Saturday, 17 August 2019

Breaking : LORI LA MAFUTA LAANGUKA ISAKA - KAHAMA


lori la Mafuta Kampuni ya Interpetrol likitokea Jijini Dar  es salaam kuelekea Burundi limeanguka katika Mji Mdogo wa Isaka wilayani Kahama Mkoani Shinyanga  leo Jumamosi Agosti 17,2019 majira ya saa nane na nusu mchana.



Lori hilo limesababisha mafuta aina ya diesel kumwagika ambapo tayari vyombo vya Ulinzi na usalama vya Wilaya ya Kahama vikiongozwa na Mkuu wa wilaya hiyo Anamringi Macha vimewasili eneo la tukio.
Share:

Nafasi za kazi Mzumbe University August 2019

Nafasi za kazi Mzumbe University. Mzumbe Jobs. Find a latest Lecturers Jobs in Mzumbe University. Nafasi za kazi chuo kikuu cha mzumbe: ajira mpya Mzumbe University. MZUMBE UNIVERSITY (CHUO KIKUU MZUMBE)  VACANCIES The Mzumbe University invites applications from suitably qualified and competent Tanzanians to fill the following vacant posts: ASSISTANT LECTURER – (5 Posts) (a) Qualification and Experience… Read More »

The post Nafasi za kazi Mzumbe University August 2019 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

MANYANYA AWAONYA WANAOENEZA PROPAGANDA CHAFU NA KUKIMBIZA WAWEKEZAJI TANZANIA


Na Lydia Lugakila - Malunde1 blog
Serikali imesema haikuwafumbia macho watanzania watakaojaribu kuikashfu nchi kwa maneno ya propaganda zinazosababisha kuwakatisha tamaa wawekezaji kutoka nje na ndani ya nchi.

Kauli hiyo imetolewa Agosti 16 2019, na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Eng.Stella Manyanya akiwa mkoani Kagera katika hitimisho la wiki ya Uwekezaji Kagera iliyofanyika katika uwanja wa Gyamkana uliopo Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.


Manyanya alisema kuna baadhi ya watu wenye tabia ya kutoa maneno ya propaganda ya kuikashfu nchi ya Tanzania jambo linalokatisha tamaa wawekezaji mbalimbali wa ndani na nje ya nchi kuwekeza hapa nchini.

"Hatutokuwa tayari kuwakumbatia wanaokwamisha maendeleo, propaganda na maneno havina nafasi, serikali imejipanga kikamilifu na hatutamuonea huruma mtu yeyote anayetaka kujaribu kuichafua nchi hii iliyojawa amani na upendo",alisema.

"Watanzania tuache kuiuza nchi yetu kwa maneno ya Propaganda. Huu sio muda wa maneno maneno badala yake watu wajitathmini na kuona ni wapi wamefanikiwa na ni wapi wanakwama kibiashara kwa kukaa kwa pamoja na kujadiliana na kuinua uchumi wa mkoa wa Kagera na taifa kwa ujumla",aliongeza Manyanya.

Aliwataka wafanya biashara kuzingatia bidhaa bora huku akimpongeza Rais Magufuli kwa kuondoa utitiri wa kodi zilizokuwa zikikwamisha biashara nchini.

Aidha aliahidi ushirikiano na wana Kagera katika suala la kibiashara na kumpongeza mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Elisha Marco Gaguti katika kubuni wiki ya uwekezaji Kagera kwani hadi sasa Kagera imenoga kwa kuwa na fursa nyingi za uwekezaji.





Share:

Maombi ya kujiunga na veta 2019- VETA Call for application 2019

VETA CALL FOR APPLICATION: FURSA ZA KUJIUNGA NA MAFUNZO KATIKA VYUO VIPYA VYA VETA 2019, veta certificate, veta long courses,TANGAZO NAFASI ZA KUJIUNGA NA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI STADI KATIKA VYUO VYA VETA 2019, veta application form, veta courses 2019,  veta courses 2019, , fomu za kujiunga na veta 2019, sifa za kujiunga na veta 2019, sifa… Read More »

The post Maombi ya kujiunga na veta 2019- VETA Call for application 2019 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

SERIKALI YAPONGEZWA KUTIMIZA AHADI YA UMEME BUSINDE - KIGOMA

Na Rhoda Ezekiel -Malunde1 blog Kigoma
Wananchi wa kata ya Businde Manispaa ya Kigoma Ujiji,mkoani Kigoma wameishukuru serikali kwa kuwatatulia kero ya muda mrefu ya umeme na kuomba shirika la umeme kuongeza nguzo ili waweze wananchi wote wanaohitaji huduma hiyo nao wapate umeme.

Wakizungumza jana wakati wa zoezi la ufunguzi wa Umeme wa REA  katika kata hiyo uliyozinduliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Samson Anga, Mwenyekiti wa mtaa wa Businde Husein Yaga alisema kwa muda mrefu wananchi walingoja kufikishiwa huduma hiyo na sasa serikali imetimiza ahadi yake ya kuwapatia umeme. 

Hata hivyo alisema  eneo lililopata umeme ni dogo,   hivyo kuliomba  Shirika la umeme kuongeza maeneo ya kuunganisha umeme ili wananchi wote wapate kuunganishiwa umeme  hasa katika maeneo ya taasisi za dini na sokoni.

Naye Diwani wa kata ya Businde Masoud Masoud aliomba  Shirika la Umeme (TANESCO) kuwaongezea nguzo 76 ili waweze kuunganisha umeme kwa asilima 80% katika eneo hilo kwani wananchi wengi wanahitaji wa umeme.

Meneja  wa TANESCO Mkoa wa Kigoma  Masangija Lugata, aliwataka wananchi ambao nyumba zao sio kubwa kutumia kifaa cha Umeta  ambacho gharama yake ni shilingi elfu 27 pamoja na elfu 32 ya vifaa vingine ili kuepuka gharama na usumbufu wa wakandarasi katika uvutaji wa umeme.

Alisema Serikali ilitoa maelekezo Businde ipatewe umeme, kiasi cha shilingi  Milioni  122  zilitolewa kwaajili ya kukamilisha zoezi la umeme wa  kilovoti 21 na kuunganishia  wateja waawali 156  ambao wamefungiwa umeme katika kata ya Businde. 

Alisema baadhi  ya wananchi wamefanyiwa mchakato wa kupatiwa umeme na utaratibu wa kuunganisha umeme unaendelea.

Mkuu wa wilaya ya Kigoma Samson Anga, alisema aliahidi kutatua kero ya umeme katika kata hiyo na alizingumza na viongozi wanaohusika na kero hiyo na tayari imetatuliwa, hivyo Tanesco wanatakiwa kuongeza nguzo ili wananchi wote waweze kunufaika na huduma hiyo.

Alisema kitu kikubwa kinachochochea maendeleo ni umeme hivyo ana uhakika baada ya wananchi kupata umeme huo, wataanzisha shughuli mbalimbali ili waweze kujikwamua na umaskini.

Aidha kuhusu changamoto ya maji ambayo ni kero nyingine, aliahidi serikali itatauta kero hiyo kabla ya mwezi wa kumi na moja maji yataaanza kutoka katika kata ya Businde na kuepukana na changamoto ya ukosefu wa maji.
Meneja wa TANESCO Kigoma Masangija Lugata akionyesha Wananchi kifaa cha Umeta kinachotumia gharama kidogo katika kuunganisha umeme.

Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Samson Anga  akiwa na Meneja wa TANESCO Kigoma Masangija Lugata  na Diwani wa Kata ya Businde  wakati wa uzinduzi wa Umeme Businde
Share:

PICHA: Marais 12 kati ya 16 Wahudhuri Mkutano wa SADC Tanzania

Marais wa nchi 12 wamehudhuria mkutano wa kilele wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc) unaofanyika jijini Dar es Salaam leo Jumamosi Agosti 17, 2019 na kesho.

Mkutano huo umeanza saa 3:49 asubuhi na kuhudhuriwa na marais na mawaziri kutoka nchi wanachama, marais wastaafu, viongozi na washiriki mbalimbali.

Marais hao ni John Magufuli (Tanzania),  Cyril Ramaphosa (Afrika Kusini), Azali Assoumani (Comoro),  Danny Faure (Shelisheli),  Joao Manuel Goncalves (Angola).

Wengine ni Edgar Lungu (Zambia), Felix Tshisekedi (DRC),  Andry Rajoelina (Madagascar), Emerson Mnangagwa (Zimbabwe), Filipe Nyusi (Msumbiji) na Dk Hage Geingob (Namibia).

Nchi  ya Eswatin imewakilishwa na waziri mkuu,  Ambrose Dlamini;  Lesotho pia imewakilishwa na waziri mkuu, Motsahai Thabane  huku Malawi ikiwakilishwa na makamu wa rais sambamba na Botswana na Mauritius zilizotuma wawakilishi.


Share:

Tanzania Yamwagiwa SIFA Kwa Kuwa Nchi Pekee ya SADC Ambayo Uchumi Wake Unakua Kwa Asilimia 7

Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya SADC  Dr. Stergomena Lawrence Tax ameipongeza Tanzania kuwa nchi pekee ambayo imeongoza kwa kukidhi vigezo vya ukuaji wa uchumi, kwa kufikia asilimia 7, ikiwa ni tofauti na nchi nyingine.

Kauli hiyo ametoa wakati wa mkutano wa kwanza wa SADC uliofanyika jijini Dar es salaam, ambapo viongozi mbalimbali wa jumuiya hiyo wakiwemo viongozi wastaafu na Mawaziri wamehudhuria.

Dk.Tax amesema kwa nchi za jumuiya hiyo pamoja na mambo mengine kwenye eneo la uchumi kuna malengo ambayo yamewekwa kwa nchi wanachama na Tanzania ni nchi pekee ambayo uchumi wake unakuwa kwa asilimia saba na hivyo wanastahili kupongezwa.

 "Uhimilivu wa uchumi ni nyenzo muhimu katika maendeleo, nchi wanachama zimekidhi vigezo vya SADC kiuchumi, takwimu zimeonesha Tanzania inafanya vizuri, na kwa vigezo pekee Tanzania ndiyo nchi pekee ambayo imefikia ukuaji wa asilimia 7, mjipongeze." Amesema Dr Tax na kuongeza;
 

"Katika kufikia uchumi wa Viwanda nchi wanachama hawana budi kukuza uzalishaji wa umeme, kwa kuwa ni kitu muhimu kwenye ujenzi wa viwanda, nashukuru katika wiki ya Viwanda  hata Tanzania ,  tumeona mradi mkubwa wa umeme katika maporomoko ya mto Rufiji ambao ujenzi wake unaendelea"


Share:

Bashe ataka Bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko kuwa kiungo cha biashara ya mazao Baina ya Kenya na Tanzania

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
NAIBU Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe amesema kikao cha kwanza baina ya timu ya wataalamu wa masuala ya Mazao ya Chakula hapa nchini ikiongozwa na Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) na ya wenzao kutoka Kenya zinakutana hapa nchini leo Agosti 17, 2019 ili kujadiliana namna bora ya kufanya biashara ya mazao hayo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana usiku Agosti 16, 2019 kwenye ofisi za Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC), jijini Dar es Salaam, Mhe. Bashe alisema, kikao hicho ni makubaliano baina ya nchi hizo mbili kukutana na kujadili namna gani wafanyabiashara wa Kitanzania na wenzao wa Kenya watafanya  biashara ya mazao ya chakula na iwe biashara endelevu.

“Biashara tayari imekwisha anza na wakati tunaendelea mpaka sasa wenzetu wa Kenya wamekwishanunua jumla ya tani 34,000 kupitia kwa wafanyabiashara wetu na biashara hiyo inaendelea.” Alifafanua.

Alisema timu ya wataalamu kutoka Tanzania itaongozwa na watu kutoka Wizara ya Kilimo, Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mamlaka ya Viwango Tanzania (TBS) ili wakae chini na wakubaliane utaratibu wa namna gani  wafanyabiashara wa Tanzania na wenzao wa Kenya watafanya biashara ya mazao ya chakula.

“Sisi Wizara ya Kilimo jukumu letu ni kufanya mambo makubwa mawili, kuhamasisha uzalishaji wa mazao na kufungua masoko ya wakulima wetu ili waweze kufanya biashara.” Alifafanua.

Alisema katika kikao hicho wametaka mamlaka za viwango za Kenya na Tanzania zijumuishwe kwenye majadiliano hayo ili wazalishaji wa sembe waliosajiliwa Tanzania waweze kusajiliwa Kenya Bureau of Standards ili bidhaa zao ziweze kwenda katika soko la Kenya bila vikwazo vyovyote.

“Tunatengeneza Government Agreement ambayo itaonyesha mpango kazi (frame work) ya namna biashara hii itafanyika, tumeshaiteua Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko ambayo ndiyo itakayokuwa kiongozi msimamizi na kiungo wezeshi katika biashara hiyo.” Alibainisha Mhe. Bashe.


Share:

Ufahamu Ugonjwa Wa Ngiri Na Tiba Yake

Tatizo la Ngiri Linavyosababisha Upungufu wa Nguvu za Kiume na Maumbile Kusinyaa, Dalili zake Hizi Hapa..Makala
51 minutes ago

Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).

Dalili za Ngiri
Tumbo kuunguruma, kiuno kuuma, kupata choo kama cha mbuzi, kushindwa kufanya tendo la ndoa, mishipa ya uume kulegea, kutokuwa na hamu ya kulundia tendo la ndoa, korondani moja kuvimba, mgongo kuuma.

Dalili zingine za ugojwa wa ngiri ni pamoja na;

Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu kama Direct Scoratal inguinal Hernia.


Uvimbe unaojitokeza tumboni na kuteremka hadi ndani ya korodani, uvimbe huu hauumi na unaweza kurudishwa kwa urahisi iwapo mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole, uvimbe huu.


Na pindi ukikubali kurudi ndani ndipo unapoitwa Reduible direct scrotal inguinal hernia.


Na pia endapo utashindikana kurudi tumboni ndipo unapoitwa Irreduible direct scrotal inguinal hernia.


Ugojwa huu wa ngiri unaweza kutibika

Mpate mpenzi wako unayempenda na kumfunga mume,mke mpenzi asitoke kwa mwingine .

Kwa Ushauri na Msaada wa Wasaliana na  0714006521


Share:

Dkt. Slaa Awakemea Watanzania Wanaoikosoa Serikali Mitandaoni

Balozi wa Tanzania nchini Sweden Dkt. Wilbord Slaa amekemea tabia ya baadhi ya watanzania kubeza miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali ya awamu ya tano huku akibainisha kuwa vitendo vya kutumia mitandao ya kijamii kukosoa utendaji wa serikali unawapa shida mabalozi kuitetea nchi huko walipo,kwasababu vitendo hivyo vinawakatisha tamaa wahisani wanaotaka kuisaidia Tanzania.

Dkt. Slaa ametoa kauli hiyo wakati akifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Startv wakati wa ziara ya mabalozi wa Tanzania kutoka nchi mbalimbali duniani walitembelea mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa SGR eneo la Soga Mkoani Pwani.

Ametoa mfano kutokana na kauli aliyoitoa kongozi fulani ambaye hakumtaja imesababisha watalii 100 kutoka Sweden kuahirisha safari ya kija Tanzania kwa ajili ya kutalii.

Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali wapo katika ziara ya kutembelea na kuijonea utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali ya awamu ya tano kwa fedha za ndani.

Credit: Startv.


Share:

LIVE: Mkutano Wa 39 Wa Wakuu Wa Nchi Za SADC - Dar Es Salaam Tanzania

LIVE: Mkutano Wa 39 Wa Wakuu Wa Nchi Za SADC - Dar Es Salaam Tanzania


Share:

Jela Miaka 30 Kwa Kumpa Mimba Mwanafunzi

Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Kigoma imemuhukumu miaka 30 jela mkazi wa kata ya Mwanga manispaa ya Kigoma Ujiji, Isack Balayabala (25)  baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumpa ujauzito mwanafunzi wa kidato cha nne shule ya Sekondari Kaulananga.

Akisoma hukumu hiyo jana Ijumaa Agosti 16, 2019  hakimu wa mahakama hiyo, Eliya Baha alisema mshtakiwa alitenda kosa hilo Desemba 2018 kwa  kumpa ujauzito mwanafunzi huyo.

Katika kesi hiyo ya  jinai namba 46 ya mwaka 2019 mahakama hiyo imesema  imeridhishwa na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na hivyo kwa kuzingatia  kifungu cha sheria cha 60A kifungu kidogo cha (3) cha sheria ya elimu namba 353 ya mwaka 2002 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2016, mtuhumiwa atatumikia kifungo cha miaka 30 Jela


Share:

Polepole: Rais Magufuli amenituma niwaeleze kwamba hataongeza hata dakika tano Muda wake wa Uongozi Ukiisha

Katibu wa Itikadi na unenezi wa Chama cha mapinduzi (CCM) Humphrey Polepole amesema kuwa ametumwa na Mwenyekiti wa chama hicho ambaye pia ni Rais wa Tanzania Dr. John Magufuli awaeleze watanzania wote kuwa hayupo tayari kuendelea kuongoza nchi mara baada ya muda wake wa uongozi kufika kikomo kama ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakitaka iwe hivyo.

Polepole amezungumza hayo  jana akiwa mkoani Dodoma wakati akizungumza na baraza kuu la umoja wa wanawake wa chama hicho (UWT) ambapo amewataka wanachama hao kuacha kuendeleza mjadala huo ambao Mwenyekiti wao amesema unamkwaza.

Kwa mujibu wa Polepole, aliitwa na Mwenyekiti wa CCM Rais Magufuli na kumtaka awatangazie Watanzania kwamba nchi inaongozwa na katiba na sheria.

Alisema Rais alisikia watu wakizungumza kuhusu kuongezewa muda baada ya kumaliza ukomo wa muda wa uongozi wake na kusema ni jambo linalomkwaza.

Alisema muda wake wa kumaliza uongozi ukifika mwisho atang'atuka mara moja na hataongeza hata dakika tano kwa kuwa uongozi ni mgumu.

"Wale wanachama wenzangu ambao mnaendeleza huu mjadala wa kuongezwa muda wa uongozi naomba muuwache maana Mwenyekiti anasema anakwazwa,"alisema Polepole.

Kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa, aliwataka katika kuteua wagombea wajiepushe na walaghai na wasio kubalika na jamii kwa kuwa inawavunja moyo wanawake ambao ni wapiga kura waaminifu.

"Wapiga kura waaminifu ni wanawake lakini tungesema wanaume wakapige kura tungeshaliwa kitambo. Tusiwavunje moyo wanawake kwa kuwateulia wagombea wasio na uwezo,"alisema.

Sambamba na hilo, Katibu alisisitiza kuendelea kuwatumia wanawake kwenye nafasi mbalimbali za uongozi kwa kuwa watalisaidia taifa kupiga hatua zaidi kimaendeleo.


Share:

Serikali Yaahidi Kuendelea Kutatua Changamoto Za Utalii Nchini.

Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imesema itaendelea kupunguza adha mbalimbali  zinazowakabili Wadau wa Utalii likiwemo suala la  polisi wa usalama barabarani kusimamisha magari yenye watalii mara kwa mara.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu alipokuwa akizungumza na Wadau wa Utalii nchini  katika kongamano la Utalii lililofanyika mkoani Arusha.

Amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau wa utalii nchini imejenga vituo vya ukaguzi wa magari vya utalii ili kupunguza usumbufu kwa watalii barabarani.

Amesema vituo  hivyo vitashughulikia masuala ya msingi likiwemo suala madereva wenye watalii kupimwa kilevi.

Amesema mbali na kilevi, Vituo hivyo vitashughulikia vitendo vyote ya uhalifu watakavyofanyiwa watalii.

Aidha, Mhe.Kanyasu amesema lengo la Serikali ni kupunguza kero kwa watalii ili wafikie milioni mbili mwaka 2019.

Akizungumza kwenye kongamano hilo, Mhe.Kanyasu amesema licha ya  kujengwa vituo hivyo  vya ukaguzi lakini  bado kuna kero ambazo  zinafanyiwa  kazi lengo likiwa ni kuboresha sekta ya utalii.

Kwa upande wake, Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Jonathan Shana amewataka wadau wa utalii kufuata sheria lakini akataka kupewa taarifa za polisi wanaowakwaza.

"Nipigieni simu hata saa nane za usiku kwa askari wanawaomba rushwa nishughulike nao" Alisisitiza Shana.

Naye Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe.Mrisho Gambo amesema lengo la Arusha kuanzisha vituo vya ukaguzi magari ni kupunguza kero.

Amesema uwepo wa vituo hivyo vitafanya  mazingira bora kwa  watalii na wafanyabiashara.

Mwenyekiti wa Chama cha Wasafirishaji Watalii (TATO) Wilbard Chambulo amesema ujenzi wa vituo hivyo ni hatua muhimu ya kuwahakikishia watalii usalama wao pindi  wakiwa barabani pamoja na mali zao.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Prof.Adolf Mkenda amesema mkoa wa Arusha ni mfano wa kuigwa kwa mikoa mingine kwa kujenga vituo hivyo ili kupunguza kero kwa watalii.


Share:

Rais Wa Zambia Edgar Lungu Aongoza Kikao Cha Siasa,ulinzi Na Usalama Cha SADC Troika Jijini Dar

Rais wa Zambia Mh. Edgar Changwa Lungu,ambaye ni  Mwenyekiti wa Taasisi ya Siasa, Ulinzi na Usalama (SADC Troika) pichani kati akiongoza kikao cha ulinzi na usalama kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika – SADC (SADC) kilichofanyika  jana jioni  kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo kwa nchi za Kusini mwa Afrika – SADC, Dkt Stergomena Tax.

Rais wa Angola Mh. Joao Lourenco Mwenyekiti wa Taasisi ya Siasa, Ulinzi na Usalama (SADC Troika) anayemaliza muda wake akiwa katika kikao hicho kilichofanyika jana jioni kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Rais wa Zimbabwe Mh. Emmerson Dambudzo Mnangagwa anayechukua nafasi ya Uenyekiti wa Taasisi ya Siasa, Ulinzi na Usalama (SADC Troika) akipitia baadhi ya nyaraka za kikao hicho kilichofanyika jana  jioni kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.


Share:

MENO BANDIA YAKWAMA KOONI KWA WIKI MOJA..ASHINDWA KUMEZA VITU

Mgonjwa mmoja nchini Uingereza amejikuta katika maumivu makali baada ya meno yake ya bandia kunasa kooni kwa wiki moja.

Mgonjwa huyo mwenye miaka 72 alikuwa akilalamika kupata maumivu makali wakati wa kumeza vitu na kukohoa damu katika kipindi chote hicho.

Bwana huyo, alimeza meno hayo wakati akifanyiwa upasuaji wa tumbo.

Undani wa tukio hilo umechapishwa kwenye jarida la kisayansi la BMJ ambapo watunzi wake wamewataka madaktari kuhakikisha wagonjwa wao wanaondoa meno ya bandia kabla ya upasuaji.

Siku sita tu baada ya upasuaji huo uliofanyika mwaka 2018, bwana huyo alienda kwa daktari na kulalamika kuwa anashindwa kumeza vyakula vizito.

Madaktari awali waliamini kuwa hiyo ni athari ya kuwekewa mpira kwenye kinywa wakati wa upasuaji, na kumpatia dawa za kukabiliana na maumivu na maambukizi ya koo.

Lakini baada ya bwana huyo kurudi tena baada ya siku mbili akiwa na malalamiko zaidi, madaktari ikabidi wamfanyie uchunguzi zaidi wa koo.

Vipimo vya miale ya X-Ray vikaonesha kuwa kuna meno ya bandia matatu na chuma chake cha kuyashikilia.

Baada ya hapo, mzee huyo akawaambia madaktari kuwa alipoteza meno yake ya bandia katika kipindi ambacho alilazwa hospitalini kwa upasuaji wa tumbo.

Ikalazimika afanyiwe upasuaji wa haraka wa koo, lakini akarudi hospitali mara nne zaidi ili kuongezewa damu.Hospitali ya Chuo Kikuu cha James Paget imesema imejifunza kutokana na makosa ya upasuaji huo.

Watafiti wameeleza katika ripoti yao kuwa kuna zaidi ya mkasa mmoja wa watu kumeza meno ya bandia wakati wakipigwa dawa za usingizi.

Uwepo wa meno bandia ama kifaa chochote cha bandia kinywani, unatakiwa uripotiwe kabla nda baada ya upasuaji, wamesisitiza kwenye ripoti ya jarida hilo.

Hazel Stuart, ambaye ni mkurugenzi wa matibabu katika hospitali ya Chuo Kikuu cha James Paget ambapo upasuaji huo ulifanyika amesema uchunguzi wa kina ulifanyika juu ya tukio hilo.

"Baada ya tukio hilo, michakato yetu imepitiwa upya, na maboresho yamefanyika katika kila eneo la mahitaji, na tuliyojifunza tumehakikisha yanawafikia wafanyaki wetu wote ili kuepuka makosa," amesema.
Chanzo - BBC
Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi 17 August

















Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger