Sunday, 3 July 2016
Friday, 1 July 2016
Mtumishi wa umma atakayekwenda kusomea 'first degree' sasa kuchukua likizo isiyo na malipo
Mtumishi atakayekwenda kusomea FIRST DEGREE anatakiwa achukue LIKIZO
ISIYO NA MALIPO na hastahili kulipwa chochote na Mwajiri wake ikiwa ni
pamoja na kutolipwa Mshahara kwakuwa HAYUPO KAZINI.
Hakuna malipo yoyote ya UHAMISHO kwa Mtumishi atakayehamishwa umbali usiozidi kilometa 10.
Hakuna malipo yoyote ya UHAMISHO kwa Mtumishi atakayehamishwa umbali usiozidi kilometa 10.
MPYA: Serikali imezuia Benki kupandisha viwango vya tozo katika miamala yake
TRA wamesema taasisi za fedha wanapoongeza makato ya miamala ya fedha wanakosea kwa kupandishia wananchi kwa kuwa sheria hiyo inahusu fedha ambayo mwanachi alikuwa anakatwa na taasisi hizo ambayo hapo mwanzoni zilikuwa azilipiwi kodi kwa hiyo hizo ndizo zitakazokatwa 18%.
Mfano kama umetoa fedha ukakatwa 1000 na taasisi ya fedha ilikuwa haikatwi kodi lakini kwa sheria hiyo ada hiyo ndio itakatwa 18% na sio mwananchi kuongezewa makato kama ilivyofanyika kwa baadhi ya taasisi za fedha.
PICHA :Ajali Ya basi iliyotokea Mkoani Morogoro -imeua 11
Habari iliyoripotiwa hivi punde na kituo cha ITV ni kuhusu ajali ambayo imetokea eneo la Veta Dakawa mkoani Morogoro ikihusisha magari matatu ambayo ni lori la mafuta, kontena lililobeba mchele pamoja na basi.
Taarifa hiyo inasema kuwa watu 11 wamefariki dunia na wengine ambao idadi yao bado haijajulikana wamejeruhiwa.
Tunaendelea kufuatilia taarifa zaidi kuhusu ajali hiyo.
Waziri Mkuu: Serikali Itatoa Waraka Juu Ya Ukusanyaji Mapato Kupitia Mawakala
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema Halmashauri zitaelekezwa kwa waraka ni
vyanzo vipi vitahitaji kutumia wawakala wa ukusanyaji mapato kwani siyo
kila chanzo cha mapato ya Halmashauri kitakusanywa kwa ufanisi kwa
kutumia au kwa kutotumia mawakala.
Waziri
Mkuu ametoa agizo hilo jana mchana (Alhamisi, Juni 30, 2016) wakati
akitoa hoja ya kuhitimisha mkutano wa tatu wa Bunge la 11 la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.
Alisema
katika ukusanyaji wa mapato, baadhi ya vyanzo vitapaswa kukusanywa na
Halmashauri zenyewe kwa kuzingatia miongozo iliyotolewa na Serikali.
“Moja
ya miongozo hiyo ni kwamba kuanzia sasa, iwe kwa kutumia mawakala au
Halmashauri zenyewe ni lazima fedha zinazokusanywa ziwekwe kwenye
akaunti ya Halmashauri na kutumia mifumo ya kielektroniki ili kupunguza
au kumaliza kabisa masuala ya kutumia malipo kwa fedha taslimu (cash
transactions),” alisema.
Alisema
katika kutekeleza agizo hilo, Halmashauri itabidi zikubaliane na wakala
ni kiasi gani cha asilimia ya makusanyo kitalipwa kwa wakala na malipo
yafanyike baada ya kukusanya na kuingizwa kwenye akaunti ya Halmashauri.
Alisema
Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa Sura ya 290, inazipa uwezo Mamlaka
za Serikali za Serikali za Mitaa kutoza na kukusanya kodi, ushuru na
ada mbalimbali kama vyanzo vya mapato vya Mamlaka za Serikali za Mitaa.
“Sheria
hiyo pia inazipa mamlaka hizo kuteua mawakala wa kukusanya mapato hayo
kwa niaba ya Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kuzingatia sheria, kanuni
na taratibu. Lakini Serikali imebaini changamoto za kiufundi katika
kufanya tathmini ya vyanzo vya mapato; ugumu katika kupata mawakala
wenye weledi katika ukusanyaji mapato na kubuni vyanzo vipya vya mapato,
na wakati mwingine watumishi wenyewe kujipa uwakala kinyume na taratibu
zinazomzuia mtumishi kufanya biashara na taasisi yake,” alisema.
Alisema
hatua ya Mamlaka za Serikali za Mitaa kutumia mawakala ni miongoni mwa
mikakati ya kuboresha ukusanyaji mapato na pia kutoa muda mwingi zaidi
kwa watumishi wa mamlaka hizo kushughulika na majukumu ya msingi ya
Halmashauri na hasa utoaji wa huduma kwa wananchi na usimamizi wa miradi
ya maendeleo.
“Pamoja
na dhamira nzuri ya hatua hizo, tunayo mifano ya baadhi ya Halmashauri
kama vile Nzega ambayo baadhi ya wahusika wameshinikiza wakitaka zabuni
zote wapewe madiwani. Jambo hili halikubaliki na tena ni kinyume cha
maadili ya utumishi,” alisisitiza.
Katika
hatua nyingine, Waziri Mkuu ameziagiza Halmashauri zote nchini kwamba
kuanzia Julai Mosi, 2016 zihakikishe zinatumia mifumo ya kielektroniki
katika kukusanya mapato, katika kulipa, kuweka na kutekeleza kikamilifu
mikakati madhubuti ya kuboresha makusanyo iwe yanakusanywa na
Halmashauri au na wakala.
Alisema
Mamlaka za Serikali za Mitaa zina wajibu wa kutoa taarifa kwa wananchi
kuhusu mapato na matumizi ya Serikali pamoja na michango ya wananchi
licha ya kuwa uzoefu unaonesha kuwa mamlaka hizo zina tatizo la kukaa na
fedha kwa muda mrefu kabla ya kuzielekeza kwenye matumizi
yaliyokusudiwa.
“Kuchelewesha
kutoa fedha zilizotengwa kwa shughuli zilizopangwa ni kuchelewesha
kufikisha huduma muhimu kwa wananchi. Napenda kuhimiza uzingatiaji wa
utaratibu wa kutoa taarifa kwa wananchi kuhusu mapato na matumizi ya
fedha za Serikali katika ngazi zote ili kuongeza uwazi na uwajibikaji
katika sekta ya umma,” aliongeza.
Mkutano
huo wa tatu wa Bunge ulioanza Aprili 19, 2016 ulikuwa mahsusi kwa ajili
ya kujadili na kupitisha bajeti ya kwanza ya Serikali ya Awamu ya Tano
pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
Bunge limeahirishwa hadi Septemba 6, mwaka huu litakapokutana tena mjini
Dodoma.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S.L. P. 980,
DODOMA.
ALHAMISI, JUNI 30, 2016
Thursday, 30 June 2016
MPYA:MKURUGENZI WA TBS ATUMBULIWA JIPU,PIA MENEJA WA FEDHA APIGWA CHINI
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage leo amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa shirika la Viwango Tanzania TBS Bwana Joseph B. Masikitiko ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili.
Pia Waziri Mwijage ameagiza Bwana Emmanuel M. Ntelya Meneja wa Fedha, Mipango na Utawala wa TBS, asimamishwe kazi mara moja kwa kipindi chote ambacho uchunguzi utakuwa unaendelea. Aidha waziri amemteua Dkt Egid B. Mubofu, Mkuu wa Idara ya Kemia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kukaimu nafasi ya Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania.
KESI YA UCHOCHEZI:TUNDU LISSU APEWA DHAMANA,YAHAIRISHWA HADI AGOSTI 12 2016
UPDATES:
Lissu anatetewa na wanasheria 17 wakiongozwa na John Mallya Peter Kibatala na timu nyingine toka makao makao makuu ya Chama.
Viongozi wote wa makao makuu wameshawasili,
Tunasubiri Hakimu tu aingie kwenye ukumbi wa mahakama...
UPDATES,
Tayari Hakimu anayesikiliza shauri ameshawasili, sasa ni utambulisho wa mawakili wa pande zote,
Kesi inaanza kusomwa,
Mwendesha mashitaka: Tundu Lisu anashitakiwa kwa makosa ya uchochezi, mnamo tarehe 28/06/2016 akiwa eneo la mahakama kwania ya kudhalau umma dhidi ya mamlaka yao walioyoichagua kihalali, alisema huyu dikteta uchwara lazima tumpinge kila kona"
Hakimu: Mshitakiwa, unakubali au unakataa?
Lissu: nakataa yote
Mwendesha mashitaka: Mh Hakimu ushahidi wa shauri hili umekamilika, tunaomba tarehe ya kuanza usikilizwa,
Hakimu: Mawakili wa utete mnalololote la kusema?
Wakili: Mheshimiwa kwamjibu wa kifungu cha sheria na.... Mshitakiwa kosa aliloshitakiwa linadhaminika, hapa tunao wadhamini na zaidi mshitakiwa ni mbunge na mwanasheria wa chama, hivyo anadhaminika, na zaidi mshitakiwa aliliripoti mwenyewe mbele ya polisi baada ya kuitwa tu kwa simu. Ni hayo tu mh
Mwendesha mashitaka: Mshitakiwa aliyembele yako, mnamo tarehe 28 mwenzi huuhuu alifikishwa mahakamani kwa kosa...... Aaah nimesahau sina nakala ya mashitaka, na wenzake watatu na kudhaminiwa. Hivyo akatenda kosa hili, huyu ana nidhamu mbovu, ameona kutenda kosa ni kawaida,
Hakimu: Kwanini unamhukumu kwa kosa ambalo mahakama hii haikumtia hatiani...na siajabu akitoka hapa atatenda kosa tena....
Wakili: Mh hakimu nashindwa kujua huyu wakili wa serikali anajipa kazi ya hukumu kwa kesi iliyopo mahakamani, nimshauri arudi kwenye kesi iliyopo mezani kwakuwa kesi ya nyuma ni tuhuma tu na sio hukumu inayoweza kutumika kama kielekezo hapa.
Mwanasheria: Mh huyu mtuhumiwa ni mzoefu wa kutenda makosa...... Watu wanaangua kicheko kwa kwa kwa...
Hakimu..... Wakili
Wakili: Kwanza Mh hakimu naomba ifahamike kwamba upande wa serikali wamekubali kuwa suala la dhamani liko wazi, hili liweke katika kumbukumbu... Haya anayoyaleta sasa huyu mwanasheria hayana msingi, kwani kwa mjibu wa vifungu vya sheria na.....na... Vinampa haki yakupata dhamana, izingatiwe kuwa katika dhamana ya kesi ya mwanzo hakukuwa na mashariti ya mtuhumiwa kutotoa maoni ama kutenda kosa nje ya lile.. Izingatiwe kuwa sababu za kukidhi dhamana tumeshazitoa
Hakimu: Mahakama inaamua kuwa mtuhumiwa apewe dhamana, wadhamini wa mtyhumiwa waje mbele...kuhakiki nyaraka zao
Mwanasheria: Anainuka... Mh Hakimu...
Hakimu anasema Jamhuri haijajenga hoja za kutosha kuzuia dhamana.Kwahiyo hakuna Pingamizi la Dhamana
Anawaita Wadhamini
Wamejitokeza Mbunge Susan Lyimo, Madiwani Humphrey Sambo na Rose Moshi Kwa ajili ya kudhamini
Amepewa dhamana.Asanteni
UFAFANUZI KUHUSU SIFA, VIGEZO NA MASHARTI YA KUPATA MKOPO 2016/2017
Kwanza natumaini mu wazima wa afya,pia kwa upande wangu namshukuru Mungu nipo fresh kabisa.
Leo nimeamua kufafanua kwa kina vigezo na masharti ya Kupata mkopo mwaka wa masomo 2016/2017.
NANI ANAFAA KUPATA MKOPO?
mwanafunzi anaehitaji mkopo lazima akidhi vigezo vifuatavyo;
1.yatima aliepoteza mzazi/wazazi asiezidi miaka 30
2. Mwanafunzi mwenye disiability au mzazi wake hajiwezi asiezidi
miaka 30 pia awe na cheti
kinachotambuliwa na doctor wa wilaya.
3.Mwanafunzi anaetoka ktk familia maskini na awe anatambuliwa
na jamii.
4.Mwanafunzi ambae alikuwa akisomeshwa na wafadhili kutokana
na kutokujiweza.
VIGEZO VITAKAVYOKUFANYA UPATE MKOPO 2016/2017.
1.Lazima uwe mtanzania
2.Lazima uombe mkopo thru online system.
3.Lazima uwe umechaguliwa na chuo chochote kikuu either thru TCU au NACTE.
4.lazima awe mwanafunzi aliefaulu na anaendelea na masomo(hii inawahusu waliopo chuoni)
5.Asiwe mwanafunzi anaedhaminiwa na mtu yeyote au organization.
SIFA ZA NYONGEZA ZITAKAZOKUFANYA UPATE MKOPO 2016/2017
1.Kwa form 6 ,Uwe umemaliza kati ya mwaka 2014-2016-DIRECT
2.Kwa diploma uwe umemaliza kati ya mwaka 2014-2016-INDIRECT
KOZI KIPAUMBELE MWAKA 2016/2017
Zifuatazo ni kozi ambazo ni kipaumbele kwa mwaka wa masomo 2016/2017 ktk kupewa mkopo,kozi hizi zimegawanyika mara mbili Kuna PART A NA PART B
PART A
Priority courses include: -
i) Education (Science) and Education (Mathematics);
ii) Health Sciences (Doctor of Medicine, Dental Surgery,
Veterinary Medicine, Pharmacy, Nursing, Midwifery, BSc in
Prosthetics and Orthotics, BSc in Physiotherapy, BSc in Health
Laboratory Sciences, BSc in Medical Laboratory Sciences and
BSc in Radiotherapy Technology) and other Health Sciences;
iii) All Civil and IrrigationEngineering;
iv) All Petroleum and Gas Engineering;
NOTE:wanafunzi wote mtakaochaguliwa katika kozi hizi za PART A mtapewa mkopo wote bila kuangalia kigezo cha MWAKA ULIOMALIZA SHULE.
PART B:
wanafunzi hawa wote wanasifa za kupata mkopo,hivyo basi watapewa mkopo kulingana na mahitaji yao waliyonayo tofauti na PART A ambapo wote watapata mkopo bila kuangalia kigezo chochote.
Priority courses cluster II include:
i) Engineering Programmes (Civil, Mechanical, Electrical, Mining, Mineral and Processing, Textile, Chemical and Processing, Agriculture, Food and Processing, Automobile, Industrial, Electrical and Electronics, Legal and Industrial Metrology, Maritime Transportation, Marine Engineering Technology, Electronics and Telecommunication, Computer, Computer Science Software, Information Systems and Network, Environmental, Municipal and Industrial Services, and Bio-Processing and Post-Harvest)
iii) Agricultural and Forestry Sciences Programmes (Agriculture, Agronomy, Horticulture, Agricultural Economics and Agribusiness,
Forestry, Aquaculture, Wildlife Management, Life Sciences, and Food Science and Technology)
iv) Animal Sciences and Production
v) Science Programmes (BSc General, BSc in/with Applied Zoology, Botanical, Chemistry, Physics, Biology, Microbiology, Molecular Biology and Biotechnology, Fisheries and Aquaculture, Aquatic Environmental Sciences and Conservation, Geology, Petroleum Geology, Petroleum Chemistry, Mathematics, Mathematics and Statistics, Environmental Science and Management, Environmental Health, Biotechnology and Laboratory, Wildlife and Conservation and Computer)
vi) Land Sciences Programmes (Architecture, Landscape and Architecture, Interior Design, Building Survey, Building Economics, Urban and Regional Planning, Land Management and Valuation, and Geospatial Sciences).
NOTE:wanafunzi wote mtakaochaguliwa kozi hizi ili upate mkopo lazima uwe umemaliza kati ya mwaka 2014-2016
KWA KOZI ZOTE ZA ARTS NA BIASHARA AMBAZO HAZIJAORODHESWA HAPO JUU KTK PART A NA B
Wanafunzi watakaochagua kozi hizi wanahesabiwa kama wapo katika kozi ambazo ni NON PRIORITY ,hivyo basi WATAPATA MKOPO TU endapo wote waliochagua kozi PRIORITY PART A na B kuwa wamepata.
KAMA UTACHAGULIWA OPEN UNIVERSITY
*wanafunzi wote waliochaguliwa open univeristy watapewa MKOPO wa BOOKS AND STATIONARY ONLY
ENDAPO UTAPATA MKOPO,HUU NDIO MCHANGANUO
i. Meals and Accommodation charges
ii. Books and Stationery expenses
iii. Special Faculty Requirements expenses
iv. Field Practical Training expenses
v. Research expenses
vi. Tuition Fees
KUHUSU DIVISION I AND II AU UPPER SECOND CLASS KUPEWA MKOPO
Jamani kwa ambao hamuelewi swala hili ni kwamba,hii inawahusu wanafunzi watakaodahiliwa katika kozi za MEDICINE,VETERNARY MEDICINE NA LABORATORY ndio watapewa GRANT,means hawatarudisha pesa yoyote hivyo basi wakimaliza chuo inabidi waifanyie serikali kazi si chini ya miaka 5 kwanza.
JINSI YA KUOMBA MKOPO
A:LIPIA MPESA
1. To get MPESA Menu dial *150*00# (Piga *150*00#)
2. Choose option 4 for Pay by MPESA (Lipa kwa MPESA) |
3. Choose option 3 for Choose Business (Chagua aina ya Biashara unayolipa) |
4. Enter 8 for Education Services(Ingiza 8 kwa Huduma za Elimu) |
5. Enter 2 for HESLB(Ingiza 2 kwa HESLB) |
6. Enter 1 for Reference Number (Ingiza 1 kwa namba ya kumbukumbu) |
7. Enter Account Number (Ingiza namba yako ya kumbukumbu), which is your formatted 15 character form 4 index number e.g. S0143.0012.2009 |
8. Enter the amount in Tshs to pay either 30,000 or 10,000 based on your application category |
9. Enter your 4 digit PIN |
10. Enter 1 to confirm |
11. A confirmation Message will be displayed. N.B: Please keep this message privately B:BONYEZA HAPA KUOMBA>>>>>>>>>>http://olas.heslb.go.tz/index.php/olas/olas/trans_add |
MWISHO
Napenda kumaliza kwa kuwapa wito kwamba muombe mkopo kwani deadline ni 31 july 2016,Hivyo basi mtu asikutishe kuhusu kutopewa mkopo ,kikubwa muombe MUNGU akuongoze katika kujaza form,USIDANGANYE wala kusema uongo,kama baba ako ni MKUU WA MKOA,we andika ukweli.kwani hata mwaka hata miaka iliyopita kulikuwa na non priority course na mkopo walipata.
siku zote UKWELI UMUWEKA MTU FREE!
NAKUTAKIA MAOMBI MEMA,ILA ENDAPO UTAHITAJI USHAURI /MSAADA NITAKUSAIDIA BE FREE!
NADHANI NIMEJIBU MASWALI YALIYOKUWA YANAWAUMIZA WENGI.
SHARE NA MWENZAKO
wako;
BLOGGER BOY
MASWAYETU BLOG TEAM!
Breaking news:Wabunge wa CHADEMA Joseph Mbilinyi, Kubenea na James Millya wasimamisha kuhudhuria vikao vya Bunge
Wanajamvi wasalaam!
Leo hii kamati ya haki,maadili na madaraka ya bunge leo inataraji kusoma taarifa ya shauri la Mbunge Joseph Mbilinyi baada ya kutoa ishara ya matusi bungeni na kunaswa na kamera za bunge!
Tunataraji Mbunge Mbilinyi kupewa adhabu kali ili iwe fundisho kwa vizazi na wabunge wa aina yake ndani na nje ya bunge!
Kwakuwa Joseph Mbilinyi alitoa ishara ya matusi kwa bunge na wabunge tulitegemea chama chake cha CHADEMA kingempa adhabu lakini wamenyamaza kimya!
Joseph Mbilinyi (Mb) amekiri kunyoosha kidole cha kati juu wakati akitoka bungeni baada ya kusika mbunge amemtusi mama yake. Mh. Mbilinyi amejitetea kuwa ni kweli alinyoosha kidole cha kati juu baada ya kumsikia mbunge wa CCM akimtusi mama yake mzazi hivyo kupata short temper na kujikuta akitenda kosa hilo.
Pia Joseph Mbilinyi amesema kuwa alinyoosha kidole cha kati juu kama kupinga kile kilichokuwa kinafanyika na mbunge huyo wa CCM, alipoulizwa na Kamati ya Maadili inayoongozwa na Mh. Mkuchika, Mh. Mbilinyi alisema kuwa kunyoosha kidole cha kati juu hakina maana ya moja kwa moja hivyo kwa uelewa wake yeye alikuwa anapinga kitendo cha mbunge wa CCM.
Kamati ya maadili imeridhika kuwa kitendo cha Joseph Mbilinyi (Mb) kuonesha kidole cha kati juu ni kosa na kutoheshimu mamlaka ya Spika wa bunge baada ya kupitia matoleo ya maana mbalimbali ya (Kuonesha kidole cha kati juu) nchi tofauti tofauti.
Maazimio ya Kamati Maadili
Bunge limeazimia kuwa mbunge wa Mbeya Mh. Joseph Osmond Mbilinyi asimamishwe kuhudhuria vikao 10 vya bunge la 11 kuanzia kikao cha leo Juni 30 mpaka hapo adhabu itakapokuwa imekamilika. Bunge limepitisha kwa kauli moja adhabu hiyo.
Leo hii kamati ya haki,maadili na madaraka ya bunge leo inataraji kusoma taarifa ya shauri la Mbunge Joseph Mbilinyi baada ya kutoa ishara ya matusi bungeni na kunaswa na kamera za bunge!
Tunataraji Mbunge Mbilinyi kupewa adhabu kali ili iwe fundisho kwa vizazi na wabunge wa aina yake ndani na nje ya bunge!
Kwakuwa Joseph Mbilinyi alitoa ishara ya matusi kwa bunge na wabunge tulitegemea chama chake cha CHADEMA kingempa adhabu lakini wamenyamaza kimya!
Joseph Mbilinyi (Mb) amekiri kunyoosha kidole cha kati juu wakati akitoka bungeni baada ya kusika mbunge amemtusi mama yake. Mh. Mbilinyi amejitetea kuwa ni kweli alinyoosha kidole cha kati juu baada ya kumsikia mbunge wa CCM akimtusi mama yake mzazi hivyo kupata short temper na kujikuta akitenda kosa hilo.
Pia Joseph Mbilinyi amesema kuwa alinyoosha kidole cha kati juu kama kupinga kile kilichokuwa kinafanyika na mbunge huyo wa CCM, alipoulizwa na Kamati ya Maadili inayoongozwa na Mh. Mkuchika, Mh. Mbilinyi alisema kuwa kunyoosha kidole cha kati juu hakina maana ya moja kwa moja hivyo kwa uelewa wake yeye alikuwa anapinga kitendo cha mbunge wa CCM.
Kamati ya maadili imeridhika kuwa kitendo cha Joseph Mbilinyi (Mb) kuonesha kidole cha kati juu ni kosa na kutoheshimu mamlaka ya Spika wa bunge baada ya kupitia matoleo ya maana mbalimbali ya (Kuonesha kidole cha kati juu) nchi tofauti tofauti.
Maazimio ya Kamati Maadili
Bunge limeazimia kuwa mbunge wa Mbeya Mh. Joseph Osmond Mbilinyi asimamishwe kuhudhuria vikao 10 vya bunge la 11 kuanzia kikao cha leo Juni 30 mpaka hapo adhabu itakapokuwa imekamilika. Bunge limepitisha kwa kauli moja adhabu hiyo.