Thursday, 10 October 2019

DIWANI AHAMASISHA WANANCHI KUJITOKEZA KUJIANDIKISHA DAFTARI LA MPIGA KURA


Diwani wa viti maalumu Manispaa ya Shinyanga Mhe. Mariam Nyangaka, ametoa wito kwa wananchi wa Shinyanga kujitokeza kwa wingi kwenda kujiandikisha kwenye daftari la mtaa la mpiga kura, ili siku ya uchaguzi wakafanye maamuzi sahihi ya kuchagua viongozi bora ambao watawaletea maendeleo.

Nyangaka ametoa wito huo jana Oktoba 9,2019  kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye mtaa wa Kitangili Kata ya Kitangili manispaa ya Shinyanga ukiwa na lengo la kusoma utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Amesema wananchi wanapaswa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari hilo la mpiga kura , ili siku ya uchaguzi Novemba 24 mwaka huu wapate fursa ya kupiga kura na kuchagua viongozi makini, waadilifu, na watakaopigania maslahi ya wananchi katika kuwaletea maendeleo.

Pia ametoa wito kwa wanawake kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu za kugombea nafasi za uongozi kwenye uchaguzi huo wa Serikali za mitaa, ili wapate kufikia usawa wa 50 kwa 50 kwenye uongozi, na kuacha kuogopa kushindana na wanaume ikiwa wanawake ni viongozi watendaji wazuri kuliko wanaume.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa huo wa Kitangili Habiba Jumanne, akisoma utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM kwenye mtaa wake, amesema ametegengeza barabara kilomita mbili za Changalawe, amefanikisha upimaji wa viwanja likiwamo eneo la soko, ametatua migogoro ya ardhi, pamoja na kujenga matundu ya vyoo na madawati kwenye shule ya msingi Kitangili.

Uandikishaji wa daftari la mtaa la mpiga kura umeanza Oktoba 8 na unatarajiwa kuhitimishwa Oktoba 14 mwaka huu.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI

Diwani wa viti Maalum Manispaa ya Shinyanga Mhe. Mariam Nyangaka akizungumza na wananchi wa Mtaa na Kata ya Kitangili mjini Shinyanga  na kuwataka wajitokeze kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la mtaa la mpiga kura ili wapate fursa ya kupiga kura na kuchagua viongozi bora watakao waletea maendeleo. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde 1 blog

Diwani wa viti maalum manispaa ya Shinyanga Mhe. Mariamu Nyangaka akizungumza na wananchi wa Mtaa na Kata ya Kitangili mjini Shinyanga  na kuwataka wanawake wajitokeze kuchukua fomu ya kugombea uongozi kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa.

Mwenyekiti wa mtaa wa Kitangili Habiba Jumanne akisoma utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM kwenye mtaa huo.

Baadhi ya wananchi wa Mtaa wa Kitangili Kata ya Kitangili manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye mkutano wa hadhara na kutakiwa wajitokeze kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la mtaa la mpiga kura.

Baadhi ya wananchi wa Mtaa wa Kitangili Kata ya Kitangili manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye mkutano wa hadhara na kutakiwa wajitokeze kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la mtaa la mpiga kura.

Baadhi ya wananchi wa Mtaa wa Kitangili Kata ya Kitangili manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye mkutano wa hadhara na kutakiwa wajitokeze kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la mtaa la mpiga kura.

Mwananchi Zuhura Ramadhani wa Mtaa wa Kitangili akiuliza swali kwenye mkutano wa hadhara.

Mwananchi Jastine Thobias wa Mtaa wa Kitangili akiuliza swali kwenye mkutano wa hadhara.

Wananchi wa Mtaa wa Kitangili wakitawanyika baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara.

Picha na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog


Share:

JAJI MKUU: SHERIA ITUMIKE IPASAVYO KUDAI TAARIFA

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akizungumza na Mwenyekiti wa MISATAN Tanzania, Bi. Salome Kitomari (hayupo pichani) pindi ujumbe kutoka Taasisi hiyo ulipomtembelea Ofisini kwake, Mahakama ya Rufani jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa MISATAN-Tanzania, Bi. Salome Kitomari akizungumza jambo na Mhe. Jaji Mkuu (hayupo pichani). Mhe. Jaji Mkuu akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo hayo. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano, Mahakama ya Tanzania, Bw. Nurdin Ndimbe, wa kwanza kushoto ni Katibu wa Mhe. Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Adrian Kilimi, kulia ni Maafisa kutoka MISATAN na Mahakama. Maafisa kutoka MISATAN-Tanzania, (kushoto), Mwenyekiti, Bi. Salome Kitomari na Afisa Habari na Utafiti kutoka Taasisi hiyo, Bi. Neema Kasabuliro kwa pamoja wakinukuu masuala yaliyokuwa yakitolewa na Mhe. Jaji Mkuu. Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka MISATAN-Tanzania na baadhi ya Watumishi wa Mahakama walioshiriki katika mazungumzo hayo, wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa MISATAN Tanzania, Bi. Salome Kitomari, wa pili kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano, Mahakama ya Tanzania, Bw. Nurdin Ndimbe, wa kwanza kushoto ni Afisa Habari na Utafiti kutoka Taasisi hiyo, Bi. Neema Kasabuliro na wa kwanza kulia ni Salum Tawan, Mkutubi-Mahakama ya Tanzania. (Picha na Mary Gwera, Mahakama) Na MISA Tanzania Ujumbe wa taasisi ya MISA Tanzania ukiongozwa na Mwenyekiti wake Bi. Salome Kitomari umemtembelea na kufanya mazungumzo na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim Juma ofisini kwake jijini Dar es Salaam. 

Katika mazungumzo hayo, Bi. Kitomari ameitambulisha MISATAN pamoja na kuelezea majukumu yake mbalimbali kwa Mhe. Jaji Mkuu ikiwemo kutetea na kufanya uzengezi kuhusu utoaji na upataji taarifa nchini. 

 Mwenyekiti wa MISA amezungumzia uhusiano mzuri uliopo baina ya taasisi yake na Mahakama ya Tanzania ambao umejikita ktk kuimarisha na kutetea haki ya utoaji na upatikanaji wa taarifa zenye maslahi kwa umma. 

“Katika hili, MISA kwa kushirikiana na Mahakama ya Tanzania tumeendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi zaidi ya 300 wa kada mbalimbali za Mahakama kuhusu namna bora ya kuwahudumia wateja na mbinu za utoaji wa taarifa kwaumma” alifafanua Bi. Kitomari.



Kwa mujibu wa tathmini iliyofanywa na MISA Tanzania, mafunzo haya yameongeza weledi kwa washiriki na kuleta mabadiliko chanya katika utoaji wa taarifa za Mahakama hapa nchini. 

Aidha, Mwenyekiti wa MISA alisisitiza haja ya kuimarisha ushirikiano uliopo baina ya taasisi hizi mbili pamoja na kuhusisha taasisi nyingine za kihabari ili kupanua wigo wa utoaji na upatikanaji wa taarifa za kimahakama zenye maslahi ya umma. Bi. Kitomari ameshauri kufanyika mikutano kati ya MISA TAN, Mahakama ya Tanzania na taasisi nyingine za Habari ili kuimarisha ushirikiano, imani na uwajibikaji katika mchakato mzima wa utoaji na upatikanaji wa taarifa kwa wananchi. 

Pia, ameshauri kuwepo kwa mafunzo endelevu ya huduma kwa mteja na upatikanaji wa taarifa kwa kuhusisha viongozi wa juu wa Mahakama wakiwemo Majaji, Mahakimu na afisa tawala. 

 Kwa upande wake, Mheshimiwa Jaji Mkuu wa Tanzania ameipa changamoto MISATAN na taasisi nyingine za Habari nchini kuitekeleza ipasavyo Sheria Namba 6 ya Upatikanaji wa Habari ya mwaka 2016 katika kudai taarifa zenye maslahi kwa umma na taifa. 

“Sheria hii inatoa shurti ya kutoa taarifa zinazotakiwa na umma, hivyo sio Fadhila bali ni amri. Hivyo ni vyema kuangalia ni kwa namna gani tunatumia sheria hii kushurutisha utoaji wa taarifa sahihi kwa wananchi” alisisitiza Mhe. Jaji Mkuu.

 Aliongeza kwamba ni wajibu wa kila mmoja kutimiza wajibu wake kikamilifu katika kutekeleza sheria hii ipasavyo. “Kwa kufanya hivyo tutakua tumetekeleza takwa la Kikatiba na kisheria” amehimiza Mhe. Jaji Mkuu. 

 Kwa upande mwingine, Mhe. Prof. Juma amevitaka vyombo vya Habari kuzingatia weledi katika kuhabarisha umma ili kuepusha mifarakano katika Jamii. 

Amewahimiza waandishi wa habari nchini kujikita zaidi katika kuandika habari za kiuchunguzi badala ya kutegemea habari za matukio. 

“Habari za kiuchunguzi huhusisha utafiti na ushahidi wa jambo. Kuripoti habari hizi kutapunguza malalamiko na mifarakano katika jamii” amehitimisha Mhe. Jaji Mkuu.
Share:

Watuhumiwa Wizi Wa Madini Wafikishwa Mahakamani

Na Tito Mselem Tarime,
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imewafikisha Mahakamani Watuhumiwa Wanane (8) kwa makosa mbalimbali likiwemo la kuingia katika Mgodi wa North Mara na kuiba mifuko 15 ya Mawe yenye Dhahabu yanayokadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 234 za kitanzania.

Watuhumiwa hao waliingia Mgodini kwa nyakati tofauti kati ya tarehe 15 Septemba na 25 Septemba 2019 walikamatwa wakiwa na mawe mifuko 15 kinyume na Sheria.

Miongoni mwa watuhumiwa hao ni Zabron John (43), Jemes Makune (35), Jonathan Chuwa (27), Amos Raphael (28), Mseti Chacha (29), Chacha Marwa (29), Petro Mariba (32), na Samson Mathayo (17).

Akiwasomea mashtaka, Wakili wa Serikali Peter Ilole alitaja makosa yao ni pamoja na kosa la kuhujumu uchumi, kutakatisha fedha, kuingia mgodini bila kibali, kuiba mawe ya dhahabu pamoja na kukutwa na madini bila kuwa na leseni ya uchimbaji au biashara ya madini.

Aidha, Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Tarime mkoani Mara Mohamed Robert Silii, hakuwaruhusu watuhumiwa hao kujibu lolote kwa sababu Mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza mashtaka yanayowakabili na hivyo wakarudishwa rumande na kesi yao kuhairishwa hadi Oktoba 23, 2019 itakapotajwa tena.

Kosa la Kwanza ni kwa walishitakiwa wote Nane (8) kupanga njama kinyume na sheria Wilayani Tarime Mkoa wa Mara na kuiba mawe ya dhahabu katika mgodi wa Mgodi wa North Mara, kosa la Pili watuhumiwa walikutwa wakiwa na mawe yenye madini bila ya kuwa na leseni yoyote, Kosa la Tatu ni wizi wa mawe yenye dhahabu ambayo ni mali ya Mgodi wa North Mara, Kosa la Nne ni utakatishaji wa fedha na Kosa la Tano ni kuingia kwenye Mgodini bila ya kibali na kuiba mawe yenye dhahabu yenye thamani ya shilingi 234,590,832/=

Akizungumzia tukio hilo, Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo amevipongeza Vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa kuwakamata watuhumiwa hao na kutoa rai kwa watu wengine wenye tabia kama hizo kuachana na wizi wa madini kwani Serkali iko macho kwa mtu yeyote anayejihusisha na wizi wa madini.

Pia, Naibu Waziri Nyongo amevitaka Vyombo vya Ulinzi na Usalama vihakikishe vinamkamata kiongozi wao Kitabo Ryoba Molel, ambaye ndiye aliyedhamini wizi huo na baada ya kukamatwa alitoroka katika kituo cha polisi Wilaya Tarime.

Ameongeza kitendo hicho cha kuwafikisha Mahakamani ni moja ya jitihada zinazofanywa na Serikali katika kudhibiti wizi wa madini unaojitokeza katika Migodi Mikubwa ambapo wafanyakazi wa Migodi hiyo wanashirikiana na watu wa nje kuiba mali za wawekezaji.

Vilevile, Nyongo amewasisitiza wafanyabiashara wa madini kuyatumia masoko ya madini kufanya biashara zao na kwa atakayebainika kufanya biashara ya madini nje ya soko atakamatwa na kufikishwa Mahakamani huku akiwaonya wale wote wanaokwepa kulipa kodi ya Serikali kuacha mara moja.


Share:

Tanzania na Kenya zaongoza kwa idadi ya mabilionea Afrika Mashariki

Kenya na Tanzania zinaongoza kwa idadi ya watu matajiri katika jumuiya ya Afrika Mashariki kulingana na utafiti uliofanywa.

Kwa mujibu wa ripoti ya 2019 kuhusu utajiri barani Afrika iliyochapishwa mwezi Septemba na Benki ya AfrAsia, Kenya inaongoza ikiwa na mabilionea 356, Ikifuatiwa na Tanzania ambayo ina mabilionea 99.  Nchi ya Uganda ni ya tatu ikiwa na matajiri 67 huku Rwanda ikifunga orodha hiyo na mabilionea 30.

Ripoti hiyo inasema kwamba matajiri hao wana utajiri wa dola bilioni 10 na kwamba Tanzania ina tajiri mmoja wa dola bilioni moja.

Barani Afrika ripoti hiyo inasema kwamba Afrika Kusini inaongoza kwa matajiri ikiwa na mabilionea 2,169, Misri 932 na Nigeria 531.

Katika miji mikuu, mji wa Nairobi unaongoza ukiwa na utajiri wa dola bilioni 49 mbele ya mji wa Dar es Salaam ambao umeorodheshwa namba 11 na una utajiri wa dola bilioni 24.

Mji mkuu wa Uganda Kampala una utajiri wa dola bilioni 16 huku Addis Ababa ikiwa na utajiri wa dola bilioni 14.

Kulingana na ripoti hiyo mabilionea wa Afrika ni asilimia 16 pekee ya idadi ya mabilionea wote duniani, huku Afrika ikiwa na asilimia moja pekee ya utajiri wote duniani.

Utajiri unaomilikiwa na bara la Afrika ni dola trilioni 2.2 kwa jumla ambapo asilimia 42 ya utajiri huo unalimikiwa na watu wenye utajiri wa kiwango cha juu.

Ripoti hiyo inasema kwamba kuna matajiri 140,000 wanaoishi barani Afrika kila mmoja wao akiwa na mali yenye thamani ya dola milioni 10.

Credit: BBC


Share:

WAZALISHAJI WA CHUMVI MKOANI TANGA WAJENGEWA UWEZO KUONGEZA UZALISHAJI BORA

Share:

Serikali yaitaka Bodi ya mikopo elimu ya juu kutochelewesha fedha......Yapiga Marufuku Matumizi ya Neno "Mkopo Zero"

 Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia William Ole Nasha ameitaka Bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu HESLB kutochelewesha fedha za mikopo kwa wanufaika 
 
Akizungumza jijini Dar es salaam Ole Nasha amesema serikali imeshataoa fedha kwa Bodi ya Mikopo kiasi cha shilingi Bilioni 125 ili kuwezesha utoaji mikopo hiyo.

 "Bodi ya Mikopo pamoja na kuendelea kutoa mikopo kwa wanafunzi hakikisheni wanafunzi 5,593 ambao taarifa zao zilikua na matatizo zinashughulikiwa kwa haraka kwa kufungua dirisha dogo la maombi ili nao wapate haki yao ya msingi," amesisitiza Naibu Waziri Ole Nasha.

Aidha naibu waziri huyo amepiga marufuku kwa wanafunzi wa vyuo vikuu wanaopata mkopo wa shilingi milioni 2 na laki nne kwa mwaka kwa ajili ya malazi na chakula kuacha kuita mkopo huo kuwa ni mkopo ziro.

"Kuanzia leo tunapiga marufuku matumizi ya neno 'Mkopo Zero' , haiwezekani Serikali yao ijitahidi kuwatafutia fedha ya mkopo kwa ajili ya maradhi na Chakula halafu useme Mkopo Sifuri, ni marufuku kutumia msamiati huo"- Amesema Naibu Waziri, William Ole Nasha

Naye Mkurugenzi Mtendaji Bodi ya mikopo HESLB Abdul-Razaq Badru amesema baadhi ya wanafunzi wanafanya makosa wakati wa uombaji hali ambayo inawakwamisha kupata mikopo kwa wakati.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Taasisi za Wanafunzi wa Vyuo Vikuu TAHLISO Alex Stephano ameiomba bodi hiyo kutatua changamoto ambazo bado zinazowakabili wanafunzi wa vyuo vikuu wakati wa kujaza fomu hizo za maombi.


Share:

Rais Magufuli atembelea Hifadhi ya Taifa ya Katavi

Rais Magufuli jana ametembelea Hifadhi ya Taifa ya Katavi na kisha kuzungumza na Maafisa na Askari Wanyamapori wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) ambapo amewapongeza kwa kazi nzuri ya kuhifadhi wanyamapori ikiwemo kukabiliana na ujangili hali iliyowezesha kuongezeka kwa idadi ya wanyama wakiwemo wale waliokuwa hatarini kutoweka lakini amewasihi wachache miongoni mwao ambao wanashirikiana na wahalifu waache tabia hiyo.

“Wapo wenzenu wachache wanaoshirikiana na majambazi, waache na wakipatikana wa namna hiyo, peleka mahakamani wafunguliwe kesi," amesema Rais Magufuli.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia wanyama aina ya viboko katika hifadhi ya Taifa ya Katavi  mara baada ya kusimama wakati akielekea Mpanda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akichagua nyama ya porini mara baada ya kujumuika na wadau mbalimbali, Wafanyakazi wa TANAPA, Askari wa Wanyama Pori, Wabunge, Mawaziri katika mbuga ya wanyama ya Katavi wakati akielekea Mpanda mkoani Katavi.



Share:

Dawa Komesha Ya Maumbile Madogo , Nguvu Za Kiume Na Magonjwa Mengineyo

*NGETWA MIX*/
√Hii ndio dawa bora ya mitishamba kiboko ya maumbile Madogo(KIBAMIA) Hurefusha na kunenepesha maumbile  mafupi pia  yaliyoingia ndani kutokana na kitambi ama kuathirika na punyeto

*📌SUPER MORINGA MIX*/
Ni dawabora ya nguvu za kiume yenye mchanganyiko wa miti shamba 10 yenye maajabu yafuatayo:/
🔖(1)Inatibu upungufu wa nguvu za kiume mara dufu na kuimarisha misuri   ilio legea na kusinyaa wakati wa tendo la ndoa/
🔖(2)Kuongeza hamu ya tendo kukufanya uweze kurudia tendo hadi mara tatu bila kuchoka
🔖(3)Itakufanya uchelewe kufika kileleni dk 15-30 kwa tendo la Kwanza na utakuwa na uwezo wa Kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara 3-4 bila hamu kuisha na inatibu kabisa/
.
*MATATIZO HAYA HUSABABISHWA NA*/
🔖(1)Tumbo kujaa gesi, na kuunguruma chini ya kitovu/
🔖(2) Choo kuwa kama Cha mbuzi/
🔖(3)Ngiri/
🔖(4)Kama umejichua sana punyeto/
🔖(5)Kisukari/
🔖(6)Presha ya kupanda na kushuka/
🔖(7)Vidonda vya tumbo,/
.
Na haya yote husababisha/
📍Kuishiwa kwa nguvu za kiume 📌/
. _______________________
Bado hujachelewa dawa hizi ni mpya kabisa  ni tofaut na ulizo wahi kutumia pia zimeonesha mafanikio kwa watu wengi sana/

Pia tuna tibu  KISUKARI,PRESHA,VIDONDA VYA TUMBO N.K/
._______________________
DR .SELEMANI OMARY ANAPATIKANA  DAR ES SALAAM , PIA UNAWEZA KULETEWA POPOTE ULIPO  NDANI NA NJE YA NCHI .SIMU NO:/
*📞+255788468114*


Share:

Video Mpya: Chemical – Najisikia

Video Mpya:  Chemical – Najisikia


Share:

Wimbo Mpya: Mimi Mars - EX

Wimbo Mpya: Mimi Mars - EX


Share:

Uturuki yaanza kufanya mashambulizi nchini Syria

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ametangaza kuanza rasmi kwa mashambulizi ya jeshi la nchi yake dhidi ya wapiganaji wa kundi la Wakurdi Kaskazini mwa Syria.

Haya yanajiri baada ya Marekani kuwaondoa wanajeshi wake katika eneo hilo, jambo ambalo Wakurdi wanalichukulia kama usaliti.

Wanaharakati nchini Syria wamethibitisha kuanza kwa mashambulizi hayo, wakisema ndege za kivita za Uturuki zimelenga shabaha katika mji wa Ras al-Ayn ulio upande wa Syria katika mpaka baina ya nchi hizo.

Ripoti za vituo vya televisheni nchini Uturuki zimearifu kuwa mashambulizi hayo yalizipiga ngome za wapiganaji wa Kikurdi zilizo karibu na mpaka huo.

Katika tangazo lake kupitia mtandao wa twitter, Rais Erdogan amesema madhumuni ya mashambulizi hayo ni kuzuia kuundwa kile alichokiita ''ukanda wa kigaidi'' karibu na mpaka wa kusini wa Uturuki, na kuleta hali ya amani katika eneo hilo.

Aidha, rais huyo ameongeza kuwa kwa ushirikiano na jeshi la taifa la Syria, Uturuki inafanya mashambulizo hayo yaliyopachikwa jina la ''Operesheni Chipuko la Amani.

Umoja wa Ulaya umeitaka Uturuki kusitisha mara moja mashambulizi hayo, na kueleza bayana kuwa hautagharimia shughuli za kuweka ukanda salama kwa wakimbizi wa Syria watakaoondolewa nchini Uturuki.

Urusi ambayo ni mshirika mkubwa wa serikali ya Syria mjini Damascus, imesema haitajiingiza katika mzozo huu mpya baina ya Syria na Uturuki.

Msemaji wa kundi la wapiganaji wa Kikurdi la SDF Mustafa Bali amethibitisha kuanza kwa mashambulizi dhidi ya kundi lake, akisema yanalenga maeneo yanayokaliwa na raia, ambao kwa mujibu wa maelezo yake wamejawa na taharuki.

Bado hakuna ripoti za upande ulio huru kuhusu maeneo yanayolengwa katika operesheni hiyo.
 
Mashambulizi haya yalikuwa yakitarajiwa muda wowote, baada ya rais wa Marekani Donald Trump kutangaza Jumapili iliyopita, kuviondoa vikosi vya nchi yake kutoka eneo hilo.

Baadaye aliionya Uturuki kwamba ikiwa itaingia kijeshi ndani kabisa ya Syria, angeusambaratisha vibaya uchumi wa nchi hiyo.

Uamuzi huo wa Trump ulikosolewa vikali na watu mbali mbali, miongoni mwao wakiwemo maafisa wa chama chake cha Republican, waliomtuhumu kuwatoa muhanga Wakurdi ambao wamekuwa washirika wa muda mrefu wa Marekani, na kionyesha Marekani kama kigeugeu.

Credt:DW


Share:

Mafuriko Yaua Watu 6 Tanga

Watu sita wamefariki dunia na kaya kadhaa Wilayani Korogwe hazina mahala pa kuishi baada ya nyumba zao kuanguka na zingine kujaa maji kutokana na mvua kubwa iliyonyesha kuanzia saa 2 usiku wa Oktoba 8 hadi majira ya saa 9 alasiri Oktoba 9.

Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga SACP Edward Bukombe alisema kuwa mvua hiyo iliyonyesha katika vijiji vya Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe katika milima ya Usambara ilisababisha barabara kuu ya Arusha -Segera -Dar eneo la Msambiazi Korogwe mjini kutopitika na kufungwa kwa muda kwa tahadhari za kiusalama.

Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa alithibitisha kwa barabara hiyo kufungwa kwa muda na hadi kwa muda wa saa mbili na baadae kuendelea na safari zake kati ya Tanga, Dar es salam, Lushoto, Moshi, Arusha na Nairobi kupitia Namanga mkoani Arusha yaliruhisiwa.

Akizungumzia vifo vya watu sita, Kamanda Bukombe amesema kuwa watu hao ambao majina yao bado hayajulikana ni katika kijiji cha Dindira mwanamke mmoja na watoto wake wawili waliangukiwa na nyumba usiku wakati katika kijiji cha Bungu msichana mmoja anayejulikana kwa jina la Asha Yahaya Ambanyonge alikuwa kalala na wadogo zake wawili ambapo nao wameangukiwa na nyumba na kufariki papo hapo.

Wilayani Muheza katika barabara ya Amani -Muheza kata ya Mbaramo eneo la Msangazi mawasiliano ya barabara yalifungwa kwa muda kutokana na mafuriko yaliyoziba njia.


Share:

Mfanyabiasha Yusufu Ally Maarufu Kwa Jina la 'Mpemba Wa Magufuli' Aandika Barua kwa DPP Kukiri Makosa Yake

Mfanyabiashara Yusufu Ally, maarufu kwa jina la mpemba wa Magufuli na wenzake,wanaokabiliwa na mashitaka ya  uhujumu uchumi ikiwemo kujihusisha na biashara ya meno ya tembo, wameandika barua kwa Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) kuomba kukiri mashitaka yao hayo.

Katika kesi hiyo, mbali ya Mpemba washitakiwa wengine ni Charles Mrutu, Benedict Kungwa, Jumanne Chima, Ahmed Nyagongo na Pius Kulagwa.

Wakili wa Serikali, Elizabeth Mkunde amemueleza dai Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kwamba washitakiwa wameshaandika barua hivyo, anaomba mahakama iwape muda kwa ajili ya kuingia katika makubaliano.

Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 16, mwaka huu 2019 kwa ajili ya kutajwa.

Washitakiwa hao  wanakabiliwa na mashitaka manne ya kujihusisha na biashara ya meno ya tembo yenye thamani ya Sh milioni 785.6 .

Inadaiwa katika tarehe tofauti kati ya Januari, 2014 na Oktoba, mwaka huu wakiwa Dar es Salaam, Tanga, Iringa na Mtwara, walijihusisha na mtandao wa ujangili kwa kukusanya na kuuza nyara za serikali ambazo ni vipande vya meno ya tembo 50 vyenye thamani ya Dola za Marekani 180,000 sawa na Sh  milioni 392.8  bila kuwa na kibali cha Mkurugenzi wa Wanyamapori.

Pia inadaiwa Oktoba 26, mwaka huu, washitakiwa hao wakiwa Mbagala Zakhem, walikutwa na vipande vya meno ya tembo10 vyenye   uzito wa kilo 13.85 vya thamani ya Dola za Marekani 30,000 sawa na Sh milioni 65.4.

Wanadaiwa kuwa  Oktoba 27, mwaka huu, wakiwa Tabata Kisukuru washitakiwa hao walikutwa na vipande vinne vya meno hayo ya tembo yenye uzito wa kilo 11.1 na thamani ya Dola za Marekani 15,000  sawa na Sh milioni 32.7 .

Pia, Oktoba 29, mwaka huu walikutwa na vipande 36 vya thamani ya Sh  milioni 294.6   bila kuwa na kibali cha Mkurugenzi wa Wanyamapori.


Share:

Wachina Waamriwa Kulipa Milioni 70 Baada Ya Kukiri Makosa Yao ikiwemo la kusafirisha Kucha 25 za Simba.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu Raia wawili wa China, Li Ling na Chen Guo kulipa faini ya Sh.Mil 70 baada ya kukiri makosa yao ikiwemo la kusafirisha Kucha 25 za Simba.

Pamoja na kuachiwa huru, mahakama hiyo imetaifisha gari aina ya Toyota Prado T 982 CDH na mashine mbili za washtakiwa hao na kuwa mali ya Serikali huku ikimtaka mshtakiwa Chen Guo kulipa faini ya Sh. Milioni 1 kwa kosa la kuishi nchini bila kibali.

Hatua hiyo, imekuja baada ya upande wa mashtaka kuwafutia washtakiwa hao mashtaka ya uhujumu uchumi na kuwasomea mashtaka mawili ya kujihusisha na nyara za serikali na kuishi nchini bila kibali.

Hata hivyo washtakiwa wengine wanne waliokuwa katika kesi hiyo ambao ni raia wa China wamegoma kukiri mashtaka yao yanayowakabili hivyo wamerudishwa rumande.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi ambapo amesema mshtakiwa Li Ling anapaswa kulipa fidia ya Sh. Mil 45 na mshtakiwa Chen Guo atalipa Sh. Mil 25 na faini ya Sh. Milioni 1 au kwenda jela mwaka mmoja.

Pia amesema, gari aina ya Toyota Prado na mashine mbili zinataifishwa na kuwa mali ya Serikali na amewataka washtakiwa hao kuondoka nchini mara moja kwa kuwa sio raia wa Tanzania. .

Kabla ya kutolewa adhabu hiyo, Wakili wa Serikali, Salim Msemo alidai hawana kumbukumbu ya nyuma ya makosa kwa washtakiwa hivyo, anaiomba mahakama itoe adhabu kulingana na makubaliano ili iwe fundisho kwao na wengine.

Mapema, akisoma makubaliano hayo, Wakili Msemo alidai kuwa wameingia makubaliano na washtakiwa hao baada ya kukiri kosa la kujihusisha na nyara za serikali na kuishi nchini bila kibali, hivyo wameamua kuondoa mashtaka ya uhujumu uchumi.

Baada ya kusoma makubaliano hayo, Hakimu Shaidi aliwaapisha washtakiwa na kuwauliza kama walisaini kwa hiari yao na kudai alifanya hivyo kwa hiari yao.


Share:

TAKUKURU Yaieleza Mahakama Ilivyomnasa Mhadhiri Akiomba Rushwa ya Ngono Kwa Mwanafunzi

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeelezwa kuwa, maafisa wa Takukuru walimkuta Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Samson Mahimbo (68) akijiandaa kufanya ngono na mwanafunzi wake.
 

Hayo yameelezwa jana Jumatano Oktoba 9, 2019 na wakili wa taasisi hiyo ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini Tanzania,  Faraja Salamba wakati akimsomea maelezo ya awali mshtakiwa huyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shahidi. 

Salamba amedai wakati wa tukio hilo mhadhiri huyo alikuwa mwajiriwa wa NIT akifundisha wanafunzi wa muhula wa kwanza wa masomo wa mwaka  2015/2016 somo la usimamizi wa barabara na usafirishaji.

Amedai Januari 5 na 11, 2017 mshtakiwa alitumia madaraka yake vibaya kwa kuomba rushwa ya ngono na alimpigia simu Victoria na kumsisitiza wakutane katika baa ya Shaniiliyopo maeneo ya Mwenge.

Walipokutana , mshitakiwa alikuwa na mtihani wa marudio ambao Victoria alitakiwa kufanya, karatasi ya majibu na marking scheme ambapo alimsahihishia na kumpa alama 67 na baada ya kumaliza wakuhamia kwenye baa na nyumba ya kulala wageni inayoitwa Camp David , iliyopo Mlalakuwa Mwenge.

Amedai wakiwa pale walikunywa na kulewa kisha wakachukua chumba na kuingia ndani na kwamba mshitakiwa alianza kuvua nguo na kubaki na nguo ya ndani.

"Mshitakiwa alianza kumkumbatia Victoria na kuanza kumvua nguo zake na mara walisikia mlango ukigongwa na Victoria aliufungua na kuingia maofisa wa Takukuru, muhudumu wa baa na mjumbe. Walikuta nguo zipo juu ya meza," alidai.

Mshtakiwa alikamatwa na Januari 12, 2017 alienda kuandika maelezo Takukuru na Agosti 14, mwaka huu aliletwa mahakamani.Mshitakiwa alikana maelezo hayo na kukubali majina yake na mahali anapokaa.

Upande wa mashitaka ulidai kuwa wanamashahidi sita na vielelezo saba ili kuthibitisha mashitaka hayo huku mshitakiwa huyo alidai atakuwa na mashahidi wanne.

Maimu alifikishwa mahakamani hapo akikabiliwa na mashitaka ya kuomba rushwa ya ngono kwa mwanafunzi wa chuo hicho.


Mhadhiri huyo anadaiwa akiwa mwajiriwa wa NIT alikuwa akifundisha wanafunzi wa muhula wa kwanza wa masomo wa mwaka 2015/16.

Anadaiwa alitenda kosa hilo Januari 12, mwaka 2017 katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Camp David

Ilidaiwa kuwa mshitakiwa huyo akiwa mwajiriwa wa NIT katika kozi ya Usimamizi wa Barabara na Usafirishaji namba LTU 07101 alitumia mamlaka yake alimlazimisha mwanafunzi huyo kutoa rushwa ya ngono.

Ilidaiwa kuwa, aliomba rushwa hiyo ili aweze kumfaulisha katika mtihani wake wa marudio katika kozi ya Usimamizi wa Barabara na Usafirishaji uliokuwa unafanyika Januari 5 ,mwaka 2017.

Mshitakiwa yupo nje kwa dhamana na keshi itaanza kusikilizwa Novemba 11, mwaka huu.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi October 10




Share:

Wednesday, 9 October 2019

IGELEKE FC BINGWA WA SAUTI YA SIMBA SUPER CUP 2019

Diwani Nguvu Chengula wa kata ya Mwangata na mkurugenzi wa shule za Sun Academy ambaye alikuwa  ndiye mdhamini wa mashindano hayo ya  Sauti ya Simba Super Cup 2019 akiongea baada ya kupatikana kwa mshindi wa kombe hilo
Diwani Nguvu Chengula wa kata ya Mwangata na mkurugenzi wa shule za Sun Academy ambaye alikuwa  ndiye mdhamini wa mashindano hayo ya  Sauti ya Simba Super Cup 2019 akionyesha jezi ambazo alizigawa kwa mshindi wa kwanza na wapili wa mashindano hayo 
Diwani Nguvu Chengula wa kata ya Mwangata na mkurugenzi wa shule za Sun Academy ambaye alikuwa  ndiye mdhamini wa mashindano hayo ya  Sauti ya Simba Super Cup 2019 akitoa mpira kwa mshindi wa tatu wa mashindano hayo 
***
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

MASHINDANO ya Sauti ya Simba Super Cup 2019 kata ya Mkimbizi yamefikia tamati siku ya jana baada ya kuchezwa fainali kati ya Mkimbizi FC na Igeleke FC katika viwanja vya shule ya msingi Mkimbizi na Igeleke FC kuibuka mshindi.

Mashindano haya ya mpira wa miguu yaliyokua yanahusisha zaidi ya timu nane ambazo ni Mkimbizi fc, Masoko fc,Mtwivila fc,Romanithelc Rc,Rutherana kkkt,Igereke fc,Bima fc na Vetaran fc za kata ya Mkimbizi yalikuwa yanadhamini na mkurugenzi wa shule za Sun Academy ambaye pia ni diwani wa kata ya Mwangata Nguvu Edward Chengula kwa kuwa amekuwa mdau mkubwa kwenye sekta ya michezo manispaa ya Iringa

Na ikumbukwe kuwa hivi karibuni diwani Nguvu Chengula alidhamini mashindano makubwa yaliyofanyika kata ya Kihesa yaliyokwenda kwa jina la Bidii Cup mashindano hayo yalikuwa yana msisimko na mvuto wa hali ya juu sana na  vijana walionesha uwezo mkubwa wa kusakata kabumbu kiasi kwamba wadau na viongozi wanaohusika na michezo katika mkoa wa Iringa walikunwa na uwezo uliooneshwa na vijana.

Akizungumza wakati wa kuwakabidhi zawadi mshindi wa kombe hilo Chengula alisema kuwa mpira wa miguu kwa sasa umekuwa unatoa ajira na kuwaajiri watu wengi hivyo vijana wanatakiwa kuonyesha vipaji vyao.

“Saizi mnatakiwa kuonyesha vipaji vyenu kweli kweli kwa kuwa kwa sasa mpira wa miguu umekuwa ajira ambayo wachezaji wamekuwa wanalipwa mamilioni ya fedha tofauti na miaka ya nyuma ilivyokuwa” alisema Chengula

Chengula alisema kuwa amekabidhi jezi seti moja na mpira mmoja kwa mshindi wa kwanza,mshindi wa pili alijinyakulia jezi seti moja huku mshindi wa tatu alijinyakulia mpira mmoja.

Aidha Chengula aliwataka wananchi kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari za mpiga kura kwa kuwa kila mkazi wa wanahaki wa kujitokeza kujiandikisha na kupata haki ya kumchagua kiongozi wanaemtaka.

“Hii ni fursa pekee ya kuhakikisha unapata nafasi ya kumchagua kiongozi ambaye atasaidia kukuletea maendeleo kwenye mtaa au kijiji chako kwa kipindi cha miaka mitano hivyo wakazi wote nawaomba mjitokeze kwa wingi kujiandikisha” alisema Chengula

Lakini Chengula aliwakumbusha vijana kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi kujiandikisha na kugombea nafasi mbalimbali za kiuongozi kwa kuwa nao wanahaki ya kuwa viongozi wa kuongoza mitaa ambayo wanaishi kwa maendeleo ya jamii.


Vilevile Chengula ndiye alikuwa mdhamini mkuu wa mashindano ya kusaka vipaji vya vijana wanaoweza kuimba na kucheza (dancers) mashindano hayo yalikwenda kwa jina la Mwangata House of Talent na yalikuwa na msisimko mkubwa kwa kuwa vijana waliimba na kujishindia zawadi mbalimbali zikiwemo fedha tasilimu laki sita,vijana wote walioonesha uwezo mkubwa katika mashindano hayo chama cha mapinduzi (CCM) Iringa waliahidi kuviendeleza vipaji hivyo

Katika maswala ya soka mkurugenzi wa shule za Sun Academy amekua mstari wa mbele kabisa kuhakikisha vijana wanapata burudani, wanajenga afya zao na wanapata nafasi ya kujitengenezea ajira kupitia vipaji vyao vya kusakata soka, mpaka sasa emesaidia pia mashindano ya mpira pale kata ya Mlandege na kuwasaidia vijana kwa kuwapa vitendea kazi ikiwemo mipira na jezi katika mashindano yale.

Vijana hawahitaji mambo mengi,vijana wanahitaji kupata kile wanachokipenda. Suala la michezo kwa vijana ni suala mtambuka na linalopendwa na kila kijana. Vijana wana vipaji na uwezo mkubwa sana hasa wanapopewa nafasi ya kuonesha vipaji vyao. Hivyo kama kiongozi anayejali ni lazima aliangalie kundi hili kwa umakini mkubwa.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger