Saturday, 4 May 2019

Picha : MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI....SERIKALI YASISITIZA MAJADILIANO KUBORESHA SEKTA YA HABARI


Serikali imesema haina mpango wa kuendelea kuvifungia vyombo vya habari vinavyokiuka kisheria kwenye utekelezaji wa majukumu na badala yake itaendelea kutumia njia ya majadiliano pale inapotokea changamoto ya kiutendaji.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas aliyasema hayo jana jijini Dodoma wakati akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwenye kilele cha maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2019.

Dkt. Abbas alisema ni vyema wadau wa habari wakaunda kamati maalum itakayoketi na kujadiliana na Serikali kuhusiana na changamoto mbalimbali wanazodhani ni vikwazo kwenye utekelezaji wa majukumu yao ikiwemo vifungu na sheria za habari.

Aidha Dkt. Abbas aliwahimiza wadau wa habari kuzisoma na kuzielewa vyema sheria hususani Sheria ya Huduma za Huduma za Vyombo vya Habari ya mwaka 2016 ili wanapokutana na Serikali kwenye majadiliano wawe na uelewa wa kutosha kuelezea vifungu vyenye changamoto tofauti na hivi sasa ambapo baadhi wanalalamika bila kuweka wazi vifungu gani vina mapungufu.

Katika maadhimisho hayo, washiriki walipendekeza maazimio 16 ikiwemo kuunda kamati itakayoketi na Serikali kujadiliana baadhi ya changamoto zinazokwamisha uhuru wa habari kama vile kufungia vyombo vya habari pamoja na kanuni zenye vikwazo kwenye Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari ya mwaka 2016.

Taasisi mbalimbali zilishiriki kufanikisha maadhimisho hayo ikiwemo MISA Tanzania, Ubalozi wa Marekani, Internews, FES, IMS, Umoja wa Mataifa, UTPC, TMF, TEF, UK Aid, TAMWA, MCT, Unesco na Serikali ya Tanzania huku kauli mbiu ikiwa ni “wajibu wa vyombo vya habari kwa demokrasia, tasnia ya habari na uchaguzi nyakati za upotoshaji wa taarifa”.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dkt. Inmi Patterson akizungumza kwenye maadhimisho hayo ambapo alisisitiza juu ya uhuru wa vyombo vya habari katika kutimiza majukumu yake bila kuingiliwa.
Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe. Sarah Cooke akitoa salamu zake kwenye maadhmisho hayo.
Mkurugenzi wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Abubakary Karsan akichangia mada kwenye maadhimisho hayo.
Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa ofisi ya Tanzania, Stella Vuzo akitoa salamu za Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres kwenye maadhimisho hayo.
Washiriki wa maadhimisho hayo wakifuatilia ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres kwa njia ya vidio.
Fuatilia matukio katika picha kwenye maadhimisho hayo.
Washiriki wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2019 kitaifa jijini Dodoma wamesimama kwa muda kama ishara ya kumuombea aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT) na pia mmiliki wa makampuni ya IPP, Dkt. Reginald Mengi aliyefariki usiku wa kuamkia jana nchini Dubai akiwa na miaka 77.
Washiriki wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Washiriki wakifuatia mada kwenye maadhimisho hayo.
Mkurugenzi wa Misa Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Dkt. Hassan Abbas (kushoto) baada ya kuwasili kwenye maadhimisho hayo.


Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Dkt. Hassan Abbas akiwa na Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dkt. Inmi Patterson pamoja na viongozi kutoka taasisi mbalimbali kutembelea mabanda ya maonyesho ya kitaaluma kwenye maadhimisho hayo.
Wachezaji wa ngoma za asili kutoka kabila la Wagogo walinogesha mapokezi ya washiriki na viongozi mbalimbali.

Picha na KD Mula
Share:

ZARI AFIKA NYUMBANI KWA MAREHEMU DR. REGINALD MENGI KUTOA POLE ZA MSIBA


Mfanyabiashara na Mwanamitindo Zari Hasan @zarithebosslady ambaye ni raia wa Uganda amekuwa miongoni mwa watu waliofika nyumbani kwa marehemu Dr. Reginald Mengi
Kinondoni Dar es Salaam kutoa pole na kusaini kitabu cha maombolezo leo Mei 4,2019.
Share:

Picha : MAKAMU WA RAIS WA BUNGE LA AFRIKA AKUTANA NA WABUNGE WAPYA WA BUNGE LA AFRIKA

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika Mheshimiwa Stephen Masele amekutana na Wabunge wapya wa Bunge la Afrika wataoapishwa siku ya Jumatatu Mei 6,2019 wakati wa Mkutano wa Pili wa Bunge la Tano la Bunge la Afrika jijini Johannesburg Afrika kusini.

Mkutano huo wa kuwajengea uwezo kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu Bunge la Afrika ikiwemo kuwaeleza historia na jinsi bunge hilo linavyofanya kazi umefanyika katika ukumbi mdogo wa makao makuu ya Bunge la Afrika uliopo Midrand,jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini.

Mheshimiwa Masele ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini nchini Tanzania,amewapongeza hao wabunge 26, kutoka nchi tano zikiwemo Eswatini, Msumbiji, Uganda, Zambia na Algeria kwa kuchaguliwa kuwakilisha katika Bunge la Afrika.

Kikao cha Pili cha kawaida cha Bunge la Tano la Afrika kinatarajiwa kuanza siku ya Jumatatu Mei 6,2019 ambapo wabunge zaidi ya 250 watajadiliana juu ya kauli mbiu ya Umoja wa Afrika ya mwaka huu “Mwaka wa Wakimbizi na Watu Waliopotea” na suluhisho la kudumu juu ya tatizo la wakimbizi barani Afrika.

Mijadala mingine itahusu  taarifa juu ya amani na usalama katika bara ikiwa ni pamoja na maendeleo ya hivi karibuni na hali ya kisiasa Libya, Sudan, Algeria na mchakato wa amani nchini Sudan Kusini. 

Na Kadama Malunde – Johannesburg,Afrika Kusini.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika Mheshimiwa Stephen Masele akizungumza wakati wa mkutano na wabunge wapya wa Bunge la Afrika leo,katika ukumbi mdogo wa Bunge la Afrika,Johannesburg nchini Afrika Kusini - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika Mheshimiwa Stephen Masele akiwakaribisha wabunge wapya wa Bunge la Afrika.
Sehemu ya wabunge hao wakimsikiliza Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika Mheshimiwa Stephen Masele.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika Mheshimiwa Stephen Masele akielezea jinsi Bunge la Afrika linavyofanya kazi.
Sehemu ya wabunge hao wakiwa ukumbini.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika Mheshimiwa Stephen Masele akizungumza ukumbini.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika Mheshimiwa Stephen Masele akiwaelezea jambo wabunge hao wakati akiwatembeza katika jengo la ofisi za utawala za Bunge la Afrika.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika Mheshimiwa Stephen Masele akielezea jambo wakati wabunge wapya wa Bunge la Afrika wakitembelea ofisi za Bunge la Afrika nchini Afrika Kusini.
Mheshimiwa Masele akiwaeleza jambo wabunge hao.
Mheshimiwa Masele akizungumza na wabunge hao.
Mheshimiwa Masele akiwaeleza jambo wabunge hao.
Picha ya pamoja,Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika Mheshimiwa Stephen Masele na wabunge wapya wa Bunge la Afrika.
Picha ya pamoja,Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika Mheshimiwa Stephen Masele na wabunge wapya wa Bunge la Afrika.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Share:

KUTANA NA NYOKA WA AJABU...ANA MACHO MATATU

Maafisa wa wanyama pori wamesambaza picha za nyoka mwenye macho matatu aliyepatikana katikati ya barabara kaskazini mwa Australia.

Shirika la huduma kwa wanyama pori na bustani za wanyama Northern Territory Parks and Wildlife Service wameeleza kwamba nyoka huyo ambaye picha zake zilisambaa pakubwa katika mitandao ya kijamii, ni wa "kustaajabisha".

Amepewa jina la Monty Python, nyoka huyo aina ya chatu alifariki wiki kadhaa tu baada ya kugunduliwa mnamo Machi,2019.

Wataalamu wanasema jicho la tatu la nyoka huyo lililo juu ya kichwa chake limeonekana kuwa ni mabadiliko ya asili

Maafisa walimgundua nyoka huyo katika mji wa Humpty Doo, 40km kusini mashariki mwa Darwin.

Ana urefu wa 15 inchi na alikuwa akipata tabu kula chakula kutokana na ulemavu wake, maafisa wameiambia BBC.
'Hali' ya kawaida

Shirika hilo la huduma kwa wanyama pori limesema picha za X-ray zimeonyesha kwamba hakuwa na vichwa viwili kwa pamoja.

"Badala yake alionekana kuwa na fuvu moja la kichwa na jicho la ziada ukijumlisha, macho matatu yanayofanya kazi sawasawa," lilieleza kwenye Facebook.Alikuwa akipata tabu kula chakula kutokana na ulemavu wake

Mtaalamu wa nyoka Profesa Bryan Fry amesema mabadiliko ya maumbile ni sehemu ya kawaida ya kuumbwa.

"Kila mtoto hupitia mabadiliko ya kiwango fulani - huyu alishuhudia mabadiliko yasio ya kawaida," amesema Profesa Fry, kutoka chuo kikuu cha Queensland.

"Sijaona nyoka mwenye macho matatu awali, lakini tumeona chatu mwenye vichwa viwili katika maabara yetu - ni aina tofuati ya mabadiliko kama tunavyoona kwa pacha wachanga wanaozaliwa wakishikana."

Ameashiria kwamba huenda jicho hilo la tatu likawa " sehemu ya mwisho ya pacha wa nyoka huyo aliyefyonzwa".
Chanzo - BBC
Share:

MAITI YACHOMOKA KWENYE JENEZA WAKATI WA MAZISHI

Familia chini Ghana huwapa mkono wa buriani wapendwa wao waliofariki dunia kwa mtindo wa aina yake huku wengi wao hata wakiwaajiri kwa muda wasakata densi kushiriki majira ya mwisho ya kumpa buriani marehemu.

 Mtindo huu wa kuwaajiri watakaolibeba sanduku la maiti huku wakisakata densi kwa nyimbo umeonekana kushika kasi mno na ni bayana kuwa utakuwepo kwa muda mrefu zaidi. 

Hata hivyo, kwenye tukio moja mambo yameonekana kwenda mrama katika hafla ya mazishi.

 Katika video moja iliyosambaa kwa kasi mitandaoni, jamaa wa marehemu wameachwa na mshtuko baada ya maiti ya mpendwa wao kuteleza na kuanguka kutoka katika sanduku lililombeba.

 Hii ni baada ya wanadensi waliokuwa wamelibeba sanduku hilo kupoteza mwelekeo wakila uhondo na kupelekea maiti kuchomoka kwa bahati mbaya na kuanguka. 

Familia ya mwendazake na waombolezaji walisika wakimaka kwa mshangao kufuatia kihoja hicho huku jamaa hao wakiwa katika harakati ya kuufunika mwili wa marehemu.
Share:

IGP Sirro: Tutafuatilia Yote Yanayosemwa Mitandaoni Kuhusu Reginald Mengi...Kwa Sasa Tumalize kwanza Msiba

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amesema  Jeshi lake litafuatilia kwa kina maneno yote yanayosemwa  mitandaoni kuhusu Kifo cha Reginald Mengi ili kubaini kama yanaukweli wowote ili sheria ichukue mkondo wake.

IGP Siiro ametoa kauli hiyo leo baada ya kufika nyumbani kwa Dr Mengi ili kutoa Pole ya msiba.

”Mzee Mengi alikuwa mshauri mzuri sana kwenye masuala ya ulinzi na usalama pamoja na misaada midogo midogo kwa vijana wetu wanapokuwa na shida. Zaidi alikuwa ‘very humble’ mara zote alikuwa anajishusha sana.

"Yako mengi yanayoongelewa kwa sasa mitandaoni, lakini jambo la msingi tumalize kwanza msiba, hayo yanayozungumzwa mitandaoni tutafuatilia,” amesema Sirro.

==>>Msikilize hapo chini


Share:

: Ajali ya Hiace yaua watu 7 na kujeruhi 12 Kigoma

Watu 7 wamefariki dunia na wengine 12 kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupasuka tairi la nyuma na kupinduka mkoani Kigoma.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Martin Ottieno amesema ajali hiyo ilitokea jana saa 12 :15 jioni katika kijiji cha Mlela wilayani Uvinza mkoani humo.

Alisema gari hiyo iliyokuwa inatokea wilayani Uvinza kwenda Kigoma mjini ilipasuka tairi la nyuma upande wa kushoto na kupinduka.

Majeruhi wote wamepelekwa Hospitali ya Mkoa ya Maweni.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger