Thursday, 1 August 2019

TOUFIQ: Tanzania Kinara Katika Udahili Wa Wanafunzi Elimu Ya Awali Barani Afrika.

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
IMEELEZWA kuwa Tanzania ni kinara katika suala la udahili wa wanafunzi katika elimu ya awali barani Afrika na hivyo kuifanya kupiga kubwa katika utekelezaji wa maelengo ya maendeleo endelevu(SDGs).  

Mafanikio hayo yanatokana na serikali kutoa elimu bure bila malipo ambao umechangia kuongeza udahili wa watoto wengi kupata fursa ya kupata elimu. 

Hayo yamebainishwa na Mbunge wa Viti maalum FATUMA TOUFIQ ambaye ni pia champion wa masuala ya SDGs bungeni wakati akitoa mrejesho kwa waandishi wa habari kuhusu mkutano aliohudhuriwa wa ‘High level political forum’ uliofanyika Umoja wa Mataifa(UN) hivi karibuni. 

Amesema katika mkutano huo waliwasilisha malengo 6 ya SDGs ambayo kwa ujumla wake Tanzania imefanya vizuri ikiwemo ujenzi wa miundombinu na kutoa wito kwa serikali. 

TOUFIQ ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika linalojishughulisha na wanawake na watoto(Wowap), amesema katika mkutano huo alipelekwa kwa ufadhili kutoka Shirika la Equal Measure 2030 la nchini Marekani  linalojihusisha na masuala ya usawa wa kijinsia na kusaidia nchi zinazoendelea kufikia malengo hayo ili kuhakikisha kunakuwa kuna usawa kwenye mambo mbalimbali ikiwemo elimu. 

Mkutano huo ulikuwa kwa ajili ya utoaji taarifa jinsi nchi ilivyofanya katika utekelezaji wa SDGs na Tanzania ndio ilikuwa mara yake ya kwanza kutoa ripoti yake iliyowasilishwa na Waziri wa Fedha Dk.Philipo Mpango.


Share:

Rais Magufuli Kuzindua Uwanja wa ndege wa Julius Nyerere terminal 3 Leo

Rais John Magufuli leo Alhamisi Agosti Mosi, 2019, anatarajia kuzindua mradi wa upanuzi wa Uwanja wa ndege wa Julius Nyerere la terminal 3, ambao umetekelezwa kwa miaka6 kwa gharama ya Sh788.6 bilioni.

Mradi huo ulianza kujengwa 2013 na awali ulipangwa kutekelezwa kwa Sh705.3 bilioni lakini kutokana na kubadilika kwa taratibu za kikodi, mchoro wa mradi (Design) na gharama ya mradi huo iliongezeka kwa Sh85.3 bilioni.

Wakati mradi unaanza ulitarajiwa kuwa ungekamilika Desemba 2017, baadaye ukaongezewa mwaka mmoja hadi Desemba 2018, lakini haukukamilika badala yake umekamilika Mei, mwaka huu.

Kampuni iliyotekeleza mradi huo ni BAM International ya Uholanzi ambayo ndiyo iliyofanya kazi za kikandarasi na Arab Consulting Engineers (ACE) ya Misri, ilifanya kazi za ushauri.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi 01 August



























Share:

Wednesday, 31 July 2019

Waziri Mkuu Majaliwa Akagua Maandalizi Ya Mapokezi Ya Wajumbe Wa Mkutano Wa Sadc Kwenye Kiwanja Cha Ndege Cha Julius Nyerere

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua jengo la tatu la abiria kwenye kiwanja cha ndege cha Mwalimu Nyerere ili kuona maandilizi ya mapokezi kwa wajumbe wa mkutano wa SADC.

Akizungumza na watendaji wa Serikali pamoja na Kamati ya maandalizi uwanjani hapo leo jioni (Jumatano, Julai 31, 2019), Waziri Mkuu amesema maandalizi ni mazuri isipokuwa kwa kasoro chache zilizobakia.

“Nimepita VIP hakuna shida. Pale terminal 2, sehemu ya Uhamiaji iko vizuri, uchunguzi wa afya nayo iko vizuri, lakini vyoo inabidi vibadilishwe haraka sana. Vile vyoo pale nje vimechoka, vibadilishwe mara moja, siyo tu kwa ajili ya ugeni, bali ni kwa faida yetu pia,” amesema huku akimwagiza meneja wa uwanja huo, Bw. Paul Lugasha aharakishe zoezi hilo.

Katika jengo la tatu la abiria kwenye uwanja huo, Waziri Mkuu amekagua eneo ambalo viongozi wakuu wa nchi watashukia, watakagua gwaride la heshima na kuangalia vikundi vya ngoma. Pia amekagua vyumba ambavyo watapumzikia kabla ya kuelekea mjini.

Amesisitiza kuwa usafi wa barabarani bado hauridhishi sababu kuna mawe, udongo na michanga kwenye barabara kuu ya kutoka uwanja wa ndege hadi mjini. “Tulikubaliana kuwa zile bustani ziboreshwe, vyuma vya barabarani vitengenezwe lakini hata leo nimepita kwenye fly-over, bado kuna mawe na michanga, hata sijui vinatokea wapi,” alisema.

Amewataka wahusika waweke banners za kutosha za aina mbalimbali na picha za wanyama kutani, uwanjani hapo ili kuonesha kwamba kuna mkutano mkubwa unafanyika hapa nchini.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu amewataka Watanzania watumie fursa ya uwepo wa mkutano huo mkubwa kuendesha biashara zao na ujasiriamali.

“Ziko fursa nyingi za uwepo wa mkutano huu. Kila mmoja atumie nafasi hii kuweza kuongeza na kuboresha kazi yake inayomletea uchumi,” amesema.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,       
JUMATANO, JULAI 31, 2019.


Share:

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan Awataka Wadau Wa Mazingira Kutekeleza Sheria,kanuni,na Taratibu Za Mazingira.

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
MAKAMU wa Rais SAMIAH SULUHU HASSAN amewataka wadau wa mazingira kutekeleza Sheria,Kanuni na maandiko ili kuhimiza utunzaji wa rasilimali misitu na kurahisisha upatikanaji wa rasilimali za maji. 

Akizindua jukwaa la maendeleo endelevu kuhusu usimamizi bora wa misitu kwa upatikanaji wa rasilimali maji endelevu leo jijini Dodoma Makamu wa Rais amesema misitu ndio chanzo kikubwa cha rasilimali maji hivyo isipotunzwa na kusimamiwa vizuri watakuwa wanahatarisha upatikanaji wa maji kwa matumizi ya kijamii,kibiashara na kuimarisha mazingira. 

Ametaja mambo yanayosababisha athari kubwa kwa uhai wa rasiliamli maji kuwa ni kilimo kisichokuwa endelevu,ujenzi holela,uchomaji mkaa,ukataji kuni,uvunaji haramu wa magogo na ufugaji usiozingatia kanuni. 

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira GEORGE SIMBACHAWENE amesema haridhishwi na hali ya mazingira ilivyo na kuwataka wadau hao kupeleka fedha katika mazingira yanayoharibika badala ya kutumia kwenye makongamano. 

Kwa upande wake mkuu wa Mkoa wa Dodoma dokta BINILITH MAHENGE amesema ni vyema jamii ikijikita katika kulinda na kutunza mazingira na kwa viongozi kutekeleza yale wanayoazimia. 

Naye mkuu wa taasisi ya uongozi profesa JOSEPH SEMBOJA amesema  sekta ya maji na misitu ni muhimu hivyo ni vyema sera, mikakati na taasisi zinazohusu sekta hiyo  zikafungamana ili ziweze kufnaya kazi kwa ufanisi.
 
Jukwaa la maendeleo endelevu lilianzishwa mwaka 2012 ili kuwakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya maji na misitu ili waweze  kujadili mpango wa maendeleo endelevu.


Share:

KISANDU ACHAGULIWA KUWA NAIBU MEYA MANISPAA YA SHINYANGA




Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga John Kisandu

Na Marco Maduhu - Malunde1 blog Shinyanga

Diwani wa Kata ya Chibe manispaa ya Shinyanga John Kisandu (CCM) amechaguliwa kwa mara nyingine tena kuwa Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga, na kumshinda mpinzani wake Zena Gulamu (Chadema).


Uchaguzi huo wa Naibu Meya umefanyika leo Julai 31,2019 kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa baraza la madiwani wa kumchagua Naibu Meya pamoja na Kamati mbalimbali, ambazo zitasimamia utekelezaji wa maendeleo ya Manispaa hiyo, ikiwamo kamati ya fedha ya kudumu, uchumi, elimu na afya, miundombinu, ukimwi, maadili pamoja na Jumuiya ya Serikali za Mitaa (ALAT).

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo, mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi, amesema John Kisandu kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) ameibuka mshindi kwa kupata kura 15, dhidi ya mpinzani wake Zena Gulam kutoka Chadema ambaye amepata kura tano ,ambapo wajumbe waliopiga kura walikuwa 20.

Akizungumza mara baada ya kupata ushindi huo, Kisandu ameomba ushirikiano kutoka kwa madiwani hao na kuwa kitu kimoja katika kuisimamia halmashauri kwa maslahi mapana ya wananchi na kuwaletea maendeleo.

Aidha madiwani hao wameendelea kujadili ajenda mbalimbali zikiwamo za afya, elimu, maji, miundombinu, fedha, kwa ajili ya mustakabali wa maendeleo ya manispaa hiyo.

TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI

Diwani wa Kata ya Chibe Manispaa ya Shinyanga kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM John Kisandu, akiomba kuchaguliwa kuwa Naibu Meya kwa mara nyingine tena, ambapo alishinda kiti hicho kwa kura 15.

Diwani wa viti wa maalumu Manispaa ya Shinyanga Zena Gulamu kupitia tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema(, akiomba kuwa naibu meya wa manispaa ya Shinyanga, ambapo alipata kura tano.

Madiwani wakipiga kura kumchagua Nibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga.

Upigaji kura ukiendelea.

Upigaji kura ukiendelea wa kumchagua Naibu Meya wa manispaa ya Shinyanga.

Upigaji kura ukiendelea wa kumchagua Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga.

Upigaji kura ukiendelea wa kumchagua Naibu Meya wa manispaa ya Shinyanga.

Upigaji kura ukiendelea wa kumchagua Naibu Meya wa manispaa ya Shinyanga.

Naibu meya wa manispaa ya Shinyanga John Kisandu akijipigia kura ya kuchaguliwa kuwa Naibu Meya kwa mara nyingine.

Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi akimtangaza diwani wa Kata ya Chibe John Kisandu kuwa mshindi wa Kiti cha Unaibu Meya kwa mara nyingine.

Naibu meya wa manispaa ya Shinyanga John Kisandu akizungumza mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa kiti hicho tena, na kuwataka madiwani kushirikiana kwa pamoja kusimamia maendeleo ya halmashauri.

Madiwani wakiendelea na baraza mara baada ya kumaliza kuchaguzi wa Naibu Meya wa manispaa ya Shinyanga na wajumbe wa kamati mbalimbali.

Madiwani wakiendelea na baraza.

Baraza la madiwani likiendelea.

Baraza la madiwani likiendelea.

Diwani wa Kata ya Kitangili Hamisi Ngunila (CHADEMA), akizungumza kwenye baraza hilo.

Diwani wa Kata ya Ndala Wiliamu Shayo(CHADEMA) akizungumza kwenye baraza.

Baraza likiendelea.

Watendaji wa manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye baraza la madiwani.

Watendaji wa manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye baraza la madiwani.

Naibu meya wa manispaa ya Shinyanga John Kisandu, akifunga mkutano wa mwaka wa baraza la madiwani na kuwataka watendaji na madiwani kila mtu awajibike kwenye nafasi yake ili kuleta maendeleo kwenye manispaa hiyo.

Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger