Monday, 6 May 2019

ASKOFU SIMIYU AJIUA BAADA YA MKEWE KUMNYIMA CHAKULA CHA USIKU

Askofu Emmanuel Nyongesa Simiyu mwenye umri wa miaka 45 wa kanisa la Mwamba Faith by Works Ministry kutoka kijiji cha Lurambi eneo la Kiungani kaunti ya Trans Nzoia nchini Kenya ameripotiwa kujitoa uhai baada ya madai kuwa mkewe alimnyima chakula cha usiku.

Inaelezwa kuwa Askofu Nyongesa alifika nyumbani kwake Jumamosi Mei 4 kutoka ziarani akihisi njaa ila mkewe hakuwa amemwandalia chakula chochote 

 Imeripotiwa kuwa Nyongesa alirejea nyumbani Jumamosi Mei 4, akihisi njaa na akiwa mchovu, alimuuliza mkewe ampatie chakula ila hakikuwepo. 

Mkewe alidai kuwa hakumuachia pesa za kununua chakula na hivyo asingeweza kumuandalia chochote.

 Akiwa mwenye hasira, Nyongesa alienda chumbani kulala bila kula chochote ila alitishia kufanya kitendo kitakachomtikisa mkewe pamoja na waumini wake.

 "Umekataa kuniandalia chakula? utajionea maajabu, nitafanya kitendo cha kusikitisha sana ambacho kitakutisa pamoja na waumini wangu," Askofu Nyongesa alisema.

Jumapili Mei 5, askofu aliripotiwa kwenda jikoni akijifanya kuwa yuwapika kiamsha kinywa na hivyo ndivyo alijiua. Mwanawe aliupata mwili wake ukining'inia kwenye paa la nyumba.
Chanzo - Tuko
Share:

LIPULI FC YAICHARAZA YANGA 2 - 0


Timu ya Lipuli FC ya Iringa imefanikiwa kuingia fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya vigogo, Yanga SC Uwanja wa Samora mjini Iringa.

Sasa Lipuli FC itamenyana na Azam FC katika mchezo wa fainali ya michuano hiyo itakayofanyika Uwanja wa Ilulu mjini Lindi mapema mwezi ujao. 

Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Shomary Lawi wa Kigoma, mabao ya Lipuli FC yalifungwa na mshambuliaji wa zamani wa Yanga SC, Paul Nonga dakika ya 27 na Daruwesh Saliboko dakika ya 38.

Wazi Yanga haitashiriki michuano ya Afrika mwakani baada ya kipigo cha leo, kwani kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara ubingwa umekaa vizuri zaidi kwa watani waol Simba SC.

Na kipigo hiki kinakuja siku moja baada ya kuchaguliwa kwa uongozi mpya wa klabu chini ya Mwenyekiti, Dk. Mshindo Mbette Msolla, Makamu Mwenyekiti Frederick Mwakalebela na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji Hamad Islam 1,206, Mhandisi Bahati Faison Mwaseba 1,174, Dominick Ikute, Kamugisha Kalokola, Arafat Haji, Salum Ruvila, Saad Khimji na Rodgers Gumbo.
Uchaguzi huu umefuatia kujiuzulu kwa viongozi wote waliongia madarakani Juni 11 mwaka 2016, Mwenyekiti Yussuf Manji, Makamu Mwenyekiti, Clement Sanga na wajumbe wao, Siza Augustino Lymo, Tobias Lingalangala, Samuel Lukumay, Hussein Nyika, Omary Said Amir, Salum Mkemi, Ayoub Nyenzi na Inspekta Hashim Abdallah.

Kikosi cha Lipuli FC kilikuwa; Yusuph Mohammed, Haruna Shamte, Paul Ngalema, William Lucian ‘Gallas’, Ally Sonso, Freddy Tangalu, Miraj Athumani ‘Madenge’/Novaty Lufunga dk81. Jimmy Shoji, Paul Nonga, Dariwesh Saliboko na Zawadi Mauya/Steven Maganga dk89.

Yanga SC; Klaus Kindoki, Paul Godfrey, Mwinyi Hajji Mngwali, Abdalla Shaibu ‘Ninja’, Andrew Vincent ‘Dante’, Feisal Salum, Mrisho Ngassa, Mohammed Issa ‘Banka’/Amissi Tambwe dk47, Heritier Makambo, Papy Kabamba Tshishimbi na Ibrahim Ajibu/Juma Abdul dk60.
Chanzo -Binzubeiry blog
Share:

Serikali Yataja Sababu za mradi wa makaa ya mawe wa Mchuchuma na Liganga kutachelewa kuanza

Serikali imesema mradi wa makaa ya mawe wa Mchuchuma na Liganga utachelewa kuanza kutokana na mazungumzo na mwekezaji kuchukua muda mrefu tofauti na ilivyotegemewa.

Hayo yamebainika baada ya swali la Mbunge wa Ludewa, Francis Ngalawa (CCM), ambaye alitaka kujua lini Serikali italipa fidia kwa wananchi walioachia maeneo yao kupisha mradi huo.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Stella Manyanya ameliambia Bunge leo Jumatatu Mei 6, kuwa kazi ya uthaminishaji mali kwa wananchi lilikamilika tangu Agosti mwaka 2015 lakini ulipaji fidia haukuweza kufanywa.

“Serikali ilifanya uthaminishaji mwingine Desemba mwaka jana na kubainisha malipo stahiki yanayopaswa kulipwa pindi taratibu za msingi za maandalizi zikikamilishwa na Serikali,” amesema Manyanya.


Share:

Hakimu Wa Mahakama Wilaya Na Mawakili Wa Serikali Kizimbani Arusha

Na Ahmed Mahmoud Arusha
Hakimu wa mahakama ya wilaya mkoani Arusha Benard Nganga,na wenzake wanne wakiwemo mawakili wa serikali wamepandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka kumi na moja yakiwemo ya uhujumu wa uchumi na utakatishaji wa fedha.

Akisoma mashtaka hayo mbele ya Hakimu mfawidhi Niku Mwakatobe wa mahakama ya hakimu mkazi Arusha Mwendesha mashtaka wa serikali Javelin Rugailuza amewataja washtakiwa wengine ni Maneno Mbunda wakili wa shirika la hifadhi za Taifa (Tanapa),Fortunatus Mhalila na Tumaini Mdee wote ni mawakili wa serikali na mfanyabiashara Nelson Kangero.

Mwendesha mashtaka huyo ameeleza kuwa kati ya tarehe 1 mwezi wa sita mwaka 2018 katika maeneo tofauti jijini Arusha na mkoani Arusha washtakiwa kwa pamoja walitenda makosa mbali mbali ya uhujumu wa uchumi na kujipatia rushwa na uundwaji wa genge la mtandao wa uhalifu.

Makosa mengine wanayokabiliana nayo ni pamoja na kutoa na kupokea rushwa ya million 31.5 kwa lengo la kushawishi wa kuwezesha kuwachiwa huru kwa mhalifu na ,kuhuaribu ushahidi, na kuchoma jalada la kesi,pamoja na kuwasilisha nyaraka za uongo.

Baada ya mwendesha mashtaka huyo kuwasomea mashataka hayo hawakutakiwa kujibu chochote kwani mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo hivyo kuahirishwa hadi tarehe 20 mwezi huu.

Wakati huo huo Mshatakiwa Nelson Kangero alisomewa shatka mmoja la kukutwa na meno 15 ya Tembo ambayo ni nyara za serikali zenye thamani ya million 100.8 kinyume cha sheria.

Akisoma shtaka hilo mbele ya hakimu mfawidhi Mwakatobe Mwendesha mashtaka wa serikali Javelin Rugailuza alisema kuwa mnamo disemba 15 mwaka 2017 katika eneo la kichwa cha nyumbu Wilayani Mwanga Mkoani Kilimanjaro mtuhumiwa alikutwa na Meno ya tembo yenye thamani ya dola za Kimarekani 15000 mali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Mshtakiwa hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo hivyo kupelekwa rumande hadi mei 20 mwaka huu kesi itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.

Wakati huo huo Mkurugenzi wa Makosa ya jinai wa Jeshi la Polisi (DCI)Robert Boaz amesema kuwa hali ya uhalifu nchini imepungua kwa asilimia 3.4 ukilinganisha na makosa kama hayo mwaka jana ambayo yalikuwa 14,866 na robo mwaka huu ni 14,355.

Akizungumzia makosa makubwa yakiwemo ya Unyang’anyi wa kutumia silaha na Ujangili Boaz alisema yamepungua kwa asilimia 4.7 ambapo mwaka jana yalikuwa 6897 na mwaka huu ni makosa 6573,hatua hiyo imetokana na Jeshi hilo kuunda timu ya kufuatilia uhalifu na kufanikisha mbaroni wa husika na vifaa vyao vya kazi.


Share:

Picha : RAIS WA SHIRIKISHO LA BARAZA LA TAIFA LA FALME ZA KIARABU (UAE) AFUNGUA MKUTANO WA PILI WA BUNGE LA AFRIKA

Rais wa Shirikisho la Baraza la Taifa la Falme za Kiarabu (United Arab Emirates – UAE),Dr. Amal Abdullah Al Qubaisi akifungua bunge la Afrika leo nchini Afrika Kusini - Picha na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Rais wa Shirikisho la Baraza la Taifa la Falme za Kiarabu (United Arab Emirates – UAE),Dr. Amal Abdullah Al Qubaisi amefungua Mkutano wa pili wa kawaida wa Bunge la Afrika ulioanza leo Mei 6,2019 jijini Johannesburg,Afrika Kusini kwa kukutanisha wabunge kutoka nchi 54 barani Afrika.

Akitoa hotuba yake, Dr. Amal Abdullah Al Qubaisi amesema Bunge la Nchi za Falme za Kiarabu (United Arab Emirates- UAE) zimekubaliana kushirikiana na Bunge la Afrika katika kumaliza changamoto zinazowakabili wananchi barani Afrika.

“Uhusiano wa Umoja wa Falme za Kiarabu na Bara la Afrika umekuwa mkubwa,tumekuwa tukisaidia mambo kadha wa kadha barani Afrika,tunataka kuona usalama unazidi kuimarika Afrika,kwani bila usalama katika nchi zetu hakuna maendeleo yanayoweza kufikiwa”,alisema Dr. Amal.

“Masuala ya vitendo vya kigaidi yana athari kubwa,tunatakiwa kwa pamoja kushirikiana kuyatafutia ufumbuzi ili wananchi wetu wawe salama lakini pia kuwa na suluhisho la kudumu juu ya wakimbizi wanaorejea nyumbani na wakimbizi wa ndani,tunafurahi kuona wakimbizi wakirudi kwenye nchi zao kwa amani”,alisema.

Kwa upande wake,Rais wa Bunge la Afrika,Mhe. Roger Nkodo Dang alisema ili ushirikiano na umoja madhubuti unahitajika ili kufikia suluhu za kudumu juu ya masuala ya amani na usalama barani Afrika.

Ufunguzi wa Mkutano wa pili wa kawaida wa Bunge la Afrika umekwenda sanjari na wabunge 26 wapya wa bunge la Afrika kutoka nchi mbalimbali kula kiapo.

Kauli mbiu ya Bunge la Afrika mwaka huu ni “2019 mwaka wa Wakimbizi,wanaorejea nyumbani na wakimbizi wa ndani : Kuelekea kupata masuluhisho ya kudumu katika kulazimishwa kuhama makazi katika Afrika.

Mwandishi wetu,Kadama Malunde ametuletea picha za matukio mbalimbali yaliyojiri wakati wa Bunge la Afrika likifunguliwa leo..Tazama hapa chini
Rais wa Shirikisho la Baraza la Taifa la Falme za Kiarabu (United Arab Emirates – UAE),Dr. Amal Abdullah Al Qubaisi akitoa hotuba yake wakati akifungua Mkutano wa pili wa kawaida wa Bunge la Afrika leo Mei 6,2019 Midrand, jijini Johannesburg,Afrika Kusini. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Rais wa Bunge la Afrika,Mhe. Roger Nkodo Dang akitoa hotuba yake Mkutano wa pili wa kawaida wa Bunge la Afrika leo Mei 6,2019.
Rais wa Shirikisho la Baraza la Taifa la Falme za Kiarabu (United Arab Emirates – UAE),Dr. Amal Abdullah Al Qubaisi (katikati),Rais wa Bunge la Afrika,Mhe. Roger Nkodo Dang na washiriki wa Mkutano wa pili wa kawaida wa Bunge la Afrika wakiwa wamesimama kuimba wimbo  wa Umoja wa Afrika.
Wabunge wa Bunge la Afrika wakiwa wakiimba wimbo  wa Umoja wa Afrika.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mhe. Stephen Masele (kulia) na viongozi mbalimbali wa bunge la Afrika wakiwa katika ukumbi wa bunge la Afrika leo Jijini Johannesburg.
Wabunge wa Bunge la Afrika wakiwa ukumbini.
Bunge linaendelea.
Wabunge wakiwa ukumbini.
Aliyekuwa Mjumbe wa Uongozi wa Bunge la Afrika Dr. Bernadette Lahai kutoka Sierra Leone akitoa tamko na ujumbe wa mshikamano barani Afrika.
Wabunge wakiwa ukumbini.
Wabunge wakiwa bungeni.
Wabunge wapya wa bunge la Afrika kutoka Swaziland wakila kiapo bungeni leo. Hao ni miongoni mwa wabunge 26 kutoka nchi mbalimbali walioapishwa leo.
Wabunge wapya wa bunge la Afrika wakiendelea kiapo
Zoezi la kula kiapo likiendelea
Wabunge wakiwa ukumbini.

Wageni mbalimbali wakiwa ukumbini.
Wageni mbalimbali wakiwa ukumbini.
Picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa Mkutano wa pili wa kawaida wa Bunge la Afrika.
Rais wa Shirikisho la Baraza la Taifa la Falme za Kiarabu (United Arab Emirates – UAE),Dr. Amal Abdullah Al Qubaisi (wa nne kulia) akiondoka katika bunge la Afrika,Johannesburg,Afrika Kusini baada ya kufungua Mkutano wa pili wa kawaida wa Bunge la Afrika ulioanza leo Mei 6,2019.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Share:

Waziri Mkuu Aupongeza Uongozi Wa Benki Ya DCB.....Autaka Uimarishe Kitengo Cha Elimu Kwa Umma

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameupongeza uongozi benki ya DCB kwa kufanikiwa kubadili muundo kutoka benki ya jamii na kuwa ya biashara.

“Benki nyingi za jamii zimekufa baada ya kushidwa kujiendesha lakini ninyi DCB mmeweza kumudu kujiendesha hadi kufikia kuwa benki ya biashara.”

Hata hivyo, Waziri Mkuu ameutaka uongozi wa benki hiyo uimarishe kitengo cha elimu kwa umma ili jamii ifahamu huduma wanazozitoa.

“Nendeni kwa wananchi mkawape elimu juu ya umuhimu wa kufungua akaunti na pia rahisisheni mazingira ya kutolea huduma kwa wateja.”

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatatu, Mei 6, 2019) alipokutana na uongozi wa benki hiyo ofisini kwake Bungeni jijini Dodoma.

Kadhalika, Waziri Mkuu ameitaka benki hiyo isogeze huduma kwa wananchi hususan maeneo ya pembezoni ambayo bado hayajafikiwa.

Amesema ni muhimu wananchi wakasogezewa huduma za kibenki ili waweze kuhakikishiwa usalama wao pamoja na fedha zao.

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya DCB, Bw. Godfrey Ndalahwa alisema tangu benki hiyo ianzishwe imefanikiwa kukuza amana za wateja kutoka sh. bilioni mbili mwaka 2002 hadi sh. bilioni 75 Desemba mwaka jana.

“Pia mikopo imeongezeka kutoka sh. bilioni moja mwaka 2002 na kufikia sh. bilioni 90, Desemba 2018, faida ikiwa ni sh. bilioni 17.7 baada ya kodi.”

Mkurugenzi huyo alisema katika kipindi cha miaka 16 ya utendaji wake, benki hiyo imeshatoa gawio la zaidi ya sh. bilioni 11 kwa wanachama wake.

Pia, Mkurugenzi huyo alitumia fursa hiyo kuipongeza Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli kwa kuboresha maendeleo.

Alisema katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wake, wameona mabadiliko makubwa katika sekta mbalimbali nchini.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,


Share:

Picha: Jeneza lenye mwili wa marehemu Dr. Reginald Mengi likiingizwa kwenye gari tayari kwa safari ya kuelekea Hospitali ya Lugalo.




Share:

Kaburi la Dr Reginald Mengi Laendelea Kuandaliwa


Uchimbaji kaburi atakalozikwa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni za IPP, Reginald Mengi umeanza leo asubuhi Jumatatu Mei 6, 2019 nyumbani kwake Kijiji cha Nkuu Sinde Machame Mashariki, mkoani Kilimanjaro, eneo ambalo walizikwa wazazi wake na mwanae, Roodney Mengi aliyefariki mwaka 2005.

Mfanyabiashara huyo maarufu ndani na nje ya Tanzania alifariki dunia usiku wa kuamkia Alhamisi   Mei 2, 2019 akiwa Dubai, Falme za Kairabu alikokuwa akipatiwa matibabu.

Mwili wa Mengi umewasili  leo Jumatatu saa 9:00 alasiri katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam (JNIA), kisha utapitishwa barabara mbalimbali hadi Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo.

Kesho mwili huo utaagwa katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, baadaye utapelekwa nyumbani kwake Kinondoni utakapolala hadi Jumatato asubuhi utakaposafirishwa kwenda Machame kwa mazishi yatakayofanyika Alhamisi hii  Mei 9, 2019.



Share:

Rais Magufuli Akutana Na Mkurugenzi Wa Idara Ya Afrika Wa Imf Ikulu Jijini Dar Es Salaam Leo




Share:

Serikali yasema ni ngumu kulipa fidia kwa walioathiriwa na wanyamapori

Waziri wa Maliasili na utalii amesema ni ngumu kwa serikali kuahidi kutekeleza ulipaji wa fidia kwa wananchi ambao wataathiriwa na wanyama pori au mazao yao, lakini inachoweza kulipa ni kifuta machozi.

==>>Msikilize hapo chini


Share:

Serikali yataifisha magari 6 ya wakili Median Mwale

Mkurugenzi wa Mashitaka (DDP), Biswago Mganga amesema serikali imetaifisha rasmi mali za Wakili maarufu jijini Arusha, Median Mwale zenye thamani ya Sh bilioni 1.2 kutokana na makosa ya kutakatisha fedha haramu.

Mganga amesema, mali hizo zilizotokana na zao la utakatishaji fedha haramu baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, kumtia hatiani na kuamuru mali hizo zitaifishwe na serikali.

Akizungumzia na waandishi wa habari jana mjini Arusha wakati wa makabidhiano kati ya ofisi ya DPP na Hazina, Mganga alitaja mali hizo kuwa ni magari sita ya kifahari yanayoshikiliwa Kituo Kikuu cha Polisi Arusha.

Mali zingine zilizotaifishwa ni nyumba mbili ikiwemo iliyopo Plot Namba 261 Block C Njiro na nyumba nyingine iliyopo Plot Namba 22 iliyopo eneo la Ilikyurei ambayo ilikuwa mali ya Wakili Loomo Ojale na shamba moja la ekari 10 lililopo eneo la Ngaramtoni.

Alisema hatua hiyo imekuja kufuatia Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, kutaifisha mali hizo na kwamba Aprili 14,2019 mahakama hiyo ilitoa kibali cha kuzitaifisha rasmi na kuwa mali ya serikali.

“Kwa mujibu wa sheria mali zinapotaifishwa kuwa mali ya serikali zinakuwa chini ya Katibu Mkuu Hazina” alisema.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Mali za Serikali Hazina, Benezeth Rutta alisema kuwa Mali hizo baada ya kukabidhiwa kutoka kwa DPP zinakuwa chini ya uangalizi wa Wizara ya Fedha na zinapangiwa matumizi kadri serikali itakavyoona inafaa.

“Mali hizi baada ya kukabidhiwa serikalini zitapangiwa matumizi kadri serikali itakavyoona inafaa na kama itaonekana mali hizo hazifai kwa matumizi ya serikali zitauzwa kwa mnada” alisema Rutta.

Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Selemani Nyakulinga amesema mwaka 2011 alipata taarifa kutoka kitengo cha udhibiti wa fedha haramu kuwa kuna watu waligushi na kutaka kuiba fedha dola za Marekani milioni 17.2.

Alisema fedha hizo zilikuwa zinaibwa kutoka mfuko wa Global Fund kwa ajili ya kusaidia kutibu Ukimwi nchini Tanzania zikitoka Hazina ya nchi ya Marekani.

Amesema walibaini kuwa waliohusika na wizi huo ni raia wa Kenya, wakishirikiana na Watanzania akiwemo Wakili Mwale

Alisema baada ya kufuatilia walifanikiwa kuwatia mbaroni wahusika wote na baadae mahakama ilibaini kuwa wahusika walishanunua mali mbalimbali, zilizotokana na zao la utakatishaji wa fedha hizo na mahakama kuridhia na kutaifisha mali hizo kuwa za serikali.

Credit: Habarileo


Share:

Masauni: Hakuna ushahidi wa ajali iliyosababishwa na trafiki kuvizia barabarani

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amesema hakuna ushahidi wowote unaoonesha kuwa kumetokea ajali iliyosababishwa na askari wa usalama barabarani 'kujificha' wakiwa barabarani.

==>>Msikilize hapo chini


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger