Sunday, 11 September 2016
Saturday, 10 September 2016
MPYA:KUHUSU MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA VYUO VYA AFYA,UALIMU,KILIMO,MIFUGO,UVUVI NK.CHETI NA DIPLOMA SECOND SELECTION 2016/2017

Kutokana na NACTE kutangaza kwamba tarehe 5 sep wangetangaza majina ya wanafunzi ambao watakuwa wamechaguliwa kujiunga na vyuo mbalimbali awamu ya pili,hali haikuwa hivyo na kuamua MASWAYETU BLOG kufuatilia swala hili.
Ukweli ni kwamba SELECTION ZIPO TAYARI ,UNAWEZA KU LOGIN KWENYE PROFILE YAKO NA KUANGALIA KAMA UMECHAGULIWA.Kama ikitokea hujachaguliwa tafadhali badilisha machaguo yako kabla ya sep 15 kwani system ipo wazi.
Maswayetu Blog tunakupenda sana.
Kulogin kwenye profile yako bonyeza hapo>>LOG IN NACTE
Official VIDEO | King Crazy GK - Mzuri Pesa | Watch/Download
MPYA:HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA SCHORALSHIP ZA ALGERIA 2016/2017
Selected Algeria Scholarships 2016-2017
RAIS MAGUFULI ATEUA MAKATIBU TAWALA WA MIKOA,WAKURUGENZI WA HALMASHAURI 13
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe
10 Septemba, 2016 amemteua Bw. Eliya Mtinangi Ntandu kuwa Katibu Tawala
wa Mkoa wa Songwe.
Taarifa
iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa
nafasi ya Katibu Tawala Mkoa wa Songwe ilikuwa wazi na uteuzi huu
umeanza leo.
Bw.
Eliya Mtinangi Ntandu pamoja na Makatibu Tawala walioteuliwa jana
tarehe 09 Septemba, 2016 ambao ni Ado Steven Mapunda aliyeteuliwa kuwa
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara na Bw. Tixon Tuliangine Nzunda
aliyeteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa wataapishwa katika
tarehe itakayotangazwa baadaye.
Wakati
huo huo, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa Wakurugenzi
wa Halmashauri za Wilaya 11, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji 1 na
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa 1 ili kujaza nafasi zilizokuwa
wazi katika Halmashauri hizo.
Wakurugenzi walioteuliwa ni kama ifuatavyo;
1. Godwin Emmanuel Kunambi - Manispaa ya Dodoma
2. Elias R. Ntiruhungwa - Mji wa Tarime
3. Mwantumu Dau - Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
4. Frank Bahati - Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe
5. Hudson Stanley Kamoga - Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu
6. Mwailwa Smith Pangani - Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo
7. Godfrey Sanga - Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama
8. Yusuf Daudi Semuguruka - Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
9. Bakari Kasinyo Mohamed - Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea
10. Juma Ally Mnwele - Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo
11. Butamo Nuru Ndalahwa - Halmashauri ya Wilaya ya Moshi
12. Waziri Mourice - Halmashauri ya Wilaya ya Karatu
13. Fatma Omar Latu - Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo
Wakurugenzi
wa halmashauri wote 13 walioteuliwa wanatakiwa kuripoti Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mkoani Dodoma siku ya
Jumanne tarehe 13 Septemba, 2016 kwa ajili ya kupata maelekezo zaidi.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
10 Septemba, 2016
MTANGAZAJI WA CLOUDS TV ATEULIWA NA RAIS MAGUFULI KUWA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBULU

Leo Septemba 10, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya 11, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji 1 na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa 1 ili kujaza nafasi zilizokuwa wazi katika Halmashauri hizo.
Miongoni
mwa Wakurugenzi wa Halmashauri walioteuliwa, yumo pia mtangazaji wa
kipindi cha Clouds 360 cha Clouds Tv kinachorushwa kila siku kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa.
Hudson
Stanley Kamoga ameteuliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuwa
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara.
Hii
sio mara ya kwanza kwa Rais Magufuli kuteua watangazaji kushika
nyadhifa mbalimbali kwani alimteua aliyekuwa Mtangazaji wa ITV, Godwin
Gondwe kuwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni.
Wakurugenzi wengine walioteuliwa leo ni pamoja na;-
- Mwailwa Smith Pangani – Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo
- Godfrey Sanga – Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama
- Yusuf Daudi Semuguruka – Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
- Bakari Kasinyo Mohamed – Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea
- Juma Ally Mnwele – Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo
- Butamo Nuru Ndalahwa – Halmashauri ya Wilaya ya Moshi
- Waziri Mourice – Halmashauri ya Wilaya ya Karatu
- Fatma Omar Latu – Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo
- Godwin Emmanuel Kunambi – Manispaa ya Dodoma
- Elias R. Ntiruhungwa – Mji wa Tarime
- Mwantumu Dau – Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
- Frank Bahati – Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe









































