Saturday, 11 May 2019

Picha : AGAPE YAENDESHA BONANZA LA MICHEZO KUTOA ELIMU YA AFYA YA UZAZI NA UJINSIA KIJIJINI

Shirika lisilo la kiserikali AGAPE AIDS CONTROL PROGRAM la Mkoani Shinyanga linalojishughulisha na masuala ya jamii, limetoa elimu ya afya ya uzazi na ujinsia kwa njia ya bonanza la michezo kwenye vitongoji vya Buchamike,Shabuluba, Mwagala na Uswahilini vilivyopo pembezoni mwa kata ya Usanda Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.


Bonanza hilo limeendeshwa Ijumaa Mei 10, 2019 kwenye viwanja vya michezo vya kitongoji cha Buchambi kata ya Usanda ambapo kumefanyika michezo mbalimbali ikiwemo kukimbiza kuku, mbio za baiskeli pamoja na mpira wa miguu na washindi wamezawadiwa zawadi mbalimbali ikiwamo kupewa kuku pamoja na mbuzi.

Akizungumza kwenye bonanza hilo Mratibu wa mradi  wa afya ya uzazi na ujinsia kutoka Shirika hilo la Agape Lucy Maganga, amesema wameamua kutoa elimu hiyo kwa njia ya michezo ili kufikisha elimu kwa wananchi, kuachana na masuala kupenda kuozesha wanafunzi ndoa za utotoni, pamoja na kuwapatia ujauzito na hatimaye kuacha masomo yao.

Alisema Shirika hilo limekuwa likiendesha mradi huo wa afya ya uzazi na ujinsia kwenye kata hiyo tangu mwaka 2017, kwa ufadhili wa shirika la Sida la nchini Sweden ambao unatarajiwa kuisha mwezi Juni 2019, lakini walikuwa hawafikii wananchi walio pembezoni kutokana na changamoto ya miundo mbinu ya barabara, lakini kwa sasa wameamua kufika hadi maeneo hayo ili elimu hiyo iweze kusambaa maeneo yote.

“Tumeendesha bonanza hili la michezo kwenye vitongoji ambavyo vipo pembezoni mwaka kata ya Usanda ili kutoa elimu ya afya ya uzazi na ujinsia kwa rika zote, ambayo itabadilisha mitazamo ya wananchi na kuachana na masuala ya kutongoza wanafunzi pamoja na kuwaozesha ndoa za utotoni ili waweze kutimiza malengo yao,”amesema Maganga.

“Pia tumewataka wananchi kuachana na masuala ya kufanya ngono zembe, ambayo yataweza kuwasababishia kupata magonjwa mbalimbali, na hatimaye kubakia kujiuguza na kushindwa kufanya shughuli za kimaendeleo na kushindwa kuinuka kiuchumi,”ameongeza.

Naye Kaimu mtendaji wa kata hiyo ya usanda Ester Pembelada,ametoa shukrani kwa shirika hilo la AGAPE kwa kutoa elimu hiyo ya afya ya uzazi na ujinsia, ambayo imekuwa na msaada mkubwa katika kupunguza tatizo la mimba na ndoa za utotoni tofauti na hapo awali.

Amesema amefarijika  shirika hilo kufika kutoa elimu hiyo ya afya ya uzazi na ujinsia hadi kwa wananchi ambao wapo pembezoni,kwani wengi wao elimu kama hizo huwa wanazikosa mahali ambapo ndipo kwenye matatizo makubwa ya wanafunzi wengi kukatishwa ndoto zao.

Baadhi ya wananchi waliohudhuria bonanza hilo akiwemo Edward Ngassa na Lidya Jeremia, wameipongeza AGAPE kwa elimu hiyo ya afya ya uzazi na ujinsia na kubainisha kuwa itawasaidia kutambua umuhimu wa kusomesha watoto hasa wa kike pamoja na kulinda afya zao kwa kutopatwa na magonjwa.

TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI


Mratibu wa mradi wa elimu ya afya ya uzazi na ujinsia kutoka Shirika la Agape Lucy Maganga akisalimia na wananchi wa vitongoji viliyopo pembezoni mwa kata ya Usanda kabla ya kutoa elimu hiyo ya afya ya uzazi na ujinsia kwa rika zote. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog

Mratibu wa mradi wa elimu ya afya ya uzazi na ujinsia Lucy Maganga akitoa elimu ya afya ya uzazi na ujinsia kwa wananchi wa vitongoji vya kata ya usanda ambavyo ni Buchamike,Shabuluba, Mwagala, pamoja na Uswahilini, ili kuachana na masuala ya kutongoza wanafunzi na kuwaozesha ndoa za utotoni pamoja na kuacha ngono zembe ili kutopatwa na magonjwa.

Kaimu mtendaji wa kata ya usanda Ester Pembelada, akionya wanaume kuendekeza masuala ya michepuko, pamoja na kupenda kuozesha wanafunzi kwa tamaa ya kutaka kupata mifugo.

Wananchi wakisikiliza elimu ya afya ya uzazi na ujinsia kutoka Shirika la Agape.

Wananchi wakiendelea kusikiliza elimu ya afya ya uzazi na ujinsia kutoka shirika la Agape na kutakiwa kuacha tabia ya kuozesha wanafunzi ndoa za utotoni na kuwapatia ujauzito na kuzima ndoto zao.

Wananchi wakiendelea kusikiliza elimu ya afya ya uzazi na ujinsia kutoka Shirika la Agape kwa ufadhili wa shirika la Sida la nchini Sweden.

Wananchi wakiendelea kusikiliza elimu ya afya ya uzazi na ujinsia kutoka Shirika la Agape kwa ufadhili wa shirika la Sida la nchini Sweden.

Awali mashindano ya baiskeli yakianza kabla ya kutolewa elimu ya afya ya uzazi na ujinsia kutoka Shirika la Agape, ambapo aliyeibuka mshindi ni Jumanne Dotto.

Mashindano ya baiskeli yakiendelea kwa wanaume ambapo mshindi wa kwanza amepewa zawadi ya mbuzi.

Mashindano ya baiskeli yakiendelea kwa wanawake ambapo mshindi aliyepatikana ni Lyidia Jeremia na alipewa zawadi ya mbuzi.

Mashindano ya kufukuza kuku yakiendelea ambapo Milembe Mabula aliibuka mshindi na kuondoka na kuku wake.

Timu ya kitongoji cha Shabuluba wakiwa kwenye picha ya pamoja kabla ya kuanza mchezo wao wa fainali kwenye bonanza la elimu ya afya ya uzazi na ujinsia kutoka Shirika la Agape.

Timu ya kitongoji cha Buchamike wakiwa kwenye picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo wao wa fainali na timu ya Shabuluba kwenye Bonanza hilo ambapo waliibuka washindi kwa kupiga mikwaju ya Penati na kupata magoli manne kwa mawili.

Mchezo wa mpira wa miguu ukichezwa kwenye bonanza hilo kwa fainali ya timu ya kitongoji cha Buchamike wenye jezi nyeupe pamoja na Shabuluba wenye jezi ya kijana ambapo hadi dakika 90 zinamalizika walitoka sare ya kufungana bao moja kwa moja.

Wananchi wakiendelea kutazama soka.

Mchezaji wa timu ya Buchamike akiwa ameumia kwenye bonanza hilo.

Wananchi wakiendelea kuangalia soka.

Mchezaji wa timu ya Shabuluba akipiga penati na kupata goli.

Wananchi wakiendelea kuangalia upigaji wa penati mara baada ya timu hizo za Shabuluba na Buchamike kutoka sare ya kufungana bao moja kwa moja.

Wananchi wakishuhudia upigaji Penati ili kupata ushindi.


Mchezaji wa timu ya Buchamike akifunga penati na kupata goli la, ambapo waliibuka na ushindi wa kupata Penati 4-2.

Wananchi wa kijiji cha Buchamike wakisheherekea ushindi.

Burudani zikiendelea kutawala kwenye bonanza hilo.

Mgeni rasmi kwenye bonanza hilo,Kaimu mtendaji wa Kata ya usanda Ester Pembelada mkono wa kulia akitoa zawadi ya kuku kwa mshindi Milembe Mabula. Kushoto ni mratibu wa mradi wa elimu ya afya ya uzazi na ujinsia kutoka Shirika la Agape Lucy Maganga.

Kaimu mtendaji wa Kata ya Usanda Ester Pembelada (kulia) akitoa zawadi ya kuku kwa mshindi wa pili wa mbio za baiskeli kwa wanawake Juke Mashema, ambapo mkono wa kushoto ni mratibu wa mradi wa elimu ya afya ya uzazi na ujinsia kutoka Shirika la Agape Lucy Maganga.

Kaimu mtendaji wa kata ya Usanda Ester Pembelada akitoa zawadi ya Mbuzi kwa mshindi wa kwanza wa mbio za baiskeli Lyidia Jeremia.Kushoto ni mratibu wa mradi wa elimu ya afya ya uzazi na ujinsia kutoka Shirika la Agape Lucy Maganga.

Kaimu mtendaji wa Kata ya usanda Ester Pembelada mkono wa kulia akitoa zawadi ya mbuzi kwa mshindi wa kwanza wa mbio za baiskeli Jumanne Dotto.Kushoto ni mratibu wa mradi wa elimu ya afya ya uzazi na ujinsia kutoka Shirika la Agape Lucy Maganga.

Kaimu mtendaji wa Kata ya usanda Ester Pembelada akikabidhi zawadi ya mbuzi kwa washindi wa pili wa timu ya mpira wa miguu ya Shabuluba.

Kaimu mtendaji wa kata ya Usanda Ester Pembelada akikabidhi  zawadi ya Mbuzi wawili kwa mshindi wa kwanza wa mpira wa miguu kutoka imu ya Buchamike, .Kushoto ni mratibu wa mradi wa elimu ya afya ya uzazi na ujinsia kutoka Shirika la Agape Lucy Maganga.

Na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

Share:

Friday, 10 May 2019

Taarifa Kwa Umma Kuhusu Taarifa Inayosambaa Mitandaoni Kuhusu mifuko ya Plastiki




Share:

MAHAKAMA YAFUTA WAKURUGENZI KUSIMAMIA UCHAGUZI TANZANIA


Na James Magai, Mwananchi 

Dar es Salaam. Mahakama Kuu Tanzania imebatilisha vifungu vya Sheria ya Uchaguzi vinavyowapa mamlaka wakurugenzi wa halmashauri za majiji, miji, wilaya na manispaa kuwa wasimamizi wa uchaguzi kwa niaba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Uamuzi huo umetolewa leo Ijumaa Mei 10, 2019 na jopo la majaji watatu wa Mahakam a Kuu, ambao waliongozwa na Jaji Atuganile Ngala. Wengine ni Dk Benhajj Masoud na Firmin Matogolo.

Kesi hiyo namba 6 ya mwaka 2018, ilifunguliwa na watetezi na wanaharakati wa haki za binadamu na demokrasia kwa kushirikiana na vyama vya siasa, vilivyowakiwakilishwa na mwanachama wa Chadema, Bob Wangwe dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Kwa mujibu wa hati ya madai ya kesi hiyo, Wangwe ambaye alikuwa mdai pekee alikuwa anapinga wakurugenzi wa halmashauri za wilaya, manispaa na au majii kuwa wasimamizi wa uchaguzi.

Pamoja na mambo mengine alikuwa akidai kuwa wakurugenzi hao ni wateule wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye kwa sasa ndiye mwenyekiti wa CCM, ambacho pia huwa kinashiriki katika uchaguzi.

Pia alikuwa anadai kuwa sheria hiyo ni kinyume cha Ibara ya 74 (14 ) ya Katiba ambayo inapiga marufuku mtu yeyote anayehusika na uchaguzi kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa na kwamba ana haki ya kupiga kura tu.

Katika uamuzi wake leo, mahakama hiyo imekubaliana na hoja za mdai dhidi ya hoja za Serikali iliyokuwa ikitetea wakurugenzi hao kuendelea kuwa wasimamizi wa uchaguzi kwa madai kuwa suala hilo haliathiri uchaguzi kwa kuwa uteuzi wao ni kwa mujibu wa sheria.

Akisoma uamuzi huo, Jaji Ngala alisema vifungu 7(1) na 7(3) vya Sheria ya Uchaguzi ni vinakiuka Katiba kwa kuwa vinakwenda kinyume na matakwa ya kikatiba ya uhuru wa Tume ya Uchaguzi.

Kifungu cha 7(1) ndicho kinachowapa mamlaka wakurugenzi kuwa wasimamizi wa uchaguzi kwa niaba ya NEC.

Hata hivyo, akisoma uamuzi huo Jaji Ngala amesema vifungu hivyo vinakinzana na Katiba ya Nchi kwa kuwa wakurugenzi ni wateule wa Rais na hawako chini ya tume na kwamba Katiba inaelekeza Tume yan Uchaguzi iwe huru.

Jaji Ngwala amesisitiza kuwa sheria hiyo haihakikishi kuwa wakurugenzi hao watakuwa huru katika utekelezaji wa majukumu yao.

Amesema wameridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mdai kuwa wakurugenzi wengi ni wanachama wa CCM kwa kuwa kuna wakurugenzi 74 ambao orodha yao imewasilishwa mahakamani ambao ni wanachama wa chama hicho tawala.

Kifungu 7(3) kinaeleza kwamba NEC inaweza kumteua mtu yeyote kuwa msimamizi wa uchaguzi.

Mahakama hiyo imesema kuwa hata kifungu hicho hakiweki ulinzi kuhakikisha kuwa watu hao wanakuwa huru na kwamba lazima kuwe na ulinzi kwa kuhakikisha kuwa anayeteuliwa si mwanachama wa chama chochote cha siasa.

“Kwa hiyo tunatamka kwamba vifungu hivi ni kinyume cha Katiba ya nchi inayotaka kuwe na uhuru wa tume katika utekelezaji wa majukumu yake,” amesema Jaji Ngwala.

Akuzungumza baada ya uamuzi huo, Fatme Karume, ambaye alikuwa wakili wa Wangwe, amesema kwa uamuzi huo sasa hakuna wasimamizi wa uchaguzi na kwamba itabidi NEC itumie kifungu cha 7(2) cha sheria hiyo kuteua wasimamizi huru.

Karume ameleezea kufurahishwa na uamuzi wa mahakama kwa kutotoa amri kwa Serikali ya kufanya marekebisho ya sheria hiyo wala kuipa muda, akisema kwa uamuzi huo kuanzia sasa kifungu hivyo ni batili.

Amesema kwamba maana yake imevifuta moja kwa moja badala ya kuipa serika nafasi .

“Kwa hiyo nimefurahi sana, sana kwa uamuzi huu kwa sababu hatukuwa na tume huru kwa kuwa wale waliokuwa na jukumu la kuhesabu na kuhakikisha kuwa kura ziko salama hawakuwa huru,” amesema Wakili Karume.

“Kwa sababu hawako chini ya Tume bali wako chini ya Rais na chama tawala.”

Kwa upande wake, Wangwe amesema amefurahishwa na ushindi huo na kwamba si wake wala Karume pekee, bali ni wa watu wote wapenda demokrasia na hata wale wasiopenda harakati hizo.

“Hili ni fundisho kwamba katika kupigania utawala bora katika nchi, katika kupigania demokrasia katika nchi hii, ni suala la kila Mtanzania, kila mtu anangalie wapi kuna mapungufu, sheria gani ambazo ni mbovu, mahakama hizi ziko kwa ajili yetu,” amesema Wangwe.
Share:

UGOMVI WA WANANDOA WAUNGUZA NYUMBA 300 KIBERA

Haijulikani chanzo cha ugomvi wenyewe, lakini matokeo ya ugomvi huo yamezua hasara kubwa.

Kwa mujibu wa tovuti ya gazeti la Star la nchini Kenya, ugomvi wa wanandoa hao uliotokea Jumanne usiku ulianzia kwa maneno na kisha kuvaana mwilini, katika purukushani hizo, jiko lao la gesi likadondoka na kulipuka.

Moto ukatanda ndani ya nyumba yao, na baada ya muda mfupi ukazikumba nyumba nyingine pia.

Eneo ulipozuka moto huo ni kitongoji maarufu cha Kibera jijini Nairobi ambacho wakaazi wake ni masikini sana.

Makaazi katika eneo hilo hayajapangiliwa na nyumba zimekaribiana sana, hivyo linapotokea janga la moto, ni kawaida kwa zaidi ya nyumba moja kuathirika.

Hata hivyo, si jambo la kawaida kwa moto kuunguza nyumba mpaka 300, na kuacha maelfu ya wakaazi bila makao.Kitongoji cha Kibera ni moja ya maeneo wanayokaa watu masikini Nairobi na makazi yake hayajapangiliwa.

Mamlaka zimeamua kuficha utambulisho wa wanandoa hao kwa makusudi ili kuwalinda dhidi ya ghadabu ya wakaazi wengine ambao wamethirika pakubwa.

Eneo liliotokea moto huo linaitwa laini saba na tayari mwakilishi wake kwenye bunge la Kaunti ya Nairobi Cecilia Ayot amesema mvua zimefanya hali izidi kuwa mbaya.

"Watu wameachwa bila makazi. Bahati mbaya zaidi ni kuwa kwa mvua zinazoendelea, hata ile sehemu ambayo walikuwa wanajihifadhi haipo tena," amesema Ayot.

Mwakilishi huyo pia amekemea vikali ukatili wa majumbani na ugomvi: "Kuna namna nyingi za kutatua matatizo, na ugomvi si jia muafaka ya kufanya hivyo. Watu (wanaogombana) inawapasa waombe ushauri na usuluhishi badala ya kupigana, tumeona madhara ya ugomvi na jinsi ulivyoathiri maisha ya maelfu ya watu kwa kuteketeza nyumba 300.

Kikosi cha zimamoto cha jiji la Nairobi kimejitetea kuwa ujenzi wa kiholela katika eneo hilo uliwazuia kulifikia eneo hilo na kuuzima moto kwa haraka.
Chanzo - BBC
Share:

ATUPWA JELA KWA KUSAFIRISHA BUIBUI NA MENDE


Quito, Ecuador, AFP. Raia wa Japan amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela nchini Ecuador baada ya kupatikana na hatia ya kujaribu kusafirisha nje rundo la wadudu wa aina tofauti, kama buibui na mende, maofisa wa serikali wamesema.

Mtu huyo alikamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Quito mwezi Machi akiwa na wadudu 248, ambao ni mende, dondora, nyuki na vipepeo aliowaweka kwenye sanduku, msemaji wa wizara ya mazingira alisema.

Mtu huyo ambaye alijulikana kwa jina moja la Hirokazu S, pia ametozwa faini ya dola 4,000 na kuamriwa aombe radhi hadharani kwa kutumia gazeti la kitaifa, ilisema wizara hiyo.

Ecuador, nchi ndogo ya Amerika Kusini yenye watu milioni 17, ni moja ya nchi zenye aina nyingi za viumbe.

mamlaka zimepiga marufuku kukamata na kuuza wanyama mwitu, lakini biashara haramu inaendelea katika maeneo yote nchini humo.

Mjapani huyo alikuwa analenga kuwapeleka wadudu hao Hokkaido, kaskazini mwa Japan.

Share:

KAGERA SUGAR YAENDELEZA UBABE KWA SIMBA, YANGA SC NAO WAGONGWA 1 - 0 MUSOMA

TIMU ya Kager Sugar ya Bukoba imeendeleza ubabe wake wa kihistoria kwa Simba SC baada ya kuichapa 1-0 jioni ya leo Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.

Nahodha Msaidizi na beki wa kushoto wa Simba SC, Mohamed Hussein 'Tshabalala ' alijifunga dakika ya 41 akiwa katika harakati za kuokoa mpira uliopigwa na Paul Ngalyoma kutoka upande wa kulia kuipatia timu yake ya zamani bao pekee la ushindi leo.

Simba SC ilijitahidi kujaribu kusawazisha bao hilo baada ya hapo, lakini Kagera Sugar inayofundishwa na nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mecky Mexime ilikuwa imara kuzuia.

Kwa matokeo hayo, Simba SC inabaki na pointi zake 81 baada ya kucheza mechi 32 ingawa inaendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi moja zaidi ya watani wake, Yanga SC ambao hata hivyo wamecheza mechi tatu zaidi.

Kagera Sugar inafikisha pointi 43 baada ya kucheza mechi 35 na kujiinua kutoka nafasi ya 16 hadi ya 10 kwenye msimamo wa Ligi Kuu yenye timu 20. 

Uwanja wa Karume mjini Musoma, bao pekee la Tariq Kiakala dakika ya nane tu limetosha kuipa Biashara United ushindi wa 1-0 dhidi ya Yanga SC ya Dar es Salaam.

Kiakala alifunga kwa urahisi akitumia uzembe wa mabeki wa Yanga kudhani ameotea kufuatia krosi ya Wilfred Nkouluma katika mchezo ambao, Biashara United ilimaliza pungufu baada ya Nahodha wake, David David Kisu kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 90 na ushei kufuatia kugombana na beki Mwinyi Hajji Mngwali.

Kwa ushindi huo, Biashara United inafikisha pointi 40 baada ya kucheza mechi 34 na kujiinua kutoka nafasi ya 16 kutoka ya 18, wakati Yanga SC inabaki nafasi ya pili na pointi zake 80.

Dar es Salaam kikosi cha Simba SC kilikuwa; Aishi Manula, Zana Coulibaly, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Yussuf Mlipili, Erasto Nyoni, James Kotei/Jonas Mkude dk68, Hassan Dilunga/Rashid Juma dk53, Muzamil Yassin, Meddie Kagere, Emmanuel Okwi na Mohammed ‘Mo’ Ibrahim/Clatous Chama dk46.

Kagera Sugar; Said Kipao, Mwaita Gereza, David Luhende, Juma Shemvuni, Peter Mwalyanzi, Kassim Hamisi, Ally Ramadhani, Ramadhani Kapera, Paul Ngalyoma/Majjid Khamis dk69 na Evance Ludovic/ Omary Daga dk57.

Musoma kikosi cha Biashara United kilikuwa; Nourdine Balora, Kauswa Bernard/Taro Donald dk71, Wilfred Nkouluma, Tariq Kiakala, Derick Mussa, George Makang’a/Godfrey Malibiche dk85, Innocent Edwin, Lenny Kissu, Mpapi Nassib, Lameck Chamkaga na Juma Mpakala.

Yanga SC; Klaus Kindoki, Paul Godfrey, Mwinyi Hajji Mngwali, Andrew Vincent ‘Dante’, Kelvin Yondan, Papy Kabamba Tshishimbi, Mohammed Issa ‘Banka’/Mrisho Ngassa dk58, Thabani Kamusoko/Haruna Moshi dk70, Heritier Makambo, Amissi Tambwe na Raphaekl Daudi/Deus Kaseke dk58.
Share:

RAIS MAGUFULI ATEKELEZA AHADI YAKE KWA WAKAZI WA SENGEREMA


Ahadi yaRais Dkt. John Pombe Magufuli kwa wakazi wa Kata ya Nyampande, Wilaya Sengerema mkoani Mwanza ya kuwaondolea adha ya upatikanaji wa maji imeanza kutekelezwa, baada ya Serikali kusaini mkataba na mkandarasi ili kutandaza mtandao wa maji ya bomba katika
Kata hiyo.

Mkataba huowa zaidi ya shilingi bilioni moja umesainiwa Mei 09, 2019 baina ya Serikali kupitia Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira mkoani Mwanza (MWAUWASA) pamoja namkandarasi kampuni ya HALEM ya jijini Dar es salaam mbele ya Mkuu wa MkoaMwanza, John Mongella.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira mkoani Mwanza (MWAUWASA), Mhandisi Antony Sanga (kulia) pamoja na Mkurugenzi wa kampuni ya HALEM Construction ya jijini Dar es salaam, Mhandisi Happy Lebe (kushoto), wakisaini mkataba wa utekelezaji mradi wa maji Nyampande wilayani Sengerema. Aliyesimama upande wa kulia ni Mwanasheria wa MWAUWASA, Oscar Twakazi na kushoto ni Meneja Vifaa kampuni ya HALEM, Steven Malima.
Mkurugenzi wa MWAUWASA, Mhandisi Antony Sanga (kulia) pamoja na Mkurugenzi wa kampuni ya HALEM, Mhandisi Happy Lebe wakikabidhiana mkataba wa utekelezaji wa mradi wa maji Nyampande wilayani Sengerema baada ya pande zote mbili kuusaini.


Share:

Mahakama Kuu ya Tanzania Yabatilisha vifungu vya sheria vinavyowapa mamlaka Wakurugenzi wa Halmashauri kusimamia Uchaguzi

Mahakama Kuu ya Tanzania  imebatilisha sheria inayowapa mamlaka Wakurugenzi wa Halmashauri kusimamia Uchaguzi Mkuu.

Uamuzi huo umetolewa na Jaji Atuganile Ngwala kwenye kesi ya msingi namba 6 ya mwaka 2018 iliyofunguliwa na mtoto wa marehemu Chacha Wangwe ambaye ni Bob Chacha Wangwe.

Katika kesi hiyo ya Kikatiba, Jaji Ngwala amebatilisha vifungu viwili vya Katiba cha 7 (1) ambapo kinaeleza kuwa ‘Kila Mkurugenzi wa Jiji na Halmashauri wanakuwa wasimamizi wa Uchaguzi Mkuu’

Pia imebatilisha Kifungu cha 7 (3) kinachoeleza kuwa Tume inaweza kumchagua mtu yoyote kuwa msimamizi wa Uchaguzi wakati katiba inasema huwezi kuwa Mwanasiasa na ukawa msimamizi wa uchaguzi bali inatakiwa achaguliwe mtu huru.

Baada ya kueleza hayo, Jaji Ngwala amesema anazifuta sheria hizo na kama kuna upande haujaridhika ukate rufaa.


Share:

Taarifa Ya Mwenendo Wa Hali Ya Hewa Hususan Mvua Za Mfululizo Zinazoendelea Kunyesha Katika Baadhi Ya Maeneo Hapa Nchini.

Taarifa hii inatoa mwenendo wa hali ya hewa hususan mvua za mfululizo zinazoendelea kunyesha katika baadhi ya maeneo hapa nchini.

Mvua zinazoendelea kunyesha hapa nchini hususan katika maeneo ya pwani ya kaskazini, nyanda za juu kaskazini mashariki na kanda ya ziwa Victoria ni sehemu ya mvua za Masika. 

Mvua hizi zinatokana na kuimarika kwa ukanda wa mvua (ITCZ). Mvua za mfululizo katika baadhi ya maeneo ya pwani ya kaskazini (mikoa ya Tanga, Dar es salaam na Pwani pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba) zinatarajiwa kuendelea kwa kipindi cha siku mbili zijazo (mpaka siku ya jumapili tarehe 12 Mei 2019). 

Aidha vipindi vya mvua za mfululizo vinatarajiwa kujirudia kuanzia katikati ya mwezi Mei, 2019. Mamlaka itatoa taarifa za mara kwa mara za mwenendo wa mvua hizo katika taarifa zake za utabiri.

ANGALIZO: Pamoja na kwamba mvua za masika zinatarajiwa kupungua katika maeneo mengi mwishoni mwa mwezi Mei, 2019; athari za mvua kubwa zilizonyesha katika kipindi cha wiki moja mfululizo katika ukanda wa pwani ya kaskazini pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba zimesababisha kutuama kwa maji na mafuriko. 

Hivyo kutokana na ardhi kuwa na unyevunyevu mwingi, ongezeko kidogo la mvua linaweza kuendelea kusababisha athari kama zilizokwisha jitokeza.

USHAURI: Wananchi wanashauriwa kuendelea kufuatilia taarifa za utabiri kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania na kuzingatia tahadhari zilizotolewa na mirejeo yake pamoja na kupata na kuzingatia ushauri na miongozo ya wataalam katika sekta husika ili kupunguza athari zinazoweza kujitokeza.


Share:

Waziri wa Fedha Dkt. Mpango Aagana Na Mwakilishi Wa UNICEF Tanzania.

Na Josephine Majura, WFM, Dodoma
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.  Dkt.  Philip Isdor Mpango amelishauri  Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto (UNICEF), kuweka namna bora ya kuingiza ajenda ya uwekezaji kwa watoto katika mikutano mbalimbali  inayofanyika Barani Afrika.

Hayo ameyasema alipokuwa akiagana na Mwakilishi Mkazi wa  Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto (UNICEF) Bi.  Maniza Zaman, anayehamia nchini Kenya.

Dkt. Mpango alisema Shirika hilo linatakiwa kuweka mkazo huo ili kuhakikisha nchi za Afrika zinaweka mipango ya kuwekeza kwa ajili ya watoto kwa kuwa kundi hilo  ndiyo Taifa la kesho.

Alisema Serikali ya Tanzania kwa kutambua umuhimu wa Sekta ya Elimu Nchini, imekuwa ikitoa kipaumbele katika elimu kwa kutoa elimu ya awali, msingi na sekondari bure kwa lengo la kutoa nafasi kubwa kwa watoto ili wapate haki yao ya msingi.

Aidha Dkt. Mpango alisema kuwa katika kuboresha Sekta ya Elimu Duniani ni vema pia masuala ya lishe bora kwa mtoto yakatiliwa mkazo kwani lishe bora inachangia afanye vizuri dararasani lakini pia itamsaidia mtoto kuwa na afya bora itakayomfanya aweze kufikiri vizuri.

“Nitahakikisha agenda za kulinda haki ya mtoto nchini inapewa kipaumbele kwenye mikutano yetu mikubwa tunapokuwa tukijadili masuala ya maendeleo kwa ujumla”, alisisitiza Dkt. Mpango.

Aliongeza kuwa jukumu la kumlinda mtoto ni la kila mmoja kwakuwa wote walishawahi kuwa watoto hivyo ni vema kila mmoja atomize jukumu hilo.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto (UNICEF) Tanzania Bi.  Maniza Zaman, anaye hamia nchini Kenya, ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kufanya nae kazi vizuri kwa kipindi chote alichokaa nchini.

“Tanzania ni nchi nzuri, watu wake wana upendo, wana utu na wakarimu  karibu kwa mikoa yote 19 hadi 20 niliyowahi kutembelea wakati wa kutekeleza majukumu yangu”, alisema Bi. Maniza.

Alitoa wito kwa Serikali, kuendelea kutoa kipaumbele kwa ajili ya Sekta ya Elimu na Afya kwa kuongeza angalau asilimia moja ya bajeti kila mwaka kwakua zimekuwa na changamoto nyingi kutokana na ongezeko kubwa la  idadi ya watu kila siku.

Pia aliiomba Serikali ibuni mbinu na kuweka mipango endelevu kwa ajili  ya watoto itakayowasaidia katika siku zijazo kwa kuwa takwimu zinaonesha kuwa takriban watoto milioni 2 huzaliwa kila mwaka.

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango alimuahidi aliyekuwa Mwakilishi mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto (UNICEF) Bi.  Maniza Zaman, kuwa Wizara yake itaendelea kuhakikisha Sekta hizo zinapata bajeti ya kutosha katika mgawanyo.

Dkt. Mpango amemshukuru kwa kufanya kazi nchini na kumkaribisha tena na tena hasa kipindi cha mapumziko ambapo amesema milango ipo wazi muda wowote atakapojisikia kutembelea Tanzania.


Share:

Naibu Waziri Mavunde Akutana Na Kufanya Mazungumzo Na Mwakilishi Wa UNICEF Nchini

Na; Mwandishi Wetu
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa UNICEF nchini Bi. Maniza Zaman ambaye amemaliza muda wake alipomtembelea Ofisi kwake iliyopo Jijini Dodoma.

Katika mazungumzo yao, Mhe. Mavunde amelipongeza Shirika la Umoja wa Mataifa la UNICEF kwa kushirikiana na Serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo na kwa kutoa misaada katika sekta mbalimbali nchini.

“UNICEF imekuwa ikishirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu katika masuala mbalimbali yaliyolenga kuboresha na kuimarisha utekelezaji wa Sera ya Hifadhi ya Jamii (Social Security Policy of 2003), kuwapatia mafunzo watumishi katika masuala ya virutubishi na hifadhi ya jamii, pia kuwapatia vitendea kazi kama vile komputa na magari ambayo yanatumika kwenye miradi mbalimbali,” alieleza Mavunde. 

Aliongeza kuwa, Serikali imeguswa na jitihada za UNICEF na itaendeleza ushirikiano na shirika hilo katika kutekeleza jukumu la kuhudumia Watoto.

Aidha, Naibu Waziri Mavunde alimpongeza Bi. Maniza Zaman kwa kazi nzuri aliyofanya kipindi cha muda wake na kumsihi kuendelea kuwa balozi mzuri wa masuala ya Watoto.

“Tutakukumbuka kwa juhudi na ushauri uliokuwa ukitupatia katika masuala ya elimu na haki za Watoto,” alisema Mavunde. 

Kwa upande wake, Bi. Maniza Zaman amesema anaishukuru Serikali kwa ushirikiano iliompatia kwa kipindi chote alichokuwa hapa nchini.
 


Share:

Serikali Yatoa Wito Kwa Wadau Kuunga Jitihada Za Ujenzi Kituo Cha Kumbukumbu Za Baba Wa Taifa

Na Anitha Jonas – WHUSM
Serikali yatoa wito kwa wadau mbalimbali kujitokeza kuunga mkono jitihada za ukarabati na ujenzi  kituo cha kitalii Wilayani Kongwa Jijini Dodoma ambacho kitahifadhi kumbukumbu za Baba wa Taifa Hayati Mwl.Julius Nyerere .

Wito  huo umetolewa leo bungeni  jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Habari  Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza  alipokuwa akijibu Swali la Msingi la Mbunge wa Mtera Livingstone Lusinde (CCM) lililokuwa likiuliza ni lini serikali itajenga maktaba yenye kumbukumbu za kazi za Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambapo kituo hicho kitakuwa sehemu ya utalii na kitajengwa Makao Makuu ya nchini  ya Jijini Dodoma.

“Katika utekelezaji wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika,Serikali imeteua Wilaya ya Kongwa kuwa Kituo Kikuu cha Kumbukumbu za ukombozi nchini na katika kituo hicho kitakuwa na miundombinu kadhaa ya uhifadhi wa historia za viongozi ambazo zitajengwa ikiwemo kazi adhimu za Baba wa Taifa,”alisema Mhe.Shonza.

Akiendelea kuzungumza wakati akijibu swali hilo la msingi Naibu Waziri huyo alisema Serikali kwa kushirikiana na UNESCO imekarabati Studio za Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD) zilizopo Barabara ya Nyerere na kuwa kituo adhimu cha hifadhi rejea ya kazi za Baba wa Taifa.

Pamoja na hayo Mheshimiwa Shonza  akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum Dodoma (CCM) Felister Bura lililohoji lini ujenzi wa kituo hicho cha kumbukumbu cha Kongwa utaanza,Mheshimiwa Shonza alisema ujenzi wa kituo hicho umekwishaanza tangu mwaka 2015 ambapo ukarabati wa kituo hicho ulikwisha anza na unaendelea na pia kuna mipango mikubwa katika kituo hicho ikiwemo kujenga miundombinu ya kisasa mfano hoteli za nyota tano na kiwanja cha ndege.

Halikadhilika katika swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum Tabora (CCM)Mwanne Mchemba lini serikali itaingiza katika orodha kituo cha Tabora kutambulika rasmi kama kituo cha kumbukumbu za Baba wa Taifa kutokana na historia yake na mambo aliyoyafanya Mkoani hapo,ambapo Mheshimiwa Shonza alimuhakikishia Mbunge huyo kuwa Mkoa wa Tabora ni miongoni mwa Mikoa Kumi na Tano iliyoteuliwa kupitia Programu ya Urithi wa Ukombozi  wa Bara la Afrika kuwa vituo vya uhifadhi wa historia hiyo.

Pamoja na hayo serikali inaunga mkono juhudi za taasisi mbalimbali zinazofanya uhifadhi wa amali za Urithi wa kumbukumbu za Baba wa Taifa na baadhi ya taasisi hizo ni Maktaba ya Taifa Dar es Salaam,Makumbusho ya Taifa  Dar es Salaam,Makumbusho ya Mwl.Nyerere Butiama,Taasisi ya Mwalimu Nyerere na Vituo vya Televisheni vya TBC na ITV.


Share:

Mbunge Ataja Sababu za Wananchi Wa Lindi Kuwa Wafupi

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Lindi, Riziki Lulida (CUF), amesema wananchi wa mkoa huo wanakuwa wafupi kwasababu ya kubeba mizigo kichwani kwa kukosa usafiri kupitia barabara.

Lulida ameyasema hayo bungeni bungeni leo Mei 10, ambapo amesema kuwa Mkoa huo umekuwa ukitengwa kila mwaka kwa kunyimwa miradi mikubwa ya kiuchumi ikiwamo ya barabara.

Lulida ametolea mfano wa barabara za jimbo la Liwale kwamba hazikuwahi kujengwa kwa kiwango cha lami tangu serikali ya awamu ya kwanza.

“Mheshimiwa Naibu Spika kuna ubaguzi unafanywa na mawaziri katika kugawa miradi hapa nchini, huko Lindi  Liwale tumekuwa kama Guantanamo,  ninashauri Bunge tutengue kauli ya kuapa kwa kutumia biblia au quran, tutumie katiba badala ya hiyo misahafu kwa sababu hivyo vitabu havitaki uongo.

“Niwaambie huko Lindi mnazuia kangomba ya korosho wakati hamjengi barabara,  wale wafanyabiashara wanaamua kupeleka magari yao hata kwa shida lakini mnawazuia kununua korosho, je mnataka watu wafanyeje, leo hii watu wa Lindi wamekuwa wafu


Share:

Polisi na Askari Magereza wapigana makonde hadharani, mabomu na risasi zarindima stendi ya mabasi

Polisi na Askari wa Jeshi la Magereza wilayani Masasi Mkoani Mtwara, wamepigana makonde hadharani katika eneo la stendi kuu ya mabasi barabara kuu iendayo Tunduru.

Akizungumzia tukio hilo,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Blasius Chatanda, alisema tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 6 mchana baada ya askari polisi kumkamata askari Magereza ambaye inadaiwa alikuwa anaendesha pikipiki bila ya kuvaa kofia ngumu.

Hata hivyo, Kamanda Chatanda hakutaja majina ya askari huyo na polisi.

Chatanda alisema baada ya kutokea kwa ugomvi huo, Polisi walifyatua risasi hewani na kurusha mabomu ya machozi hali ambayo ilisababisha taharuki kubwa kwa wananchi wilayani humo.

Alisema muda kidogo walitokea askari Magereza watano ambao walifika eneo la tukio kwa ajili ya kumuokoa mwenzao, ndipo polisi na askari wa Magereza walipoanza kupigana.

Kamanda Chatanda alisema polisi huyo alikuwa doria katika operesheni ya kawaida ya ukamataji wa vyombo vya moto hasa pikipiki maarufu kama bodaboda, ambao wamekuwa wakiendesha bila ya kufuata sheria za usalama barabarani.

Alisema baada ya Polisi huyo kumshika askari magereza ambaye alikuwa kiendesha pikipiki bila ya kuvaa kofia ngumu na kumtaka kwenda kituo cha polisi au kuiacha pikipiki yake, alipinga ndipo mzozo ulipoanza.

“Baada ya muda kidogo kundi la askari magereza walifika kumuokoa mwenzao mara baada ya kumuona ameshikwa na Polisi, pia kundi la askari polisi walifika nao kumuokoa mwenzao, ndipo makundi hayo mawili ya jeshi walipoanza kuchapana makonde na kufyatua risasi hewani,” alisema Kamanda Chatanda.

Kamanda Chatanda alisema kufuatia tukio hilo, Jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi wa kujua chanzo zaidi ya vurugu hizo ikiwamo kufanya vikao vya dharura kati ya Jeshi la Polisi na Magereza, na kwamba uchunguzi utakapokamilika sheria itachukua mkondo wake.

 
Chanzo: Nipashe.


Share:

Iran Yaijibu Marekani Kuhusu Kufanya Mazungumzo......"Trump si mtu wa kuaminika"

Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amejibu madai ya rais wa Marekani kuhusu mazungumzo na Iran na kusema: "Donald Trump si mtu wa kuaminika".

Majid Takht-Ravanchi Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa ameyasema hayo wakati  akijibu swali la mtangazaji wa Televisheni ya NBC ya Marekani kuhusu iwapo Iran iko tayari kufanya mazungumzo na Marekani. Takht-Ravanchi aliongeza kuwa: "Awali Rais Donald Trump wa Marekani anapaswa kufafanua ni kwa nini alijiondoa katika meza ya mazugumzo."

Aidha Takht-Ravanchi amesema Trump aliondoka katika meza ya mazungumzo wakati ambao ulimwengu mzima ulikuwa katika meza ya mazungumzo na hata Baraza la Usalama liliidhinisha mazungumzo hayo.

Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa ameongeza kuwa, yamkini mazungumzo yakianza, rais wa Marekani kwa mara nyingine atajiondoa katika mazungumzo kwani anapinga na kubatilisha sheria za kimataifa.

Takht-Ravanchi aidha ameashiria madai ya rais wa Marekani kuwa anataka kufanya mazungumzo na Iran kwa lengo la kuizuia kupata silaha za nyuklia

Rais Trump wa Marekani jana aliandika katika ukurasa wake wa Twitter kuwa: "Nataka viongozi wa Iran wanipigie simu ili tuzungumze kuhusu mapatano mazuri mapatano ambayo yatawasaidia kuondoka katika mgogoro wa kiuchumi." 

Trump amedai kuwa, hataki mengi kutoka Iran isipokuwa tu kuhakikisha Iran haimiliki silaha za nyuklia.

Ikumbukwe kuwa mnamo Mei 8 mwaka 2018, Rais Trump wa Marekani aliamua kuondoa nchi yake katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA, ambayo ni mapatano ya kimataifa, na baada ya hapo akarejesha vikwazo dhidi ya Iran.


Share:

Rais wa Marekani Donald Trump Kasema Yuko Tayari Kufanya Mazungumzo na Iran

Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa yuko tayari kufanya mzungumzo na viongozi wa Iran, kama watamtafuta. 

Akizungumza na waandishi wa habari katika Ikulu ya Marekani, Trump alisema anatarajia viongozi wa Iran wampigie simu. 

Aidha rais huyo amesema kuwa aliamuru kupelekwa kundi la manowari zinazobeba ndege za kivita katika Ghuba ya Mashariki ya Kati kwa sababu ya vitisho vya Iran.

 Mwaka jana, Trump alijiondoa kutoka mkataba wa nyuklia na Iran na kisha akaongeza vikwazo dhidi ya nchi hiyo. Umoja wa Ulaya umetoa wito wa kuwepo suluhisho la kidiplomasia kwa mzozo huo. 

Hapo jana, viongozi wa jumuiya hiyo wakiongozwa na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel walisisitiza kuhusu dhamira yao ya kuuheshimu muafaka huo wa mwaka wa 2015, lakini wakasisitiza kuwa hawatakubali masharti yoyote.


Share:

WAZIRI BITEKO AZINDUA SOKO KUU LA MADINI MWANZA


Waziri wa Madini, Doto Biteko (pichani) amefanya uzinduzi wa Soko Kuu la Madini Mwanza na kutumia fursa hiyo kuwahimiza wachimbaji na wafanyabiashara wa madini kutumia soko hilo kuuzia madini yao na kuachana na tabia ya utoroshaji wa madini.

Uzinduzi wa soko hilo unganishi Kanda ya Ziwa umefanyika Mei 08, 2019 katika jengo la Rock City Mall ambapo Biteko amebainisha kwamba uanzishwaji wa masoko ya madini nchini umesaidia ongezeko la kiwango cha uuzaji madini tofauti na hapo awali ambapo yalikuwa yakiuzwa kiholela na hivyo kuikosesha Serikali mapato.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Mwenyekiti Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula akitoa salamu za tume kwenye uzinduzi huo.
Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila akitoa taarifa ya hali ya uanzishwaji masoko ya madini nchini ambapo amebainisha kwamba zaidi ya mikoa 10 tayari imeanzisha masoko hayo.
Mfanyabiashara wa madini, Kakono Kaniki akitoa salamu kwa niaba ya wafanyabiashara wa madini mkoani Mwanza.

Mongella ajivunia Soko Kuu la Madini Mwanza "tunataka nchi ifaidike"


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger