Wednesday, 8 May 2019

Jeshi la Polisi Lasema Askofu Gwajima Si Mtuhumiwa bali ni Muathirika wa Tukio hilo la Video Chafu.....Wananchi Waonywa Kuisambaza

Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa leo Jumatano April 8, 2019 amezungumzia tena sakata la video ya ngono inayodaiwa kuwa ya Askofu Josephat Gwajima na kusema kuwa Askofu huyo kwa sasa sio mtuhumiwa, bali ni muhanga aliyeathiriwa na tukio hilo.

Amesema  kwa kushirikiana na mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai (DCI), Jeshi la Polisi limeanza uchunguzi wa video  hiyo ya ngono inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii.

"Jeshi la Polisi Kanda Maalumu limeanza uchunguzi wa video hiyo mara moja na linapenda kuwapa taarifa wananchi (kuwa) Gwajima siyo mtuhumiwa, ni muathirika wa tukio hilo kwani tukio hilo linaweza kufanywa na mtu yeyote kwa nia ya kutaka kuharibu heshima yake kwa jamii na waumini," amesema Mambosasa.

Mambosasa ametoa wito kwa wananchi kuacha kusambaza video hiyo kwa maelezo kuwa ni kosa la jinai na kuwataka waumini wa kanisa hilo kuwa watulivu kwani uchunguzi unaendelea ili kubaini aliyeisambaza na lengo la kufanya hivyo.


Share:

Mamia ya Wananchi wa Kilimanjaro Waupokea Mwili wa Dr Reginald Mengi......Waziri Mkuu Majaliwa Kuongoza Mazishi yake Kesho

Mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kampuni tanzu za IPP, Dk. Reginald Mengi, umewasili Kilimanjaro tayari kwa mazishi yatakayofanyika kesho Alhamisi Mei 9, kijijini  kwake Nkuu Sinde, wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.

Mwili wa Mengi uliwasili leo Jumatano Mei 8, saa 3:30 asubuhi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na kupokewa na viongozi mbalimbali akiwamo Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mughwira na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro.

Mughwira amesema Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, anatarajiwa kuongoza maelfu ya wakazi wa Mkoa wa Kilimanjaro na maeneo jirani.

Mbali na kiongozi huyo pia Spika wa Bunge, Job Ndugai, wabunge, mawaziri, wakuu wa mikoa, mabalozi pamoja na viongozi wa dini wanatarajiwa kushiriki katika mazishi hayo.

“Hadi sasa nimepata taarifa kwamba Rais atatuma Mwakilishi ambaye ni Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa atashiriki katika mazishi japo sijapata uthibitisho… pia Spika wa bunge letu atakuwepo pamoja na viongozi wengine mbalimbali wa kiserikali na dini,” amesema.


Share:

Kutana na shariff Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH Adam shariff Mwenye Uwezo wakufanya Dua mbalimbali Na Kutafsiri Ndoto

Kutana  na shariff Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH Adam shariff  Mwenye UWEZO wakufanya dua mbali mbali  Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na  Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?

Wasilina na Adam shariff Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO   Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? . Adam shariff Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..

Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN  . Anatafsiri Ndoto. , KUSAFISHA NYOTA. Mvuto wa Mwili na Biashara.


Mawasiliano: (+255 )715971688 au (+255  )756914036



Share:

POLISI WAANZA KUCHUNGUZA VIDEO YA NGONO INAYODAIWA KUWA YA ASKOFU GWAJIMA

Share:

VIDEO: Tazama Hapa Alichokisema Mke wa Askofu Gwajima Kuhusu Video ya Ngono Inayosambaa Mitandaoni

Leo  Jumatano May 8, 2019, Askofu Gwajima ameita waandishi wa habari kuongelea video ya ngono inayosambaa mitandaoni. Gwajima amekana kuhuika na video hiyo. Amesema imetengenezwa kwa lengo la kumchafua.

Katika mkutano huo, mke wa Gwajima alipata nafasi ya kuongea yafuatayo:“Mimi ni Jasiri kama Simba, ukweli ninaufahamu, Mume wangu ninamfahamu na ninamuamini, na ukweli huo hakuna anayeweza kuubadilisha, niko pamoja na yeye, nitasimama na yeye na Mungu akiwa upande wetu hakuna atakayeweza kuwa juu yetu"

Msikilize hapo chini


Share:

BREAKING: Askofu Gwajima Aikana Video ya Ngono Inayosambazwa Mitandaoni......Kasema Sio Yeye, Imetengenezwa

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima leo Jumatano Mei 8, 2019 ameikana video ya ngono inayosambaa mitandaoni kwa kusema kuwa video hiyo imetengezwa kwa kuchukua sehemu ya mwili wake na mwili wa mtu mwingine.

Gwajima amesema mkono unaooneka katika video ile sio wa kwake, bali ni wa Baunsa lakini akakiri kuwa kifua kilichotumiwa ni picha yake ambayo aliipiga miaka 10 iliyopita akiwa na familia yake.

==>>Hapo chini ni nukuu ya baadhi ya maneno aliyosema


"Mimi nasema siwezi kufa hata kutekwa kilichotokea juu yangu ni mpango wa kunichafua tu, tutavishinda hivi vita mapema na kwa ukubwa.

"Ukiangalia ule mkono ni wa baunsa, sio mkono wangu mimi, hata kwa kutumia akili tu, ni nani arekodi video akiwa anajamiana halafu aisambaze yeye?

"Picha ya kifua wazi iliyotumika na kusambazwa ni picha ya familia niliyopiga nikiwa na mke wangu na watoto wangu. Na sio vibaya kupiga picha kifua ukiwa na familia. Na picha ile nilipiga zaidi ya miaka 10 iliyopita. 

"Nimetuma taarifa TCRA wamtafute huyo mtu aliyepost video zile na wakala wa huyo aliyetuma taarifa hizo yupo hapa kwenye mkutano huu. 

"Wataalamu walitaka kuja kuwaeleza namna video ile ilivyotengenezwa, nimekataa nikawaambia haina haja, huyo aliyetengeneza ameonyesha mimi ni mwanaume wa Kisukuma kamili, kuzaa naweza, nina watoto.

"Nafuatilia ni nani ambaye anatengeneza hizi video lakini ambaye anapost yupo hapa Tanzania ntaendelea kuwapa updates na ikifika Jumapili mtu huyu mwenye mkakati huu ovu asipojitokeza ntamuangukia jumla jumla.
 
"Rais alishahoji kuhusu kutekwa kwa MO Dewji lakini hadi leo hakuna kitu, sio Serikali inayohusika kwenye utekaji, bali kuna mtu mmoja mpumbavu au kikundi cha watu wanataka kuharibu taswira ya nchi.

"Hata kama video ile ilikuwa ni ya kweli, kutokana na kuwa aina ya video ile haipaswi kuonwa na kila mtu, basi unajua moja kwa moja kuwa nia ya huyo mtu si nzuri. Sasa mimi simpigi mtu aliyeko mbele, nilikaa kimya nimjue kwanza aliyeko nyuma, ili nimpige yeye
 
"Uchaguzi unakaribia mwaka 2020, sasa kuna watu wanahofu kwamba ninaweza kuwa na sauti nikawazidi hivyo wanajaribu kuniharibia. Niwaambie tu, ndio wananiongezea sauti, na wamethibitisha kuwa mimi ni mwanaume wa kweli. 

"Amewathibitishia watu kwamba Mimi ni Mwanaume kamili, kwamba kufanya tendo la ndoa naweza kufanya sawa sawa, kila Mwanaume anafanya tendo la ndoa, tofauti hufanyia chumbani.

"Mimi nilijua Vita imeisha kabisa sababu mnapomaliza ugomvi hakuna sababu ya mvutano kuendelea Kila mtu anatakiwa kuweka silaha zake chini iwe mundu iwe panga" Amesema Askofu Gwajima


Share:

LIVE: Askofu Gwajima Akizungumza Kuhusu Video Ya Faragha Inayodaiwa Kuwa Yake

LIVE: Askofu Gwajima Akizungumza Kuhusu Video Ya Faragha Inayodaiwa Kuwa Yake


Share:

Tahadhari ya Mvua kubwa Mwishon mwa Wiki hii

Mamlaka  ya Hali ya Hewa (TMA) imesema mvua kubwa zaidi inatarajiwa kunyesha mwishoni kwa wiki katika maeneo mbalimbali ya nchi na imewataka wananchi kuchukua tahadhari mapema.

Akizungumza na waandishi wa habari  Dar es Salaam jana, Meneja wa Utabiri, Samuel Mbuya alisema mvua hiyo ni mwendelezo wa mvua ya masika  inayoendelea kunyesha maeneo mbalimbali ya nchi baada ya kutonyesha mwezi uliopita kutokana na kuwapo  kimbunga Kenneth ambacho kilibadili hali ya hewa.

Alisema kutokana na hali hiyo, wananchi wanapaswa kuchukua tahadhari mapema huku wakiendelea kufuatilia taarifa za hali ya hewa   waweze kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza.

“Mwishoni mwa wiki hii tunatarajia kupata mvua kubwa zaidi katika maeneo mbalimbali ya nchi yanayopata mvua za masika, hivyo basi ni muhimu kwa wananchi kuchukua tahadhari mapema,”alisema Mbuya.

Mbuya alisema  juzi kituo cha kupima mvua cha Pemba kilionyesha kiasi cha mvua ni milimita 105.3 wakati jana iliongezeka na kufikia milimita 181.0.

Alisema  kituo cha kupima mvua kilichopo Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA), juzi kilipima kiasi cha mvua kuwa milimita 64.4 na jana iliongezeka hadi kufikia milimita 79.0, wakati Zanzibar ilionyesha 127.3.

Alisema kutokana na hali hiyo  mvua itakayonyesha mwishoni mwa wiki  inaweza kufikia kiwango hicho au kuongezeka zaidi hasa katika Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Tanga, Zanzibar na Pemba.

Alisema Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini na Mikoa ya Kanda ya Ziwa itaendelea kupata mvua ya masika kama kawaida, hivyo basi wakulima wanapaswa kufuatilia taarifa za hali ya hewa.


Share:

Gwajima Kuongea na Vyombo Vya Habari Leo Saa Tano..... Polisi Wamtaka Aripoti Polisi Sakata La Video Ya Ngono

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima leo Jumatano Mei 8, 2019 anatarajiwa kuzungumza na waandishi wa habari kanisani kwake Ubungo Jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku moja baada ya kuhusishwa na video ya ngono.

Taarifa hiyo imekuja kufuatia kusambaa kwa video ikimuonyesha mtu anayedhaniwa ni yeye akiwa faragha na mwanamke wakifanya mapenzi.

Jana baada ya kusambaa kwa video hiyo Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa alinukuliwa akisema tayari wameshamwita Gwajima kwa ajili ya kutoa maelezo kuhusu video hiyo.

“Tayari askofu Gwajima ameitwa polisi kwa ajili ya kuhojiwa na ataripoti kesho (leo) asubuhi , akichelewa atakamatwa na tumemuita sababu hakuna aliyelalamika lakini tumeona ni kitendo cha ukiukwaji wa maadili, awe askofu awe mtu wa kawaida ule ni unyama, “alisema Mambosasa


Share:

LIVE: Kutoka Moshi kwenye maandalizi ya safari ya mwisho ya Dkt Mengi.

LIVE: Kutoka Moshi kwenye maandalizi ya safari ya mwisho ya Dkt Mengi.


Share:

Marekani yapeleka manowari ya kijeshi mashariki ya kati

Marekani inapeleka kundi la manowari za kivita zinazobeba ndege za kivita katika eneo la mashariki ya kati kabla ya muda uliopangwa na kuonya kwamba Iran na jeshi lake zinaonesha hali ya mbaya ya kuongezeka kwa ishara za uwezekano wa shambulio dhidi ya majeshi ya Marekani katika eneo hilo.

Kile kinachosababisha hatua hiyo bado hakijajulikana, lakini kinaonesha hali ya kuongezeka kwa wasi wasi kati ya utawala wa rais Donald Trump na taifa hilo la Kiislamu. 

Mshauri wa usalama wa taifa John Bolton amesema Jumapili usiku kwamba Marekani inapeleka meli ya kivita ya USS Abraham Lincoln pamoja na kikosi cha mashambulizi kwenda katika eneo la mashariki ya kati, hatua inayokusudiwa kutoa ujumbe kwamba nguvu kubwa itatumika dhidi ya shambulio lolote dhidi ya vikosi vya jeshi la Marekani ama washirika wake. 

Bolton ameongeza kwamba Marekani haitafuti kupiga vita na utawala wa Iran, lakini majeshi ya nchi hiyo yamejitayarisha kujibu shambulio lolote.


Share:

Mkuu wa Upelelezi Ilala Afariki kwa Ajali

Mkuu wa upelelezi Mkoa wa Kipolisi Ilala, Aanael Mbise (50) na Frank Macha (35) mkazi wa Dar es Salaam ambaye ni fundi umeme wamefariki dunia na mmoja kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kugongana na gari jingine mkoani Kilimanjaro.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamisi Issah amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyotokea Jana eneo la Kiverenge Wilaya ya Mwanga.

Issah amesema ajali hiyo imehusisha gari aina ya Toyota Prado iliyokuwa ikitokea Same kuelekea Moshi na basi dogo la kampuni ya KVC iliyokuwa ikitokea Moshi kuelekea Same..

Amemtaja aliyejeruhiwa katika ajali hiyo kuwa ni Samson Macha (23) ambaye ni Mkazi wa Dar es salaam na amevunjika mguu wa kushoto na anaendelea kupatiwa matibabu Hospitali ya Wilaya ya Same akisaidiwa na ndugu yake Daniel Macha.



Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya May 8




Share:

Tuesday, 7 May 2019

JAMAA HOI HOSPITALI BAADA KUUMWA ULIMI NA MCHEPUKO WAKIPIGANA BUSU

Hali iliyotarajiwa kuwa ya furaha na mahaba tele kati ya wapenzi wawili huko Funyuka, Kaunti ya Busia nchini Kenya imegeuka na kuwa karaha baada ya mwanamke kumuuma mwenzake ulimi. 


Michael Otieno ambaye ni bawabu alinyemelea na kuingia katika nyumba ya Philister Akinyi Jumapili, Mei 5,2019 na hapo ndipo alipokutana na masaibu yake. 

Wapenzi wakipigana busu la ndimi. Mpango wa Kando'mchepuko' amemuuma mwenzake ulimi huko Busia.

 Inadaiwa na walioshuhudia kuwa, Otieno alikimbizwa hospitalini na majirani waliofika kumsaidia akilia kwa uchungu mwingi. 

Kulingana na naibu chifu wa Namuduru Josephat Sundya, wawili hao wamekuwa wapenzi kwa karibia miaka mitano sasa tangu kifo cha mume wa Akinyi. 

Katika siku za karibuni, mahaba kati ya wawili hao yamekuwa yakishuhudia migogoro ya mara kwa mara na inadaiwa bawabu huyo, 50, ameamua kuachana na mpenzi wake na kumrudia kikamilifu mke wake halali. 

 Akizungumza katika Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Busia alikokuwa amekimbizwa na majirani kupewa matibabu, Otieno alikana madai eti walikuwa wakifanya ngono wakati kisa hicho kilipotokea.

 Alimshutumu mwanamke huyo kwa kumshambulia alipomwomba asimdhuru mke wake halali. 
Chanzo- Tuko
Share:

LIVERPOOL YAIGONGA 4-0 BARCELONA NA KUTINGA FAINALI

Divock Origi (kulia) akishangilia na Xherdan Shaqiri (kushoto) baada ya kuifungia Liverpool bao la nne dakika ya 79 ikiilaza Barcelona 4-0 usiku huu Uwanja wa Anfield kwenye mchezo wa marudiano Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.


 Origi pia alifunga bao la kwanza dakika ya saba, wakati mabao mengine ya Liverpool yamefungwa na Georginio Wijnaldum dakika ya 54 na 56 na kwa matokeo hayo Wekundu hao wanakwenda fainali kwa ushindi wa jumla wa 4-3 baada ya kufungwa 3-0 kwenye mchezo wa kwanza Hispania 
Share:

MKUU WA UPELELEZI MKOA (RCO) MBISE AFARIKI KWA AJALI YA GARI


Watu wawili wamefariki dunia na mmoja kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kugongana na gari jingine mkoani Kilimanjaro.

Waliofariki ni Mkuu wa upelelezi Mkoa wa Kipolisi Ilala, Aanael Mbise (50) na Frank Macha (35) mkazi wa Dar es Salaam ambaye ni fundi umeme.

Akizungumza leo Jumanne Mei 7, 2019 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamisi Issah amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo leo eneo la Kiverenge Wilaya ya Mwanga.

Issah amesema ajali hiyo imehusisha gari aina ya Toyota Prado iliyokuwa ikitokea Same kuelekea Moshi na basi dogo la kampuni ya KVC iliyokuwa ikitokea Moshi kuelekea Same.

"Kwenye ajali hiyo wamefariki watu wawili waliokuwa kwenye Prado, mmoja ni ofisa wa polisi mwenye cheo cha Mrakibu mwandamizi wa jeshi la Polisi na mtu mmoja amejeruhiwa na mwingine ametoka mzima," amesema

Amemtaja aliyejeruhiwa katika ajali hiyo kuwa ni Samson Macha (23) ambaye ni Mkazi wa Dar es salaam na amevunjika mguu wa kushoto na anaendelea kupatiwa matibabu Hospitali ya Wilaya ya Same akisaidiwa na ndugu yake Daniel Macha.

Akielezea chanzo cha ajali hiyo Kamanda amesema,” Gari aina ya Toyota Prado ilihama upande wake na kuja kugongana upande na basi tunaendelea na uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo."


Awali akielezea ajali hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, Thomas Apson amesema ajali hiyo ilikuwa mbaya na bado wanaendelea na uchunguzi ili kuweza kujua chanzo chake.
Na Florah Temba, Mwananchi 

Share:

MAADHIMISHO YA REDCROSS KITAIFA KUFANYIKA KIGOMA KESHO

Na Editha Karlo,Kigoma
TANZANIA  Red Cross leo inaungana na Nchi 191 ulimwenguni katika maadhimisho ya  siku ya Red Cross Duniani  Mei 8, 2019 ambapo mwaka huu kitaifa yanafanyika Mkoani Kigoma katika Viwanja vya Mwanga community center.


 Akiongea na waandishi wa habari ofisa habari wa Red cross Tanzania Godfrida Jola amesema kuwa Mgeni rasmi katika madhimisho hayo kesho anatarajiwa kuwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce L. Ndalichako.

Alisema katika maadhimisho hayo Mgeni rasmi atazindua bweni la wanafunzi katika shule ya Bitale Maalum iliyopo Mkoani humo iliyojengwa kwa michango ya wanachama na wafanyakazi wote ili kuwasaidiawatoto wenye ulemavu watimize ndoto zao.

Kauli Mbiu ya mwaka huu kimataifa ni  " Upendo ". Ujumbe huu unamaanisha kwamba Red Cross inawafikia na kuwahudumia watu na jamii nyakati zote katika hali mbalimbali bila ubaguzi wa aina yoyote kwa  upendo.

Tanzania Red Cross Society  inafanya kazi kwa bidii na kutoa huduma za Kibinadamu   kwa kufuata Kanuni  zake saba za  Ubinadamu, Uadilifu,  Kutopendelea, Uhuru, kujitolea, Umoja, na Kushirikiana Kimataifa, hii inaifanya jamii kuiamini na kukisaidia kutimiza majukumu yake kwa ufanisi zaidi.

Jola alisema Red Cross imekuwa mstari wa mbele katika kutoa huduma wakati wa maafa na dharura mbalimbali ikiwemo mafuriko, njaa, tetemeko, ajali mbalimbali za nchi kavu na majini, kushiriki juhudi za kuboresha afya ya jamii na kuhamasisha upatikanaji damu salama, huduma kwa watu wanaoishi na maambukizi. Kwa miaka zaidi ya 20 imekuwa ikitoa huduma za kibinadamu kwa Wakimbizi, kwa sasa inatoa huduma za afya  kwa zaidi ya  wakimbizi 300,000 katika kambi za Nyarugusu (Wilaya ya Kasulu) na Mtendeli (Wilaya ya kakonko), pia inatoa huduma za kuwaunganganisha wana ndugu waliopoteana (Restoring Family Links).

Katika maadhimisho ya mwaka huu, kupitia matawi yake ya mikoa na wilaya Tanzania Red Cross imefanya shughuli za kijamii ikiwemo, kusafisha mazingira, kusaidia vikundi vilivyo katika mazingira hatarishi na kuhamasisha watu uchangiaji damu kwa hiari, michezo,  kambi ya vijana, kupanda miti na mafunzo kuhusu huduma za afya ikiwemo huduma ya kwanza.

Alisema pia Wilaya ya Kasulu, kwa kushirikiana na Halmashauri husika TRCS imejenga maabara za kisasa katika vituo vya afya vitatu kikiwemo cha Rusesa katika kata ya Rusesa, Nyenge (Kurugongo)na hospitali ya Kimwanya iliyopo katika Kata ya Nyachenda.

Pia katika Wilaya ya Buhigwe, Mkoani Kigoma TRCS kwa ushirikiano na Belgium Red Cross inaendelea kutekeleza mradi wa Maji na afya ya msingi kwa kuwasaidia wanachi kujenga vyoo vya kisasa na kujenga uzio katika vyanzo vya maji katika vijiji saba vya Buhigwe, Kavomo, Murela, Songambele, Bulimanyi, Nyamugali na Munyegera ambapo hadi sasa  familia 200 wamesaidiwa vifaa na kujenga vyoo vya kisasa.

"Tunaiomba jamii kuendelea kutoa huduma za kijamii kwa kufuata maadili ya kibaadam na kyifikia jamii popote ilipo na kila wakati"alisema
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger