Sunday, 10 April 2016

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI APRIL TAREHE 10.4.2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI APRIL 10 2016
Share:

Saturday, 9 April 2016

MATOKEO MECHI YA YANGA VS ALHALY LEO TAREHE 9.4.2016 NI 1-1

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

YANGA imelazimishwa sare ya bao 1-1 katika mechi ya ligi ya Mabingwa wa Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri, mechi hiyo imechezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kwa matokeo hayo Yanga inahitaji nguvu za ziada ili kuweza kutinga hatua ya makundi kwenye michuano hiyo katika mechi ya marudiano itakayochezwa April 9 huko Misri.

Al Ahly ndo walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa mchezaji wao Amri Gamal baada ya mabeki wa Yanga kufanya madhambi na mwamuzi Dennis Dembele kutoka Ivory Coast kuamuru ipigwe faulo kuelekea lango la Yanga ikiwa ni dakika ya 11.

Dakika ya 19, Yanga walisawazisha bao hilo baada ya  Issoufou Boubacar kupewa pasi nzuri na Haji Mwinyi ambapo Issoufou alipiga mpira uliomkuta beki wa Al Ahly, Ahmed Hegazy ambaye alijifunga.

Dakika ya 34, Dembele alimpa kadi ya njano kipa wa Al Ahly kwa kuchelewesha mpira wakati Donald Ngoma akipiga shuti kali dakika 37 na kipa kudaka ikiwa ni pasi nzuri ya Juma Abdul.

Yanga ilifanya shambulizi kali kupitia kwa Salum Telela baada ya kupokea pasi ya Deus Kaseke hata hivyo shuti lake lilitoka nje huku Al Ahly wakikosa bao dakika ya 46 kupitia kwa Gamal ambaye mpira wake uligonga mwamba.

Mwamuzi Dembele aliendelea kutoa kadi za njano ambapo dakika ya 54 Telela alipewa kadi hiyo kwa kumchezea rafu Hassam Ghaly huku Thaban Kamusoko akikosa bao dakika ya 56 ikiwa ni pasi ya Kaseke.

Dakika ya 60, Kamusoko alimpa pasi nzuri Amissi Tambwe lakini alishindwa kufunga kwani tayari kipa wa Al Ahly aliuwahi na kuudaka huku kocha wa Yanga Hans Pluijm akifanya mabadiliko dakika ya 61 kwa kumtoa Issoufou nafasi yake ikichukuliwa na Geofrey Mwashiuya.

Ngoma alizidiwa ujanja dakika ya 66 na mabeki wa Al Ahly baada ya kumpora mpira akiwa anaelekea kuipatia Yanga bao la pili lakini mpira huo ukapigwa nje ya uwanja.

Pluijm alifanya mabadiliko mengine dakika ya 74 ambapo alimtoa Tambwe nafasi yake ilichukuliwa na Simon Msuva wakati Al Ahly nao waliwatoa Ramadhan Sobhi, Ghaly pamoja na Moaem Zakaria na kuwaingiza Walid Souliman, Housan Ashour na Malick Evouma.

Kipa wa Yanga, Ally Mustafa 'Berthez' alishindwa kuendelea na mchezo baada ya kuumia hivyo Deogratius Munishi 'Dida' alichukuwa nafasi yake ikiwa ni dakika ya 81 huku Ngoma akishindwa kufunga dakika ya 82 kwani shuti lake lilitoka nje ikiwa ni pasi ha Abdul.
Share:

RAIS WA ZANZIBAR ATANGAZA BARAZA LA MAWAZIRI LA MAPINDUZI YA ZANZBAR ,13 NA MANAIBU WAZIRI 7

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
1-ISSA HAJI USI GAVU-OFISI YA RAIS NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI.
2-HAROUNA ALI SULEIMAN-OFISI YA RAISI KATIBA,SHERIA,UTUMISHI WA UMMA.
3-HAJI OMAR KHERI-OFISI YA RAISI TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ.
4-MOHAMED ABOUD-OFISI YA MAKAMO WA PILI YA RAISI.
5-DR.KHALID SALUM MOHAMED-WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO.
6-MAHMOUD THABIT KOMBO-WAZIRI WA AFYA.
7-RIZIKI PEMBE-WAZIRI WA ELIMU.
8-AMINA SALUM ALLY-WAZIRI WA VIWANDA NA MASOKO
9-ALI KARUME-WAZIRI WA UJENZI,MAWASILIANO NA UCHUKUZI.
10-HAMAD RASHID-WAZIRI WA KILIMO MALIASILI MIFUNGO NA UVUVI.
11-RASHID ALI JUMA-WAZIRI WA HABARI, UTALII,UTAMADUNI NA MICHEZO
12-NURDIN KASTIKO-WAZIRI WA UWEZESHAJI,WAZEE,WANAWAKE NA WATOTO
13-SALMA ABOUD TALIB-MAJI, ARDHI,NISHATI NA MAZINGIRA.
MANAIBU WAZIRI:-
1-HAROUS SAID SULEIMAN-AFYA
2-JUMA KHAMIS MAALIM-KATIBA
3-CHUM KOMBO-HABARI
4-LULU MSHAM KHAMIS-KILIMO
5-JUMA MAKUNGU JUMA-ARDHI
6-MOHAMED AHMED SALUM-UJENZI
7-MMANGA MJENGO MJAWIRI-ELIMU
Share:

MECHI ZA LEO LIGI KUU UINGEREZA -EPL LEO TAREHE 9.4.2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY


Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) inataraji kuendelea leo Jumamosi, Aprili, 9 kwa michezo saba ikiwa ni michezo ya 33 kwa baadhi ya vilabu na vingine vikiwa bado vimecheza michezo michache.

Michezo ya leo ni;

West Ham United – Arsenal 14:45 EAT

Aston Villa – Bournemouth 17:00 EAT

Crystal Palace – Norwich City 17:00 EAT

Southampton – Newcastle United 17:00 EAT

Swansea City – Chelsea 17:00 EAT

Watford – Everton 17:00 EAT

Manchester City – West Bromwich Albion 17:00 EAT 
Share:

HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA SEKOMU APRIL 2016

Share:

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI APRIL TAREHE 9.4.2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
20160409_045716
20160409_045728
20160409_045902
20160409_045911 
magazeti ya leo jumamosi tarehe 9/4/2016
20160409_045924
20160409_045932
20160409_045944
20160409_045953
20160409_050011
20160409_050019
20160409_050030
20160409_050038
20160409_050047
20160409_050108
20160409_050117
20160409_050126
20160409_050136
20160409_050144
20160409_050157
20160409_050208
20160409_050218
20160409_050229
20160409_050235
20160409_050245
20160409_050252
20160409_050334
20160409_050342
20160409_050349

Magazeti ya Tanzania leo Jumamosi April 9, 2016

20160409_050424
20160409_050509
Share:

Friday, 8 April 2016

HUU HAPA UCHAFU WA TCU DHIDI YA ST.JOSEPH UNIVERSITY

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Image result for SJUIT
Habari zenu wakuu!? Ukipitia katika website ya tcu utaona habari mpya inayoonesha qualified and non qualified students wanaosoma diploma ya education st Joseph.
Kwanza mwanzoni ile ilikuwa ni program ya miaka mitano ( 5 years degree program) ila baada ya kufutwa kwa Chuo cha mtakatifu yosefu tawi la Arusha tcu ikafuta pia udahili wa wanafunzi wapya katika kozi ile na kuamrisha wanafunzi wanaoendelea watalazimika kumaliza level ya diploma kwanza.

Vigezo vya kuingia kataika kozi ile mwanzo ilikuwa ni div 4 ya pointi 26 ambayo wizara na Chuo walikubaliana pamoja na tcu!

Baadae chuo walitoa tangazo kwenye website yao kwamba kozi hii ili uweze kujiunga unatakiwa uwe na d nne tuu na mbili nikutoka katika masomo ya sayansi!

Sikujua walikubaliana tena kuweka vigezo hivyo ama ni Chuo wenyewe waliamaua! Chuo kikaanza kudahili wanafunzi kwa vigezo hivyo tangu mwaka 2013!

Baadae mwaka elfu mbili na kumi na tano TCU wakapeleka barua chuoni ya kwamba Chuo ina dahili wanafunzi wasio na sifa walikuwa wakichukua hata wanafunzi waliosoma arts na wengine hata kuwa na d moja tuu lakini walikuwa wanachukuliwa kusoma kozi hii ya masomo ya sayansi.

Majina yakatumwa na tcu ya wanafunzi ambao walikuwa hawana vigezo vya kisoma kozi hii, wanafunzi wakataka wabandikiwe hayo majina ili wajue, ila chuo wakataaa wakasema hizo habari hazina ukweli!

Wanafunzi hawakuishia hapo walifuatilia hili swala na kuagundua ni kweli ila chuo kilikuwa kinafanya uhuni tuu na kuwatishia wanafunzi atakae fuatilia anafukuzwa Chuo, na kweli wanafunzi wengi walifukuzwa Chuo kutokana na hili swala,.

Wanafunzi hawakukomea hapo wakaendelea kufuatilia na kuanzisha migomo kipindi hicho waziri wa elimu alikuwa shukuru kawambwa!

Shukuru kawambwa alifika chuoni na kukagua na alikuja asubuhi na kuondoka jioni kabisa! Baada ya pale shukuru kawambwa aksema wanafunzi wote wanasifa na hakuna ambae hana vigezo wote wanavigezo na wataendelea kusoma na hii kozi inatambuliwa na mikopo watapta.

Baadae Tcu nao walikuja kuthibitisha hilo na kusema wanafunzi wote wanasifa na waendelee kusoma!

Kilichokuja kutokea nikwamba baada ya kufutwa kwa hivi vyuo tarehe 14 mwezi 3 wanafunzi hawa wakaamuriwa na tcu wahamie main Campus ambayo ndio ile ya luguruni!

Wanafunzi waliripoti wakaambiwa watapewa maelekezo ya jinsi utaratibu mpya utakavyokuwa,

Baada kama ya wiki kupita wakawa wanalazimishwa kuingia madarasana kusoma! Wanafunzi hao wakawa wanahoji tutaingia vipi darasani wakati TCU hawajatupa utaratibu?
Na kule walikuwa wanasoma miaka mitano degree program huku wameambiwa watalazimika kusoma diploma kwanza he utaratibu upoje?

Vijana hawa kila walivyoendelea kuhoji walikuwa hawapati jibu sahihi wakaamua kwenda kwa waziri wa elimu mama ndalichako, waziri alichukua jukumu la Kuwaita wote wanaohusika pale TCU! wakaambiwa walitolee ufafanuzi wa wazi katika vyombo vya habari mgaya akalipotezea!

Kumbe walikuwa wanashindwa kulitolea maamuzi kwa kuwa kulikuwa na wanafunzi ambao walisema hawana vigozo vya kusoma kozi hiyo!

Na hilo swala wanafunzi walilifatilia mda sana na mgaya ni shahidi wa hilo ila walikaa kimaya na kuacha mabo yaende tuu!

Baadae NACTE wakasema wale walio chini ya dv 26 hawatambuliki na watakuwa wamejiondoa wenyewe.

Vijana wakendelea kukomaa wakasema tushapotezewa mda sana leo hii mnatuakatisha jujuu haiwezekani, wakaenda tena TCU mgaya siku hiyo akataka kuondoka vijana wakamkomalia kikaendeshwa kikao na majibu ya tcu yalikuwa hivi.......

Kama mngekuwa hamna vigezo mbona chuoni mmepokelewa?
Hapa sisi wenyewe tupo kwenye matope wizara ipo kwenye matope nyie wanafunzi mpo kwenye matope na Chuo pia kipo kwenye matope.
Wanafunzi wote ni qualified ila ni wanafunzi ishirina na tatu tuu ndio wanamatatizo!

Vijana wakawaambia sisi tunataka hayo ulioyatamka utupe kwa maandishi, wakagoma tena kuyathibitisha kwa maandishi!

Chuoni wakawapa barua wanafunzi ya makubaliano yao na tcu kuwa vigezo ni d nne!
Nitawaletea attachment ya hiyo barua.

Baada ya kufatilia sana tcu wakaweka majina ya disqualified dk kumi na kuyaondoa baada ya kusumbuliwa sana ndio wakaamua wayaweke sasa!

Mgaya akaambiwa na waziri wa elimu achana na yaliyopita tuangalie tulipo lizungumzie hili swala! Mgaya akapotezea tena akakaa kimya! Huko chuoni nako wahindi wanalazimisha wanafunzi waingie darasani!

Kumbe walikuwa wanacheza mchezo mchafu wanafunzi wakiingia darasan wanapiga picha wanazituma tcu kuwa wanafunzi wamekubali kuingia madarasani ili walizime juu juu.

Wanafunzi walipgundua hayo wakaatumia nguvu kuwafanya wanafunzi wenzao wasiingie madarasani!

Na lengo lao ilikuwa ni kuwapunguza kwa mtindo wa kuwafelisha!

Vijana hao wakaamua kwenda had I kwa Paul makonda mkuu wa mkoa wa dar es salaam mwanzo wa wiki hii bila mafanikio, wazo lao la mwisho ilikuwa ni kumtafuta mwana sheria ili kumwelezea swala lao kama anaweza kuwasaidia

Lakini kuna haja gani ya kutafuta mwanasheria wakati mamlaka zinazohusika zipo!?

Sasa tcu tuwaelewe vipi mwanzo walisema wanfunzi wote ni qualified leo hii mnawaambia wanafunzi hao hao ni disqualified na wengine wako mwaka wa tatu!

Inatia huruma sana watoto wa watu wameteseka sana, wazazi wao wamehangaika kuwalipia ada kwa miaka yote hiyo ada ya muhindi c mchezo,

Je kama ww ingekuwa mwanao amefanyiwa uhuni kama huo kweli utachukua hatua gani?

Wanaohusika plz nendeni pale muwasaidie watoto wa watu wa maskini wanaoteseka katika nchi yao kwa wageni wanaoshirikiana na walafi watanzania wenzetu.

Ebu tushauriane na kuwapa ushauri Hawa vijana wafanyeje, haturusu matusi wala maneno machafu ukishindwa pita kushoto.

Nitajitahidi kupata attachment zote za ushahidi wa wanafunzi ambazo ni officials kati yao, chuo , Tcu na wizara ya elimu.
Na naendelea kupata mengi kuhusu hili swala na ntafikisha kila litakaponifikia,

Source wanafunzi wa st Joseph luguruni Dar es salaam. 

wako blogger boy ni kukuletea kila kitu!
Share:

UTEUZI WA WAKUU WA WILAYA:RAIS MAGUFULI AMTEUA GELASIUS BYANKWA KUWA MKUU WA WILAYA YA HAI

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg_iFSP8zUGSzvSC2Lwwa9mU4m6Mia1uKK4hnWlEdKXXM2JjaGt7BzdyN-8v3ZNvWMew5Qko6WqnE4wdUGbc-jmJPT0R-mE4CtttjhUJ7k7mJFikAbAmr-oSbv4NylMb_OB5P1rnF_xkOI/s1600/IMG-20160408-WA0013.jpg
Share:

TRICK:JINSI YA KUVERFY ADSENSE ACCOUNT WITHOUT PIN AND OFFICIAL DOCUMENT 2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
verify adsense account
Habari zenu,

Kwa jina naitwa innocent the blogger boy,kutokana na mablogger wengi kusumbuka kuverfy adsense account,kutokana na kutokupata  barua kwa wakati husika.

Utangulizi;

Google adsense ni moja ya programme bora zaidi duniani katika mtandao ambayo inamfanya mtumiaji kujipatia kipato .Lakini tatizo kubwa ni kumba google wana sheria kali saaaana ambazo kuzifata kwake ni ngumu sana na hupelekea baadhi ya watu kufungiwa account zao.Baadhi ya sheria zao ni kwamba ukifikia threshold value ambayo huwa ni dollar 10 unatakiwa uverfy account yakokwa kutumia PIN ambazo utatumiwa na google adsense!

Baadhi ya watu hili kwao limekuwa ni tatizo kubwa kutokana na kutokupokea PIN kwa wakati husika,au kutokufika kabisa,au ufigisu unaofanywa na baadhi ya wafanyakazi wa posta kwa kuficha barua hizo wakizani ni pesa umetumia kutoka google.

Kama hutopokea PIN za kuverfy una nafasi mbili zaidi za kurequest PIN mpya.NOTE:always baada ya kutumiwa barua ya kwanza huchukua siku 21 ,kurequest new PIN ,then it takes another 21 days to request new PIN and lastly it takes last 21 days kurequest new PIN.

Kama hutopokea kwa itakubidi uverfy ur account kwa kutumia OFFICIAL DOCUMENT ambayo imethibitishwa na serikali yako.

Documents zinaruhusiwa ni pamoja na Kitambulisho cha utaifa,leseni,bill ya umeme au kitambulisho cha kupigia kura.Lakini bado kuna watu hawawezi kuverfy account hizi kutokana na sababu mbalimbali,zikiwemo majina kutokuendana,kwa na account zaidi ya moja zenye majina tofauti. NK.

TRICK YA KUFANYA NI HII
1.Tembelea this link 
2.Baada ya hapo utaulizwa je,umefikia threshold value?
3.Kubali
4.Utaulizwa umeshawahi kupokea pin,CLICK NO.
5.utaulizwa umesha request zaidi ya mara mbili,click YES
6.utapata FORM ya kujaza
7.JAZA HIYO FORM KWA USAHIHI.
8.itafikia sehemu itahitaji kua attach ur proof document
9.Hapa sasa unatakiwa ku create txt file
open>note pad in ur PC> write the following ktk order tajwa.

Name:
Contact Adress:
Phone No:
Email Address: 
Publisher ID:
Postal Address:
Country:

Baada ya kuandika kila kitu ktk form tajwa hapo juu,save it kwenye desktop ili iwe rahisi kukumbuka.
Rudi kwenye ile form uliyoambiwa ku attach txt file,click open and attach ur created txt file saved at ur desktop.
Now click submitt:
PIN HOLD KATIKA ACCOUNT YAKO ITAONDOLEWA NDANI YA SAA MOJA TU!

"Wako innocent the blogger boy napatikana kwa namba 0768260834/0652740927"ninaandaa clip yenye tricks mbalimbali za adsense!
Karibuni kwa Maswali!
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger