Sunday, 6 January 2019

WAZIRI WA KILIMO: IFIKAPO JUNI 2019 WAKULIMA WOTE WATAKUWA WAMESAJILIWA NA KUWA NA VITAMBULISHO


Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo; Tunduru-Ruvuma
Wizara ya Kilimo imeanza kuandikisha wakulima nchini kwa lengo la kuwatambua ili kuwarahisishia huduma mbalimbali zikiwemo uhitaji wa pembejeo za kilimo.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo wakati akizungumza na Wenyeviti na makatibu wa Vyama vya Msingi kwenye kikao kazi kilichofanyika leo tarehe 6 Januari 2019 katika Ukumbi wa Claster Mjini Tunduru katika Mkoa wa Ruvuma.

Akiwa katika ziara ya siku moja Wilayani Tunduma Waziri huyo amesema kuwa kumekuwa na upotoshaji mkubwa wa taarifa zinazohusu uandikishwaji wa wakulima kuwa una lengo baya, hivyo amewataka wakulima hao kutosikiliza propaganda hizo zisizo na tija kwani utambuzi wa wakulima ni jambo la kawaida kufanya utambuzi.

Alisema kuwa kuandikisha kwa wakulima ni njia pekee ya kuwa na takwimu sahihi kwa kutambua idadi ya wakulima, vijiji na Kata wanazolima ikiwa ni pamoja na kutambua ukubwa wa mashamba yao kwani kufanya hivyo serikali itakuwa na urahisi wa kuwahudumia wakulima hao.

Katika hatua nyingine Mhe Hasunga amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mhe Juma Homera kwa kusimamia vyema sakata la korosho kwa kusikiliza kesi 11 huku zikifikishwa mahakamani kwa ajili ya kutafutiwa ufumbuzi.

“Nakupongeza sana Mhe Homera kwa usimamizi madhubuti katika kudhibiti kangomba nilipata taarifa kuwa Kg 17,679 za korosho mmezikamata pamoja na zingine Kg 2,779.2 jambo hilo ni zuri endeleeni kusimamia vyema majukumu ya serikali ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya CCM yam waka 2015-2020” Alikaririwa Mhe Hasunga

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mhe Juma Homera aliipongeza Wizara ya Kilimo kwa kuanza kuwalipa wasafirishaji wa korosho kutoka maghala ya vyama vya msingi, kuwalipa gharama za uendeshaji kwa vyama vya masingi, kuwalipa watunza maghala na magunia sambamba na kuondoa mzigo kwa wakati kutokana na ghala kuezuliwa na upepo lililokuwa na jumla ya Tani 536.

Pamoja na pongezi hizo pia Homera amezitaja changamoto mbalimbali katika Oparesheni korosho kuwa ni pamoja na kuchelewa kwa malipo ya wananchi waliofanyiwa uhakiki, utaratibu wa upatikanaji wa miche ya korosho kwa msimu wa mwaka 2018/2019, na mkanganyiko wa upatikanaji wa mapato ya Halmashauri 3% ya bei ya korosho.
Share:

KINYWAJI KILICHOWEKEWA VIAGRA 'KUONGEZA NGUVU ZA KIUME' CHAZUA BALAA..JAMAA APATA TABU

Shirika la kupima viwango vya ubora wa bidhaa nchini Uganda The Uganda National Bureau of Standards (UNBS) linatarajiwa kufanya utafiti na vipimo zaidi kuhusu ubora wa kinywaji cha Natural Power SX , kinywaji cha kuongeza nguvu mwilini kinachodaiwa kuwa na dawa ya Viagra.

Kulingana na gazeti la The Sunday Monitor nchini Uganda vipimo vya maabara vilivyofanywa na Mamlaka ya Kudhibiti matumizi ya dawa nchini Uganda NDA ,vilibaini kwamba kinywaji cha Natural Power SX kina Sildenafil Citrate, ambayo hukuzwa kama Viagra.

The Sunday Monitor linasema kuwa, NDA mnamo mwezi Disemba 28 kupitia barua iliotiwa saini na bwana David Nahamya kwa niaba ya katibu wa mamlaka hiyo bi Dona Kusemererwa, liliripoti kwa Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo la ubora wa bidhaa nchini Uganda Dkt. Ben Manyindo kwamba mlalamishi alidai kwamba baada ya kutumia kinywaji hicho nguvu zake za kiume ziliongezeka kwa muda mrefu mbali na kiwango cha mipigo ya moyo pamoja na kutokwa na jasho kusiko kwa kawaida.

Kufuatia malalamishi hayo mamlaka ilichukua sampuli ya bidhaa hiyo na kuichunguza.

Kwa mujibu wa gazeti hilo matokeo yake yalionyesha kuwa bidhaa hiyo ya Slidenafil Citrate iliwekwa katika kinywaji hicho kulingana na barua hiyo .

Slidenafil , inayouzwa kwa jina maarufu kama Viagra ni dawa inayotumika kutibu matatizo ya nguvu za kiume pamoja na tatizo la shinikizo la damu. Hutumika kwa kula ama kudungwa moja kwa moja katika mishipa ya damu

Kwa mujibu wa gazeti la The Sunday Monitor kisa hicho kinajiri wakati ambapo mamlaka ya NDA inayosimamia dawa nchini Uganda mwezi uliopita ilionya kwamba dawa ya Viagra ilipatikana imechanganywa katika dawa za miti shamba.

Vyombo vya habari vilinukuu mamlaka ya NDA ikisema kwamba asilimia 55.08 ya dawa za mitishamba pamoja na dawa za vyakula tofauti zimechanganywa na Sldenafil pamoja na dawa nyengine hatari.

Swala hilo liliwasilishwa kwa shirika la ubora wa bidhaa na mamlaka ya kudhibiti utumizi wa dawa ambao wanasema kuwa walipata sampuli za Natural Power SX ambazo zilikuwa zimetiwa dawa ya Viagra baada ya kupokea malalamishi kutoka kwa mteja aliyekuwa na wasiwasi.

Chanzo- BBC
Share:

DIWANI WA CHADEMA AVULIWA UANACHAMA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jimbo la Ukonga kimemvua uanachama diwani wa viti maalum manispaa ya Ilala, Dorcus Lukiko kwa madai ya kukihujumu chama hicho kikuu cha upinzani nchini Tanzania.

Akizungumza na vyombo vya habari leo Jumapili Januari 6, 2018 mwenyekiti wa Chadema jimbo la Ukonga, Omary Sweya amesema Lukiko amevunja kanuni na katiba ya chama kwa kutoshiriki vikao mbalimbali vya chama na kutosimamia sera zake kama katiba inavyoelekeza.

Amesema Lukiko ambaye pia mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Guluka Kwalala, amedhihirika kukihujumu chama hicho wakati wa uchaguzi mdogo katika jimbo hilo, uliofanyika Septemba 16, 2018.

"Ameonekana pia baada ya uchaguzi mdogo akimzungusha maeneo mbalimbali aliyekuwa mgombea wa CCM kwa lengo la kuwashukuru wananchi kwa ushindi alioupata bila kujali hujuma alizopata mgombea wetu na chama kwa ujumla," amesema Sweya.

Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa Lukiko amekuwa akiwadhalilisha na kuwatuhumu viongozi wa chama bila kufuata taratibu na kanuni za chama kama zinavyoelekeza.

Amesema alitumiwa barua ya kuitwa mbele ya kamati tendaji ya jimbo lakini kwa dharau alitupa barua hiyo na kutoa maneno ya kejeli kwa viongozi na chama kwa ujumla.

"Kwa niaba ya kamati tendaji ya jimbo iliyoketi kikao Januari 5, napenda kuwataarifu kwamba kuanzia sasa ninapozungumza, Dorcus Lukiko si mwanachama wa Chadema. Tunatoa tahadhari kuwa kazi zozote zitakazofanywa na yeye, Chadema isihusishwe kwa namna yoyote ile," amesema.
Share:

MGONJWA MAHUTUTI KWA MIAKA 10 AJIFUNGUA MTOTO....HAJULIKANI ALIYEMPA MIMBA HOSPITALINI

Maafisa wa polisi mjini Arizona nchini Marekani wameanzisha uchunguzi wa unyanyasaji wa kingono baada ya kupokea ripoti kuhusu mgonjwa aliyekuwa katika koma kwa muongo mmoja kujifungua.



Mwanamke huyo ni mgonjwa katika kliniki moja inayosimamiwa na shirika la afya la Hacienda , karibu na mji wa Phoenix.

Klinki hiyo ya Hacienda haijatoa maelezo kuhusu tukio hilo lakini ikasema kuwa inaelewa kisa hicho.

Chombo kimoja cha habari kiliripoti kwamba mtoto aliyezaliwa yuko katika afya nzuri na kunukuu vyanzo vikisema kuwa wafanyikazi wa kliniki hiyo hawakujua kwamba mwanamke huyo alikuwa mjamzito.

Mgonjwa huyo bado hajatambulika.

Msemaji wa kituo cha polisi cha Phoenix alisema kuwa kuwa kisa hicho kwa sasa kinafanyiwa uchunguzi, lakini hakusema ni lini uchunguzi huo ulianzishwa ama hata kutoa maelezo ya kesi hiyo.

Mwanamke huyo iliripotiwa kwamba amejifungua mnamo mwezi Disemba 29. Kulingana na duru ambayo haikutajwa: hakuna aliyejua kwamba mwanamke huyo alikuwa mjamzito hadi alipoanza kuonyesha dalili za kutaka kujifungua.

Duru hizo pia zilisema kuwa mwanamke huyo alihitaji kuangaliwa kwa saa 24 na kwamba watu wengi wamekuwa wakiingia na kutoka katika chumba chake.

Mikakati ya kiusalama.

Itifaki katika hospitali hiyo imebadilika kilisema chanzo kingine na sasa wanaume wanaoingia katika vyumba vilivyo na wanawake ni sharti waandamane na wafanyakazi wanawake.

Katika taarifa, kliniki ya Hacienda ilisema '' hivi majuzi tuliarifiwa kuhusu kisa kibaya kinachohusisha afya na usalama wa ndani.

Imesema kuwa inashirikiana vizuri na maafisa wa polisi. David Leibowitz, ambaye ni msemaji wa Hacienda, aliongezea kwamba shirika hilo lilikuwa likitumia kila njia kubaini ukweli.

Idara ya afya katika jimbo la Arizona imesema kuwa imetuma wakaguzi kuwachunguza wagonjwa katika hospitali hiyo kwa lengo la kuweka sheria kali za kiusalama.

Katika tovuti yake, Kliniki ya Hacienda inasema kuwa inawaangalia vizuri wagonjwa wenye magonjwa sugu, wagonjwa vijana , watoto wachanga pamoja na wale walio na ulemavu.
Chanzo - BBC
Share:

LUGOLA AMPA WIKI MBILI KAMISHINA UHAMIAJI NCHINI KUWAONDOA WAHAMIAJI HARAMU MIKOA YA KAGERA NA KIGOMA KABLA YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

Na Mwandishi wetu-Karagwe Kagera. WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amempa wiki mbili Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini (CGI) Dkt Anna Makakara, awe amefika Mikoa ya Kagera na Kigoma kwa ajili ya kuanza maandalizi ya kufanya operesheni kubwa ya kuwaondoa Wahamiaji haramu katika Mikoa hiyo kabla ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kuanza mwezi Julai mwaka huu. Akizungumza na mamia ya wananchi wa Mji wa Karagwe katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Changarawe mjini humo, Lugola alisema kuna idadi kubwa ya wahamiaji haramu katika…

Source

Share:

KOCHA MBELGIJI WA SIMBA AMEPANIA AISEE ,AZIPANGA BUNDUKI HIZI HATARI KWENYE MECHI YA KMKM.

Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems ameamua kupanga kikosi Full Masinondo katika mechi ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya KMKM, ikielezwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi yao ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya JS Saoura ya Algeria. Mashabiki wengi walishangazwa baada ya kikosi cha Simba kuonekana kikiwa sawa na kile ambacho Simba hukitumia kwenye Ligi Kuu Bara. Sehemu ya benchi la ufundi la Simba limeeleza: “Kocha ameamua kufanya match fitness. Kutaka wachezaji wawe fiti zaidi. Baada ya mechi hiyo wataendelea na mazoezi. “Lengo ni kujiandaa na Waalgeria halafu pia…

Source

Share:

CCM YAWAONYA WALIOTEULIWA NA RAIS MAGUFULI KUANZA KUTAFUTA UBUNGE KABLA YA WAKATI


Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally akizungumza na wanachama wa CCM na wananchi katika Mji mdogo wa Lamadi, mara baada ya kuwasili Mkoani Simiyu kwa ajili ya ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM mkoaniSimiyu Januari 05, 2019

Na Stella Kalinga, Simiyu

Katibu Mkuu wa Chama cha Mpinduzi (CCM) Taifa Dkt. Bashiru Ally amewaonya baadhi ya Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, na Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma, ambao wameanza kukaa vikao kwa ajili ya kutafuta majimbo kabla ya wakati wa Chama hicho kutangaza mchakato wa kutafuta wagombea wapya wa ubunge na udiwani.

Dkt. Bashiru ameyasema hayo Januari 05, 2019 wakati akizungumza na viongozi na wanachama wa CCM pamoja na Viongozi na watendaji wa Serikali katika wilaya ya Bariadi na Itilima wakati akiwa katika ziara yake mkoani Simiyu.

Dk Bashiru amesema ikiwa viongozi hao wataendelea kufanya hivyo atawataja hadharani na akasisitiza kuwa ni vema wakaridhika na nafasi walizopewa na Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwani kushindwa kufanya hivyo ni kumdharau aliyewateua.

“Wapo wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, Makatibu tawala wa mikoa, wakurugenzi wa halmashauri, na wakuu wa taasisi na mashirika ya umma, wameanza kukaa vikao kwa ajili ya kutafuta majimbo, CCM hatujatangaza mchakato wa kutafuta wabunge au madiwani wapya, uko wakati nitawatangaza hadharani, mridhike na nafasi zenu mlizopewa na Mhe. Rais”, alisema

Katika hatua nyingine Dkt. Bashiru amesema kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika mwaka huu 2019 Viongozi wa CCM wajipange katika kuhakikisha viongozi wa Vijiji na Mitaa wanachaguliwa katika misingi ya demokrasia kwa kuzingatia sifa zao na si fedha zao(rushwa).

“ Katika mwaka huu wa kumuenzi Mwalimu Nyerere baada ya miaka 20 tunataka kufanya mchakato wa kusimamia uchaguzi uwe tofauti, wakati wa kuteua tuzingatie sifa na tuwapime viongozi kwa maisha yao na vitendo vyao......”, alisema Dkt. Bashiru.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe. Benson Kilangi ameishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa kutoa zaidi ya shilingi bilioni 26 katika kipindi cha miaka mitatu, kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Mbunge wa Jimbo la Itilima Mhe.Njalu Silanga, ameishukuru Serikali kwa kuboresha miundombinu ya barabara ambapo amebainisha kuwa kupitia Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) barabara katika jimbo hilo zimetengenezwa zinapitika na zipo ambazo zinaendelea kufanyiwa matengenezo.

Naye Katibu wa CCM Mkoa, Bw. Donald Magesa akitoa taarifa ya Chama, utekelezaji wa Ilani ya CCM mkoani humo umefanyika vizuri huku akisisitiza kuwa Viongozi wa Chama na Serikali wamejipanga kwa kushirikiana na wananchi kukamilisha maboma yaliyojengwa ili kila mwanafunzi aliyefaulu darasa la saba mwaka 2018 aweze kuanza kidato cha kwanza.

Share:

KATIBU MKUU WA CCM ASHAURI WAKUU WA MIKOA KUJIFUNZA SIMIYU


Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally amewashauri Wakuu wa Mikoa hapa nchini kwenda(kuja) mkoa wa Simiyu kujifunza namna ya kufanya kazi kwa umoja na mshikamano kati ya Chama na Serikali sambamba na ubunifu na uchapakazi wa viongozi wa mkoa huo.

Dkt. Bashiru ameyasema hayo Januari 05, 2019 wakati akizungumza na viongozi na wanachama wa CCM pamoja na Viongozi na watendaji wa Serikali, Mjini Bariadi wakati akiwa katika ziara yake mkoani Simiyu.

Dkt. Bashiru amewapongeza Viongozi wa Serikali wakingozwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kwa namna wanavyoshirikiana na viongozi wa Chama kwa namna wanavyosimamia shughuli za maendeleo.

“Niwapongeze kwa namna mnavyosimamia shughuli za maendeleo, nilikuwa hapa mwaka 2005 kama msimamizi wa uchaguzi nilizunguka maeneo mengi mengine yalikuwa hayapitiki, leo nimekuja nikazungushwa maeneo machache tu, nimeona mambo mengi sana ya tofauti kwa hiyo uongozi wa mkoa huu kwa Chama na Serikali umefanya kazi kubwa na bado mna nafasi kubwa ya kufanya mambo makubwa zaidi”, alisema.

Aidha, amesema ili uchumi uwe imara, wa kisasa na wenye manufaa ni lazima uwe jumuishi na uwalenge watu walio wengi ambao ni wazalishaji wadogo hususani katika katika sekta ya kilimo na viwanda huku akisisitiza umakini zaidi ili uwepo wa viwanda na maendeleo ya kilimo viwanufaishe wengi.

Ameongeza kuwa wakati Mkoa wa Simiyu unapanga mipango mbalimbali ya maendeleo ya kiuchumi ni vema kukawa na mpango wa matumizi bora ya ardhi, ili kuondoa migogoro kwa watumiaji ambayo inakuwa chanzo cha chuki na watu kuishi kwa wasiwasi.

Katika hatua nyingine Dkt. Bashiru amesema CCM imejipanga kuhakikisha kuwa itasimamia na kuimarisha ushirika ambao utasimamiwa na wataalam wenye taaluma na maadili ili uweze kuwanufaisha wanaushirika na kutatua changamoto zao.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema kuwa Viongozi na watendaji wa Serikali Mkoani humo watahakikisha wanasimamia utekelezaji wa Ilani ya CCM huku akisisitiza kuwa fedha zote zinazoletwa katika mkoa wa Simiyu zitasimamiwa vizuri na zitafanya kazi iliyokusudiwa.

Aidha, Mtaka amesema Mkoa wa Simiyu unafanya utafiti kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF) ili kubaini fursa za kiuchumi zilizopo katika katika kila kijiji kwa Vijiji vyote 470, ambapo utekelezaji wa Falsafa ya Kijiji Kimoja Bidhaa Moja(OVOP) unatarajiwa kuzinduliwa rasmi mwezi Februari.

Ameongeza kuwa viwanda vikubwa vitatu vyenye uwezo wa kuajiri takribani wafanyakazi 2000 kikiwepo kiwanda cha chaki na kiwanda cha vifungashio (Maswa) kiwanda cha bidhaa 18 za afya zitokanazo na pamba(Bariadi) vitajengwa mwaka huu 2019 Simiyu.

“Ndugu Katibu Mkuu mwaka jana wakati Mhe. Rais anapokea ndege ya Air Bus alicheza muziki na ukiangalia ilikuwa ni kitu kinachotoka moyoni kuonesha furaha yake, ninaamini mwaka 2019 Mhe. Rais ataucheza muziki huo hapa Simiyu”, alisema Mtaka.

Naye Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Kheri James ambaye ni Mlezi wa CCM Mkoa wa Simiyu amesisitiza viongozi na wanachama kuimarisha uhusiano mzuri, kusaidiana na kupendana katika maisha ya siasa huku akiwasihi viongozi kulinda na kuheshimu dhamana walizopewa kwa kutimiza wajibu wao.

Akitoa salamu kwa niaba ya Wabunge wa Mkoa wa Simiyu, Mbunge wa Bariadi,Mhe. Andrew Chenge ametoa wito kwa viongozi na wanachama wa CCM mkoani Simiyu kudumisha upendo, umoja na mshikamano hususani katika kipindi cha kueleka uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Na Stella Kalinga, Simiyu
Share:

MAHAKAMA YABARIKI WANAWAKE WAPEWE TALAKA KWA NJIA YA SIMU

Sheria mpya nchini Saudia inawalinda wanawake kutopewa talaka bila kujua. Kuanzia siku ya Jumapili , mahakama zitatakiwa kuwaelezea wanawake kupitia njia ya ujumbe wa simu kwamba wamepewa talaka.

Mawakili wanawake wanapendekeza kuwa hatua hiyo itamaliza kile kinachotajwa kuwa talaka za siri - ambapo wanaume hutoa talaka bila kuwaelezea wake zao.

Amri hiyo itahakikisha kuwa wanawake wanajua hali ya ndoa yao na itawalinda dhidi ya masurufu.

Mwaka uliopita marufuku ya wanawake kuendesha magari iliondolewa na mahakama nchini Saudia.

Hatahivyo wanawake bado wako chini ya usimamizi wa wanaume.

''Sheria hiyo mpya itahakikisha kuwa wanawake wanapewa haki zao za masurufu wakati wanapopewa talaka'', alisema wakili Nisreen al-Ghamdi.

Pia ina hakikisha kuwa uwezo wowote utakaotolewa na mahakama hautumiki vibaya.

''Wanawake wengi wamewasilisha malalamisihi yao katika mahakama za rufaa kwa kupewa talaka bila ya wao kujua'' , kulingana na wakili Samia al-Hindi.

Hatua hiyo mpya inasemaekana kuwa miongoni mwa mabadilikio ya kiuchumi na kijamii yalioshinikizwa na mwanamfalme Mohammed bin Salman, ikiwemo kuwaruhusu wanawake kuingia uwanjani na kutazama mechi za kandanada mbali na kufanya kazi ambazo awali zimekuwa zikifanywa na wanaume pekee.

Ni mambo gani ambayo wanawake wa Saudia hawawezi kufanya?

Kuna vitu vingi ambavyo wanawake wa Saudia bado hawaruhusiwi kufanya bila ya kuomba ruhusa kutoka kwa wasimamizi wao wa kiume kama vile waume zao , baba zao ndugu wa kiume ama watoto wao.

Vitu hivyo ni:
  • Kuwasilisha maombi ya pasipoti.
  • Kusafiri katika mataifa ye kigeni.
  • Kuolewa
  • Kufungua akaunti ya benki.
  • Kuanzisha biashara
  • Kuondoka jela
Hali hiyo ya kusimamiwa na wanaume imesababisha taifa hilo kuwa miongoni mwa mataifa ambayo usawa wa kijinsia umekandamizwa mashariki ya kati.

Chanzo- BBC
Share:

TAASISI YA PROJECT ISPIRE YAENDELEA KUWAINUA WANAFUNZI KUPENDA MASOMO YA SAYANSI.

  Na, Karoli Vinsent. Serikali ya Uingereza kwa kushirikiana na Taasisi ya Project Inspire imehaidi kuwainua wanafunzi Katika somo la teknolojia ili kuondokana na changamoto mbalimbali zinazowakabili. Akizungumza mwishoni mwa wiki kwa niaba ya barozi wa Uingereza Marc Thayre ambani ni Mkuu wa Masuala ya siasa, Habari na mambo ya ndani alisema wamehamua kuwainua vijana kwa sababu ndiyo nguvu kazi ya baadae. Alisema wapo kwa ajili ya kuwainua vijana kupitia mawazo yao mpya ya teknolojia ambayo ambayo yataweza kuleta maendeleo Katika jamii. “Tupo kwa ajira ya kuwainua vijana kupitia teknolojia…

Source

Share:

UKIMSHIKA HAPA AUNT EZEKIEL USHAMMALIZA

SUPASTAA wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel, amesema kama unataka kumjua upande wake wa pili wa shilingi, jaribu kuyafuatilia mapenzi yake na mzazi mwenzake, Moses Iyobo ambaye ni dansa wa kutegemewa katika Kundi la Wasafi Classic Baby (WCB), utakiona cha mtemakuni. “Hivi kwa nini uhangaike kuyajua maisha yangu na mpenzi wangu? Leo tumegombana au tumepatana au tunaelekea kuachana, inakuhusu nini wewe? Maana hata tulivyoanza uhusiano watu walishtukizia tuko kwenye uhusiano hivyo hata kama tukiachana wataona hivyohivyo,” alisema wakati akizungumza na Ijumaa hivi karibuni. Aliongeza: “Nimekuwa nikisikia minon’gono mingi kuhusu kuachana…

Source

Share:

ALIKIBA KWENYE TUHUMA NZITO ZA WIZI

Msanii mkonge wa muziki wa Bongo Fleva, Domo Kaya amesema kuwa wasanii wapya kwenye muziki huo wanatakiwa kuwa wabunifu, baada ya msanii Alikiba kutumia kidokezo ‘Yebaba’ ambacho alikuwa alikitumia yeye mwanzo. Domo Kaya amefunguka hayo kupitia FRIDAY NIGHT LIVE ya EATV, ambapo amesema kuwa Alikiba kutumia neno hilo sio vibaya lakini alitakiwa kuomba ruhusa kwanza kwake. “Nawasihi wadogo zetu kuwa wabunifu, na kuacha ujanja ujanja maana kutumia kitu hukatazwi lakini uombe kwa muhusika akupe baraka zake”, amesema Domo Kaya. Hivi karibuni msanii Alikiba ameonesha kutumia msemo huo ‘yebaba’ katika wimbo…

Source

Share:

MWANAMKE AKIKUJIBU HIVI,KIMBIA HARAKA

Ukiona umemtumia mpenzi wako/mchumba wako/mchepuko wako/mke wako au hata rafiki wa kike wakati mwingine SMS ya kawaida tu kwaajili ya kumsalimia lakini yeye akakujibu moja kati ya majibu yafuatayo, tafadhali sana usiendelee kuchat nae maana kinachofuata hapo ni majanga tu. KWA MFANO: 1. Ukimtumia sms ”Mambo mpenzi wangu?” akikujibu ”mambo mabaya”, usimuulize kwanini mambo mabaya, ukimuuliza atakwambia kuwa ”sina hela dear” 2. Ukimtumia sms ”Maisha yanasemaje kipenzi changu” akikujibu ”maisha magumu hubby wangu we acha tu” usimuulize kwanini, ukimuuliza kwanini atakwambia ”nimefulia mwenzio kama nini sijui” 3. Ukimtumia sms ”Mbona…

Source

Share:

DIWANI WA CCM AVAMIWA KWA SHOKA NA NONDO KAHAMA


Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Richard Abwao

Diwani wa kata ya Sabasabini halmashauri ya wilaya ya Ushetu wilayani Kahama Emmanuel Makashi (49) kupitia Chama Cha Mapinduzi amenusurika kifo baada ya watu wasiofahamika kuvunja nyumba yake kwa shoka na nondo na kumjeruhi kichwani na mkononi na kufanikiwa kupora shilingi milioni 5.


Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Richard Abwao tukio hilo limetokea Januari 3,2019 majira ya saa saba kamili usiku katika kijiji cha Ifunde, kata ya Mpunze, tarafa ya Dakama, wilaya ya Kipolisi Ushetu na mkoa wa Shinyanga.

Kamanda Abwao amesema watu watatu wasiofahamika walivunja nyumba ya Emmanuel Makashi diwani wa kata ya Sabasabini kwa kutumia shoka na nondo kisha kuiba pesa zinazokadiriwa kuwa ni Tshs 5,000,000/=.

"Katika kupambana na wahalifu hao,diwani huyo alipata michubuko kichwani na mikononi na kutibiwa katika hospitali ya Halmashauri Mji wa Kahama na hali yake inaendelea vizuri",ameeleza. 

Amesema chanzo cha tukio hilo ni kuwania mali.

“Aidha, mmoja kati ya wahalifu hao aitwaye Yohana Masanja (19) mkazi wa kijiji cha Lowa alikamatwa na kuuawa kwa kuchomwa moto na wananchi waliojichukulia sheria mkononi, Juhudi za kuwabaini na kuwakamata watuhumiwa wengine waliohusika na tukio zinaendelea”,amesema  Kamanda Abwao.

Na Kadama Malunde – Malunde1 blog

Share:

DKT. BASHIRU ASHAURI WAKUU WA MIKOA KUJIFUNZA SIMIYU

  Na Stella Kalinga, Simiyu Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally amewashauri Wakuu wa Mikoa hapa nchini kwenda(kuja) kujifunza namna ya kufanya kazi kwa umoja na mshikamano kati ya Chama na Serikali sambamba na ubunifu na uchapakazi wa viongozi wa mkoa huo.   Dkt. Bashiru ameyasema hayo Januari 05, 2019 wakati akizungumza na viongozi na wanachama wa CCM pamoja na Viongozi na watendaji wa Serikali, Mjini Bariadi wakati akiwa katika ziara yake mkoani Simiyu.   Dkt. Bashiru amewapongeza Viongozi wa Serikali wakingozwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,…

Source

Share:

DKT. BASHIRU ASHAURI WAKUU WA MIKOA KUJIFUNZA SIMIYU

  Na Stella Kalinga, Simiyu Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally amewashauri Wakuu wa Mikoa hapa nchini kwenda(kuja) kujifunza namna ya kufanya kazi kwa umoja na mshikamano kati ya Chama na Serikali sambamba na ubunifu na uchapakazi wa viongozi wa mkoa huo.   Dkt. Bashiru ameyasema hayo Januari 05, 2019 wakati akizungumza na viongozi na wanachama wa CCM pamoja na Viongozi na watendaji wa Serikali, Mjini Bariadi wakati akiwa katika ziara yake mkoani Simiyu.   Dkt. Bashiru amewapongeza Viongozi wa Serikali wakingozwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,…

Source

Share:

Video Mpya ya asili 2019 : NCHAINA MADIRISHA - MASAMVA


Msanii wa nyimbo za asili Ng'wana Nchaina 'Nchaina Madirisha' kutoka Kahama mkoani Shinyanga anatualika kutazama video yake mpya kabisa mwaka 2019 inaitwa Masamva...

Tazama video hii hapa chini
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger