitisha kuwapo kwa tukio hilo na kwamba chanzo cha kifo hicho ni ugomvi uliosababishwa na tukio la wivu wa kimpenzi.

Kamanda alimtaja mtu aliyeuawa kuwa ni Beatha Kufuru (25), ambaye alikuwa muuguzi katika Hospitali ya Wilaya ya Tunduru.

Kamanda Marwa ambaye alikuwa akizungumzia tukio hilo akiwa njiani kwenda Tunduru ili kujiridhisha na hali halisi, alisema mtuhumiwa huyo alimpiga risasi tatu kichwani na kusababisha kifo chake papo hapo.

Alisema polisi wanaendelea na uchuguzi wa tukio hilo na kwamba mtuhumiwa atafikishwa mahakamani baada ya kukamilika kwa taratibu za kisheria.


Share:

Wizara Ya Kilimo Yaja Na Mkakati Wa Kuzalisha Miche Milioni 20 Ya Kahawa

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Kilimanjaro
Moja ya changamoto katika kuimarisha ubora wa Kahawa ni uzalishaji mdogo ya Miche ya Kahawa huku mahitaji yakiwa ni makubwa kwa wakulima.

Wizara ya Kilimo imekusudia kuzalisha mbegu mpya ambazo ni bora za kahawa kwa lengo kubwa la kubadilisha mikahawa ya zamani ipatayo milioni 240 kwa kutumia aina mpya za kahawa.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo tarehe 21 Octoba 2019 wakati wa uzinduzi wa vitabu vya kanuni bora na mitaala ya ufundishaji katika zao la Kahawa katika Ofisi za Taasisi ya utafiti wa Kahawa TACRI Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro.

Alisema kuwa uzalishaji wa idadi ya miche milioni saba (7) kwa mwaka ni kidogo, ambapo itatuchukua takribani Miaka 35 kubadili aina hizi za zamani hivyo aliahidi kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau wa kilimo itahakikisha kunakuwa na mapinduzi ya Kilimo cha kahawa nchini.

Katika kuifikia dhamira ya kubadili mikahawa ya zamani serikali kupitia wizara ya kilimo imejipanga kuanza kuzalisha Miche milioni 20 ya kahawa mpya ili kuongeza tija na uzalishaji wa kahawa.

Amesema kuwa sekta ndogo ya kahawa ina umuhimu mkubwa kwenye uchumi wa taifa na huchangia takribani asilimia 24 kwa mwaka ya mapato ya mauzo ya bidhaa za kilimo nje ya nchi, ambapo ni wastani wa asilimia 4 ya pato la taifa.

Hata hivyo, pamoja na mchango huo wa sekta ndogo ya kahawa uzalishaji bado ni mdogo sana, ambapo kwa mwaka wastani wa tani 50,000 huzalishwa.

Aliongeza kuwa hali hiyo inasababishwa na tija ndogo ambapo mpaka sasa mti mmoja wa kahawa unatoa gramu 250 ikilinganishwa na wastani wa gramu 1,000 inayotakiwa kuvunwa kwa mti.

Moja ya changamoto inayosababisha tija kuwa chini katika sekta ndogo ya kahawa ni ukosefu wa elimu ya kanuni bora ya kilimo cha kahawa kwa wakulima ambapo amewataka maafisa kilimo kote nchini kuanza kutoa elimu kwa wakulima juu ya umuhimu wa mikahawa mipya.

Alisema ili kuhakisha kuwa mkulima anapata tija kubwa na kuongeza kipato kutokana na kilimo cha kahawa, ni muhimu kupata elimu ya uzalishaji wa kahawa kwa kuzingatia matumizi sahihi ya kanuni bora za kilimo cha kahawa.

Waziri Hasunga ameipongeza TaCRI kwa kuandaa vitabu vilivyozinduliwa kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu kanuni bora za utunzaji wa kahawa aina ya Arabika na Robusta pamoja na mitaala ya mafunzo ambavyo vitatumika kwa Maafisa Ugani, Wakulima na Wananchi wote wenye nia ya kujifunza mbinu bora za kilimo cha kahawa chenye  tija.

Mhe Hasunga amesema kuwa Vitabu hivyo vyenye picha na maelezo ya kutosha vimelenga kuwapa wakulima wa kahawa utaalamu wa kukuza zao la kahawa katika lugha rahisi ambapo lengo la vitabu hivyo ni kuhakisha kuwa kaya za wakulima wa kahawa zipatazo 420,000 nchini; wanakuwa na rejea ya haraka na rahisi wakati wote wawapo shambani, mahali ambapo hawana wataalamu; na pale ambapo kutakuwa na mtaalamu vitakuwa vichocheo vya mazungumzo ili kuweza kujua zaidi au kupata ufafanuzi wa kitaalamu wa masuala ya kilimo cha kahawa.



Share:

Askofu Ezekiel Yona wa kanisa la Morovian Jimbo la Magharibi apiga Marufuku kwa Makasisi wa kanisa hilo kutumia mafuta chumvi na maji katika maombi

NA SALVATORY NTANDU
Makasisi na Mashemasi  wa kanisa la morovian jimbo la Magharibi wametakiwa kutojihusisha na vitendo vya  udanganyifu vinavyofanywa na baadhi ya Watoa maombi ambao wamekuwa wakitumia chumvi na maji pamoja na mafuta kuwahadaa waumini wanao hitaji maombi badala yake wafuate maelekezo ya Yesu kristo aliyokuwa akiyatumia katika maombi.

Kauli hiyo imetolewa jana na Askofu wa kanisa la Morovian Ezekiel Yona wa Jimbo la Magharibi katika hafla maalum ya kuliweka wakifu wa jengo jipya la kanisa la moroviani la kahama mjini pamoja na kuwa kuwasimika mashemas 17.

Askofu Yona amewataka Makasisi hao kuepuka maombezi yanayokwenda kinyume na taratibu mungu na badala yake wafuate taratibu na miongozo ya kanisa hilo ambayo ni mafundisho ya kristo ili kuendelea kutangaza habari njema kwa watu wote.

“ Kinachonitatanisha ni kitu kimmoja sasa hivi wapo baadhi ya  watoa huduma za maombi wanaowanywesha mafuta waumini wao na kisha wanaanguka chini na baadae wanawaombea na kuamka,vitendo hivi msivifanye na havikubaliki katika kanisa la Mungu”alisema Askofu Yona.

Katika hatua nyingine Askofu Yona amewataka Makasisi hao kuendelea kuliombea Taifa ili amani iendelee kudumu sambamba na kumwombea Rais John Pombe Magufuli ili aendelee kuwatetea wanyonge sanjari na kurudisha nidhamu serikalini kwa kusimamia rasilimali za nchi.
  
Nao baadhi ya Makasisi wapya waliopewa daraja hilo, Emanuel Sangosango kutoka Kanisa la Morovian kituo cha (SAUTI)Mwanza na Yona Mbogo wa kanisa la Morovian kituo Singida wameahidi kuwa waaminifu katika utoaji wa huduma kwa waumini wao pamoja na kujiepusha na maombi yasiyofuata mafundisho ya Mungu.

Wamesema wapo baadhi ya Wachungaji ambao wanatumia vitu kama vile mafuta, chumvi na maji kuwahadaa waumini wao ili kupona magonjwa mbalimbali waliyonayo jambo ambalo sio la kweli na kutoa rai kwa waumini kuepuka maombi ya namna hiyo.


Share:

Waziri Jafo Awataka Wakurugenzi Wasiotimiza Ukusanyaji Mapato Kujitathimini.

Na.Faustine Galafoni.Dodoma.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa ma Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh.Selemani Jafo amewataka wakurugenzi wasiotimiza lengo la ukusanyaji mapato katika Halmashauri zao kujitathimini.

Waziri Jafo ameyasema hayo    Oktoba 21,2019 Jijini Dodoma  wakati akitoa taarifa ya mapato ya vyanzo vya ndani ya Halmashauri kwa kipindi cha Mwezi Julai hadi Septemba mwaka 2019. .

Waziri Jafo amesema kuwa katika kuzipima Halmashauri zote kwa pamoja katika kipindi hiki imeonyesha kuwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma imeongoza kwa ukusanyaji mapato kuliko Halmashauri zote kwa kukusanya Shilingi Bilioni 13.10,huku Mapato ya ndani kimkoa kwa kuzingatia wingi wa mapato Mkoa wa Dar es Salaam umeongoza kwa kukusanya kiasi cha Shilingi Bilioni 39.53

Pia Waziri Jafo amesema licha ya Serikali kuagiza ukusanyaji wa mapato kufanyika kwa njia ya kielektroniki lakini bado kuna Changamoto kwani kuna baadhi ya maeneo wanakusanya fedha na hawazipeleki benki hivyo kuwaagiza wakuu wa mikoa kusimamia suala hilo.

Ikumbukwe kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma imekuwa ya mwisho katika pato ghafi kwa kukusanya Milion 35 kwa kipindi cha miezi mitatu na hivyo kumtaka Mkurugenzi wa halmashauri hiyo pamoja wengine ambao hawajafanya vizuri kujitathimini huku uchambuzi ukionesha kuwa katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2019/20,Jumla ya Halmashauri 54 kati ya Halmashauri 185 zimefanya vizuri kwa kukusanya mapato ya ndani kwa zaidi ya asilimia 25 ya makisio ya mwaka wa Fedha 2019/20.


Share:

RC GAGUTI ATOA SIKU TATU HALMASHAURI YA BUKOBA KUHAMIA ENEO JIPYA


Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti 

Na Lydia Lugakila - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti ametoa siku 3 kwa Halmashauri ya Bukoba Mkoani Kagera kuhamia katika eneo jipya  la Bujuna ngoma lililopo katika kata ya Kemondo ili waweze kutoa huduma kwa wananchi wakitokea katika eneo hilo.

Mkuu wa mkoa wa Kagera Bligedia Jenerali Gaguti ametoa Agizo hilo jana Oktoba 21, 2019 katika kikao cha kamati ya Ushauri ya mkoa kilichofanyika katika ukumbi wa mkoa huo uliopo katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.

Mhe. Gaguti amesema tayari uongozi wa Halmashauri umeandikiwa barua kwa ajili ya kuhamia eneo hilo ambapo amewataka viongozi hao wa Halmashauri kuanza upya mchakato wa kutafuta eneo jipya la makao makuu ya Halmashauri kwa kuwashirikisha wananchi ,wadau, pamoja na viongozi kwani ndiyo watakuwa watumiaji wa mamlaka hayo.

Amesema madiwani ni sehemu ndogo ya maamuzi ya kuhamisha Halmashauri ikiwa mchakato huo unapaswa kurudi kwa wadau ili waweze kupendekeza eneo litakalohudumia watu wengi kama malengo yaliyokusudiwa.

"Natoa siku tatu huduma lazima zianze kutolewa kutokea makao makuu ya halmashauri ya wilaya ya Bukoba mpango huo uwe shirikishi kwa kina", Gaguti. 

Agizo hilo limetolewa ikiwa zimepita siku tano za baraza la madiwani wa Halmashauri hiyo kupitisha eneo la kata ya Kemondo kuwa makao makuu ya Halmashauri hiyo.

Hata hiyo akitoa matokeo ya upigaji wa kura ya kuchagua eneo la kuhamia , mwenyekiti wa halmashauri hiyo Murshid Ngeze alisema maeneo yaliyokuwa yamependekezwa ni matatu ambapo eneo la kwanza lilipata kura moja, la pili kumi na sita na eneo la Bujuna ngoma lililopo katika kata ya Kemondo kupata kura 22.

Share:

SERIKALI KUVIPATIA UMEME VIJIJI VYOTE 56 VYA WILAYA YA SIMANJIRO

Na Beatrice Mosses - Manyara
WAZIRI wa Nishati Dkt. Medadi Kalemani amesema serikali itavipatia Umeme vijiji vyote 56 vya Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara ifikapo mwezi Juni mwaka 2020.

Waziri Kalemani  aliyasema hayo juzi  katika mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro wakati wa ziara yake ya kukagua na kufuatilia utekelezwaji wa upelekaji umeme vijijini ambapo alisema mkoa wa Manyara  pekee hadi sasa umeshapokea zaidi ya shilingi Bilioni 31 kwa ajili ya upelekwaji umeme vijijini.

Waziri wa Nishati Dkt  Medadi Kalemani  alifika katika Kijiji cha Naepo na Olibili Wilayani Simanjiro  mkoani Manyara kubwa ni kukagua kazi ya upelekaji umeme kwa wananchi pamoja na kuwasha umeme shule ya msingi Naepo na shule ya sekondari Shambarai.

“Ndugu zangu wana Simanjiro mna vijiji 56 na vitongoji 275 vyote vinakwenda kupata umeme ifikapo mwishoni mwaka mwaka ujao Mh. Rais katupatia fedha kwenye mkoa mzima wa Manyara na Simanjiro ikiwemo  jumla ya sh. Bil. 31.12.

“Rais anawakumbuka kwenye mabarabara, anawakumbuka kwenye shule lakini pia anawakumbuka kwenye masuala ya umeme, leo ninyi ni mashahidi shule hii ina zaidi ya miaka 18 ilikuwa haina umeme”, Alisema Kalemani.

Aidha Dkt Kalemani aliwataka wananchi wa kijiji cha Naepo kujitokeza kwa wingi kujiandikisha ili waweze kupelekewa umeme kwenye nyumba zao kwa bei ya sh. 27,000 kwani gharama zingine serikali ilishagharamikia.

“Niwaombe wananchi kama una nyumba yako wewe na inawezekana ni ya makuti au ni ya majani zote zinastahili kuwekewa umeme hakuna nyumba isiyofaa kuwekewa umeme na ole wake Mkandarasi  au  Meneja atakaye ruka nyumba ati kwa sababu ni mbaya utakuwa wewe mbaya lakini nyumba itabaki salama”, Alisema.

Dkt Kalemani alitoa maelekezo ya kwa ofisi ya Tanesco mkoani Manyara kufungua dawati la kuwahudumia wananchi kwani kutoka wilayani hadi kijiji cha Naepo ni zaidi ya km 20.

“Kwa hiyo kituo cha kuandikisha wanaohitaji kupatiwa umeme kibaki hapahapa msiende wilayani wao watawafuata hapa hata ukiwa  na pesa kidogo unaiweka hapa ukikamilisha sh. 27,000 unaunganishiwa umeme”, Alieleza Dkt Kalemani.

Wananchi kwa upande wao wakaishukuru serikali lakini wakawa na ombi kwa Waziri wa Nishati ili aweze kuwafikishia umeme kambi ya Chokaa kwa kuwa eneo hilo lipo katikati ya vijiji ambavyo vina umeme.

Waziri Kalemani akawahakikishia wananchi wa Simanjiro  kuwa kila nyumba na Kitongoji kitapata umeme
Share:

Project Lead, Tools for Integrated Management of Childhood Illness Job Opportunity at PATH

Project Lead, Tools for Integrated Management of Childhood Illness Job Opportunity at PATH  

The post Project Lead, Tools for Integrated Management of Childhood Illness Job Opportunity at PATH appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Evaluation Specialist Job Opportunity at USAID

The Data for Development project seeks an Evaluation Specialist to join our team providing monitoring and evaluation (M&E) technical support and capacity building to USAID/Tanzania. The Evaluation Specialist will contribute to mixed method performance and impact evaluations in a variety of sectors. This assignment is based in Dar es Salaam and is a full-time position for two years.… Read More »

The post Evaluation Specialist Job Opportunity at USAID appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

5 Jobs Opportunities at Chalinze Water Supply and Sanitation Authority

5 Jobs Opportunities at Chalinze Water Supply and Sanitation Authority Deadline 03 November 2019. Chalinze Water Supply and Sanitation Authority (CHALIWASA) was officially declared in the Government Notice No. 376 on 30th November 2012 as a fully fledged authority. Initially it was known among the National Water Projects which was initiated by the Government of the United Republic… Read More »

The post 5 Jobs Opportunities at Chalinze Water Supply and Sanitation Authority appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Internal Audit Head Opportunity at EFTA

Internal Audit Head Opportunity at EFTA Deadline 27 October, 2019 Internal audit Head at EFTA Equity for Tanzania Ltd (EFTA) is an award-winning equipment finance company which provides equipment loans to small, medium and growing businesses in Tanzania. Overview: Internal auditing is an independent, objective assurance and consulting activity designed to add value and improve an organization’s operations.… Read More »

The post Internal Audit Head Opportunity at EFTA appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Communications Team Lead Job Opportunity at Abt Associates

Communications Team Lead Job Opportunity at Abt Associates Deadline 20 November 2019

The post Communications Team Lead Job Opportunity at Abt Associates appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

UNICEF JOBS: TA Communication for Development Officer Job Opportunity at Mbeya & Zanzibar

TA Communication for Development Officer Job Opportunity at Mbeya & Zanzibar Deadline 24 October 2019 TA Communication for Development Officer, NO-B, Mbeya & Zanzibar, Tanzania (Two Posts- 6 months) Job Number: 526989 | Vacancy Link Locations: Africa: Tanzania,Uni.Re Work Type : Temporary Appointment UNICEF works in some of the world’s toughest places, to reach the world’s most disadvantaged… Read More »

The post UNICEF JOBS: TA Communication for Development Officer Job Opportunity at Mbeya & Zanzibar appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Chief Executive Officer (CEO) Job at Tanzania Football Federation (TFF)

Chief Executive Officer (CEO) Job at Tanzania Football Federation (TFF) Deadline 01st November, 2019 Tanzania Football Federation (TFF) through its organ Tanzania Premier League Board (TPLB) is mandated to manage its brands’ name called ‘Premier League, First Division League and Second Division League is looking for a suitable qualified Tanzania candidates to fill a position of Chief Executive… Read More »

The post Chief Executive Officer (CEO) Job at Tanzania Football Federation (TFF) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Clinical (Assistant II) at Chalinze Water Supply (CHALIWASA)

Job Opportunity at Chalinze Water Supply (CHALIWASA), Clinical (Assistant II) Chalinze Water Supply and Sanitation Authority (CHALIWASA) was officially declared in the Government Notice No. 376 on 30th November 2012 as a fully fledged authority. Initially it was known among the National Water Projects which was initiated by the Government of the United Republic of Tanzania in the… Read More »

The post Clinical (Assistant II) at Chalinze Water Supply (CHALIWASA) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Electrical Engineer at Chalinze Water Supply (CHALIWASA)

Electrical Engineer at Chalinze Water Supply (CHALIWASA) JOB TITLE: ELECTRICAL ENGINEER– 1 PostChalinze Water Supply and Sanitation Authority (CHALIWASA) was officially declared in the Government Notice No. 376 on 30th November 2012 as a fully fledged authority. Initially it was known among the National Water Projects which was initiated by the Government of the United Republic of Tanzania… Read More »

The post Electrical Engineer at Chalinze Water Supply (CHALIWASA) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

ICT Officer at Chalinze Water Supply (CHALIWASA)

ICT Officer at Chalinze Water Supply (CHALIWASA) JOB TITLE: ICT OFFICER – 1 PostChalinze Water Supply and Sanitation Authority (CHALIWASA) was officially declared in the Government Notice No. 376 on 30th November 2012 as a fully fledged authority. Initially it was known among the National Water Projects which was initiated by the Government of the United Republic of… Read More »

The post ICT Officer at Chalinze Water Supply (CHALIWASA) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Halmashauri Ya Wilaya Ya Msalala kinara ukusanyaji wa mapato ya ndani

HALMASHAURI ya Wilaya ya Msalala imekuwa ya kwanza Kitaifa katika ukusanyaji wa mapato kwa kukusanya asilimia hamsini na mbili (52%)  ya makisio ya mapato ya ndani kwa kipindi cha robo ya kwanza ya  mwaka wa fedha 2019/20 huku Halmashauri ya Kyerwa ikiwa ya mwisho kwa kukusanya asilimi tatu tu ya makisio yake.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Selemani Jafo alipokuwa akitoa taarifa ya ukusanyaji wa mapato ya ndani ya halmashauri kwa kipindi cha Julai – Septemba, 2019

Alisema Halmashauri ya Wilaya ya Msalala imefanikiwa kukusanya mara mbili ya malengo  ya robo ya kwanza ambapo kila halmashauri inatakiwa kukusanya si chini ya asilimia 25 ya makisio ili kukamilisha asilimia 100 kwa robo nne za mwaka wa fedha.

Waziri Jafo alieleza kuwa Bajeti iliyoidhinishwa ya mapato ya ndani ya Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2019/20 ni shilingi Bilioni 765.48; Katika kipindi cha robo ya kwanza (Julai hadi Septemba, 2019) Halmashauri zimekusanya jumla ya shilingi bilioni 166.24 sawa na asilimia 22 ya makisio ya mwaka.

Alifafanua kuwa “Katika kipindi hiki Halmashauri zilipaswa kukusanya asilimia 25 ya makisio yake ya mwaka lakini halmashauri hamsini na nne tu (54) ndio zilizofanya vizuri kwa kukusanya zaidi ya asilimia 25 ya bajeti zao na halmashauri 121 hazikuweza kufikisha asilimia 25 ya mapato yake”.

Aidha, Mhe. Jafo alisema kuwa katika kuzipima Halmashauri zote kwa pamoja Halmashauri ya Jiji la Dododma imekusanya mapato mengi zaidi kuliko Halmashauri zote kwa kukusanya shilingi Bilioni 13.10 na Halmashauri ya Buhigwe imekuwa ya mwisho kwa kukusanya shilingi Milioni 35.15.

Pia Mhe Jafo aliongeza kuwa katika ngazi ya Mikoa, Mkoa wa Rukwa umeongoza kwa kukusanya wastani wa asilimia thethini na moja (31) ya makisio ya Halmashauri za Mkoa huo huku Mkoa wa Mwisho ukiwa ni Mtwara ambao Halmashauri zake zimekusanya wastani wa asilimi kumi na tatu (13) ya makisio yake.

Alisema Katika kipengele hicho cha Mikoa kwa kuzingatia wingi wa mapato Mkoa ambao unaongoza kwa kukusanya mapato ya ndani kwa wingi ni Mkoa wa Dar es salaam ambao umekusanya shilingi Bilioni 39.53 na Mkoa wa Mwisho katika wingi wa ukusanyaji wa mapato ni Mkoa wa Kigoma ambao umekusanya shilingi bilioni 2.12.

Akisoma mchanganuo wa ukusanyaji wa mapato kwa kuzingatia aina ya Halmashauri na vigezo mbalimbali Mhe. Jafo amesema kuwa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam imeongoza kundi la Halmashauri za Majiji kwa kukusanya mapato kwa asilimia 38 ya makisio yake ya mwaka huku halmashauri ya Jiji la Dodoma ikiwa ya mwisho katika kundi hili kwa kukusanya kwa asilimia kumi na nane (18%) ya makisio yake ya mwaka.

Mhe. Jafo alitaja Halmashauri za Majiji zilizokusanya mapato ya ndani kwa kigezo cha wingi (Ghafi) kuwa Jiji la Dodoma limeongoza kwa kukusanya shilingi bilioni 13.098 na Halmashauri ya Jiji la Mbeya imekuwa ya mwisho katika kundi hili kwa kukusanya shilingi bilioni 2.74 tu.

Halkadhalika Jafo alitaja Manispaa iliyoongoza kundi la Halmashauri za Manispaa kwa kigezo cha asilimia kuwa ni Manispaa ya Sumbawanga ambayo imekusanya kwa asilimia arobaini na mbili (42) na Manispaa ya mwisho katika kigezo hiki ni Manispaa ya Kigoma ambayo imekusanya kwa asilimia tisa tu ya makisio yake kwa mwaka.

“Katika kigezo cha wingi wa mapato kundi hili linaongozwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ambayo imekusanya shilingi bilioni 13.05 huku Manispaa ya Kigoma ikiwa ya mwisho tena kwa kukusanya kiasi kidogo cha fedha cha shilingi milioni 235.11 alisema Jafo”.

Akifafanua kipengele cha Halmashauri za Miji Jafo alisema kuwa Mji wa Tunduma umeongoza kwa kukusanya kwa asilimia thethini na tisa (39%) na Halmashauri ya Mji wa Nanyamba imekua ya mwisho kwa kukusanya asilimia nne (4%) ya makisio ya mapato yake ya ndani kwa mwaka.

Mhe. Jafo alisema kuwa Halmashauri ya Mji wa Geita imeendelea kuongoza kwa wingi wa mapato katika Halmashauri za Miji kwa kukusanya shilingi bilioni 2.34 na Halmashauri ya mwisho ni Mji wa Nanyamba ambayo imeksuanya shilingi milioni 74.72.

Wakati huo huo Jafo alizataja Halmashauri za Wilaya zilizofanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato kiasilimia kuwa ni Halmashauri ya Msalala ambayo imekusanya kwa asilimia hamisni na mbili (52%) na Halmashauri ya Kyerwa imekuwa ya mwisho kwa kukusanya asilimia tatu (3%) ya makisio ya mapato ya ndani kwa mwaka.

Upande wa wingi wa mapato Mhe. Jafo alitaja Halmashauri ya Wilaya iliyoongoza katika kundi hili kuwa ni Halmashauri ya Chalinze ambayo imekusanya shilingi bilioni 2.05 na ya mwisho ni Halmashauri ya Buhigwe iliyokusanya shilingi milioni thethini na tano (35) tu.

Jafo alisema kuwa katika matumizi ya mapato ya vyanzo vya ndani katika taarifa hii ya robo ya kwanza haionyeshi picha halisi ya uchangiaji wa mapato hayo katika shughuli za maendeleo kwenye sekta ya Elimu, Afya na Maji.

“Uchambuzi kamili wa uchangiaji wa kila halmashauri katika miradi ya maendeleo utafanyika katika robo ya pili na mwisho wa mwaka wa fedha 2019/20 lakini kila Halmashauri ifanye jitihada kuhakikisha inachangia mapato ya ndani kulingana na asilimia inayopaswa kuchangiwa kwa mujibu wa bajeti zake” Alifafanua Jafo.

Aidha, Mhe. Jafo alieleza kuwa katika kipindi cha Julai-Septemba,2019 Halmashauri zilitumia shilingi Bilioni 40.88 kati ya shilingi bilioni 340.68 zilizokasimiwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo swan a asilimia 12.

Mhe. Jafo alikumbushia matumizi sahihi ya mifumo ya kielektroniki ya ukusanyaji wa mapato na mashine za kukusanyia mapato (PoSs) na mifumo ya Kielektroniki ya kutolea taarifa.

Alimalizia  kuwataka viongozi kuweka mikakati madhubuti ya kukusanya mapato kutoka kwenye vyanzo vipya vinavyobuniwa na Halmashauri zao.

(mwisho)



Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger