Tuesday, 24 May 2016

MPYA:AJIRA ZA KILIMO SERIKALINI KWA WANAFUNZI WALIOMALIZA SUA DIGRII ZIFUATAZO,DEADLINE KESHO

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

1.BLS
2.FORESTRY
3.AFISA NYUKI
4.MFUGAJI NYUKI


Image result for SERIKALI YA TANZANIA

2016-05-25
Login to Apply
000663 2016-05-25
Login to Apply
000667 2016-05-25
Login to Apply
000670 2016-05-25
Login to Apply
Share:

TFDA MWANZA YATOA TAHADHARI JUU YA SUKARI YA "KK"

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Meneja kanda ya ziwa mr Moses.Mbambe

 
 
Na. Mwandishi Wetu
 
Wakati serikali ikiendelea kukabiliana na changamoto ya uhaba wa bidhaa ya sukari na ongezeko la bei ya bidhaa hiyo, Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Ofisi ya Kanda ya Ziwa imetoa tahadhari kwa wananchi juu ya matumizi ya sukari ya Kijiko Kimoja (KK).
 
Sukari ya Kijiko Kimoja inatengenezwa na kiwanda cha 21st Century Food & Packaging Ltd kilichoko Dar es Salaam. Sukari hii ni nyeupe na imetengenezwa kwa kutumia miwa kwa silimia 99.5 na asilimia 0.5 ya vikolezo vingine nyongeza vya utamu.
 
Akiongea na wajasiliamali wa jijini Mwanza katika Semina ya Elimu kwa Umma iliyofanyika katika Shule ya Sekondari ya Mwanza, Mkaguzi Mwandamizi wa Chakula wa TFDA Kanda ya Ziwa Julius Panga alisema kuwa kumekuwa na taarifa juu ya baadhi ya watumiaji wakikiuka maelekezo ya matumizi na wafanyabiashara kuuza sukari hiyo kinyume na taratabu.
 
Panga alisema kuwa sukari ya Kijiko Kimoja ni tamu kuliko sukari nyingine kwa kuwa kijiko kimoja ni sawa na vijiko viwili na kuwa kutokana na hali hiyo wazalishaji wameweka taarifa juu ya kifungashio ambazo zinatoa maelekezo juu ya namna ya kutumia bidhaa hiyo.
 
“Sukari hii ina kiwanngo cha juu cha utamu tofauti na sukari nyingine ambazo zinatumika nchini. Hali ambayo imepelekea wagonjwa wa kisukari, wanawake wajawazito na watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano kutoruhusiwa kuitumia” alisema Panga.
 
Panga aliongeza kuwa kutokana na upungu wa bidhaa ya sukari nchini baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakiiondoa sukari hii katika vifungashio vyake na kuuzwa rejareja hali ambayo ni hatari kwa mtumiaji kwani anakuwa hapati taarifa zilizoko katika kifungashio. “Watengenezaji wa sukari hii wameifungasha katika vifungashio vya kilo moja na nusu kilo. Juu ya vifungashio kuna taarifa muhimu ambazo mteja anapaswa kuzisoma kabla hujatumia. Wauzaji wanapotoa sukari katika vifungashio vyake wanamnyima mteja haki ya kupata taarifa na kufanya uamuzi. Vitendo hivi vimekuwa vikiripotiwa katika maeneo mbali mbali ya kanda ya ziwa”.
 
Pia Panga alisema kuwa wauzaji wa chai katika baadhi ya migahawa wamekuwa wakitumia sukari ya kijiko kimoja  hali ambayo ni hatari kwa afya ya wateja kutoka katika makundi yaliyoanishwa juu ya kifungashio “ Ndani ya migahawa wanaingia watu wote hata wale ambao hawaruhusiwi kutumia sukari hii. Si vizuri kutumia sukari hii katika maeneo haya. Tunashauri wafanyabiashara wa migahawa kutumia sukari nyingine ambayo inaruhusiwa kwa makundi yote” alisema.
 
Maria Paskari ni mkazi wa Kirumba jijini Mwanza, yeye anakili kutumia sukari ambayo ilikuwa tamu kuliko sukari nyingine ambayo amekuwa akitumia. “ Nilimuagiza mtoto kwenda kununua sukari robo dukani. Alileta sukari nyeupe ambayo ilikuwa ni tamu tofauti na ambayo nilikuwa nimeizoea” alisema.
Maria anasema kuwa hakuwahi kusoma maelezo yaliyokuwa katika kifungashio.
“Sijawahi kuona sukari hii ikiwa katika vifungashio vyake. Lakini na mshukuru Mungu mimi sio mjamzito na watoto hawakuitumia. Niliitumia mwenye kwa kuweka kwenye uji ambao watoto hawakuunywa” alisema
 
Kwa upande wake muuzaji wa duka la ‘Mke Mwema’ ililiko Igombe nje kidogo ya jiji la Mwanza Bw. Justin Ntahorija alisema kuwa hajawahi kuuza sukari hiyo lakini baadhi ya wateja wamekuwa wakiwatuma watoto sukari wakiwapa maelekezo kuwa wasinunue sukari nyeupe. “Juzi alikuja mtoto akitaka sukari lakini akanieleza kuwa ameagizwa asinunue sukari kama iliyokuwa kwenye kifungashio alichokuwa amekishika. Nilivyoangalia kifungashio nikakuta ni kile cha sukari ya kijiko kimoja” alisema.
 
Bw Ntahorija aliongeza kuwa katika maeneo ya Igombe kuna taarifa nyingi za kukanganya kuhusu sukari. “Zipo taarifa zinazagaa kuwa sukari nyeupe si nzuri kwa matumizi ya binadamu na atakayekutwa nayo anakamatwa.”alisema.
 
Hata hivyo Panga alisema kuwa Sukari ya Kijiko Kimoja imesajiliwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kama zilivyo bidhaa nyingine za sukari na hivyo kufaa kwa matumizi. “Wananchi hawapaswi kuogopa kununua na kutumia sukari ya Kijiko Kimoja na sukari nyingine nyeupe. Wanachopaswa kufanya ni kufuata maelekezo yaliyoko juu ya kifungashio. Pia wafanyabiashara wanao wajibu wa kuwalinda wateja wao kwa kuhakikisha wanawapatia bidhaa zinazofaa”alisema Panga huku akitoa rai kwa wananchi kujenga tabia ya kusoma taarifa juu ya vifungashio.
 
 



"God who created you without you, will not save you without you" St. Augustine of Hippo (354-430)
Share:

HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI KIDATO CHA 6 WALIOCHAGULIWA JKT KWA MUJIBU 2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
 Image result for jkt tanzania
 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEijiWbrvWgB_apuFugq2ril93oKNmtwHDbA6aX-VYomCPl_yYj6qtSFiA1CCLQj2v8Sod2q1YWzHCSyqr5jvFR585k2DZHLtLrcjHKOhF0eat0yDLheTZGKGob0XTlLHkyqCroderfRx73-/s1600/_20160520_213958.JPG
Share:

MPYA:MZUMBE UNIVERSITY YAANZA KUPOKEA MAOMBI YA NAFASI ZA MASOMO CHETI,DIPLOMA NA DIGRII MZUMBE UNIVERSITY 2016/2017

Share:

PUBLIC NOTICE - APOLOGY ON THE CHALLENGES FACED IN ACCESSING SERVICES PROVIDED BY THE COUNCIL

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
THE NATIONAL COUNCIL FOR TECHNICAL EDUCATION
(NACTE)

PUBLIC NOTICE

This release serves to inform the Public that, The National Council for Technical Education (NACTE) sincerely apologizes to its stakeholders nationwide, for the challenges faced in accessing services provided by the Council via electronic systems.
The Council acknowledges there was a problem which caused system users to experience some difficulties while using various electronic services offered by the Council for the past four days.
The Council would like to inform the public that the problem has been solved and all systems are now operational. We apologize again for all inconveniences caused.
                                   
ISSUED BY;
PUBLIC RELATIONS OFFICE
THE NATIONAL COUNCIL FOR TECHNICAL EDUCATION
24th May, 2016
Share:

Bunge Latolea Ufafanuzi Madai ya Kitwanga Kujibu Swali Bungeni Huku Akiwa Amelewa

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY


Share:

MPYA: TAARIFA KWA WAHITIMU WA CHUO CHA CBE WALIOGUSHI MALIPO YA ADA KAMPASI YA DODOMA,HAYA HAPA MAJINA YAO

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) anatoa taarifa kwa wahitimu wote waliomaliza Chuo cha Elimu ya Biashara Kampasi ya Dodoma waliohusika na kugushi Risiti za malipo ya ada. Wahitimmu hao wanaagizwa kulipa ada hizo kabla ya tarehe  31 Mei, 2016.
Kwa yeyote atakayekiuka agizo hili hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake; ikiwa ni pamoja na kufuta Tuzo za vyeti vyao vya kuhitimu Chuo cha Elimu ya Biashara na kuvibatilisha.
Ifuatayo ni orodha ya wahitimu walioghushi malipo ya ada:-
Waliogushi malipo lakini hawajachukua vyeti
Waliogushi malipo na walishachukua vyeti
Share:

New AUDIO[RMX] | KONABEATS x ALIKIBA x MI - AJE REMIX | Download

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

DOWNLOAD via HULKSHARE
http://old.hulkshare.com/dl/gu439x4cba4g/KONABEATS_x_ALIKIBA_x_MI_-_AJE_REMIX.mp3?d=1
Share:

Rais wa Zanzibar Dr Shein Amefanya Uteuzi Wa Wakuu Wa Wilaya Na Mikoa,Angalia Majina Hapa

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi wa Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kama ifuatavyo:


1. UTEUZI WA WAKUU WA MIKOA
Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu 61(1) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi wa Wakuu wa Mikoa kama ifuatavyo:

i. Mkuu wa Mkoa wa Mjini na Magharibi – Mheshimiwa Ayoub Mohamed Mahmoud
ii. Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini, Unguja – Mheshimiwa Vuai Mwinyi Mohamed

Aidha Wakuu wa Mikoa ambao Mikoa yao haikutajwa katika taarifa hii wanaendelea na dhamana zao kama kawaida.
Uteuzi huo umeanza tarehe 23 Mei 2016.

2. UTEUZI WA WAKUU WA WILAYA
Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu 61(2) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya kama ifuatavyo:

i. Mkuu wa Wilaya ya Mjini – Mheshimiwa Marina Joel Thomas.
ii. Mkuu wa Wilaya ya Magharibi “B” – Mheshimiwa Silima Haji Haji
iii. Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini “A”– Mheshimiwa Hassan Ali Kombo
iv. Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini “B” – Mheshimiwa Issa Juma Ali
v. Mkuu wa Wilaya ya Kati – Mheshimiwa Mashavu Sukwa Said
vi. Mkuu wa Wilaya ya Kusini – Mheshimiwa Idrissa Kitwana Mustafa
vii. Mkuu wa Wilaya ya Chakechake – Mheshimiwa Salama Mbarouk Khatib

Aidha Wakuu wa Wilaya ambao Wilaya zao hazikutajwa katika taarifa hii wanaendelea na dhamana zao kama kawaida.

Uteuzi huo umeanza leo tarehe 23 Mei 2016.

Viongozi wote waliotajwa wanatakiwa waripoti Ikulu, Mjini – Unguja, siku ya Jumanne tarehe 24 Mei 2016 saa 8 za mchana tayari kwa kuapishwa.
Share:

Rais Magufuli Ateua Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mshauri wa Rais Masuala ya Uchumi

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY


Share:

BREAKING NEWS:KUSITISHWA TANGAZO LA AJIRA WIZARA YA AFYA LILILOTOLEWA JANA TAR 23.5.2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Tokeo la picha la SERIKALI YA TANZANIA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA MAENDELEO YA JAMII JINSIA WAZEE NA WATOTO

TAARIFA KWA UMMA
KUSITISHWA KWA TANGAZO LA AJIRA

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto inapendakuwafahamisha kwamba tangazo la Ajira ya dharura kwa wataalam wa fani mbili za afya za Tabibu Wasaidizi(Clinical Assistant) na Wauguzi (Enrolled Nurses) zilizotangazwa tarehe 23/5/2016 limesitishwa hadi hapo maelezo mengine yatakapotolewa
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini – Afya
23/5/2016
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger