Saturday, 19 January 2019

Shambulizi la Kigaidi Kenya :Washukiwa sita wafikishwa mahakamani

Washukiwa sita, akiwemo raia wa Canada, wamefikishwa mahakamani Ijumaa nchini Kenya, kuhusiana na shambulizi la kigaidi kwenye hoteli moja mjini Nairobi na kusababisha vifo vya watu 21.

Watuhumiwa hao wametajwa kuwa Joel Ng’ang’a Wainaina, Oliver Kanyango Muthee, Gladys Kaari Justus, Osman Ibrahim, Hussein Muhamed na Guleid Abdihakim ambaye ni raia wa Canada.

Jaji wa mahakama alikubali ombi kutoka kwa upande wa mashtaka kutaka watuhumiwa hao wanne na mwanamke mmoja kubaki chini ya ulinzi kwa siku 30 wakati uchunguzi ukiendelea. Mtuhumiwa wa sita atafikishwa mahakamani wiki ijayo.

Watuhumiwa wanashutumiwa kuhusu ‘uwezekano wa kuhusika’ katika shambulizi la takriban saa 20 kwenye hoteli ya Dusit D2 na jengo la ofisi ambalo mshambuliaji bomu wa kujitoa mhanga na watu wanne walio kuwa na silaha waliuawa na majeshi ya usalama, nyaraka iliyotolewa mahakamani imesema.

“Uchunguzi kuhusiana na suala hili una mambo mengi na ni wa kimataifa na huenda ukahitaji muda zaidi na rasilimali ili kubaini mtandao mzima wa kihalifu,” taarifa kutoka kwa mkurugenzi wa mashtaka, Noordin Haji imesema.

Washukiwa 11 walikamatwa Jumanne baada ya shambulizi, hata hivyo uchunguzi kuhusiana na washukiwa wengine bado unaendelea.

Mtuhumiwa Wainaina anadaiwa ni dereva wa taxi ambaye aliwapatia usafiri washambuliaji mara kadhaa sehemu mbali mbali mjini, na Muthee ni dereva mwingine ambaye aliwapeleka baadhi ya washambuliaji kwenye eneo la tukio.

Mwanamke pekee katika kundi hili la watuhumiwa Gladys Justus anachunguzwa kwa kuhusika katika kutuma fedha, wakati raia wa Canada, Guleid Abdihakim anachunguzwa kwasababu ya mawasiliano yake na baadhi ya watuhumiwa.

Ibrahim anadaiwa kuwa alikutana na mmoja wa washambuliaji Januari 8.

Muhamed simu yake ilionyesha mawasiliano na baadhi ya wanamgambo wa kiislamu na atafikishwa mahakamani wiki ijayo siku ya Jumatano.

Washukiwa wawili bado hawajafikishwa mahakamani, Ali Salim Gichunge na Violete Kemunto Omwoyo ambayo wana kadi za simu ambazo zinaonyesha walikuwa na mawasiliano ya mara kwa mara na baadhi ya namba nchini Somalia, nyaraka za mahakama zimeonyesha.

Shambulizi ambalo inadaiwa lilifanywa na kundi la wanamgambo wa kiislamu la al-Shabaab la Somalia, lenye uhusiano na al-Qaeda limehusika kuilenga Kenya mara kwa mara katika mashambulizi.

Mwaka 2013 kundi hilo lilifanya shambuliz kwenye eneo la maduka la Westgate mjini Nairobi na kusababisha watu 67 kupoteza maisha, wakati mwaka 2015 kundi hilo liliua watu 18 katika chuo kikuu cha Garissa, mashariki mwa Kenya.

Credit: VOA


from MPEKUZI http://bit.ly/2ARPpQW
via Malunde
Share:

Alichokisema Spika Ndugai Sakata la Zitto Kabwe Kutishiwa Kuuawa

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai, ametoa kauli yake baada ya Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Zuberi Kabwe kulalamika kutishiwa uhai na mtu wa usalama wa Taifa ndani ya viwanja vya Bunge siku ya jana Januari 18, mpaka kufikia hatua ya kumuandikia Spika Barua.

Spika Ndugai amesema kwamba barua hiyo haijamfikia rasmi mezani kwake ingawa kaiona mitandaoni, hivyo hawezi kuifanyia kazi mpaka pale itakapofika mezani kwake.

“Barua haijanifikia, unajua baadhi ya matatizo tunayapata siku hizi tunayakimbizia kwenye mitandao, inatakiwa niipate rasmi kama ni ya kweli tutayafanyia kazi”, amesema Spika Ndugai.

Akiendelea kuzungumzia suala hilo Spika Ndugai amesema licha ya taarifa hizo usalama wa Wabunge uko 'guaranteed”, ingawa taarifa hizo sio za kuzipuuzia.

“Usalama wa wabunge uko 'guaranteed', wabunge wako salama kabisa, kumbuka Wabunge wote kwa ujumla wetu tuko 363, na tuna watumishi pale bungeni zaidi ya 300, kwa hiyo kuna 'community' ya watu mia sita, ukisikia mtu mmoja analalamika, wawili kwenye kundi kubwa kiasi hicho, unatakiwa ulifikirie hilo jambo, sio la kudharau hata kidogo, lakini halimaanishi kwamba hapo mahali usalama haupo, pako salama sana”, amesema Spika Ndugai.

Licha ya hayo Spika Ndugai amekanusha tuhuma za kuwazima wabunge wa upinzani pale wanapotaka kuibua hoja ya msingi kuhusu muswada wa vyama vya siasa, na kusema kwamba wakati huu wadau (wananchi) ndio wanatoa maoni yao, na wao utakapofika muda wao wataruhusiwa kutoa maoni yao, hivyo wawaache wananchi wautumie muda wao.

“Hakuna wabunge wa upinzani wanaozimishwa, kwa sababu kinachoendelea sasa hivi Kamati inasikiliza wadau, Watanzania wanakuja pale kwenye Bunge wanatoa maoni yao kuhusu ule muswada, Wabunge wanapoingia mule ndani na kuanza kuleta fujo maana yake nini wakati hii sio zamu yao wao!? Zamu yao itakuja kwenye bunge mule, sasa wao wanakuja wanaanza kuleta fujo”, amesema Spika Ndugai.

Credit:Eatv
Share:

Kiboko Ya Matatizo Ya Nguvu Za Kiume, Maumbile Madogo Mvuto Wa Mapenzi

*************************
KIBOKO YA  MATATIZO YA  NGUVU  ZA  KIUME MAUMBILE MADOGO MVUTO  WA  MAPENZI .
MAGONJWA SUGU
*************************
Wanaume  wengi wana  upungufu wa  nguvu  za kiume nakuwa  na  maumbile madogo  ya kiume magonjwa kama  kisukari, presha, ngiri  korodani kuvumba, busha, tumbo kuunguruma na kujaa  gesi  na  kutopata  choo  vizuri, punyeto  NK.
___________________________
Huchangia kwa  kiasi kikumbwa upotevu  wa nguvu  za kiume tumia dawa nzuri ya  mitishamba ambayo haina madhara kwa mtumiaji ata uwe  na  miaka 80 inatibu na kumaliza matatizo  hayo:

 SUPER SHAFT 
********'****************
HII NI DAWA  YENYE  UWEZO  MKUBWA WA  KUOGEZA  NGUVU ZA KIUME MARA  DUFU NA MAUMBILE MADOGO  YA KIUME
************************
(1) Itakufanya uwe  na nguvu za  ajabu ukiwa unafanya tendo la ndoa.
___________________________
(2 ) Inaongeza hamu ya kurudia tendo la ndoa zaidi  ya mara  tatu bila kuchoka.
___________________________
(3)Itakufanya uchelewe kufika kileleni ndani ya dk 30 nakukupa nguvu ya ajabu.
___________________________
(4) Pia itakupa nguvu za kusimamisha uume wako barabara kama msumari wakati wa tendo la ndoa.
___________________________

NYATI POWER
*****************
INAREFUSHA NA KUNENE PESHA MAUMBILE YA KIUME  SAIZI UTAKAVYO kuazia Inchi 1 -8 unene sm 2-4.
*************************
(5) Itaimarisha mirija ya uume iliyolegea au kusinyaa.
___________________________
(6)lnasaidia kisafisha mishipa ya kwenye uume na hivyo kusaidia kuogeza kasi ya msukumo wa damu kwenye mishipa ya uume.
___________________________
(7) Usaidia kuurudisha nje uume ulioingia ndani.
___________________________
(8) Inasaidia kuogeza  manini  nyingi abazo vinaviini vya  uzazi.
___________________________
(9)Husaidia kutibu  madhara ya punyeto.
___________________________
Matumizi makali ya madawa  ya kizungu mirungi, bangi na  sigara.
*************************
TUNATIBU MAGONJWA YOTE SUGU, NGIRI, KORODANI KUVIMBA,  BUSHA BILA KUFANYIWA OPARESHENI, TEZI DUME, KISUKARI, PRESHA AINA ZOTE, UGONJWA WA MOYO STROKU. KWIKWI, KICHOMI MIGUU KUFA NGAZI NK
*************************
ANAPATIKANA MAGOMENI MIKUMI, KARIBU NA  KANISA KATOLIKI, TUMAINI HEARST CLINC NDIYO  SULUHISHO LA MATATIZO YOTE
*************************
PIGA  SIMU
📞0745495181 AU
📞0682644040 
*************************
WOTE  MNAKARIBISHWA
*************************
Kama huna nafasi ya kufika ofisini  kwetu  huduma  hii  utaletewa mahali  ulipo na wa mikoani  mtaipata kirahisi.
KWA MENGINEYO INGIA HAPA
*************************


from MPEKUZI http://bit.ly/2RBDQrI
via Malunde
Share:

Tambua Dalili Za Kupungikiwa Nguvu Za Kiume Na Chanzo Chake

Tambua Dalili Za Kupungikiwa Nguvu Za Kiume Na Uume Kuwa Mdogo Na Chanzo Chake;dalili za mwanaume kupungukiwa nguvu za kiume ni kama vile 1. mwanaume mpaka amwambie mke au mpenzi wake naomba ushike  ili usimame 2. ,kushindwa kurudia tendo,3.  kusimama na kuwa legelege 4,kuisha nguvu au kuanguka ukiwa ndani ya tendo 5,kuwai kukojoa kabla  ya mke au mpenzi wako .

NI NINI CHAZO CHA KUISHIWA NGUVU ZA KIUME,1,magonjwa ya moyo,presha,kisukari 2,usongo wa mawazo 3, utumiaji holela wa madawa  4 uume kukosa vichocheo ambavyo usababisha damu isiwe na mzunguko mzuri

NI NINI KINASABISHA UUME KUWA MFUPI? 1 unene kupita kiasi 2 kuumwa na chango hasa chini ya kitovu 3 kuvaa nguo za kubana sanasana ni wakati wa usiku,4 kufanyiwa tohara ukubwani,

SUPER MAJINJAS; ni dawa ya nguvu za kiume ambayo itakufanya urudie tendo zaidi ya Mara tatu pia itakufanya uchelewe kufika kilele dakika 10-15 kwa tendo la kwanza 

MANGUNGU NO 5 MPYA; dawa hii uboresha uume saizi upenda ichi 5,6,7,na 8 kwa urefu na unene wa sm 1-5 za upenyo dawa zetu ni ukweli na uhakika ni tofauti na ulizowai kutumia ni dawa za miti shama za vidonge unga na maji ,

ISENYE; ni dawa ya kisukari ambayo utibu kabisa tatizo dozi yake siku 21 pia ipo dawa ya uzazi 

FIKA OFISINI KWANGU BUGURUNI MALAPA morogoro yupo wakala maeneo ya stendi kuu mwanza yupo mtaa wa biza c mbeya yupo mbalizi ,na kahama mjini piga simu 0744040721. 0683645920 Dr BRUNO na utaletewa popote ulipo


from MPEKUZI http://bit.ly/2FPecZt
via Malunde
Share:

Super Mkongo: Kiboko ya Matatizo ya Nguvu za Kiume

********************************
SUPER MKONGO MPYA,
_______________________________
********************************
Ni dawa bora ya kutibu na kumaliza matatizo yote ya nguvu za kiume na sababu zake zote kama vile,

- kuwahi kufika kileleni dakika moja ushakojoa
- maumbile kusinyaa na kulegea wakati wa tendo
- kukosa hamu ya tendo la ndoa
- kushindwa kurudia tendo la ndoa
- uume kusimama kwa kulegea
- uume kulegea katikati ya tendo
- kuathirika kwa kujichua kwa muda mrefu
- kuishiwa nguvu kutokana na punyeto.

Epuka aibu hii leo kwa kutumia SUPER MCONGO MPYA, kiboko ya matatizo haya.
_______________________________
Pia kuna MCONGO POWER Kiboko ya uume mdogo inaboresha maumbile ya uume kwa kurefusha na kunenepesha kwa saizi uipendayo haijalishi umri hata kwa walioathirika na upigaji punyeto.
_______________________________
Kwanza fahamu sababu zinazopelekea kuwa na upungufu wa nguvu za kiume na uume mdogo.
_______________________________
(1) kujichua (punyeto) kwa muda mrefu maana hupelekea misuli ya uume kulegea.
(2) ngiri
(3) kuugua chango la uzazi kwa muda mrefu.
(4) kupungukiwa hormone za testosterone.
(5) ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi na visivyo na virutubisho  vya kutosha.
(6) kutokufanya mazoezi na mwenendo wa maisha.
(7) kisukari.
(8) tumbo kuunguruma na kujaa gesi.
(9) maumivu ya kiuno nk.
_______________________________
Kwanini uhangaike? Kwanini uhuzunike?
Hii ni spesho kwa waliotumia madawa mengi bila kufanikiwa hakika hautajuta kuitumia. _______________________________
WASILIANA NA:
DR. MCONGOMANI
SIMU NO:
📞0658816558
📞0682323682
Popote ulipo huduma hii inakufikia
_______________________________
********************************


from MPEKUZI http://bit.ly/2AUXFQm
via Malunde
Share:

CHURA MPWEKE DUNIANI APATA MCHUMBA

Chura anayeaminika kuwa wa mwisho wa aina yake katika ulimwengu ameondolewa upweke.

Romeo, anayejulikana kama chura wa pekee ulimwenguni, ameishi miaka 10 ya kutengwa katika hifadhi ya Bolivia.

Wanasayansi wanasema wamempatia mchumba kwa jina Juliet baada ya safari ya kwenda msitu wa Bolivia.

Chura watano wa majini walipatikana katika vidimbwi vya maji na kukamatwa, kwa kusudi la kuzalishana na kupandikiza upya wanyama hao kwenye pori.

Teresa Camacho Badani ni mkuu wa kitengo cha viumbe hai katika hifadhi asili iliyopo Cochabamba na kiongozi wa safari hiyo.

Anatarajia kwamba vyura hao wa jinsia tofauti watapaendana: "Romeo ni mtulivu na hana mizunguko," aliiambia BBC. "Romeo ana afya na anapenda kula, lakini ana aibu na mpole."

Chanzo:Bbc
Share:

Wimbo wa Kumtukuza Bwana: Niongozwe Nawe - Doreen Lifard

MWIMBAJI Wa Nyimbo za  Injili, Doreen Lifard anakukaribisha Weekend hii ujumuike naye katika kumtukuza Mwenyezi Mungu kupitia Wimbo wake Uitwao Niongozwe Nawe. Utazame Hapo chini


from MPEKUZI http://bit.ly/2FBOZT0
via Malunde
Share:

WASHUKIWA WATANO WA SHAMBULIO LA NAIROBI WAFIKISHWA MAHAKAMANI

Washukiwa watano wanaohusishwa na shambulio la Jumanne la hoteli ya Dusit mjini Nairobi wamewasilishwa mahakamani .

Watano hao ni pamoja na raia mmoja wa Canada.

Mahakama iliruhusu upande wa mashtaka kuwaweka rumande kwa siku 30 huku uchunguzi ukiendelea.

Takriban watu 21 waliuawa wakati wapiganaji walipovamia hoteli ya DusitD2 .

Wanaume wanne walisimamishwa kizimbani katika mahakama kuu jijini Nairobi huku wakificha nyuso zao.

Ni washukiwa wa kwanza kufikishwa mahakamani wakihusishwa na shambulio hilo baya katika hoteli ya DusitD2, lakini hawakusomewa mashtaka yao.

Mkurugenzi wa mashtaka ametaka kupewa muda zaidi ili kufanya uchunguzi alioutaja kuwa mgumu na wa kimataifa.

Chanzo:Bbc
Share:

MWAMUNYANGE : ITUNZENI MIUNDO MBINU MPATE MAJI SAFI NA SALAMA'


Mkurugenzi wa uzalishaji na usambazaji maji wa DAWASA, Injinia Aron Joseph (kwanza kulia) akiwaonyesha Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA iliyoongozwa na Mwenyekiti wao Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange (kwanza kulia) jinsi maji yanavyovunwa katika Mtambo wa Ruvu Juu - Ruvu Kibaha - Pwani. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Mkurugenzi wa uzalishaji na usambazaji maji wa DAWASA, Injinia Aron Joseph akiwaonyesha Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA iliyoongozwa na Mwenyekiti wao Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange (kwanza kulia) mitambo ya mashine za maji eneo la Ruvu Juu walipofanya ziara ya kwa ajili ya kujifunza.
Mkurugenzi wa uzalishaji na usambazaji maji wa DAWASA, Injinia Aron Joseph akitoa maelezo. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA na Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange wakionyeshwa mitambo ya mashine za maji.
Meneja wa DAWASA Kibaha - Pwani, Crossman Makere akitoa ripoti mbele ya Wakurugenzi Bosi ya DAWASA mara baada ya kutembelea ofisini hapo.

Msimamizi wa Mradi wa ujenzi wa kituo cha Kusukuma maji na nyumba za wafanyakazi eneo la Kibamba injinia Ishmaeli Kakwezi akitoa maelezo kwa Wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) wakiongozwa na Mwenyekiti Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange.

Msimamizi wa Mradi wa Kisarawe na Kibaha injinia Ishmaeli Kakwezi akitoa maelezo mbele ya Wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) wakiongozwa na Mwenyekiti Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange mara baada ya kufika eneo la Minarani Kisarawe, Pwani kujionea ujenzi wa tanki la maji.
Mafundi wakiendelea na kazi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Jenerali Mstaafu Mwamunyange akiwa na Wajumbe wa Bodi wakitoa ufafanuzi juu ya masuala mbali mbali yahusuyo miradi hiyo mara baada ya kufanya ziara ya kujifunza wanavyofanyakazi.
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Wananchi wametakiwa kutunza miradi na miundo mbinu ya maji ili iweze kuwahudumia na waondokane na tatizo la ukosefu wa maji.

Akizungumza baada ya kumaliza siku ya kwanza Jenerali Mstaafu Mwamunyange amewataka wananchi kutunza miundo mbinu ya maji ili iweze kuwapatia maji safi na salama.

"Niwaombe wananchi watunze miundo mbinu ya maji maana ujenzi wake ni gharama sana tofauti na wao wanavyofikiria wanapoona maji yamewafia majumba," amesema Jenerali Mstaafu Mwamunyange.

Ziara hiyo ilianzia katika chanzo cha maji cha Mto Ruvu Juu, Ofisi ya DAWASA ya Kibaha, Tenki la Kibamba lenye ujazo wa lita Milioni 10 na ujenzi wa tanki la Kisarawe lenye ujazo wa Lita Milioni sita.

Katika ziara yake Mwamunyage ametembelea pia Ujenzi wa mradi wa bomba la maji kutoka Kibamba (Bomba kuu la kusafirisha maji kutoka Ruvu juu) hadi Kisarawe utakaokuwa na uwezo wa kuzalisha maji Lita Milioni 4 kwa siku na wananchi mbalimbali wa maeneo ya Kisarawe watafaidika na maji.

Amesema kuwa, ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa tenki hilo na kama wakandarasi wataendelea hivyo kufikia mwezi Septemba mwaka huu ujenzi utakua umekamilika.

Katika mradi huo Jenerali Mstaafu Mwamunyange ametembelea tenki la maji lenye ukubwa wa lita milioni 10 kwenye eneo la Kibamba na kuoneshwa pampu nne za kusukumia maji hadi Kisarawe.

Kazi zingine zinazoendelea kutekelezwa na Mamlaka hiyo kwenye mradi wa Kisarawe ni ujenzi wa bomba la kusafirishia maji lenye kipenyo cha inchi 16 urefu wa Km 15.65, mabomba ya kusafirisha na kusambaza maji kwenda kwenye maeneo ya Viwanda lenye urefu wa Km 5.15 na kipenyo cha inchi 12 na lingine likiwa ni urefu wa Km 8 na kipenyo cha inchi 8.9

Ujenzi wa tenki la kuhifadhia na kusambaza maji lenye ukubwa wa Lita milioni 6 katika eneo la Mnarani Kisarawe na ujenzi wa Kituo cha Kusukuma maji na nyumba za wafanyakazi eneo la Kibamba.

Maeneo yatakayofaidika na mradi huo ni kata ya Kisarawe, Kata ya Kazimzumbwi pamoja na maeneo ya Kiluvya, Kisopwa, Mloganzila na maeneo maalumu ya viwanda.
Share:

SIMBA,YANGA KUTOFAUTIANA MASAA MANNE UWANJANI

Wachezaji wa Yanga na Simba kwenye mazoezi.

Klabu ya soka ya Yanga imemaliza maandalizi ya mwisho salama bila majeruhi kuelekea mchezo wake wa leo dhidi ya Stand United ambao utachezwa saa 10:00 jioni, masaa manne kabla ya mechi ya AS Vita Club na Simba.

Wakati Yanga wakicheza mchezo wa leo watakuwa wanafikisha michezo 20 ya ligi huku wapinzani wao Simba ambao saa 1:00 usiku watacheza na AS Vita Club bado wana michezo 14.

Yanga wanaongoza ligi hivi sasa wakiwa na alama 53 wakifuatiwa na Azam FC yenye alama 41 huku KMC ikiwa katika nafasi ya 3 na alama 34 na Simba wapo nafasi ya 4 wakiwa na alama 33.
Share:

KASEJA KUMPIKU MANULA STARS

Mlinda mlango mkongwe nchini Juma Kaseja, amekuwa kwenye kiwango bora siku za hivi karibuni, akiiongoza KMC kukaa katika nafasi ya 3 kwenye ligi kuu soka Tanzania bara, baada ya kutoruhusu kufungwa bao katika mechi 3 mfululizo.

Ubora wa Kaseja ulionekana alipoiongoza timu yake kushinda mabao 2-0 dhidi ya African Lyon kabla ya kushinda 1-0 dhidi ya JKT Tanzania na kumaliza mechi tatu mfululizo bila kufungwa waliposhinda 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting.

Katika mchezo wa 4 Kaseja aliruhusu mabao 2 huku timu yake ikishinda mabao 5-2 dhidi ya Coastal Union ya Tanga. Hivyo mkongwe huyo aliyewahi kuzichezea Simba na Yanga kukamilisha dakika 360 za kucheza lakini akiwa ameruhusu mabao 2 pekee.

KMC sasa ipo juu ya Simba ikiwa na alama 34 katika nafasi ya 3 na Simba wakiwa na alama 33 katika nafasi ya 4. KMC wamecheza mechi 22 huku Simba wakiwa wamecheza mechi 14.

Kaseja mwenyewe amewahi kuweka wazi  kuwa bado ana mpango wa kuichezea timu ya taifa na kwa kiwango chake cha sasa huenda ikawa ni miongoni mwa machaguo ya Emmanuel Amunike.

Endapo Kaseja ataitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars, atakumbana na upinzani mkali kutoka kwa mlinda mlango namba moja wa Simba na Stars Aishi Manula ambaye naye anafanya vizuri na klabu yake.

Share:

Rais Magufuli: Changamoto Zilizopo Sasa Zisipotatuliwa, Sidhani Kama Ajaye Atazitatua

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema hana uhakika endapo mrithi wake ataweza kutekeleza mambo anayoyafanya katika uongozi huu wa awamu ya tano.

Magufuli ameyasema hayo jana  Ijumaa Januari 18, 2019 katika hafla ya makabidhiano ya mfumo wa kusimamia uwazi katika mawasiliano ya simu (TTMS) wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Alisema katika safari ya kutatua changamoto anakutana na magumu mengi na ndiyo maana amekuwa akihitaji nguvu za Mungu kutekeleza majukumu yake.

“Viongozi wa dini endeleeni kuliweka Taifa hili kwenye mikono ya Mungu. Hii ni vita kama ilivyo nyingine na vita ya uchumi inahitaji maombi sana, bila maombi kazi hii haiwezi kufanyika,” alisema.

“Hao wanaokaa gizani hauwezi kujua ana kisu, ana panga au ameweka nyoka mfukoni lakini huko gizani huwa wanatolewa kwa maombi, yatawapumbaza huko gizani wasitake kufanya walichokusudia.”

Alisema kufanya hivyo kutawafanya viongozi wa nchi kusimamia misingi ya uadilifu na upendo wa kweli katika kulitumikia Taifa tajiri, lenye changamoto nyingi zinazohitaji kutatuliwa.


from MPEKUZI http://bit.ly/2R0Ug7A
via Malunde
Share:

Zitto Kabwe Adai Kutishiwa Kuuawa Dodoma .....Amwandikia Barua Spika wa Bunge




from MPEKUZI http://bit.ly/2VWjGHc
via Malunde
Share:

Kigwangalla Aivunja Bodi ya Utalii (TTB)

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla amevunja bodi ya wakurugenzi ya Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kuanzia jana Ijumaa na kutoa miezi mitatu kwa menejimenti kujirekebisha kinyume na hapo ataifumua.

Waziri huyo ametangaza kuunda bodi mpya ya wakurugenzi ambayo itakuwa na wajumbe vijana watakaokwenda na kasi katika kazi hiyo ya kutangaza vivutio.

Dk Kigwangalla amefikia uamuzi huo kwa kile alichoeleza kuwa TTB imeshindwa kutekeleza maelekezo yake yenye lengo la kutangaza vivutio vya utalii.

Akitoa uamuzi huo jana Ijumaa Januari 18, 2019 mbele ya waandishi wa habari Dk Kigwangalla ameeleza kutotangazwa kwa vivutio vya utalii kunaifanya Serikali inyooshewe kidole na kuonekana haifanyi kazi.

Amesema kwa kipindi cha mwaka mmoja ametoa maelekezo zaidi ya 15 lakini hayajafanyiwa kazi jambo linalosababisha yeye kutukanwa.

“Serikali ikitukanwa kwenye sekta ya maliasili na utalii maana yake natukanwa mimi naonekana sitoshi kwenye nafasi hii, “ amesema Dk Kigwangalla.

Miongoni mwa maelekezo ambayo hayajafanyiwa kaiz ni pamoja na TTB kutoweka mabango ya kutangaza utalii katika miji mikubwa ikiwemo Dar es Salaam kuanzia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)

Jingine ni kushindwa kuwatumia watu maarufu na wasanii kutangaza vivutio vya utalii, kushindwa kutangaza vivutio kwenye michezo, kutotengenezwa kwa video na filamu fupi zinazojumuisha vivutio na nyingine nyingi.


from MPEKUZI http://bit.ly/2RVOg4C
via Malunde
Share:

Alichokisema Zitto Kabwe Baada ya Spika Ndugai Kusema Anamuumiza Sana Kichwa

Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo) Zitto Kabwe amesema kuwa si kweli kwamba yeye ndiye Mbunge anayemsumbua zaidi Spika Job Ndugai kama alivyodai kwani amekuwa akifuata taratibu na kanuni bila kuvunja sheria.

Zitto ambaye pia ni Kiongozi wa ACT-Wazalendo ametoa kauli hiyo  baada ya kuulizwa kuhusu maoni yake kufuatia kauli ya Spika aliyoitoa jana akidai kuwa Zitto ni mbunge anayempa tabu kutokana na kauli zake.

"Sijui kwanini Spika amesema vile kwani mimi simpi tabu, nasimamia haki na Spika afuate kanuni tu”, amesema Zitto.
 
Januari 17 katika mkutano wake na wanahabari, Spika Ndugai amesema amekuwa akishindwa kumfukuza bungeni mbunge huyo wa Kigoma Mjini kwa kuwa ndiye pekee anayekiwakilisha chama cha ACT- Wazalendo.

"Ni kweli Zitto Kabwe ananisumbua sana lakini, ukisema umtoe Bungeni unawaza mtu mwenyewe yuko peke yake ukimsimamisha atawakilishwa na nani?. Unamuacha tu lakini wale wengine nafukuza tu maana wako wengi akikosekana kwenye mjadala atawakilishwa na wenzake, hebu nisaidieni Zitto nimfanyeje?, alihoji Spika Ndugai.


from MPEKUZI http://bit.ly/2FBmDYH
via Malunde
Share:

TEKNOLOJIA MPYA KUWASAIDIA VIZIWI KUENDESHA TAXI

Mji mkuu wa Korea Kusini umepata madereva wa kwanza wa teksi viziwi wiki hii, kwa msaada wa teknolojia ambayo imezinduliwa ya kupunguza unyanyapaa wa kuwaajiri watu walio na ulemavu huo.

Kulingana na mtandao wa habari wa Korean Times, dereva wawili viziwi walianza kusafirisha abiria kwenye mji mkuu wiki hii wakisaidiwa na teknolojia iliyoundwa na kampuni mpya ya Coactus.

Akielezea jinsi teknolojia hiyo inafanya kazia mtandao wa Yonhap unasema kuwa vifaa hivyo vimewekwa viti vva mbele na nyuma vya teksi na vimeunganishwa na kampuni kampuni za teksi za Goyohan au silent Taxi.

Teknolojia hiyo inawezesha mawasiliano ya sauti na ujumbe ulioandikwa kuwasaidia abiria kuelezea maeneo wanataka kwenda na mifumo ambayo wangependa kutumia kulipa.

Iliundwa na kundi la wanafunzi mjini humo na kuongozwa na mwanafunzi aliyefuzu na taalumaa ya uandisi Song Min-pyo.Haki miliki ya pichaGOYOHAN TAXIImage captionMkurugenzi mkuu Song Min-pyo

"Tulitaka kuwapa watu viziwi ajira zaidi," Bw Song aliliambia gazeti la Korea Times.

"Tulijua kuwa wakorea watatoka nje ya gari ikiwa dereva ataanza kuwasiliana akitumia simu na kalamu kwa hivyo tukaunda teknolojia hii.'

Yonhap anasema kuwa Coactus itapunguza unyanyapaa unaowakumba madereva visiwi nchini Korea Kusini.

Watu 255,000 wana matatizo ya kusikia nchini Korea Kusini kwa mujibu wa wizara ya afya.
Chanzo : Bbc
Share:

Wanne Watiwa Mbaroni Jijini Arusha kwa Kutengeneza Fedha Bandia

Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha limewakamata watuhumiwa sita kwa makosa mbalimbali.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Ramadhani Ng'anzi amesema jana Ijumaa Januari 18, 2019 kuwa watuhumiwa wanne ambao hakuwataja majina yao kwa sababu za kipelelezi wanajihusisha na utengenezaji wa fedha bandia.

Amesema mtuhumiwa wa kwanza alikutwa na noti bandia za dola za Marekani  zenye thamani ya dola 500 (zaidi ya Sh 1.1 milioni).

"Huyu mtuhumiwa wa kwanza aliwapeleka askari wetu nyumbani kwake eneo la Daraja Mbili ambako zilikutwa fedha bandia za mataifa mbalimbali," alisema Ng'anzi

Fedha hizo ni dola za Marekani, fedha za Umoja wa Ulaya (Euro), Kenya, Malawi, Zambia, Rwanda na Sudan.

Alisema watuhumiwa wanashikiliwa kwa ajili ya mahojiano na upelelezi ukikamilika watafikishwa mahakamani.

Katika tukio jingine, Ng'anzi amesema kuwa watuhumiwa wengine wawili ambao ni Kennedy Mbilinyi na Richard Loishiye wamekamatwa kwa kuiba gari aina Harrier lenye namba za usaili T 241 DKC na kujaribu kulivusha mpaka wa Namanga kuelekea nchi jirani ya Kenya.


from MPEKUZI http://bit.ly/2FJALhU
via Malunde
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger