Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu imesema kuwa haihusiki kumtafutia mnufaika wa mkopo ajira badala yake inahusika kumpatia mwanafunzi mkopo na akishamaliza muda wa masomo atatakiwa kurejesha mkopo wake.
Hayo yamesemwa jana
Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na
Mawasiliano kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Cosmas Mwaisobwa
wakati akijibu maswali ya wananchi kupitia kipengele cha Kikaango cha EATV.
“Bodi
ya Mikopo ya Elimu ya Juu inatoa mikopo suala la kutafuta ajira
halituhusu hivyo mnufaika yoyote asiwe na kigezo kwamba hajapata kazi ,
hiyo siyo kazi yetu, kazi yetu ni kuwawezesha kupata elimu basi” Alisema Mwaisobwa.
Aidha Mwaisobwa alisema
wanufaika wote ambao walipata mikopo wanatakiwa kukatwa asilimia 8% ya
pato la mwezi, na kama mtu anafanya kazi binafsi na hakatwi popote
atatakiwa kutoa kiwango cha 120,000/= na kwa ambao wamenufaika na
hawataki kuanza kulipa mkopo watapigwa penati ya 10% ya mkopo kwa mwaka.
Pamoja
na hayo Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu imewataka walioomba mikopo
kuvuta subira kwani Bodi inasubiri majina kutoka Tume ya Vyuo Vikuu ili
Bodi ya Mikopo iweze kufahamu vyuo walivyopangiwa na kiwango cha ada ili
haki iweze kutendeka kwa waombaji.
This is to inform all Finalists and Continuing Students of the
University of Dodoma that, Supplementary/ Special Examinations will
commence on 3rd to 7th October, 2016 at your respective Colleges.
Kindly observe the Time Table for Supplementary/Special Examinations at UDOM website (www.udom.ac.tz) two weeks before commencement of examinations.
Failure to attend such examinations will lead to discontinuation from studies.
Serikali
imekataa kuongeza fedha za kujikimu kwa wanafunzi wa elimu ya juu
wanaopatiwa mikopo na Serikali kutoka Sh8,500 hadi kufikia Sh10,000 kwa
siku.
Naibu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Stella Manyanya amelieleza
Bunge kuwa kiwango hicho kitaendelea hadi utakapofanyika utafiti baada
ya miaka miwili.
Manyanya
alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Zainabu Katimba (CCM),
aliyetaka kujua kama Serikali itakuwa tayari kuongeza fedha kwa
wanafunzi hadi kufikia Sh 10,000 kwa madai gharama za maisha zimepanda.
Amesema
bodi ya mikopo ilifanya ongezeko la fedha za kujikimu kwa wanafunzi wa
vyuo vikuu kwa Sh1,000 kutoka Sh7,500 hadi kufikia 8,500 katika mwaka
2015/16.
“Ongezeko
hilo haliendani na kasi ya mfumuko wa bei uliorekodiwa na Ofisi ya
Taifa ya Takwimu (NBS) kutoka asilimia 4.2 Februari 2015 hadi kufikia
asilimia 5.6 Februari 2016,” amesema Katimba.
Naibu
waziri amesema Serikali imekuwa ikifanya utafiti wa gharama halisi za
maisha kwa wanafunzi ambazo hujumuisha malazi na chakula.
Amesema
katika mwaka wa fedha wa 2014/15 Serikali kupitia bodi hiyo ilifanya
utafiti katika vyuo vyote nchini ili kujua gharama halisi za chakula na
malazi na kuonyesha kuwa gharama halisi ilikuwa ni kati ya Sh8,000 hadi
8,500.
Naibu
waziri amesema wizara itafanya utafiti mwingine ili kubaini gharama
halisi za chakula na malazi kwa wanafunzi hao na matokeo yake yatatumika
kupanga viwango vya fedha zitazolipwa kwa wanafunzi.
Kama kawaida yetu MASWAYETU BLOG
katika nusanusa yetu tumefanikiwa kunasa hii ambayo ilikuwa ikisubiriwa
na watu wengi,ni kuhusu majina ya wanafunzi waliochaguliwa na TCU
2016/2017 kujiunga vyuo vikuu mbalimbali 2016/2017. wale wote mlioomba vyuo kama,
Chuo Kikuu cha Ardhi, (ARU)
Chuo Kikuu cha Hubert Kairuki (HKMU),
International Medical and Technological University (IMTU)
Moshi University College of Cooperative and Business Studies(MUCOOBS-MOCCU)
Chuo Kikuu cha Mlima Meru
Chuo Kikuu cha Muhimbili (MUHAS)
Chuo Kikuu cha Morogoro (MUM)
Chuo Kikuu cha Mzumbe (MU)
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT)
Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCO)
Chuo Kikuu St. Augustine cha Tanzania (SAUT)
Chuo Kikuu St. John cha Tanzania (SJUT)
Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA)
Chuo Kikuu cha Zanzibar
Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji-TEKU
Chuo Kikuu cha Tumaini (TU)
Chuo Kikuu cha Bukoba
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), established in 1970 from the split of the Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki
Chuo Kikuu cha Dodoma,UDOM
Chuo Kikuu cha Zanzibar (ZU)
NOTE:LINK IMEKAA POA ,ANDAA USERNAME NA PASWORD YAKO ILI UONE KAMA UMECHAGULIWA KWA KU LOGIN KWENYE PROFILE YAKO! kuangalia umechaguliwa wapi bofya HAPA