Sunday, 5 May 2019

Basi la Kilimanjaro Express lapinduka mkoani Tanga

Basi la abiria la Kampuni ya Kilimanjaro Express limepata ajali eneo la Mkata, mkoani Tanga leo Jumapili Mei 5, 2019.

Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Tanga (RTO), Solomon Mwangamilo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kubainisha kuwa basi hilo limepinduka.

“Ni kweli kuna basi la Kilimanjaro Express limeacha njia na kupinduka eneo la Mkata, kwa sasa ndio naelekea eneo la tukio.

“Hatujafahamu hasa ni madhara gani yaliyotokea huko mpaka nikifika huko mwendo wa dakika 45 hivi nitawafahamisha hali halisi,” amesema Mwangamilo.


Share:

Soko la Pili la madini lafunguliwa Mkoani Shinyanga huku Gramu elfu 30 za dhahabu zikiwa zimeshauzwa

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack amefungua soko la madini Ijumaa tarehe 03 Mei, 2019 katika Wilaya ya Shinyanga likiwa ni soko la pili baada ya soko jingine kufunguliwa Wilayani Kahama mwezi mmoja uliopita.
 
Akitoa hotuba ya ufunguzi wa soko hilo katika eneo la Ofisi ya CCM Mkoa ambapo wafanyabiashara tisa (9) wa Dhahabu na Almasi wamefungua masoko yao hapo, Mhe. Telack amesema tangu agizo la Mhe. Dkt. John Magufuli la kufungua masoko ya madini, tayari madini ya dhahabu yenye gramu 30,924.44 yameshauzwa katika soko la Kahama yakiwa na thamani ya sh. Bilioni 2.9.
 
Telack amewashukuru wafanyabiashara hao kwa kuitika wito wa Serikali na kufungua soko katika Mkoa wa Shinyanga.
 
Aidha, ametoa wito kwa wachimbaji wadogo, wauzaji na wanunuzi kutumia soko hilo la madini na waache kuuziana madini sehemu zisizo rasmi na atakayekamatwa anafanya hivyo madini yatataifishwa na wahusika watashtakiwa kwa mujibu wa sheria.
 
Kaimu Afisa Madini Mkazi Mhandisi Giliard Luyoka, akisoma taarifa ya madini Mkoa, amesema hadi sasa Mkoa una wafanyabiashara wakubwa 9 na wadogo 22 na kuwa licha ya Mkoa kuwa na utajiri wa madini yenye thamani ambapo wachimbaji wadogo wanazalisha wastani wa kilo 600 za dhahabu na karati 1300 za almasi kwa mwaka, hakukuwa na masoko rasmi ya uuzaji wa madini hivyo kupelekea utoroshwaji wa madini hatimaye Taifa kutonufaika na madini hayo.
 
Naye mwenyekiti wa Chama cha Wachimba madini Mkoa wa Shinyanga Bw.Hamza Tandiko amesema kuwa, wanaunga mkono juhudi za Serikali katika kuhakikisha madini yote yanayopatikana Mkoani Shinyanga yanawasaidia wananchi wa Mkoa huu kwa kuchangia pato la Taifa.
 
“Tuendelee kumuunga mkono Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, kufikia mwaka 2025 angalau sisi tuliopo kwenye sekta ya madini tuweze kuchangia angalau asilimia 10 ya pato la Taifa kwani Serikali imeonesha uzalendo kwa kufuta kodi hivyo deni limebaki kwetu” amesema Hamza.


Share:

UTEUZI MPYA ULIOFANYWA NA WAZIRI WA MAJI PROF. MAKAME MBARAWA



Share:

STEPHEN MASELE: “MZEE REGINALD MENGI NI SHUJAA NA MWANAMAPINDUZI WA KIUCHUMI”




Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika Mheshimiwa Stephen Masele.

Na Kadama Malunde – Johannesburg,Afrika Kusini.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika Mheshimiwa Stephen Masele amesema Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP marehemu Dr. Reginald Mengi ni Shujaa na Mwanamapinduzi wa kiuchumi na anastahili kupewa heshima ya kuwa Nembo ya Uwekezaji na Sekta binafsi Tanzania. 

Mhe. Masele ambaye ni mbunge wa Shinyanga Mjini na Naibu Waziri wa Nishati na Madini wa zamani nchini Tanzania amesema hayo leo Jumapili Mei 5,2019 akiwa nchini Afrika Kusini,wakati akitoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Dr. Reginald Mengi, aliyefariki dunia Mei 2, 2019 huko Dubai. 

“Mzee Mengi ninamtambua kama Mwanamapinduzi wa Kiuchumi kwa sababu ndiye Nembo ya Uwekezaji kwa Wazalendo na ndiyo Nembo ya Sekta Binafsi katika nchi yetu”,ameeleza Masele. 

“Mzee Mengi atakumbukwa zaidi kuwa miongoni kwa Watanzania wa mwanzo kuwekeza nchini na nitafurahi zaidi akipewa heshima ya kwamba yeye ndiye Nembo ya Uwekezaji,Nembo ya Sekta binafsi katika taifa letu”,amesema Masele. 

Masele amemwelezea Mzee Mengi, kuwa alikuwa mtu mnyenyekevu,asiye na majivuno, mwenye kuheshimu watu wote bila kujali nafasi yake katika jamii licha ya kuwa na uwezo wake kifedha aliojaliwa na Mwenyezi Mungu. 

“Nadhani ni vizuri kwa sisi vijana hususani viongozi kujifunza kwamba pamoja na nafasi tulizonazo ni vyema kuwa wanyenyekevu kwa binadamu wenzetu,mbele ya Mungu lakini pia kuheshimiana bila kujali nafasi zetu katika jamii”,ameongeza Masele. 

Masele amewapa pole familia ya Mzee Mengi, marafiki,wafanyakazi wote wa Makampuni aliyokuwa anayaongoza na Watanzania wote kwa ujumla ikiwemo sekta binafsi. 

“Kwa kweli nimepokea taarifa za msiba huu kwa huzuni kubwa,nimehuzunika kuondokewa Mzee wetu nilifanya nae kazi wakati nikiwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini na yeye akiwa kiongozi wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania,tulifanya kazi kwa ukaribu sana,tulikuwa na vikao mbalimbali kuhusu masuala ya Uwekezaji.. tumuombe Mwenyezi Mungu ampe pumziko la amani Mzee wetu ,Amin”,ameongeza Masele.

Mheshimiwa Masele yupo Nchini Afrika Kusini kuhudhuria Kikao cha Pili cha Kawaida cha Bunge la Tano la Afrika kitakachoanza siku ya Jumatatu Mei 6, 2019 Jijini Johannesburg Afrika Kusini. 

Mgeni rasmi atakayefungua kikao hicho cha Bunge la Afrika ni Spika wa Nchi za Falme za Kiarabu (UAE), Dk. Amal Abdulla Al Qubaisi ambaye tayari ameshawasili nchini Afrika Kusini.


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika Mheshimiwa Stephen Masele akiwa ofisini kwake,zilizopo Makao Makuu ya Bunge la Afrika, Jijini Johannesburg,Afrika Kusini akitoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Dr. Reginald Mengi. Picha na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Share:

UDOM: FIRST ANNUAL BUSINESS PLAN COMPETITION, MAY 2019

Share:

WIZARA YA ELIMU: STUDY OPPORTUNITY OFFERED BY THE ORGANIZATION FOR WOMEN IN SCIENCE FOR THE DEVELOPING WORLD (OWSD-EARLY CAREER FELLOWSHIP) 2019/2020

Call for Application

The General Public is hereby informed that, Organization for Women in Science for the Developing World (OWSD)

has offered scholarships opportunity to Tanzanian women. The OWSD Early Career fellowship is a prestigious award of up to USD 50,000 offered to women who have completed their PhDs in Science, Technology, Engineering and Mathematics (STEM) subjects and are employed at an academic or scientific research institution in one of the listed Science and Technology Lagging Countries (STLCs). The OWSD Early Career fellows will be supported to establish an environment at their institution where they can maintain an international standard of research and attract scholars from all over the world to collaborate.Mode of Application

All details regardingPurposeFellowship supportEligibilityResearch projectRequired documentsEvaluationSelectionDownloads and how to apply are available at: https://owsd.net/career-development/early-career-women-scientists-ecws-fellowships

Note: The official language for the application is English; however, all information about the programme is also available in French at: https://bit.ly/2IKPfRZ.

Submission

Online application must be submitted not later than 30th April, 2019.

Issued by:
Permanent Secretary,
Ministry of Education, Science and Technology,
University of Dodoma,
College of Business and Law,
Block 10,
P .O. Box 10,
40479 DODOMA.

The post WIZARA YA ELIMU: STUDY OPPORTUNITY OFFERED BY THE ORGANIZATION FOR WOMEN IN SCIENCE FOR THE DEVELOPING WORLD (OWSD-EARLY CAREER FELLOWSHIP) 2019/2020 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Masauni Ayataka Madhehebu Ya Dini Kote Nchini Kuendelea Kutii Sheria Za Nchi Ili Kulinda Amani Ya Tanzania.

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Mhandisi  Hamad Masauni ametoa wito kwa viongozi   wa madhehebu ya dini  hapa nchini kuendelea kutiii sheria za nchi ili kuitunza amani ya Tanzania na kutojihusisha na Masuala ya Siasa. 

Mhandisi Masauni ametoa wito huo  Mei 4 ,2019  jijini Dodoma  wakati akifungua mkutano mkuu wa Dodoma Net Event unaoratibiwa na Kanisa la waadventista Wasabato na ukitarajiwa kuhitimishwa Mei 25 mwaka huu. 

Mhandisi Masauni amesema serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua mchango mkubwa unaofanywa na kanisa la waadventista Wasabato hivyo amelipongeza kwa kuwa na mchango mkubwa  kwa jamii katika kutoa masomo ya Afya,ujasiriamali,Kaya na Familia pamoja na kuwafundisha waumini wake kutii     Mamlaka za serikali hali ambayo inaendeleza kustawisha amani ya hapa nchini. 

Aidha Mhandisi Masauni ameyaasa madhehebu ya dini  Mengine hapa nchini kuiga mfano wa kanisa hilo kwa kuimarisha vijana   katika mazoezi na kuwafundisha uzalendo wa nchi yao      na akatoa mfano wa chama cha vijana watafuta njia wa kanisa hilo[Pathfinder]. 

Pia Mhandisi Masauni ametoa wito kwa madhehebu ya dini hapa nchini kushirikiana na serikali katika masuala ya kishirikina kwani yamekuwa yakisababisha kuawa watu wasiokuwa na hatia wakiwemo Watu wenye ualbino na vikongwe . 

Sanjari na hayo Mhandisi Masauni ametoa onyo kwa  baadhi ya vijana wanaotumia mitandao ya kijamii kukashfu na kutukana imani za watu wengine kwani inaweza kuhatarisha usalama wa Taifa huku akibainisha kuwa serikali itaendelea kuenzi na kuruhusu uhuru wa dini. 

Vilevile  Mhandisi Masauni amewaasa waumini wa kanisa la Waadventista Wasabato na watu wa Madhehebu mengine kuchangamkia Fursa zilizopo katika jiji la Dodoma kwa kuwekeza katika sekta za elimu,Afya  baada ya kurasmishwa kuwa Makao Makuu ya nchi. 

Akitoa neno  la shukrani ,mwenyekiti wa Union ya kaskazini mwa Tanzania kanisa la  Waadventista Wasabato ,Mch.Godwin Lekundayo ameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kusisitiza uhuru wa Dini  kwani ndio msingi wa Amani huku akiiomba serikali kuingilia kati kwa baadhi ya taasisi hasa za shule kuwanyima uhuru wa kuabudu wanafunzi wake na kuwalazimisha kufanya mitihani siku za ibaada [Sabato]. 

Aidha Mch.Lekundayo ameishukuru serikali kwa kuendelea kupinga kuchanganya masuala ya siasa na  dini kwani yanaweza kuhatarisha amani ya nchi. 

Neno kuu la mkutano wa injili wa Dodoma Net Event ni Uzoefu wa Nguvu ya Mungu na mtoa neno ni .Mch.Baraka Muganda Mtanzania aishie nchini Marekani.
MWISHO.


Share:

Dhana Ya Afya Moja Kutumika Kudhibiti Magonjwa Ambukizi Maeneo Ya Mipakani

Dhana ya Afya moja ambayo hujikita katika kujumuisha sekta zote za Afya katika kujiandaa, kufuatilia  na kukabili magonjwa yanayomuathiri binadamu imeendelea kufundishwa kwa Wataalamu wa sekta hizo za Afya, ikiwa ni Sekta ya Afya  ya Binadamu, Wanyamapori, Mifugo, Kilimo na Mazingira, ili wataalamu hao watumie dhana hiyo kuimarisha udhibiti wa magonjwa ambukizi kati ya Binadamu na wanyama  ambayo hutokea mara kwa mara katika maeneo ya mipakani kutokana na kuwepo kwa  mwingiliano mkubwa kati ya  watu na wanyama katika mazingira yao.

Pamoja na Mwingiliano huo wenye faida kubwa kiuchumi lakini pia unasababisha kuenea kwa vimelea   kwa uharaka zaidi na kusababisha magonjwa kwa binadamu, wanyama na mimea katika mazingira yao, hivyo ili kuimarisha Afya ya binadamu, Shirika la Chakula na Kilimo  la Umoja wa Mataifa (FAO), pamoja  na watalaamu kutoka Wizara ya Mifugo na  Uvuvi, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine wamewapa mafunzo wataalamu wa sekta za Afya wanao toka katika Halmashauri za Mkoa wa Mbeya na Songwe zilizo mipakani juu ya namna ya kujiandaa na kukabili magonjwa ambukizi kama  vile Ugonjwa wa Kimeta kwa kutumia Dhana ya Afya  moja.

Akiongea wakati wa kufunga mafunzo hayo yaliyofanyika kuanzia tarehe 29 Aprili hadi,tarehe 3 Mei, 2019, Mkoani Songwe, Mkurugenzi wa Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe, ambaye aliwakilishwa na Mratibu Kitaifa, Dawati la Kuratibu Afya Moja, Ofisi ya Waziri Mkuu, Harrison Chinyuka,  alibainisha kuwa ushirikiano wa wataalam na sekta za Afya  kwa kutumia dhana ya Afya Moja hivi sasa ni agenda ya dunia nzima. Aidha, alieleza kuwa Dhana hiyo imekusudiwa kutumika maeneo ya mipakani   ambapo mwingiliano huo huchochewa na wasafiri kutoka eneo moja kwenda jingine, ongezeko la watu duniani, mabadiliko ya tabia nchi,  utandawazi, ongezeko la mahitaji ya maji na chakula.

Awali akiongea katika mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo nchini, Dkt. Hezron Nonga alibainisha kuwa  sekta za Afya zikishirikiana katika Kudhibiti magojwa zitasaidia kuimarisha Afya ya Binadamu kwa kuwa kila sekta itakuwa inachukuwa tahadhri kwa wakati. Aidha alibainisha kuwa  vimelea vingi vinavyo sabababisha magonjwa kwa binadamu asilimia (60%) vinatoka  kwa wanyama pori na mifugo na maambukizi yanatokea pale binadamu anapoingilia maskani ya wanyama hao bila tahadhari, hivyo Afya moja ikitumika maeneo ya mipakani itasaidia kuimarisha udhibiti wa magonjwa ambukizi yanayotokana na shughuli za mwingiliano wa wanyama na binadamu zinazofanyika sana maeneo ya mipakani.

Katika kuhakikisha watalaam hao kutoka sekta za Afya wanaweza kutumia Dhana  hiyo katika kudhibiti magonjwa katika maeneo ya mipakani wameweza kujengewa uwezo wa namna ya kutoa taarifa za milipuko ya magonjwa ambukizi kama vile ugonjwa wa Kimeta, pindi unapotokea maeneo ya mipakani, Namna ya kuunda vikosi vya kufuatilia na kukabili Ugonjwa, Mawasiliano wakati wa kufuatilia na kukabili magonjwa hayo kwa kutumia Dhana ya Afya moja,  pamoja na masuala ya kutumia vifaa Kinga Binafsi vya Kitaalamu.

Tarehe 13 Februari 2018, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa alizindua Dawati la Uratibu la Afya moja chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, likiwa na lengo la kusimamia na kuratibu shughuli za Afya moja nchini. Kwa kutambua umuhimu huo  Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, kupitia Dawati la Uratibu wa Afya moja  kwa kushirikiana Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) waliandaa na kuratibu mafuzo hayo.

 


Share:

PICHA:Malecela Na Mkewe Wamjulia Hali Mtoto Wao William Malecela (Lemutuz)

Waziri Mkuu Mstaafu Mzee John Malecela na mkewe Mhe Anna Kilango-Malecela wakiwa wamemtembelea kumjulia hali mtoto  wao William Malecela maarufu kama Le Mutuzu Super Brand aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete jijini Dar es salaam kwa matibabu leo Jumapili Mei 5, 2019


Share:

WATAHINIWA 91,442 KUFANYA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA KUANZIA KESHO

 Watahiniwa 91,442 wanatarajiwa kufanya mitihani yao ya kumaliza kidato cha sita kuanzia kesho Jumatatu Mei 6 hadi 23, 2019.

Mbali na hao, watahiniwa 12,540 wanatarajiwa kufanya mitihani yao ya kumaliza kozi ya ualimu katika ngazi ya cheti na stashahada.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumapili Mei 5, 2019 Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Dk Charles Msonde, amesema kumekuwa na ongezeko la watahiniwa wa shule wanaomaliza mtihani wa kidato cha sita kwa asilimia 4 ikilinganishwa na mwaka jana huku idadi ya watahiniwa wa ngazi ya ualimu wakiongezeka kwa asilimia 41.

“Mwaka jana watahiniwa wa shule waliosajiliwa walikuwa 77,222 na watahiniwa katika ngazi ya ualimu waliosajiliwa mwaka huo walikuwa 7,422,” amesema Dk Msonde.

Akitoa ufafanuzi wa watahiniwa wa mtihani wa kidato cha sita waliosajiliwa mwaka huu, amesema kati 80,305 ni watahiniwa wa shule na 11,117 ni wa kujitegemea

“Katika watahiniwa wa shule kati yao 46,224 sawa na asilimia 57.56 ni wavulana na 34,081 sawa na asilimia 42.44 ni wasichana huku watahiniwa walio na uhitaji maalumu wapo 102 kati yao, 67 ni wenye uoni hafifu; 16 ni wasioona; 18 wenye ulemavu wa kusikia; na 1 ni mwenye ulemavu wa afya ya akili,” amesema Dk Msonde.

Katika watahiniwa wa kujitegemea waliosajiliwa 7,190 kati yao sawa na asilimia 64.68 ni wavulana, ni 3,927 wasichana sawa na asilimia 35.32.

Pia, katika watahiniwa wanaotarajiwa kufanya kozi ya kumaliza ualimu kati yao 7,594 ni ngazi ya stashahada na 4,946 ngazi ya cheti.

“Katika watahiniwa wa ngazi ya stashahada waliosajiliwa kati yao 5,615 sawa ana asilimia 74 ni wavulana; na 1,979 sawa na asilimia 26 ni wasichana.

“Na watahiniwa waliosajiliwa katika ngazi ya cheti waliosajiliwa 2,795 sawa na asilimia 57 ni wavulana na 2,151 sawa na asilimia 43 ni wasichana,” amesema Dk Msonde.
Na Aurea Simtowe - Mwananchi 
Share:

Waganga Wakuu wa Mikoa wapewa Siku 30 kutathmini utendaji wa Kamati za afya za Mikoa na Wilaya

Waganga wakuu wa Mikoa Tanzania Bara wamepewa mwezi mmoja kuhakikisha kuwa wanazifanyia tathmini ya kina kamati za Uendeshaji Huduma za Afya za Mikoa na wilaya zao kuona kama zinaendana na kasi ya mabadiliko yanayokusudiwa na Serikali ya awamu ya tano. 

Agizo hilo limetolewa jana mjini Songea na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI anayeshughulikia Afya Dkt.Dorothy Gwajima wakati akizungumza  na wajumbe wa kamati ya Uendeshaji Huduma za Afya ya Mkoa wa Ruvuma pamoja za Halmashauri za wilaya ya  Namtumbo na Songea pamoja na Manispaa ya Songea. 

Amesema anawapa siku 30 Waganga wakuu wa Mikoa yote kuhakikisha kuwa wanafanya tathmini ya wajumbe waliopo katika ofisi zao kama wanatosha kuendelea na nyadhifa zao za kusimamia jukumu la uendeshaji huduma za afya katika mikoa na halmashauri zao. 

Dkt Gwajima ameongeza kuwa endapo itabainika kuwa baadhi ya wajumbe wa kamati hizo hawana sifa zinazowafanya kushindwa kutekeleza majukumu yao ya usimamizi na uendeshaji huduma za afya katika maeneo yao, waganga wakuu wa mikoa watalazimika kuwaweka pembeni wajumbe hao na kuunda upya kamati ambazo zitaweza kuiendeleza agenda ya mabadiliko katika sekta ya afya. 

“Kinyume na hapo katika ziara hizi ninazoendelea kuzifanya mikoani nikikuta yupo Mganga Mkuu ambaye ametulia tu, mapungufu katika vituo bado yapo na amewezeshwa na serikali, ajue wazi kuwa wa kutokutosha wa kwanza atakuwa yeye,” amesema Dkt Gwajima na kuongeza: 

“Haiwezekani tukute mapungufu madogo kabisa katika vituo, ambayo yangeweza kuonwa na wao walioko huko eti hayaonekani hadi tuje sisi kutoka Tamisemi ndiyo mapungufu hao yafanyiwe kazi,”amesisitiza Dkt Gwajima. 

Naibu Katibu Mkuu huyo ameonya tabia iliyojengeka miongoni mwa wajumbe wa kamati za uendeshaji huduma ya afya kukimbilia kuomba msamaha pindi zinaposhindwa kutekeleza majukumu yake kwa makusudi. 

Amesema huu ni wakati wa kuboresha sekta ya afya katika vituo vya afya na zahanati kwa kuhakikisha kuwa mazingira ya utoaji huduma yanaboreshwa ili yaweze kuwavutia wananchi wengi kukimbilia kupata huduma katika zahanati na vituo vya afya vinavyomilikiwa na serikali. 

Dkt Gwajima amesema kuwa kamwe hatawapa nafasi wajumbe wa kamati za uendeshaji huduma za afya wa mikoa na wilaya ambao siku zote wamekuwa ni watu wa visingizio vya kuomba kusamehewa ama kupewa muda kuwa wamefahamu mapungufu yao. 

Amesema angependa kuona kamati za uendeshaji huduma za afya katika  mikoa na halmashauri zikijikita katika kuongelea mambo makubwa yanayolenga kuishirikisha sekta na serikali kuu. 

“Hivi vitu vidogo vidogo vya kitaalamu tubebe sisi wenyewe, wananchi wametuunga mkono, tumeweza kushirikiana nao kujenga zahanati na vituo vya afya katika mikoa na halmashauri zetu hivyo ni jukumu letu sasa kuhakikisha kuwa tunatoa huduma bora za afya kwa wananchi,” amesema. 

Kwa mujibu wa Dkt.Gwajima, katika ziara zake alizokwisha zifanya katika mikoa ya Morogoro, Dodoma, Njombe na Ruvuma amejionea mapungufu mbalimbali ya utoaji wa huduma bora za afya katika vituo vya afya na zahanati. 

Ameongeza kuwa mapungufu hayo ambayo ameyashuhudia kwenye vituo vya afya na zahanati zinazomilikiwa na umma yametokana na watendaji hao  kutopata usimamizi unaostahili kutoka kwa kamati za usimamizi  na uendeshaji wa huduma za afya za mikoa na halmashauri husika. 

Dkt Gwajima anaamini kuwa kushindwa kwa kamati za uendeshaji ndiko kulikopelekea kukithiri kwa uchafu katika majengo ya vituo vya afya na zahanati nchini licha ya vituo hivyo kuwa na fedha za uendeshaji wake. 

Sambamba na kuwataka waganga wakuu wa mikoa kuzitathmini kamati hizo, Dkt Gwajima amewataka waganga wakuu wote kutambua kuwa  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt John Pombe Magufuli ana agenda moja tu ya kuleta mabadiliko katika sekta ya afya. 

 “Hatutapimwa kwa idadi ya semina au vituo vya afya tulivyojenga bali kwa ubora wa kazi za kuhudumia wananchi,” amesema. 

Dkt Gwajima amebainisha mapungufu kadhaa aliyoyaona kwenye ziara yake kuwa ni pamoja kuwepo kwa malalamiko toka kwa wagonjwa na  kukosekana kwa takwimu sahihi za utendaji kazi 

Akiwa katika kituo cha afya Mjimwema Manispaa ya Songea Naibu Katibu Mkuu Dkt.Gwajima alipokea kero za wagonjwa kuhusu uwepo wa kauli mbaya toka kwa wauguzi na tatizo la ukosefu dawa hususan  akina mama wajawazito  

“Hapa Mjimwema nimebaini kasoro nyingi mojawapo kauli mbaya za watumishi na tatizo la dawa na vifaa tiba kwa wagonjwa ” Dkt .Gwajima alionya. 

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dkt.Jairy Khanga ameahidi  kuchukua hatua za mapema kufanya mabadiliko ya utendaji kazi wa kamati za usimamizi wa huduma za afya katika mkoa wa Ruvuma .
Mwisho.


Share:

Walichokisema CHADEMA Kuhusu Tukio la Mdude Nyagali (Mdude Chadema)

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), katika hali ya dharura, kinafuatilia kwa karibu, taarifa za Mdude Nyagali (Mdude Chadema) kuvamiwa kisha kuchukuliwa na watu ambao hawajatambulika, akiwa ofisini kwake, eneo la Vwawa, Mbozi, mkoani Songwe, katika tukio lenye dalili za utekaji.

Kwa mujibu wa baadhi ya mashuhuda, majira ya jana  jioni  (saa 12 kuelekea saa 1) yalifika magari mawili katika eneo la ofisini kwa Mdude, Vwawa mjini, kisha wakatelemka takriban watu wanne, ambao walimkamata kijana mmoja aliyekuwa nje ya ofisi hiyo wakampeleka kwenye mojawapo ya magari waliyokuja nayo huku wengine wakiingia ndani ya ofisi, alikokuwa Mdude.

Imedaiwa kuwa baada ya muda mfupi kulisikika purukushani, watu hao wakijaribu kumkamata Mdude huku wakimpiga na yeye akipiga kelele za kupinga kitendo hicho na kuomba msaada.

Taarifa za awali ambazo Chama kimezipata kutoka kwa mashuhuda hao zimedai kuwa baada ya kusikika kwa purukushani na kelele hizo, baadhi ya wananchi walijitokeza kutaka kujua kinachoendelea na kutoa msaada, ghafla watu hao waliokuwa wakimpiga Mdude wakatoa silaha aina ya bastola na kuwatishia wananchi hao, kitendo kilichowaogofya wananchi na kukimbia kwa hofu.

Imedaiwa kuwa watu hao walimuingiza Mdude kwenye ‘buti’ ya mojawapo ya gari hizo, wakamuachia yule kijana mwingine kisha wakaondoka na Mdude kuelekea kusikojulikana.

Tayari CHADEMA kupitia kwa Viongozi wa Chama katika eneo husika na Mbunge wa Mbozi Mashariki, Pascal Haonga, kimevitaarifu vyombo vya dola mkoani Mbeya, kwanza kutoa taarifa ya tukio hilo lenye mazingira ya utekaji pia kutaka kujua kama kuna askari waliopewa kazi ya kwenda kumkamata Mdude.

Hadi sasa haijulikani Mdude yuko wapi! Tupaze sauti zetu sote kulaani tukio hili na kutaka Mdude arudishwe au aachiliwe akiwa salama.

Katika hatua ya sasa, CHADEMA kwa nguvu zote kinalaani vikali tukio hilo. Tunavitaka vyombo vya dola, hususan Jeshi la Polisi lenye wajibu wa kulinda raia na mali zao, kufuatilia taarifa za tukio hilo kama zilivyoripotiwa kwa polisi katika eneo husika na kuhakikisha Mdude anapatikana na wahalifu waliotenda tukio hilo wanajulikana, kukamatwa na kufikishwa mbele ya sheria.

Tutaendelea kuwapatia taarifa zaidi kadri itakavyohitajika.

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA


Share:

Wizara ya elimu: Fully Funded Scholarships For Female Students by World Bank 2019

Scholarships for Tanzanians 2019| Scholarships in Tanzania 2019 | Masters Scholarships for Tanzanians 2019 |Unergraduate Degree Scholarships for Tanzanians 2019 | Scholarships 2019 | Scholarships abroad for Tanzanians | Wizara ya Elimu Scholarships | Tanzania Scholarships | Scholarships Fully Funded for Africans 2019 | Scholarships for Kenyans 2019 | East Africa Community Scholarships | World Bank Scholarships | Udhamini wa masomo | Fully Funded scholarships | scholarships Tanzania | ministry of Education Scholarships

The World Bank is partnering with eight Governments in Eastern and Southern Africa in an innovative project with the aim of improving the quality of training and research in higher education and reducing the skill gaps in key development priority areas. The Eastern and Southern Africa Higher Education Centers of Excellence (ACE II) Project supports the governments of Ethiopia, Kenya, Malawi, Mozambique, Rwanda, Tanzania, Uganda, and Zambia in strengthening selected African Centers of Excellence (ACEs) to deliver quality post-graduate education and build collaborative research capacity in the following priority areas:

(i) STEM (Science, Technology, Engineering and Mathematics) or Industry

(ii) Agriculture

(iii) Health

(iv) Education 

(v) Applied Statistics.

THE FELLOWSHIP AWARD

The provided financial support for each Fellowship Program will cover:

1)University tuition fees: Approximately USD 3,000 per year (payable directly to the Host University according to an official invoice)

2)Stipend: USD 800 per month to support living expenses such as housing, food, utilities, local transportation, medication and settlement expenses

3)Research: USD 4,800 to support student research, payable upon approval of the research proposal

4)Allowance: USD 2,000 one-off allowance to cover visa, laptop, and books

5)Air ticket: A round-trip economy fare for the most direct route between the beneficiary’s home country and the study destination of Host University

For further information about the scholarship, the fellowship awardeligibility criteria, please visit the following links: CLICK HERE

Application Process and Procedures

Interested candidates are advised to fill in the application form found at ace2.iucea.org or www.iucea.org, attach all requested documents, and send by e-mail toexsec@iucea.org with a copy to ace2rfu@iucea.org.

CLICK HERE TO DOWNLOAD THE APPLICATION FORM AND APPLY

Applications must be received not later than 5.00 PM East African Time on June 30, 2019.

Issued by:

Permanent Secretary,

Ministry of Education, Science and Technology,

University of Dodoma,

College of Business and Law,

Block 10,

P .O. Box 10,

40479 Dodoma.

The post Wizara ya elimu: Fully Funded Scholarships For Female Students by World Bank 2019 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Maduro alitaka jeshi kujiweka tayari dhidi ya uvamizi wa Marekani

Rais wa Venezuala Nicolas Maduro amevitolea wito vikosi vyake vya jeshi kujiweka tayari kwa hatua zozote za kijeshi kutoka Marekani wakati wafuasi wa kiongozi wa upinzani Juan Guaido wakikusanyika kwenye kambi za jeshi kujaribu kutafuta uungwaji mkono.

Maduro ameliamuru jeshi kujiandaa kuilinda nchi hiyo kwa kila zana zilizopo iwapo Marekani itajaribu kuchukua hatua za kijeshi katika taifa hilo la Amerika ya Kusini lenye utajrii mkubwa wa mafuta. 

Katika kusisitiza kuwa juu ya jeshi linaendelea kuuunga mkono utawala wake wa kisoshalisti, Maduro alitoa hotuba kupitia televisheni akiwa pamoja na waziri wake wa ulinzi sambamba na vikosi vya kiasi wanajeshi 5,000

 Harakati za Guaido zilipata uungwaji mpya jana Jumamosi kutoka kwa waziri wa Mambo ya kigeni wa Marekani Mike Pompeo, alietoa ukanda wa vidio akiwahimiza raia wa Venezuela kuchukua hatua akisema wakati wa mabadiliko kwa taifa hilo ni sasa. 

Marekani bado haijaondoa uwezekano wa kutumia hatua za kijeshi kumuondoa Maduro madarakani.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya May 5




Share:

Saturday, 4 May 2019

Makubwa Haya : MWANAMKE AJIFUNGUA SAMAKI

Wakazi wa eneo la Shariani jimbo la Kilifi wameachwa vinywa wazi  na kudai huenda ni ushirikina baada ya mmoja wao kudaiwa kujifungua 'samaki' aliyehai.


 Wakazi hao walifurika katika boma la Sarah Mbeyu Jabiri ili kujionea kioja cha kiumbe aliyetoka tumboni mwake. 

Mwanamke huyo alinza kutokwa damu kabla ya kuanza kuhisi maumivu makali ya tumboni. 

Kulingana na taarifa ya The Standard, mambo yalikuwa shwari kwa Jabiri hadi siku ya Alhamisi wakati alipoanza kutokwa na damu na kuhisi uchungu tumboni. 

"Nilianza kutokwa na damu Alhamisi na Ijumaa wiki jana. Baadaye nilianza kuhisi maumivu ya tumbo,uchungu ambao ulikuwa sawia na ule wa kujifungua. 

Uchungu huo ulipoa siku ya Jumapili ingawaje nilizidi kutoa na damu hadi Jumatano usiku wakati nilihisi uzito chini ya kitovu changu na hapo nikaanza kusukuma," Jabiri alidokeza.

 Mwanamke huyo ambaye ni mama wa watoto watano, alipigwa na butwaa baada ya kushuhudia kilichotoka katika mfuko wake wa uzazi na kwa haraka akamfahamisha mamaake ambaye anaishi katika eneo hilo. 

"Mimi sikuwa na mimba. Nilipohisi uzito huo nilikimbia kuchukua beseni ili nikitumbukize kidude hicho humo lakini kwa bahati mbaya kilinitoka na kuanguka sakafuni. Kiumbe hicho kilikuwa na macho na mkia. Nilishtuka sana kukiona," mwanamke huyo aliongeza.

 Familia hiyo inaamini kuwa Jabiri alifanyiwa uchawi. "Tulikitumbukiza kiumbe hicho katika ndoo iliyojaa maji na ghafla kikaanza kusonga ni kama kuogelea. Jambo hili sio la kawaida. Namsikitikia mwanangu," mamaake Jabiri alisema.

 Hata hivyo, afisa mkuu wa hospitali ya Kilifi Eddy Nzomo alipuuzilia mbali madai hayo na kusema kuwa mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 30 aliugua ugonjwa ulioathiri mfuko wake wa uzazi na kusababisha uvimbe maarufu kama molar pregnancy.

 Maradhi haya huwaathiri haswa wanawake walio zaidi ya umri wa miaka 35 au chini ya miaka 20.

 Aliongeza kuwa hali hiyo pia inaweza kuwaathiri wanawake waja wazito kabla ya kufikisha miezi saba. 

Kwa sasa, Jabiri amelazwa katika hospitali ya jimbo la Kilifi kwa uchunguzi zaidi wa matibabu na vile vile kuusafisha mfuko wake wa uzazi.

Via>>Tuko
Share:

SIKU YA WAKUNGA DUNIANI KITAIFA MWAKA 2019 KUFANYIKA SIMIYU


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(katikati) akizungumza na waandishi wa habari  ( hawapo pichani) juu ya Maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani ambayo Kitaifa yatakayofanyika kesho Mei 05, 2019 Mkoani Simiyu katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Makamu Mwakilishi Mkaazi wa UNFPA hapa nchini, Dkt.Hashina Begum(wa pili kushoto) akitoa taarifa mbele ya waandishi wa habari juu ya Maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani ambayo Kitaifa yatakayofanyika kesho Mei 05, 2019 Mkoani Simiyu katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi...
Rais Chama Cha Wakunga Tanzania (TAMA), Feddy Mwanga(katikati) akizungumza kwa niaba ya Chama hicho mbele ya mbele ya waandishi wa habari juu ya Maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani ambayo Kitaifa yatakayofanyika kesho Mei 05, 2019 Mkoani Simiyu katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi..
Baadhi ya waandishi wa habari wa mkoa wa Simiyu wakiwa katika Mkutano na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(hayupo pichani) uliolenga kutoa taarifa juu ya Maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani ambayo Kitaifa yatakayofanyika kesho Mei 05, 2019 Mkoani Simiyu katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
***
Na Stella Kalinga, Simiyu
Maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani Kitaifa mwaka 2019 yanatarajiwa kufanyika  kesho katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu, ambapo Mgeni rasmi atakuwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akimwakilisha Makamu wa Rais wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amewakaribisha wakunga wote hapa nchini na kuwahakikishia kuwa Mkoa umefanya maandalizi ya  kutosha ili maadhimisho hayo yaweze kufana.

"Nitumie nafasi hii kama Mkuu wa Mkoa kuwaalika familia ya Wakunga wote Tanzania ambao wameanza safari kuja kwenye shughuli yao ya Kitaifa ndani ya mkoa wetu, niwahakikishie kuwa tumefanya maandalizi ya kutosha kuhakikisha shughuli yao inaenda vizuri" alisema Mtaka

Katika hatua nyingine Mtaka amelishukuru Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu Duniani (UNFPA) kuwa sehemu ya kuwezesha Maadhimisho hayo Kitaifa kufanyika Mkoani Simiyu,  pamoja na  mchango mkubwa wa Shirika hilo na wadau wengine katika sekta ya afya ndani ya Mkoa.

Naye Makamu Mwakilishi Mkaazi wa UNFPA hapa nchini, Dkt.Hashina Begum amesema Kauli Mbiu ya Siku ya Wakunga Duniani mwaka 2019 inayosema"Wakunga ni Watetezi wa Haki za Wanawake" inakumbusha umuhimu wa wakunga katika kuwatetea kina mama wakati wa ujauzito, wakati wa kujifungua na baada ya kujifungua.


Ameongeza kuwa UNFPA imeendelea kushirikiana na Serikali  katika ukarabati wa vituo 38 vya afya, wodi za wazazi  na vyumba vya upasuaji, ununuzi wa vifaa na mashine za kumwezesha Mkunga kutoa huduma ya mama na mtoto kwa urahisi na kuwajengea uwezo wakunga 90 kutoka vituo vilivyokarabatiwa kutoa huduma za dharura kwa mama na mtoto.

Naye Rais Chama Cha Wakunga Tanzania (TAMA), Feddy Mwanga amesema TAMA inafanya kazi na Mkoa wa Simiyu kutoka mwaka 2016 kuwaelimisha Wakunga, ili waweze kutoa huduma za dharura kwa mama na mtoto hususani katika vituo vya pembezoni, huku akiishukuru UNFPA kwa mchango wake kifedha na utaalamu kuwezesha mafunzo hayo.

Ameongeza kuwa Dira ya TAMA ni kuona kuwa kila mama mjamzito anayejifungua na watoto wachanga wanahudumiwa na Wakunga wataalam na wanapata huduma bora, huku akitoa wito wananchi wa Simiyu kujitokeza kwa wingi katika Maadhimisho hayo ili waweze kupata huduma za upimaji bila malipo.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger