Saturday, 22 December 2018

Picha : WAFANYAKAZI MIGODI YA BUZWAGI NA BULYANHULU WASHEREHEKEA SIKU YA FAMILIA KUAGA MWAKA 2018

Wafanyakazi wa Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Acacia kupitia migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu na familia zao wamesherehekea siku ya Familia ‘Buzwagi and Bulyanhulu Family Day 2018’ kuaga mwaka 2018 na kukaribisha mwaka 2019.

Sherehe hiyo iliyofanyika leo Jumamosi Disemba 22,2018 katika Viwanja vya Mgodi wa Buzwagi wilayani Kahama,pia imehudhuriwa na wadau mbalimbali wa Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu ambapo mgeni rasmi alikuwa Meneja Mkuu anayehusika na Ufanisi wa Kampuni ya Acacia, Bi. Janeth Reuben kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Acacia Peter Geleta.

Akifungua sherehe hizo, Bi. Janeth Reuben aliwashukuru wafanyakazi wote wa migodi hiyo kwa juhudi walizofanya katika mwaka 2018 kuhakikisha kampuni ya Acacia inaendesha biashara kwa ufanisi.

“Sote tunatambua jinsi Acacia tulivyopitia katika mazingira magumu sana mwaka huu na uliopita,lakini tumepata faraja kubwa sana kutoka kwenu kwa sababu mmeweza kufikia na kuvuka malengo tuliyojiwekea ikiwemo malengo ya uzalishaji na ya kiusalama,naomba tuendelee na kasi hiyo hiyo mwaka 2019”,alieleza.

“Nawashukuru sana pia wanafamilia waliofika hapa na wale ambao hawakuweza kufika,sisi wafanyakazi hasa wa migodi tunahitaji na tunapata ushirikiano na upendo mkubwa sana kutoka kwa wenzi wetu na watoto kwa sababu mazingira ya kazi yanatulazimu wengi wetu kuwa mbali na familia”,aliongeza Bi. Reuben.

Alisema ushirikiano na upendo wa wanafamilia wakiwemo wenzi na watoto unawatia moyo hivyo kuwawezesha wafanyakazi kufanya kazi kwa amani katika kulijenga taifa la Tanzania.

Kwa upande wake,Meneja Mkuu wa Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu , Bw. Benedict Busunzu aliwashukuru viongozi mbalimbali wa serikali kwa ushauri na ushirikiano wanaotoa katika kuhakikisha Acacia inaendelea kufanya kazi kwenye mazingira stahiki na kusababisha maendeleo endelevu kwa jamii.

“Licha ya kampuni yetu kupitia katika changamoto za kibiashara,lakini tunajitahidi kadri inavyowezekana kuhakikisha tunaendelea na shughuli za uzalishaji na kwa wakati huo huo kuhakikisha ustawi wa wafanyakazi wetu”,alisema Busunzu.

Akielezea kuhusu Siku ya Familia yenye kauli mbiu ya ‘Tufanikiwe pamoja’, Busunzu alisema kwa mara ya kwanza mwaka huu Acacia inaadhimisha siku ya familia kwa kukutanisha pamoja migodi miwili ya Buzwagi na Bulyanhulu ili kuimarisha zaidi mahusiano ya kijamii na kiutendaji kazi.

“Hii ni siku maalumu kwa ajili ya kufurahi pamoja na familia zetu na wadau wetu,kupitia siku hii,ninayo matumaini kwamba ushirikiano na mahusiano yetu na familia na wadau wetu yataimarika ili kutengeneza kesho iliyo bora zaidi kwa sisi sote”,aliongeza Busunzu.

Maadhimisho ya Siku ya Familia Buzwagi na Bulyanhulu yameongozwa na shughuli mbalimbali ikiwemo wanafamilia kutembelea mgodi wa Buzwagi,maonesho ya kazi za wadau wa Acacia,michezo na burudani kadha wa kadha zikiongozwa na Wasanii Banana Zoro na Barnaba.

Mwandishi wetu,Kadama Malunde ametuletea picha za matukio yaliyojiri...Tazama hapa chini
Meneja Mkuu anayehusika na Ufanisi wa Kampuni ya Acacia, Bi. Janeth Reuben akifungua sherehe za Siku ya Familia ya Buzwagi na Bulyanhulu niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Acacia Peter Geleta leo Disemba 22,2018 katika viwanja vya Mgodi wa Buzwagi uliopo katika wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.
Meneja Mkuu wa Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu , Bw. Benedict Busunzu akielezea kuhusu Siku ya Familia ya Acacia mwaka 2018. Alisema kwa mara ya kwanza wameamua kuadhimisha siku ya Familia kwa kuwaleta pamoja wafanyakazi wa migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu na familia zao ili kuimarisha ushirikiano zaidi.
Wanafamilia kutoka kwa wafanyakazi wa migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu wakiangalia eneo la wazi la uchimbaji madini katika mgodi wa Buzwagi.
Muonekano wa eneo ambapo madini ya dhahabu huchimbwa katika mgodi wa Buzwagi.
Wanafamilia wakiangalia mgodi wa Buzwagi.
Wanafamilia wakiangalia eneo la uchimbaji madini katika mgodi wa Buzwagi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Siku ya Familia Buzwagi na Bulyanhulu, Kambula Lumbu akitambulisha wajumbe waliofanikisha maadhimisho ya sherehe hiyo.
Wanafamilia wa Buzwagi na Bulyanhulu wakicheza muziki.
Kiongozi wa Usalama na afya katika migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu, Dk. Antonette George akimtangaza Hermangild Seki kutoka mgodi wa Bulyanhulu na Elizabeth Sambuka kutoka mgodi wa Buzwagi kuwa ndiyo wafanyakazi bora mwaka 2018 kutokana na kuwa mstari wa mbele katika kuimarisha usalama mgodini.
Meneja Mkuu anayehusika na Ufanisi wa Kampuni ya Acacia, Bi. Janeth Reuben aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Acacia Peter Geleta akimkabidhi cheti cha pongezi Hermangild Seki kutoka mgodi wa Bulyanhulu (kushoto).Katikati ni Meneja mkuu wa migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu, wa kwanza kulia ni Meneja Uboreshaji Tija migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu ,Shukuru Mwainunu. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Mgodi wa Buzwagi, Blandina Munghezi.
Meneja Mkuu anayehusika na Ufanisi wa Kampuni ya Acacia, Bi. Janeth Reuben aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Acacia Peter Geleta akimkabidhi cheti cha pongezi Elizabeth Sambuka kutoka mgodi wa Buzwagi. Katikati ni Meneja mkuu wa migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu, wa kwanza kulia ni Meneja Uboreshaji Tija migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu ,Shukuru Mwainunu.
Hermangild Seki kutoka mgodi wa Bulyanhulu na mkewe wakipokea zawadi ya majiko ikiwa ni zawadi ya ushindi iliyotokana na kuwa mstari wa mbele kuimarisha usalama mgodini.
Elizabeth Sambuka kutoka mgodi wa Buzwagi akipokea zawadi ya majiko ya kupikia.
Picha ya pamoja,viongozi wa Acacia na wafanyakazi bora mgodi wa Buzwagi na Bulyanhulu na familia zao.
Watoto wa wafanyakazi wa migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu picha ya pamoja na viongozi wa Acacia kabla ya kukabidhiwa zawadi.
Meneja Mkuu anayehusika na Ufanisi wa Kampuni ya Acacia, Bi. Janeth Reuben aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Acacia akikabidhi zawadi ya madaftari na kalamu kwa watoto wa wafanyakazi wa migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu.
Msanii Banana Zoro akitoa burudani wakati wa sherehe za Siku ya Familia Buzwagi na Bulyanhulu,
Banana Zoro akiendelea kutoa burudani kupitia B Band.
Ashura Mahenge kutoka B Band akiimba nyimbo Live.
Msanii Barnaba akiimba na kucheza na watoto wa wafanyakazi wa migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu.
Msanii Barnaba akigawa zawadi ya pipi kwa watoto.
Wanafamilia wakifuatilia burudani.
Wanafamilia wakiwa eneo la tukio.
Wanafamilia wakiwa eneo la sherehe.

Watoto wakiendelea na michezo yao.
Watoto wakiendelea kucheza.
Watoto wanaendelea kucheza.

Watoto wakipewa zawadi ya vitafunwa.
Watoto wakiendelea kupewa zawadi.
Wafanyakazi wa Acacia wakipiga picha ya kumbukumbu.
Wafanyakazi wa Acacia na familia zao wakiwa katika viwanja vya mgodi wa Buzwagi kushuhudia michezo mbalimbali.
Mchezo wa kukimbiza kuku ukiendelea
Mtoto akiwa na kuku wake baada ya kufanikiwa kumkamata.
Wanafamilia wakiangalia michezo iliyokuwa inaendelea.
Mchezo wa kubeba wenza ukiendelea...kila mmoja kabeba mke wake.
Washindi wa shindano la kubeba wenza wakinyoosha mikono kuonesha wamekuwa wangapi... walipewa zawadi ya Shampen.
Mbio za magunia nazo zilikuwepo.
Meneja Mkuu anayehusika na Ufanisi wa Kampuni ya Acacia, Bi. Janeth Reuben aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Acacia akimpa zawadi mshindi wa mbio za magunia, Imani Abdalah.
Wanafamilia wanaangalia michezo iliyokuwa inaendelea.
Mchezo wa kuvuta kamba pia ulikuwepo...hapa wanajiandaa kuvuta kamba.
Washiriki wakijiandaa kuvuta kamba.
Meneja Mkuu anayehusika na Ufanisi wa Kampuni ya Acacia, Bi. Janeth Reuben aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Acacia akishikana mkono na Meneja Mkuu wa Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu , Bw. Benedict Busunzu ambaye ni miongoni mwa wachezaji wa timu ya mpira wa kikapu 'Basket ball' kabla ya mechi kuanza. 
Mpira wa kikapu ukiendelea.
Wanafamilia wa Acacia wakiangalia mpira wa kikapu.
Wafanyakazi wa Acacia wakiwa eneo la tukio.
Wanafamilia wakipata huduma ya chakula.
Wanafamilia wakiwa eneo la tukio.
Sherehe inaendelea.
Sherehe inaendelea
Wanafamilia wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea.
Meneja Mkuu anayehusika na Ufanisi wa Kampuni ya Acacia, Bi. Janeth Reuben kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Acacia,akikagua mabanda wakati wa sherehe za Siku ya Familia Buzwagi na Bulyanhulu. Hapa ni katika banda la Acacia akipata maelezo kutoka kwa Mwandindi Charles namna wanavyofanya shughuli za uchimbaji katika mgodi wa Buzwagi.
Andrewe Milambo akionesha mchoro kuhusu shughuli za uchimbaji madini katika mgodi wa Bulyanhulu.
Mchoro kuhusu shughuli za uchimbaji madini katika mgodi wa Bulyanhulu.
Meneja wa NHIF mkoa wa Shinyanga Imani Emmanuel akitoa maelezo kuhusu bima za afya.
Hapa ni katika banda la Jubilee Insurance life.
Hapa ni katika banda la benki ya NMB.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Acacia Janeth Reuben akiangalia mafuta ya kupaka yaliyotengenezwa kwa asali na kikundi cha wajasiriamali wa Mwendakulima waliowezeshwa na Acacia.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Acacia Janeth Reuben  akinunua batiki iliyotengenezwa na wajasiriamali waliowezeshwa na Acacia.
Wajasiriamali waliowezeshwa na Acacia wakipiga picha ya kumbukumbu kwenye banda lao la maonesho.
Mtaalamu wa Mawasiliano Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu,Mary Lupamba na mmewe na mtoto wao mchanga wakipiga picha ya kumbukumbu.
Wafanyakazi wa Acacia wakipiga picha ya kumbukumbu.
Ma DJ waliofanikisha sherehe ya Familia ya Buzwagi na Bulyanhulu wakiwa katika pozi.
Burudani kutoka B Band ikiendelea.
Msanii Banana Zoro kutoka B Band akicheza na wafanyakazi wa migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Share:

VYAMA 10 WA UPINZANI TANZANIA VYACHACHAMAA

Vyama 10 vya upinzani nchini Tanzania vimemtaka Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi kurejesha ratiba za vikao vya Baraza la Vyama vya Siasa ili kupata fursa ya kujadili Muswada wa Marekebisho ya Vyama vya Siasa kabla ya kuanza kwa vikao vya kamati za Bunge.

Akisoma tamko la vyama hivyo, leo Jumamosi Desemba 22, 2018 jijini Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Salum Mwalimu amesema kuwa Msajili na ofisi yake wana nia ya kuvuruga kikao hicho ambacho walikubaliana kuketi Desemba 21 na 22, 2018 kabla ya kikao kijacho cha Bunge.

Mwalimu amesema wameshtushwa na uamuzi wa Msajili kwa kile wanachokidai kuahirisha kikao hicho na kukwamisha lengo lao la kujiandaa kutumia fursa hiyo kuzungumzia muswada ambao wamedai kuwa ni kandamizi na usiofaa.

"Tumeshtushwa kwanza na utaratibu uliotumika wa kuahirisha kikao ambacho tayari kilishakuwa kimepangwa na Kamati ya Uongozi ya Baraza la Vyama vya Siasa ambalo ndilo lenye jukumu la kikao chake," amesema.

"Tunataka Jaji Mutungi aseme amemshirikisha nani kufanya uamuzi huo, mwenyekiti wetu wa baraza ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya uongozi hakuwa na hiyo taarifa ya ahirisho la hicho kikao, " ameongeza.

Moja ya vifungu vinavyopendekezwa kufanyiwa marekebisho ni kifungu cha 19, ambacho kinapendekeza kurekebishwa ili kumwezesha msajili wa vyama vya siasa kufuta usajili wa chama cha siasa kitakachobainika kupata usajili kwa njia zisizo za halali.

Muswada pia unapendekeza kufuta kifungu cha 21A na kifungu cha 21B kinapendekezwa kufanyiwa marekebisho ili kuliwezesha Baraza la Vyama vya Siasa kupata fedha kutoka katika bajeti ya Serikali na wafadhili.

Pia, inapendekeza kufanyiwa marekebisho ili kumpa mamlaka waziri mwenye mamlaka ya kutengeneza kanuni za uandaaji wa taarifa za hesabu za vyama vya siasa na mambo yatakayojumuishwa katika katiba za vyama vya siasa.

Muswada huo umesomwa kwa mara ya kwanza bungeni ambako Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge alisema Spika wa Bunge, Job Ndugai ataipangia Kamati ya Bunge itakayofanya uchambuzi.
Share:

OLESENDEKA AMVAA MCH. MSIGWA KUHUSU SAKATA LA USHOGA

Na Amiri kilagalila Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka ametangaza vita dhidi ya mwanasiasa yeyote atakayeingia katika mkoa wa Njombe na kumjaribu kumtikisa kwa kuhubiri ndoa ya jinsia moja (ushoga) kama ambavyo baadhi ya wanasiasa na wanaharakati wanavyozungumza wakiwa katika maeneo mengine. Mkuu wa mkoa wa Njombe akiteta jambo na meneja wa TRA mkoa. Olesendeka ameyasema hayo wakati akizungumza na wadau wa kodi katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya mji wa Njombe huku akionyesha kukasilishwa na watanzania ambao wamekuwa wakishabikia vitendo ambavyo vimekuwa vikipingwa hata katika vitabu…

Source

Share:

DC RUANGWA: WAJASIRIAMALI WASIOTAKA KULIPIA VITAMBULISHO WATACHUKULIWA HATUA

Na Bakari Chijumba, Lindi. Katika kutekeleza zoezi la ugawaji wa vitambulisho kwa wajasiriamali kama ilivyoagizwa na Rais Magufuli, mkuu wa wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi, Hashim Mgandilwa amewataka wajasiriamali kujitokeza kwa wingi kulipia na kupata vitambulisho hivyo ili kujiepusha na hatua zitakazochukuliwa dhidi ya wale watakaopuuzia zoezi hilo. Baadhi ya watendaji kata,vijiji,makatibu tarafa, wakuu wa idara na kamati ya ulinzi na usalama wakiwa katika kikao kazi kilichoendeshwa na mkuu wa wilaya ya Ruangwa, Hashim Mgandilwa kuhusu ugawaji wa vitambulisho wilayani humo. Mgandilwa ametoa tamko hilo katika kikao kazi kilichofanya mjini…

Source

Share:

HATIMAYE SASA MUSIBA KUBURUZWA MAHAKAMANI,MDOMO WAKE WAMPONZA,MEMBE AKOMAA NAYE KISA–

NA KAROLI VINSENT HATIMAYE anayeejiita na kuitwa Mwanaharakati mzalendo ,Cyprian Musiba, amefunguliwa kesi kwenye mahakama ya Kuu ya Tanzania akitakiwa alipe mabilioni ya fedha kutokana na hatua yake ya kumchafua aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa kimataifa,Benard Membe. Katika shauri hilo ambalo limesajiliwa kwenye Mahakama kuu ya Tanzania tangu wiki iliyopita ni shauri namba 220 ya mwaka 2018 ,washtakiwa wakiwa ni Musiba ,Mhariri wa Gazeti la Tanzania,na wachapishaji gazeti hilo wakidaiwa sh bilioni 10 kwa kumchafuwa Membe ambaye aliwai kuwania Urais ndani ya Chama cha Mapinduzi Mwaka…

Source

Share:

RAY C : AMKA RUGE WE NDO MSIRI WANGU, NAKUPIGIA SIKUPATI

Na Bakari Chijumba, (Beca Love), Mtwara. Mtangazaji wa zamani wa Clouds Fm ambaye pia ni msanii, Rehema Chalamila maarufu kama ‘Ray C’ amefunguka na kuandika ujumbe mzito kwenye ukurasa wake wa instagram akielezea masikitiko yake na vile anavyoguswa na kuugua kwa Mkurugenzi wa Vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba, ambaye kwa wakati huu yupo nje ya nchi kwa matibabu. Kupitia akaunti ya Ray C ya instagram ameandika: “Amka bwana, nashachoka kusubiri, msg zangu hujibu, simu hupokei, na stori kibao nataka kukwambia ingawa najua utanchamba lakini nishazoea kukwambia…

Source

Share:

MDOGO WAKE ROSTAM AZIZ AHUKUMIWA MIAKA 20 JELA

Na Bakari Chijumba, Mtwara. Mdogo wake mfanyabiashara maarufu nchini Rostam Aziz, Akram Azizi amehukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kulipa faini ya Sh.milioni 259.5 au kwenda jela miaka 20 jela baada ya kukiri mashtaka 73 ya kukutwa na nyara za Serikali zikiwemo silaha. Hukumu hiyo imetolewa jana 21 December 2018, mahakamani hapo ambapo Akram amefanikiwa kulipa faini kwa kulipa fedha hizo, hivyo amekwepa kifungo cha kwenda jela miaka 20 jela. Hata hivyo Mahakama imeamua kuitaifisha nyara hizo na kuwa mali ya Serikali na kuamuru silaha zote ziwe chini ya…

Source

Share:

MAREHEMU AHUKUMIWA JELA MIAKA MITANO

Mahakama ya Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi imemhukumu aliyekuwa Meneja wa Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini (Tarura) Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, Godfrey Majuto ambaye ni marehemu sasa, kulipa faini ya Sh milioni 3.6 au kutumikia kifungo cha miaka mitano jela.



Hiyo ni baada ya kupatikana na hatia ya makosa matatu ya kupanga ya uhujumu uchumi, baada ya Majuto na wengine wanne kushtakiwa kwa kosa la kuisababishia Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda hasara ya Sh 61,157,342. 


Aidha, mahakama hiyo imeamuru yeyote atakayeteuliwa kuwa msimamizi wa mirath ya marehemu Majuto atalipa faini ya Sh milioni 3.6 ili fedha hiyo iingine serikalini.


Mbali na Majuto, washitakiwa wengine katika kesi hiyo walikuwa ni Naomi Nko ambaye wakati huo alikuwa ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda, Peter Mwanoni, Beatus Bisesa, mkandarasi na Chiyando Matoke.

Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwanasheria wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Katavi, Bahati Haule, kuwa washitakiwa hao walitenda kosa hilo la kuhujumu uchumi kwa nyakati tofauti.

Alidai walitenda kosa hilo Januari 2, 2012 wakiwa watumishi wa Halmashauri ya Mpanda wakidai kuandaa hati ya malipo ya uongo ya kutaka kuonyesha sehemu ya Barabara ya Kasokola kwenda Mtapenda kuwa imetengenezwa kwa gharama ya Sh 64,376,152 wakati si kweli.

Katika kosa la pili lililowahusu washitakiwa wa kwanza hadi wa tatu, walishtakiwa kwa kosa la matumizi mabaya ya ofisi kwa kupitisha malipo hayo kwa Kampuni ya Matoke huku wakijua barabara hiyo haikujengwa kwa gharama hiyo.

Haule alidai kuwa shitaka la tatu liliwahusu washitakiwa wote watano walioshitakiwa kwa kosa la kuisababishia halmashauri hiyo hasara ya Sh 61,157,342.

Baada ya kusikiliza pande zote mbili za mashitaka na utetezi, Hakimu Luoga, aliiambia mahakama hiyo kuwa washitakiwa wa kwanza, wa tatu na wa nne wamepatikana na hatia katika kosa la kwanza huku Majuto naye ametiwa hatiani katika kosa la pili na la tatu.

Pia washtakiwa akiwamo wa pili na wa tano hawakutiwa hatiani kwa kosa lolote lile na waliachiwa huru.

Baada ya maelezo hayo, Haule aliiomba mahakama hiyo itoe adhabu kali kwa washitakiwa kwa kuwa wameisababishia hasara Serikali.

Akisoma hukumu hiyo, Luoga alisema pamoja na mahakama kupokea hati ya kifo cha Majuto kilichotokea Desemba 4, mwaka huu huko Songea ambako alikuwa akifanya kazi kama Meneja wa Tarura wa Manispaa ya Songea, alikohamia kabla ya mauti hayajamfika alikuwa ameshatoa utetezi wake mahakamani hivyo hakuwa na sababu ya kuifanya mahakama ishindwe kutoa adhabu kwake.

Luoga alisema katika shitaka la kwanza Majuto akiwa na washitakiwa wa tatu na wa nne wamepatikana na hatia ya kifungu cha Sheria namba 22 ya kupambana na rushwa ya mwaka 2007, hivyo wameadhibiwa kulipa faini ya Sh 600,000 kwa kila mmoja au kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela.

Katika kosa la pili na la tatu limemtia hatiani Majuto peke yake na kosa la pili kwa mujibu wa Sheria namba 31 sura namba 11 ya mwaka 2007, amehukumiwa kulipa faini ya Sh 1,000,000 au kifungo cha miaka mitatu jela.

Katika kosa la tatu, Majuto chini ya kifungu cha Sheria namba 57 (1)na kifungu namba 60 (1) cha Sheria ya Uhujumu Uchumi, makosa ya kupanga, sura 200, marejeo ya 2002 amehukumiwa kulipa faini ya Sh 2,000,000 au kifungo cha miaka mitano jela.

Hakimu Luoga alisema hukumu hiyo amekukumiwa Majuto na mahakama inaagiza yeyote atakayeteuliwa kuwa msimamizi wa mirathi ya marehemu alipe faini hiyo ili fedha hizo ziende serikalini.
Share:

WANAWAKE WANNE WAVAMIWA NYUMBANI KISHA KUBAKWA KWA ZAMU


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwalubambo.

Wanawake wanne (majina yamehifadhiwa) wakazi wa kijiji cha Buganzu kata ya Lunzewe Mashariki, Wilayani Bukombe Mkoani Geita wamebakwa na wanaume zaidi ya mmoja baada ya kuvamiwa na watu hao wakiwa majumbani mwao.


Tukio la kubakwa wanawake hao limetokea Desemba 11 majira ya saa nane usiku katika kijiji hicho, walipovamiwa na wanaume wanne wakiwa wamelala kisha kubakwa na kila mmoja na kupelekea kuwasababishia maumivu makali.

Akizungumza Mkoani Geita Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwalubambo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba watuhumiwa waliofanya unyama huo wamekwishakamatwa ambapo amewataja kuwa ni pamoja na George Deogratius(42) maarufu (Tolu) mkazi wa Ibamba, Josephat Emmanuel(25) mkazi wa Kabuhima, Rashid Maganga(18)) na Albert Makisio maarufu Kamkono wote wakazi wa Ibamba.

Kwa mjibu wa Kamanda Mponjoli, matukio mengine ni pamoja na watu wawili kuuawa Desemba 19 majira ya usiku, na wananchi wenye hasira kali wakiwa katika jaribio la kutenda uhalifu katika kijiji cha Nyakahengere kata ya Lukalanga Mjini Geita.
Share:

DISCO TOTO YAPIGWA MARUFUKU DAR

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema hatarajii kuona 'disco-toto' ikifanyika popote pale jijini Dar katika kuadhimisha sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya.

Ameeleza kuwa hadi sasa hakuna aliyepeleka maombi kwa jeshi hilo ili kutoa huduma hiyo kwenye siku za sikukuu, ili ukaguzi wa kina ufanyike kwenye kumbi hizo kwa ajili ya usalama wa watoto.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumamosi Desemba 22, 2018 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa.

Mambosasa ametoa kauli hiyo wakati akieleza jinsi polisi walivyojipanga kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka.


Amewataka wazazi kuwa makini na watoto wao katika kusherehekea sikukuu hizi ili kuepusha matukio ya watoto kupata ajali, kupotea na kuzama kwenye fukwe, kama ilivyokuwa ikitokea miaka ya nyuma.

“Wazazi katika kipindi hiki cha sikukuu kila mmoja atimize wajibu wake wa kuhakikisha anajilinda yeye mwenye na watoto wake kwa kufanya hivyo sikukuu hii haitakuwa na madhara kwao.

“Ngoma za vigodoro haziendani na ustaarabu wa Dar es Salaam na niseme tu kwamba tutakushugulikia kabla hata haujaanza kucheza ngoma hiyo”.


Kamanda Mambosasa pia ametoa wito pia kwa wakazi wa Dar es Salaam kuhakikisha wanazingatia sheria na taratibu zote katika maadhimisho ya sikukuu hizo ili kuwepo na amani na usalama.
Share:

BASATA YAKANUSHA KUWAFUNGULIA DIAMOND NA RAYVANNY

Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) nchini Tanzania limekanusha kuwafungulia wasanii Diamond Platnumz na Rayvanny wanaotumikia adhabu ya kutojihusisha na sanaa kwa muda usiojulikana baada ya kufanya makosa mbalimbali ndani ya kipindi cha miezi miwili.

Taarifa ya Naibu Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Onesmo Kayanda iliyotolewa leo Jumamosi Desemba 22, 2018 imesema haijawaondolea adhabu hiyo na kuwakata wafuate maagizo waliyopewa ikiwamo kutofanya maonyesho nje ya nchi.

Jana, wasanii hao kupitia mtandao wa Instagram waliomba radhi kwa mamlaka mbalimbali nchini na jioni walionekana wakifanya mkutano na wanahabari nchini Kenya kutangaza maonyesho yao yanayoendelea.

"Ikumbukwe kuwa Desemba 18 tuliwafungia kutojihusisha na sanaa kwa kipindi kisichojulikana kwa kuimba kwa makusudi wimbo Mwanza tulioufungia kwa sababu za kimaadili,

"Baraza linasisitiza kuwa halijawafungulia wasanii hao, pia linawaonya kuacha kutoa taarifa za uongo kabla halijawachukulia hatua kali zaidi," imesema taarifa hiyo ya Kayanda.

Diamond na Rayvanny wameingia matatani wakituhumiwa kufanya makosa mbalimbali ikiwamo la kutumbuiza wimbo uliofungiwa, kufanya tamasha mkoani Mwanza bila kibali, kutoa lugha ya matusi jukwaani mkoani Mtwara na kutofuata taratibu za usajili wa matamasha.
Share:

DRC: UPINZANI WAONYA DHIDI YA KUAHIRISHA TENA UCHAGUZI

Muungano wa kisiasa unaomuunga mkono mgombea wa upinzani Felix Tshisekedi umemshutumu Rais Joseph Kabila kukosa dhamira ya kuandaa uchaguzi na kuondoka madarakani, lakini ukawataka wafuasi wao kuendelea kuwa watulivu.



Muungano huo ujulikanao kama CACH, umeonya kwamba hauwezi kuvumilia kuahirishwa kwingine kwa uchaguzi, hata kwa siku moja baada tarehe mpya iliyotangazwa na tume ya uchaguzi, tarehe 30 Desemba.

Mgombea mwingine wa upinzani, Martin Fayulu pia ametoa tamko kama hilo la muungano wa CACH, akisema hatua za kuendelea kuchelewesha uchaguzi haziwezi kuvumiliwa, na kuwabebesha lawama kikamilifu Rais Kabila na Mkuu wa tume ya uchaguzi, Corneille Nangaa. 


Tangazo la Fayulu limetiwa saini na vigogo wawili wa kisiasa waliozuiliwa kugombea, gavana wa zamani wa jimbo la Katanga Moise Katumbi, na aliyekuwa kiongozi wa waasi, Jean Pierre Bemba.


Na katika makala iliyoandikwa na mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel Dakta Denis Mukwege na kuchapishwa katika gazeti maarufu la New York Times la nchini Marekani, Mukwege amemtaka Kabila na wale aliowaita vibaraka wake mafisadi, kukabidhi madaraka, akionya juu ya uwezekano wa kuzuka ghasia kubwa ikiwa wataendelea kung'ang'ania uongozini.


Mkwege amesema kuna haja ya dharura nchini Kongo ya kupata serikali ya wataalamu, ambayo itaipa nchi mwelekeo na kuandaa uchaguzi wa kuaminika.


Huku haya yakijiri, juhudi za tume ya uchaguzi, CENI zimepata pigo, baada ya ndege aina ya Antonov iliyokodiwa na tume hiyo kusafirisha karatasi za kura, kuanguka karibu na mji wa Kinshasa jana jioni, ilipokuwa ikirejea katika mji mkuu kutoka katika mji wa katikati ya nchi wa Tshikapa, ambako ilikuwa imepeleka vifaa vya uchaguzi.


Kuna taarifa zinazotofautiana kuhusu idadi ya waliokufa katika ajali ya ndege hiyo inayomilikiwa na kampuni ya Gomair. Afisa wa ukaguzi wa safari za ndege katika uwanja wa ndege wa Tshikapa, amesema ndani ya ndege hiyo walikuwemo wahudumu 5 na msafiri mmoja, na kwamba wote wameuawa.


Lakini balozi wa Urusi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Alexei Senteboff, amenukuliwa na mashirika ya habari akisema ndege hiyo ilikuwa na wafanyakazi watatu, wote raia wa Urusi, na wote wamekufa. 


Alisema kwamba awali kulikuwepo taarifa ambazo hazikuthibitishwa, zilizodai kwamba walikuwemo watu 23 ndani ya ndege iliyoanguka, wakiwemo wafanyakazi watatu raia wa Urusi.


Hadi sasa hakuna ripoti zozote za machafuko, kufuatia tangazo la CENI la juzi jioni, la kuahirisha kwa wiki moja uchaguzi uliotarajiwa kufanyika kesho Jumapili.


Credit:DW
Share:

RAIS MAGUFULI ATAKA POLISI WANAOUA MAJAMBAZI WASISHTAKIWE

Rais John Magufuli ametaka askari wa Jeshi la Polisi kutoshtakiwa kutokana na makosa yanayojitokeza wakati wakitekeleza majukumu yao ikiwamo kutuhumiwa kuua wahalifu.

Akizungumza jana wakati wa sherehe za kufunga mafunzo kwa askari wa jeshi hilo katika Chuo cha Taaluma za Polisi, Kurasini jijini hapa, Rais Magufuli huku akiahidi kuwa nao bega kwa bega alisema askari wanafanya kazi kubwa ya kuimarisha usalama wa nchi.

Alisema wakati mwingine askari wamekuwa wakishtakiwa kutokana na makosa ambayo hawajayafanya wakati wakitekeleza majukumu yao ikiwamo kutuhumiwa kuua wahalifu na kwamba kufanya hivyo ni kuwavunja nguvu wale wanaojitoa kwa ajili ya Taifa.

“Nataka Jeshi la Polisi linalochukua hatua sio askari anaenda anachukua hatua anashtukia amewekwa ndani, askari amekwenda kupambana na jambazi bahati mbaya jambazi likijipiga lenyewe risasi likafa kule unakuja unamshika askari, hapana,” alisema.

Rais Magufuli ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu alisema askari wa namna hiyo wamejitoa muhanga kulinda amani ya nchi hivyo ni lazima waongezewe vyeo ili kutoa motisha kwa wengine kujitoa kwa ajili ya Taifa lao.


Katika mahafali hayo, jumla ya askari 513 walihitimu kozi za mofisa na wakaguzi wasaidizi wa Polisi baada ya kumaliza mafunzo ya miezi sita huku Mkuu wa chuo hicho, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP), Anthony Rutta akisema watatu walifariki dunia wakiwa mafunzoni.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger