Tuesday, 17 May 2016

MAGAZETI YA LEO JUMANNE MAY TAREHE 17.5.2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY



























Share:

Walimu 35,411 wa Shule za Msingi na Sekondari Kuajiriwa Mwezi wa 7 Mwaka Huu

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Walimu 35,411 nchini wataajiriwa katika shule za msingi na sekondari katika mwaka wa fedha 2016/2017.


Watakaokaidi kwenda kuripoti katika mikoa ya pembezoni, hawataajiriwa na serikali.


Hatua hiyo imeelezwa kwamba imetokana na serikali kupokea maombi mengi ya kazi kwa walimu, ambao mwaka jana hawakuripoti katika vituo walivyopangiwa pembezoni mwa miji kwa kutegemea kuajiriwa na shule binafsi, lakini hawakufanikiwa.


Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jaffo alisema hayo alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mchinga, Hamidu Bobali (CUF) aliyetaka kufahamu serikali inafanya nini kwa walimu waliopangiwa kwenda mikoa ya pembezoni, ikiwemo Lindi na kwingineko, lakini hawakuripoti.


Jaffo alisema ni kweli kuna walimu wengi ambao hawakuripoti katika mikoa ya pembezoni. Alisema si Lindi peke yake, bali na mikoa mingine, ikiwemo Katavi na Kigoma.


Alisema kwa mwaka huu, wataajiri walimu 35,411, lakini ambaye hataripoti katika mikoa hiyo na kuishia mijini tu, hawataajiriwa tena serikalini, kama wanavyoomba tena baada ya kukosa katika shule binafsi.
Share:

Monday, 16 May 2016

WAZIRI WA ULINZI AJIBU SWALI KUHUSU FORM SIX MWAKA HUU 2016 KWENDA JKT

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY


Share:

12 Wakamatwa Wakituhumiwa Kuhusika na Mauaji ya Watu 7 Jijini Mwanza

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Siku chache baada ya watu saba wa familia moja kuuawa kwa mapanga wilayani Sengerema mkoani Mwanza, polisi wamefanikiwa kuwatia mbaroni watu 12 kwa tuhuma za mauaji hayo huku mmojawapo akikamatwa kwa mganga wa kienyeji alikokuwa akijitibu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema hadi jana upelelezi wa tukio hilo lililozua hofu kwa wakazi wa Kijiji cha Sima unaendelea na tayari watuhumiwa 12 wamekamatwa.

“Hakuna jiwe litakalobaki bila kugeuzwa katika upelelezi wa jambo hili, tutawasaka na kuwakamata wote waliohusika kwa njia moja au nyingine na mauaji haya ya kinyama,” alisema Msangi.

Habari zilizopatikana kutoka kwa mtu wa karibu na familia ya marehemu Zakaria Mbata iliyopoteza mama na watoto watatu katika tukio hilo, zinaeleza kuwa wauaji walilenga kupora fedha zilizohifadhiwa kwenye mtandao wa simu.

Pia, chanzo kimoja cha habari kilisema kuwa polisi walimkamata mmoja wa watuhumiwa hao akiwa kwa mganga wa kienyeji alikokuwa akijitibu jeraha alilopata siku ya tukio.

“Katika purukushani za mauaji hayo, huyo mhalifu alijeruhiwa usoni, inaonekana alipigwa na kitu kizito, akakutwa kwa mganga wa kienyeji na amekamatwa kwa mahojiano,” kilisema chanzo hicho
 
Tukio Lenyewe
Usiku wa kuamkia Mei 11, watu wasiojulikana walivamia familia ya Zakaria Mbata na kuua watu saba kwa kuwakata mapanga sehemu mbalimbali za mwili.

Waliouawa katika tukio hilo ni mama wa familia hiyo, Augenia Philipo (62), mdogo wake Maria Philipo (56) na watoto wake; Yohana Mabula (20), Regina Aloyce (12) na Mkiwa Philipo (13).

Wageni wawili wa familia hiyo, waliojulikana kwa jina mojamoja ya Donald na Samson nao pia waliuawa katika tukio hilo.
Share:

UVCCM Wafikishana Polisi

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Sakata la uuzwaji kinyemela wa zaidi ya hekari 200 za shamba la Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Iringa limechukua sura mpya baada ya aliyekuwa katibu wa mkoa huo, Ally Nyawenga kukamatwa na polisi.

Shamba hilo lililopo eneo la Igumbiro, nje kidogo ya mji wa Iringa, linadaiwa kuuzwa mwaka jana kwa zaidi ya Sh800 milioni baada ya baadhi ya viongozi kubadili matumizi yake na kuwa viwanja.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, John Kauga alisema jana kuwa kiongozi huyo alikamatwa Morogoro siku chache zilizopita.

“Tulituma askari wetu na leo hii wanamleta. Taarifa za kumkamata ni hizo za uuzwaji wa shamba hilo kwa hivyo tutafanya naye mahojiano zaidi, lakini kwa sasa sina taarifa zaidi ya hapo labda tuwasiliane kesho (leo),” alisema.

Nyawenga alisimamishwa kazi mwishoni mwa mwaka  jana, akituhumiwa kusimamia uuzwaji wa shamba hilo kinyume cha utaratibu wa jumuiya hiyo. 

Mali zote za jumuiya hiyo zipo chini ya Baraza la Wadhamini, linaloongozwa na Mwenyekiti, Dk Emmanuel Nchimbi.

UVCCM ilianza kumiliki shamba hilo miaka ya 1970 likitumika kwa ajili ya kilimo kwa kukodisha vijana kwa bei nafuu ili kuwasaidia kujiendeleza kiuchumi.

Ally Simba aliyedaiwa kuwa msimamizi wa shamba hilo alikana nafasi hiyo huku akisema hakuhusishwa katika mipango hiyo.

“Sikuwa msimamizi, bali mjumbe tu wa kamati ya utekelezaji, msimamizi alikuwa Katibu wa UVCCM,” alisema Simba ambaye kwa sasa ni Katibu wa UVCCM Wilaya ya Mbinga.

Alisema kabla ya kuondoka Iringa mwaka 2014, hakuwahi kusikia vikao wala mipango ya uuzaji wa shamba hilo na kwamba hahusiki.

Akizungumzia kukamatwa kwa Nyawenga, Katibu wa UVCCM Mkoa wa Iringa, Abdulkarim Halamga alisema: “Kwa sababu ni mali ya vijana na katibu aliyekuwapo anahusika, hivyo kwa kushirikiana na polisi, tumemkamata baada ya waliouziwa viwanja kuanza kutudai huku vijana wakipinga kuuzwa kwa eneo lao. Kwa sababu hakuwa peke yake, taratibu nyingine zitafuatwa akishafikishwa Iringa.”

Mjumbe wa kamati ya utekelezaji ya UVCCM mkoani hapo, Thom Muyinga alisema kuuzwa kwa shamba hilo kumesababisha mpasuko ndani ya umoja huo. “Vijana wanataka mali yao, haiwezekani mali hiyo iuzwe kinyemela na kunufaisha kundi la watu wachache,” alisema.

Mmoja wa vijana hao, Katula Kalinga alisema japo tayari tume ya UVCCM ya kuchunguza mgogoro huo ilishakwenda Iringa, hakuna kinachoendelea.

Alimuomba Rais John Magufuli kufuta hati za viwanja hivyo ili shamba hilo, lirejeshwe kwa UVCCM.

Pia, walimuomba Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete kutumbua majipu yanayokitafuna chama kwenye mkoa huo, ili vijana waendelee kunufaika na mali yao.

Walitaka kamati ya utekelezaji jumuiya hiyo Mkoa wa Iringa isimamishwe wakati uchunguzi ukiendelea.
Share:

Tanesco Mkoa Wa Pwani Yamakamata Mmiliki Wa Yadi Ya Magari Kwa Wizi Wa Umeme

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Mkoa wa Pwani limemkamata mmoja wa wamiliki wa eneo la maegesho ya magari la White Star, Munira Mbowe akidaiwa kujiunganishia umeme kinyume cha sheria.

Mbowe ambaye ni mmiliki wa eneo hilo lililopo Kiluvya kwa Komba nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, alikamatwa jana baada ya kufanyika msako wa kushtukiza kwa watu wanaodaiwa kujiunganishia umeme kinyume cha sheria.

Inadaiwa kuwa Mbowe amelisababishia shirika hilo hasara ya Sh50 milioni.

Akizungumza kwenye eneo hilo, Ofisa Usalama wa Tanesco Mkoa wa Pwani, Henry Byarugaba alidai kuwa baada ya kufanya ukaguzi waligundua umeme uliokuwa ukitumika katika eneo hilo haukuunganishwa na Tanesco.

“Tumekuwa tukibuni mbinu mpya kila kukicha ya kuwatia mbaroni wateja wetu wanaotuhujumu na leo (jana), tumembana huyu anayedaiwa ni mmiliki wa yard hii ya White Star baada ya kukuta anatumia umeme wa wizi uliounganishwa katika njia tatu,” alidai Byarugaba.

Alisema tayari wameshamfikisha Kituo cha Polisi Kibaha na hatua zingine za kisheria zinaendelea kuchukuliwa.

Hata hivyo, alidai kuwa hiyo siyo mara ya kwanza kwa Mbowe kukamatwa kwa kosa hilo. Alidai mwaka jana Tanesco ilipofanya msako, ilimkamata akiwa amejiunganishia umeme na alichukuliwa hatua za kisheria.

Alipoulizwa  kama tuhuma hizo zina ukweli, Mbowe alijitetea kuwa hajui ni nani aliyemuunganishia njia hizo tatu za umeme kwa sababu mara nyingi hufanya shughuli zake jijini Dar es Salaam, mara chache hufika kwenye yard hiyo kufanya kazi zingine ambazo ni chache.

“Ni kweli tumekutwa na kosa la kuiba umeme, lakini jamani nataka niwaeleze kuwa mimi sihusiki na kingine, nawaomba msinitoe kwenye vyombo vya habari, haya ni maisha tu, sio vizuri kunitoa jamani mimi sihusiki kabisa katika wizi huu,” alijitetea Mbowe.

Kaimu Meneja wa Taneso Mkoa wa Pwani, Selemani Mgwila alisema kitendo alichokifanya mteja wao huyo ni kosa kwani umeme waliokuwa wanautumia umesababisha upotevu wa mapato makubwa ya shirika.

“Tunalalamika kila siku mpaka shirika linaonekana halifanyi kazi kwa sababu ya hawa watu wachache, safari hii lazima sheria ichukue mkondo wake,” alisema.
Share:

Kiwanda Cha Bia Serengeti Breweries Limited (SBL) Chapigwa Faini

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira na Muungano), Luhaga Mpina amekiamuru Kiwanda cha Serengeti Breweries Limited (SBL), kulipa faini ya Sh16 milioni kwa kosa la kutiririsha maji yasiyo salama kwenye makazi ya watu.

Uamuzi huo ulichukuliwa mwishoni mwa wiki iliyopita mbele ya baadhi ya viongozi wa SBL kilichopo Chang’ombe Manispaa ya Temeke na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (Nemc), baada ya kujiridhisha kuwa kilikiuka taratibu za utunzaji mazingira na kutotekeleza amri halali kwa zaidi ya miaka miwili.

Mpina aliigiza kiwanda hicho, kulipa faini ndani ya siku saba na kwamba asieleweke vibaya kuhusu uamuzi huo, bali anasimamia sheria.

“Nasimamia sheria wala sina nia mbaya na kiwanda chenu, naomba nieleweke hivyo na faini hii mlipe kwa wakati,” alisema Mpina.

Mkurugenzi Mkuu wa Nemc, Bonaventure Baya alisema baraza hilo limejijengea utaratibu wa mara kwa mara kufuatilia kanuni za afya za kiwanda hicho hasa majitaka yanayotiririka kuelekea kwenye makazi ya watu.

Meneja Mhandisi Biashara wa SBL, Peter Mkongwa alikanusha tuhuma hizo na kwamba, maji hutibiwa kwa dawa kabla ya kutiririshwa katika makazi ya watu. Alisema: “Tunasubiri mashine maalumu ya kuvuta maji hayo ili yaingie katika bomba.”
Share:

Auawa Kwa Kuchomwa Visu Akituhumiwa Kutoka Kimapenzi na Mtalaka Wake

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Mkazi wa Kijiji cha Chala B, Tarafa ya Chala wilayani Nkasi, Mkoa wa Rukwa, Moses Nambasita (48) ameuawa kwa kuchomwa visu kutokana na kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Akisimulia mkasa huo mwishoni mwa wiki iliyopita, Mwenyekiti wa Kitongoji hicho, Vincent Mwanambuu alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 10 jioni baada ya kuvamiwa na kijana mmoja alipokuwa akitoka nyumbani kwake kwenda nyumba jirani, alishambuliwa kwa kuchomwa visu.

Mwanambuu alisema baada ya kupata taarifa hizo alitoa taarifa Kituo kidogo cha Polisi Chala, askari walifika na kuchukua mwili kwa ajili ya uchunguzi na kuanza msako dhidi ya mtuhumiwa.

Akielezea chanzo cha mauaji hayo, Mwanambuu alisema mtuhumiwa alipata taarifa kuwa Nambasita ana uhusiano na mtalaka wake, ambaye walikuwa wameachana kipindi kirefu.

Alidai kuwa kutokana na taarifa hizo, mtuhumiwa alipeleka shauri la ugoni katika Mahakama ya Mwanzo Chala.

“Lakini kabla hata shauri hilo halijamalizika, tunashangaa kuona mtuhumiwa ameamua kujichukulia sheria mikononi, baada ya kutekeleza unyama huo alikimbia na kutokomea kusikojulikana,” alisema.

Mtendaji wa Kijiji cha Chala, Godfrey Mwanakatwe alisema kutokana na mazingira hayo polisi wanawashikilia watu wanne kwa kosa la kushiriki mauaji hayo.

Hatua hiyo inatokana na baada ya wao kutoa taarifa kwa muuaji kuwa Nambasita ana uhusiano wa kimapenzi na mtalaka wake, ambaye mpaka sasa haijulikani alipo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba, baada ya uchunguzi wa polisi ndugu wa marehemu waliruhusiwa kuuzika mwili huo.

Mwaruanda alisema chanzo cha kifo hicho ni wivu wa mapenzi na kuongeza kuwa mtuhumiwa alianza vizuri kwa kufuata sheria, lakini haijulikani kilichosababisha kuchukua uamuzi huo wa kinyama.

Alisema wanawashikilia watu watatu wakituhumiwa kushiriki mauaji hayo, kwa kutoa taarifa kwa mtuhumiwa kwamba Nambasita alikuwa na uhusiano na mtalaka wake.

Kamanda Mwaruanda aliwataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mikononi, hivyo wafuate taratibu kupata haki zao.
Share:

Mbarawa ‘Kuvaa Viatu’ vya Magufuli Kesho Bungeni

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Waziri  wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa wiki hii anatarajiwa kuanza kuvaa viatu vya Rais John Magufuli bungeni.

Kesho Profesa Mbarawa anatarajiwa kuwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

Mbunge huyo wa kuteuliwa atakuwa na jukumu kubwa la kuwasilisha bajeti hiyo ambayo kwa takriban miaka 10 ilikuwa jukumu la Dk Magufuli.

Magufuli alikuwa Waziri wa Ujenzi kwa miaka mingi kabla ya kujitosa kuwania urais kupitia CCM ambako aliteuliwa na kushinda Uchaguzi Mkuu, Oktoba mwaka jana.

Sekta tatu alizopewa Profesa Mbarawa ni nyeti na ngumu, hivyo Watanzania wanasubiri kuona atakavyoanza bajeti yake ya kwanza kesho tangu kuteuliwa na Dk Magufuli kushika nafasi hiyo.

Ujenzi bado ni sekta inayotegemewa na Taifa katika kuingiza mapato na pia kusaidia huduma za jamii. Masuala ya ujenzi wa barabara, madaraja, mawasiliano na uchukuzi vyote ni muhimu kwa uchumi. Hayo yanatiwa nguvu na jitihada za Rais Magufuli za kukusanya mapato tangu aingie madarakani.

Suala la bandari ni eneo mojawapo litakalogusa bajeti ya Profesa Mbarawa. Kuliibuka masuala mengi ya ufisadi katika bandari ya Dar es Salaam, mambo yanayotegemewa kuligusa Bunge.

Mbali ya hayo, masuala ya mawasiliano yatakuwa pia na nafasi katika bajeti ya Profesa Mbarawa.
Share:

Atiwa Mbaroni Kwa Kudandia Helkopta

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Polisi wa Kenya wanamshikilia mtu mmoja mjini Bungoma baada ya kuning’inia kwenye helikopta iliyoubeba mwili wa aliyekuwa mfanyabiashara Jacob Juma.

Mtu huyo, Saleh Wanjala ambaye hakutoa sababu za kufanya hivyo, alishikiliwa na polisi huku akipata matibabu kwenye Hospitali ya Rufaa Bungoma.

Wanjala alionekana akining’inia kwenye helikopta iliyobeba mwili wa mfanyabiashara huyo wakati ikipaa kutoka kwenye Uwanja wa Posta mjini Bungoma baada ya wananchi kutoa heshima za mwisho.

Wanjala aliamua kuidandia helikopta hiyo wakati ikiondoka kupeleka mwili wa Juma nyumbani kwake katika Kijiji cha Mungore.

Akisimulia mkasa huo, Wanjala alisema alikuwa karibu na helikopta hiyo wakati ikianza kupaa na kwamba aliumia baada ya mguu wake kukwama.

“Nilikuwa nimeketi chini ya helikopta na wakati ilipokuwa inaanza kupaa, mguu wangu ulikwama hapo ikabidi nijishikilie vizuri ili nisianguke,” alisema Wanjala.

Rubani wa helikopta hiyo alilazimika kumpeleka hadi uwanja wa ndege wa Bungoma mita 700 kutoka kwenye uwanja huo lakini Wanjala aliamua kuruka na kuumia vibaya miguu na mikono. Muuguzi wa Hospitali ya Bungoma, Leah Atsewa alisema bado wanamfanyia uchunguzi. 
Share:

MAGAZETI YA LEO JUMATATU MAY TAREHE 16.5.2016

Share:

Sunday, 15 May 2016

Bunge larejesha Safari za nje za Ulaya na Marekani

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema Bunge limetenga fedha kwa ajili ya ziara za wabunge nje ya nchi.

Ziara hizo ni pamoja na zile za kwenda kujifunza namna mabunge mengine yanavyofanya kazi.

image.jpeg

Chanzo: Nipashe

Hawa ndio wanasiasa wetu na utashangaa hata wabunge wazoefu nao watashiriki ziara hizi licha ya ukweli kwamba kama ni kujifunza walishakwenda kujifunza tangu enzi za Sitta na Mama Makinda.

Huku ndio kubana matumizi kwa waheshimiwa kwenda kujifunza Ulaya na Marekani.

Watumishi wa umma kazi kwenu.
Share:

Matokeo ya Kidato cha Nne ya Mbuge wa CCM aliyekataa Bunge Live

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Kwa Matokeo haya kama Agnes Marwa (Ccm) ndio huyo Mbunge Aliyelia ili Bunge lisionyeshwe Live anahaki kabisa ya kulia na kusema vile... Kumbe shule ndio tatizo

IMG-20160515-WA0011.jpg


Elimu yake:

image.png

 
Share:

Happy Birthday Dayna Nyange

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Jumapili ya Leo Mei 15 ya 2016, Mtandao Huu, Unaungana na mkali wa muziki wa bongo fleva toka mkoani Morogoro mwana dada Dayna Nyange katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa. Dayna Nyange anayetamba na wimbo wake wa sasa wa Angejua leo hii ametimiza umri wa miaka kadhaa tangu kuzaliwa kwake.



Mtandao Huu unakutakia maisha marefu yenye kheri na baraka tele mrembo wetu wa nguvu.
Share:

Ronaldo Amaliza Msimu na Rekodi ya Dunia

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Licha ya Real Madrid kushindwa kutwaa kombe la Ligi Kuu y Hispania (La Liga) lakini hilo halijamzuia staa wa klabu hiyo, Cristiano Ronaldo kumaliza msimu na rekodi ambayo haijawahi kuwekwa awali.

Katika mchezo wa mwisho wa La Liga ambao Real Madrid iliibuka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Deportivo la Coruna na Ronaldo kufunga magoli mawili ambayo yamemwezesha kuweka rekodi ya dunia.

Magoli hayyo yalikuwa ya 35 kwa La Liga msimu huu na katika michuano ya Ulaya amefunga magoli 16 hivyo kuweza kufikisha magoli 51.

Rekodi hiyo ni kufunga magoli zaidi ya 50 kwa misimu sita mfulizo, rekodi ambayo hapo awali hhaijawahi kuwekwa na mchezaji yoyote katika historia ya soka.

Kwa kipindi chote ambacho Ronaldo amechezea Real Madrid ameifungia klabu hiyo magoli 364 katika michezo 347. 
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger