Friday, 8 April 2016

NAFASI MPYA ZA AJIRA/KAZI

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Serikali imeanzisha mpango maalumu wa mafunzo kwa wahitimu kutambua ujuzi katika sekta zisizo rasmi, ili kuwajengea vijana wigo mpana wa ajira kwa fani walizosomea.

Mpango huo unalenga kutoa mafunzo ya ufundi katika fani mbalimbali kwa vijana walioishia darasa la saba, kidato cha nne au sita na wanaohitimu vyuo mbalimbali.

Lengo ni kuwawezesha vijana kupata ajira na waajiri nao kupata watu wenye ujuzi wa kutosha.

Akizungumzia mpango huo juzi, Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Ajira Ofisi ya Waziri Mkuu, Robert Masingiri alisema changamoto kubwa kwa vijana ni ukosefu wa ajira hasa wanaomaliza shule bila kuwa na fani yoyote.

Masingiri alisema baada ya Serikali kuona upungufu huo, imeandaa mpango maalumu unaofadhiliwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) ili kutoa mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi na wahitimu wa vyuo mbalimbali.

“Licha ya kutoa mafunzo hayo, tutatambua ujuzi uliopatikana kwa mfumo usio rasmi. Tutawapa wataalamu hao baada ya kukaa nao na kuona uwezo wao, hiyo itawasaidia kupata ajira hasa zinapokuja kampuni za uwekezaji au viwanda,” alisema.

Masingiri aliongeza kuwa nia ya Serikali ni kuongeza ujuzi kwa wafanyakazi ambao wako kazini, mpango huo utaanza na vijana 5,000.

Mkurugenzi wa ILO nchini, Mary Kawar alisema Tanzania imefanikiwa kuandaa mpango utakaosaidia vijana wengi kupata ajira 
“Kwa muda mrefu kumekuwa na pengo kati ya elimu ya darasani na utendaji. Naamini mafunzo haya yatatoa fursa ya pekee kuziba pengo hilo na kuongeza sifa za kuajiriwa,” alisema Kawar.

Mkurugenzi wa Taarifa za Soko la Ajira Ofisi ya Waziri Mkuu, Ahmed Makbel alisema mpango huo utakuwa na manufaa kwa waajiri na waajiriwa, kwa sababu wote watapata wanachohitaji.
Share:

NEWS:HAYA HAPA MAJINA 157 YA WANAFUNZI WA ST.JOSEPH DIPLOMA YA UALIMU WALIORUHUSIWA KUENDELEA NA MASOMO LEO TAR 8.4.2016

Share:

WANAFUNZI 424 WA ST.JOSEPH LUGURUNI WATEMWA NA TCU,BAADA YA KUONEKANA HAWANA SIFA YA KUSOMEA DIPLOMA YA UALIMU LEO APRIL TAREHE 8.4.2016

Share:

MAGAZETI YA LEO IJUMAA TAREHE 8.4.2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Share:

Thursday, 7 April 2016

DADA AKE TUNDU LISSU,CHRISTINA LISSU AFARIKI DUNIA

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

ALIYEKUWA MBUNGE WA CHADEMA CHRISTINA LISSU AFARIKI DUNIA

Aliyekuwa Mbunge Viti Maalum (Chadema) Mh.Christina Mughwai Lissu amefariki dunia muda mfupi uliopita katika hospitali ya Aga Khan jijini Dar. Marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa saratani tangu mwaka jana. Mungu ampumzishe kwa amani.![​IMG]
Share:

MKURUGENZI WA HANANG ASIMAMISHWA KAZI

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY


Mkuu wa mkoa wa Manyara Dkt Joel Bendera ametangaza kumsimamisha kazi mkurugenzi wa halmashauri ya Hanang Bw Felex Mabula kutokana na tuhuma za ubadhirifu wa fedha zaidi ya milioni 600 ambapo uamuzi huo umeutoa mbele ya watumishi pamoja na madiwani wa hlamshauri hiyo.

Dkt Joel Bendera ametangaza uamuzi huo wa kumsimamisha kazi Bw. Felex Mabula kutokana na tuhuma za ubadhirifu wa fedha zaidi ya milioni 600 ambapo ubadhirifu huo umeibuliwa na baraza la madiwani baada ya kupokea ripoti ya mkaguzi wa ndani wa halmshauri ya hii ya Hanang.

Nalo baraza la madiwani wa halmshauri hii ya Hanang kupitia mwenyekiti wake limesemakuwa halitakuwa tayari kutoa ushirikiano wa kikazi bw Mabula endapo uchunguzi utafanyika na kubaini kuwa msafi na kurejeshwa katika kiti chake.

Hata hivyo mkuu mkoa wa Manyara Dkt Joel Bendera baada ya kutangaza kumsimamisha kazi bw Mabula pia amemtaja Bw Werasare Munisi kuchukua nafasi ya mkurugenzi huyu ambapo munisi alikuwa mhandisi wa maji halmashauri ya Hanang. 
Share:

TAARIFA ZA UZUSHI KUHUSU WALIMU KUSHONEWA SARE INAYOSAMBAZWA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
 
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI, TEKNOLOJIA NA UFUNDI

TAARIFA KWA UMMA

YAH: TAARIFA ZA UZUSHI KUHUSU WALIMU KUSHONEWA SARE INAYOSAMBAZWA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII

Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi inakanusha taarifa inayosambazwa katika mitandao ya kijamii yenye kichwa cha habari “NDALICHAKO NA WALIMU TZ”.

Taarifa hiyo inadai kuwa Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof. Joyce Ndalichako amesema kuwa walimu wanaandaliwa sare watakazo vaa wakati wa kazi.

Tunapenda kuufahamisha umma kuwa Taarifa hizi si za kweli. Aidha, Wizara inawataka watu wanaoeneza taarifa za kizushi za aina hii waache kufanya hivyo ili kuepusha usumbufu unaojitokeza. Hatua za kisheria zitachukuliwa kwa watakaobainika kuanzisha na kueneza uzushi huu.

IMETOLEWA NA

KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
07/04/2016
Share:

NAFASI ZA KAZI UTUMISHI APRIL 5 2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Details for Tangazo la Kazi-5-4-2016

PropertyValue
Name:Tangazo la Kazi-5-4-2016
Description:Dead line for Application is 19-04-2016
Filename:wcf.pdf
Filesize: 250.62 kB
Filetype:pdf (Mime Type: application/pdf)
Creator:psrsweb
Created On: 04/06/2016 00:32
Viewers:Everybody
Maintained by:Editor
Hits:14276 Hits
Last updated on: 04/06/2016 00:33
Homepage:

Share:

TAARIFA KWA UMMA - KUCHELEWA KWA TATHMINI YA VYETI NA ULINGANISHO WA TUZO ZINAZOTOLEWA NA “NCC EDUCATION NA ASSOCIATION OF BUSINESS EXECUTIVES- ABE, UK”

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
 
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI
(NACTE)

 

TAARIFA KWA UMMA
KUCHELEWA KWA TATHMINI YA VYETI NA ULINGANISHO WA TUZO ZINAZOTOLEWA NA “NCC EDUCATION NA ASSOCIATION OF BUSINESS EXECUTIVES- ABE, UK”

Baraza la Taifa la Elimu Ufundi (NACTE), linapenda kuujulisha umma kuwa limechelewesha utoaji wa majibu ya maombi ya tathmini ya vyeti na ulinganisho wa tuzo zinazotolewa na NCC Education, UK na Association of Business Executives- ABE, UK kwa kushirikiana na Taasisi binafsi za Elimu ya Ufundi hapa nchini. Hii ni kutokana na kufanya upya uchambuzi wa maombi hayo baada ya kubaini kuwepo kwa dosari katika hatua mbalimbali za utoaji wa mafunzo hayo kama vile sifa za udahili, uendeshaji wa mafunzo, upimaji na vyeti. 

Kulingana na taratibu za Baraza, ni haki ya mwombaji wa huduma hiyo kupewa majibu ndani ya siku 30 baada ya kukamilisha taratibu zote za kutuma maombi. Baraza linatambua kuwa uamuzi wake wa kuchambua upya na tathmini ya maombi yote yaliyotumwa umeleta usumbufu kwa waombaji. Hivyo linaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.

Baraza litakamilisha kazi ya kuchambua na kutathmini vyeti na ulinganisho wa tuzo hizo na kutoa majibu kwa waombaji wote kabla ya tarehe 30/04/2016.  
Asanteni kwa ushirikiano wenu.  

IMETOLEWA NA;
OFISI YA KATIBU MTENDAJI
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI
Tarehe 6/4/2016
Share:

Serikali yabaini watumishi hewa 1855 nchini

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Serikali yabaini watumishi hewa 1855 nchini
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mheshimiwa George Simbachawene amewataka wakuu wa mikoa ambayo imekutwa na watumishi hewa kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi waliohusika kulipa na kupokea mishahara hewa.
Akizungumza na wakuu hao wa mikoa mara baada ya kukabidhiwa ripoti hizo, Waziri Simbachawene aliwataka viongozi hao kuhakikisha kuwa wanawakamata watumishi hao kwa makosa waliyobainika nayo na hatua stahiki.
"Wananchi wanataka kusikia hawa waliokuwa wanaiibia serikali wamechukuliwa hatua gani mara baada ya kutangazwa badala ya kuishia kuwatangaza kuwa ni watumishi hewa na wanalipwa mishahara," alisema.
Jumla ya watumishi hewa 1855 wamebainika kuwepo katika mikoa mbalimbali nchini huku mkoa wa Mwanza ukiwa na watumishi hewa 334, Arusha 270 na Sungida 202.
Mikoa ya Mwanza, Arusha na Singida inaongoza kwa kuwa na watumishi hewa wengi.
Kwa mujibu wa taarifa hizo kutoka kwa wakuu wa mikoa, watumishi waliobainika kuwa ni hewa ambao wamekuwa wakilipwa mishahara ni walimu na madaktari ambao ni marehemu na wastaafu.
Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya Rais John Magufuli, kuwaagiza wakuu hao wa mikoa kuwasilisha ripoti ya watumishi hewa ambayo waliikabidhi kwa Simbachawene jana jijini Dar es Salaam kabla ya kuiwasilisha kwa Waziri wa Utumishi na kujumilisha na ripoti za sekta zote nchini na hatimaye kumfikishia Rais.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongela alisema jumla ya watumishi hewa 334 walibainika kwenye mkoa huo hususani katika Halmashauri ya jiji la Mwanza ambalo lina watumishi hewa 72 pekee.
Katika mkoa wa Arusha jumla ya watumishi hewa 270 walibainika katika kipindi cha wiki mbili na kusababisha upotevu wa Sh. bilioni 1.188 kwa mwezi March pekee.
Katika mkoa wa Singida jumla ya watumishi hewa 202 walibainika na mkoa wa Kigoma wenye watumishi hewa 171 ambao wamesababisha hasara ya Sh. milioni 114.6 kwa mwezi.
Mikoa mingine ni Kilimanjaro wenye jumla ya watumishi hewa 111 ambao waliolipwa Sh. milioni 281.4 kwa mwezi mmoja na Dodoma watumishi hewa 101 waliolipwa Sh. bilioni 297 kwa muda wa miezi sita.
Pia katika mkoa wa Morogoro watumishi hewa waliobainika ni 122 ambao walilipwa Sh. milioni 450.79 kwa mwezi March pekee na mkoa wa Mara watumishi hewa 94 ambao walilipwa Sh. milioni 121.1 kwa mwezi mmoja.
Mkoa wa Mbeya ambao umeungana na mkoa mpya wa Songwe ulibainika kuwa na watumishi hewa 98 ambao walilipwa mishahara kiasi cha Sh. milioni 459.6.
Katika jiji la Dar es Salaam watumishi hewa waliobainika ni 73 ambao wamelipwa Sh. milioni 379 kwa mwezi mmoja.
Mikoa mingine ni mkoa wa Pwani uliobainika kuwa na watumishi hewa 150, Ruvuma watumishi hewa 37 ambao walilipwa Sh. milioni 58. 4, Njombe watumishi hewa 34 ambao walilipwa Sh. Milioni 20.107 na mkoa wa Rukwa wenye watumishi hewa 18 waliolipwa mishahara Sh. Milioni 55.64.
Watumishi wengine hewa walibainika katika mikoa ya Simiyu 33 ambao walilipwa Sh. Milioni 320.993 , Tabora jumla ya watumishi hewa 48 ambao walilipwa Sh. Milioni 118, Tanga watumishi hewa 24 na Lindi watumishi 57 waliolipwa Sh. Milioni 36.
Mikoa mingine ni Katavi wenye watumishi hewa 21 ambao walilipwa Sh. milioni 120 kwa miezi sita, kagera 14 ambao walilipwa Sh. milioni 49. 147 kwa mwezi, Geita wenye watumishi hewa nane na Manyara wenye watumishi hewa watano.
Aidha katika mkoa wa Shinyanga haukubainika kuwa na watumishi hewa kutokana na malengo waliyokuwa wamejiwekea tangu mwaka 2014, ikiwamo kukagua idadi ya watumishi walioko kazini na wanaotakiwa kulipwa mishahara kila mwezi.
Pia katika ripoti hizo walibainika watumishi watoro ambao walikuwa wakiendelea kulipwa mishahara licha ya kutokuwepo kazini kwa muda mrefu.
Katika mkoa wa Dodoma jumla ya watumishi watoro 38 walibainika, Iringa 145 na Kagera watumishi 248 ambao pia wanaendelea kuchunguzwa.
Mkoa wa Manyara jumla ya watumishi watoro 50, Mtwara watumishi 285 watoro, Mwanza watumishi watoro 205, Pwani watumishi watoro 50 , Rukwa watumishi watoro 139 na Simiyu watumishi watoro 62.
Mkoa wa Singida watumishi watoro 29 na Tanga jumla ya watumishi watoro 502.
Watumishi hao watoro ni wale walioacha kazi lakini wamekuwa wakiendelea kulipwa mishahara na wengine walio kwenye matatizo ya kiutumishi.
Share:

Waziri Simbachawene azipongeza halmashauri 10

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Waziri Simbachawene Azipongeza Halmashauri 10
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.George Simbachawene amezipongeza halmashauri 10 zilizofanya vizuri katika vigezo vya kutoa takwimu kwa usahihi, kupanga walimu katika shule zenye upungufu na kutuma ruzuku shuleni kwa wakati.
Aidha Waziri Simbachawene aliwataka wasimamizi wa mpango huo ambao umewekwa na serikali kwa lengo la kuinua kiwango cha elimu nchini wahakikishe kuwa wanautekeleza kwa ufanisi wa hali ya juu ili uweze kufanikisha malengo yaliyo kusudiwa.
Akizungumza kwenye hafla maalum iliyoandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi kwa ajili ya kutoa motisha kwa halmashauri kumi bora zilizofanya vizuri Mhe.Simbachawene aliwataka viongozi wa Halmashauri 10 zilizofanya vizuri pamoja na halmashauri ambazo hazikufanya vizuri katika vigezo vilivyowekwa kujituma na kuhakikisha wanafanya kazi kwa ubunifu ili kuleta tija katika elimu nchini.
Aliongeza kuwa kuwa taifa linapaswa kujenga misingi imara ya elimu ya awali ili kuwa na wahitimu wa elimu ya juu ambao wameandaliwa vizuri na wanaoweza kukabiliana na changamoto za ajira za sasa.
Aliwataka kutekeleza majukumu yao kwa weledi mkubwa utakaoleta mabadiliko katika utoaji huduma na kufanya kazi kwa matokeo na kutekeleza malengo waliyojiwekea kwa wakati na kuzingatia viashiria vilivyoanishwa na kuvitekeleza ipasavyo.
Aidha, aliwakumbusha umuhimu wa kuweka takwimu na kutumia fedha zitakazoletwa kwa mujibu wa taratibu za serikali kwani huo ndio msingi wa kuleta tija katika maeneo yao ya kazi.
Halmashauri 10 kati ya 181 zilizopo nchini ambazo zimefanya vizuri katika vigezo vilivyowekwa na serikali ni halmashauri za Mbinga, Nkasi, Chato, Busega, Lushoto, Liwale, Sikonge, Mbarali, Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda na Halmashauri ya Wilaya ya Tabora.
Share:

HAYA HAPA MAJINA YA WATUMISHI WALIORUHUSIWA KUHAMA KUANZIA MWAKA 2012-2015

Share:

MATOKEO UEFA TAREHE 6.4.2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger