Thursday, 9 May 2019

Mdude Chadema Apatikana Akiwa Katika Hali Mbaya

Mdude Nyagali ‘Mdude Chadema’ , ambaye ni kada maarufu wa  Chadema amepatikana eneo la Inyala Mbeya Vijijini baada ya kudaiwa kutekwa na watu wasiojulikana Jumamosi jioni wiki iliyopita mjini Vwawa-Mbozi mkoani Songwe.

Taarifa za kupatikana kwa Mdude, zilitolewa na Diwani wa Kata ya Nsalala, Mbalizi, Kisman Mwangomale akisema amepigiwa simu na watu wa eneo la Makwenje Kijiji cha Inyala Mbeya vijijini, wakiomba msaada wa haraka kwenda kumbeba.
 
Mdude alidaiwa kutekwa Jumamosi wiki iliyopita na watu wasiojulikana ambao walifika ofisini kwake wakiwa na magari mawili yenye rangi nyeupe kisha kumchukua kwa nguvu na kumuingiza kwenye moja ya magari yao na kuondoka naye na kwenda kusikojulikana.


Share:

BARABARA ZAFUNGWA MOSHI IBADA YA MAZISHI YA DR. MENGI

Haijapata kutokea. Ndivyo unavyoweza kusema kutokana na umati wa watu waliojitokeza katika ibada ya mazishi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Kampuni za IPP, Reginald Mengi.

Barabara zote za kuingia na kutoka katika Kanisa Kuu la Usharika wa Moshi mjini wa Dayosisi ya Kaskazini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), zimefungwa kwa kuwekewa utepe wa njano na polisi.

Barabara ya kuelekea kanisa hilo ukitokea ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro imefungwa kuanzia jengo la NSSF Commercial Complex, wakati ile ya kutokea barabara ya Boma kuelekea kanisani imefungwa kuanzia ilipo benki ya KCB.

Na Daniel Mjema, Mwananchi
Share:

MDUDE WA CHADEMA APATIKANA AKIWA HOI MBEYA


Kijana Mdude Nyagali, mfuasi wa Chadema amepatikana eneo la Inyala Mbeya Vijijini baada ya kudaiwa kutekwa na watu wasiojulikana Jumamosi jioni wiki iliyopita mjini Vwawa-Mbozi mkoani Songwe.

Akizungumza kwa simu jana usiku huu, mmoja wa watu waliokwenda kumbeba eneo la tukio, Anangisye Kwame amesema wameshamchukua na kuelekea naye Hospitali kwa ajili ya matibabu.

"Ndio, tupo nae kwenye gari, tunarudi mjini, anaongea vizuri. Ila tunaenda naye kwanza hospitali," amesema.

Awali, taarifa za kupatikana kwa Mdude, zilitolewa na Diwani wa Kata ya Nsalala, Mbalizi, Kisman Mwangomale akisema amepigiwa simu na watu wa eneo la Makwenje Kijiji cha Inyala Mbeya vijijini, wakiomba msaada wa haraka kwenda kumbeba.

Mwangomale ameliambia Mwananchi, "kweli yupo mikononi mwetu kwa sasa baada ya mimi kupigiwa simu na watu wa kule, ndiyo nikaona njia ya haraka ni kuandika kwenye magroup ya whatsapp."

Mdude alidaiwa kutekwa Jumamosi wiki iliyopita na watu wasiojulikana ambao walifika ofisini kwake wakiwa na magari mawili yenye rangi nyeupe kisha kumchukua kwa nguvu na kumuingiza kwenye moja ya magari yao na kuondoka naye na kwenda kusikojulikana.

Na Godfrey Kahango, Mwananchi
Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya May 9























Share:

Wednesday, 8 May 2019

WANAWAKE WANNE WAGOMBANIA MAITI YA MWENDESHA BODABODA


Maafisa wa polisi kutoka kituo cha polisi cha Kerugoya kaunti ya Kirinyaga nchini Kenya wamelazimika kuingilia kati na kutuliza hali baada ya wanawake wanne kujitokeza na kuanza kuzozania mwili wa mwendesha bodaboda.

 Janet Wambui, Lydia Wanjiru, Susan Wakuthii, na mwingine wa nne kutoka kijiji cha Kimbimbi walifika katika hifadhi ya wafu hospitali ya rufaa ya kaunti ya Kirinyaga kila mmoja akitaka kuuchukua mwili wa marehemu Peter Mwangi akidai ni mumewe.

 Kizaazaa kilizuka pale ambapo kila mwanamke alidai kuwa mke halali wa marehemu na kutaka apatiwa fursa ya kumzika.

La kushangaza kila mwanamke alikuwa na mtoto wa kiume ambaye alijaliwa na marehemu aliyefariki dunia Jumapili Aprili 28 kwa njia isiyoeleweka. 

Baada ya mvutano mkali kati ya wanne hao, familia ya marehemu iliamua kumzika marehemu nyumbani kwa mjomba wake ambapo hafla ya mazishi ilifanyika bila tatizo. 
Chanzo - Tuko
Share:

PICHA: Mwili wa Reginarld Mengi Ulivyopokelewa Kijini Kwake Nkweseko Machame




Share:

Waziri Mbarawa Atengua Uteuzi wa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Uchimbaji Visima na Uchimbaji Mabwawa- DDCA




Share:

KONDOO WAANDIKISHWA SHULE ILI KUJAZA NAFASI YA WANAFUNZI DARASANI

Mkulima mmoja nchini Ufaransa amewaandikisha shule kondoo wake 15 ili kuongeza namba ya wanafunzi baada ya mamlaka za kijiji kimoja kutangaza kutaka kusitisha masomo.

Shule ya Jules Ferry iliyopo kwenye kijiji cha Crêts-en-Belledonne, kwenye safu za milima ya Alps karibu na jiji la Grenoble, kimekuwa kikikumbwa na tatizo la kushuka kwa namba ya wanafunzi wanaoandikishwa kwa masomo.

Hali hiyo inatishia kufungwa kwa shule hiyo.

Lakini kama hatua ya kupinga kufungwa kwa shule, mfugaji na mkulima Michel Girerd ameamua kuwaandikisha baadhi ya kondoo wake kama wanafunzi.

Baadhi ya kwanafunzi hao ambao ni kondoo wanafamika kwa majina kama Baa-bete, Dolly na Shaun.
Bw Girerd alienda shuleni hapo akiwa na kondoo 50 kuhudhuria sherehe maalumu iliyohudhuriwa na watu 200 wakiwemo wanafunzi, walimu na maafisaa wengine.

Meya wa eneo hilo, Jean-Louis Maret alikabidhiwa vyeti vya kuzaliwa vya 'wanafunzi' hao wapya. Pia akaonesha kukerwa kwake na suala la kutishia kufunga shule hiyo kutokana na uhaba wa wanafunzi.

"Sasa hakutakuwa na tishio la kufungwa kwa kitu chochote," moja ya wazazi Gaelle Laval amesema, na kuongeza kuwa mfumo wa elimu "hauangalii hoja zilizopo katika eneo hilo, na badala yake unaangalia idadi (ya wanafunzi) tu."

Wanafunzi waliohudhuria sherehe hiyo walibeba mabango yalikuwa na ujumbe kuwa: "Sisi siyo kondoo".

Chanzo - BBC
Share:

HAT TRICK PACHA ZA KAGERE, OKWI GUMZO, KAGERE AITAFUTA REKODI YA TAMBWE, OKWI AMFIKIA KAGERE


Washambuliaji nyota wa Simba, Emmanuel Okwi na Messy Kagere wameweka rekodi ya kufunga mabao sita yaani hat trick mbili ndani ya mechi moja.

Wachezaji hao wote wenye asili ya Uganda kwa kuwa Okwi ni Mganda na Kagere ni Mnyarwanda mwenye asili ya Uganda, wamefunga bao hizo sita wakati Simba ikiitwanga Coastal Union kwa mabao 8-1 katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Mabao hayo, yanamfanya Kagere kufikisha mabao 20 msimu katika ligi kuu akifikia rekodi ya mabao 20 ya Okwi msimu uliopita lakini akibakiza bao moja kufikia idadi ya mabao 21 aliyofunga Amissi Tambwe msimu wa 2015/16 akiwa mfungaji bora.

Kwa mabao hayo 14, Okwi naye amemfikia nahodha wake John Bocco aliyekuwa benchi katika mechi ya leo akishuhudia 'vijana wake" wakiwagaragaza Wagosi wa Kaya.

Mabao mengine yalifungwa na Hassan Dilunga na Cleotus Chama raia wa Zambia na kuifanya Simba iandike ushindi huo mnono zaidi.

Kwa ushindi wa leo, Simba imefikisha pointi 81 na kupaa kileleni ikiwaacha Yanga wenye pointi 80 waliokuwa wamekaa kileleni kwa muda mrefu zaidi.

Yanga wamecheza 34 huku Simba wakiwa wamefikisha mechi 31 baada ya kucheza mechi yao ambayo wametoa kipigo kikali kwa Wagosi wa Kaya.
Share:

MWANAMUZIKI BERESA KAGERE AKUTWA AMEFARIKI DUNIA


Mwimbaji mkongwe wa muziki wa dansi nchini, Beresa Kakere leo Jumatano asubuhi amekutwa amefariki chumbani kwake ilhali akiwa hana jeraha lolote.

Mdogo wa mwanamuziki huyo ambaye naye ni mwanamuziki wa dansi, Juma Kakere, amethibitisha kutokea kwa kifo cha kaka yake.

Juma Kakere alisema kaka yake amefariki dunia asubuhi Tanga Barabara ya Nne katika chumba alichokuwa akiishi baada ya majirani zake kugundua maiti yake walipovunja mlango.

“Alikuwa amechelewa kuamka, wakamgongea mlango bila ya mfanikio ndipo wakavunja na kumkuta amefariki dunia,” alisema Juma Kakere akiwa safarini kwenda Tanga.

Juma alisema mara ya mwisho kuwa na kaka yake ilikuwa wiki mbili zilizopita na hakuwa akiiumwa, bali amefariki ghafla.

“Kwa kweli kaka yangu Beresa ni mtu ambaye alinisapoti katika kazi yangu ya muziki na ndiye aliyegundua kipaji change na alikuwa anajitahidi sana kuimba nyimbo zangu nilizokuwa nikizitunga kabla sijawa mwanamuziki,” alisema Juma.

Kakere alizaliwa Tanga na alimaliza masomo yake katika Shule ya Sekondari ya Karimjee mwaka 1969.

Marehemu alianza kujifunza muziki katika Bendi ya Jamhuri Jazz chini ya John Kijiko na baadaye alipiga muziki katika bendi mbalimbali za Nairobi na Mombasa za Kenya.

Alirejea nchini mwaka 1976 alipojiunga na Biashara Jazz na kutamba na Kibao cha Clara.

Januari, 1978 aliingia studio na Bendi ya Dar International na kurekodi nyimbo kadhaa ukiwamo utunzi wake wa Magreti.

Mwaka 1979, alijiunga na Juwata Jazz akiwa na marehemu Kassimu Mponda na kupata umaarufu mkubwa alipotunga kibao cha Sogea Karibu na vingine vya Utu ni Tabia Njema na Nimekubali Makosa.

Hata hivyo, hakudumu sana katika bendi hiyo baadaye alijiunga na Bima Lee na kutamba na nyimbo za Asia, Remmy, Ombi na nyingine nyingi hadi alipoamua kustaafu shughuli za muziki mwaka 1982.
Kwa mujibu Juma Kakere, Beresa hakuacha mke wala mtoto.

Na Rhobi Chacha - Mwanaspoti 


Share:

SIMBA WAITWANGA KIBABE COASTAL UNION 8 - 1

Simba imeitwanga Coastal Union kwa mabao 8-1 katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Pamoja na ushindi wake mnono, washambuliaji wake wawili, Emmanuel Okwi na Meddy Kagere kila mmoja amefunga mabao matatu, yaani hat trick.

Kwa mabao hayo, Kagere amefikisha mabao 20 msimu katika ligi kuu huku Okwi akifikisha 14 na kulingana na nahodha wa Simba, John Bocco aliyekuwa benchi katika mechi ya leo.

Mabao mengine yalifungwa na Hassan Dilunga na Cleotus Chama raia wa Zambia na kuifanya Simba iandike ushindi huo mnono zaidi.

Kwa ushindi wa leo, Simba imefikisha pointi 81 na kupaa kileleni ikiwaacha Yanga wenye pointi 80 waliokuwa wamekaa kileleni kwa muda mrefu zaidi.

Yanga wamecheza 34 huku Simba wakiwa wamefikisha mechi 31 baada ya kucheza mechi yao ambayo wametoa kipigo kikali kwa Wagosi wa Kaya.
Share:

ZANTEL YAZINDUA OFA YA MFUNGO WA RAMADHAN


Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohamed Khamis Mussa (katikati) akiwaonyesha waandishi kipeperushi cha maelezo ya ofa za mfungo wa Ramadhan zilizotolewa na kampuni ya Zantel kurahisisha mawasiliano na kupata taarifa mbalimbali za mfungo wakati wa uzinduzi wake uliofanyika mjini Zanzibar.Wengine pichani (kushoto ) ni Mkuu wa Bidhaa wa Zantel, Aneth Muga, na ( kulia ) ni Katibu wa Mufti za Zanzibar, Fadhil Soraga.
Katibu wa Mufti za Zanzibar, Fadhil Soraga, akiongea katika mkutano wa waandishi wa habari wakati wa hafla ya uzinduzi wa ofa za mfungo wa Ramadhan zilizotolewa na kampuni ya Zantel kurahisisha mawasiliano na kupata taarifa mbalimbali za mfungo wakati wa uzinduzi wake uliofanyika wiki hii mjini Zanzibar. Wengine pichani (kushoto) ni Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohamed Khamis Baucha na (kulia) ni Mwanasheria Katika ofisi ya Mufti, Haji Habib Kombo.
Mkuu wa Bidhaa wa Zantel, Aneth Muga,akifafanua ofa hiyo katika mkutano wa waandishi wa habari
---
Kampuni ya mawasiliano ya Zantel, imezindua ofa maalum ya mwezi mtukufu wa Ramadhan kwa wateja wake, ambayo itawawezesha kufanya mawasiliano kwa gharama nafuu sambamba na kupata taarifa muhimu kuhusiana na kipindi cha mfungo.

Akitangaza ofa hiyo mjini Zanzibar, Afisa Mwandamizi wa Mawasiliano na Habari wa Zantel, Rukia Mtingwa alisema “Ramadhani ni muda muafaka wa kujenga mahusiano mazuri na ndugu, jamaa na marafiki, ofa hii ni ishara ya Zantel kuwasaidia wateja wake kuweza kuungana na kuwasiliana kwa urahisi zaidi na wapendwa wao na kupata taarifa muhimu za mwezi huu mtukufu”.

Mtingwa alisema ofa hii ya Ramadhani imelenga kuwazawadia wateja wa Zantel watakaojiunga na vifurushi mbalimbali vya muda wa maongezi vya siku, wiki na kifurushi cha mwezi.

Wateja ambao wataweka kifurushi cha muda wa maongezi wa shilingi 999/- kila siku wataweza kupata jumbe za maneno za bure kati ya mtandao wa Zantel kwa Zantel, jumbe mbalimbali kuhusu mwezi wa Ramadhan, jumbe za kukumbusha wakati wa swala 5 na nukuu mbalimbali za maandiko ya Koran takatifu.

Alisema wateja watakaoweka kifurushi cha wiki cha shilingi 4,999/ wataweza pia kupata jumbe za maneno za bure kati ya mtandao wa Zantel kwa Zantel, jumbe mbalimbali kuhusu mwezi wa Ramadhan, jumbe za kukumbusha wakati wa swala 5, kuwakumbusha muda wa kufuturu na nukuu mbalimbali za maandiko ya Koran takatifu.

Hali kadhalika wateja wataoweka kifurushi cha mwezi cha shilingi 14,999/ wataweza kupata jumbe za maneno za bure kati ya mtandao wa Zantel kwa Zantel, jumbe mbalimbali kuhusu mwezi wa Ramadhan, jumbe za kukumbusha wakati wa swala 5, kuwafahamisha muda wa kufuturu na nukuu mbalimbali za maandiko ya Koran takatifu.

Vifurushi vyote hivi vya Ramadhan vitapatikana kwa kujiunga kwa kupiga *149*15# na mteja anachagua aina ya kifurushi anachotaka kujiunga nacho.
Share:

Serikari Kuwasilisha Taarifa Ya Utekelezaji Wa Malengo Ya Maendeleo Endelevu Umoja Wa Mataifa

Na Josephine Majura na Farida Ramadhani, WFM, Dodoma

Katika kutekeleza ajenda za Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG’s), Serikali imejipanga kuwasilisha Taarifa ya Mapitio ya Hiari (VNR) katika Jukwaa la Siasa la Umoja wa Mataifa (HLPF) mwezi Julai mwaka huu mjini Newyork nchini Marekani.

Hayo yameelezwa na  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango (Sera), Bw. Adolf  Ndunguru wakati akifungua kikao cha kujadili Taarifa ya utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG’s).

Bw. Ndunguru alisema kuwa uwasilishwaji wa taarifa hiyo utakuwa ni wa kwanza miongoni mwa mfululizo wa taarifa za mapitio mengine ambayo yanatokana na mapitio hayo yanayoonesha namna nchi inavyotekeleza Malengo hayo.

Alisema kikao hicho ambacho kinahusisha wadau wa ndani na nje ya nchi, ni muhimu kwa maendeleo ya nchi na wananchi kwa ujumla kwa kuwa kitajadili taarifa mbalimbali za utekelezaji wa Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu (SDG’s) kwa kuangalia maeneo muhimu kama elimu, afya na uchumi.

Bw. Ndunguru alisema kikao hicho kinatoa fursa kwa wadau hao kujadili rasimu ya awali ya taarifa ya utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG’s) na kutoa nafasi kwa wadau hao kuchangia  maoni yao kuhusu namna ya kuboresha taarifa hiyo kabla ya kuiwasilisha Umoja wa Mataifa.

“Tukiwa kama wananchama wa Umoja wa Mataifa, tumekubali kuingia mkataba wa kuutekeleza  Maendeleo Endelevu katika ajenda ya 2030 , kwa lengo la kuboresha maisha ya watanzania, kwa kuhakikisha tunapeleka elimu bora, afya bora  na kuboresha miundombinu”, alisema Bw. Ndunguru.

Bw. Ndunguru alibanisha kuwa mpaka sasa Tanzania inatekeleza kwa kasi ajenda hiyo ya 2030 ya Maendeleo Endelevu  kwa kuchukua hatua kadhaa ikiwemo kutoa kipaumbele katika masuala ya elimu, afya na kukuza uchumi wa nchi.

Naye mdau wa mkutano huo ambaye ni  mwakilishi wa Umoja wa Asasi za Kiraia nchini, Prisca Kowa alilisema kwa sasa nchi inaonekana imejipanga kisawasawa kutekeleza Maendeleo Endelevu kwa kuwa imeweza kuyahusisha maendeleo hayo katika mipango mikubwa ya maendeleo ya nchi.

 Ametoa wito kwa Serikali, Wizara, Taasisi na wadau wa maendeleo  kufanya kazi kwa kushirikiana ili kuhakikisha taarifa sahihi za utekelezaji wa Maendeleo Endelevu zinapatikana kwa usahihi na kwa wakati.


Share:

Serikali Kuendelea Kutoa Elimu Ya Matumizi Ya Mbolea Ya Asili -Naibu Waziri wa Kilimo

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Serikali kwa kushirikiana na taasisi za sekta binafsi imeendelea kutoa elimu ya kilimo bora inayojumuisha matumizi sahihi ya mbolea za asili, viuatilifu vya asili, mbegu bora na hifadhi ya mazingira ili kuzalisha mazao kwa tija na kuwa na kilimo endelevu.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) ameyasema hayo bungeni Jijini Dodoma leo tarehe 8 Mei 2019 wakati akijibu swali la Mbunge wa Chambani Mhe Yussuf Salim Hussein aliyetaka kufahamu Serikali imeweka mikakati gani ya kutoa elimu ya mbolea ya asili kwa wakulima na hatua Serikali inayoichukua ili kuona kuwa Tanzania ni nchi inayoongoza kwa kuzalisha mazao yasiyotumia mbolea za viwandani.

Alisema kuwa katika kutekeleza mpango wa muda mrefu wa matumizi sahihi ya virutubisho vya udongo, Serikali kupitia Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) inafanya utafiti wa afya ya udongo katika Kanda zote saba za kiikolojia za kilimo nchini.

Utafiti huo unalenga kubaini aina za virutubisho na tabia za udongo katika maeneo mbalimbali nchini ili kuweza kutoa elimu kwa wakulima kuhusu kiasi, aina na matumizi sahihi ya mbolea za viwandani na asili. Utafiti huo umeanza kwa kuchukua sampuli za udongo katika Kanda za Nyanda za Juu Kusini, Kanda ya Kati, Kanda ya Kaskazini na sehemu ya Kanda ya Mashariki (Mkoa wa Morogoro) na utaendelea katika maeneo mengine nchini na kukamilika Juni 2020.

Alisema, kwa kutambua ongezeko la mahitaji ya mazao na bidhaa za kilimo zinazozalishwa kwa kutumia mbolea za asili na viuatilifu vya asili, Serikali imeboresha mtaala wa mafunzo katika vyuo vya kilimo ambapo mada za kilimo hai na hifadhi ya mazingira zimejumuishwa ili kuwawezesha maafisa ugani na wakulima kupata elimu hiyo.

Mhe Mgumba aliongeza kuwa Serikali kwa kushirikiana na Tanzania Organic Agriculture Movemet (TOAM), Sustainable Agriculture Tanzania (SAT), Ecology Agriculture chini ya SWISSAID, Zanzibar Organic Producers (ZANOP), Tanzania Alliance for Biodiversity (TABIO) na TANCERT inatoa elimu ya kilimo hai kwa wakulima na kutoa vyeti vya ubora wa mazao kwa ajili ya masoko maalum. Baadhi ya mazao ambayo yanazalishwa katika mfumo wa kilimo hai hapa nchini ni pamoja na kakao, kahawa, pamba na viungo.

Kadhalika, akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe Easter Michael Mmasi aliyetaka kufahamu kuhusu ushiriki wa wanawake kwenye sekta ya kilimo, Mhe Mgumba alisema kuwa Sekta ya Kilimo inajumuisha sekta ndogo za kilimo mazao, mifugo, uvuvi na misitu.

Bajeti za Wizara za Sekta ya Kilimo zinajumuisha bajeti za Wizara za sekta husika, Bodi za mazao na Taasisi mbalimbali zilizo chini ya Wizara za Kisekta. Utekelezaji wa bajeti hizo huwawezesha  wanaume na wanawake katika shughuli za kilimo. Wanawake wanachangia asilimia 90.4 ya nguvukazi ya wanawake inayotumika katika shughuli za kilimo na kuchangia wastani wa asilimia 70 ya mahitaji ya chakula nchini. 

Mhe Mgumba alisema kuwa katika kutatua changamoto hizo Serikali inaendelea kusimamia utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ya mwaka 2004 kupitia mifuko ya uwezeshaji ikiwemo Mfuko wa Maendeleo wa Wanawake (Women Development Fund - WDF) ambao huchangiwa asilimia 4 ya mapato ya Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kila mwaka. Katika mwaka 2017/2018, jumla ya Shilingi 15,633,312,764.91 zimetolewa kwa vikundi 2,919 vya wanawake na vijana vyenye jumla ya wanawake wajasiriamali 29,190 katika Halmashauri mbalimbali nchini.

Aidha, alisema kutokana na umuhimu wa wanawake katika kilimo Serikali imeielekeza Benki ya Maendeleo ya Kilimo (Tanzania Agricultural Development Bank – TADB) katika mikopo inayotoa asilimia 20 ya mikopo itolewe kwa vikundi vya wanawake. Hadi Januari 2019, asilimia 33 ya mikopo imetolewa katika vikundi vya wanawake kupitia Benki ya TADB. Vilevile, benki za NMB na Azania zimeanzisha dirisha maalumu la kutoa mikopo kwa vikundi vinavyo jishughulisha na kilimo na miradi mbalimbali. Pia Serikali imehamasisha wanawake kujiunga kwenye vikundi vya ushirika wa akiba na mikopo kama SACCOS, VICOBA ili kupata huduma za kifedha na mikopo kwa urahisi ili kuongeza mitaji yao katika kilimo.

Mhe Mgumba aliongeza kuwa, Serikali imeuelekeza Mfuko wa Pembejeo za Kilimo (Agricultural Input Trust Fund - AGITF) kutoa kipaumbele kwa vikundi vya wanawake vinavyoomba mikopo ya kuendeleza kilimo. Vile vile, Serikali imeendelea kutoa hati miliki za ardhi za kimila na hati miliki za ardhi kwa ajili ya kuwawezesha wanawake kumiliki ardhi na kuzitumia kama dhamana kukopa katika taasisi mbalimbali za kifedha ili waweze kupata mitaji ya kununua pembejeo na zana bora za kilimo ili kuongeza uzalishaji, tija na kuanzisha viwanda vidogo vidogo vya usindikaji wa mazao ya kilimo.



Share:

Serikali Yasema Ipo katika maandalizi ya muswada wa marekebisho ya Sheria ya VVU na UKIMWI ili kuruhusu watu kujipima wenyewe

Serikali iko mbioni kukamilisha muswada wa Sheria ya Bima ya Afya kwa wote na kuuwasilisha bungeni Septemba.

Pia wizara hiyo ipo katika maandalizi ya muswada wa marekebisho ya Sheria ya VVU na Ukimwi sura Na 431 ili kuruhusu watu kujipima wenyewe na kushusha umri wa mtu kupima bila ridhaa ya mzazi au mlezi kutoka miaka 18 hadi 15.

Waziri wa  Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, akisoma bajeti ya wizara yake kwa mwaka 2019/20 bungeni jana, alisema maandalizi ya mpango huo yamekamilika ikiwamo mkutano wa kuelimisha wabunge kuhusu mkakati wa uboreshaji mfumo wa ugharamiaji wa bima  za afya.

Katika maandalizi hayo, alisema wabunge 19 walifanya ziara nchini Rwanda na Ghana Disemba mwaka jana kwa lengo la kupata uzoefu wa namna nchi hizo zilivyoweza kutekeleza mfumo huo wa bima kwa wote.

Katika hotuba hiyo, waziri Ummy alitaja vipaumbele vya wizara hiyo kwa mwaka 2019/20 kuwa ni pamoja na kuendelea kununua na kusambaza chanjo kulingana na mahitaji, kuwakinga watoto wa umri chini ya mwaka mmoja na magonjwa yanayozuilika kwa chanjo ambapo Sh bilioni 30 zimetengwa.

Kuhusu ukimwi, Ummy alisema huduma za tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na maambukizi na VVU zimeendelea kutolewa na idadi ya watu wanaotumia dawa ya kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi imeongezeka kufikia wati 1,103,016 mwa Machi.

Alisema pia wizara yale kwa kushirikiana ile ya Viwanda na Biashara na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na Bohari ya Dawa imeandaa mwongozo unaoainisha fursa mbalimbali za uwekezaji katika viwanda vya dawa na vifaa tiba.

Mwongozo huo utarahisisha upatikanaji wa taarifa katika uwekezaji wa viwanda vya dawa nchini ambapo hadi kufikia Machi mwaka huu viwanda nane vya dawa vinaendelea kujengwa nchini.


Share:

Kutana na Sheikh Omary Mwenye Uwezo wakufanya Dua mbalimbali za Matatizo Yako Na Kutafsiri Ndoto kwa kutumia Vitabu vya QUR-AN

Sheikh Omary Ni bigwa wa kutatua matatizo kwa haraka, ni mtu aliye jaliwa kubuli Shufaa pia anatoa Duah  za Ruhia. Ukija na Maradhi yanaondoka hapo hapo bila kungoja kesho,  UKIPEWA MKONO  na Sheikh Omary .
 
Wasiliana na Mtaalam Huyu Kwani yeye hufaulu Pale wote waliko Shindwa na Pia Humaliza kazi zilizo Shindikana ama Zilizo Achwa ndani ya Siku Moja 1.
 
Sheikh Omary ni Mtaalamu wa Nyota za Binadamu  Mwenye Uwezo wa Kubaini Tatizo lako tu Pindi Utakapo Fanya Mawasiliano Kupitia Wasaa Husika.
 
Je una NUKSI  zisizo kwisha.!? JE umekimbiwa na Mume/Mke na Anaishi na Mtu Mwingine..!? Muone Akutatulie,
 
Una kosa bahati ya wanaume au mume wa kukuoa..Unataka nyota ing'ae Au huna hamu na Mkeo/ Mumeo.
 
Jini mahaba. Kama Unakasirika ovyo ukiwa na bwana au mwanamke wako na  kumchukia Mpaka  kushindwa kufanya nae tendo la ndoa.
 
Njoo umuone Sheikh Omary  na ujuwe  yanayo kusibu.Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN

Mawasiliano: Sheikh Omary 0673531992 WhatsApp/Call
Tembelea Page ya @Mtabibu_Omar  @Mtabibu_Omar
Usome Makala Tofauti Tofauti Kama.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger