Wednesday, 12 April 2017

BREAKING NEWS:HAYA HAPA MAJINA AJIRA MPYA ZA WALIMU 2016/2017

Hatimaye serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetangaza majina ya walimu walioajiriwa mwaka 2016/2017.

MASWAYETU BLOG tumejipanga na tumewawekea majina hayo bila taabu yoyote.
Share:

TAARIFA MUHIMU KWA WALIMU WAPYA KUHUSU SIKU YA KURIPOTI KATIKA KITUO CHAKO CHA KAZI 2016/2017




 

JAMHURI YAMUUGANO WA TANZANIA

Share:

MAGAZETI YA LEO JUMATANO APRIL TAREHE 12.4.2017

Share:

Tuesday, 11 April 2017

VIDEO:BAADHI YA WANANCHI WALIOPO MASWA MJINI WAKILALAMIKA KUHUSU TATIZO LA MAJI

Wananchi waliopo mjini Maswa ni kati ya watu wanaosumbuka zaidi kwa swala hili la maji.
 Image may contain: 1 person, child and outdoor
Share:

TAARIFA MUHIMU KUHUSU SIFA ZA KUJIUNGA NA VYUO VYA AFYA MWAKA WA MASOMO 2017/2018

 Image result for SERIKALI YA TANZANIA
Habari zenu wadau,

Kama kawaida yetu MASWAYETU BLOG TEAM tupo kukupa kitu roho inapenda ,na tunakuomba sana samahani kwa kutokuwa hewani kwa siku kadhaa.

Nipende kukuahidi kwamba,Tumerejea kwa kasi ya ajabu kabisa,kama unaswali unaweza kutu contact na utajibiwa bila shida.

Leo tumekuletea sifa za kujiunga na vyuo vya afya vilivyopo Tanzania katika ngazi ya diploma na cheti kwa kozi za afya mwaka huu wa masomo 2017/2018.

SIFA ZA KUJIUNGA NA KOZI ZA AFYA KWA WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDATO CHA NNE MWAKA 2016 KURUDI NYUMA

PRE-SERVICE ENTRY QUALIFICATION
1. Basic Technician Certificate Level Pharmaceutical Sciences

Holders of Certificate of Secondary Education Examination (CSEE) with four (4) passes including ‘D’ passes in Biology and Chemistry;


2. Technician certificate level Nursing, Clinical medicine, Environmental health and Pharmaceutical Sciences

Holders of Certificate of Secondary Education Examination (CSEE) with four (4) passes in non-religious subjects including ‘D’ passes in Physics/Engineering Sciences, Chemistry and Biology;and ‘D’ passes in Chemistry and Mathematics;


 Health Records and Information Technology
Holders of Certificate of Secondary Education Examination (CSEE) with ‘C’ pass in Chemistry and Biology; and ‘D’ pass in English and Mathematics;


 Medical Laboratory Sciences
Holders of Certificate of Secondary Education Examination (CSEE) with ‘C’ pass in Chemistry and Biology, and ‘D’ passes in Physics, English and Mathematics


3. Ordinary Diploma level

Nursing, Clinical medicine, Clinical Dentistry, Environmental Health Sciences, Dental Laboratory Technology and Pharmaceutical Sciences, Physiotherapy
Holders of Certificate of Secondary Education Examination (CSEE) with four (4) passes in non-religious subjects including ‘C’ pass in Chemistry and Biology; and ‘D’ pass in Physics/Engineering Sciences


 Optometry
Holders of Certificate of Secondary Education Examination (CSEE) with ‘C’ pass in Physics/Engineering Sciences and Biology; and ‘D’ passes in Chemistry and Mathematics;


 Health Records and Information Technology
Holders of Certificate of Secondary Education Examination (CSEE) with ‘C’ pass in Chemistry and Biology; and ‘D’ pass in English and Mathematics;


Medical Laboratory Sciences
Holders of Certificate of Secondary Education Examination (CSEE) with ‘C’ pass in Chemistry and Biology, and ‘D’ passes in Physics, English and Mathematics
Note: For Government institutions, applicants are required to have completed O’ Level between 2012 and 2015 (inclusively).


KUDOWNLOAD GUIDEBOOK YA KOZI NA VYUO VYA AFYA
Share:

MPYA:HII HAPA LIST YA WALIMU WANAOSUBIRIWA KUAJIRIWA MDA WOWOTE KUANZIA SASA

Image result for SERIKALI YA TANZANIA
Share:

JINSI SIMBA ILIVYOPATA USHINDI WA KIHISTORIA DHIDI YA MBAO UWANJA WA CCM KIRUMBA MWANZA

Simba wamepata ushindi wa kihistoria dhidi ya Mbao FC mechi ya ligi kuu Tanzania bara iliyochezwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba mkoani Mwanza.

Mbao FC walianza kwa kutangulia kupata magoli mawili kipindi cha kwanza na kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kuibuka na pointi tatu katika mchezo huo. Magoli ya Mbao yamefungwa na Bernard dakika ya 18 na dakika ya 33.
Hadi dakika ya 80 Simba ilikuwa nyuma kwa magoli 2-0 matokeo ambayo kama yangebaki hivyo dakika 90 zinamalizika basi Wekundu wa Msimbazi wangekuwa kwenye nafasi finyu ya kutwaa taji la ligi kuu msimu huu.
Mabadiliko yaliyofanywa na benchi la ufundi la Simba kwa kumtoa Pastory Athanas na nafasi yake kuchuliwa na Said Ndemla, Blagnon na Mavugo wakaingia kuchukua nafasi za Liuzio na Hamad ndiyo yaliyo badili mchezo na kuipa Simba ushindi wa kwanza Kanda ya Ziwa msimu huu baada ya kuchapwa 2-1 na Kagera Sugar Jumapili iliyopita.
Magoli ya Simba yamefungwa dakika za lala salama ambapo goli lao la kwanza limefungwa dakika ya 82 na Frederick Blagnon. Uzembe wa golikipa wa Mbao Erick Ngwegwe ambaye aliuacha mpira udunde kisha akashindwa kuudaka kwa usahihi ulitua miguuni mwa Blagnon akafunga goli la pili dakika ya 90+1 na kufanya matokeo kuwa 2-2.
Wakati kila mmoja akiamini mchezo utamalizika kwa sare ya Mbao 2-2 Simba, Mzamiru Yassin akaifungia Simba goli la tatu dakika ya 90+7 kwa shuti kali baada ya beki wa Mbao kupiga kichwa mpira ambao ulitua kwa Mzamiru kisha kiungo huyo wa Simba kuachia mkwaju uliomshinda mlinda mlango wa Mbao.
Ushindi huo unaifanya Simba ifikishe pointi 58 ikiwa imecheza mechi 26 na kurejea kwenye nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi kwa pointi mbili zaidi ya Yanga wanaoshuka kwenye nafasi ya pili lakini wakiwa na faida ya mechi moja mkononi.
Mbao inaendelea kubaki na pointi zake 27 ikiwa katika nafasi ya 13 kwenye msimamo wa ligi, pointi nne zaidi ya Toto Africans ambayo ipo katika timu tatu zitakazoshuka daraja.
Simba wataendelea kubaki jijini Mwanza wakisubiri kucheza dhidi ya Toto Africans timu ambayo imekuwa mwiba kwa ‘mnyama’ hususan mechi inapochezwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba.
Mbao FC wamefungwa mechi zao zote (mbili) walizokutana na Simba msimu huu. Kabla ya kuchapwa 3-2 leo April 10, 2017, walifungwa 1-0 kwenye mchezo wa raundi ya kwanza uliochezwa October 20, 2016 kwenye uwanja wa Uhuru, Dar.
Swali ambalo mashabiki wengi wa Simba huenda wakawa hawajalipatia majibu ni kwanini Ibrahim Ajib, Laudit Mavugo, Said Ndemla na golikipa Daniel Agyei kuanzia nje wakati wanne hao wamekuwa wakifanya vizuri kwenye mechi za hivi karibuni?
Kikosi cha Simba kilichoanza kwenye mechi dhidi ya Mbao kiliongozwa na Juuko Murshid (nahodha), Peter Manyika Jr (GK), Hamadi Juma, Mohamed Hussein, Bessala Bokungu, James Kotei, Mzamiru Yassin, Juma Liuzio, Mohamed Ibrahim na Pastory Athanas.
Walionzia benchi ni Daniel Agyei, Mwinyi Kazimoto, Frederick Blagnon, Hija Ugando, Ibrahim Ajib, Said Ndemla na Laudit Mavugo.
Matokeo kutoka uwanja wa Manungu Complex, Turiani, Morogoro
Mtibwa Sugar 0-0 Azam FC
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger