Wednesday, 3 April 2019

Ngoma Mpya ya Asili : NYANDA MADIRISHA OBHADO - BHADEMI


Hii hapa ngoma mpya ya Nyanda Madirisha Obhado 'Maliganya' inaitwa Bhademi... Bonge moja la ngoma Mwanawane..Itazame hapa chini
Share:

Video Mpya : NYANDA MAJABALA 'KISIMA' - TANZANIA KWANZA


Hii hapa video mpya ya Nyanda Majabala ' Kisima' inaitwa Tanzania Kwanza
Share:

Ngoma Mpyaaaa!!!! KISIMA - LIMI


Hii hapa ngoma nyingine kali na matata ya Msanii wa Nyimbo za asili Kisima  inaitwa Limi... Ngoma  kali balaa mtu wangu..
Itazame hapa chini

Share:

Ngoma Kali Balaa!! KISIMA - WATOTO WA MITAANI......DUDE KALI KINOMA NOMA


Hii hapa video mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Kisima kutoka mkoani Simiyu inaitwa Watoto wa Mitaani
Share:

Ngoma Mpya ya Asili : KISIMA - MBINA



Nakualika kutazama video mpya ya Msanii wa nyimbo za asili Nyanda Majabala 'Kisima The Greatest Singer' kutoka mkoani Simiyu, inaitwa Mbina... Ngoma kali sana mtu wangu,itazame hapa chini

Share:

MECHI YA SIMBA NA JKT YAAHIRISHWA


Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Simba na JKT Tanzania uliokuwa upigwe katika dimba la Jamhuri mjini Morogoro, umeahirishwa kutokana na mvua.

Mvua kubwa iliyonyesha mchana mjini Morogoro, imesababisha Uwanja wa Jamhuri kujaa maji kiasi cha mpira kushindwa kudunda. Baada ya kusubiri kwa nusu saa, wasimamizi wa mechi wakaamua kuahirisha na kuahidi kuupangia ratiba nyingine.

Charles Mwakambaya ambaye ni Katibu wa chama cha soka mkoani Morogoro na msimamizi wa TFF kituo cha Morogoro, akizungumza baada ya mchezo kuahirishwa amesema kuwa hawatoweza kuipangia ratiba Simba kucheza kesho kwa sababu ya mchezo wa Klabu Bingwa Afrika, Jumamosi dhidi ya TP Mazembe.

"Hatuwezi kusema kuwa mchezo uchezwe kesho kwa sababu Simba ina ratiba ya mchezo wa TP Mazembe Jumamosi hii, kwahiyo wakicheza kesho tutakuwa tumewanyima masaa 48 ya kujiandaa dhidi ya mchezo mwingine", amesema Mwakambaya.

Kuhusu mashabiki ambao walishalipia tiketi zao, Mwakambaya amesema kuwa hela hazitorudishwa lakini utafanyika utaratibu mzuri na mambo yatakuwa sawa kwa mashabiki hao.

Simba sasa itarejea Jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo huo wa Klabu Bingwa Afrika dhidi ya TP Mazembe ambao inaelezwa kuwa wameshatua nchini.
Share:

Picha : RAIS MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA BARABARA YA MTWARA-NEWALA-MASASI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na Viongozi wengine wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mkoa wa Mtwara, Wabunge na viongozi wengine akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mitambo itaayotumika katika ujenzi wa Barabara ya Mtwara-Newala-Masasi km 210 sehemu ya Mtwara-Mnivata km 50 katika hafla iliyofanyika sehemu ya Naliendelea mkoani Mtwara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na Viongozi wengine wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mkoa wa Mtwara, Wabunge na viongozi wengine akivuta utepe kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Barabara ya Mtwara-Newala-Masasi km 210 sehemu ya Mtwara-Mnivata km 50 katika hafla iliyofanyika sehemu ya Naliendelea mkoani Mtwara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa Naliendele mkoani Mtwara kabla ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Barabara ya Mtwara-Newala-Masasi km 210 sehemu ya Mtwara-Mnivata km 50.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wanachi wa Naliendele mkoani Mtwara wakati akielekea kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Barabara ya Mtwara-Newala-Masasi km 210 sehemu ya Mtwara-Mnivata km 50.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wanachi wa Naliendele mkoani Mtwara wakati akielekea kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Barabara ya Mtwara-Newala-Masasi km 210 sehemu ya Mtwara-Mnivata km 50.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mbunge wa zamani wa Mtwara mjini Murji mara baada ya kuweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi huo wa barabara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Nanguruwe mkoani Mtwara wakati akielekaea Newala.
Wananchi wa Nanguruwe Mtwara vijijini wakishangilia mara baada ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuwatatulia sehemu itakapojengwa hospitali katikka eneo hilo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Nanyamba mkoani Mtwara wakati akielekea Newala. PICHA NA IKULU
Share:

NCHI HAINA TAZIZO LA MZUNGUKO MDOGO WA FEDHA

Serikali imesema kuwa kwa sasa nchi haina tatizo la mzunguko mdogo wa fedha katika soko kutokana na hatua mbalimbali ilizozichukua kukabiliana na tatizo hilo ikiwemo kuongeza ukwasi kwenye uchumi.


Hayo yameelezwa leo Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Momba Mhe. David Silinde (Chadema), aliyetaka kujua sababu za mzunguko mdogo wa fedha.

Dkt. Kijaji alisema kuwa, katika kutatua changamoto ya kupungua kwa mzunguko wa fedha katika soko, Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ilichukua hatua  mbalimbali za kuongeza ukwasi kwenye uchumi ikiwemo kushusha riba ya Benki Kuu (discount rate) kutoka asilimia 16 kwa mwezi Machi, 2017 hadi asilimia 7, Agosti 2018.
“Benki Kuu ilipunguza kiwango cha kisheria cha sehemu ya amana kinachotakiwa kuwekwa Benki Kuu na mabenki ya biashara(Statutory Minimum Reserve Requirement, (SMR)) kutoka asilimia 10 hadi asilimia 8 mwezi April 2017 pamoja na kuruhusu mabenki kutumia asilimia 10.0 ya sehemu ya SMR kama chanzo kimojawapo cha kusaidia hali ya ukwasi kwenye uchumi”, alisema Dkt. Kijaji.
Alisema Benki Kuu ilianzisha utaratibu wa kutoa mikopo ya muda maalumu kwa mabenki pamoja na kununua fedha za kigeni kutoka kwenye soko la jumla la mabenki ili kuongeza ukwasi kwenye uchumi.
Alifafanua kuwa mzunguko wa fedha katika uchumi unaendana na malengo pamoja na mahitaji halisi ya shughuli za kiuchumi zizopo kwa sasa.
Aidha, Dkt. Kijaji alisema Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania inatekeleza Sera ya Fedha inayolenga kusimamia mzunguko wa fedha unaoendana na mahitaji halisi ya uchumi kwa lengo la kudumisha utulivu wa mfumuko wa bei na hivyo kuweka mazingira mazuri ya ukuaji wa uchumi.
Na Josephine Majura, WFM, Dodoma
Share:

SERIKALI: WAZABUNI WATIA KIBINDONI SHILINGI BILIONI 199


Serikali imeleeza kuwa imeshawalipa Wazabuni 2048 kiasi cha Shilingi 199 tangu kutolewa kwa tamko la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 3 Januari, 2018 Ikulu Jijini Dar es Salaam la kutaka Wazabuni wote wanaoidai Serikali walipwe.

Hayo yameelezwa Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa (CCM), Mhe. Ritta Kabati, aliyetaka kujua baada ya tamko la Mhe. Rais kuhusu Wazabuni wote wanaoidai Serikali walipwe ni Wazabuni wangapi wameshalipwa.

Akijibu swali hilo Dkt. Kijaji alieleza kuwa kati ya Wazabuni 2048 waliolipwa na Serikali, Wazabuni 1,277 walihudumia Sekretarieti za Mikoa na 771 walihudumia Wizara, Taasisi na Wakala za Serikali.

Dkt. Kijaji alifafanua kuwa Shilingi 3,729,605,175 zimetumika kulipa Wazabuni waliotoa huduma kwa Sektretarieti za Mikoa na Shilingi 195,334,409,791.64 zimetumika kulipa Wazabuni wa Wizara, Taasisi na Wakala za Serikali.

“Ikumbukwe kuwa madeni yote haya yalilipwa baada ya uhakiki kufanyika”, alisisitiza Dkt. Kijaji.

Aliongeza kuwa Serikali itaendelea kulipa madai mbalibmali ya wazabuni kulingana na upatikanaji wa fedha, sambamba na uhakika wa madai husika.

Dkt. Kijaji amesema kuwa ili kukamilisha zoezi la uhakiki kwa wakati, wazabuni wote wanatakiwa kutoa ushirkiano, hususan kuwasilisha taarifa na vielelezo sahihi vya madai yao pindi wanapotakiwa kufanya hivyo.

Katika swali la nyongeza Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Kabati alitaka kujua vigezo vilivyotumika kuwalipa wazabuni hao.

Akijibu swali hilo la nyongeza Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji alisema kuwa vipo vigezo vingi ambavyo Serikali imevitumia kulipa madeni hayo moja ikiwa umri wa deni, madeni ambayo yamekaa kwa muda mrefu na ambayo tayari yamehakikiwa ndiyo yanapewa kipaumbele katika malipo.

Aliongeza kuwa kigezo cha pili ni riba Serikali imekuwa ikitoa kipaumbele kwa madeni ambayo riba yake inakuwa kulingana na muda, ili Serikali isiendelee kuumia wala mwananchi asiendelee kuumia.

Na Farida Ramadhani na Josephine Majura, WFM, Dodoma
Share:

Spika Ndugai kuwataja wabunge waliotelekeza watoto

Spika wa Bunge, Job Ndugai, amesema anayo orodha ya baadhi ya wabunge waliotelekeza watoto hivyo amewataka wahusika kulimaliza suala hilo kabla hajawataja.

Spika Ndugai ametoa kauli hiyo bungeni leo wakati wa kipindi cha maswali na majibu mara baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola kujibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Tauhida Galloos (CCM), aliyetaka kujua Serikali ina mkakati gani juu ya raia wa kigeni wanaopewa vibali vya kuja kufanya kazi nchini kwa muda na kuwazalisha watoto.

Akijibu swali hilo Lugola amesema sheria tayari ipo hivyo aliwaomba kina mama ambao wamekimbiwa wafuate sheria.

“Sheria tayari tunayo, niwaombe kina mama wote ambao wameathirika na jambo hili kwa kuwa ni la jinai waende katika vituo ambavyo vipo jirani wafungue kesi ili serikali tutumie kesi hizi kuwarejesha nchini wajibu mashtaka,” amesema Lugola.

Baada ya kujibu swali hilo, Spika Ndugai alisem; “Nakubaliana kabisa na maneno ya Waziri wa Mambo ya Ndani kwa asilimia 100 na mimi nishuhudie ninayo mawasiliano kadhaa ya kina mama kutoka sehemu mbalimbali za nchi wakiwalalamikia wabunge wanaume kutelekeza watoto.

“Naomba kila anayehusika na jambo hili achukue hatua ipo siku hapa nitakuja na orodha patakuwa hapatoshi hapa,” amesema Spika Ndugai


Share:

Spika Ndugai Aanika Madeni ya Mbunge Godbless Lema.....Amtimua Mbunge wa CHADEMA

Spika Job Ndugai ameagiza Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA), afike mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge leo saa 8:00 mchana kujibu tuhuma zinazomkabili za kulidharau na kulidhalilisha Bunge

Spika amesema kuwa Bunge analoliongoza si dhaifu na yeyote atayeingia kwenye 18 zao anaalikwa kwenye mchezo huo.

Aidha, asemema huwa Mbunge huyo wa Arusha Mjini ana msongo wa mawazo kwani tangu aingie Bungeni, amekopa Tsh. Milioni 644.

 
“Yapo mambo ambayo hawasemi wacha tuseme kidogo amekopa Sh 644 milioni…Sasa hivi ameshalipa lipa zimefika Sh 419 milioni huu ni msongo wa mawazo ndio maana anafika mahali anajilipua tu na kadhalika,”amesema.

Katika hatua nyingine amemfukuza ndani ya Ukumbi wa Bunge, Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko(CHADEMA) baada ya kupiga kelele kumpinga kiongozi huyo kutaja deni la Lema.


Share:

WANANCHI KAGEZI WAISHUKURU SERIKALI KWA KUWAPATIA KITUO CHA AFYA

Wananchi wa kijiji cha Kagezi wilayani Kibondo Mkoani Kigoma Wameishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kupanua majengo katika Zahanati yao na kuifanya zahanati hiyo kuwa kituo cha Afya kinachotoa huduma zote.

Wananchi hao walisema wamekuwa wakiteseka kutembea mwendo wa masaa manne kufuata huduma wilayani kwa kuwa huduma zilizokuwa zikitolewa katika zahanati ni za awali tu lakini endapo kituo hicho kitakamilika wana hakika ya kupata huduma bora na kupunguza changamoto zilizo kuwepo.

Silvanus Ntabandi ambaye ni Mkazi wa Kagezi alisema mwanzoni wanawake wote walikuwa wanakwenda kujifungulia katika hospitali ya Wilaya, wapo baadhi walikuwa wanapoteza maisha kutokana na kukosa huduma mapema lakini kwa sasa serikali imeamua kujenga kituo cha afya ambacho kitatoa huduma zote.

Aidha aliiomba Serikali kuongeza watumishi na kuhakikisha kituo hicho cha Afya kinafanya kazi siku zote, tofauti na sasa ambapo kituo hicho kinafanya kazi Jumatatu hadi Ijumaa tu na wao wanahitaji huduma hiyo siku zote.

Justina Gerald alisema kwa sasa hali ni safi katika kijiji hicho na huduma zimesogezwa karibu serikali inawajali na kuhakikisha watu wote wanapata huduma karibu na maeneo yao na kuhakikisha hakuna mtu anapoteza maisha kwa kukosa huduma.

Alisema ukifika katika kituo hicho cha afya sasa hivi wanapatiwa dawa zote kwa wakati na watu wanatibiwa tofauti na mwanzo ulikuwa ukiwa na mgonjwa ambaye ana shida sana wanalazimika kumkimbiza hospitali ya wilaya ili aweze kupata huduma.

Hata hivyo aliiomba Serilika kuwasaidia kupata gari lingine la kubebea wagonjwa kwa kuwa gari lililopo linatumiwa na vijiji vitatu na watu ni wengi na wanahitaji gari kwa kipindi hiki ambacho huduma hazijaanza kutolewa iliwaweze kusafirisha wagonjwa wanaoshindwa kupata huduma katika kituo hicho.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa wilaya ya Kibondo Daudi Mapunda ujenzi wa kituo cha afya Kagezi ulianza Februari 2018 na mpaka Juni wanatarajia majengo yawe yamekamilika na kuanza kutoa huduma.

Alisema ujenzi huo umefadhiliwa na serikali ya awamu ya tano, kupitia mfuko wa kuboresha huduma za afya na awamu hii wamepokea kiasi cha shilingi milioni 620 zitakazotumika kujenga jengo la huduma ya baba mama na mtoto, jengo la upasuaji, jengo la kuhifadhia maiti, jengo la kufulia, jengo la wodi ya watoto , wazazi na jengo la nyumba ya mganga.

Mpaka sasa ujenzi wa kituo hicho cha afya umekamilika kwa asilimia 90% shughuli zilizobaki ni ndogo na katika fedha hizo wanatarajia kuokoa kiasi cha fedha kitakacho baki na kitafanya shughuli nyingine katika kituo hicho.

Mbali na fedha hizo serikali kupitia wakala wa madawa na vifaa tiba wametoa kiasi cha shilingi milion mia nne kwa ajili ya upatikanaji wa vifaa tiba vyote na baada ya majengo hayo kukamili wananchi wataanza kupata huduma zote.

Alisema kituo hicho kikikamilika kitaanza kutoa huduma za Upasuaji na huduma zote za muhimu kwa kuwa vifaa vyote vinaletwa pamoja na wataalamu wa vifaa hivyo.

Hata hivyo Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kibondo, Hamis Tahilo aliwapongeza wasimamizi wa miradi hiyo na kuwaomba wananchi kutumia vizuri majengo hayo kwa kuwa serikali inajitahidi kuboresha hudima za afya na wananchi wanatakiwa kulinda miundombinu.

Alisema Serikali ya Chama Cha Mapinduzi iliahidi kuboresha huduma za afya na sasa wamejitahidi kufanya hivyo na kuwaomba wananchi kuendelea kuwa na imani na chama hicho kwa kuwa ni chama kinachowajali wanyonge.
Na Rhoda Ezekiel - Kigoma 
Wajumbe wa kamati ya siasa ya Wilaya ya Kibondo wakiongozwa na Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Kibondo Daudi Mapunda katika ukaguzi wa Kituo cha Afya Kagezi.
Share:

Waziri Mkuu Amuahidi tiketi ya ndege Pierre Konki Liquid kwenda kuishabikia Taifa Stars AFCON

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa Pierre Liquid ataambatana na Timu ya Taifa, Taifa Stars katika fainali za AFCON zitakazofanyika nchini Misri.

Amemhakikishia hilo wakati akizungumza naye katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma, ambapo Piere alikwenda kutembelea kwa mwaliko wa Spika wa Bunge, Job Ndugai.

Hayo yanajiri ikiwa zimepita siku kadhaa tangu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kutoa kauli ya kukosoa tabia ya watu kuvipa muitikio mkubwa vitu visivyo na msingi, akitolea mfano Mchekeshaji huyo aliyejizolea umaarufu kwenye vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii.

Katika hafla iliyoandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo ambayo ilikuwa na malengo ya kutokomeza ziro katika wilaya hiyo, Makonda alisema kwamba watu wa 'hovyo' kama Pierre hawapaswi kupewa nafasi kwenye vyombo vya habari, hali iliyozua gumzo kubwa.


Share:

Rais wa Algeria Bouteflika atangaza kujiuzulu

Rais wa Algeria Bouteflika (82) ambae anatumia wheelchair kutembelea amejiuzulu wadhifa wake baada ya kukaa madarakani kwa miaka 20, hatua hiyo inakuja baada ya Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Algeria Ahmed Gaid Salah kumtaka Rais huyo ajiuzulu haraka iwezekanavyo.

Kulikuwa na shangwe na vifijo kwenye mji mkuu Algiers baada ya kutangazwa uamuzi huo jana usiku. Televisheni ya taifa ilitangaza kuwa Bouteflika alilishauri rasmi Baraza la Katiba kuwa anaachia madaraka kama Rais wa Algeria. 

Alisema uamuzi huo uliochukuliwa kwa dhati unalenga kuchangia katika kuituliza mioyo na fikra za Waalgeria, na kuwawezesha kuiongoza Algeria kuwa na mustakabali mzuri na ambao wana haki ya kuufanikisha. 

Video ilimuonyesha Bouteflika, akiwa kwenye kiti cha walemavu, akikabidhi barua yake ya kujiuzulu kwa mkuu wa Baraza la Kikatiba Tayeb Belaiz.


Share:

Rais Magufuli atoa onyo kwa Wakurugenzi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amewaonya Wakurugenzi ambao watanaoesha nia kudai ushuru kufuatia uamuzi wa Serikali, kununua zao la korosho kwa bei elekezi ya shilini 3300, baada ya mvutano wa muda mrefu baina ya wakulima na wafanyabiashara wa korosho.
 
 Magufuli ametoa kauli hiyo akiwa mkoani Mtwara wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa barabara kutoka Mtwara kuelekea Newala na Masasi, ambapo amesema serikali haiwezi kuamua kuwasaidia wananchi halafu Halmashauri ijitokeze kutaka ushuru.
 

"Halmashauri mmeshindwa kusimamia korosho, baada ya kupewa bei nzuri wanapewa 1500, tukasema hapana tukakopa ili tuwalipe, nione Mkurugenzi ananiomba hizo hela, aone kama ataendelea kuwa Mkurugenzi, utaombea kijijini ukiwa unalima".
 

"Haiwezi Serikali imepanga bei ya korosho 3300, halafu ianze kulipia kodi kwenye Halmashauri ambayo ilishindwa kununua korosho, mkitaka ushuru msimamie vizuri bei ya korosho, siwezi nikakusanya hela mikoa mingine nije niwalipe nyinyi."Amesema Rais Magufuli


Share:

Rais Magufuli Akerwa na Wakandarasi Wasiofanya Kazi Zao Vizuri na Kwa Wakati

Rais John Magufuli amewajia juu wakandarasi wasiofanya kazi zao vizuri na kwa wakati na kuitaka Wizara ya Ujenzi kuwachukulia hatua za kisheria ikibidi wafukuzwe kazi kwani wameifanya Tanzania ni nchi ya majaribio.

Ametoa kauli hiyo leo jumatano Aprili 3, wakati akizungumza na wananchi katika ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani Mtwara ambapo ameweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Barabara kutoka Mtwara -Newala – Masasi yenye urefu wa kilomita 210.

“Wakandarasi mliosajiliwa katika nchi hii mbadilike na wizara muendelee kutumia sheria namba 17 ya mwaka 1997 na wale wasiofanya kazi vizuri wafukuzwe Tanzania isiwe nchi ya majaribio, Oktoba nitatenga muda kuja kuangalia kama huu mradi umekamilika na ole wenu nikute haujakamilika tutazungumza lugha nyingine.

“Tunataka lami na nikuombe Waziri pamoja na kazi nzuri mnayoifanya katika bajeti ya mwaka huu muhakikishe mnatangaza kilomita nyingine 50 kwenda mbele na mwaka mwingine tena 50 au 100 itategemeana fedha tutakazokuwa nazo,” amesema

Aidha amewataka wananchi wa Mtwara kudumisha amani na mshikamamo kati yao na kuachana na tabia ya kubaguana ili waweze kusaidiana kukuza uchumi wa nchi kwa kufanya kazi kwa pamoja.

“Tukishakuwa na miundombinu mizuri, umeme na maji Mtwara patakuwa ni mahali ambapo kila mtu atataka kupakimbilia endeleeni kuwa na mshikamano msibagueni kwaajili ya vyama wala dini mimi ni rais wa wote lengo ni kupeleka maendeleo ya nchi mbele,” amesema


Share:

Jeshi La Polisi Mkoa Wa Kigoma Limefanikiwa Kuuwa Majambazi 24, Kukamata Silaha 14 Aina Ya Smg Na Risasi 350.

Jeshi la Polisi Tanzania limeendesha Operesheni sehemu mbalimbali za nchi ili kupambana na wahalifu waliokuwa wanavamia majumani na kuteka magari njiani kwa kutumia silaha za moto.

Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi Nchini  CP, Liberatus Sabas amesema operesheni hiyo iliyofanika katika Mkoa wa Kigoma imefanyika ndani ya miezi mitatu ambayo ilianza mwezi wa kwanza mpaka mwezi wa tatu mwaka huu na kufanikiwa kukamata silaha 14 aina ya SMG na risasi 350 pamoja na mafanikio hayo Jeshi la Polisi limefanikiwa kuua majambazi 24 katika majibizano ya kurushiana risasi na polisi ambapo katika mapambano hayo askari wawili walijeruhiwa na majambazi ila mpaka sasa wanaendelea na matibabu.

Aidha kamishna Sabas, amesema wahalifu hao wanaotoka nchi za jirani ambazo hazina utulivu wa kisiasa, huku akiwaonya wahalifu hao wanaotoka  nchini jirani kuwa wajue wataingia ila hawatatoka na wakae wakijua hakuna mwalifu atakaebaki salama pia akiwataka wale wanaoingia nchini kwa kutumia miamvuli ya wakimbizi na wao hawatakuwa salama kwani wakae wakijua Tanzania ni kisiwa cha amani.

Kamishna Sabas amewataka  wananchi kuendelea kutoa ushirikiano baina yao na Jeshi la Polisi ili kukabiliana na wahalifu wa ndani na wale wanaotoka nje ya nchi na kuwatumia salamu kuwa Tanzania si sehemu salama kwa wahalifu.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger