Saturday, 4 May 2019

PICHA: IGP Sirro na Viongozi Wengine Msibani kwa Reginald Mengi

IGP Simon Sirro akiwa nyumbani kwa Dr. Mengi kutoa salamu za pole kwa familia.
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akiwa  nyumbani kwa Dr. Mengi, kuomboleza msiba wa mpendwa wetu.
Naibu Waziri wa Kilimo Omary Mgumba, akiwa  msibani kutoa salamu za rambirambi nyumbani kwa Dr. Mengi.



Share:

Rais Mstaafu Benjamin Mkapa Amlilia Dr. Reginald Mengi.....Kasema Wakati wa Uongozi wake Alimfanya Awe Rais Bora

Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa ametuma salamu zake  za Rambi Rambi Kufuatia Kifo Cha Dkt Reginald Mengi  akisema Mengi alikuwa miongoni mwa Watanzania wachache waliokuwa wazalendo ambao Taifa halitawasahau.

“Nimemfahamu Mengi miaka mingi iliyopita na kwangu ananirudisha katika historia kama mzalendo aliyesimamia nafasi yake kwa jamii,” alisema Mkapa kupitia ujumbe wake wa rambirambi .

Alimtaja Mengi kuwa ni kati ya wazalendo wachache walioanzisha viwanda, aliyejitolea kwa ajili ya maisha ya wengine na kupambana kuondokana na umaskini ambaye Taifa litaendelea kujivunia.

“Wakati wa urais wangu, Dk Mengi kupitia shughuli mbalimbali alinifanya niwe Rais mzuri. Alikuwa mkweli katika maoni yake hata kama yalikuwa tofauti na misimamo yangu na hilo lilinifanya kufaidika na busara zake,” alisema Rais huyo mstaafu.

Alisema utumishi wa Mengi katika sekta binafsi umeendelea kuilea hadi leo na anatambulika kama mtu aliyemshawishi kila anayetamani kuona nchi ikiendelea.

Alisema namna pekee ya kumuenzi ni kufuata njia na mifano aliyoionyesha, kwamba kupambana na umaskini siyo jukumu la Serikali peke yake bali ni la kila mtu.


Share:

RC mbeya awashukuru wananchi na viongozi mbalimbali kwa kufanikisha ziara ya Rais Dkt. magufuli

Ndugu zangu wana Mbeya Tunawashukuru sana wote Kwa umoja wenu na upendo wenu mliouonesha Kwa Mh Rais wetu Dkt John P. Magufuli. 

Mlikuwa wengi na mmefunika. Najua zipo changamoto nyingi ambazo watu wetu waliamua kuandika mabango ili Mh Rais atatue. Nitumie nafasi hii kuwajulisha wote kujenga utamaduni wa kufika ofsn kwangu au kwa wasaidizi wangu maana tumepewa kazi ya kusikiliza na kutatua kero.

Nawashukuru sana CCM Mbeya, Chini ya Uongozi wa Mzee Mwakasole Mwenyekiti, hakika mmetenda haki katika ziara hii. Chama n mshauri na Mwajiri wa Serikali, umoja na mshikamano ndio msingi wa kufika mbele. Nashukuru sana viongozi wa Dini zote Kwa umoja wenu. 

Mmeshikamana na hakika mmetusaidia sana kumsimika Mungu baba katika kila kona ya ziara yetu. Asante sana. Pia nawashukuru sana snaa wafanyabiashara na wadau wengine wote kwa namna mlivyonibeba na kuwa pamoja na mimi katika sherehe za MEI MOSI mmeonesha umoja sana. Assnte sana.

Umefika wakati wa kuijenga Mbeya Kwa kasi na umoja. Sote tuwe na dhamira ya kuifanya Mbeya big city... asante sana sana sana Wana Mbeya, Mbarali, Chunya, Busokelo, Kyela, na kata zake zote.

Mawaziri na Wabunge wote nawashukuru sana. Mh Lukuvi, Mh. Jafo, Mh. Hasunga, Mh. Naibu Speaker, Mh. Biteko, Mh. Kakunda, Mh. Mwanjelwa, Dkt Mwakyembe na Mh Naibu waziri wa ujenzi Pamoja na Mawaziri wengine wote. Wabunge wote wa mkoa huu mmenipa heshima kubwa. Assnte sana Jeshi la Police Kwa kazi nzuri ya kulinda amani chini ya mzee Wangu Kamanda wa Police Mkoa Matei Asante sana

Wakuuu wa Wilaya, Ma DAS na Wakurugenzi wote Ndio mmekuwa kiungo namba Sita katika ziara hii yote. Yote tuliyoagizwa tutatekeleza kama yalivyo. Mmechapa kazi vzr thanks sana.

Asanteni sana snaa. Mimi na wenzangu wote katika ofisi yangu nawashukuru sana

Albert Chalamila
RC Mbeya
03/05/2019


Share:

Boeing 737 Yashindwa kutua na kuishia kuingia mtoni nchini Marekani.

Ndege aina ya Boeing 737 imeshindwa kutua na kuishia kuingia mtoni nchini Marekani.

Hiyo ni aina ile ile ya ndege iliyopata ajali na kusababisha vifo vya mamia ya watu nchini Ethiopia na Indonesia.

Kwa mujibu wa habari,ndege hiyo ilitoka katika barabara yake na kuingia mtoni wakati ikitaka kutua Florida nchini Marekani.

Tukio hilo limetokea katika uwanja wa ndege wa Jacksonville,ambapo ndege hiyo ya abiria iliyokuwa imebeba abiria 136 ilishindwa kutua na mwisho kuingia katika mto wa St.John.

Hata hivyo hakuna aliyeripotiwa kupoteza maisha. Watu wawili wamejeruhiwa.



Share:

Trump na Rais wa Urusi Vladimir Putin Wateta kwa Simu Kuhusu Mgogoro wa Venezuela, Korea Kaskazini

Rais wa Marekani Donald Trump alizungumza kwa njia ya simu na Rais wa Urusi Vladimir Putin hapo jana kuhusu suala la nyuklia, uwezekano wa kuishawishi China kusaini mkataba wa kudhibiti silaha za nyuklia, pamoja na mgogoro wa Venezuea ambako Urusi inaunga mkono upande wa serikali na Marekani inaunga mkono upinzani. 

Msemaji wa ikulu ya Marekani Sarah Sanders amesema katika mazungumzo hayo ya zaidi ya saa nzima, viongozi hao wawili pia walijadili suala la Ukraine, Korea Kaskazini, na biashara kati ya Urusi na Marekani. 

Baada ya mkutano, Trump aliandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba alikuwa na mazungumzo marefu na rais wa Urusi na kwamba kuwa na uhusiano mzuri na Urusi pamoja na China ni jambo zuri kwa Marekani.


Share:

Korea Kaskazini Yarusha Makombora Mengine Leo Kwa Mara ya Kwanza

Korea Kaskazini imerusha makombora ya kwanza tangu 2017. Msururu wa makombora ya masafa mafupi yamerushwa Juammosi na kuangukia karibu na Bahari ya Japan.

Korea Kaskazini imerusha makombora kadhaa ya masafa mafupi kutoka pwani yake ya mashariki Jumamosi, limesema jeshi la Korea Kusini. 

Wachambuzi wanasema Korea Kaskazini inaongeza shinikizo dhidi ya Marekani kwa kushindikana kupatikana makubaliano ya maana katika kutano wa kilele wa Febuari, Hanoi.

Jeshi la Korea Kusini awali lilisema yaliyorushwa ni makombora lakini baadae likashidwa kutoa maelezo zaidi.

Iwapo itathibitishwa kuwa ni uzinduzi wa makombora ya masafa mafupi basi yatakuwa ni ya kwanza kurushwa na Korea Kaskazini tangu uzinduzi wake wa mwezi Novemba 2017. 

Baada ya uzinduzi huo, Korea Kaskazini ilitangaza kwamba uwezo wake wa kinyuklia umekamilika, na ikakubali kuanzisha tena mazungumzo na Marekani pamoja na Korea Kusini.

Msemaji wa Ikulu ya Marekani Sarah Sanders amesem: "Tunanazo taarifa kuhusu hatua za Korea Kaskazini za usiku huu. Tutaendelea kuzifuatilia."

Korea Kusini imesema makombora hayo yalirushwa kutoka mji wa Wonsan wa Korea Kaskazini milango ya saa tatu asubuhi leo saa za Korea. Korea Kusini imeeleza kwamba inafanya uchunguzi kuhusu makombora hayo, ikishirikiana na Marekani.

Waziri wa Ulinzi wa Japan amesema makobora hayo yameanguka karibu na pwani na nchi hiyo, na kwamba Japan haiko katika kitisho chochote cha usalama.

Ijumaa, Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kusini Kang Kyung-wha alisema Korea Kaskazini inalazimika kuonyesha "hatua za uhakika" za kusitisha shughuli zake za kinyuklia iwapo inataka kuondolewa vikwazo ilivyowekewa.

Mapema wiki hii, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kaskazini Choe Son Hui ameonya juu ya matokeo yasiyofurahisha iwapo Marekani haitobadilisha msimamo wake kuhusu vikwazo vya kiuchumi ilivyoiwekea nchi yake.

"Hatua hii inaonyesha wazi kwamba Korea Kaskazini imekasirishwa na msimamo wa Marekani wa kuishinikiza nchi hiyo kusimamisha mpango wake wa kinyuklia lakini bila ya kuikubalia kuiondolea vikwazi ilivyoiwekea," amesema Harry Kazianis wa gazeti la Marekani la masuala ya kimataifa la The National Interest.

Wachambuzi wanasema haijalishi ni makombora ya aina gani yaliyorushwa, ujumbe uliokusudiwa na Korea Kaskazini bila shaka  umeshaifikia Marekani.


Share:

Video: Richa Zone Ft. Janjaro - Tunapeta

Msanii wa muziki Bongo, Rich Zone anakukaribisha kutazama video ya wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Tunapeta akiwa amemshirikisha Dogo Janja. Itazame hapa.


Share:

Wananchi Wasisitizwa Kufuata na Kuzingatia Sheria za Uhifadhi

Naibu  Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu amewataka wananchi wafuate sheria  kwa kujiepusha kuendesha shughuli za kibinadamu ndani ya Hifadhi ili kujenga mahusiano mazuri baina yao na Wahifadhi.

Pia, amewataka  wananchi kuwachukulia Wahifadhi hao   kama rafiki wa umma na watendaji waliotumwa na Serikali kulinda Maliasili  kwa niaba yao.

Akizungumza na  Watumishi  wa Pori la Akiba la Swagaswaga katika wilaya ya Chemba  jijini Dodoma,  Mhe. Kanyasu amesema Wahifadhi wamepewa jukumu la   kulinda hifadhi za Taifa na wamekuwa  wakifanya kazi nzuri ya kuifanya Tanzania iendelee kuwa na maeneo mazuri yaliyohifadhiwa.

''Sisi ni wa moja hakuna haja ya kujengeana uhasama kati  yetu,  Wananchi wafuate sheria za Uhifadhi  na Wahifadhi fuateni sheria wakati mnapokabaliana na Wananchi'' amesisitiza Kanyasu.

Amesema Wahifadhi wa Wanyamapori na Misitu wanazilinda rasilimali hizo kwa ajili wote, vitu kama mvua, hali ya hewa safi pamoja na mvua ni moja ya faida za moja kwa moja zinazopatikana kutokana na maeneo yaliyohifadhiwa vizuri.

Amesema Wahifadhi hao wameajiriwa kwa mujibu wa sheria hivyo hutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia maadili ya kazi zao na pale wanapokiuka sheria mamlaka zinazohusika huwachukulia hatua.

“Sisi kama Wizara tunaamini kwamba wahifadhi wetu wanafanya kazi nzuri, pale ambapo wamekuwa wakilaumiwa kwa kuwapiga na kuwanyanyasa watu kwa namna yoyote ile tumetuma Tume maalum kuchunguza na kuchukua hatua” Amesema

Mhe, Kanyasu amesema uchunguzi unapofanyika na ikathibitika kuwa tukio lililofanyika halikuongozwa na matumizi ya sheria na kuwepo kwa haki wizara imekua ikichukua hatua.

Ameeeleza kuwa Wahifadhi ni watu muhimu saba kwa vile bila wao hakuna uhifadhi unaoweza kuendelea nchini akibainisha kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakipinga juhudi za uhifadhi kwa kuwatetea watu wanaovunja sheria.

Kuna watu wanatamani kuona  misitu na wanyamapori wote tunawamaliza ili wapate maeneo ya malisho na kilimo, Nawambieni tukithubutu kufanya hivyo huu ndo utakuwa mwisho wetu wa maisha" Amesisitiza Mhe.Kanyasu

Amesema yapo madhara makubwa yanayoweza kutokea kama hakutakuwa na uhifadhi imara ikiwemo maeneo mengi ya nchi kugeuka kuwa jangwa kutokana na uharibifu wa misitu, ukosefu wa mvua, ukosefu wa maji, chakula na ukosefu wa hewa safi.

Kwa upande wake, Meneja wa Pori la Akiba la Swagaswaga, Alex Choya  amesema kuwa kumekuwa na tuhuma za vitendo vya ukatili dhidi ya raia vinavyofanywa na baadhi ya askari wa hifadhi za Taifa na kutoa wito kwa wananchi wote wenye ushahidi na taarifa juu ya vitendo hivyo kuziwasilisha ili hatua stahiki zichukuliwe.

Amesisitiza kuwa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) hairuhusu askari kufanya vitendo vya ukatili na unyanyasaji dhidi ya raia badala yake imekua ikiwahamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika ulinzi wa rasilimali zinazowazunguka.


Share:

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini (THRDC) Waliomba Jeshi la Polisi kuchunguza Wakili aliyepotea Arusha

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini (THRDC) umeliomba Jeshi la Polisi, kufanya uchunguzi wa kutoweka kwa Wakili, Maneno Mbunda wa mkoani Arusha ili ajulikane alipo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Mei 3, jijini Dar es Salaam, Mratibu wa mtandao huo kitaifa, Onesmo Olengurumwa, amesema wamesikitishwa na taarifa za kutoweka kwa wakili huyo huku wakiviomba vyombo vya usalama kufanya uchunguzi wa haraka ili apatikane.

Amesema taarifa za kutoweka kwa Mbunda, ambaye pia ni Mwanasheria wa Hifadhi ya Wanyama  Arusha, zilitolewa Aprili 28 mwaka huu zinashangaza wengi na kuomba suala hilo lichukuliwe kwa uzito ili wakili huyo apatikane.

Olengurumwa amesema kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa rafiki wa karibu wa Wakili huyo,  magari yaliyotumika kumkamatia hayakuwa na namba za gari na alikamatwa eneo la USA River jijini Arusha, na hajulikani alipo hadi sasa.

“Matukio ya kupotea kwa watu na mawakili na watetezi wengine wa haki za binadamu yamekuwa yakiongezeka hapa nchini na hakuna jitihada zozote zinazochukuliwa na hata kupatiwa ufumbuzi wa kudumu.

“Ikumbukwe  kwamba ni takribani miaka minne sasa tangu wakili wa kujitegemea, Philibert Gwagilo, alipopotea na hadi sasa hajulikani alipo, matukio haya ya kupotea kwa watu yanapojitokeza ni lazima hatua za haraka za kiuchunguzi zichukuliwe ili kusaidia upatikanaji wake,” amesema.

Naye dada wa Wakili Mbunda, aliyejitambulisha kwa jina la Upendo, huku akibubujikwa na machozi amesema kaka yake alipotea tangu Aprili 28 mwaka huu, ma kwa mujibu wa maelezo ya rafiki yake aliyekuja kutoa taarifa nyumbani kwao alidai kuwa alikamatwa na watu waliojitambulisha kuwa ni maaskari.

Upendo amesema tangu tarehe hiyo mpaka leo kaka yake hajaonekana wala hawajafanikiwa kumpata katika kituo chochote cha polisi hapa nchini jambo ambalo anadai limewashtua na linaendelea kuwatia hofu kwakuwa hawana baba wala mama na walikuwa wakimtegemea yeye katika familia yao.

Hata hivyo namba ya Kamanda Polisi, Mkoa wa Arusha, ilipopigwa ili kuelezea tukio hilo kama wanalifahamu simu ilipokelewa na  mtu aliyejitambulisha kuwa ni msaidizi wake na kusema atamuelezea mkuu wake kuhusu suala hilo.


Share:

Rais Magufuli Akemea Tabia Ya Wanafunzi Kuendekeza Mapenzi Badala ya Kusoma

Rais John Magufuli amewataka wanafunzi wa vyuo vikuu kutumia muda wao vizuri kujisomea na kuwashukia walimu akiwataka kuwa wakali kwa sababu katika elimu hakuna siasa.

Ametoa kauli hiyo jana Ijumaa Mei 3 mkoani Mbeya katika Chuo cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (Must)  baada ya kukasirishwa na tabia ya wanafunzi kutumia muda wao kufanya mambo yasiyo ya msingi hasa kukumbatiana hadharani.

Akiwa katika ziara yake mkoani Mbeya, Magufuli amesema taifa linawekeza fedha nyingi kwa wanafunzi wakati zingeweza kwenda kwa watu wengine kama wakulima, wafugaji, wavuvi lakini imeamua kuziweka katika elimu kwasababu asilimia kubwa inatoka katika familia maskini.

“Mnapokuja hapa vyuoni msidanganyike na makundi, someni wanangu, nilipokuwa nikija hapa nilimuona kijana mmoja amekumbatiana na binti mmoja nikawa najiuliza huyu angekuwa binti yangu ningeteremka hapa ningewazaba vibao wote wawili.”

“Ndiyo ukweli nani atakubali binti yake ambaye amempeleka kusoma atembee njiani ameshikwa na lijamaa ambalo halijatoa hata mahari, lakini ni nani pia mzazi ambaye utamuona kijana wako umemtuma kwenda kusoma kazi yake iwe kukumbatia wasichana.”

 “Haya ndiyo matatizo muda mwingine wa vijana wetu, wanashindwa kuelewa walipotoka, walipo na wanakoelekea, Serikali inatumia fedha nyingi kukudhamini kukulipia kila kitu unafikiri huyo akienda darasani atafaulu hapana,” alisema.


Share:

Rais Magufuli Aipa TCU Siku 10.....Amtumbua Meneja wa TANESCO Mbeya

Rais John Magufuli, amemtumbua Meneja wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco), Mkoa wa Mbeya, kwa kushindwa kufika kwenye hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi kwa ajili ya upanuzi wa Kiwanda cha Saruji cha Mbeya.


Rais Magufuli alimwagiza Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani, kumhamisha mtendaji huyo kwa kushindwa kufika eneo hilo.

Aliagiza meneja huyo ambaye amefanya kazi katika Mkoa huo kwa miaka minne, atolewe arudishwe alikotoka na apangwe mtumishi mwingine atakayeshughulika na masuala ya umeme.

“Yuko wapi huyo Meneja wa Tanesco, angekuwa hapa si angejibu maswali, Waziri Lukuvi mpigie simu Kalemani, ateue Meneja mwingine wa Tanesco Mbeya kuanzia kesho (leo) aje aanze kazi mara moja,” alisema Rais Magufuli.

Alihoji sababu za meneja huyo kulala nyumbani ilihali mameneja wengine wa idara tofauti katika mkoa huo, walikuwa wamefika katika ziara yake hiyo.

“Mpaka meneja wa Baraza la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) yupo hapa nikimsimamisha kazi hapa nitakuwa nimefanya kosa? Wangapi wanakubaliana na mimi, safi kabisa, kuanzia leo yeye ‘out’ akajifunze vizuri kutafuta umeme hatufai tena hapa Mbeya,” Rais Magufuli alisema.

Pia Rais Magufuli aliahidi kufanyia kazi changamoto ya kukatika umeme katika kiwanda hicho linalosababisha hasara kwamba serikali italifanyia kazi.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli ameutaka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), kuboresha utendaji kazi wao na endapo wataendelea kuwa wazembe taasisi za umma ziwanyime zabuni za ujenzi.

Rais Magufuli aliyasema hayo jana jijini Mbeya wakati akiweka jiwe la msingi katika upanuzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia (Must) ikiwa ni siku yake ya tisa ya ziara zake mkoani humo.

“Natoa wito tena kwa mara ya pili kwa TBA waanze kujipanga, wasipofanya vizuri hata kama ni chombo cha serikali msiwape kazi,” alisema Rais Magufuli

Alisema TBA ina wajibu wa kutekeleza majukumu yao kwa wakati katika kazi wanazopatiwa ili kuwahisha miradi ya maendeleo.

“Kwanini mlihangaika kutafuta mkandarasi wa kufanya upembuzi yakinifu na kujenga maktaba wakati kuna wataalam wanafunzi ambao wangefanya kazi ya usanifu? Matokeo yake wamemtafuta mkandarasi aliyewachelewesha kwa miaka saba,” alisema Rais Magufuli.

Rais Maguli alihoji sababu ya kuendelea kuikumbatia TBA ambaye amechelewesha mradi huo kwa miaka yote ilihali wizara yenye dhamana ipo.

Alisema ujenzi wa jengo la maktaba katika chuo hicho, ulianza mwaka 2012 lakini haujakamilika kwa muda wa miaka saba.

Rais Magufuli alisema enzi za Hayati Mwalimu Julias Nyerere, chuo hicho kilijengwa kwa miaka minne kuanzia mwaka 1982 hadi mwaka 1986 lakini maktaba hiyo imejengwa kwa miaka saba na bado haijakamilika.

Aidha, aliahidi kusaidia kulipa deni linalodaiwa chuo hicho la Sh. bilioni 2.9 kwa ajili ya kumalizia kazi awamu ya pili na tatu ya ujenzi wa maktaba hiyo.

Alisema mkandarasi ameshalipwa Sh. bilioni 2.5 na bado hajapatiwa Sh. bilioni 2.9 kwa ajili ya kukamilisha kazi hiyo.

“Hizo Sh. bilioni 2.9 mwezi huu wa tano zitakuja zote sasa ole wenu mzichakachue. Tumuone na huyo mkandarasi kama atashindwa kumaliza kazi,” alisema Rais Magufuli.

Aidha, Rais Magufuli aliahidi kutoa Sh. bilioni 5 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ya chuo hicho ili kuwafanya wanafunzi wasome kwa uhuru.

Mbali na hilo, Rais Magufuli, aliwaagiza watendaji kumfukuza kazi mkandarasi raia wa China anayejenga barabara ya kuingia katika chuo hicho endapo ataendelea kusuasua kukamilisha mradi huo.

“Hela yote ipo, Sh. bilioni 10.4 ipo, tena mumwambie afanye kazi kwa saa 24 na huu mradi nitaufuatilia mimi. Wamezoea hawa watu wanaomba kazi wakipewa wanaanza kusua sua,” Rais Magufuli alisema.

Aidha, alimwagiza Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Prof. Charles Kihampa, kupeleka ithibati ya mitaala ya kufundishia fani walizoomba chuo hicho ndani ya siku 10.

Alisema uongozi wa chuo hicho umekuwa ukiomba ithibati kwa muda mrefu bila kupewa hali inayochelewesha kuongeza fani nyingine.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya May 4



















Share:

Friday, 3 May 2019

Mbunge wa Nsimbo atishia kuvua nguo bungeni kisa maji

Mbunge wa Nsimbo, Richard Mbogo (CCM), ametishia kuvua nguo bungeni ikibidi ili yapatikane maji safi na salama kwenye jimbo lake.

Mbogo ametishia hivyo wakati akichangia mjadala wa Wizara ya Maji bungeni leo Mei 3, ambapo amesema suala la maji halina mbadala hivyo Serikali itatue tatizo hilo jimboni mwake.

Amesema kama ilivyokuwa kwa mtumishi wa Mungu, Ibrahimu, alikuwa tayari kumchinja mwanawe, lakini baadaye Mungu alimpatia mwanakondoo wa kuchinja, mwanawe akanusurika.

“Mheshimiwa mwenyekiti, suala la maji safi na salama si la mzaha, ikibidi niko tayari kuvua nguo hapa bungeni ili nipate suluhisho la upatikanaji wa maji Nsimbo.

“Kama kuonyesha niko ‘serious’ kwa jambo hili niko tayari kufanya lolote, kama kuna jambo mnaweza kufanya mtuambie tufanye, tozo hii ya Sh. 50 ni muhimu sana,” amesema Mbogo.


Share:

Heche Apinga nyongeza ya Sh, 50 kwenye petroli na dizeli

Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche (CHADEMA), amepinga hoja ya baadhi ya wabunge wenzake wanaotaka nyongeza ya Sh, 50 kwa kila lita ya petroli na dizeli ili ziende kusaidia Mfuko wa Taifa wa Maji.

Heche ametoa kauli hiyo bungeni leo Mei 3, wakati akichangia mjadala wa Wizara ya Maji, ambapo amesema tozo hiyo sio dawa ya suluhisho la kupatikana kwa fedha za miradi ya maji kwani hata bajeti iliyopitishwa na Bunge kwa mwaka wa fedha 2018/2019 inaonyesha fedha zilitolewa ni pungufu.

“Mheshimiwa Mwenyekiti siungi mkono kuendelea kuwanyonga wananchi kwa kisingizio cha kuongeza fedha kwenye maji wakati hata tulizowaidhinishia hazijatoka.

“Niwaombe wabunge tuibane serikali itoe fedha, kila kitu tutakuwa tunaongeza kwenye mafuta hadi lita ifike Sh, 4, 000?,” amehoji Heche.


Share:

Breaking : HIACE MBILI ZAGONGANA NA KUUA WATU KIGOMA

Habari zilizotufikia hivi punde zinasema watu wanaokadiriwa kuwa Saba wamefariki dunia baada ya Hiace mbili kugongana katika kijiji cha Mlela wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma.

Taarifa za awali kutoka eneo la tukio ajali hiyo imetokea leo jioni Ijumaa Mei 3,2019 inaelezwa kuwa watu 7 wamefariki dunia na wengine  12 wamejeruhiwa na wamekimbizwa katika hospitali ya Rufaa  Maweni kwa ajili ya matibabu. 

Taarifa kamili tutawaletea hivi punde

Share:

RC ZAINAB TELACK AFUNGUA SOKO LA PILI LA MADINI MKOANI SHINYANGA


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akikata utepe kuashiria ufunguzi wa soko hilo
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wanunuzi wa madini aliyefungua soko leo
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akisisitiza jambo wakati akizungumza na wananchi waliohudhuria ufunguzi wa soko la pili la madini katika Mkoa wa Shinyanga leo tarehe 3 Mei, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga akiwasili katika eneo la soko la madini na kupokelewa na viongozi wa Chama cha wachimba madini Mkoa wa Shinyanga mapema leo tarehe 3 Mei, 2019.
Katibu wa Chama cha Wachimbaji madini Mkoa wa Shinyanga Bw. Gregory Kibusi akitoa neno katika ufunguzi wa soko la madini lililopo Wilaya ya Shinyanga leo tarehe 03 Mei, 2019.
Baadhi ya wananchi na wadau wa madini waliohudhuria ufunguzi huo wakimsikiliza mgeni rasmi Mhe. Mkuu wa Mkoa (hayupo pichani).
Mwenyekiti wa Chama cha Wachimba madini Mkoa wa Shinyanga Bw. Hamza Tandiko akizungumza katika tukio hilo mapema leo tarehe 03 Mei, 2019 - Picha ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga
****

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack amefungua soko la madini leo tarehe 03 Mei, 2019 katika Wilaya ya Shinyanga likiwa ni soko la pili baada ya soko jingine kufunguliwa Wilayani Kahama mwezi mmoja uliopita.

Akitoa hotuba ya ufunguzi wa soko hilo katika eneo la Ofisi ya CCM Mkoa ambapo wafanyabiashara tisa (9) wa Dhahabu na Almasi wamefungua masoko yao hapo, Mhe. Telack amesema tangu agizo la Mhe. Dkt. John Magufuli la kufungua masoko ya madini, tayari madini ya dhahabu yenye gramu 30,924.44 yameshauzwa katika soko la Kahama yakiwa na thamani ya sh. Bilioni 2.9.

Telack amewashukuru wafanyabiashara hao kwa kuitika wito wa Serikali na kufungua soko katika Mkoa wa Shinyanga.

Aidha, ametoa wito kwa wachimbaji wadogo, wauzaji na wanunuzi kutumia soko hilo la madini na waache kuuziana madini sehemu zisizo rasmi na atakayekamatwa anafanya hivyo madini yatataifishwa na wahusika watashtakiwa kwa mujibu wa sheria.

Kaimu Afisa Madini Mkazi Mhandisi Giliard Luyoka, akisoma taarifa ya madini Mkoa, amesema hadi sasa Mkoa una wafanyabiashara wakubwa 9 na wadogo 22 na kuwa licha ya Mkoa kuwa na utajiri wa madini yenye thamani ambapo wachimbaji wadogo wanazalisha wastani wa kilo 600 za dhahabu na karati 1300 za almasi kwa mwaka, hakukuwa na masoko rasmi ya uuzaji wa madini hivyo kupelekea utoroshwaji wa madini hatimaye Taifa kutonufaika na madini hayo.

Naye mwenyekiti wa Chama cha Wachimba madini Mkoa wa Shinyanga Bw.Hamza Tandiko amesema kuwa, wanaunga mkono juhudi za Serikali katika kuhakikisha madini yote yanayopatikana Mkoani Shinyanga yanawasaidia wananchi wa Mkoa huu kwa kuchangia pato la Taifa.

“Tuendelee kumuunga mkono Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, kufikia mwaka 2025 angalau sisi tuliopo kwenye sekta ya madini tuweze kuchangia angalau asilimia 10 ya pato la Taifa kwani Serikali imeonesha uzalendo kwa kufuta kodi hivyo deni limebaki kwetu” amesema Hamza.
Share:

KAMATI YA UONGOZI BUNGE LA AFRIKA YAKUTANA NA MABALOZI WA AFRIKA,MASELE ASEMA TABIA YA UBAGUZI NA UNYANYASAJI WA WAGENI HAIKUBALIKI AFRIKA

Kamati ya uongozi ya Bunge la Afrika ‘The Pan African Parliament Bureau’ imekutana na Mabalozi ‘Ambassadors’ wanaowakilisha mataifa mbalimbali barani Afrika katika nchi ya Afrika Kusini. 

Mkutano huo wa Bunge la Afrika na Mabalozi kimefanyika leo Ijumaa Mei 3,2019 katika Ukumbi wa Makao Makuu ya Bunge la Afrika kama sehemu ya mkutano wa maandalizi ya Mkutano wa Pili wa Bunge la Tano la Bunge la Afrika jijini Johannesburg Afrika Kusini.

Akizungumza wakati wa mkutano huo wa Mabalozi wa Afrika walioidhinishwa na Jamhuri ya Afrika Kusini, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika Mheshimiwa Stephen Masele ambaye ni mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini na Naibu Waziri wa zamani nchini Tanzania alisema Bunge la Afrika litajadiliana na kutoa Azimio juu ya tabia ya Xenophobic nchini Afrika Kusini.

“Suala hili linapaswa kuchukuliwa kwa umakini, kuna vitendo vya uhalifu vinavyofanywa na vikundi tofauti kutoka nje inaonekana kama Afrika Kusini haitaki wageni katika nchi yao… La hasha lakini kwa undani kuna matendo ya uharifu kwa kivuli cha Xenophobia”,alisema Mhe. Masele. 

“Ninafurahi na kuhamasishwa na hatua zilizochukuliwa na serikali ya Afrika Kusini ili kukabiliana na mambo yote ya uhalifu.Tutakuwa makini sana wakati tunajadiliana jambo hili kwa sababu hatutaki kuingilia kati mambo ya ndani ya Afrika Kusini au kuingilia kati vyombo vya usalama kutekeleza majukumu yao”,aliongeza.

Masele aliomba mamlaka ya Afrika Kusini kushughulikia suala la tabia ya Xenophobic katika Afrika kwani haikubaliki.

“Sisi kama Wabunge wa Afrika tunatarajia kuona hatua kali zikichukuliwa dhidi ya waharifu wote, wanaharibu sifa nzuri ya Afrika Kusini na Afrika. Bunge la Afrika litapaza sauti na kukemea suala hili..Vikwazo vya hali yoyote dhidi ya watu binafsi au nchi huumiza watu wasiokuwa na hatia hususani wanawake na watoto na huzuia jitihada za maendeleo za watu wetu na nchi ambazo zina vikwazo”,aliongeza.

Kikao cha Pili cha kawaida cha Bunge la Tano la Afrika kinatarajiwa kuanza mnamo Mei 6, 2019 huko Midrand - jijini Johannesburg Afrika Kusini.

Pamoja na mambo mengine , watajadiliana juu ya Kauli mbiu ya Umoja wa Afrika ya mwaka huu “Mwaka wa Wakimbizi na Watu Waliopotea",ambapo pia Bunge la Afrika litajadili Suluhisho la Kudumu juu ya tatizo la wakimbizi barani Afrika.

Hali kadhalika Bunge pia litajadili taarifa juu ya Amani na Usalama katika bara ikiwa ni pamoja na maendeleo ya hivi karibuni na hali ya kisiasa Libya, Sudan, Algeria na mchakato wa amani nchini Sudan Kusini. 

Masele anahimiza pande zote zinazohusika katika majadiliano ya amani kuwa zisio na upendeleo kwa lengo la kutimiza ahadi zetu kwa watu wa Afrika.

Angalia picha za matukio wakati wa mkutano

Wajumbe wa Kamati ya uongozi ya Bunge la Afrika na Mabalozi wanaowakilisha mataifa mbalimbali barani Afrika katika nchi ya Afrika Kusini wakiwa kwenye mkutano leo Ijumaa Mei 3,2019 jijini Johanesburg Afrika Kusini. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika Mheshimiwa Stephen Masele akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Makao Makuu ya Bunge la Afrika,Midrand,Johanesburg,Afrika Kusini.

Rais wa Bunge la Afrika,Mheshimiwa Roger Nkodo Dang kutoka nchi ya Cameroon akizungumza wakati wa mkutano wa Kamati ya uongozi ya Bunge la Afrika na Mabalozi wa nchi za Afrika nchini Afrika Kusini.

Kulia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika Mheshimiwa Stephen Masele akiandika dondoo muhimu wakati wa mkutano wa Kamati ya uongozi ya Bunge la Afrika na Mabalozi wa nchi za Afrika nchini Afrika Kusini.

Wajumbe wa Kamati ya uongozi ya Bunge la Afrika na Mabalozi wanaowakilisha mataifa mbalimbali barani Afrika katika nchi ya Afrika Kusini wakiendelea na mkutano.

Wajumbe wa Kamati ya uongozi ya Bunge la Afrika na Mabalozi wanaowakilisha mataifa mbalimbali barani Afrika katika nchi ya Afrika Kusini wakiwa wamesimama kuwakumbuka watu waliofariki dunia kutokana na majanga yaliyotokea katika baadhi ya nchi za Afrika yakiwemo mafuriko na Kimbunga Keneth.

Mkutano ukiendelea.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger