Wednesday, 1 May 2019

Waziri Mhagama Awaonya Waajiri Wote Kutonyanyasa Wanawake

NA.MWANDISHI WETU
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Jenista mhagama amewataka waajiri wote nchini kutonyanyasa wanawake katika masuala ya kazi ili kuwa na usawa maeneo ya kazi.

Ameitoa kauli hiyo hii jana tarehe 30 Aprili, 2019 alipokuwa akifungua semina ya siku moja ya viongozi wanawake kutoka vyama mbalimbali vya wafanyakazi nchini walipokutana kujadili masuala yanayowahusu wawapo kazini ikiwemo; haki na wajibu wao wawapo kazini iliyofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Paradise Inn Jijini Mbeya.

Waziri alieleza kuwa waajiri hawana budi kubadili mitazamo hasi iliyopo katika jamii ya kuona wanawake ni viumbe dhaifu na wenye majukumu mengi yanayoweza kukwamishi jitihada zao wawapo kazini badala yake wawaone kuwa ni viungo muhimu katika kuchangia uzalishaji na maendeleo nchini.

“Mchango wa wanawake ni mkubwa endapo utatambuliwa na kuthamini katika nyanja zote za ukuaji wa uchumi, hivyo ni vyema maeneo ya kazi waajiri watimize wajibu wao kwa kundi hili kwa kuzinigatia sheria zilizopo na wasinyanyaswe na waendelee kuheshimiwa na kupewa haki na stahiki zao kama wafanyakazi wengine.”alisisitiza Waziri Mhagama.

Waziri alieleza jitihada za serikali ni kuhakikisha inasimamia vyema sheria na taratibu za kazi nchini kwa kuliangalia kundi hili ili kuwa na waajiriwa wenye kuzingatia usawa wa kijinsia.

“Ninakemea vitendo vya unyanyasaji wa haki za wanawake kazini ikiwemo kukoseshwa haki zao na vyama hivi vya wafanyakazi viendelee kuleta tija katika kukemea matendo hayo,”alisistiza Waziri Mhagama.

Aidha Waziri aliwataka wanawake kuendelea kuvitumia vyama vya wafanyakazi kama jukwaa maalum la kueleza na kutatua changamoto zao.

Aliongezea kuwa, pamoja na changamoto wanazokutana nazo wanawake hawana budi kujiendeleza kielimu ili kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia yaliyopo katika masuala ya kazi.

“Wanawake umefika wakati kuendelea kujiendeleza katika eneo la elimu ili kuwa na vigezo mahususi vitakavyo wapa nafasi nzuri katika maeneo yenu ya kazi.”alisisema Waziri Mhagma.

Naye rais wa Shirikizo la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw. Tumaini Nyamhokya alimpongeza waziri pamoja na changamoto zilizopo katika kufikia haki sawa kwa wote , alieelza umuhimu wa kuendelea kuliinua kundi hili ili kuwasaidia wanawake wa Kitanzania katika kupata haki na usawa kwenye maeneo yao ya kazi.

“Wanawake wana uwezo mkubwa hivyo tuendelee kujali na kutunza nafasi zao wawapo kazini ili kuwezesha Taifa kuendelea kuwa na maendeleleo,” alisisitiza Nyamhokya.

Kwa upande wake Mwenyekiti Kamati ya Wanawake Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Bi. Rehema Ludanga alieleza kuwa, ni wakati sahihi kuendelea kuchangamkia fursa za maendeleo ikiwemo uanzishwaji wa viwanda vya wanawake vitakavyosaidia kuondokana na hali ya utegemezi na kuchangia katika ongezeko la uzalishaji nchini.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya May 1



Share:

Tuesday, 30 April 2019

MUUMINI ACHOMWA MOTO NA MCHUNGAJI KANISANI AKIOMBEWA MAPEPO


Taarifa kutoka mkoani Mara zinasema kwamba Kijana Frank Elias (22) mkazi wa Kakonko mkoani Kigoma, amelazwa hospitali akiwa na hali mbaya baada ya kuchomwa moto na mchungaji wake.

Tukio hilo limetokea Aprili 28 katika kanisa la Cag Calvari katika kijji cha Musati limethibitishwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara, Jma Ndaki, na kusema kwamba tayari Polisi wameshamkamata mchungaji huyo aliyejulakana kwa jia la Anna Butoke.

Asimulia alivyochomwa moto

Akisimulia tukio hilo jinsi lilivyokuwa, Frank amesema kwamba alienda kanisani hapo kuombewa kwa kuwa anasumbuliwa na kichwa, akaambiwa apige magoti na afumbe macho na kutii, ndipo akamwagiwa mafuta ya taa, alipowashiwa moto, akaanza kuungua huku akiombewa na kuambiwa kuwa mizimu yote itakwisha na atapona.

"Nilianza kuungua huku wao wakizidi kuomba, hali ikawa ngumu nikapiga kelele ndipo wakaanza kuuzima moto huku wakisema hiyo ni nguvu ya Mungu, watu wakaanza kujitokeza nikapelekwa Kituo cha Polisi Kenyana na kukimbizwa hospitali kwa matibabu”, amesema Frank

Naye Mchungaji Anna Butoke amekiri kuwa wao walikuwa wanachoma mikoba ya kijana huyo ajabu akawa anaungua yeye.

"Alifika kujaribu kutaka kuteketeza mchungaji na viongozi wengine lakini akazidiwa nguvu, tukamwambia alete vifaa vyake vya uchawi, tukavimwagia mafuta ya taa na kuwasha moto akiwa amevishika badala ya kuungua vifaa hivyo akawa anaungua yeye nasi tulishangaa”, amesema Mchungaji Anna.

Kamanda Ndani amesema kwamba jeshi la polisi linamshikilia Mchungaji huyo huku wakiendelea na uchunguzi kujua iwapo alishawahi kufanya matukio kama hayo siku za nyuma, na kuwataka wananchi kuwa makini na masuala ya imani kwani mengine yanaweza yakagharimu uhai wao.
Share:

WCF YASHINDA TUZO KATIKA MASUALA YA AFYA NA USALAMA MAHALA PA KAZI


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akimkabidhi Tuzo na Cheti Bw. Masha Mshomba
Mkurugenzi Mkuu wa WCF. Mfuko umekuwa Mshindi katika masuala ya afya na usalamakazini baina ya Taasisi za Bima na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. Tuzo hiyo imetolewa katika Maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi Duniani, 2019.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akimkabidhi Cheti cha ushiriki wa Siku ya Afya na Usalama Duniani Mkurugenzi wa Huduma
za Tiba na Tathmini Dkt. Abdulssalaam Omary jijini Mbeya.
Tuzo na Cheti katika masuala ya afya na usalama
kazini baina ya Taasisi za Bima na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.  Tuzo hiyo imetolewa katika Maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi Duniani,
2019.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama(wa kwanza kushoto) akipata maelezo ya Mfuko kutoka kwa Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Dkt. Abdulssalaam Omary (wa pili kulia) alipo tembelea banda hilo. Wa tatu kushoto ni Mwakilishi wa ILO Afrika Bw. Jealous G. Chirove na Naibu waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Anthony Mavunde (katikati kulia)
Mkurugenziwa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Bw. Masha Mshomba (katikati) akifurahiapamoja na wafanyakazi wa Mfuko baada ya Mfuko kuwa Mshindi katika masuala ya
afya na usalama kazini baina ya Taasisi za Bima na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.
Mkurugenzi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Bw. Masha Mshomba (wa pili kushoto) pamoja na wafanyakazi wengine wa WCF mara baada ya kupata Tuzo na Cheti cha ushindi wa huduma bora za Bima.
Wafanyakazi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) wakifurahia baada ya kupata wakifurahia
pamoja na wafanyakazi wa Mfuko baada ya Mfuko kuwa Mshindi katika masuala ya afya na usalama kazini baina ya Taasisi za Bima na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu Wenye Ulemavu), Stella Ikupa (aliyeketi) akipata maelezo ya mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kutoka kwa Mkurugenzi wa huduma
za Tiba na Tathmini Dkt. Abdulssalaam Omary (wa pili kulia) walipo tembelea banda hilo.
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini Dkt. Abdulssalaam Omary akimpa maelekezo Dkt. Kiva Mvungi kutoka Geita Gold Mine kuhusiana na viwango vya ulemavu kwa mujibu wa Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi.
Afisa Matekelezo Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bi. Amina Likungwala akitoa zawadi kwa wadau mbali mbali waliotembelea banda la WCF wakati wa maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya Duniani, 2019 yaliyofanyika kitaifa jijini Mbeya.
Wadau mbalimbali waliotembelea banda la Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) wakipata maelezo juu ya mafao na shughuli za Mfuko wakati wa maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya Duniani, 2019 yaliyofanyika kitaifa jijini Mbeya.
Afisa afya na usalama mahali pa kazi kutoka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi Bw. Robert Duguza akitoa maelezo juu ya huduma na mafao yatolewayo na WCF kwa mdau aliyetembelea banda la Mfuko huo.
Watu mbalimbali wakiendelea kutembela katika Banda la Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) wakati wa maadhimisho ya siku ya usalama na afya Duniani ambapo kitaifa imefanyia mkoani Mbeya. 
Afisa Mwandamizi, Afya na Usalama Mahali pa Kazi kutoka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, Bi. Tumaini Kyando akitoa maelezo ya Mafao yanayotolewa na WCF kwa wageni na wadau waliotembelea banda la Mfuko huo.
Meneja Tathmini, Vihatarishi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Bi. Naanjela Msangi akifafanua umuhimu wa kufanya tathimini ya vihatarishi katika maeneo ya kazi kwa wadau waliotembelea banda la Mfuko wakati wa maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya Duniani, 2019 yaliyofanyika kitaifa jijini Mbeya.
Afisa Mwandamizi wa Mahusiano kwa Umma kutoka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Bw. Sebera Fulgence akimkabidhi Kava la Gurudumu mdau aliyetembelea Banda la WCF.
Afisa Matekelezo Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bi. Amina Likungwala akitoa zawadi kwa wadau mbali mbali waliotembelea banda la WCF.
Baadhi wa WCF wakiwa katika banda lao.
Kikundi cha ngoma kikitumbuiza mbele ya Banda la Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya Duniani, 2019 yaliyofanyika kitaifa jijini Mbeya.
Share:

CHUO CHA UONGOZI WA MAHAKAMA LUSHOTO(IJA) CHAWANOA WADAU MBINU ZA KUENDESHA MASHAURI YA WATOTO


Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha,Mosses Mzuna akifungua mafunzo ya wadau wa haki za Mtoto katika mikoa ya Arusha na Manyara jijini Arusha ,kushoto ni Mratibu wa mafunzo,Mwanabaraka Mnyukwa na Mkurugenzi wa Chuo Kikuu Huria kituo cha Arusha,Marcel Masalu. 
Afisa Ustawi wa Jamii Mahakama ya Watoto Kisutu,Asha Mbaruku akizungumza wakati wa mafunzo ya wadau haki za mtoto yaliyoandaliwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto(IJA). 
Naibu Msajili Msajili wa Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam,Nyigulila Mwaseba akizungumza wakati wa mafunzo ya siku tano ya wadau haki za mtoto yanayofanyika jijini Arusha. 
Hakimu Mkazi wa Mahakama ya wilaya Arusha ,Chrisanta Chitanda akizungumza wakati wa mafunzo hayo. 
Hakimu Mkazi wa Mahakama ya wilaya Arumeru,Benard Nganga(katikati),Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo,Amelia Mushi(kushoto) na Hakimu Mkazi mahakama ya wilaya ya Arusha,Chrisanta Chitanda wakibadilishana mawazo wakati wa mapumziko .


Mwandishi Wetu,Arusha

Maafisa wa Mahakama wametakiwa kuwa makini katika kufatilia na kuendesha mashauri yanahusu watoto ili kulinda haki zao zinazotajwa katika mikataba ya kimataifa,katiba ya nchi na sheria mbalimbali.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya Arusha,Mosses Mzuna amesema hayo wakati akifungua mafunzo ya siku tano kwa Mahakimu,Waendesha Mashtaka wa serikali,Mawakili wa kujitegemea na maafisa ustawi wa jamii yanayofanyika jijini hapa.

Alisema katika kuweka umuhimu wa kulinda haki za watoto serikali ilianzisha mahakama ya watoto iliyoanzishwa kupitia ibara ya 97 ,Sura ya 21 ya mwaka 2009 na mafunzo hayo yamekuja wakati muafaka ili kuwapa uwezo maafisa wanaohusika katika mashauri ya watoto.

Mratibu wa mafunzo ambaye ni Mkufunzi katika Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto(IJA) walioandaa mafunzo hayo kwa kushirikiana na Mahakama nchini,Mwanabaraka Mnyukwa alisema mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo maafisa hao kuendesha mashauri wakiwa na uelewa wa sheria ya mtoto.

“Mtoto ni sehemu muhimu katika jamii kutokana na uwezo wao wanashindwa kujitetea dhidi ya matukio mabaya wanayotendewa ndio maana ipo sheria inayowalinda lakini inapotokea wamefanyiwa mambo ambayo ni kinyume cha sheria zifuatwe taratibu zinazostahili kuwalinda watoto na kuwaadhibu watuhumiwa,”amesema Mnyukwa.

Alisema wadau hao wanajengewa uwezo baada ya shirika la kimataifa linahusu watoto(UNICEF) kufadhili mafunzo hayo katika kanda za kimahakama kwenye mikoa ya Mbeya,Mara,Tanga,Tabora,Mwanza ,Dar es Salaam na sasa Arusha.

Naibu Msajili wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,Augustine Rwizile alisema Tanzania ikiwa mojawapo ya nchi nyingine duniani imeridhia mikataba ya kimataifa inayolinda haki za binadamu pamoja mtoto kwa ujumla.

Alisema licha ya changamoto ya watoto kushindwa kujieleza mahakamani kutokana na mazingira yalivyobado jamii na maafisa wanaohusika katika michakato ya mashauri hayo wanaowajibu wa kuhakikisha haki inatendeka. 
Share:

WAKALA WA SERIKALI MTANDAO WAJA NA MFUMO WA KUONGEZA UFANISI SERIKALINI


Mtendaji Mkuu wa Wakala, Dk. Jabiri Bakari,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kuwa Wakala wa Serikali Mtandao umetengeneza mfumo wa matumizi ya Tehama katika kuboresha utendaji kazi Serikalini.
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakifuatilia kwa usikivu Taarifa ya Mtendaji Mkuu wa Wakala, Dk. Jabiri Bakari, leo jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kuwa Wakala wa Serikali Mtandao umetengeneza mfumo wa matumizi ya Tehama katika kuboresha utendaji kazi Serikalini.
Sehemu ya wafanyakazi wa Wakala wa Serikali Mtandao wakifuatilia taarifa ambayo ilikuwa inatolewa na Mtendaji Mkuu wa Wakala, Dk. Jabiri Bakari, leo jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari

Picha na Alex Sonna-Fullshangwe blog

WAKALA wa Serikali Mtandao umetengeneza Mfumo Shirikishi wa Kusimamia Shughuli na Rasilimali za Taasisi (ERMS) utakaowezesha kusimamia, kufuatilia, kukagua na tathmini ya utekelezaji wa shughuli zote za umma kwa ufanisi.

Hayo yamebainishwa na Mtendaji Mkuu wa Wakala, Dk. Jabiri Bakari,wakati akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dodoma amesema kuwa hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa matumizi ya tehama katika kuboresha utendajikazi serikalini.

Dk.Bakari amesema kuwa wameamua kutumia utaalamu wetu wa kidigitali kutengeneza mfumo wa ERMS ambao ni dirisha moja linalounganisha shughuli zote za ndani ya taasisi kuongeza ufanisi katika utendajikazi na utoaji huduma bora kwa umma.

Aidha amesema kuwa kuwa mfumo huo utakuwa na moduli 18 zinazounganisha shughuli mbalimbali za utendajikazi zinazotegemeana kuwezesha kubadilisha taarifa miongoni mwa idara na kusimamia rasilimali watu, fedha na vitendea kazi.

Dk.Bakari amesisitiza kuwa mfumo huo unawezesha ushughulikiaji wa miamala kutoka idara moja hadi nyingine zikiwemo ankara za bidhaa na huduma, mapato na matumizi, ufuatiliaji na utekelezaji wa shughuli kulingana na mipango na bajeti.

"Pia utawezesha usimamizi wa majukumu ya watumishi, ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi, utekelezaji wa shughuli za manunuzi na utayarishaji wa taarifa mbalimbali za utendaji'',amesema Dk.Bakari

Hata hivyo amesema kuwa mfumo huu utawawezesha maofisa masuuli na watumiaji wengine wa mfumo kupata taarifa mbalimbali kulingana na mahitaji yao.

Dk. Bakari amesema kuwa mfumo huo wa ERMS unaweza kuunganishwa na kubadilishana taarifa na mifumo mingine mikuu ya serikali ikiwemo Mfumo Mkuu wa Uhasibu, Mfumo wa Usimamizi wa Taarifa za Rasilimaliwatu (HCMIS), Mfumo wa Malipo ya Serikali Kieletroniki (GePG), Mfumo wa Barua pepe Serikalini (GMS) na Mfumo wa Ofisi Mtandao.

Pia amesisitiza kuwa moduli za mfumo huo zinaweza kuongezwa au kupunguzwa bila kuathiri utendaji kazi wa moduli nyingine au mfumo kwa ujumla.

Amezitaja baadhi ya mifumo mingine ambayo wakala umeitengeneza katika utekelezaji wa jitihada za serikali mtandao ambao ni tovuti kuu ya serikali, tovuti kuu ya ajira, mfumo wa barua pepe serikalini ambao unatumiwa na taasisi za umma 402 zikiwemo ofisi za ubalozi nje ya nchi kwa ajili ya kubadilishana taarifa serikalini.

Aidha Dk. Bakari amezitaka taasisi za umma kuendelea kutumia tehama katika kuboresha utendaji kazi serikani na utoaji huduma kwa umma kwa kuzingatia miongozo na viwango vya serikani mtandao.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger