Friday, 13 May 2016
Thursday, 12 May 2016
MSANII KINYAMBE AFARIKI DUNIA
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
May 12 2016 ripoti zilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kwa
baadhi ya mastaa wa filamu na Muziki nchini, kuhusiana nataarifa ya
kufariki kwa mmoja kati ya wachekeshaji maarufu nchini Tanzania,
Mohammed Abdallah (Kinyambe) kutoka kwenye maigizo ya Vituko Show.
WATU 7 WAUAWA SENGEREMA KWA KUKATWA MAPANGA
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Watu
saba wa familia moja katika kitongoji cha Nyigumba kijiji cha Sima
wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza, wameuawa kwa kukatwa katwa mapanga
usiku wa kuamkia leo.
Tukio hilo lililoacha simanzi katika kitongoji hicho, limehusisha
ndugu watano wa tumbo moja wakiwamo wanafunzi watatu, waliovamiwa usiku
wa manane na watu wasiojulikana na kuanza kucharangwa mapanga.
Baadhi ya wakazi wa kitongoji hicho wamesikitishwa na tukio hilo
ambalo limetokea majira ya saa tisa usiku wa kuamkia Mei 11, huku
wakiiomba serikali kuchukua hatua kali dhidi ya watu watakaobainika
kuhusika na mauaji hayo.
Inadaiwa kuwa watu wawili waliokuwa na mapanga walikwenda katika
nyumba ya wanafamilia hao na kuanza kuwashambulia huku wakianza na
marehemu Donald ambaye alipambana na wauaji hao lakini alizidiwa nguvu
kabla ya kuangushwa chini na kukatwa katwa mapanga, huku mama wa familia
hiyo ambaye naye ameuawa katika tukio hilo akijaribu kufungua mlango wa
chumba walicholala wajukuu na watoto wake, hali iliyowapa mwanya wauaji
hao kuingia ndani ya nyumba hiyo na kuanza kuwashambulia kwa mapanga.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella ambaye pia ni mwenyekiti wa
kamati ya ulinzi na usalama amefika katika eneo la tukio na kusema
kitendo kilichofanywa na wauaji hao hakiwezi kuvumiliwa.
Kwa mujibu wa diwani wa kata ya Sima Makoye Lugata watu waliouwa ni
pamoja na mama mwenye nyumba Augenia Kiwitega, Maria Philipo na Leonard
Thomas ambaye anasoma kidato cha nne katika shule ya sekondari Sima,
wengine ni Leornad Aloys mwanafunzi wa darasa la saba, Mkiwa Philipo wa
darasa la tano katika shule ya msingi Ijinga.
Marehemu wengine wamefahamika kwa jina moja la Samson na Donald
kutoka wilayani Ngara mkoani Kagera ambao walikuwa wanafanya kazi ya
kilimo kwenye familia hiyo.
Katika tukio hilo watoto wawili (majina yamehifadhiwa) wa familia
hiyo wamenusurika kuuawa baada ya kujificha chini ya uvungu wa kitanda.
Wednesday, 11 May 2016
MPYA:SUA YAPOKEA CHETI CHA UBORA WA ELIMU TANZANIA,YASHIKA NAFASI YA 2,DUNIANI NI YA 1837
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
The Sokoine University of Agriculture (SUA) recently received a Certificate of Academic Performance from the University Ranking by Academic Performance (URAP) for 2015-2016 ...
Read More >>
Certificate
SUA receives certificate of Academic Performance
Read More >>
Certificate
ZANZBAR:MAOMBI YA MIKOPO MWAKA WA MASOMO 2016/2017
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU ZANZIBAR INAWATANGAZIA VIJANA WANAOHITAJI KUENDELEA NA MASOMO YA ELIMU YA JUU KWA MWAKA 2016/2017, KWAMBA FOMU ZA MAOMBI YA MIKOPO ZITAANZA KUTOLEWA KUANZIA TAREHE 02/05/2016 KATIKA OFISI ZAKE ZA UNGUJA NA PEMBA.KWA MAELEZO ZAIDI FUNGUA.
SIFA ZA WAOMBAJI.
VIPAU MBELE VYA WATAALAMU.
BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU ZANZIBAR INAWATANGAZIA VIJANA WANAOHITAJI KUENDELEA NA MASOMO YA ELIMU YA JUU KWA MWAKA 2016/2017, KWAMBA FOMU ZA MAOMBI YA MIKOPO ZITAANZA KUTOLEWA KUANZIA TAREHE 02/05/2016 KATIKA OFISI ZAKE ZA UNGUJA NA PEMBA.KWA MAELEZO ZAIDI FUNGUA.
SIFA ZA WAOMBAJI.
VIPAU MBELE VYA WATAALAMU.
Breaking news:WANAFUNZI WA CHUO KIKUU SUA WAUA MWIZI MAENEO YA NEW HOSTEL BAADA YA KUIBA NGUO
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Wanafunzi wa chuo kikuu cha sua wanaoishi maeneo ya New hostel wamaefanikiwa kumuua jamaa mmoja alieiba nguo hostel hapo.Tukio hili ,limetokea usiku wa kuamkia leo asubuhi ambapo walimhisi jamaa huyo sio mwanafunzi ,na kuamua kumuamshia kipigo.
Maswayetu blog ikiongea na Mwanafunzi mmoja wa wanafunzi anaishi hapo hostelini amesema kwamba Wameamua kufanya hivyo kutokana na kukithiri kwa vitendo vya wizi hostelini hapo ikiwepo wizi wa simu,baiskeli,laptop na nguo.
MASWAYETU BLOG
Tanzania inatarajia kuanza kuzalisha umeme wa jotoardhi zaidi ya megawati 20 ifikapo mwaka 2018
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Tanzania inatarajia kuanza kuzalisha umeme wa jotoardhi zaidi ya
megawati 20 ifikapo mwaka 2018 mradi utakaopunguza gharama za nishati
hiyo nchini.
Kiwango cha nishati hiyo kitakachozalishwa kutoka
miradi minne inayoendelea kufanyiwa kazi kwa sasa, kinatarajiwa
kuongezeka mpaka megawati 200 ifikapo mwaka 2025.
Mkurugenzi wa
Kampuni ya Jotoardhi nchini (TGDC), Mhandisi Boniface Njombe aliwaeleza
wajumbe wa mkutano wa wataalamu wa jotoardhi jana kuwa, mbali na mpango
huo wa muda mfupi, wamejiwekea malengo ya kuzalisha zaidi ya megawati
200 ndani ya miaka tisa ijayo.
“Hii ni nishati salama na rafiki
wa mazingira,” alieleza bosi huyo wa TGDC ambayo ni kampuni tanzu ya
Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco).
Mpaka sasa miradi
inayoendelea kufanyiwa kazi ikiwa kwenye hatua mbalimbali ni Ngozi na
Mbaka iliyopo mkoani Mbeya, Kisaki wa Morogoro, Mlima Meru na Ziwa
Natron kwenye Mlima Lengai.
Alisema, TGDC inashirikiana na
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Mazingira (UNEP) kufanya
mapitio ya jotoardhi, kuendeleza na kuchakata nishati hiyo kabla
haijaanza kutumika.
Akifungua mkutano huo, Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Nishati na Madini, Dk Juliana Pallangyo alisema Tanzania ina
hazina ya takriban megawati 5,000 ya nguvu za kuzalisha nishati hiyo na
kwamba ipo karibuni kuanza kuitumia.
Alisema mpango wa Serikali
ni kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda na utafikiwa endapo kutakuwa
na nishati ya kutosha kwa matumizi ya nyumbani na viwandani.
Polisi Kizimbani kwa Kupokea Mshahara wa Jeshi Hilo Kwa Miezi 7 Bila Kufanya Kazi
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Aliyekuwa
askari wa Jeshi la Polisi wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, Kuyani
Mkunjera (36), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mjini Moshi,
kwa kupokea mshahara wa jeshi hilo huku akiwa ameacha kazi kwa kipindi
cha miezi saba.
Hakimu
mkazi wa mahakama hiyo, Antony Ngowi alisema mshtakiwa alijinufaisha
pasipo kufanyia kazi kitu anachonufaika nacho na alipokea fedha kiasi
kinachozidi Sh4.6 milioni ambayo ni kinyume cha kifungu cha 23 (1) (a)
cha Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Sheria namba 11 ya mwaka 2007.
Ngowi
alisema mshtakiwa kuanzia Oktoba 12, 2015 hadi Aprili 28, mwaka huu
alijipatia kiasi hicho cha fedha kwa kujinufaisha pasipo kukifanyia kazi
kitu anachonufaika nacho, huku akiwa siyo mfanyakazi wa jeshi hilo na
akiwa ameajiriwa na taasisi nyingine.
Mshtakiwa
alikana shitaka hilo na yupo nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti
yaliyomtaka awe na kiasi cha Sh3 milioni za ahadi na wadhamini wawili
wenye barua za kuwatambulisha, vitambulisho na picha za paspoti.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 23, kwa ajili ya kuanza kusikilizwa.
Madaktari Wataka Bohari Kuu ya Dawa nchini (MSD) Itumbuliwe
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Waganga
wafawidhi wa Manispaa ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam, wamesema
Bohari Kuu ya Dawa nchini (MSD) ni “jipu” linalohitaji kutumbuliwa
kutokana na kuwa na mfumo usioridhisha wa utoaji huduma za dawa.
Wakizungumza
na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi, madaktari hao walisema MSD
inahitaji kufanyiwa marekebisho makubwa ya utendaji kazi wake, kama siyo
kutumbuliwa kutokana na kuwafanya wafanye kazi katika mazingira magumu
na yasiyo na dawa.
Mganga Mkuu wa wilaya hiyo, Azizi Msuya
alisema changamoto iliyopo ni upatikanaji wa dawa na mara nyingi
wanachoomba MSD sicho wanachopata na kinawaletea uhasama na chuki kwa
wagonjwa.
“Wao wananunua palepale na sisi tungeruhusiwa
tungenunua. Maduka kama Salama, kopo moja la dawa aina ya paracetamol ni
Sh7,000, lakini tukinunua kwao inakuwa Sh15,000 la sivyo turuhusiwe
kununua wenyewe kuliko kusubiri dawa mwezi mzima,” alisema Msuya.
Alisema
unaweza kuomba dawa aina nyingi zikiwamo za kuponya maisha haraka kama
za kuzuia damu kutoka, kuzuia kifua kubana, ukapata nyingine hizo
ukakosa. Hivyo kuna hatari ya kufiwa na mgonjwa mkononi.
Dk
Emmanuel Kombe, Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Makongo alisema
Serikali inapeleka fedha na vituo vina fedha yake, lakini cha kushangaza
utata wa kupatikana mahitaji yaliyoagizwa kila siku upo palepale.
“Wauguzi
wanatukanwa, wanakuwa maadui wa wananchi kwa sababu hospitali hazina
dawa, hakuna mwananchi anayefahamu kama MSD ndiyo hawajaleta,” alisema
Kombe.
Dk Sebastian Mapunda Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya
Kigogo alisema hiyo ni changamoto ya muda mrefu na wao kama watendaji
wanaoshughulika na wagonjwa inawapa shida.
Alisema wananchi
wanapoona dawa katika maduka binafsi halafu hospitali hakuna, wanaona
kama kuna mchezo unafanywa, kumbe MSD wapo kati kukwamisha.
Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi alisema atamwandikia barua Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amuombe Rais atumbue jipu la MSD.
Tangu aapishwe kuwa Mkuu wa Wilaya, hiyo ndiyo taasisi ya kwanza kukutana nayo na kusikiliza kero zao.
Alisema
ameanza na afya kwa sababu ndiyo sekta yenye changamoto nyingi ikiwamo
hiyo ya dawa. Hivyo atalishughulikia suala hilo kwa kila njia ikiwamo
kumshirikisha Mkuu wa Mkoa.
“Haiwezekani fedha ipo dawa hakuna
na hakuna jibu la msingi, na haiwezekani dawa kusubiri taratibu mwezi
mzima, wiki tatu kama hakuna ielezwe hakuna ili ufanyike utaratibu wa
kununua zinakopatikana kwa sababu afya za binadamu hazitambui Sheria za
Ununuzi,” alisema Hapi.
Ofisa Habari wa (MSD), Eti
Kusiluka alipingana na madai hayo akieleza kuwa hakuna utaratibu wa
kupokea fedha wanapoagiza dawa zaidi ya kupokea mahitaji ya wateja wao
na kuyafanyia kazi.
“Serikali ina mipango ya ununuzi na muombaji
hupata mahitaji aliyoomba ndani ya siku 14 na 45 na siyo kweli kuwa
fedha zao zinang’ang’aniwa,” alisema Kusiluka.