Tuesday, 14 May 2019

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumanne Ya May 14




Share:

Waziri Kigwangallah Azindua Mpango wa kuwafungaTembo Mikanda ya GPS Utakaogharimu sh Milioni 800

Zaidi ya sh 800 milioni zinatarajiwa kutumika katika zoezi la kuwafunga mikanda ya mawasiliano ya kijiographia(GPS) Tembo ambao wanapatikana hifadhi ya jamii ya wanyamapori ya Makao na Pori la Akiba la Maswa.

Waziri wa Maliasili na Utalii,Dk Hamis Kigwangallah jana  amezindua mpango huo katika eneo la Makao WMA ambalo imewekeza kampuni ya Mwiba Holding moja ya kampuni zilizochini ya Taasisi ya Friedkin Conservation Fund(FCF)

Waziri Kigwangala alisemaVifaa hivyo il vya GPS vitawezesha Tembo kufatiliwa mienendo yao na kudhibitiwa matukio ya Tembo kuvamia mashamba na masuala ya ujangili.

Alisema katika mpango huo pia kutakuwa na uzio wa technolojia ya kielekronik ambao utawezesha kuonekana Tembo ambao wanatoka maeneo ya hifadhi kabla ya kufanya madhara.

Waziri Dk Kigwangallah alipongeza taasisi ya Friedkin Conservation Fund(FCF) kwa kufadhili mradi huo na kueleza wizara yake ilifanya utafiti na kubaini taasisi hiyo ni miongoni mwa taasisi safi zinazoendekeza uhifadhi.

Waziri Kigwangallah pia alipongeza watafiti kutoka taasisi ya utafiti wa wanyamapori(TAWIRI) kwa kuendesha zoezi hilo.

Mkurugenzi wa Friedkin Conservation Fund(FCF) Nicholas Negri alisema mradi huo utasaidia sana uhifadhi nchini na kuvutia watalii zaidi.

Alisema FCF itaendelea kishirikiana na serikali katika kuendeleza uhifadhi kwani pia tayari wamefadhili mradi wa kuwafunga vifaa vya mawasiliano Faru ili kuwalinda na ujangili.

Mtafiti Mkuu wa TAWIRI, Dk Edward Kohi amesema mradi huo,unatarajia kugharimu dola 300,000 ambazo ni zaidi ya sh 800 milioni.

Amesema katika eneo la hifadhi ya jamii ya makao na pori la akiba la Maswa Tembo 18 watafungwa vifaa vya GPS na katika maeneo mengine tayari Tembo 95 wamefungwa GPS.

Mtafiti wa Tawiri Dk Emmanuel Masenga amesema hadi sasa Tembo 95 wamefungwa mikanda ya GPS maeneo mbali mbali ya hifadhi nchini.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo ,Mkuu wa mkoa wa Simiyu,Anthony Mtaka alisema mpango huo wa kuwafunga Tembo GPS utasaidia kuondoa migogoro baina ya wa hifadhi na jamii.

Alisema wananchi wamekuwa wakipiga simu mara kadhaa kuomba msaada pale Tembo wanapovamia mashamba yao.

“Sasa Tembo kufungwa GPS ni faraja kwetu lakini pia tunapongeza mwekezaji wetu Mwiba Holdings kwa  mradi huo” alisema


Share:

Maamuzi ya Serikali baada ya Wakurugenzi kuzuiwa kusimamia Uchaguzi

SERIKALI imewasilisha notisi katika Mahakama ya Rufaa kupinga uamuzi ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kuhusu kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na Bob Wangwe dhidi ya mwanasheria mkuu wa Serikali (AG) na wenzake.

Uamuzi huo wa Serikali umebainishwa jana Jumatatu, Mei 13, 2019 na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Profesa Aderladus Kilangi, wakati akizungumza na wanahabari kutoa msimamo wa Serikali kuhusu hukumu hiyo ya Mahakama Kuu.

Ijumaa iliyopita Mahakama Kuu katika hukumu yake iliyotolewa na jopo la majaji watatu, Dk. Atuganile Ngwala, Dk Benhajj Masoud na Firmin Matogolo ilibatilisha kifungu cha 7(1) cha Sheria ya Uchaguzi kinachoipa mamlaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuwateua wakurugenzi wa majiji, manispaa na miji kuwa wasimamizi wa uchaguzi.

Pia ilibatilisha kifungu cha 7(3) kinachoipa NEC mamlaka ya kuteua mtu yeyote miongoni mwa watumishi wa umma kuwa msimamizi wa uchaguzi.

Katika hukumu hiyo mahakama hiyo ilisema kwamba vifungu hivyo ni kinyume cha Katiba ya nchi ikibainisha kuwa wakurugenzi hao huteuliwa na Rais aliyeko madarakani ambaye hutokana na chama tawala na kwamba wengine ni wanachama wa chama cha mamlaka inayowateua jambo ambalo huathiri utendaji wao katika kutenda haki.

Pia ilisema kwamba sheria haijaweka ulinzi kwa NEC kumteua mtumishi yeyote wa umma kuhakikisha kuwa anakuwa huru katika kutekeleza majukumu yake..


Share:

Monday, 13 May 2019

TAASISI YA UTAFITI WA WANYAMAPORI(TAWIRI ) NA FRIEDKIN CONSERVATION FUND LIMITED(FCFL) WAFUNGA VIFAA MAALUMU TEMBO 18


Waziri wa Maliasili na Utalii,Dk Hamis Kigwangala(wa pili kushoto) akiwa pamoja na Mkuu wa mkoa wa Simiyu,Anthony Mtaka ,Mkuu wa wilaya ya Meatu,Dk Joseph Chilongani(kulia) na Meneja wa shirika linalojihusisha na uhifadhi la Friedkin Conservation Fund Limited(FCFL),Nana Grosse alipowasili kwenye uwanja mdogo wa ndege wa Mwiba Wildlife Ranch kushuhudia uwekaji mikanda maalumu ya ufatiliaji mienendo ya Tembo eneo la Maswa Game Reserve.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Dk Hamis Kigwangala akizungumza kabla ya kushudia uwekaji wa mikanda maalumu ya ufatiliaji mienendo ya Tembo kwenye Pori la Maswa Game Reserve uliofadhiliwa na shirika linalojihusisha na uhifadhi la Friedkin Conservation Fund Limited(FCFL) katika eneo la Mwiba Wildlife Ranch.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Dk Hamis Kigwangala(kulia) akishuhudia uweka uwekaji wa mikanda maalumu ya ufatiliaji mienendo ya Tembo kwenye Pori la Maswa Game Reserve uliofadhiliwa na shirika linalojihusisha na uhifadhi la Friedkin Conservation Fund Limited(FCFL) katika eneo la Mwiba Wildlife Ranch . 
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (Tawiri),Dk Janemary Ntalwila akionesha mchoro wa namna kifaa maalumu cha ufatiliaji mienendo ya Tembo kwenye Pori la Maswa Game Reserve uliofadhiliwa na shirika linalojihusisha na uhifadhi la Friedkin Conservation Fund Limited(FCFL) katika eneo la Mwiba Wildlife Ranch . 
Mtafiti Mwandamizi wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (Tawiri),Dk Edward Kohi akizungumza mienendo na tabia za Tembo huku Waziri wa Maliasili na Utalii,Dk Hamis Kigwangala akimsikiliza kwa makini. 
Waziri wa Maliasili na Utalii,Dk Hamis Kigwangala akifurahia jambo baada ya zoezi la uwekaji kifaa hicho kukamilika,jumla ya Tembo 18 wamewekewa mikanda yenye vifaa maalumu ya kuwafuatilia mienendo yao. 
Wataalamu wakimfuatilia mmoja wa Tembo ambaye alifungwa kifaa maalumu 
Wataalamu wa Wanyamapori wakimfuatilia mmoja wa Tembo aliyefungwa kifaa hicho kinachowawezesha kufahamu mienendo yake katika ikolojia ya uhifadhi.
Share:

Picha : BUNGE LA AFRIKA LAZITAKA SERIKALI KUTATUA VYANZO VYA WIMBI LA WAKIMBIZI..MHE. SILINDE AKOMALIA UONGOZI BORA


Wabunge wa bunge la Afrika wameziomba nchi zinazokabiliwa na tatizo la wakimbizi barani Afrika kutatua vyanzo vinavyochangia wimbi la wakimbizi ambavyo ni vita na migogoro,ukosefu wa ajira kwa vijana,ubaguzi na kutokuwa na usawa wa kijinsia na ukiukwaji wa haki za binadamu.

Wabunge hao wametoa ushauri huo leo Jumatatu,Mei 13,2019 wakati wa kikao cha tano cha Mkutano wa pili wa Bunge la tano la Afrika kinachoendelea jijini Johannesburg, Afrika Kusini.

Kikao hicho kilijikita zaidi kujadili kauli mbiu ya Umoja wa Afrika mwaka 2019 ambayo ni "Mwaka wa Wakimbizi,Wahamiaji waliorejeshwa kwao na wakimbizi wa ndani Barani Afrika : Mchango wa Bunge la Afrika katika kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa tatizo la uhamiaji wa kulazimishwa barani Afrika".

Wabunge hao wamesema ili kumaliza tatizo la watu kukimbia nchi zao barani Afrika, ni vyema serikali zikapiga vita vyanzo vya ukimbizi ikiwemo kuzingatia demokrasia na utawala bora huku viongozi wakiacha tabia ya kung'ang'ania madarakani.

Akichangia hoja bungeni,Mhe. David Silinde kutoka Tanzania alisema watu hawawezi kurudi kwenye nchi yao kama ile amani iliyokuwa imepangwa kuwepo haipo kwa hofu ya kulipiziwa kisasi na hata kupoteza maisha yao wakirudi kwenye maeneo yao.

"Kwa hiyo sisi tunatakiwa tujikite kwenye kuhakikisha kunakuwa na uongozi bora katika nchi zetu,tuondoe siasa mbaya ambayo imekuwepo kwa kipindi kirefu kama watu kung'ang'ania madaraka na tutokomeze vita ya wenyewe kwa wenyewe,kwa kufanya hivyo tutakuwa sasa tumetatua chanzo kikubwa kinachohusu watu wengi kukimbia katika nchi husika",aliongeza Mhe. Silinde.

Alieleza kuwa,kutokana na kwamba dunia inafahamu na Afrika inajua nchi zote ambazo zina matatizo yanayohusika na wakimbizi wengi,ni vyema nchi za Umoja wa Afrika zikashirikiana kulitatua tatizo la wakimbizi kwa kuanza na wao wenyewe na wala siyo kusubiri msaada kutoka Umoja wa Mataifa.

Kwa upande wake mbunge, Mboni Mhita ambaye pia anatoka Tanzania  alisema ili kuwa na suluhisho la kudumu la wakimbizi ni vyema kutatua tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana,migogoro ya kisiasa na dini huku akiyashauri Mashirika yanayohudumia wakimbizi kusaidia kutatua vyanzo vya ukimbizi.

Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR),takwimu za mwaka 2017 zinaonesha kuwa duniani kote kuna wakimbizi milioni 23 kati yao Afrika kuna wakimbizi milioni 7 huku masuluhisho ya kudumu yakitajwa kuwa ni wakimbizi kurudi nyumbani kwa hiari,kupewa uraia/makazi ya kudumu katika nchi iliyowapokea,kusaidiwa kupewa makazi mapya ama mkimbizi mwenyewe kwenda nchi ya tatu mfano kujiunga na familia yake,ajira au masomo.

ANGALIA PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI BUNGENI
Wabunge wa bunge la Afrika wakifuatilia mjadala kuhusu kauli mbiu ya Umoja wa Afrika mwaka 2019 ambayo ni "Mwaka wa Wakimbizi,Wahamiaji waliorejeshwa kwao na wakimbizi wa ndani Barani Afrika : Mchango wa Bunge la Afrika katika kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa tatizo la uhamiaji wa kulazimishwa barani Afrika". Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog Afrika Kusini.
Mhe. David Silinde kutoka Tanzania akichangia hoja katika bunge la Afrika.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mhe. Stephen Masele akimsikiliza Mhe. David Silinde kwa umakini ukumbini.
Mhe. Mboni Mhita akichangia hoja bungeni.
Wabunge wakiwa ukumbini.
Bunge likiendelea.
Wabunge wakiwa bungeni.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Share:

Ufahamu Ugonjwa Wa Ngiri Na Tiba Yake

Tatizo la Ngiri Linavyosababisha Upungufu wa Nguvu za Kiume na Maumbile Kusinyaa.
 
Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).

Dalili za Ngiri
Tumbo kuunguruma, kiuno kuuma, kupata choo kama cha mbuzi, kushindwa kufanya tendo la ndoa, mishipa ya uume kulegea, kutokuwa na hamu ya kurudia tendo la ndoa, korondani moja kuvimba, mgongo kuuma.

Dalili zingine za ugojwa wa ngiri ni pamoja na;

Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu kama Direct Scoratal inguinal Hernia.
Uvimbe unaojitokeza tumboni na kuteremka hadi ndani ya korodani, uvimbe huu hauumi na unaweza kurudishwa kwa urahisi iwapo mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole, uvimbe huu.
Na pindi ukikubali kurudi ndani ndipo unapoitwa Reduible direct scrotal inguinal hernia.
Na pia endapo utashindikana kurudi tumboni ndipo unapoitwa Irreduible direct scrotal inguinal hernia.

Tiba ya Ngiri
Tiba yake ni kufanyiwa upasuaji , ama kutumia dawa za asili ili kupona kabisa tatizo hilo. Wasiliana Nami Kwa Ushauri zaidi wa Tatizo hili. Simu: 0714006521


Share:

Shamim Mwasha na mumewe wafikishwa mahakamani kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imewapandisha kizimbani Shamim Mwasha na mume wake, Abdul Nsembo kwa tuhuma za kusafrisha dawa za kulevya aina ya Heroin Hydrochloride zenye uzito wa gramu 232.70.

Akisoma hati ya mashtaka wakili wa Serikali, Costantine Kakula mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Kelvin Mhina, alidai  kuwa Mei Mosi mwaka huu kwa pamoja washtakiwa hao wakiwa meneo ya Mbezi Beach walisafirisha dawa za kulevya zenye uzito wa gramu 232.70 huku wakijua kufanya hivyo ni kosa la kisheria.

Kakula alidai upelelezi bado haujakamilika na aliiomba mahakama hiyo ipange tarehe nyingine.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo Hakimu Mhina alisema washtakiwa hao hawatakiwi kujibu chochote kwa kuwa kosa wanaloshtakiwa nalo ni la uhujumu uchumi hivyo mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo na hawana dhamana.

Wakili wa utetezi, Hajra Mungula aliuomba upande wa mashtaka kuharakisha upelelezi ili hatua nyingine ziweze kuendelea.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 27, 2019 itakapotajwa tena.


Share:

Kuwa Wakwanza Kupokea Habari Zetu....Download App Yetu Kwa Kubonyeza Hapa, Huhitaji tena kuwa na Computer

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa urahisi kabisa kupitia simu yako ya mkononi muda wowote hata usiku wa manane au ukiwa kazini...

Pata kurasa za mbele Magazetini, habari za kitaifa, matukio yote ya kisiasa, burudani na udaku   kupitia simu yako ya mkononi.

Huhitaji tena kuwa na Computer. Ingia Play Store, pakua App yetu  tukuhabarishe masaa 24.



Share:

Chadema yaitaka NEC kutekeleza uamuzi wa mahakama

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeitaka Serikali na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuanza kujipanga kutekeleza uamuzi wa Mahakama Kuu kuhusu wakurugenzi kusimamia uchaguzi.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema, alisema hukumu hiyo itasaidia kutengeneza uwanja sawa wa wapigakura.

“Hatutegemei CCM na serikali yake wakate rufaa kwa lengo la kutuchelewesha, tunaamini wataheshimu uamuzi wa mahakama tutengeneze uwanja sawa wa wapigakura ili kila mtu ashinde kwa usawa,” alisema Mrema.

Chama hicho kilidai kuna wakurugenzi 86 ambao ni makada wa CCM kinyume na Ibara ya 74 (14) ya Katiba ambayo inapiga marufuku mtu anayehusika na uchaguzi kuwa mwanachama wa chama cha siasa.

“Mahakama Kuu imeona na kwa ushahidi kuna makada katika halmashauri 86 ambao walikuwa wanasimamia uchaguzi kinyume na Katiba.

“Wengi waligombea mwaka 2015 wakashindwa kwenye majimbo na kata na wengine walishindwa kura za maoni. Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unasimamiwa na makatibu tawala na wengi ni makada wa CCM, tunaomba washeshimu uamuzi wa Mahakama Kuu,” alisema.

Chama hicho pia kilipendekeza iundwe tume huru ya uchaguzi na uwepo utaratibu wa kuwapata makamishna wa tume sambamba na kuwa na mfuko maalumu ili ifanye kazi kwa uhuru.

“Kenya, Malawi na nchi zingine watu huwa wanaomba hiyo kazi ya ukamishna na si kuteuliwa, na zuio la kuishtaki tume liondolewe,” alisema Mrema.

Kwa mujibu wa Mrema, pendekezo lingine ni haki ya mgombea kukata rufaa pale ambapo wasimamizi wa uchaguzi wanakataa kupokea fomu au wanaondoka ofisini.

Chadema kilipendekeza pia wananchi wapewe fursa za kupiga kura za ndio au hapana iwapo mgombea atapita bila kupingwa na kama ikitokea hatavuka asilimia 50 asitangazwe mshindi.

Wiki iliyopita Mahakama Kuu ilibatilisha vifungu vya Sheria ya Uchaguzi vinavyowapa mamlaka wakurugenzi wa halmashauri za majiji, miji, wilaya na manispaa kuwa wasimamizi wa uchaguzi kwa niaba ya NEC.


Share:

Upungufu Wa Nguvu Za Kiume Unaotokana Na Kisukari (Diabetic Nephropathy)

Ugonjwa wa kisukari (Diabetes Mellitus) huambatana na ongezeko la sukari(glucose) katika damu kwa kiwango kinachozidi kawaida. 

Homoni aina ya insulin ambayo hutolewa na kongosho ama hushindwa kufanya kazi yake vema kwa sababu ya kasoro za seli au hutolewa kwa kiasi kisicho kidhi uhitaji wa kuratibu sukari katika damu. 

Kwa hivyo sukari hubaki katika damu kwa wingi na kuleta madhara kadhaa.Wagonjwa wa kisukari pia huweza kuwa na kiwango kikubwa cha lehemu (cholesterol) katika damu. Na zaidi huweza kuwa na tatizo la mgandamizo wa damu (hypertension) au presha. Asilimia 55 ya wanaume wenye kisukari hupatwa na tatizo la nguvu za kiume.

Mambo haya matatu, Sukari, lehemu (Cholesterol) na Mgandamizo wa damu, Huweza kusababisha upungufu wa nguvu za kiume.(Erection dysfunction).

1. Sukari.
Sukari nyingi katika damu huweza kupelekea kuharibiwa kwa kuta za mishipa ya damu. Kisha kuta hizi hushindwa kuzalisha homoni aina ya Nitrogen Oxide ambayo husaidia kutanua mirija ya damu kwa ajili ya kupitisha damu kwa ufasaha. Ikitokea katika mirija ya damu inayotiririsha katika uume kushindwa kutanuka vema, ni wazi kuwa uume utapungua uimara wake.

2. Lehemu (Cholesterol).
Lehemu huganda kwenye kuta za mirija ya damu mithiri ya mafuta yanavyoganda katika chupa. Hali hii hupelekea kupungua kipenyo (diameter) cha mirija ya damu na kushindwa kupitisha damu vizuri.

3. Mgandamizo wa damu au Presha (Hypertension).
Katika hali hii moyo hushindwa kusukuma damu vizuri na hivyo kupungua kwa kasi na ujazo wa damu katika maeneo yaliopo mbali na moyo, ikiwa ni pamoja na viungo vya uzazi.

Pia, Mishipa ya fahamu (nerves) au Neva za fahamu huweza kuharibiwa na kupunguza ufanisi wake.Katika hali hii, maeneo yanayohudumiwa na neva hizo hupungua hisia na wakati mwengine kupata ganzi ya kudumu. Uume pia huweza kuathiriwa kwa namna hiyo.

 Kumbuka
Ili  mgonjwa  wa  kisukari  aweze  kupata  tiba  ya  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume, ni  lazima   apate  pia  tiba   itakayo  saidia  ku- control  sukari  kwenye  damu   yake.

Hivyo  basi ,  tiba  ya  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume  kwa  mgonjwa  wa  kisukari  inatakiwa  kwenda   sanjari  na  tiba  ya  ku - control  sukari  kwenye  damu  ya  mgonjwa.

Hii  ina  maana  kuwa,   ili  tiba  ya  nguvu  za  kiume  kwa  mgonjwa  wa  kisukari  iweze  kufanya  kazi  barabara, ni  lazima  mgonjwa  huyo, pamoja  na   kutumia  tiba  ya  nguvu  za  kiume , apate  pia  tiba  ya  sukari.


Kama unatatizo la Kisukari, lililosababisha upungukiwe nguvu za kiume basi wasiliana nami kwa ushauri zaidi. Simu:   0759208637 au 0620510598


Share:

Kutana na Sheikh Omary Mwenye Uwezo wakufanya Dua mbalimbali za Matatizo Yako Na Kutafsiri Ndoto kwa kutumia Vitabu vya QUR-AN

Sheikh Omary Ni bigwa wa kutatua matatizo kwa haraka ni mtu aliye jaliwa KUBULI SHUFAA pia anatoa DUAH   za RUHIA. Ukija na Maradhi yanaondoka hapo hapo bila kungoja kesho, Kama una Majini wa Kichawi pia yanaondoka UKIPEWA MKONO  na Sheikh Omary .
 
Wasiliana na Mtaalam Huyu Kwani yeye hufaulu Pale wote waliko Shindwa na Pia Humaliza kazi zilizo Shindikana ama Zilizo Achwa ndani ya Siku Moja 1.
 
Sheikh Omary  ANAWASHUKURU WALE WOTE WANAOPIGA SIMU ZA SHUKRANI NA KUTOA SHUHUDA WALIVYOSAIDIWA(Rudisha Mahusiano yako Ndani ya Saa 6 tu)
 
Sheikh Omary ni Mtaalamu wa Nyota za Binadamu na ANATIBU KWA KUTUMIA QUR AN. Mwenye Uwezo wa Kubaini Tatizo lako tu Pindi Utakapo Fanya Mawasiliano Kupitia Wasaa Husika.
 
Je una NUKSI  zisizo kwisha.!? JE umekimbiwa na Mume/Mke na Anaishi na Mtu Mwingine..!?
 
Hupati kazi kwa mda mrefu na vyeti unavyo
Una kosa bahati ya wanaume au mume wa kukuoa
Unataka nyota ing'ae ukiongea usikilizwe Ipo TARASIMU kwa Ajili yako...
 
Jini mahaba. Kama Unakasirika ovyo ukiwa na bwana au mwanamke wako na  kumchukia Mpaka  kushindwa kufanya nae tendo la ndoa. Kama umezulumiwa Mali irudi ikiwa haija pita Mwezi .
 
Njoo umuone Sheikh Omary  na ujuwe  yanayo kusibu ni mtu mkarimu mpenda watu,Anahudumia  MASKINI  na TAJIRI, NJOO ATAKUSAIDIA.. Sheikh Omary 0673531992 WhatsApp/Call


Share:

Kutana na shariff Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH Adam shariff Mwenye Uwezo wakufanya Dua mbalimbali Na Kutafsiri Ndoto

Kutana  na shariff Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH Adam shariff  Mwenye UWEZO wakufanya dua mbali mbali  Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na  Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?

Wasilina na Adam shariff Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO   Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? . Adam shariff Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..

Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN  . Anatafsiri Ndoto. , KUSAFISHA NYOTA. Mvuto wa Mwili na Biashara.


Mawasiliano: (+255 )715971688 au (+255  )756914036



Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger