Sunday, 23 December 2018

WATANO WAFARIKI DUNIA KUFUATIA MAPOROMOKO YA UDONGO HUKO BUKAVU DRC

Kinshasa, DRC. Maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na mvua kubwa yamesababisha watu watano kupoteza maisha katika mkoa wa Bukavu, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). Ofisa wa serikali katika mkoa huo, Hypocrate Marume, ameliambia shirika la habari la AFP kuwa, miili mitano ya wanawake wanne na mtoto mmoja imepatikana katika kijiji cha Kadutu, baada ya kutokea maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mvua zilizonyesha usiku kucha katika mkoa wa Bukavu. Meya wa mji huo, Mh Munyole Kashama, amethibitisha kutokea vifo hivyo na kuongeza kuwa, watu wengine wanne wamejeruhiwa na kwamba…

Source

Share:

CCM WAMTUHUMU MBATIA KUTAKATISHA FEDHA

Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Moshi Vijijini kimeitaka serikali kuichunguza Taasisi ya Maendeleo Jimbo la Vunjo (VDF) kwa madai ya utakatishaji wa fedha.

Katika taarifa iliyosainiwa na Katibu wa CCM wilaya hiyo, Miriam Kaaya, chama hicho kimeitaka VDF ieleze ilianza na kiasi gani cha fedha na bajeti ya barabara inazozijenga ni kiasi gani.

“Tunaitaka VDF itamke wazi kuzithibitishia mamlaka za serikali ilianza na kiasi gani cha fedha katika akaunti yake na bajeti nzima ya mradi wa barabara za moramu kwa Jimbo la Vunjo,” imesema taarifa hiyo.

"Kwa kufanya hivyo itaondoa uwezekano mkubwa wa asasi hiyo kutumika katika vitendo vya utakatishaji fedha, hivyo tunaitaka serikali kusitisha shughuli za taasisi hiyo wakati uchunguzi ukiendelea. ” taarifa hiyo imesema.

Miongoni mwa viongozi wa bodi ya VDF ni Mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia ambaye na mwenyekiti wake wamekanusha tuhuma hizo.

Mwenyekiti wa VDF ambaye ni Askofu mstaafu wa Dayosisi ya Kaskazini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Martin Shao amesema hawajapokea fedha yoyote kutoka nje na kwamba fedha wanazotumia kutekeleza miradi zinatoka kwa wananchi.
Share:

WANAOSAMBAZA VIDEO YA TRAFIKI AKIPOKEA RUSHWA KUKIONA CHA MOTO

Jeshi la Polisi nchini, limeelezea kuchukizwa na ujumbe wa video unaoendelea kusambazwa unaomwonyesha askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani akipokea rushwa.

Mkuu wa Jeshi hilo, Inspekta Jenerali (IGP) Simon Sirro, ametoa onyo kali kwa raia wanaosambaza tukio hilo la zamani na kusema lengo la wahusika ni kudhalilisha jeshi hilo.


Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa Jeshi hilo Makao Makuu ya Polisi, Naibu Kamishna (DCP) Ahmed Msangi, ilisema tukio hilo lilitokea Novemba, 2016 eneo la Kabuku mkoani Tanga.

IGP Sirro alisema askari anayeonekana kwenye video hiyo alichukuliwa hatua za kinidhamu kwa kufukuzwa kazi na taratibu zingine za kisheria kufuatwa.

Aidha, alisema katika siku za karibuni kumeibuka kikundi cha watu wanaosambaza video inayomwonyesha askari huyo akipokea fedha kutoka kwa dereva wa gari dogo.

Aliwataka wananchi kuacha kusambaza video hiyo yenye lengo la kulichafua Jeshi la Polisi hasa Kikosi cha Usalama Barabarani.

“Tayari uchunguzi wa kuwabaini waliosambaza umeshaanza na yeyote atakayebainika kuhusika kusambaa kwa video hii atachukuliwa hatua za kisheria,” alisema Sirro.


Aliwataka wananchi wote kuacha kutumia vibaya mitandao ya kijamii badala yake waitumia kupeana taarifa zinazochangia kuleta maendeleo nchini.


IGP Sirro alisema Jeshi la Polisi linazingatia weledi katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu zinazoliongoza.


“Wananchi endeleeni kushirikiana na Jeshi la Polisi katika vita dhidi ya uhalifu kwa kutoa taarifa za wahalifu na uhalifu,” alisema IGP kwenye taarifa hiyo.
Share:

KATIBU MKUU WA CCM ATANGAZA KUMNG'OA MBUNGE WA CHADEMA WILFRED LWAKATARE

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Bashiru Ally amewataka wanachama wa chama hicho kumuunga mkono Mbunge wa Bukoba Mjini (CHADEMA), Wilfred Lwakatare, ili aweze kumng'oa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

Akizungumza na baadhi ya wanachama na viongozi nje ya ofisi za CCM Mkoa wa Kagera, mjini Bukoba, jana Desemba 22, 2018 Dkt. Bashiru ametaja sababu za kumuunga mkono kuwa Wilfred Lwakatare ni Mbunge halali, muungwana na hapotoshi wananchi.

Hata hivyo, pamoja na sifa hizo alisema mbunge huyo ajiandae kung'oka mwaka 2020, huku akiagiza kabla ya kuondoka mkoani Kagera apatiwe maelezo ya sababu ya kufa kwa kilimo cha zao la chai alilodai lilikuwa mkombozi kwa wananchi ambao walifanikiwa kujiongezea kipato na kusomesha watoto.

Dkt. Bashiru amesisitiza kuwa Taifa lina uwezo wa kujitegemea huku akitaja baadhi ya changamoto zilizopo zikiwemo ukosefu wa ajira na kuagiza wakuu wa mikoa nchini kutatua kero za wananchi pamoja na kuondoa uonevu kwa wafanyabiashara wadogo.

Katibu mkuu huyo amesema amekwenda mkoani Kagera, ambako ni nyumbani kwake kwa ajili ya mapumziko ya mwishoni mwa mwaka yatakayokwenda sambamba na ziara hadi Januari 2, 2019 kwa kutembelea wilaya mbalimbali za mkoa huo.
Share:

Wimbo Mpya : CHRISTINA SHUSHO - JINA LAKO YESU

Tazama Wimbo Mpya wa Christina Shusho - JINA LAKO YESU
Advertisement
Share:

WAINDONESIA WAANDAMANA KUPINGA UKANDAMIZAJI DHIDI YA WAISLAMU WALIOKO UYGHUR HUKO CHINA

Jakarta, INDONESIA. Maelfu ya Waindonesia wamefanya maandamano mbele ya ubalozi wa China mjini Jakarta wakipinga sera za serikali ya nchi hiyo na mwenendo wake dhidi ya Waislamu wa jamii ya Uyghur. Maandamano mengine kama hayo ya kupinga ukandamizaji wa Waislamu wa Uyghur yamefanyika katika miji mingine kadhaa ya Indonesia. Waandamanaji hao wamelaani sera za serikali ya China za kuwakandamiza Waislamu wa jamii ya Uyghur katika jimbo la Xinjiang na kutoa wito wa kufukuzwa balozi wa China mjini Jakarta. Jumuiya za masuala ya kiraia na kijamii za Indonesia pia zimetoa taarifa…

Source

Share:

WANANCHI WA KIBEREGE KUNUFAIKA NA HUDUMA YA MAHAKAMA HIVI KARIBUNI.

Kilombero,Morogoro Wananchi wa kata ya Kiberege wilayani Kilombero mkoani Morogoro,hivi karibuni wataondokana na adha ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma za mahakama,baada ya ujenzi wa jengo la mahakama ya mwanzo kuonekana kuendelea vizuri na kutarajiwa kukamilika kwa wakati. Ujenzi huo unafuatia maombi ya mwananchi mmoja Bwana,Ismail Limbenga kwa Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Dk.John Pombe Magufuli alipokuwa anaongea na wananchi wa wilaya ya Kilombero katika mji wa Ifakara tarehe 5, Mei 2018 alipofanya safari ya kikazi Wilayani Kilombero. Mwananchi huyo alimuomba Rais awasaidie mabati ya kuezekea jengo hilo…

Source

Share:

MAZOEZI YA KIJESHI YA MTUME SAW-12 YAFANYIKA KUSINI MWA IRAN

Qaeshm, IRAN. Mazoezi makubwa ya kijeshi yaliyopewa jina la Mtume Mtukufu SAW-12, yamefanyika kwa mafanikio katika kisiwa cha Qeshm kusini mwa Iran katika Ghuba ya Uajemi. Taarifa zinasema kuwa, awamu ya mwisho ya gwaride la Mtume Mtukufu SAW-12 lilianza leo asubuhi kisiwani Qeshm na kwamba lengo kuu lilikuwa mazeozi ya kistratijia ya kubadilisha kujihami na hujuma na kuhamishia vita katika kitovu cha ardhi ya adui kwa lengo la kulinda mipaka ya Iran. Jenerali Mohammad Ali Jaafari, mmoja wakuu wa vikosi hivyo vya jeshi amesema mazoezi hayo yamefanyika kwa mafanikio makubwa.…

Source

Share:

UTAFITI:ZAIDI YA RAIA 10,000 WA TUNISIA WALIJIUNGA NA MAGAIDI HUKO IRAQ NA SYRIA

Washington DC, MAREKANI. Kituo kimoja cha utafiti cha huko Marekani kimetangaza kuwa, karibu raia elfu kumi na moja (11,000) wa Tunisia walijiunga na magenge ya kigaidi katika nchi za Iraq na Syria. Kwa mujibu wa shirika la habari la IRIB limesema kituo hicho cha utafiti chenye makazi yake mjini Washington, kimetangaza matokeo ya uchunguzi wake uliopewa jina la ‘Vikosi vya Tunisia katika nchi za Iraq na Syria na kusema kuwa, raia elfu kumi na 860 wa Tunisia walijiunga ma magenge ya kigaidi katika nchi hizo mbili. Hadi kufikia mwezi Machi…

Source

Share:

WAKURUGENZI WA SERA NA MIPANGO NA MAAFISA UTUMISHI WAANDAMIZI WAJENGEWA UWEZO WA MASUALA YA WATU WENYE ULEMAVU

Na; Mwandishi Wetu Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na SHIVYAWATA wametoa mafunzo ya kuwajengea uwezo Wakurugenzi wa Sera na Mipango na Maafisa Utumishi Waandamizi juu ya masuala ya Watu wenye Ulemavu. Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu wakati wa ufunguzi wa mkutano huo Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu Bw. Peter Kalonga amesema kuwa masuala ya Watu wenye Ulemavu ni mtambuka, hivyo ili kuifikia jamii jumuishi ni vyema kuhakikisha masuala ya wenye Ulemavu yanajumuishwa vyema katika mipango mkakati wa…

Source

Share:

JICHO LA UBINADAMU AACHIWA HURU BAADA YA MWAKA MMOJA

Riyath, SAUDIA. Buthaina Muhammad Mansour al-Raimi, binti mdogo wa Kiyemeni ambaye amekuwa maarufu kwa jina la ‘Jicho la Ubinadamu’ hatimaye ameachiliwa huru kupitia makubaliano ya kubadilishana mateka kati ya Yemen na Saudi Arabia, baada ya kushikiliwa kwa muda wa mwaka mmoja na utawala wa Aal Saud. Buthaina, anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka mitano aligeuzwa yatima na kuwa manusura pekee wa familia yake, baada ya baba, mama na kaka zake watano kuuawa katika shambulio la kinyama lililofanywa tarehe 25 Agosti mwaka jana na ndege za kivita za muungano vamizi wa…

Source

Share:

MOROCCO:POLISI WAWAKAMATA WALIOWAUA WATALII WA NORWAY NA DENMARK

Rabat, MOROCCO. Serikali ya Morocco imesema imewatia nguvuni watu tisa (09) wanaotuhumiwa kuwa ndio waliowaua watalii wawili wa kike kutoka nchi za Denmark na Norway. Hapo jana jeshi la polisi katika mji wa Rabat limetangaza kuwakamata watuhumiwa hao, ambao waliwaua kwa kuwadunga kisu Louisa Vesterager Jespersen kutoka Denmark na Maren Ueland wa Norway. Maiti za watalii hao zilikutwa katika maeneo ya milimani ya kusini magharibi mwa nchi hiyo zikiwa na alama za kudungwa kisu. Watalii hao waliuawa wakiwa njiani kuelekea kwenye mlima mrefu zaidi wa kaskazini mwa Afrika wa Toubkal.…

Source

Share:

WAJASIRIAMALI WAASWA KUONGEZA THAMANI YA BIDHAA,MWANZA

Mbunge wa jimbo la nyamagana, Mheshimiwa Stanslaus Mabula,amewataka wajasiriamali jijini Mwanza kuongeza thamani ya bidhaa zao ili kuteka soko la Afrika Mashariki. Mhe.Mabula,alibainisha hayo katika ufunguzi wa maonesho ya kwanza ya vikundi vya vijana wajasirimali kutoka wilaya za Nyamagana na Ilemela mkoani Mwanza wanao dhaminiwa na taasis ya SOS Children’ Village katika kituo chao cha vijana. Mhe. Mabula alisema,uongezaji wa thamani wa bidhaa,usafi wa mazingira ya kutengenezea bidhaa, vifungashio bora, pamoja na jina la bidhaa kunawezesha wajasirimali wa Tanzania kuteka soko la ndani sanjari na ushindani sawia katika Soko la…

Source

Share:

JE WAJUA ZAIDI YA 54% YA WANAJESHI WA ISRAEL HUTUMIA MADAWA YA KULEVYA?

Jerusalemu, ISRAEL. Gazeti moja la Kizayuni la Yedioth Ahronoth limeripoti kuwa mtandao wa magendo ya mihadarati na usambazaji wa madawa ya kulevya umegunduliwa, na umekuwa ukifanywa na askari wa Israel kwenye mipaka ya kaskazini ya eneo la Ukanda wa Gaza. Toleo la  Desemba 21 la gazeti hilo limeripoti kuwa, baada ya askari mmoja wa Israel kutiwa mbaroni katika mipaka ya kaskazini mwa eneo la Gaza, alikutwa na kiwango kikubwa cha madawa ya kulevya. Askari huyo amekiri kuwa, huwa anasambaza madawa hayo kwenye kambi za jeshi la utawala huo wa Kizayuni.…

Source

Share:

HUYU NDO MARIE-JOSÉE IFOKU, MWANAMKE PEKEE ALIYEWANIA URAIS DRC

Kinshasa, DRC. Baada ya Uchaguzi Mkuu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuahirishwa hadi Desemba 30, wananchi wa taifa hilo la Afrika ya kati, wana imani kuwa, Tume ya Uchaguzi (CENI), haitabadilisha tena tarehe hiyo. Tangazo la uchaguzi kuahirishwa liliwakasirisha na kuwavunja moyo wapiga kura waliokuwa wamejiandaa kumchagua rais mpya tarehe 23, baada ya miaka 17 ya Rais Joseph Kabila. Tume ya uchaguzi ilieleza kuwa ilichukua uamuzi huo kwa sababu ya kuteketea kwa vifaa vya kupigia kura katika jengo la CENI jijini Kinshasa, na walihitaji wiki moja zaidi ili kupata…

Source

Share:

Saturday, 22 December 2018

KIVULINI, I4ID WAWASILISHA MAPENDEKEZO YA ZOEZI LA UGAWAJI VITAMBULISHO KWA WAJASIRIAMALI ILEMELA


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, John Wanga akizungumza kwenye kwenye kikao maalum/ cha dharura cha Baraza la Madiwani kilicholenga kujadili mapendekezo ya utekelezaji wa zoezi la ugawaji vitambulisho kwa wajasiriamali wadogo,  leo Disemba 22, 2018.
Mhadhiri kutoka Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Dkt. Nasibu Mramba akiwasilisha mada kwenye kikao maalum/ cha dharura cha Baraza la Madiwani kilicholenga kujadili mapendekezo ya utekelezaji wa zoezi la ugawaji vitambulisho kwa wajasiriamali wadogo.
Mhadhiri kutoka Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Dkt. Nasibu Mramba akiwasilisha mada kwenye kikao maalum/ cha dharura cha Baraza la Madiwani kilicholenga kujadili mapendekezo ya utekelezaji wa zoezi la ugawaji vitambulisho kwa wajasiriamali wadogo.
Mratibu wa Sekta isiyo rasmi Manispaa ya Ilemela, Raphael Mphuru (kulia), akiwasilisha mapendekezo ya utekelezaji wa zoezi la ugawaji vitambulisho kwa wajasiriamali wadogo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Shiriki la kutetea haki za wasichana na wanawake KIVULINI, Yassin Ally.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, Renatus Mulunga (katikati), Kaimu Naibu Meya Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, Alfred Wambura (kushoto) pamoja na Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, Shukrani Kyando (kulia), wakifuatilia mada wakati wa kikao maalum/ cha dharura cha Baraza la Madiwani kilicholenga kujadili mapendekezo ya utekelezaji wa zoezi la ugawaji vitambulisho kwa wajasiriamali wadogo.

Shirika la kutetea haki za wasichana na wanawake KIVULINI kwa kushirikiana na taasisi ya I4ID limewasilisha mapendekezo ya zoezi la ugawaji vitambulisho kwa wajasiriamali wadogo katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza.

Mapendekezo hayo yamewasilishwa leo Disemba 22,2018 kwenye kikao cha dharura cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Ilemela, kabla ya zoezi hilo la ugawaji vitambulisho kwa wajasiriamali wadogo kuzinduliwa rasmi Alhamisi Disemba 27,2018.

Hatua hiyo imejiri baada ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kuzishirikisha taasisi hizo kama mdau wa maendeleo katika Halmashauri hiyo lengo likiwa ni kuhakikisha zoezi hilo linakuwa na mafanikio makubwa hususani vitambulisho hivyo kuwafikia walengwa.

Miongoni mwa mapendekezo yaliyowasilishwa ni pamoja na uundaji wa Kamati Maalum ya kusimamia zoezi la ugawaji vitambulisho hivyo ambayo inajumuisha Watendaji wa Kata, Watendaji wa Mtaa, Polisi Kata, Maafisa Maendeleo, Maafisa Biashara, Viongozi wa Wajasiriamali wadogo (Mwenyekiti na Katibu), Mwakilishi wa Wajasiriamali Wanawake pamoja na Mwakilishi wa Wajasiriamali Vijana.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela, John Wanga pamoja na Mkurugenzi wa KIVULINI, Yassin Ally kwa pamoja wamesema lengo ni kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa na mafanikio makubwa na Halmashauri hiyo inakuwa ya mfano nchini kwa kutekeleza vyema zoezi la ugawaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Share:

WIZARA YA ELIMU YAPIGA MAARUFUKU KUSAMBAZA NYARAKA ZA SERIKALI KATIKA MITANDAO YA KIJAMII


Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. William Ole Nasha akizungumza na washiriki wa Wizara hiyo (hawapo Pichani) waliohudhuria mafunzo ya Huduma kwa Mteja na Utunzaji wa Kumbukumbu ambayo yamekamilika leo mkoani Morogoro.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. William Ole Nasha akimkabidhi cheti mmoja wa washiriki wa mafunzo ya siku tano ya Huduma kwa Mteja na Utunzaji wa Kumbukumbu ambayo yamefungwa leo mkoani Morogoro.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya Huduma kwa Mteja na Utunzaji wa Kumbukumbu.

.............................

Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. William Ole Nasha amesema ni kosa kusambaza nyaraka za serikali katika mitandao ya kijamii bila idhini ya Mamlaka husika, hivyo ameagiza kuchukuliwa hatua za kinidhamu na za kisheria kwa watumishi watakaobainika kusambaza nyaraka hizo.

Naibu Waziri Ole Nasha ametoa agizo hilo mkoani Morogoro wakati akifunga semina ya mafunzo ya Huduma kwa Mteja na Utunzaji wa Kumbukumbu kwa baadhi ya Maafisa wa Wizara hiyo na kusisitiza kuwa hakuna mtumishi yeyote wa serikali asiyefahamu kuwa kutoa nyaraka za serikali bila idhini ni kosa la jinai.

“Kumekuwa na usambazaji wa nyaraka za serikali katika mitandao ya kijamii bila idhini na kwa bahati mbaya wakati mwingine unakuta nyaraka imewekwa mhuri wa siri lakini bado unaikuta huko, watumishi wa serikali lazima watambue kuwa kuna utaratibu wa kutoa nyaraka za serikali na kuna sheria ambazo zinawabana wale wote wanaotoa taarifa hizo bila kuidhinishwa”alisisitiza Naibu Waziri Ole Nasha.

Mhe. Ole Nasha amewataka watumishi hao kutambua kuwa hakuna taasisi yeyote inayoweza kufanya kazi bila kuwa na kumbukumbu au nyaraka hivyo amewataka kuhakiksha utunzaji mzuri na salama wa nyaraka hizo kwani ni nguzo muhimu katika kufanikisha utendaji wa majukumu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Rasilimali watu, Moshi Kabengwe amesema mafunzo hayo yametolewa ili kusaidia watumishi kufanya kazi ambazo zitaleta tija kwa jamii inayohudumiwa na kuondoa changamoto ambazo zimebainika katika utoaji wa huduma.

Mafunzo hayo yamefanyika kwa siku tano na yameshirikisha watumishi zaidi ya 50 kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Makao Makuu, Vyuo vya Ualimu vilivyopo Morogoro na baadhi ya watumishi kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA).

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger