Saturday, 11 May 2019

Angalia Picha : MWENGE WA UHURU WATUA KWA KISHINDO MANISPAA YA SHINYANGA




Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga umekimbia jumla ya kilomita 102 na umezindua miradi nane na kuweka mawe ya msingi, yenye jumla ya shilingi Bilioni 1.3 ambapo hakuna hata mradi mmoja uliokutwa na dosari na kukataliwa.


Mwenge huo umekimbizwa leo Mei 11, 2019 katika Manispaa ya Shinyanga na kuzindua, kutembelea pamoja na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi ya maendeleo mbalimbali ikiwamo ya Sekta ya afya, elimu, maji na kiuchumi.

Akizungumza wakati akipokea Mwenge huo wa uhuru mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, amewataka wananchi wa Manispaa ya Shinyanga kuitunza miradi hiyo ya maendele ili iweze kuwa na tija katika kuwatatulia changomoto zinazowakabili.

“Nawaomba wananchi wa manispaa ya Shinyanga muitunze miradi hii na kutoiharibu ili idumu kwa muda mrefu na kuwatatulia changamoto ambazo zilikuwa zikiwakabili ikiwa Serikali inatumia gharama nyingi hadi kuikamilisha,”amesema Mboneko.

Kwa upande wake kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa Mzee Mkongea Ali, amewataka watendaji wa serikali wakiwemo wahandisi kuwa wanaisimamia vizuri miradi ya maendeleo ili ipate kudumu kwa muda mrefu na kuondoa kero kwa wananchi.

Amesema huu ni wakati sasa wa watendaji wa serikali ambapo wanapaswa kufanya kazi kwa kujituma, uadilifu, pamoja na kuwa wabunifu.na siyo kusubiri hadi kuanza kusukumwa hali ambayo wataisaidia serikali kufikia kwenye uchumi wa kati.

Katika hatua nyingine amewataka wananchi wa Manispaa ya Shinyanga kujitokeza kushiriki kwenye uchuguzi wa serikali za mitaa ili kuchagua viongozi ambao watawafaa kuwaongoza na kuwatatulia kero zao.

Aidha Mwenge huo uhuru umezindua miradi mbalimbali ya maendeleo na kuweka mawe ya msingi ukiwamo ujenzi wa madarasa matano ya shule ya msingi viwandani na ofisi ya walimu, nyumba za polisi na Ofisi ya tarafa ya Ibadakuli.

Miradi mingine ni mradi wa maji Masekelo,zahanati ya Mwawaza, huku ya watu binafsi ikiwa ni ya ufugaji wa samaki uliopo kata ya Kizumbi ambao unamilikiwa na Mwananchi Garage pamoja mradi wa Petrol Station.

Kauli mbiu ya mwenge wa uhuru kitaifa mwaka huu (2019) inasema ,'Maji ni uhai tutunze vyanzo vyake ,wananchi washiriki kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa'.


TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI


Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko mkono wa kushoto akipokea Mwenge wa uhuru kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha (kulia), tayari kwa kuukimbiza kwenye Manispaa ya Shinyanga Kilomita 102 pamoja na kuzindua, kuona na kuweka mawe ya msingi Miradi Nane ya maendeleo yenye jumla ya Shilingi Bilioni 1.3. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko (kushoto) akimpokea mkimbiza Mwenge wa uhuru kitaifa Mzee Mpongea Ali tayari kwa kwenda kukagua,kuzindua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi ya maendeleo.

Viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye mapokezi ya Mwenge huo wa Uhuru.

Mwenge wa uhuru ukianza kukimbizwa tayari kwa uzinduzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo Manispaa ya Shinyanga pamoja na kuweka mawe ya msingi.

Mwenge wa uhuru ukianza na uzinduzi wa mradi wa ufugaji Samaki katika kata ya Kizumbi unaomilikiwa na Mwananchi Garage.Pichani ni Meneja mradi huo wa samaki,Hanry Kimario akisoma risala kuwa mradi huo umegharimu kiasi cha shilingi milioni 120.

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa Mzee Mpongea Ali akikagua mradi wa ufugaji samaki kabla ya kuuzindua rasmi.

Ukaguzi wa mradi wa samaki ukiendelea.

Samaki wakionekana.

Meneja mradi wa ufugaji Samaki Hanry Kimario mwenye tisheti ya bluu, akitoa maelezo namna wanavyoendesha ufugaji wa samaki hao pamoja na namna ya kuwahudumia.

Ukaguzi wa mabwawa ya samaki ukiendelea.

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa Mzee Mpongea Ali, akiweka vifaranga vya samaki kwenye mradi huo kama ishara ya kuuzindua rasmi.

Uwekaji wa vifaranga vya samaki ukiendelea.

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Mzee Mpongea Ali, akipanda mti kwenye mradi huo wa kufuga samaki.

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa Mzee Mpongea Ali, akiuzindua rasmi mradi huo wa kufuga samaki mara baada ya kulizika nao.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa Mzee Mpongea Ali, akikagua ujenzi wa madarasa matano na ofisi katika shule ya msingi viwandani Manispaa ya Shinyanga.

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa Mzee Mpongea Ali,akizungumza huku akiwa ameshika makablasha mara baada ya kumaliza kukagua ujenzi wa madarasa matano na ofisa katika shule hiyo ya viwandani manispaa ya Shinyanga na kuweka jiwe la msingi.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru kitafia Mzee Mpongea Ali, akiweka jiwe la msingi na kuzindua mradi kwenye kituo cha mafuta, kinachomilikiwa na mtu binafsi ambacho kimegharimu shilingi milioni 700.

Wananchi wakishuhudia uzinduzi wa mradi wa kituo cha mafuta.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Mzee Mpongea Ali, akiwataka wamiliki wa vituo vya kuuzia mafuta wafanye biashara zao kwa uaminifu na kuacha uchakachuaji wa mafuta hayo.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2019 Mzee Mpongea Ali, akikagua nyaraka mbalimbali kwenye ujenzi wa ofisi ya tarafa ya Ibadakuli manispaa ya Shinyanga kabla ya kuweka jiwe la msingi.

Wakimbiza Mwenge wa uhuru Kitaifa wakiwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko na wataalamu wa manispaa ya Shinyanga wakiendelea na ukaguzi wa jengo la ofisi ya tarafa ya Ibadakuli.

Mmoja wa viongozi wakimbiza Mwenge kitaifa akivunja tofali kwenye Tanki la maji taka katika ofisi ya taarafa hiyo ya Ibadakuli ili kujiridhisha kama yana kiwango.

Muonekano wa Jengo la tarafa ya ofisi ya Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga, ambalo limegharimu shilingi milioni 25.4.


Kaimu Meneja ufundi mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Shuwasa manispaa ya Shinyanga Yusuf Katopola akisoma risala ya mradi wa maji uliopo Kata ya Masekelo manispaa ya Shinyanga kabla ya kuzinduliwa na Mwenge wa uhuru.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa Mzee Mpongea Ali, akikagua mradi wa maji wa SHUWASA kabla ya kuweka jiwe la msingi na kuuzindua rasmi ambao umegharimu kiasi cha Shilingi Milioni 179.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa Mzee Mpongea Ali, akimtwisha mmoja wa wanawake ambao wamehudhulia kwenye uzinduzi huo wa mradi wa maji SHUWASA.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa Mzee Mpongea Ali, akifungua rasmi mradi huo wa maji wa SHUWASA ambao upo kata ya Masekelo, kwa lengo na kuwaondolea adha wakazi wa eneo hilo la kutumia maji machafu.

Wananchi wakishuhudia uzinduzi wa mradi huo wa maji na Mwenge wa uhuru.

Mwenyekiti wa ujenzi wa nyumba 10 za askari polisi mkoani Shinyanga Inspekat Cosmas Taligula akisoma taarifa ya ujenzi wa nyumba hizo kabla ya kukaguliwa na kuwekewa jiwe la msingi na Mwenge wa uhuru, ambazo zimegharimu kiasi cha Shilingi Milioni 225.

Wakimbiza Mwenge wa uhuru kitafia mwaka 2019 wakikagua ujenzi wa nyumba za Askari Polisi Shinyanga Mjini.

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa Mzee Mpongea Ali, akipanda mti mbele ya nyumba za askari polisi Shinyanga Mjini.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa Mzee Mpongea Ali, akiweka jiwe la msingi kwenye makazi ya nyumba za askari polisi Shinyanga Mjini.

Muonekano wa nyumba 10 za makazi ya askari polisi Shinyanga Mjini.


Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa Mzee Mpongea Ali, akiwataka vijana wa kikundi cha bodaboda, ambao wamepata mikopo ya bodaboda saba na bajaji moja wazingatie sheria za usalama barabarani pamoja na kuwa wanavaa kofia ngumu.

Bodaboda saba na Bajaji moja ambazo wamekopeshwa vijana kupitia asilimia 10 za mapato ya ndani ya halmashauri ya manispaa ya Shinyanga zilizogharimu shilingi Milioni 24.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa Mzee Mpongea Ali, akikagua risala ya utii ya manispaa ya Shinyanga.

Wanafunzi kutoka shule mbalimbali za msingi manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye Mwenge huo wa uhuru.

Baadhi ya watumishi wa manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye Mwenge wa uhuru.

Burudani zikitolewa kwenye mbio hizo za Mwenge wa uhuru manispaa ya Shinyanga.

Burudani zikitolewa kwenye Mbio hizo za Mwenge wa uhuru manispaa ya Shinyanga.

Na Marco Maduhu-Malunde 1 blog

Share:

Clinical Officers Training Centre Lindi

Clinical Officers Training Centre Lindi is a government technical college located in Lindi Town. Lindi Clinical Officers Training Centre offers Health and Allied Sciences Programmes.

For more details about the Clinical Officers Training Centre Lindi

Institute Details
Registration No REG/HAS/016
Institute Name: CLINICAL OFFICERS TRAINING CENTRE LINDI
Registration Status: Full Registered Institute Establishment Date: 01-Jan-2000
Registration Date: 10-Feb-2009 Accreditation Status: Not Accredited
Ownership: Government Region: Lindi
District: Lindi Municipal Counci Fixed Phone 023-2202295
Phone: 023-2202295 Address: P. O. BOX 278 LINDI
Email Address: cotcld@yahoo.com Web Address:
Programmes offered by Institution
SN Programme Name NTA Level(s)
1 Clinical Medicine 4 – 6

 

Technician Certificate in Clinical Medicine REQUIREMENTS:
Programme: Technician Certificate in Clinical Medicine
REQUIREMENTS: Holders of Certificate of Secondary Education Examination (CSEE) with four (4) Passes in non-religious Subjects including “D” Passes in Chemistry, Biology and Physics/Engineering Sciences; AND Possession of Basic Technician Certificate (NTA Level 4) in Clinical Medicine.

 

The post Clinical Officers Training Centre Lindi appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

MKANDARASI ASAINI MKATABA MRADI WA MAJI NYASHIMO WILAYANI BUSEGA


Serikali kupitia Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira jijini Mwanza (MWAUWASA) imesaini mkataba na mkandarasi kampuni ya BENNET Contractors, kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa maji kwa wakazi wa Kata ya Nyashimo, Wilaya Busega mkoani Simiyu.

Mkataba huo umesainiwa Mei 10, 2019 na kushuhudiwa na wananchi pamoja na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa Simiyu, Antony Mtaka aliyebainisha kwamba kukamilika kwa miradi mbalimbali ya maji wilayani Busega, kutaongeza idadi wananchi wanaofikiwa na mtandao wa maji safi na salama kutoka asilimia 39 za sasa hadi asilimia 79.

Mkurugenzi wa MWAUWASA, Mhandisi Antony Sanga amesema utekelezaji wa mradi huo wenye thamani ya shilingi bilioni 1.8 ni sehemu ya ahadi ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli aliyoitoa wakati akizungumza na wakazi wa Kata ya Nyashimo.

Naye Mkurugenzi wa kampuni ya BENNET Contractors, Sabatho Boaz ameahidi kukamilisha mradi huo kwa ubora na kwa muda wa miezi 15 kama mkataba unavyoelekeza ili kuwaondolea wananchi wa Kata ya Nyashimo adha ya upatikanaji wa maji safi na salama.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Antony Sanga (kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa kampuni ya BENNET Contractors, Sabatho Boaz (kulia) wakisaini mkataba wa utekelezaji mradi wa maji ya bomba katika Nyashimo wilayani Busega. Wanaoshuhudia ni viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa Simiyu, Antony Mtaka.
Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Antony Sanga (kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa kampuni ya BENNET Contractors, Sabatho Boaz (kulia) wakibadilishana mkataba wa utekelezaji mradi wa maji ya bomba katika Kata ya Nyashimo wilayani Busega.
Mkuu wa Mkoa Simiyu, Antony Mtaka (katikati), akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Antony Sanga (kushoto) baada ya kusaini mkataba wa mradi wa maji Nyashimo wilayani Simiyu. Kulia ni Mkurugenzi wa kampuni ya BENNET Contractors, Sabatho Boaz.
Mkuu wa Mkoa Simiyu, Antony Mtaka akizungumza kwenye zoezi hilo la kusaini mkataba wa mradi wa maji Nyashimo wilayani Busega.
Mkuu wa Wilaya Busega, Tano Mwera amesisitiza mradi huo kukamilika kwa wakati ndani ya kipindi kilichopangwa.
Makamu Mwenyekiti Bodi ya MWAUWASA, Edith Mdogo akitoa salamu zake wakati wa zoezi la kusaini mkataba huo.
Mbunge wa Jimbo la Busega, Dk Raphael Chegeni (CCM), ameishukru Serikali kupitia Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutoa fedha kutekeleza mradi wa maji Nyashimo.
Diwani wa Kata ya Nyashimo wilayani Busega, Mickness Mahela akitoa salamu zake kwenye wakati wa zoezi la kusaini mradi wa maji Nyashimo.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa Mwanza, Hellen Bogoye akitoa salamu zake kwenye zoezi hilo la kusaini mradi wa maji Nyashimo wilayani Simiyu utakaosaidia kumtua mama ndoo kichwani.
Viongozi mbalimbali akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Antony Sanga (wa pili kushoto) wakiwa kwenye zoezi hilo.
Baadhi ya wakazi wa Kata ya Nyashimo wilayani Busega wakifuatilia zoezi hilo.

Tazama Video hapa chini


Share:

Halmashauri Zijiandae Kukabiliana Na Ugonjwa wa Pumu

Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo amezitaka halmashauri kuhakikisha zinatenga bajeti kwa ajili ya visanduku vya huduma ya kwanza kwa ugonjwa wa pumu katika shule zote za msingi na sekondari.
 
Pia amesema ni lazima wakurugenzi katika halmashauri zote kuwa na visanduku huduma ya kwanza kwa ugonjwa wa pumu na mengineyo katika ofisi zao jambo ambalo litawasaidia wafanyakazi wenye matatizo hiyo kupewa huduma ya kwanza kabla ya kufika hospitalini.
 
Jafo alitoa maagizo hayo jijini hapa baada ya maandamano ya kuadhimisha Siku ya Pumu Duniani ambayo huadhimishwa Mei 7 kila mwaka.
 
Alisema tatizo la pumu ni kubwa na takwimu zinaonesha kuwa nusu ya watu wenye pumu ni watoto ambao wengi wako mashuleni na hawana uwezo wa kujisaidia.
 
“ Ukiangalia takwimu za Shirikala afya zinasema vifo vinavyotokana na pumu hapa nchini ni zaidi ya 2,000, sasa kama nusu ya hao ni watoto hii inamaanisha tunapoteza shule mbili nzima, yaani wanafunzi wa shule iliyokamili kutoka Darasa la Kwanza hadi la Saba. Hii inaonesha tatizo hili ni kubwa na kama taifa tunahaja ya kutathimini kama taifa.”
 
Kutokana na hali hiyo, Jafo aliagiza halmashauri katika bajeti ya mwaka 2020/2021, halmashauri zitenge fedha Sh laki 100,000 kwa kila shule katika eneo lake ili kununua visanduku viwili vya huduma ya kwanza kwa ugonjwa wa pumu.
 
“ Ghamara ya first aid kit moja ya huduma ya kwanza kwa ugonjwa wa pumu ni Sh 50,000 hivyo kila shule ikitengewa kits mbili haitakuwa fedha kubwa, Hivyo kwa shule zote zaidi ya 17,000 kutenga Sh bilioni 1.7 kwa hili sio fedha nyingi. Maadamu bajeti imeshipata, tutakapoanza maandalizi ya bajeti nyingine, halimashauri iliingize hili.”
 
Jafo alisema jamii kubwa ya Watanzania haina ufahamu wa tatizo la ugonjwa wa pumu, dalili na namna ya kutoa huduma ya kwanza kwa mgonjwa wa aina hii hivyo aliwataka maadhimisho hayo kupewa kipaumbele kwa Waganga wakuu wa mikoa na wilaya katika maeneo yao kuadhimisha siku hii kwa kutoa elimu katika jamii na mashuleni.
 
Pia aliaziagiza halmashauri na mipango miji kutenga maeneo kwa ajili ya mazoezi ili kukabiliana na magonjwa yasiyo ya kuambukizo, akiutaka mkoa wa Dodoma kuangalia namna ya kutenga siku moja kwa mwezi kwa walimu na wanafunzi kushiriki katika mazoezi
 
Jafo pia alisema kwa kushikiana na wizara nyingine wataangalia namna ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kuhudumia magonjwa yasiyoambukiza na kuangalia namna ya magonjwa haya kuingizwa kwenye mitaala ya elimu ili wanafunzi wapate elimu ya awali kama ilivyo kwa HIV.
 
Aidha, Jafo aliwapongeza waandhaaji wa madhimisho hayo kwa kazi ya kuwafundisha walimu 40 ambao wamepewa mafunzo ya namna ya kutoa huduma kwa wananfunzi wenye ugonjwa wa pumu na kushauri toa mafunzi kwa walimu wa walimu na kushauri wigo wa kufundisha walimu hao kuo
 
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Magonjwa ya Mfumo wa Hewa (TARD) ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Magonjwa Yasiyoambukuzia(Tancida), Dk Digina Riwa alisema takwimu za WHO zinaonesha dunia inawagonjwa zaidi ya milioni 3 huku nusu ya wagonjwa hao ni watoto.
 
Alisema kwa Tanzania tawkimu hizo zinaoneshwa kuwa vifo 2,491 vinatokana na ugonjwa wa pumu na kuwa kutokana na makadirio ya kuwa wagonjwa wa pumu wanaweza kuongezeka kwa asilimia 30, Shirikisho hilo likajikita katika kutoa elimu.
 
Akizungumzia sababu ya maadhimisho hayo jiji Dodoma, Riwa alisema ni baada ya kubaniki kuwapo kwa tatizo hilo na kutoa takwimu kuwa kwa mwaka jana pekee wilaiaya ya Mpwapwa ilikuwa na wagonjwa 1,223, Kongwa ni 1,101, Chemba ni 1,459 na Chamwino wagonjwa 1512.
 
Alisema katika kuadhimisha mwaka huu wameamua kufanya upimaji katika shule za msingi na sekondari ambao wameweza kuwapata wale ambao wanajitambua kuwa na ugonjwa, lakini idadi kubwa ya wanafunzi walikuwa wahajitambui.
 
Naye Mkuu wa Wilaya ya Bahi na ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mwanahamisi Mukunda alihidi kuwa mkoa utaedeleza mkakati wa kutambua na kubaini watoto wenye matatizo ya ugonjwa wa pumu.
 
“ Kwetu sisi mmetusaidia kubaini ukubwa wa tatizo, tumekuwa hatufanyi vizuri kwenye ufaulu kwenye mitihani ya taifa na tulikuwa tunatafuta mchawi, kumbe mmoja wa mchawi ni tatizo la pumu ambalo linachangia wanafunzi kukosa masomo.”alisema


Share:

Wawili Watiwa Mbaroni Kwa Mauaji ya Mtoto Mkoani Mbeya

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu wawili waliofahamika kwa majina ya 1. JAPHET YAHAYA NGUKU [37] na ANDREW ANGANILE MWAMBULUMA kwa tuhuma za mauaji ya mtoto wa miaka sita [06] aitwaye ROSE JAPHET Mkazi wa Kijiji cha Msewe, Wilayani Mbarali.

Ni kwamba mnamo tarehe 03.05.2019 majira ya saa 21:00 usiku huko Kijiji cha Msewe kilichopo Kata ya Igurusi, Tarafa ya Ilongo, Wilaya ya Mbarali, Mkoa wa Mbeya katika msitu wa hifadhi wa Chimala Mtoto aitwaye ROSE JAPHET [06] alikutwa ameuawa kwa kunyongwa shingo na kukatwa kanyagio la mguu wa kulia ambapo kanyagio la marehemu limekutwa limefukiwa huko Mbalizi, Wilaya ya Mbeya Vijijini.

Chanzo cha tukio hili ni tamaa ya kupata utajiri ambapo baba mzazi wa marehemu aitwaye JAPHET YAHAYA NGUKU alimtoa mwanae kwa ANDREW ANGANILE MWAMBULUMA ambaye ni mfanyabiashara kwa malipo ya Tshs 5,000,000/= ili auwawe na kisha kukatwa kanyagio la mguu wa kulia na kupatiwa mfanyabiashara huyo ili apeleke kwa mganga ili amtengenezee ndagu (dawa ya utajiri) ili afanikiwe katika biashara zake za Shule anayoimiliki iitwayo HAPPY iliyopo Mbalizi.

Mfanyabiashara huyo ANDREW ANGANILE MWAMBULUMA amekiri kuhusika na tukio hilo. Ufuatiliaji unaendelea ikiwa ni pamoja na msako mkali wa kumtafuta mganga huyo kwa hatua zaidi za kisheria.

Imetolewa na:
[ULRICH O. MATEI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA


Share:

Serikali Yasisitiza Kuhusu Katazo La Matumizi Ya Mifuko Ya Plastiki Kuanzia Juni 1/2019

 Ndugu Wanahabari:
Mtakumbuka kuwa 9 Aprili 2019 Serikali ilitoa Tamko la kusitisha matumizi ya Mifuko ya plastiki hapa nchini ifikapo Juni Mosi 2019. Katazo hili linalenga kuepusha athari za kiafya na mazingira zinazoendelea kujitokeza kutokana na matumizi ya mifuko hiyo. 

Katazo hilo lililotolewa na Waziri Mkuu Mhe. Kasssim Majaliwa linahusu kupiga marufuku uzalishaji, uingizaji, usafirishaji nje ya nchi, usambazaji, uuzaji na matumizi ya mifuko ya plastiki ya aina zote.  

Ndugu Wanahabari:
Ofisi ya Makamu wa Rais imekuwa ikitoa taarifa mbalimbali ili kuwaelimisha wananchi kuhusu katazo hilo kupitia Vyombo vya Habari ikiwa ni pamoja na magazeti, Runinga na Redio, Mitandao ya Kijamii, Mikutano ya wadau na kupitia mikusanyiko ya watu ikiwa ni pamoja na taarifa kusomwa katika nyumba za ibaada. 

Mpaka sasa Serikali imetekeleza yafuatayo:
1.    Ofisi ya Makamu wa Rais imeandaa Kanuni kuhusu Katazo hili. Kanuni hizi zitaanza kutumika tarehe 1 Juni 2019. Kwa mujibu wa Kanuni hizi, itakuwa ni marufuku kuzalisha, kuingiza nchini, kusambaza na kutumia mifuko ya plastiki iliyotajwa katika Katazo hili. Kiwanda, Kikundi cha Watu au Mtu Binafsi atakayebainika kukiuka matakwa ya Kanuni hizi atakuwa ametenda kosa la jinai na hivyo sheria itachukua mkondo wake.
2.    Tumetoa maelekezo Mahsusi kwa Sekretariet za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhusu utekelezaji wa katazo hii ambapo baadhi yao wameanza kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya uhifadhi wa shehena ya mifuko itakayosalimishwa
3.    Kwa kushirikiana na Makampuni ya Simu ya Vodacom, Tigo, Airtel na Halotel tumefanikiwa kutuma ujumbe mfupi kwa njia ya simu kwa watumiaji wa mitandao hiyo ambapo watumiaji milioni 11 wa Tigo, Milioni 15.5 wa Vodacom wameshapata ujumbe huu, hii itakuwa endelevu kila wiki
4.    Tumeandaa na kusambaza taarifa kwenye taasisi za dini ili nao watusaidie kufikisha ujumbe huu kwa waumini wao, tunawashukuru sana wameitikia wito vizuri.
5.    Tumekutana na wazalishaji wa mifuko mbadala wa plastiki na wamepanga kuongeza kasi zaidi uzalishaji wa bidhaa hii na baadhi wameshaagiza mitambo ya kuzalisha mifuko mbadala.
6.    Tunaendelea kutoa matangazo kwa kutumia vipaza sauti katika ngazi ya Kata, Mitaa na Vijiji kila wiki
7.    Tumeendelea kutoa elimu kupitia Vyombo vya Habari ikiwa ni pamoja na kufanya Media Tour, kutoa ‘Count down’ kwenye magazeti, kutumia redio za kijamii na redio za mikoani kutoa matangazo juu ya katazo hili. Pia tumetumia mitandao ya kijamii (Tovuti, blogs, facebook, twitter na istagram) bila kusahau katuni ili kuhakikisha ujumbe unafika kote.
8.    Tumetengeneza Bronchure, fliers, Banners na stickers na tunahakikisha tunawasambazia watu wote ili wapate uelewa ikiwa ni pamoja na wasafiri katika Vyombo vya usafiri
9.    Tunaendelea na utoaji wa Makala maalumu katika magazeti na kutumia redio kurusha matangazo yetu. 

Ndugu Wanahabari:
Jitihada zote hizi zinapaswa kuungwa mkono na si kubezwa, pia nitoe rai kwa watanzania wote kutopotosha jambo hili kama ilivyofanywa juzi katika kipande cha video (Clip) iliyosambazwa katika mitandao ya kijamii. Na kipande hiko ni cha mwaka jana 2018 wakati wa kikao kilichoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kuzungumza na Wadau wa mifuko. 

Ikumbukwe kuwa ifikapo tarehe 1 Juni 2019, Serikali itaendesha operesheni kabambe nchi nzima ya kusaka mifuko hii. Operesheni hii itahusisha Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa na Wilaya, Mamlaka za Serikali za Mitaa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Shirika la Viwango la Taifa (TBS), Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, pamoja na Mamlaka za Viwanja vya Ndege, Bandari, Forodha, Uhamiaji, na Usafiri wa Nchi Kavu. 

 Kwa wale ambao watakuwa tayari kusalimisha kwa hiari shehena ya mifuko watakayokuwa nayo, utaratibu utatolewa wa mahali rasmi wanapotakiwa kuisalimisha kwenye maeneo yao.  

Kwa taarifa zaidi kuhusu utekelezaji wa katazo hili Wananchi  kwa ujumla mnashauriwa kutembelea Ofisi za Kanda za Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) zilizopo Dar es Salaam, Mtwara, Dodoma, Mbeya, Mwanza, Kigoma na Arusha. Aidha, wanaweza pia kuwasiliana na Wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa Miji na Wilaya. 

Nirudie tena kutoa rai kwa Watanzania wote kuzingatia maelekezo haya ya Serikali pamoja na matakwa ya Kanuni za kupiga marufuku matumizi na biashara ya mifuko ya plastiki nchini kwa mustakabali wa uhifadhi wa mazingira ya nchi yetu. 

Asanteni kwa kunisikiliza,
  Imetolewa na:
Balozi Joseph E. Sokoine
NAIBU KATIBU MKUU, OFISI YA MAKAMU WA RAIS
11 MEI, 2019

 


Share:

Breaking news : WATU WENYE SILAHA WASHAMBULIA HOTELI YA KIFAHARI

Wanaume wapatao watatu wenye silaha wamevaimia hoteli ya kifahari huko Gwadar katika jimbo la Balochistan, nchini Pakistan utawala wa nchi hiyo umeeleza.

Vikosi vya usalama vimelizunguka eneo la hoteli hiyo ya ' Pearl Continental'katika mji wa Gwadar baada ya shambulio lililofanywa na watu watatu wenye silaha. Gazeti la Dawm limeripoti.

Milio ya risasi ikiwa inaendelea kusikika kutokea ndani ya hoteli. Ripoti kamili inayoeleza idadi ya wageni waliokolewa bado haijatoka.

Mji huo ambao ni kituo cha mabilionea wa uwekezaji wa miradi kutoka China.

Aidha hoteli hiyo inatajwa kuwa na wageni wengi kutoka nje ya nchi ambao ni watalii na wafanyabiashara, lakini bado haijajulikana ni wangapi walikuwa katika hoteli hiyo.

Mashambulio ya aina hiyo ni mengi katika jimbo la Balochistan, eneo ambalo ni la watu maskini zaidi katika nchi hiyo ya Pakistani.

Habari zaidi zitafuata baada ya muda mfupi
Chanzo - BBC
Share:

Picha : WANAHARAKATI WA HAKI ZA BINADAMU WAKUTANA NA BUNGE LA AFRIKA KUJADILI ELIMU KWA WATOTO WA KIKE



Wanaharakati wa haki za binadamu na viongozi wa asasi za kiraia kutoka nchi mbalimbali barani Afrika wamekutana na viongozi wa Bunge la Afrika kwa ajili ya kujadili masuala ya haki za binadamu hususani haki ya mtoto wa kike kupata elimu.

Kikao hicho kilichofunguliwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mheshimiwa Stephen Masele kimefanyika leo Jumamosi Mei 11,2019 katika ukumbi wa kawaida wa Bunge la Afrika jijini Johannesburg,Afrika Kusini ambapo pia wanafunzi kutoka vyuo vikuu mbalimbali nchini Afrika Kusini wameshiriki. 

Wajumbe wa kikao hicho wamejadili kwa kina kuhusu upatikanaji wa elimu kwa watoto  hususani haki ya elimu kwa watoto wa kike wanaopata ujauzito wakiwa shuleni na walio nje ya shule (Out of school girls in education systems)

Angalia picha za matukio hapa chini
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mheshimiwa Stephen Masele akifungua kikao cha Bunge la Afrika na viongozi wa asasi za kiraia,wanaharakati,wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Afrika Kusini leo. Mhe. Masele alisema ni vyema nchi za Afrika zikawa na sheria na sera zinazompa mtoto wa kike haki ya kupata elimu. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mheshimiwa Stephen Masele akizungumza wakati wa kikao hicho.

Katibu wa Bunge la Afrika,Yusupha Jobe akizungumzia kuhusu nafasi ya asasi za kiraia kushirikiana na Bunge la Afrika katika kupigania haki za binadamu.
Katibu wa Bunge la Afrika,Yusupha Jobe (kulia) akizungumza.
Washiriki wa kikao hicho wakiwa ukumbini.
Wa kwanza kushoto mbele ni Afisa Uraghibishaji kutoka shirika la Under The Same Sun (UTSS) nchini Tanzania linalojihusisha na masuala ya watu wenye Ualbino Perpetua Senkoro akifuatiwa na Mkurugenzi wa Shirika la Haki za Binadamu na Biashara nchini Tanzania (wa tatu kutoka kushoto),Flaviana Charles wakiwa kwenye kikao hicho.
Kikao kinaendelea.

Kikao kikiendelea.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Share:

Waziri Mkuu Achangia Mifuko 300 Ya Saruji

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amechangia mifuko 300 ya saruji na fedha sh. milioni moja kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa la Waadventista wa Sabato (SDA) la Magomeni, Mwembechai, jijini Dar es Salaam.

Ametoa mchango huo leo (Jumamosi, Mei 11, 2019) kwenye sherehe za kutimiza miaka 100 ya Idara ya Huduma za Familia ya Kanisa la Sabato Ulimwenguni zilizofanyika kwenye kanisa hilo jijini Dar es Salaam. 

Akizungumza na waumini wa makanisa mbalimbali ya kanisa la SDA waliohudhuria sherehe hizo, Waziri Mkuu amesema Serikali inatambua mchango unaotolewa na taasisi za dini na akalishukuru kanisa la SDA kwa kuamua kutoa huduma za elimu, afya na maji bila ubaguzi wowote wa dini.

“Mbali na kutoa huduma za kijamii, kanisa hili pia linamiliki vyombo vya habari vya Morning Star Radio FM, Adventist World Radio (AWR) na Hope Channel Tanzania TV ambavyo hutoa elimu kwa watu mbalimbali. Kupitia elimu mnayotoa, mmesaidia watu wote kwa maisha ya sasa na ya baadaye,” amesema.

Ametoa wito kwa maaskofu na wachungaji waendelee kuhimiza waumini wao wafanye kazi kwa bidii ili kuendana na maono ya kanisa hilo yanayotaka watu wafanya kazi, watoe sadak a na zaka na kisha walipe kodi.

“Maaskofu na wachongaji mundelee kuhamasisha utendaji kazi kwa Watanzania wote. Pia muwahamasishe vijana wajiunge kwenye vikundi na kubuni miradi ya kujiletea maendeleo kwani Serikali haiwezi kutoa ajira kwa wahitimu wote,” amesema.

“Wahimizeni pia vijana wajifunze stadi za kazi ili waweze kupata ujuzi. Na Serikali hii tunahimiza ujenzi wa viwanda, kwa hiyo tunahitaji vijana wenye ujuzi ili kuendana na kauli ya Serikali isemayo Tanzania ya Viwanda ifikapo mwaka 2025.”

Amewapongeza viongozi wa kanisa kwa kuamua kutafsiri kitabu cha Tumaini kwa Familia za Leo ambacho kinalenga kuhuisha mahusiano katika familia. “Nimesikia mahubiri yakihimiza mahusiano baina ya wanandoa na baina ya wazazi na watoto. Nakubaliana na mafundisho ya Baba Askofu kwamba Taifa imara siku zote, msingi wake ni familia imara. Ni vema kila Mtanzania akasoma kitabu hiki. Kila mmoja apate nakala ikiwemo Waislamu na Wakristo wa madhehebu mengine.”

Mapema, akitoa mahubiri kwenye sherehe hizo, Askofu SDA Jimbo la Kusini, Mch. Mark Malekana alisema Mungu aliandaa ndoa ili iwe mahali pa furaha, amani, upendo na maelewano lakini kwa sasa shetani ameamua kuharibu mpango wa Mungu kwa kuweka migogoro baina ya wanandoa.

Alisema kanisa la SDA liliamua kuwa na idara ya familia lengo kuu likiwa ni kuzirudisha ndoa kwenye kusudi la Mungu. Mwenza wako ameumbwa awe ni wa kufaana nawe, siyo kufanana na wewe. Kama unadhani mke wako kufikiri tofauti na wewe ni tatizo, kuabnzia leo futa hiyo dhana. Mmeumbwa tofauti ili mmsaidiane kusinga mbele,” alisema.

“Matokeo ya migogoro ya kwenye ndoa ni kuongezeka kwa watoto wa mitaani; tembea kokote kule hapa nchini au nje ya nchi utabaini kuwa hii ni tatizo kubwa. Wanandoa tutimize wajibu wetu kwa malezi ya familia ili ndoa zetu zirudi Eden,” alisisitiza.

Akisoma risala mbele ya Waziri Mkuu, Katibu Mkuu wa Jimbo la Kusini, Mch, Dkt. Rabson Nkoko alisema kanisa hilo linatoa huduma za elimu, uchapishaji, afya, vyombo vya habari, maafa na kwenye maendeleo.

“Kanisa linamiliki taasisi ya Adventist Development and Relief Agency (ADRA) ambayo mwaka 2018 ilitoa misaada yenye thamani ya dola za Marekani 89,031 (sawa na sh. milioni 204.77) kwa watu 18, 332 katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu; watu waliopatwa na mafuriko Meru na Arusha; na watu wenye ulemavu wa ngozi nchini na maeneo mengine,” alisema Mch. Nkoko.

(mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,


Share:

Wimbo Mpya: Bill Nass X Whozu - Naleft

Wimbo Mpya: Bill Nass X Whozu - Naleft


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger