Nacte wametoa majina ya wanafunzi waliofanikiwa kuchaguliwa katika vyuo mbalimbali afya,ualimu ,kilimo na mifugo kwa level ya cheti na diploma.
Pia inakaribisha maombi mapya kwa wanafunzi wapya.
Baraza linapenda kutoa taarifa kuwa
Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) umefunguliwa tena kuanzia tarehe 22
Julai 2016 ili kujaza nafasi za udahili zilizo wazi baada ya Baraza
kuchagua waombaji udahili waliowasilisha maombi yao kuanzia tarehe 4
Machi 2016 hadi tarehe 3 Juni 2016. Mwisho wa kuwasilisha maombi ni
tarehe 5 Agosti 2016 saa sita usiku. Waombaji wapya na baadhi ya waombaji
walioshindwa kukamilisha maombi yao kupitia mtandao ilipofika tarehe 3
Juni 2016, wanaarifiwa kuanza kuwasilisha maombi ya udahili kupitia
Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) ili kujaza nafasi zilizo wazi. Waombaji
wanahimizwa kutumia muda huu wa nyongeza ili kuwasilisha maombi. Baraza linapenda pia kuwaarifu
waombaji udahili na umma kwa ujumla kuwa vikao vya Kamati za kuidhinisha
majina ya waombaji udahili kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS)
vilipitisha orodha ya majina ya wenye sifa za udahili kulingana na
nafasi za udahili kwa kila kozi zitolewazo na vyuo husika kati ya tarehe
18 Julai 2016 na 21 Julai 2016. Majina ya waombaji waliochaguliwa kwa
kila kozi itolewayo na chuo husika yamekabidhiwa vyuoni kupitia Mfumo wa
Udahili wa Pamoja (CAS). Waombaji waliochaguliwa nao wamearifiwa
kupitia kurasa (profile) zao binafsi au kwa kubofya hapa. Waombaji ambao hawakuchaguliwa wamejulishwa sababu zilizowafanya wasichaguliwe kupitia kurasa (profile) zao pia. Kwa waombaji wa Shahada ya Kwanza
waliowasilisha maombi yao kupitia NACTE, Baraza linapenda kuwaarifu
kuwa, mashauriano kati ya NACTE na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU)
yanaendelea kufanyika ili kufanikisha udahili wa waombaji wa kozi za
Shahada ya Kwanza kama Serikali ilivyoagiza.

Kufuatia
zoezi linaloendelea la kuhakiki wanafunzi wanufaika kwa mikopo kupitia
bodi ya Mikopo, Chuo kimeagizwa kusogezwa mbele mafunzo kwa vitendo
yaani "Field practical and Teaching Practice session"
Waziri wa TAMISEMI amesema kwamba awamu ya pili inasubiri nafasi zitakazojitokeza kutokana na
wanafunzi watakao acha kuripoti kwa kupelekwa na wazazi wao kwenye
shule binafsi au vyuo binafsi na vya serikali.
Pia Mheshimiwa Simbachawene aliziagiza mamlaka zinazohusika na kuwapokea
wanafunzi wapya wa kidato cha tano kuhakikisha kuwa miundombinu yote
muhimu inakamilika ikiwemo mabweni, madarasa vyoo na Maabara, samani
(vitanda, Meza na Viti huduma za Maji na Umeme zinatekelezwa na
kukamilika kwa wakati.
Katika mwaka 2016 jumla ya shule mpya za kidato cha tano 50 zimeanzishwa
kutokana na maombi ya mikoa kwenye maeneo yao ili kuendana na lengo la
Serikali la kuongeza Shule za Kidato cha Tano na Sita.
Hivyo, Waziri Simbachawene amewataka Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na
Wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha kuwa shule zote zina walimu na
vitabu vya kujifunzia na kufundishia na pia kuhakikisha chakula kwa
wanafunzi wa bweni kinaandalaiwa kabla wanafunzi wapya wa kidato cha
tano hawajaripoti.
Habari yenu? Kutokana na wadau weng kuuliza kuhusu ushauri wa kozi gani za kuchagua kutokana na matokeo aliyopata,nimeamua kuweka hapa ushauri ambao naamini kwa asalimia zaidi 90% nitagusa kila mtanzania,mwenye haja ya kujua haya mambo.
KAMA ULISOMA PCB/CBG
PCB ni moja ya combination ambayo inajumuisha masomo ya PHYSICS,CHEMISTRY NA BIOLOGY.Wengi wa wanafunzi wanaoenda kusoma masomo haya a level,ndoto zao ni kuwa madaktari,wafamasia,lab technologist na nursing.
Ukweli ni kwamba baada ya matokeo ya kidato cha sita malengo ya wengi huwa yanapotea kutokana na kupata maksi ambazo haziridhishi kwenda chuo kikuu kusomea masomo hayo ya afya.
Nina recommend:kama umepata PCB DIV III pts 13 kwenda-14,15 etc.Ninakushauri usisumbuke kuomba MEDICINE/PHARMACY hii inawahusu wote wenye D D,C E, kupata kozi hizo ni ngumu sana kwa vyuo vya MUHIMBILI,BUGANDO,KCMC,UDSM sio kwamba hauna sifa,sifa unazo ila tatizo ni competition.
Ninakushauri uombe kozi za kilimo -zilizopo SUA kama agronomy,agri general,hortculture,aqualculture,animal science,food science and technology,human nutrition etc.zipo pale sua.
Nursing:Vile vile kama hauna matokeo mazuri ya form six ninakuomba usiombe kozi hii,hii ni kutokana na competition.
Ninakushauri kama kwenu wanuwezo wa kukulipia ada ya kuongezea omba chuo cha KAMPALA UNIVERSITY lakini ada yake ni kubwa sana.
Ushauri wangu huu nakuomba uuzingatie kwa umakini sana hii ni kutokana na KUFUTWA KWA KOZI ZA MEDICINE UDOM,IMTU,ST.JOSPEH,ST.FRANCIS maana yake competition itakuwa ni kubwa sana.
hivyo kukufanya wewe ukose chuo.
Pia unaweza kutazama tcu guide book course mbalimbali mpya zitolewazo hapa tanzania,lakini kwa swala la MEDICINE/PHARMACY/NURSING ni ngumu kupata kutokana na matokeo hayo.
MADHARA YA KUKOSA CHUO AWAMU YA KWANZA
Endapo hutazingatia ushauri wangu na ukachagua kozi hizo za afya na wakati ufaulu wako ni mdogo sana,utakosa chuo baada ya hapo,itakulazimu uchague kozi mpya kutoka kwenye vyuo vingine ambavyo vitakuwa vinanafasi. Hapo ndipo ndoto za wengi hupotea kutokana kulazimika kusoma kitu mabacho hikupendi.FANYA MAAMUZI SAHIHI SASA,KABLA HUJAKOSA FISRT ROUND.
Mwaka jana walikosa zaidi ya wanafunzi 13,000 fisrt round.