Thursday, 17 October 2019

DC MWEGELO : CHAGUENI VIONGOZI WA KUENDANA NA KASI YA RAIS MAGUFULI


Mhe. Joketi Mwegelo 

Na Shushu Joel
Mkuu wa wilaya ya Kisarawe ambaye anakaimu Ukuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Mhe. Joketi Mwegelo amewataka wananchi wa Halmashauri ya Chalinze kuwachagua viongozi wenye utayari na uwezo wa kuendana na kasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Rai hiyo ameitoa wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Bwilingu kwenye viwanja vya kituo cha mabasi cha Barabara ya Morogoro.

Mkuu huyo wa wilaya aliwakumbusha na kuwasisitiza wananchi hao kutambua dhamana kubwa waliyonayo na yupi ni kiongozi atakayekuwa ni kiungo kikubwa kwa viongozi wa juu na anayeweza kuendana na utendaji wa Rais Magufuli.

Pia Mkuu huyo wa wilaya aliwataka wananchi kuendelea kujitokeza kwenye zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la kupiga kura huku akiwapa msisitizo kuwa ni wale watakaokuwa kwenye orodha ndani ya daftari la wapiga kura tu ambao watapata fursa ya kupiga kura.

 "Wananchi wenzangu wale ambao wanadhani kuwa kile kitambulisho cha kupiga kura kitawawezesha kushiriki uchaguzi huu, hapana. Uchaguzi huu tunatumia daftari hivyo ni muhimu kwenda kujiandikisha".

"Jambo la kuwa na vitambulisho kuwa kigezo si kweli bali ni wewe tu kuweza kufika kituoni na inakuchukua dakika 2 tu",alisema.

Katika hatua nyingine,Mhe, Mwegelo amempongeza Mbunge wa jimbo la  Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete kwa utekelezaji na ufanikishaji wa miradi mbalimbali katika jimbo lake na jinsi alivyojitokeza yeye akishirikiana na wananchi kuhamasisha uandikishaji.

Aidha amewataka wananchi hao kuwa na viongozi watakaochaguliwa kwenye vitongoji na vijiji wawe wachapakazi kwa ajili ya kufanya kazi nzuri ya kuleta maendeleo.

"Ninyi wenyewe mashuhuda na Mbunge ameeleza jinsi Miradi mikubwa kama ya maji,afya,madarasa, miundombinu na umeme ilivyotekelezwa kwa asilimia kubwa sana. Nakupongeza Mhe. Mbunge kwa utekelezaji mzuri wa majukumu",alisema.

Naye mzee Zaidi Lufunga (78) akizungumza kwa niaba ya Wana Chalinze amempongeza mkuu huyo wa wilaya kwa kujionea mafanikio makubwa yaliyofanywa na serikali ya awamu ya tano katika jimbo la Chalinze.

"Miaka yetu changamoto zilikuwa nyingi sana, lakini kipindi hiki cha Rais Magufuli kwa kushirikiana na mbunge wetu Ridhiwani Kikwete mafanikio tunayapata na kazi nzuri inaonekana. Kutokana na utekelezaji wa miradi mikubwa na iliyokuwa ndiyo ndoto zao ni tu tutachagua viongozi wenye hofu ya Mungu",alisema Mzee Lufunga.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete amempongeza mkuu huyo wa wilaya kwa ujio wake wa kujionea jinsi Wanachalinze wanavyojitokeza katika zoezi la kujiandikisha.

Amewapongeza wakazi wa kata ya Bwilingu kwa kujitokeza kwa wingi ili kumsikiliza mkuu wa wilaya akieleza kuwa hilo ni jambo kubwa na kwa hakika linatoa dalili kuwa wananchi wako tayari. 

Hadi kufikia jana Halmashauri ya Chalinze ilikuwa imefikia Asilimia 74 ya Uandikishaji na baada ya kukatika kwa mvua kumekuwa na wingi wa wananchi kujiandikisha. Zoezi hili linatarajiwa kuisha tarehe 17 Oktoba ambapo matarajio ya kuandikisha watu 136,000 utafikiwa huku hadi jana watu zaidi ya 90,000 wakiwa wamejitokeza kujiandikisha.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMIS OKTOBA 17,2019


Share:

KAULI YA UONGOZI WA SHULE YA LITTLE TREASURES BAADA YA KUSHIKA NAFASI YA NNE KITAIFA, YA KWANZA KIMKOA MATOKEO DARASA LA SABA 2019


Muonekano wa madarasa ya shule ya msingi Little Treasures
Jengo la utawala shule ya msingi Little Treasures

Hii hapa kauli ya Uongozi wa Shule ya Little Treasures baada ya kufanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka 2019.

"Kwa niaba ya Familia ya Little Treasures napenda kutumia fursa hii kwanza kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema na baraka zake kwetu sote! Pia tunawashukuru viongozi wa dini  mbalimbali kwa sala na maombi Yao.

Pili, kwa namna ya kipekee niwashukuru viongozi wetu wote wa serikali kwa kuwa bega kwa bega na shule yetu,wamekuwa washauri wazuri  katika kuifanya  Little Treasures kuwa shule bora.  Pia tunapenda kuwashukuru sana wazazi na walezi wa wanafunzi wetu kwa ushirikiano wao na shule katika kufikia malengo yetu. 

Hali kadhalika shukrani ziwaendee watumishi wote wa LTS ambao wametumia muda wao mwingi katika kuwalea na kuwapa maarifa mbalimbali wanafunzi wetu. 

Na pia kwa nafasi hii tunapenda kuwapongeza wanafunzi wetu kwa utayari wao katika kujifunza na umakini wao katika mitihani na hatimaye kufanya vizuri katika mtihani wa darasa la saba 2019 ngazi ya wilaya,kimkoa na kitaifa.

Mwisho, Tunawashukuru sana wadau wote ambao mmekuwa mkishirikiana nasi kuifanya Little Treasures kuwa mahali pazuri kwa watoto wetu. Naomba tuendelee kushirikiana kwa matokeo mazuri zaidi. Mungu ibariki LTS ! Mungu Ibariki Tanzania!  Mungu tubariki sote.

Mkurugenzi Little Treasures - Lucy Dominic👏👏👏"

Shule ya Little Treasures iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga imekuwa shule ya nne kati ya shule 10 bora kitaifa katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka 2019 .

Nafasi ya kwanza kitaifa imeshikwa na shule ya Graiyaki,nafasi ya pili shule ya Twibhoki na nafasi ya tatu Kemebos,nafasi ya tano Musabe,sita Tulele,saba Kwema Modern ya Shinyanga,nane Peaceland, tisa Mugini na kumi Rocken Hill ya Shinyanga.

Katika matokeo hayo, Mwanafunzi Daniel Ngassa Daniel kutoka shule ya Little Treasures ameshika nafasi ya saba kitaifa.
Mbali na kushika nafasi ya nne ngazi ya taifa,Shule ya Little Treasures pia imekuwa shule ya kwanza katika ngazi ya halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga,nafasi ya kwanza ngazi ya mkoa



Share:

BRELA KUTOA HUDUMA ZA URASIMISHAJI WA BIASHARA KWENYE FURSA MJINI DODOMA

Kaimu Mkurungezi Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA)  Emanuel Kakwezi akizungumza

WAKALA wa Usaji wa Biashara na Leseni nchini (BRELA) unatarajiwa kutoa huduma za urasimishaji wa biashara Octoba 18 na Octoba 19 Jijiji Dodoma  kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma wakati wa Fursa 2019


Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Mkurungezi Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela)  Emanuel Kakwezi  ambaye pia alifanya  ukaribisho kwa wana Dodoma alisema watatoa huduma mbalimbali wakati wa fursa 2019 huku wakiwataka wakazi wa mkoa huo kuchangamkia fursa hiyo muhimu

Alisema kwamba huduma ambazo zitatolewa wakati wa Fursa Dodoma ni usajili wa Majina ya Biashara, Kampuni, Nembo za Biashara na huduma, Hataza, Leseni Daraja A, 
Leseni za Viwanda.

Kaimu Mkurungezi Mkuu alisema wameamua kishiriki kwenye Fursa  mwaka huu kutokana uhitaji wa wananchi juu ya ujarasimishaji Biashara zao  Pia wameamua kushiriki kutokana na kauli mbiu ya mwaka huu inayosema “Leta  Solution” ikiwa kama Taasisi ya Brela ni moja ya solution kwenye Biashara  na ubunifu wa wasajiriamali ili kuendana na Serikali ya Viwanda ya sasa

Kikubwa zaidi kilichofanya kushiriki ni kuwafikia wananchi kwa ukaribu 
zaidi na kuwahidumia kwa ukaribu zaidi

Kakwezi alisema Brela pia Itashiriki kwenye Fursa mikoa yote ambayo  imebaki baada ya Dodoma na watakuwa wanatoa huduma zote zinazotolewa na  Brela, ambapo mikoa hiyo ni Tanga, Arusha na Dar Es Salaam 

Hata hivyo alitoa  rai kwa wananchi wote kutumia fursa hii  ili kuweza kupata huduma za Brela  kwani kutakuwa na team ya Brela ambayo  itatowa huduma zote na wananchi watakao kidhi masharti kama ya kuwa na  Namba ya Kitambulisho cha NIDA na vingezo vingine wataweza kuondoka na  vyeti vya Usajili
Share:

Wednesday, 16 October 2019

MAHAKAMA YA RUFAA YATENGUA HUKUMU NA AMRI YA MAHAKAMA KUU KUZUIA WAKURUGENZI KUSIMAMIA UCHAGUZI MKUU

Mahakama ya Rufani Tanzania imetengua uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania iliyobatilisha sheria inayowapa mamlaka Wakurugenzi wa Halmashauri kusimamia Uchaguzi Mkuu.

Kutokana na hatua hiyo, kuanzia sasa Wakurugenzi wapo huru kusimamia uchaguzi.

Uamuzi wa Mahakama ya Rufani, umetolewa na Msajili Elizabeth Mkwizu baada ya Serikali kukata rufaa kupinga uamuzi uliotolewa na Mahakama Kuu juu ubatilisho wa sheria hiyo.

Katika uamuzi uliosomwa na Msajili wa Mahakama, Mkwizu amesema kuwa miongoni mwa hoja ni kwamba;

Wakurugenzi hawawi wasimamizi wa Uchaguzi moja kwa moja kwa kuteuliwa kwao bali kuna mchakato wa kisheria wanapitia ikiwemo kula kiapo, kutunza siri na kukana uanachama wa Chama walichokuwa nacho kabla ya uteuzi.

Mei 13, 2019 Serikali ilitangaza kukata rufaa kupinga uamuzi wa Mei 10, 2019 uliotolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania ambayo ilibatilisha sheria inayowapa mamlaka Wakurugenzi wa Halmashauri kusimamia Uchaguzi Mkuu.

Uamuzi huo ulitolewa na Jaji Atuganile Ngwala katika kesi ya msingi namba 6 ya mwaka 2018 iliyofunguliwa na mtoto wa marehemu Chacha Wangwe ambaye ni Bob Chacha Wangwe.

Katika kesi hiyo ya Kikatiba, Jaji Ngwala alibatilisha vifungu viwili vya Katiba cha 7 (1) ambapo kinaeleza kuwa ‘Kila Mkurugenzi wa Jiji na Halmashauri wanakuwa wasimamizi wa Uchaguzi Mkuu’

Pia alibatilisha Kifungu cha 7 (3) kinachoeleza kuwa Tume inaweza kumchagua mtu yoyote kuwa msimamizi wa Uchaguzi wakati katiba inasema huwezi kuwa Mwanasiasa na ukawa msimamizi wa uchaguzi bali inatakiwa achaguliwe mtu huru.
Share:

VIKAO VYA BUNGE LA TANZANIA KUANZA OKTOBA 21

Vikao vya Kamati 14 za Kudumu za Bunge, vinatarajia kuanza tarehe 21 Oktoba 2019 hadi Novemba Mosi mwaka huu.
Taarifa hiyo imetolewa leo tarehe 16 Oktoba 2019 na Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa cha Ofisi ya Bunge.

Taarifa hiyo imeleeza kuwa, miongoni mwa shughuli zitakazofanyika katika vikao hivyo, ni uchambuzi wa Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kuhusu hesabu zilizokaguliwa za Serikali za Mitaa na Serikali Kuu.

Pia, Kamati hizo zitafanya uchambuzi wa Taarifa ya Msajili wa Hazina kuhusu uwekezaji wa mitaji ya umma katika mashirika na taasisi mbalimbali nchini.

Na uchambuzi wa Sheria ndogo zilizowasilishwa wakati wa mkutano mkuu wa kumi na sita wa Bunge.Pamoja na Kupokea na kujadili taarifa ya mapendekezo ya mwongozo wa kutayarisha Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha wa 2020/2021.
Share:

UPEPO WA KISULISULI WA MCHUNGAJI GETRUDE LWAKATARE WATUA BAKITA


Mchungaji wa Kanisa la mlima wa moto Getrude Rwakatare

Baada ya uwepo wa baadhi ya Video fupi, zinazotembea kwenye mitandao ya kijamii, zikimuonesha Mchungaji wa Kanisa la Mlima wa Moto, Mama Getrude Lwakatare, kuhusu upepo wa kisulisuli, Baraza la Kiswahili la Tanzania (BAKITA), limesema maana ya neno hilo ni upepo mkubwa unatokea ghafla.

Akizungumza na EATV&EA Radio Digital, leo Oktoba 16, 2019, Msanifu Lugha Mkuu kutoka Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), Consolata Mushi, ameielezea maana halisi ukiachana na ile ya kiimani, kupitia Kamusi sanifu ya Kiswahili Fasaha.

''Muktadha wa neno kisulisuli nikiangalia ni kwenye masuala ya imani, kumbukeni masuala ya imani kwao ni kusadiki jambo ambalo, hujaliona na kuliamini kwamba litatokana kama lilivyo kwa mujibu wa msamiati wa Kiswahili, neno Kisulisuli lina maana ya upepo unosafiri na kuzunguka na kwenda kwa kasi au kwa haraka'' amesema Consolata.

Aidha Consolata ameongeza kuwa, Mama Lwakatare alizungumza neno hilo katika muktadha wake na kumaanisha kwamba ni jambo ambalo litatokea kama kimbunga kwa sababu upepo wa aina hiyo hutokea ghafla.

''Kama yeye alitumia kama mchumba anaweza akaja kama upepo wa kisulisuli ni muktadha wa imani, kwamba wapo na watajitokeza bila kutarajia, sasa msije mkaiingiza kwamba atajitokeza anazunguka kama upepo Laa! hasha! muktadha uongozwe kwenye kupata maana ya maneno, kwamba umekwenda kanisani ni msichana ama mvulana bila mwenzio lakini pale baada ya sala na imani akatokea mwenzio hukutarajia, hukupanga'' ameongeza Consolata.
Chanzo - EATV
Share:

SHULE YA ROCKEN HILL NI MWAMBAAA!! YANG'ANG'ANIA KWENYE 10 BORA MARA NNE MIAKA MITANO


Kama ulikuwa hujui basi ni kwamba...Shule ya Msingi Rocken Hill imeingia kwenye orodha ya shule 10 bora kitaifa mara nne katika kipindi cha miaka mitano hadi kufikia mwaka huu 2019.


Shule hii ipo wilayani Kahama mkoani Shinyanga imeingia kwenye orodha ya shule 10 bora mwaka 2015, 2016, 2018 na 2019 ikifuatiwa na shule zingine.

Shule kutoka Kanda ya Ziwa zinazoifuatia Rocken Hill ni shule ya Twibhoki (Mara) ambayo iliingia mwaka 2015, 2018 na 2019; Mugini ya Mwanza (mwaka 2015, 2016 na 2019) na Kwema Modern ya Shinyanga (mwaka 2016, 2018 na 2019).

Katika matokeo ya mwaka huu, shule 10 bora kitaifa ni Graiyaki (Mara), Twibhoki (Mara), Kemebos (Kagera), Little Treasures (Shinyanga), Musabe (Mwanza), Tulele (Mwanza), Kwema Morden (Shinyanga), Peaceland (Mwanza), Mugini (Mwanza) na Rocken Hill (Shinyanga).

Shule Bora Mwaka 2018 ni Raskazone (Tanga), Nyamuge (Mwanza), Twibhoki (Mara), Kwema Modern na Rocken Hill (Shinyanga), St Anne Marie (Dar es Salaam), Jkibira (Kagera), St Akleus Kiwanuka (Kagera), St Severine (Kagera), Rweikiza (Kagera).

Shule Kumi mwaka 2017 ni St. Peters (Kagera), St Severine (Kagera), Alliance (Mwanza), Sir. John (Tanga), Palikas (Shinyanga), Mwanga (Kagera), Hazina (Dar es salaam), St. Anne Marie (Dar es salaam), Rweikiza (Kagera) na Martin Luther (Dodoma).

Mwaka 2016, shule zilizoingia 10 bora ni Kwema Modern (Shinyanga), Rocken Hill (Shinyanga), Mugini (Mwanza), Fountain of Joy (Dar), Atlas (Dar) na Gift Skillfull (Dar), Mudio Islamic (Kilimanjaro), St. Achileus (Kagera) na Carmel (Morogoro).

Mwaka 2015 ulikuwa na shule kama vile Waja Springs (Geita), Enyamai, Twibhoki (Mara), Mugini, Rocken Hill, Karume (Kagera), Alliance (Mwanza), Little Flower (Mara), Palikas (Shinyanga) na St Caroli (Mwanza).

Share:

DC,DED NACHINGWEA WAMKOROGA RAIS MAGUFULI

Rais wa Tanzania John Magufuli amewabana Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea (DC) Rukia Muwango na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bakari B Bakari baada ya wananchi kulalamikia ucheleweshwaji wa miradi ya maendeleo.

Tukio hilo limetokea leo Jumatano Oktoba 16, 2019 wakati Rais akihutubia wananchi katika wilaya ya Nachingwea ikiwa ni sehemu ya ziara yake katika mkoa wa Lindi.

Baada ya hotuba za viongozi mbalimbali, Rais alimuomba Mwenyekiti wa CCM, Mzee Hashim Mkanjauka aeleze matatizo yote yanayowakabili wakazi wa Nachingwea.

Mkanjauka alianza kuelezea miradi ya maendeleo iliyokwama hali iliyowafanya wananchi waibuke kwa shangwe na hivyo kumfanya Rais atake kujua Zaidi kero hizo.

“Viongozi wetu siyo wakweli, miradi wilaya ya Nachingwea vijijini haitekelezeki, stendi ya wajasiriamali hakuna, soko halina kitu mkandarasi waliyempa hajamaliza, redio imenunuliwa na kufungwa kwa fedha za wananchi zaidi ya Sh100 milioni lakini haifanyi kazi. Maji yamekuja na mwenge yameondoka na mwenge Nachingwea ni wilaya kongwe,” amesema Mzee Mkanjauka.

Baada ya maelezo hayo Rais alimuita Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo akimtaka atoe majibu ya kwanini miradi hiyo inasuasua na mingine imesimama kabisa.

“Sh200 milioni ilijenga sehemu ya kupumzikia wasafiri , mabanda 12 ya biashara sisi tulikuta imefungwa tuliwekeza kwa kuweka mabanda kwa mapato ya ndani ya Sh81 milioni, kujenga mabanda 26 kumalizia choo na kuanza kwa kuwa ni kubwa maeneo tuliyotenga kwa ajili ya wajasiriamali itabidi tuyapimie wameshapimiwa na wanaohitaji miundombinu ni mama lishe.”

Majibu hayo yalizalisha maswali zaidi kwamba ni kiasi gani hasa kilichotumika kwa upande wa soko pekee, Mkurugenzi huyo alijibu kuwa ni Sh71 milioni.

Baadaye Rais aliamua kushuka katika gari na kutembea mita kadhaa eneo la soko ili kujiridhisha kama kweli ujenzi unaendana na thamani ya fedha inayotajwa.

Via Mwananchi
Share:

MWANAFUNZI BORA KITAIFA MATOKEO DARASA LA SABA 2019 BALAA SANA...MWENYEWE AFUNGUKA


Mwanafunzi bora kitaifa kwa upande wa wavulana katika mtihani wa darasa la saba 2019, Francis Hussein Gwagi amesema anataka kuwa mwanafunzi bora mitihani ya sekondari kama ilivyokuwa shule ya msingi.

Mtoto huyo aliyehitimu Shule ya Msingi Paradise wilayani Chato mkoani Geita amekuwa mwanafunzi wa pili kitaifa kwa matokeo ya jumla. Msichana Grace Manga wa Shule ya Msingi Graiyaki ya mkoani Mara ametangazwa kuwa wa kwanza kitaifa katika matokeo ya mtihani huo.

Gwagi amesema kwa masomo ya sekondari anatamani kusoma katika shule za Ilboru, Mzumbe, Mpwapwa au Pugu kwa kuwa zimekuwa na matokeo mazuri. 

Kwa mujibu wa mtoto huyo, wakati anasoma shule ya awali alirushwa darasa na kupelekwa darasa la pili kwa kuwa kila walipofanya mtihani alikuwa anaongoza.

“Na hapo sikuanza vibaya nilimaliza nikiwa number three (namba tatu) darasa la pili, nikaingia darasa la nne nikafanya mtihani wa Taifa, straight A in all the subjects (A kwenye masomo yote), mpaka naingia darasa la tano maendeleo yangu yalikuwa mazuri sana,” alisema Gwagi.

Aliongeza, “nimeshika number one standard six from January to Desember (kwa kwanza darasa la sita tangu Januari hadi Desemba), na mpaka naingia standard seven I have been number one from January to September (Darasa la saba wa kwanza tangu Januari hadi Septemba.”
Share:

TMA YATADHARISHA MVUA KUBWA KUNYESHA KUANZIA KESHO


Mkurugenzi wa Mamlaka ya hali ya hewa nchini (TMA) Dkt Agnes Kijazi
Mamlaka ya hali ya hewa nchini (TMA), imetoa tahadhari ya mvua kubwa kwa siku mbili mfululizo, kuanzia Oktoba 17 na 18, 2019, katika mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani na Visiwa vya Unguja na Pemba, hali itakayopelekea kusimama kwa muda kwa shughuli za kiuchumi katika maeneo hayo.

Taarifa hiyo imetolewa leo Oktoba 16, 2019, na mamlaka hiyo kwa lengo la kuwatahadharisha wananchi hususani waishio mabondeni, ambapo athari hizo pia zinaweza kujitokeza Kaskazini mwa mkoa wa Morogoro.

Aidha taarifa hiyo imesema kuwa upo uwezekano wa mvua hiyo kutokea kwa wastani na kiwango cha athari zinazoweza kutokea ni baadhi ya makazi kuzungukwa na maji pamoja na ucheleweshwaji wa usafiri.
Chanzo - EATV
Share:

MTUMWA WA KIKOLONI AIBUKA KUHAMASISHA WANANCHI KUJIANDIKISHA


Katika hali isiyokuwa ya kawaida, kijana mmoja anayefahamika kwa jina la Ikuzi Kicheko (Mzalendo Halisi), ameshangaza watu kwa kuvaa mavazi yaliyokuwa yakivaliwa na watumwa enzi za ukoloni, huku akiwa amebeba bango linalohamasisha watu kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura.

Ikuzi Kicheko, amesema lengo kubwa la kufanya hivyo ni kufuatia kuwepo kwa muamko hafifu wa wananchi kwenye zoezi la kujiandikisha, hali iliyopelekea Serikali kuongeza muda wa zoezi hilo.

"Unajua nilivaa yale mavazi ni kuashiria kuwa kama Watanzania, tunawajibu wa kujiandikisha kwenye daftari la kupiga kura ili kuwapata viongozi tunaowahitaji na kuachana viongozi ambao wanafanana na Mfalme Sultani, ambao walikuwa wanaangalia zaidi maslahi yao binafsi na kuwa mfano wa kiongozi mbaya" amesema Kicheko.

Aidha Kicheko ameongeza kuwa, "lengo langu sio kuwaambia watu kuna utumwa, ila ni kuwaambia nenda kajiandikishe kwenye daftari la kupiga kura, epuka kuwa mtumwa nenda kajiandikishe ili upate kiongozi unayemtaka, maanake ni kwamba usipopiga kura utapata kiongozi usiyemtaka".

Kesho Oktoba 17, 2019, ndiyo mwisho wa kujiandikisha kwenye daftari la kupiga kura ili kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika November, 2019.
CHANZO - EATV
Share:

WAITARA ATAKA VIONGOZI KUTOA TAARIFA KWA WAZAZI KUCHANGIA MICHANGO SHULENI


Naibu Waziri Ofisi ya Rais (TAMISEMI ) anayesimamia Sekta ya Elimu Mhe. Mwita Waitara

Na Lydia Lugakila - Kagera
Naibu Waziri Ofisi ya Rais (TAMISEMI ) anayesimamia Sekta ya Elimu Mhe. Mwita Waitara amewaagiza viongozi mbalimbali nchini kupitia bodi za shule,kamati za shule, vikao vya wazazi ,mabaraza na mikutano ya hadhara kutoa taarifa kwa wazazi kuchangia baadhi ya michango ya watoto wao shuleni kwa mpango mahususi ili kukuza sekta ya elimu nchini.

Naibu Waziri Mwita Waitara ametoa agizo hilo leo Oktoba 16, 2019 wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani Kagera katika ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua miradi ya elimu sambamba na kuongea na watumishi mkoani Kagera

Agizo hilo la Mhe. Mwita kwa viongozi mbalimbali na wadau wa elimu nchini juu ya utoaji taarifa kwa wazazi kuhusu kuchangia ya michango ya watoto wao shuleni kwa mpango mahususi limekuja baada ya kusomewa taarifa fupi na Afisa Elimu Mkoa wa Kagera Juma Mhina kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa huo Profesa Faustin Kamuzora iliyoelezea hali ya elimu katika mkoa huo zikiwemo changamoto na ufaulu wa mtihani wa darasa la saba mwaka 2019.

Afisa Elimu mkoa wa Kagera Juma Mhina amesema licha ya juhudi kubwa za Rais Magufuli katika utoaji elimu bila malipo changamoto nyingi zimeendelea kuwepo katika sekta hiyo kwani kuna baadhi ya wazazi wamekuwa hawawezi kujitoa kikamilifu katika kushirikiana na serikali katika kuchangia baadhi ya michango ya maendeleo ya watoto wao shuleni.

Katika taarifa hiyo Mhina amesema mkoa huo umefanikiwa pa kubwa katika baadhi ya masuala ikiwemo la uandikishaji wa wanafunzi wa elimu ya awali na darasa la kwanza ambapo katika elimu ya awali wameandikisha wanafunzi kwa asilimia 97 na darasa la kwanza kwa asilimia mia moja na nane 

Afisa elimu  amesema miongoni mwa changamoto zilizopo kuwa ni pamoja upungufu wa madawati 48,509 kwa shule za msingi 48 elfu 509, upungufu wa madawati katika shule za sekondari 17,000 vyumba vya madarasa , upungufu wa walimu wa sekondari kwa upande wa masomo ya sanaa ambao ni 48,000 ambapo kwa masomo ya sayansi ni 1060 huku akitaja upungufu wa walimu upande wa elimu msingi kufikia 6,571. 

Akiipokea taarifa hiyo Naibu Waziri huyo ameupongeza mkoa huo kwa ufaulu mzuri wa matokeo ya darasa la saba kwa kushika nafasi ya 4 kitaifa kwa ufaulu wa 88.11% ikilinganishwa na mwaka uliopita ambapo ulishika nafasi ya 5.

Naibu Waziri huyo amesema kuwa wazazi wanapaswa kutambua kuwa serikali ila ilizuia kitendo cha walimu kujikita kuchangisha fedha kwa watoto ambao hawana fedha na kusababisha watoto hao kujengewa chuki.

"Katika hali ya kawaida serikali haiwezi kufanya kila kitu viongozi mbali mbali wadau wa elimu Viongozi wa elimu hakikisheni mnatoa taarifa kwa wazazi kuchangia baadhi ya maendeleo ya shule, viongozi wa shule wanapotoa maelezo kuwa kuna baadhi ya vitu ambavyo huhitaji kuchangiwa,baadhi ya wazazi ambao hawaungi mkono juhudi hizo.

Kuna changamoto ambazo wazazi viongozi wanatakiwa kuchangia kwa kushirikiana na serikali ili kufanikisha sekta ya Elimu kusonga mbele’’,alisema Waitara.

Amesema ili ufaulu uendelee kuwepo ni lazima watoto wapate chakula shuleni jambo ambalo baadhi ya wazazi hawataki kuchangia 

"Wazazi wamekuwa wakishangilia mahafali kuliko kuchangia maendeleo ya mtoto shuleni, mkoa wa Njombe umefanya vizuri katika uchangiaji wa chakula shuleni",alisema.

Adha alieleza kuridhika na Usimamizi wa miradi ya elimu mkoani Kagera na kuwa tayari serikali imetenga shilingi bilioni 12 na laki 5 kukamilisha kila boma kwa kiwango walichokubaliana huku akiwahimiza Viongozi nchini kusimamia vizuri fedha zinazokuja ili ziweze kutoa matokeo chanya na kuwa serikali inatarajia kumaliza changamoto ya upungufu wa walimu mwaka huu

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa kagera Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti amemhakikishia Naibu Waziri huyo kuwa atahakikisha wananchi wanashirikiana katika kuchangia maendeleo ya shule ili kuongeza ufaulu mkoani Kagera.

Share:

ALIYETAJWA NA RAIS MAGUFULI KUIBA SH MILIONI 7 KWA DAKIKA AACHIWA HURU


 Hatimaye mfanyabiashara Mohamed Yusufali, aliyekuwa akikabiliwa na kesi mbili tofauti za uhujumu uchumi akidaiwa kukwepa kodi na kuisababishia Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) hasara ya zaidi ya Sh27 bilioni, katika kesi zote mbili yeye na wenzake, amerejea uraiani.

Yusufali ambaye aliwahi kutajwa na Rais John Magufuli kuwa alikuwa akiibia Serikali Sh7 milioni kwa dakika kupitia mashine za kodi za kielektroniki (EFD), alirejea uraiani jana baada ya kukaa mahabusu kwa miaka mitatu kutokana na kukabiliwa na mashtaka ya utakatishaji fedha.

Hivyo Yusufali aliachiwa jana rasmi baada ya kukamilisha mchakato wa msamaha wa Rais kisheria mahakamani, kwa mujibu wa makubaliano yake na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) katika kesi ya pili iliyokuwa imebaki.

Na James Magai, Mwananchi

Share:

ANGALIA HAPA MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE YA MSINGI GAMBOSI..ILIYOPO KIJIJI CHA GAMBOSHI

Shule ya Msingi Gambosi iliyopo katika kijiji Maarufu nchini Tanzania cha Gamboshi kata ya Gamboshi halmashauri ya wilaya ya Bariadi Vijijini Mkoani Simiyu ni miongoni mwa shule zilizofanya vizuri katika Matokeo ya Darasa la Saba mwaka 2019.



 Shule ya Msingi Gambosi inayoangukia kwenye kundi la shule zenye wanafunzi 40 au zaidi imeshika nafasi ya 17 kati ya 58 za halmashauri ya Bariadi Vijijini, ya 26 kati ya shule 357 kimkoa huku ikishika nafasi ya 434 kati ya shule 9929 kitaifa ikiwa na watahiniwa 65.




Share:

MUHAS: List Of Selected Students All Rounds (including Round 4) 0ctober 2019 Final

MUHAS: List Of Selected Students All Rounds (including Round 4) 0ctober 2019 Final The Muhimbili University of Health and Allied Sciences (MUHAS) started as the Dar es salaam medical school in 1963. The school then transformed into the faculty of medicine of the university of Dar es salaam that in 1991 was upgraded and became a college–the Muhimbili… Read More »

The post MUHAS: List Of Selected Students All Rounds (including Round 4) 0ctober 2019 Final appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Nafasi 9 za kazi UDSM-Jobs at UDSM October 2019

VACANCIES AT UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM The University of Dar es Salaam invites applications from suitably qualified Tanzanians to be considered for immediate employment to fill the following vacant posts:  Job Title: Laboratory Scientist III (2 posts) in the following  University Units: College of Natural and Applied Sciences:  (a) Qualifications and Experience:  Laboratory Scientist III – Department… Read More »

The post Nafasi 9 za kazi UDSM-Jobs at UDSM October 2019 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger